2015年4月8日 星期三

Jinsi Ya kuomba


Wewe ni nani?

 

“Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika Imani…”

2 Wakorintho 13: 5
 

Wewe umezaliwa na Mungu kwa mujibu wa Neno la Mungu, kwa kuwa linaonyesha vizuri kuwa wewe ni mtoto wake. Moyo wako uwe na uhakika mbele zake. Kila aliyeligundua Neno la Mungu, hatahisi na kujua ukweli katika kipindi hicho, katika uwepo wa Mungu, kuwa ni mtoto wake. Swali, siyo wewe? Ni nani sasa? Je, Roho ya uwana imo moyoni mwako sasa? Chunguza moyo wako sasa, wewe ni hekalu la Roho Mtakatifu? Anaishi ndani yako? 

Haupo kwenye kipindi cha pumziko kupitia ubatizo, lakini roho wa Kristo na utukufu wake hayupo juu yako? Au ule mwanga uliokuwa ndani yako umebadilika na kuwa giza? Kwako ninasema, “Lazima uzaliwe mara ya pili”. Umesoma alama za watoto wa Mungu. Wote wasio nazo mioyoni mwao haijalishi wamebatizwa au hawajabatizwa, lazima wataangamia milele.

 Bwana Yesu! Naomba kila mmoja aliyejiandaa kwa moyo wake kuutafuta uso wako, apokee Roho ya uwana na aweze kulia, “Abba, yaani Baba”. Wafanye sasa wawe na uwezo wa kuliamini Jina lako ili wawe watoto wa Mungu na wajue wamekombolewa kwa damu na kusamehewa dhambi. 
 

Njia ya Maombi

 
“Basi ninyi saline hivi”

Mathayo 6: 9
 

Yeye anayejua vizuri namna tunavyotakiwa kusali na jinsi tunavyotakiwa kusali, hitaji gani, jinsi anavyowasilisha. Litampendeza yeye mwenyewe na mazuri yatakuwa yetu. Haya ndiyo maombi (sala) sahihi na yanayojulikana. Yanaelezea mahitaji yetu yote, yanaelezea shauku zetu zote kisheria na mwongozo kamili na Roho Mtakatifu yupo kutuongoza kuomba, kwa vitu; muda mwingine, kwa Neno kwa kifupi, kwa ukaribu, kikamilifu. Maombi ya sehemu tatu, Utangulizi na hitimisho. 

Utangulizi: “Baba yetu wa mbinguni”. Inajenga msingi wa maombi. Inahusisha jinsi tunavyomjua Mungu kabla hatujaomba kwa ujasiri, inaonyesha imani yetu, na upendo wa Mungu na mtu anayemwendea Mungu kwa maombi. “Baba yetu” ambaye ni mwema na wa neema kwa wote, Muumbaji, anayetutunza, Baba wa Bwana wetu, tupo kwa ajili yake, ni watoto wake kwa neema, siyo Baba yangu tu bali Baba wa ulimwengu, malaika na watu wote. “Wa mbinguni” – amekaa mbinguni na duniani na anatawala kila kitu mbinguni na duniani, anajua kila kimbe na kazi yake, na kila tukio milele na milele.

Bwana mwenyezi na mtawala wa kila kitu. Kuomba mkate wa kila siku:- Chakula na neema utupe leo riziki yetu, Mathayo 6:11, “Jina lako litukuzwe”. Naomba, Ooh Baba, ujulikane na viumbe vyote kwa ufahamu mzuri, uheshimiwe, upendwe uogopwe na watu mbinguni na duniani, na malaika wote na watu wote, “Ufalme wako uje” – Ufalme wako uje haraka na umeze falme zote za dunia, watu wote wakupokee, kristo, ufalme wako uaminiwe kwa jina lako.

Watu wafunikwe na haki, amani, furaha, utakatifu na shangwe mpaka utakapokuja kutuchukua kwenye ufalme wenye utukufu na kukaa na wewe milele. “Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni” naomba viumbe vyote vinavyoishi duniani vifanye mapenzi yako kama malaika watakatifu!.

 a hili lifanyike kwa kuendelea bila kuingiliwa na mapenzi yao na wawe wakamilifu. Roho wa neema kwa damu ya Yesu, ya Agano la milele, wafanye wakamilifu kwa kila tendo jema sawasawa na mapenzi yako. Na kazi zao zikupendeze mbele ya macho yako. “Tupe” - Baba (hatujafanya jema lolote bali kwa rehema). “Leo” -  (Kwa kuwa hatuna wazo lolote kwa kesho). “Mkate wetu wa kila siku”. Kila kinachohitajika katika miili yetu na nafsi zetu, siyo tu nyama inayoharibika lakini meza ya mkate na neema yako; chakula kinachodumu milele.

 “Utusamehe deni zetu kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu” – tupe, Bwana, ukombozi katika damu yako, utusamehe dhambi zetu. Kama unavyotuwezesha kuwasamehe kabisa; ili nasi tusamehewe maovu yetu “Na usitutie majaribuni lakini utuokoe na yule mwovu” kila tunapojaribiwa, Bwana unayetusaidia katika udhaifu wetu, usituruhusu tukashindwa; lakini utufanyie njia ya kutokea ili kwamba tuwe zaidi ya washindi kwa pendo lako juu ya kila dhambi na mtokeo yake.

Kanuni ya kila uhitaji (tamaanio) katika moyo wa mkristo ni utukufu wa Mungu. (Mathayo 6:9-10) na unachohitaji kwa ajili yako ni mkate, riziki ya kila siku na nguvu ya ukombozi dhidi ya dhambi (mathayo 6:11-13) hakuna zaidi ya hivyo, mkristo akafanya mapenzi yake. Kwa hiyo sala hiyo inapeleka matamaanio yetu yote. Maisha ya milele ni matokeo ya utakatifu.

Mwisho; Ufalme ni wako “Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu na utukufu hata milele, amina” Mathayo 6:13.

 Hitimisho: - “Kwa kuwa ufalme ni wako” - “Uweza wa pekee, kwa kuwa anamiliki kila kitu katika ufalme wake usio na mwisho. “Na utukufu” – Sifa kwa kila ulichokiumba, kwa nguvu zako, kwa kazi zako za ajabu, na uweza wa ufalme wako unadumu miaka yote daima. Amina.
 

Maombi ya mtu aliyeamka

 

“Hivyo husema, amka, wewe usinziaye, ufufuke katika wafu, na kristo atakutangaza”

Waefeso 5: 14

Jitambue mwenyewe! Kama wewe ni miongoni mwa maskini wanaojidanganya wenyewe, Amka! Je, ujasiri wako ni ujasiri unaotokana na nafsi yako mwenyewe ili kukupa ushuhuda kwamba wewe ni mtoto wa Mungu, na kwamba umewashinda maadui zako?

 Aha! Umepimwa katika mzani na umeonekana kupungua. Neno la Mungu limeijaribu nafsi yako na imeonekana kama fedha iliyojaribiwa. Wewe si mnyenyekevu wa moyo, kwa hiyo hujapokea Roho wa Yesu bado. Wewe si mpole na mtulivu, ni mwenye hasira pia. Kwa hiyo, furaha yako haina thamani, si furaha katika Bwana. Huzitunzi amri zake; kwa hiyo humpendi, na wewe si mshirika na Roho Mtakatifu. Ni uhakika na uthibitisho kama Neno la Mungu linavyofanya kazi; Roho wake hawezi kuishuhudia roho yako kuwa wewe ni mtoto wa Mungu.

Mlilie ili maganda yaliyopo katika macho yako yadondoke katika macho yako ili uweze kujijua, kama Mungu anavyokujua wewe: maskini, usiyestahili, mwenye dhambi. Omba ili uweze kupokea ile hali ya hukumu ya dhambi mpaka utakaposikia Sauti inayofufua katika wafu, ikisema “changamka”. Dhambi zako zimesamehewa. Enenda kwa amani; imani yako imekuponya:. Na Roho wake atakushuhudia kuwa wewe ni mtoto wake.

 

Omba, Tafuta, Bisha

 

“Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa”

Luka 11: 9

 

Wale ambao wanashauku na neema ya Mungu wanapaswa kuingojea, kwanza, kwa njia ya maombi; hiki ni kielelezo cha moja kwa moja cha Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe. Katika hotuba ya mlimani, baada ya kuelezea kwa marefu kila kilichomo ndani ya dini na kuelezea mapana yake, aliongeza, “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata bisheni, nanyi mtafunguliwa” (Mathayo 7: 7 – 8 na Luka 11: 9-10).

Kwa uwazi zaidi, tunaelekezwa hapa kwamba ili tuweze kupokea, au kama njia ya kupokea, kutafuta, ili kupata neema ya Mungu, lulu ya thamani kubwa; bisheni, yaani - endelea kuomba na kutafuta, ikiwa tutaingia katika ufalme wake. Ili kusiwepo na mashaka yoyote. Bwana wetu anatupa mithali ya pekee ya Baba mwenye shauku ya kutoa vipawa vyema kwa watoto wake, akimalizia na maneno, “Je, Baba yenu aliye mbinguni hatawapa Roho Mtakatifu wale wamwombao?” (Luka 11: 13).

Yesu anatupa maelekezo ya kuomba, pamoja na ahadi ya hakika kwamba kwa njia hii tutapata majibu ya maombi yetu: “Ingia katika chumba chako cha ndani ... bali mbele za Baba yako aliye sirini; na ... Baba yako aonaye sirini atakujaza” (Mathayo 6: 6).

 

Omba na kuvumilia

 

“Bwana, tufundishe sisi kusali”.

Luka 11: 1-2

 

Mara baada ya Bwana wetu kujibu ombi (hapo juu) la wanafunzi wake, akiwaonyesha ulazima wa kutumia maombi, ikiwa tunataka kupokea kipawa kutoka kwa Mungu. Aliwaeleza habari za mtu alimwomba rafiki yake usiku wa manane, amkopeshe mikate mitatu. Ingawa rafiki yake hakuamka na kumpa kwa sababu alikuwa ni rafiki yake, bali kwa sababu ya bughudha isiyokoma. Rafiki yake ataamka na kumpa. Yesu alisema, “Nami nawaambia, ombeni, nanyi mtapewa”.

 Je! Ni kwa jinsi gani Bwana wetu ameielezea njia hii kwa uwazi zaidi – kuomba kwa kung’ang’ania - ambako tunaweza kupokea kutoka kwa Mungu vile ambavyo tusivyoweza kuvipokea kabisa? Aliwaambia mithali nyingine tena, mwisho wake alisema imewapasa kumwomba Mungu siku zote, wala wasikate tamaaa”. (Luka 18:1). Kuvumilia mpaka wamepokea walichokuwa wamemwomba Mungu; “akasema, palikuwa na kadhi katika mji fulani hamchi Mungu wala hajali watu.

 Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, nipatie haki na adui wangu. Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, ijapokuwa simchi Mungu; wala sijali watu, lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake asije akanichosha kwa kunijia daima” (Luka 18: 2-5).

Bwana wetu mwenyewe aliwahakikishia wale wanaolia mchana na usiku; “nawaambia, atawapatia hiki upesi; walakini atakapokuja mwana wa Adamu, Je! Ataiona imani duniani?” (Luka 18: 8).

 

Maombi yanapokuwa uponyaji wa nafsi yenye giza

 

“Ee Bwana, unijaribu na kunipima: unisafishe mtima wangu na moyo wangu:

Zaburi 26: 2

 

Kwa kufikiri kwamba uponyaji ni ule ule katika maeneo yote ni kosa kubwa - lakini linalofahamika kwa wengi. Uponyaji wa kiroho, kama ulivyo wa kimwili-magonjwa huwa ya namna mbalimbali kama vyanzo vyake visivyofanana. Jambo la kwanza, kuchunguza kilichosababisha (chanzo). Kilichosababisha ugonjwa ndicho kinachotoa au kueleza ni tiba gani inayohitajika.

Kwa mfano: Je, ni dhambi ndiyo iliyosababisha giza? Je, ni dhambi gani? Je, dhamiri yako inakushitaki kwa kutenda dhambi yoyote ambayo humhuzunisha Roho Mtakatifu? Je, unaweza kutarajia nuru na amani kurudi bila kuondoa kitu hicho na kupokea msamaha? Au pengine ni baadhi ya kutofanya uliyopaswa uyafanye (sin of omission). Je, unawakemea wanaotenda dhambi mbele yako? Je, unatembea kwa kutumia njia ambazo Mungu amekupa: mbele za watu, familia, katika maombi ya faragha? Kama ki-mazoea, umekataa majukumu yanayojulikana, mpaka dhambi (yakutofanya ulipaswa kufanya, au kufanya uliyokuwa hupaswi kuyafanya) itakapoondolewa, faraja yote ni batili na ya uongo. Usitafute kuwa na amani moyoni mpaka umekuwa na amani ya mungu, ambayo haiweze kuwepo bila mazingira ya toba sahihi.

Au je, kuna baadhi ya dhambi (ndani) ambazo zinainuka kukusumbua? Je, umewahi kufikiri zaidi kuhusu nafsi yako zaidi ya jinsi ikupasavyo kufikiri? Je, umejitukuza zaidi kuhusu kitu fulani kuliko Yesu Kriso? Je, umekuwa na fikra ya kuwa na mafanikio uliyo nayo ni matokeo ya nguvu, hekima, na ushujaa wako mwenyewe? Kama ni hivyo, ona njia unayopaswa kuiendea: jinyenyekeze chini ya mkono wa Mungu, na kwa wakati wake atakuinua.

 

Maombi ya asubuhi na mapema

 

“Ee Mungu, nitakutafuta mapema”

Zaburi 63: 1

 

Je, unaiona namna gani siku yako? Wakristo wengi, kama hawana majukumu ya kila siku ya kwenda kazini, huamka saa bili au saa tatu asubuhi baada ya masaa manane, tisa au zaidi ya kulala usingizi. Sisemi kwamba wote wanaofanya hivi wanakwenda kuzimu. Lakini hata hivyo siwezi kusema wanakwenda mbinguni, au wamejikana wenyewe na kubeba msalaba wao kila siku. Kutokana na uchunguzi wa zaidi ya miaka sitini, kwa wastani wanaume wanapaswa kulala (kupumzika) si zaidi ya masaa sita mpaka saba, na wanawake wenye afya wanapaswa kulala (kupumzika) si zaidi ya masaa saba mpaka nane katika saa 24.

Huu muda wa kulala (kupumzika) unafaida kwa mwili na nafsi; ukilinganisha na madawa yoyoyte ninayoyajua; madawa ya kinga, na kuondoa dosari za mishipa ya fahamu.

 

Kumtafuta Mungu

 

“Basi si zaidi damu yake Kristo ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi wa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhambi zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?”

Waebrania 9: 14

 

Liweke neno hili ndnai ya moyo wako, kwamba matendo ya kawaida hayawezi kutoa faida. (manufaa katika maisha ya kiroho) Hakuna nguvu iwezayo kuokoa katika matendo hayo, isipokuwa katika Roho wa Mungu, na katika damu ya Kristo. Hata kile ambacho hukitoa kwetu pasipo neema ndani ya nafsi zetu hakiwezi kuwa na faida bila kumtegemea Mungu pekee. Kwa upande mwingine, yeye anayemtegemea Mungu kwa dhati hawezi kupungukiwa neema ya Mungu, hata kama ataondolewa katika kila jambo linalowafanya watu wasiomcha Mungu kuishi duniani.

Katika kutumia njia zote, mtafute Mungu peke yake na kupitia kitu chochote, tazama pekee nguvu za Roho wake, na kazi ya ukombozi pale msalabani. Jihadhari, usije ukabaki katika matendo pekee; ikiwa utafanya hivyo, yote itakuwa ni kazi isiyokuwa na matunda. Katika neema, hakuna kitu kisichokuwa na Mungu, kinachoweza kuitosheleza nafsi yako. Kwa hiyo mwangalie yeye katika mambo yote, na yote kupitia yeye, na juu ya yote. Kwa kuwa nguvu zote, na mafanikio yote yatolewa kwake pekee.

Pia, kumbuka kutumia njia zote kama njia au namna – kama zilivyokusudiwa na Mungu na siyo kama jinsi zilivyo kwa namna yake, lakini kwa ajili ya kufanya upya nafsi (NIA) katika haki na utakatifu wa kweli. Kwa hiyo, kama kweli zimekusudiwa kufanya hivyo, ni vema; lakini kama si hivyo, ni sawa na kinyesi (mavi), na hasara.

 

Ona umuhimu wa kuwa Mtakatifu

 

“Angalieni msimkatae yeye anenaye, (kutoka mbinguni)

Waebrania 12: 25

 

Jitahidi kuingia katika mlango ulio mwembamba. Strive, (Jitahidi, weka bidii, au juhudi) katika hali ya uchungu wenye kumcha Mungu imetolewa ahadi ya kuingia katika starehe au pumziko lake (Angalia Waebrania 4: 9-11). Jitahidi ili usije ukaikosa starehe au pumziko, jitahidi; yaani katika hali ya kuwa na shauku, kiu, au kuugua kusikoweza kutamkwa. Jitahidi katika maombi pasipo kukoma. Wakati wote, mahali popote, uinue moyo wako kwa Mungu. Usimwache apumzike, kama mwimba zaburi, “Amka na mfano wa Mungu” na kwa njia hii unaweza kupata utoshelevu.
 
Hitimisho: Jitahidi kuingia katika mlango ulio mwembamba. Jitahidi, siyo tu kwa uchungu wa nafsi, wa kushuhudiwa, wa huzuni, wa aibu, wa shauku, wa hofu, wa maombi yasiyokoma. Jitahidi, vivyo hivyo kwa kuweka vema mazungumzo yako yote, maisha yako yote, kwa kutembea kwa nguvu zote katika njia zote za Mungu – njia ya kutokuwa na hatia, kuwa na rehema. Ondoa kila namna ya uovu. Tenda mema yaliyo ndani ya uwezo wako kwa watu. Kana (kataa) mapenzi yako katika mambo yote, na kisha chukua msalaba wako kila siku. Uwe tayari kujitenga na kila kitu kinachoweza kukuzuia, na kukitupa mbali nawe. Uwe tayari kupata hasara ya mali, marafiki, kiafya katika mambo yote – hapa duniani – ili uweze kuingia katika ufalme.

 

Mngojee Bwana

 

“Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake”

Zaburi 62: 11

 

Kwa ujumla wakristo wamekuwa na mapokeo ya kutumia baadhi ya sala au maombi. Sasa, labda wewe ni mmoja ambaye bado unaendelea kutumia namna hiyo ya maombi kama ulivyokuwa mtoto. Lakini, hakika kuna “njia iliyo bora” (1 Wakorintho 12: 31) ya namna ya kuwa mbele za Bwana Mungu. Tathmini hali yako ya ndani naya nje na kisha ulinganishe na maombi unayoomba.

Kwa mfano, wewe ni mtu mwenye afya, mtulivu, na una aina za mahusiano, majirani wema, na uhusiano mzuri na marafiki. Ni wazi kwamba, haki yako ya nje huwafanya watu wakusifu na kuona kwamba wewe ni mtu mwema na mwenye sifa kwa Mungu.

Upande mwingine, kama umo katika dhiki (maskini), au mhitaji, udhia, hatari, au katika maumivu au Ugonjwa, na utamimina moyo wako mbele za Mungu kupitia maombi sambamba na hali yako.

Vivyo hivyo, kujitoa katika maombi yako kutaendana na hali yako ya ndani, au hali ya ufahau wako. Je, wewe ni mzito, pengine kutokana na hali ya dhambi au kutokana na majaribu mbalimbali? Hivyo maombi yako sharti yawe na sehemu ya kuungama, kusali na dua ambazo zinakubaliana na hali ya ufahamu ulio na taabu.

Tofauti na hapo, je, una amani katika nafsi yako? Je, unamfurahia Mungu? Je, faraja zake ni kuu juu yako? Basi, useme na mwimba zaburi “wewe ni Mungu wangu, na nitakupenda.. nitakusifu”. Kusoma na kutafakari zaburi ya sifa kwa kawaida kuinua moyo wa shukurani “Njia iliyo bora zaidi” kuliko yoyote.

 

Usijisumbue kwa lolote

 

“Kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme”

Luka 12:  32

 

Ni kwa kiasi gani inaweza kupendeza Baba wa mbunguni kutupatia vyakula na mahitaji yetu? Kwa kuwa mna urithi huu, msifikiri au kusumbuka na mali za dunia. Vivyo hivyo, Mtume Paulo aliwaandikia (Wafilipi 4: 6), “Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru na haja zenu zijulikane na Mungu”. Kama wanadamu hawatakuwa wanyenyekevu kwako, hata kama si katika hili au jambo jingine lolote, usijisumbue, lakini omba.

Uangalifu na maombi haviwezu kukaa pamoja. “katika kila neno omba” liwe kubwa au dogo “haja zenu na zijulikane na Mungu”; na wale kwa ajili ya aibu au kujifunika na kutokuwa waaaminifu, wakiendelea katika shauku zao, kama kwamba walikuwa wadogo sana au wakubwa sana, lazima waangaliwe kwa makini. “Kwa Mungu” - mara zote si sahihi kuyaweka wazi (kuwajulisha wanadamu) mbele za watu “kwa kusali” ambayo ni kwa mapana na kuzidi kusihi kwa dua “Na kushukuru” - uhakika wa hali ya juu wa nafsi iliyo huru kutoka katika taabu na maombi ya kudhiri kwa kweli.

Na hii hali ya shukurani hufuatwa na amani. Amani na shukurani huwekwa pamoja (Wakolosai 3: 15). “Kesho itajisumbukia yenyewe”. Hivyo uwe mwangalifu an kesho ijapo. Leo uwe huru mbali na masumbufu.

 

Ukane au ukatae u-mimi ili kumtii Bwana

 

“Mkiwa na juhudu katika roho … katika kweli”

Warumi 12: 11-12

 

Huyu ni mmoja ambaye hajaitupia mbali (kuikana) iman. Ambaye bado ana roho ya kufanywa mwema, ambayo huendelea kushuhudia na roho yake kuwa yeye ni mwana wa Mungu. Hata hivyo haendelei katika ukamilifu. Haendelei, kama hapo awali, akiwa na njaa na kiu kuifuata haki; akitaka sana kuwa na sura ya Mungu na utimilifu wa wote wa kumfurahia Mungu kama Ayala aioneavyo shauku mito ya maji (zaburi 42: 1). Vinginevyo ni udhaifu na amezimia na kuchoka katika ufahamu wake, akiwa ameatamia kati ya Uhai na mauti.

Kwa nini yako hivyo? Kwa sababu amelisahau neno la Mungu, ambalo husema kwamba “na kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yake” -  (Yakobo 2: 22). Hatumii bidii yake yote katika kufanya kazi ya Mungu. Wala haendelei katika maombi ya mara kwa mara – yeye binafsi au kujumuika na wengine. Vile vile amepungua katika kushiriki ushiriki wa meza ya Bwana, au kusikia Neno la Mungu, katika kutafakari, kufunga, na kuhudhuria makongamano ya kikristo. Kama huwaachii baadhi ya njia hizi za neema, angalau huwa hazitumii kwa bidii.

Kwa nini sasa, haendelei katika maombi? Kwa sababu katika nyakati za ukame, ni ngumu na ni taabu kwake. Huwa hawaendelei kusikiliza neno la Mungu katika nafsi zote huupenda usingizi. Kwa hiyo imani yake si kamilifu, wala hawezi kukua katika neema, kwa sababu hataweza kujikana mwenyewe na kuubeba msalaba wake.

 

Maombi – silaha ya kuvaa kama taji

 

“Kwa sala zote na maombi – mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo… na kudumu kuwaombea watakatifu”

Waefeso 6: 18

 

Kielelezo cha silaha zote za Mungu kinatuonyesha jinsi inavyopendeza kuwa mkristo. Upungufu wa kimojawapo hutufanya tusiwe wakamilifu. Ingawa anaweza kuwa na kweli ki-imani, akawa na dini, viatu miguu, ngao ya imani, upanga wa Roho; hata hivyo kitu kimoja zaidi kinahitajika: mkisali kila wakati: wakati wote na katika matukio yote, katikati ya matendo (shughuli zote, kwa ndani “Omba bila kukoma” “By the spirit” - kupitia ushawishi.

“Kwa sala zote” yaani maombi ya namna zote: katika ibada, faragha, katika ufahamu, kwa sauti. Usiwe na bidii tu katika aina moja ya maombi na kisha ukaweka aina nyingine; ikiwa tunataka shauku za maombi yetu kujibiwa, tutumie njia zote. Baadhi hutumia maombi ya akili (ufahamu) tu, wakidhani kwamba ni njia ya kuabudu iliyo bora kuliko nyingine. Lakini inahitaji neema ya juu zaidi ili kuwezeshwa kumiminika maombi ya kung’anga’ania na yanayoendelea – kuliko kutumia maombi ya akili.

“Kuomba” – kurudia na kuhojiana katika maombi kama Kristo alivyofanya katika bustani ya Edeni’ “kesheni” - kwa ndani haya maombi yamekusudia Mungu, kujua mapenzi yake, na kupata nguvu za kuyafanya hayo mapenzi ya Mungu na kufikia Baraka tunazozionea shauku. “Kudumu katika kuwaombea watakatifu wote” endelea mpaka mwisho katika zoezi hili takatifu ili wengine waweze kufanya mapenzi ya Mungu na kuwa imara. Pengine tunapokea majibu machache ni kwa sababu hatufanyi maombezi ya kutosha kwa ajili ya wengine.

 

Furahini siku zote: Omba shukurani

 

“Furahini siku zote; Ombeni bila kukoma:

Wathesalonike 5: 16-18

 

“Furahini siku zote”. Katika furaha isiyoingiliwa katika Mungu. “Ombeni bila kukoma” ambayo ni tunda la “furahini siku zote” katika Bwana. “Shukuruni kwa kila jambo”, ambalo ni tunda la yote yaliyopita. Huu ni utimilifu wa kikristo. Zaidi ya hapa hatuwezi kwenda, na hatupaswi kupungukiwa vitu hivi - (furaha na maombi).

Bwana wetu alinunua furaha na haki, kadhalika, kwa ajili yetu. Ni mtindo wa Injili, kwamba kuokolewa katika hatia, tunapaswa kuwa na furaha katika Kristo. Maombi yanaweza kusemwa, kama pumzi ya maisha yetu ya kiroho, yeyote anayeishi hawezi kuacha kupumua. Hivyo ni zaidi sana tunapokuwa tumefurahia uwepo wa Mungu, ni zaidi sana katika maombi na sifa tuzitoazo “Bila kukoma”, vinginevyo furaha yetu itakuwa kama kiini  macho tu.

Shukurani haiwezi kutengwa na maombi ya kweli, imeunganishwa ki umuhimu na maombi. Yeyote anayeomba hutoa sifa, iwe ni kwa raha au maumivu au kwa sababu ya mafanikio, au kwa shida nzito. Humbariki Mungu kwa mambo yote, huwatazama wanapokuwa wakimwendea, naye huwapokea kwa ajili yake mwenyewe tu si kwa kuchagua, wala kukataa, kwa kupanda, au kwa kutopanda, iwe chochote, lakini tu kama inakubaliana au kutokukubaliana na mapenzi yake makamilifu.

“Katika hili” – kwamba mnapaswa kufurahi, kuomba, kutoa shukurani, “ni mapenzi ya Mungu” wakati wote ni mema, mara zote hutuelekeza kwenye wokovu wetu!.

 

Maombi na neema

“Mkiishi kujitakasa roho zetu kwa kutii kweli”

1 Petro 1: 22

 

Ni jambo lisilopingika kwamba kristo ndiyo njia pekee ya neema. Nina jibu, hii ni njia ya kawaida ya kutumia maneno. Elezea neno lenyewe, na hali ya kupinga ukweli huu hutoweka. Tunaposema” maombi ni njia ya neema”, unamaanisha kuwa yeye ndiye gharama na mnunuzi wa neema hiyo, kwamba “hakuna ajae kwa Baba isipokuwa kwa njia ya yeye”. Ni nani anayeikana kweli hii?

Lakini andiko (limepingwa pia) halitudekezi kungojea wokovu? Je, Daudi hasemi “nafsi yangu yamngoja Bwana; na kutoka kwake napaka wokovu? Je, Isaya hatufundishi jambo lile lile, akisema, “Ee Bwana tumekungoja?” haya yote hayawezi kupingwa, kukanika. Bila mashaka, tunapaswa kumngoja Bwana, lakini tutamngoja kwa namna gain? Je, tumeweza kupata njia iliyo bora zaidi ya kumngoja Bwana kuliko ile ambayo yeye mwenyewe ameichagua? Tafakari vema maneno ya Nabii Isaya. Sentensi yote inasema, “naam katika njia ya hukumu zako (maagizo) sisi tumekungoja ee Bwana”. Na Daudi naye alimngoja Bwana kwa mamna hiyo: “Ee Bwana unifundishe njia ya amri zako, nami nitaishika hata mwisho” (Zaburi 119: 33).

 

Omba kwa Imani

 

“Ila na aombe kwa imani pasipo shaka yoyote”

Yakobo 1: 6

 

Kuhusu matumizi ya maombi kama njia ya neema, maelekezo ambayo Mungu ametupa kupitia Mtume Yakobo yako wazi kabisa. Pamoja na maombi ya kila aina, ya kusanyiko au faragha, na Baraka huambatana naye, anasema, “Lakini mtu wa kwenu amepungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote kwa ukarimu, wala hakemei naye atapewa” (Yakobo 1:5). Kama wakiomba; vinginevyo “wala hamna kitu kwa kuwa hamuombi” (Yakobo 4:2). Ikiwa wataomba, hawakemei, lakini anasema, “naye atapewa” - (Yakobo 1:5).

Kwa sababu Mtume anaongeza, “aombe kwa imani” baadhi wanaweza kupinga na kusema kuwa haya siyo maelekezo kwa wasio amini (wanaotafuta), kwa wale wasiojua neema ya msamaha wa Mungu. Nimejibu, maana ya neon “FAITH” (Imani) katika sehemu hii limewekwa na Mtume Mwenyewe, kwa kusudi la kudhibiti upinzani huo. Maneno yanayofuata baada ya hapa ni “Kutokuchukuliwa na mawimbi”, bila mashaka. Asione shaka lakini Mungu asikie maombi yake na kutimiza shauku ya moyo wake; kutampa neema, kwa hekima anayoomba.

Lazima tuhitimishe, kuomba andiko linaloonyesha kwamba wote walio na shauku ya neema wanapaswa kuingoja kwa njia ya maombi.

 

Maombi ya familia

 

“Na hao walio wenye hekima katika watu watafundisha wengi”

Daniel 11: 33

 

Tunandaa nyumba zetu katika utumishi kwa kuwafundisha watu wa familia zetu. Tunahakikisha kuwa kila mtu katika dari zetu anakuwa na maarifa ya msingi ili kupata wokovu. Ni wajibu wetu kuona kwamba wenzi na watoto wetu wamefundishwa mambo ambayo yanahusiana na amani ya milele. Panga, hasa katika siku ya Bwana, ili kwamba wote waweze kuhudhuria ibada kwa ajili ya mafundisho. Vile vile kuhakikisha kwamba wana muda wa kusoma Neno, kutafakari, na kuomba. Isipite siku yoyote pasipo familia kuomba kwa kumaanisha.

Kadhalika, unapaswa kujitahidi kuwafundisha watoto wako mapema, waziwazi, mara kwa mara na kwa uvumilivu. Mtoto anapoanza kuongea, unaweza kuwa na uhakika kwamba lengo la mafundisho linaanza kufanyiwa kazi kuanzia muda huo, usipoteze muda wa kusema mambo ya Mungu. Lakini ongea kwa uwazi, ukitumia maneno ambayo watoto wanaweza kuyaelewa-ambayo hutumiwa na watoto.

Fanya hivyo mara kwa mara, inua moyo wako kwa Mungu ili afungue ufahamu wao na kumimina nuru yake ndani yao. Lakini haya yote hayawezi kuwa na ufanisi bila kuvumilia. Kamwe usiache mpaka umeona matunda ya mafundisho yako kwa watoto. Kufanya hivi, unahitaji kuvikwa uweza kutoka juu. Pasipo hili, ninashawishika kusema, hakuna yeyote ambaye anaweza kuwa na utoshelevu wa uvumilivu kwa kazi hiyo.

 

Kujenga kwa maombi na Imani

 

“Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki”

Warumi 10: 10

 

Rafiki, chukua hatua zaidi, usiridhike na matendo mema: kuwalisha wenye njaa, kuwavika walio uchi, kuwatembelea yatima na wajane katika dhiki zao, au wagonjwa na hao wali magerezani, na wageni. Je, una hubiri kweli ya Yesu katika jina la Kristo? Je, ushawishi wa Roho Mtakatifu na nguvu za Mungu hukuwezesha kuwaleta wenye dhambi katika nuru, kuwatoa katika nguvu za shetani na kuwaleta katika nguvu za Mungu?

Kisha nenda na ujifunze ulichofundisha: kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani;… wala si kwa matendo…. Bali kwa rehema zake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa mara ya pili na (Waefeso 2:8, Tito 3:5)

Jifunze kuweka yote juu ya msalaba, huku ukihesabu yote uliyofanya kuwa ni uchafu na kinyesi. Kama unaamini, omba, bwana Oo niongezee imani. Au kama huna imani, omba nipe imani hii, ingawa imekuwa ni kama punje ya haradari. Ni imani tu iokoayo, imani ambayo hujenga juu ya mwamba, simama imara wakati mafuriko na upepo vinapovuma. Na hii imani iokoayo ndiyo hasa hudhihirika katika matendo mema ya haki.

 

Baba yako anajua

 

“Maana Baba yenu anajua mnayoyahitaji kabla ninyi hamjamwomba”.

Mathayo 6: 8

 

Katika maneno yake, kabla ya maneno hayo, Bwana wetu alikuwa akionya dhidi ya kurudia rudia. Kurudia maneno yeyote pasipo kumaanisha ni kurudia bure. Kwa hiyo, tunapaswa kuwa waangalifu katika maombi yote ili kumaanisha tunachosema na tunasema tu kile tunachomaanisha katika mioyo yetu.

Hii ni sababu ya msingi kwa nini wengi hukiri kidini, ni aibu. Hakika maneno yote katika ulimwengu si sawasawa na shauku takatifu. Maombi mazuri au yaliyo bora ni yale yanayotokana na maneno yanayorudiwa ambayo ni lugha ya Mungu ndani ya moyo wa mwamini.

“Na Baba yenu anajua yale mnayoyahitaji”. Hatuombi ili kumjulisha Mungu mahitaji yetu. Anayajua yote kama alivyo, hahitaji kujulishwa kitu chochote ambacho hakukijua hapo kabla. Na mara zote yuko tayari kutupatia mahitaji yetu. Kitu kikubwa tunachopungukiwa ni ili nafsi ya kupokea neema na Baraka zake. Na kusudi moja kuu la maombi ni kuonyesha hali ya kutokustahili ndani yetu ili kumtegemea Mungu, na kuongeza shauku ya vitu tuviombavyo, na kutufanya makini na mahitaji yetu ili tusije tukaacha kupambana mpaka tupate ushindi ili kupata Baraka zetu (Mwanzo 32:24- 30).

 

Kuomba ili kuondoa giza

 

“Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu, wala kuwahuzunisha”

Maombolezo 3: 33

 

Pamoja na sababu mbalimbali za hali ya jangwa, siwezi kuthubutu kupinga au kwenda kinyume na mapenzi ya Mungu kwa sababu yeye hufurahishwa na mafanikio ya watumishi wake na hapendi kuwahuzunisha au kuwatesa wanadamu. Mapenzi yake huleta utakaso katika maisha yetu, kamwe hapendi kuondoa vipawa katika maisha yetu. - (Warumi 11:29); kamwe hatuachi, kama baadhi wanavyosema bali sisi ndiyo tunaomwacha.

Sababu kuu na inayofahamika ya kuwa na giza ndani yetu ni dhambi za namna Fulani, pengine ya kutotenda tuliyopaswa, au kutenda tusiyopaswa.

Hii dhambi huwa na lengo la kutia giza katika nafsi ya mtu, hasa kwa ile dhambi inayojulikana, kwa makusudi; lakini mara kwa mara, nuru hutoweka ili kuipa nafsi dhambi ya kutotenda aliyopaswa mtu kutenda. Mara nyingi dhambi hii Roho Mtakatifu huiondoa kwa haraka, lakini ni kwa taratibu sana. Iwapo Kutokuwa na maombi ya faragha, au kuomba kwa kurashiarashia. Pengine inaweza kuwa ni dhambi ya kutotenda yaliyopaswa kutendwa. Upungufu huu hauwezi kutokana na njia nyingine; na matokeo yake ni uhai wa Mungu huanza kuoza na kutoweka kwa taratibu.

Kutokutenda kwa namna nyingine ambako kunaweza kuleta giza ndani ya nafsi ya mwamini ni kutokumkemea “jirani” tunapomwona amekosa lakini tunachukua dhambi kwa ajili yake - (Mambo ya walawi 19:17). Kwa kuacha kumrudi au kumuonya, tunaifanya dhambi yake kuwa yetu. Hivyo tunawajibika kwa hilo. Kwa sababu hiyo tumekuwa tukimhuzunisha Roho Mtakatifu, na kupoteza nuru ya mwangaza wa sura yake.

 

Maombi kama ya neema

 

“Lakini, kueni katika neema na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo”

2 Petro 3: 18

 

Njia kuu za neema ni maombi (yawe ya faragha au katika kusanyiko); kuchunguza maandiko (ambako hujumlisha kusoma, kusikiliza, na kutafakari Neno la Mungu); kushiriki meza ya Bwana (kula mkate na kunywa divai kwa kumbukumbu ya Bwana Yesu). Haya yanaaminika ni njia za kuleta maana yake katika nafsi zetu.

Ndivyo ilivyokuwa katika kanisa la kwanza, lakini kadri muda ulivyokuwa unaendelea upendo wa wengi ukapoa. Baadhi wakaanza kukosa kwa kutumia vibaya, na kuiweka dini kwa kufanya yale mambo yaliyoonekana kwa macho badala ya kufanya yale ambayo ni matokeo ya moyo uliofanywa upya katika sura ya Mungu. Sasa, uthamani wa njia hutegemea hasa utumishi wao wa kidini. Hivyo njia hizi zote-zinapoondolewa au kutengwa zinakuwa hazina maana. Ikiwa hazituleti au kutuongoza katika kumjua na kumpendeza Mungu hazikubaliki mbele za Mungu. Hazina tofauti na machukizo na uvundo katika pua zake. Huchoshwa nazo. Na zinapotumika ili kujaribu kutimiza matakwa ya kidini ambayo wanapaswa kuyatumikia, huugeuza mkono wa Mungu kinyume chao na kuuondoa ukristo nje ya moyo badala ya kuwa njia inayoingia ndani ya mioyo.

 

Kuomba rehema

 

“Si kwa katika uwezo wa yule atakaye, bali wa Yule arehemuye, yaani Mungu:

Warumi 9: 19

 

Wokovu kwa njia ya imani ni fundisho lisiloleta furaha kwa wale ambao hujihesabia haki - (self-righteousness). Shetani huongea kama alivyo bila (kweli au aibu) anapotamka kutokufurahishwa, kwa kuwa wokovu kwa njia ya imani ndiyo fundisho pekee lenye kufurahisha, limejaa faraja kweli, kwa wote walijiharibu maisha yao, na wanaojihukumu kwa dhambi zao, yeye amwaminiye hata aibika: na Bwana yule yule ni juu ya wote – ni tajiri kwa wote wamwitao. Hii ni faraja iliyo juu zaidi ya mbingu, yenye nguvu kuliko mauti!.

Kwa nini! Huwarehemu wote? Kwa zakayo, aliyekuwa mtoza ushuru kwa udanyanyifu? Kwa mariamu Magdalena, na kwa mwanamke mzinifu? Hivyo, mtu anaweza kusema, “Ni mimi, naweza kutarajia rehema zake!” Na wewe unaweza, uliyeteswa, usiyekuwa na mtu wa kukufariji Mungu hatayadharau maombi yako.

Labda anaweza kusema, sasa ijayo, “changamka, dhambi zako zimesamehewa” Umesamehewa kiasi kwamba hazitakutawala tena. Ndiyo, na Roho Mtakatifu atakushuhudia katika roho yako kwamba wewe ni mtoto wa Mungu.

Habari njema ya furaha ku iliyoletwa kwa watu wote! Kwake yeye aliye na kiu, njoo unywe maji; na wewe usiyekuwa na pesa, njoo, ununue, na ule - (Isaya 55:1). Dhambi zako zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu, ikiwa zitakuwa zaidi ya nywele au kichwa chako (idadi), mrudie Bwana, na atakurehemu; naye atakusamehe.

 

Maombi kupitia majaribu

 

“Basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu”

2 Petro 2: 9

 

Kama giza limesababisha majaribu mengi, mazito na yasiyo tarajiwa; njia pekee ya kuondoa na kuzuia ni kuwafundisha wakristo kutarajia majaribu wakati wowote. Wanaishi katika ulimwengu wenye uovu, katikati ya waovu, wenye roho za uchafu, na wenye mioyo ya kutenda uovu. Wanapaswa kushawishika kwamba kazi yake ya utakaso kwake si timilifu kwao, kama wanavyodhani; bali ni mchakato kupitia mambo hayo wanapoamini mara ya kwanza, kama watoto wachanga ambao hukua taratibu. Wanapaswa kutarajia dhoruba nyingi kabla ya kufikia utimilifu wa kimo cha kikristo.

Zaidi ya yote wafundishwe, dhoruba hii inapokuwa juu yao, hawapaswi kutafakari pamoja na shetani bali ni kuomba. Na wamimine mioyo yao kwa Mungu na kumwonyesha shida zao. Watu wa jinsi hii wanapaswa kutumia ahadi kuu na za thamani. Siyo kwa wajinga, mpaka ujinga utakapoondolewa.

Kwa wale waliojaribiwa, tunaweza kutangaza wema wa Mungu wetu. Unategemeana na uaminifu na nguvu zake katika damu iliyomwagika kwa ajili yetu ili kutusafisha dhambi zetu. Mungu atalishuhudia neon lake na kuwatoa katika shida zao. Atasema, “Amka, uangaze; kwa maana nuru yako imekuangazia”. Hakika, hiyo nuru, ikiwa utatembea kwa unyenyekevu na kuwa na Mungu, itakuangazia zaidi katika siku kamilifu (Ona Mithali 4:18).

 

Maombezi ya Yesu kwa ajili yetu

 

“Na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa Imani”

Waebrania 10:22

 

Kwa hiyo imani katika maisha, kufa na maombezi kwa ajili yetu tunazidi kufanywa upya kila mara, na tunazidi kufanywa weupe na safi. Siyo tu kwamba hatuhukumiwi, lakini pia hakuna adhabu mbaya kama ilivyokuwa hapo kwanza, Bwana akitusafisha mioyo yetu na maisha yetu.

Kwa imani hiyo hiyo, tunahisi nguvu ya Kristo ikiwa juu yetu kila wakati, ambayo kwa hiyo tuko kama tulivyo leo. Kwa hii imani pekee, tunawezeshwa kuendelea katika maisha ya kiroho. Na pasipo hiyo, bila kujali utakatifu wetu wa sasa, tungepaswa kuwa mashetani muda mchache ujao.

Maadam tumewaka imani yetu kwake, tunateka maji kutoka katika visima vya wokovu. Tunamtegemea mpendwa wetu, Kristo ambaye ni tumaini la utukufu wetu, ambaye hukaa ndani ya mioyo yetu kwa imani.

Kadhalika yeye anaendelea kufanya maombezi kwa ajili yetu ikiwa mkono wa kuume wa Mungu; tunapokea msaada kutoka kwake ili kufikiri, kuongea, na kutenda au kufanya yote yanayopaswa mbele ya macho yake.

Yeye hututangulia katika yote tuyatendayo, ili kuomba mtindo, maisha, mazungumzo na matendo yalioanza, yaliyoendelea na yaishie katika yeye. Yeye pia husafisha mawazo ya mioyo yetu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu, ili tuweze kumpenda kikamilifu, na kwa kumhimidi kwa kumstahi kupitia jina lake Takatifu.

 

Je, tunapaswa kumngoja kwa namna gani?

 

“Mtafuteni Bwana, maadam anapatikana, mwiteni maadam, yu karibu?

Isaya 55: 6

 

Fikiri mtu amejua wokovu ni kipawa na ni kazi ya Mungu, na akafikiri baadaye kwamba ameshawishika pia kwamba hana kipawa, je, anawezaje kukipata?

Kama ukisema, “Amini, na utaokoka” wajibu, “kweli, lakini je, nitaamini namna gani” Unawajibu, “mngoje Bwana”.

“Vema, lakini ninapaswa kumngoja Bwana jinsi gani? Ukitumia njia ya neema, au hapana? Je, ninapaswa kuingoja neema ya Mungu, ambayo huleta wokovu, kwa kutumia njia ya neema, au kwa kuitupia mbali neema, au kwa kuitupia mbali neema hiyo?”

Haiingiliki akilini kwamba neno la Mungu haliwezi ktuoa maelekezo katika suala muhimu kama hili au kwamba mwana wa Mungu, ambaye alikuja kutoka mbinguni kwa ajili yetu na kwa ajili ya wokovu wetu, anaweza kuwa ametuacha bila maelekezo hasa kuhusu wokovu unaotuhusu.

Na ki urahisi, hakutuacha pasipo maelekezo; ametuonyesha njia ambayo tunapaswa kuiendea. Tunapaswa kulisoma Neno la Mungu. Na kuuliza kwa kutafuta kilichoandikwa. Tukifanikiwa kukua katika hicho, hakuna shaka litakalosalia ndani yetu.

Kwa mujibu wa maandiko matakatifu, wote wenye shauku na neema ya Mungu wanapaswa kuingoja kwa kupitia njia ambazo Mungu ameziandaa – kwa kuzitumia, na siyo kuziweka mbali, maombi,  kusikiliza, kusoma, na kutafakari maandiko; na kushiriki meza ya Bwana.

 

Upendo katika moyo

 

“Pendo la Mungu limemiminwa ndani ya mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi”

Warumi 5: 5

 

Alama ya tatu ki maandiko ya wale waliozaliwa mara ya pili, na ambayo ni kuu kuliko zote, ni upendo. Ni upendo wa Mungu, ambao umemiminwa ndani ya mioyo yetu na Roho Mtakatifu tunapozaliwa mara ya pili na roho wa Mungu. “Kwa sababu ninyi ni wana”. Mtakatifu Paulo aliwaandikia Wagalatia, “Mungu alimtuma Roho wa mwanaye mioyoni mwetu, aliyae “Abba, yaani Baba” - (Wagalatia 4:6) kwa njia ya huyo Roho, wanamwangalia Mungu kwa bidii kama mpatanishi wa Baba mpendwa.

Wanamlilia kwa ajili ya (riziki) mkate wa kila siku, kwa ajili ya mahitaji yote yawe ni ya kiroho nay a kimwili. Wanamimina mioyo yao kwa dhati mbele ya Bwana Mungu, wakijua kwamba wanazo haja wamwombazo - (Ona 1 Yohana 5:14-15) furaha yao ni katika yeye; ni furaha ya mioyo yao. Shauku ya nafsi zao ni kumwendea yeye; kufanya mapenzi yake huleta utoshelevu mkuu ndani yao. Wanampenda Mungu kama mwokozi wao. Wanampenda Yesu Kristo kwa dhati; wameungwa na Bwana na kuwa roho mmoja. Nafsi zao zinamtegemea Bwana Yesu na humkubali yeye ni mkuu miongoni mwa maelfu. Wanajua kile alichokiandika mwandishi wa Zaburi kina maana gani; wewe mzuri sana kuliko wanadamu; Neema imemiminwa midomoni mwako - (Zaburi 45:2).

 

Mungu ni mtoaji

 

“Kila kutoa kuliko kwema na kitolewacho kilichokamilika ….. hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga”

Yakobo 1: 17

 

Ni kweli kwamba dini kwa nje haina thamani (maana) pasipo na dini ndani ya moyo; “Mungu ni Roho; na hao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli” - (Yohana 4:24). Kwa hiyo ibada ya nje ni kazi bure pasipo moyo uliojitoa kwa Mungu. Maagizo ya Mungu katika mambo ya nje huwa na hatua na thamani ikiwa yatakuwa yalianzia ndani katika utakatifu. Lakini hayakuanzia ndani (badiliko) hayana faidia na utupu. Ikiwa yatatumika katika nafsi inayopaswa kutumiwa na mambo ya ndani ya roho ya mwanadamu, mambo hayo ni chukizo.

Njia zote kwa nje bila kujali ni zipi ikiwa ziko mbali na Roho Mtakatifu haziwezi kuwa na faida kabisa, haziwezi kutuongoza kumjua au kumpendeza Mungu. Pasipo utata, msaada unaofanyika juu ya uso wan chi, anafanya yeye mwenyewe. Ni yeye pekee ambaye, kwa nguvu zake kuu, anatenda ndani yetu yanayompendeza mbele zake. Mambo yote ya nje, Mungu asipotenda ndani yako, yana hali ya kawaida na yaliyodhaifu. Tunajua kwamba hakuna nguvu ya kawaida katika maneno yatumikayo katika sala katika kusoma maandiko, katika mkate na divai inayopokelewa katika ushirika wa meza ya Bwana. Ni Mungu pekee ambaye hutoa kila kilicho chema, na mwanzilishi wa neema. Nguvu zote ni zake, na kwa hiyo kupitia chochote – kati ya hivi, kuna Baraka yoyote ambayo huachiliwa ndani yetu.

 

Maombi ya ahadi za Mungu.

 

“Ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mnahuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali”.

1 Perto 1: 6

 

Wakati wa magonjwa na maumivu, shetani hutusonga sana kwa nguvu zote, “Je, Mungu hasemi, ‘pasipo utakatifu hakuna mtu atakaye muona Bwana”’, unajua utakatifu ni utimilifu wa sura ya Mungu, na jinsi jambo hili lilivyo mbali na macho yako! Huwezi kuingia katika hali ya utakatifu huu. Umeteseka katika mambo yote bure. Na bado upo katika dhambi zako, na hatimaye lazima utaangami”.

Ikiwa macho yako hayakumwangalia yeye (Bwana) aliyezibeba dhambi zako zote, shetani atakuleta tena chini ya hofu ya kifo ambamo uliwahi kuwa katika utumwa kwa njia hii hudhoofisha, kama siyo kukuharibu kabisa, Amani na furaha yako katika Bwana. Sasa amani ya Mungu ndani ndiyo njia ya thamani ya kuendelea katika siura ya Mungu. Kuna msaada kidogo kutuleta katika utakatifu kuliko huu-ufahamu, na roho iliyomwelekea mungu, kupata pumziko katika damu ya Yesu.

Pasipo hii, ni shida kukua katika neema na katika kumjua Bwana wetu Yesu Kristo. Kwa hiyo, shika sana mwanzo wa ujasiri ulioimarika mpaka mwiso. Bila shaka utapokea ahadi ya Mungu, kwa wakati huu na kwa ajili ya umilele. Usijisumbue kwa lolote. Pia mahitaji yako yajulikane bila shaka au hofu, lakini kwa shukurani kwake yeye aliyeahidi ahadi hizi zote (Angalia Wafilipi 4:6)..

 

Ninyi kwa ujumla

 

‘Mungu kwa amani mwenyewe awatakase kabisa”.

1Thesalonike 5: 23

 

Mungu wa amani hutakasa kwa kutumia amani ambayo huitumia kutenda kazi ndani yetu, ambayo ni njia kuu ya utakaso. Neno lililotumika katika tafsiri ya asili linamaana, ‘kwa ujumla na kikamilifu” - kila sehemu na yote yanayohusiana nasi “Ujumla wenu” Mtume anaendelea, “roho na nafsi ya mwili” mhifadhiwe mwe kamili bila lawama” Anaonyesha kwamba alitaka hali yao ya kiroho ihifadhiwe kikamilifu, vile vile akiwa na shauku kuona afya ya hali yao ya asili.

Ili kuelezea hili zaidi: nafsi na mwili pekee ni sehemu za asili ya kibinadamu lakini kipawa cha Ki-Mungu, kinachopatikana ndanai ya wakristo pekee. Ili kuwatia moyo wakristo wa Thesalonike, Mtakatifu Paulo aliongeza “yeye aliyewaita, ni mwaminifu, naye atafanya’ (Mstari 24); Ikiwa hamtazimisha Roho, ambaye kwa yeye alikuwa ameandika kusudi lake (Mstari 19). Mahali popote alipo Roho amani hii huwepo. Huwepo katika pendo takatifu, katika furaha, katika maombi; na shukurani.

Oh, usimzimishe, kwa kumwacha pembeni, au kwa kukataa, kutenda mema, au kwa kutenda ouvu! Kama njia kuu ya kujiepusha na hili, aliondoka. “furahini siku zote; omba bila kukoma; shukuruni kwa kija jambo” Onyo la Baraka, hata katika siku zetu!

 

Je, hasira yako ya ndani ni ipi?

 

“Kwamba watubu…. wakiyatenda matendo yanayopatana na kutubu kwao”

Matendo 26: 20

 

Kama dhamiri ya waaminio iko hai, dhambi kiasi gani hutamani matendo yao? Matendo yao siyo kwa ajili ya utukufu wa Mungu; na mara kwa mara hawakukusudia kutenda kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Wengi hufanya mapenzi yao wenyewe na wakitafuta kujipendeza wenyewe kama siyo kumpendeza Mungu.

Wakati wakijitahidi kutenda wema kwa jirani yao, je, hawajisikii hisia za hasira ya namna Fulani? Hata hivyo, matendo yao mema, mambo yao ya rehema yamechafuliwa na mchanganyiko wa uovu. Je, si suala hilo hilo wanapokuwa wakitoa sadaka ya maombi kwa Mungu, katika mkusanyiko au katika faragha, au kujiingiza katika huduma muhimu? Je, mioyo yao mara zote haitangitangi kuelekea miisho ya dunia?

Tena, dhambi ngapi za kutotenda waliyopaswa kuyatenda zinazowahukumu! Tunajua maneno ya mtume Yakobo, “Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi”. - (Angalia Yakobo 4:17). Je, hawaoni kupungukiwa au kutowepo kwa upendo ndani yao, na hasira takatifu, na makosa mengine ya ndani yasiyokuwa na idadi; ili kwamba walie pamoja na Ayubu, “kwa sababu hiyo najichukia nafsi yangu, na kutubu katika maumivu na majivu”. (Ayubu 42:6).

 

Maombi na kujikana mwenyewe

 

“Na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku anifuate”

Luka 9: 23

 

Ufahamu wa neema ya Bwana wetu katika meno haya ni wa muhimu sana. Kila hatua ya maisha ya kiroho, kuna aina mbalimbali za vizingiti vinavyozuia kupata neema na kukua katika neema hiyo. Hata hivyo, yote yanategemeana na mjumuisho wa maneno hayo: kutokujikana wenyewe, au  kutokuibeba msalaba wetu.

Hili suala ambalo hupigwa sana na maadui wengi na wenye nguvu. Asili zetu huinuka kinyume na kweli hii. Wala ambao huchukua asili kuliko neema kwa ajili ya mwongozo huiharibu  kweli hili; Adui mkubwa wa nafsi zetu anajua fika umuhimu wake na mweka kikwazo dhidi ya kweli ya kujikana na kuubeba msalaba.

Hata wale ambao kwa kiasi Fulani wameitikisa na kuiharibu nira ya shetani na kupata ujuzi wa neema ndani ya mioyo yao si marafiki wa hili fundisho la kikristo. Ijapokuwa limesisitizwa kwa upekee na Bwana wao, baadhi yao ni wajinga kabisa kana kwamba hakukuwepo na neno kama hilo katika Biblia.

Wengine huendelea katika hali ya kutokufahamu na hivyo kuwa kinyume na kweli hii ya kujikana na kubeba msalaba. Hueleza fundisho la kujikana na kubeba msalaba katika namna na sura mbalimbali. Huliita fundisho hili “kuutafuta wokovu kwa matendo au kutafuta kujithibitisha sisi wenyewe”. Uko katika hatari endelevu ya kunyanyaswa, au kuwa mjinga wa fundisho hili muhimu la Injili. Maombi yenye  bidii yakutangulie, yakiambatana na kufuata kile ambacho anatarajia.

 

Mungu anafanya mambo makuu

 

“Kwa sababu hiyo, msiwe wajinga, bali mfahamu nini yaliyo mapenzi ya Bwana”.

Waefeso 5: 17

 

Ufalme wa mbinguni kwa ndani hukaa ndani ya mioyo ya wote waliotubu na kuamini injili, ni haki, amani na furaha katika Roho Mtakatifu. Lakini hayo matunda au matokeo tu. Wakati hizi Baraka zinapokuwa kwa uchache, hata hivyo bado tunategemea kuona makuu zaidi.

Tunategemea kumpenda Bwana Mungu wetu siyo tu kama tunavyofanya sasa, kwa udhaifu ingawa kwa uthabiti wa moyo, bali kwa mioyo yetu yote, akili zetu zote, nafsi zetu zote na nguvu zetu zote. Ni kweli tunatarajia kufanywa kamili katika Upendo” (1Yohana 4:18). Tunatafuta nguvu ili tufurahi siku zote, kuomba bila kukoma, kutoa shukurani kwa kila jambo. Tunaamini kwamba ile nia iliyokuwepo ndani ya Kristo itakuwa ndani yetu pia (Angalia Wafilipi 2:5) Na tunatarajia kutakaswa kutoka katika sanamu zote na kuokolewa kutoka katika uchafu wetu wote wa ndani wan je pia (Angalia Ezekieli 36:29) - ili kutakaswa, kama yeye alivyo Mtakatifu.

Tunatafuta ongezeko la jinsi hiyo katika ujuzi wa kumjua na kumpenda Mungu mwokozi wetu ili atuwezeshe kutembea katika nuru wakati wote kama yeye alivyo katika nuru. Tunatumaini katika ahadi zake yeye asiyeweza kusema uongo kwamba wakati utafika ambapo yote tunayotenda  yatakuwa yakitendeka kwa ajili ya utukufu wa Mungu Lengo la shetani katika kuharibu ni kuharibu kazi ya Mungu ndani ya nafsi zetu, au kuzuia ongezeko lake, kwa taraja letu katika hiyo kazi kubwa. Hata hivyo kuna njia ya kudhibiti hiyo mishale na kuinuka juu zaidi dhidi ya kile alichokikusidia ili kutuangusha.

 

Njia za wokovu.

 

“Wakati wa usiku nimelikumbuka jina lako, Ee bwana, nikaitii sheria yako’

Zaburi 119: 55.

 

Tayari imegundulika kwamba kuna utaratibu ambao katika huo Mungu kwa ujumla amependezwa kutumia njia hizi katika kuwaleta wenye dhambi kwake. Japokuwa hatupati amri katika maandiko Matakatifu kwa ugunduzi uliofanyika. Njia za jinsi watu tofauti walivyoongozwa, na jinsi walivyopata Baraka za Mungu, zinatofautiana kiviwango, na njia hizi zikiwa na utofauti mara maelfu.

Hata hivyo hekima yetu ni kufuata uognozi wa ki-ungu na Roho wake zaidi sana kama jinsi njia zilivyo ni sisi wenyewe kutafuta neema ya Mungu. Kwa sababu yeye hutuongoza kwa sehemu kupitia Uungu wake kwa nje, na hutupa nafsi wakati mwingine njia moja, na wakati mwingine njia nyingine na kwa sehemu kupitia uzoefu wetu na Roho wake hupendezwa sana kufanya kazi ndani yetu.

Katika wakati huo huo, kwa hakika na kuhitimisha jumla, wote ambao huugua kwa ajili ya wokovu wa Mungu ni hili nafsi inapotokea, tumia njia zote ambazo Mungu aliweka wakfu, kwani ni nani ajuaye ni kupitia njia ipi katika njia za Mungu ametupa, atakutana na wewe kwa neema iletayo wokovu?

 

Kumngoja Mungu

 

“Kwamba kwa Bwana …. Miaka elfu ni kama siku moja”

2 Petro 3: 8

 

Kama tutashikilia kwa bidii; “Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka… Yesu Kristo” na “Nimehesabiwa haki bure kwa neema”, bado shetani anahoji, “Lakini mti hutambulikana kwa matunda yake; je, una matunda ya haki? Je, nia uliyonayo ndivyo ilivyokuwa ndani ya Yesu Kristo? Je, umekufa kwa habari ya dhambi na kwamba uko hai katika haki?

Na kisha, tukilinganisha matunda madogo tunayoyaishi ndani ya nafsi zetu pamoja na utimilifu wa ahadi: tutakuwa tayari kuhitimisha, “Hakika Mungu hajasema kwamba dhambi zangu zimesamehewa. Hakika, sijapokea msamaha wa dhambi zangu, je, nina fungu gani miongoni mwa hao waliotakaswa?

Lakini fugnu hili katika shingo yako; uziandike juu ya moyo wako; “Nimekubaliwa mbele za Mungu, kwa haki ya Mungu kwa imani; uwe na shauku zaidi ya neema ya Mungu kama alivyofanya yeye katika kumtoa mwanae wa pekee, kwa ulimwengu, ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele (angalia Yohana 3:16). Ndipo amani ya Mungu itakapoanza kutiririka, licha ya milima uovu. Itakuwa tambarare wakati wa mchana bwana atakapokuja kuchukua nafsi na kutawa moyo wako. Bwana hawezi kukosa muda wa kutimiza kazi ambayo ilipaswa kutimizwa ndani ya nafsi yako. Muda-wakati wake ni wakati sahihi zaidi. Kwa hiyo, mwambie na umtumaini yeye, kwa sababu huwezi kuzuia chochote kwako ambacho ni chema.

 

Kazi ya wito wako

 

“Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika”

 

Yohana 6:27

 

Je, ni kwa kusudi gani unafanya na kufuata kazi au shughuli za kidunia? “Ili kupata mambo au mahitaji muhimu kwa ajili yako na familia pia”. Jibu lenye utoshelevu “kwa kadri linavyoendelea, lakini haliwezi kufika mbali hasa kwa mkristo lazima twende zaidi ya hapo tena. Kusudi letu katika mambo yote ni kumpendeza Mungu, kutofanya mapenzi yetu bali kufanya mapenzi ya Mungu hapa duniani kama malaika wa navyofanya mbinguni. Tunafanyia kazi kile kinachodumu hata milele.

Tena, ni kwa jinsi gani tunafanya shughuli zetu za kidunia (ki maisha)? Ninaimani kwa bidii yote, kwa nguvu zako zote. Na kwa haki: tukiyafanya yote kwa wakati wake katika kila mazingira. Na katika rehema; tukifanya kila mmoja, kama ipasavyo na ndivyo watakavyotufanyia. Lakini wakristo wameitwa kwenda zaidi ya hapo: kuongoza huruma katika haki; kuchanganya  na maombi –  maombi ya moyo – katika kazi zote za mkono yao. Pasipo hii juhudi yote na haki inawaonyesha kuwa waaminifu. Lazima tutembee “katika njia iliyo bora zaidi” - kuliko waaminifu wapagani.

Ni “roho” gani ambayo unatenda kazi kwayo? Je, ni katika roho ya dunia au Roho wa Kristo? Kama unatenda katika roho wa Kristo; unafanya yote katika roho ya dhabihu, ukitoa mapenzi yako katika mapenzi ya Mungu. Utaendelea kukusudia, bila ya kusita, au kutaka fahari; au kuwa tajiri wa chochote zaidi ya utukufu wa Mungu. Hii ni njia iliyo bora zaidi ya kufuatilia shughuli zetu za kila siku hapa duniani.

 

Kuulilia wema wa Mungu

 

“Tuzidi katika dhambi ili neema izidi, La hasha!”

Warumi 6: 1-2.

 

Inaweza kuwa baadhi hawapendi kuzungumzia rehema za Mungu zinazo okoa na kutuhesabia haki bure kwa imani kwa sababu wanaamini kwamba zinatia watu moyo kuendelea katika dhambi: kweli,  inawezekana pengine! Wengi wataendelea kutenda dhambi ili neema izidi, lakini damu yao iko juu ya vichwa vyao wenyewe. Wema wa Mungu unapaswa kuwaongoza katika toba, na hivyo huwa kwa wale walio na moyo mnyoofu. Wale wamtafutao Bwana kwa bidii wanajua kwamba kuna msamaha kwa Mungu, hulia kwa sauti ili dhambi zao ziweze kusamehewa pia, kupitia imani iliyo katika Yesu.

Kama watalia kwa bidii pasipo kuzimia, ikiwa watamtafuta kwa njia zote alizoziweka, ikiwa watakataa kufarijiwa, mpaka amekuja, atakuja, na hata kaa (Waebrania 10:37). Na ataweza kufanya kazi kubwa kwa muda mfupi, Matendo ya mitume imerekodi mifano mingi ya utendaji wa ki Mungu kwa imani ndani ya wanadamu, kama mwangaza kutoka mbinguni. Wakati huo huo Paulo na Sila walipoanza kuhubiri, askari alitubu, aliamini, na akabatizwa. Ndivyo ilivyo tokea kwa watu elfu tatu katika siku ya Pentecoste ambapo walitubu na kuamini, wakati Petro, Mtume akihubiri kwa mara kwanza. Na, abarikiwe Mungu, kuna uthibitisho wa kutosha kuwa Mungu, “hodari katika kuokoa”.

 

Kumtafuta Bwana na utii

 

“Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu”

1Samweli 15: 22

 

Kifungu kingine ambamo maelezo, “simama imara” yameonekana yakisomeka: “wakaja watu waliomwambia Yehoshaphati, wanakuja jamii kubwa juu yako watokeao Shamu, ng’ambo ya Bahari … Yehoshaphati akaogopa, akauelekeza uso wake amtatute Bwana; akatangaza mbiu ya watu kufunga katika Yuda yote, Yuda wakakusanyika wote ili wamtafute Bwana; hata kutoka miji yote ya Yuda wakaja kumtafuta Bwana. Yehoshaphati akasimama katika kusanyiko … nyumbani mwa Bwana… ndipo Roho ya Bwana akaja juu ya Yahazaeli, … akasema, Sikieni ... hivi ndivyo asemavyo Bwana kwenu, 2 Nyakati 20:2-23.

Huo ndiyo wokovu ambao wana wa Yuda waliuona. Walitii, Waliimba na walimsifu Bwana. Ni kwa namna gani yote haya yanathibitisha kwamba hatupaswi kuongoja neema ya Mungu katika njia ambayo ameiweka.

 

Kuutunza (kuujali) mwili

 

“Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu”

1 Wakoritho 10: 31

 

Hizi “nyumba za udongo” ambazo huhifadhi roho zetu zinahitaji fidia au utunzaji, au vinginevyo itatoweka mapema kabla ya wakati wake. Chakula cha kila siku ni muhimu kuzuia vifo vya ghafla au vya mapema. Kabla ya wakati ili kurekebisha uharibifu wa mwili. Ilikuwa ni desturi katika ulimwengu wa kipagani; walipokaribia kila chakula, wangemwaga kiasi kidogo cha kinywaji kama ishara ya heshima kwa Mungu wao (ijapokuwa mungu wa kipagani alikuwa ni shetani – 1 Wakorintho 10:19 – 21). Ilikuwa ni jambo la kawaida – kidesturi katika nchi hii. Je, isingekuwa ni njia iliyo bora zaidi kama kila kiongozi wa familia angeomba Baraka kutoka kwa Mungu juu kila ambacho walitaka kukila na kurudisha shukurani kwa mtoaji wa Baraka?

Kama ilivyo kwa wingi vyakula, baadhi ya watu hawali kupita kiasi; ili wasije wakajiletea madhara kupitia vyakula. Kama ilivyo desturi ya ulaji, wakati wote hakina tatizo, kuchanganya na vinywaji ambavyo inasemekana kwamba husaidia uyeyushaji wa chakula. Maadamu itakuwa ni kiasi kidogo, ubora wa chakula ambao husaidia kuleta afya ya mwili na akili. Inasemekana kwamba, njaa ni kichocheo cha hamu ya chakula lakini pia njaa inayotosheleza huleta au kisababisho cha uchangamfu wenye shukurani, na chakula kinacholiwa au kupatikana na wakati wake kunafaa.

 

Uimbe upendo wake

 

“…. Asema Bwana. Nitawapa sheria zangu katika nia zao, na katika mioyo yao nitaziandika; … na dhambi zao sitazikumbuka tena”

Waebrania 8: 10, 12

 

Baada ya kutumia miongoni mwa njia hizi za neema, uwe mwangalifu na jinsi unavyojitathimini mwenyewe, jinsi unavyojipongeza baada ya kufanya mambo makuu. Hii ni kugeuza yote kuwa sumu. Sababu ya ukombozi wetu siyo matendo yetu au haki yetu lakini ni wema na upendo wa Mungu mwokozi wetu …. Sawa sawa na rehema zake … ili tuwe warithi wa uzima wa milele (angalia Tito 3:4-7) kwa muda Fulani, fikiri, kama Mungu hakuwepo, kutumia njia hizi kuna faida gani? Je, siongezi dhambi juu ya dhambi?

Ee, Bwana, niokoe, vinginevyo nitaangamia! Usinihesabie dhambi hizi! “Kama Mungu alikuwepo pale, kama upendo wake uliingia ndani ya moyo wako, tayari umekwisha sahau matendo ya nje. Unaona, unajua, unahisi, Mungu ni yote katika yote. Shuka mbele zake, mpe sifa zote. Mungu atukuzwe katika mambo yote, kupitia Kristo Yesu. Lia kutokea ndani ya moyo wako, “fadhili za Bwana nitaziimba milele, kwa kinywa changu nitavijulisha vizuri nyote uaminifu wako” - (Angalia Zaburi 89:1 na Zaburi 100:5).

 

Kuomba Neema

 

“Ee Bwana unifundishe njia yako, na kuniongoza katika njia iliyonyoka”

Zaburi 27: 11

 

Kwa kuangalia utaratibu ambao Mungu huutumia ili kumwongoza mwenye dhambi, tunaweza kujifunza ni njia ipi tunaweza kupendekeza kwa mtu yeyote. Kama kitu chochote kinaweza kumfikia mwenye dhambi asiyejali, inaweza kuwa kusikiliza au kuwasiliana, kama aliwahi kuwa na wazo kuhusu wokovu. Kwa mwingine ambaye huanza kuhisi uzito wa dhambi: siyo, kwa kusikiliza neno la Mungu tu bali kwa kusoma pia, na pengine vitabu Fulani, inaweza kuwa njia ya kuonyesha jinsi alivyoshawishiwa na Roho Mtakatifu. Anaweza kushauriwa kutafakari alichosoma ili kiweze kuwa na uzito katika moyo wake. Tukisema ukweli, hasa kwa wale ambao wako katika hali hiyo hiyo. Wakati shida na uzito unapomshika, anapaswa kuumimina moyo wake kwa bidii mbele za Bwana, na hasa hasa kuomba bila kukata tamaaa. Na ikiwa hatajisikia hali ya kutoona uthamani wa maombi yake, mkumbushe.

Aende katika nyumba ya Bwana ili aombe pamoja na wale wamchao Bwana. Lakini anafanya hivi ili neno la Bwana wake litakumbushiwa kushiriki meza ya Bwana. Tunapaswa kuendelea zaidi kwa Roho wa Baraka, anayeongozwa na hatua kwa hatua, kupitia njia zote ambazo Mungu aliziweka (aliziandaa) - si sawa sawa na mapenzi yetu, lakini kama Mungu na Roho wa Mungu anavyotangulia na kufungua njia.

 

Kutunza hali ya kuzaliwa kiroho

 

“Kadhalika aliyezaliwa kwa Roho”

Yohana 3: 8

 

Mtu anapozaliwa na Mungu, huzaliwa na Roho, ndiyo hata namna  ya kuishi kwake inabadilika! Utu wake wa ndani unaanza kuwasiliana na Mungu, na anaweza kusema kwa hakika katika ujuzi “uko kando ya kutenda, na kando ya njia yangu”. Roho au pumzi ya Mungu inaivuvia nafsi ya mtu na kuifanya kuwa kiumbe kipya. Na pumzi hiyo hiyo ambayo hutoka kwa Mungu, hurudi kwa Mungu tena. Kama jinsi inavyopokelewa njia ya imani, vivyo hivyo hurejeshwa kwa njia ya upendo, maombi, sifa na shukurani. Upendo, maombi, na sifa ni pumzi ya kila nafsi ambayo imezaliwa kweli kweli. Kwa kupitia hivyo, maisha ya kiroho hayahuishwi tu, bali hongezeka siku kwa siku.

Macho ya moyo wake yako wazi sasa, kumwona yeye ambaye haonekani. Anaweza kutambua upendo wa msamaha wa Mungu. Kumwelekea yeye na ahadi zake zilizo kuu na za thamani. Masikio yake sasa yako wazi, sauti ya Mungu haiiti bure. Anajua sauti ya Mchungaji wake – anasikia na kutiii wito wa mbinguni.

Hisia zake za kiroho zimeamshwa, (He has the clear communication with the invisible world). Sasa anajua jinsi ambavyo amani ya Mungu ilivyo: furaha katika Roho Mtakatifu na upendo wa Mungu unaomiminwa ndani ya mioyo yao waaminio. Utaji umeondolewa; hakuna chochote katika nafsi isipokuwa nuru, maarifa na upendo wa Mungu.

 

Kwa ujumla Mkristo: Ni upendo wa Mungu

 

“Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wote”

Mathayo 22: 37

 

Kwa mara nyingine tunakuja katika suala linalomwelezea mkristo kwa ujumla. Kwanza, upendo wa Mungu. Neno lake linasema: ”utampenda Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, Kwa akili zako zote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote.” (Marko 12:30) Upendo huu hujaa ndani ya moyo wote, na hutawala hisia za moyo wote, hujaza uwezo wote wa nafsi, na maeneo mengine yote ya binadamu.

Yeye apendaye huendelea kufurahia upendo katika Mungu, furaha yake iko katika Mungu, Bwana wake na yote yanayohusiana na Mungu, kwa huyu hutoa shukurani katika kila Jambo. Shauku zake zote ni za kumwelekea Mungu na kwa kumbukumbu jina lake. Moyo wake hulia; Nani aliye katika mbingu ila wewe na hakuna duniani nimwoneae shauku zaidi yako”.

Hakika, ni nini aweza kukionea shauku ila Mungu? Siyo ulimwengu, kwa mambo ya ulimwengu na ulimwengu umesulubiwa kuhusu yeye. Amesulubiwa katika shauku za mambo ya mwilini, shauku (tamaaa) za macho, na kiburi cha uzima. Amekufa na kila aina ya kiburi: kwa kuwa “Upendo haujivumi” Akaaye katika pendo, hukaa katika Mungu, na Mungu hukaa ndani yake, na yeye si kitu machoni pake mwenyewe, kwa kuwa upendo wa Mungu ni alama ya jumla ya mkristo.

 

Hesabu ya maombi.

 

“Si kila aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa Mbinguni”

Mathayo 7: 21

 

Maelezo ya Bwana wetu katika kifungu hiki yanamaanisha (kuanzia katika hali ya chini) maneno yote mazuri, matendo yote ya kidini. Inajumlisha imani yoyote tuikiriyo, ukiri wa imani tuipokeayo, idadi ya maombi tuyarudiayo, shukurani tunazozisoma au kumwambia Mungu.

Tunaweza kulitaja au kulitamka vema jina lake na kutangaza wema wake kwa watu wote. Tunaweza kutamka (kuzungumza) matendo yake makuu ya kuwaeleza wokovu wake siku kwa siku.

Tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni, tunaweza kuonyesha maana ya neno la Mungu. Tunaweza kuelezea siri ya ufalme ambao ulifichwa tangu mwanzo wa ulimwengu.

Tunaweza kunena kwa lugha za malaika kuliko za wanadamu kuhusu mafumbo ya Mungu. Tunaweza kutangaza kwa wenye dhambi, “Tazama, mwana kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” - (Yohana 1:29).

Ndiyo, na tunaweza kufanya hili kwa kadiri ya nguvu za Mungu na udhihirisho wa Roho Mtakatifu, ili kuweza kuokoa nafsi nyingi katika mauti na kusitiri wingi wa dhambi.

Hata hivy inawezekana, yote haya yasiwepo zaidi ya kusema, “Bwana, Bwana,” Ninaweza nikahubiri kwa mafanikio makubwa na kunyakua nafsi nyingi katika moto, na bado nikadondokea hapo baada ya kufanya yote. Mungu na aturehemu sote.

 

Kuomba kwa ajili ya wokovu

 

“Maagizo ya Bwana ni ya adili, hufurahisha moyo”

Zaburi 19: 8

 

Kuna aina Fulani ya utaratibu ambao Mungu mwenywe hupendezwa kuutumia ili kumleta mwenye dhambi katika kupata wokovu. Mtu anaweza kuenenda katika hali ya kutokujua katika njia. Na Mungu huja kwake bila yeye kuelewa – kwa kutumia ujumbe wa kumwamsha au mazugumzo, na hali Fulani ya ki Mungu au kushawishiwa na Roho wake bila njia yoyote ya kawaida. Kisha huanza kuwa na shauku ya kukimbia ghadhabu ya Mungu, kwa kusudi kuendelea kusikiliza jinsi itakavyofanyika. Akipata mhubiri ambaye anongea na moyo wake, anastaajabu na anaanza kuchunguza maandiko.

Kwa kadiri anavyosikia na kusoma, ndivyo anavyozidi kushawishiwa, ndiyo anavyozidi kutafakari mchana na usiku. Kwa njia hizi, mishale ya ushawishi na Roho mtakatifu inazidi kuzama ndani ya nafsi yake. Huanza kuongea vitu kuhusu Mungu na kuomwomba Mungu kwa hakika akijua anachopaswa kusema. Labda ni katika “kuugua kusikoweza kutamkwa’, labda kuwa na shaka kama Mungu aliye juu atamsikia kama alivyo. Anakwenda kuomba pamoja na hao wanaomjua Mungu, katika kusanyiko. Anawaona wengine wakishiriki meza ya Bwana. Anafikiri “Kristo amesema, fanyeni hivi”. Inakuaje, Mimi siombi? Mimi ni mwenye dhambi nyingi wala sistahili.

Anahangaika kidogo, na hatimaye anapata upenyo, na hivyo anaendelea katika njia ya Mungu; katika kusikia, kusoma, kutafakari, kuomba na kushiriki meza ya Bwana; katika jinsi ambavyo atampendeza Bwana, Mungu anasema, “imani yako imekuokoa. Nenda kwa amani”.

 

Kuwa na mfano wa utauwa

 

“Wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake”

2 Timetheo 3: 5

 

Wale wenye mfano wa utauwa hawajitengi tu kwa kawaida na uovu unaoonekana kwa nje, katika kufanya mema yanayowezekana. Pia wanatumia njia ya neema katika nafsi zote, hasa katika kuhudhuria nyumba ya Mungu mara kwa mara kwa kadiri iwezekanavyo. Hawaendi wakiwa wamefumbwa macho pamoja na tofauti zisizo na maana. Pia huwatendi kana kwamba mungu amelala, kuzungumza mmoja na  mwenzake au kwa kawaida wakiona kutumia kumwomba Mungu kutumia kwa ajili ya Baraka zao.

Hapana, wanaendelea kwa umakini na kwa macho katika kila huduma muhimu, hasa hasa katika ushirika wa meza ya Bwana. Kwao si tabia ya mazoea, lakini ni idara ambayo inasema tu, “Mungu anirehemu mimi mwenye dhambi.

Kama ni viognozi wa familia, hufanya maombi ya pamoja na familia na huweka muda maalum kwa ajili ya kuongea na Mungu. Wale wenye mfano wa utauwa, wakiwa wakristo, wakiwa hasa na kanuni za kidini ndani yao, unyenyekevu, ambapo haya matando ya nje hudhihirika.

Hakika bila unynyekevu hakuna anayeweza kuwa mwaminifu, kwa kuwa, hata wapagani hufanya tofauti kati ya wale ambao huepuka dhambi kwa kuogopa adhabu na wale ambao hutenda, na ndiyo inavyokuwa. Kwa watauwa ambao hujiepusha na dhambi ili kuwa na upendo wa nguvu zake. Pasipo kanuni za ndani za uaminifu, hakuna hata mmoja anayeweza kuwa mkristo. Anaweza tu kuwa mnafiki.

 

Kulinda kwa njia ya maombi

 

“Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzishinda siku za uovu, mkiisha kuyatimiza yote, kusimama”

 

Waefeso 6: 11-13

 

Jilinde dhidi ya roho ambazo hushinda dhidi yetu ili kuweka hali ya kutokuamini, kiburi, ibada ya sanamu, wivu, hasira, chuki: katika ulimwengu wa roho,  ambapo palikuwa ni makao yao hapo awali na ambapo wanapotamaani ikiwa wataruhusiwa. Kwa hiyo tunahitaji silaha zote za Mungu.

Siku ya uovu, (Mstari 13) - vita ni endelevu, lakini wakati mwingine vita yetu inaweza kuwa si ya muda mrefu, na nyingine ni zaidi ya siku, yenye vurugu nyingi. Siku ya uovu – inaweza kuwa inayoelekea mauti, au uzima. Hiyo vita inaweza kuwa ndefu au fupi, na isiyokuwa na idadi ya siku sahihi za mapambano.

Ili uendelee kuvaa silaha za Mungu na kisha kusimama, lazima ukeshe na kuomba. Hivyo, utawezeshwa kustahimili mpaka mwisho na kisha kusimama kwa furaha kabla ya kukutana na mwana wa Adamu, “katika siku ya mwisho”.

Ili uweze kuwa tayari kwa kila hatua, vaa kweli kiunoni, siyo tu kwa kweli ya Injili, bali kwa, “Kwa kweli katika utu wa ndani” - (zaburi 51:6) Vivyo hivyo Bwana wetu anaelezwa (Isaya 11;5) Pasipo kweli katika utu wetu ndani, maarifa yetu yote ya kweli na ki ungu yatathibitisha lakini kujifunga ki udhaifu katiak siku ya uovu. Na kwa kadiri mwamume na mwanamke aliyejifunga huwa tayari kusonga mbele, kwa hiyo hii inaonyesha moyo wa uasi (kutotii), na utashi uliotayari, na marafiki wasiotengana - (Imani na upendo).

 

 

Huwazuia mbali na uovu

 

“Maana mbali ya uovu yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi”

Waebrania  12: 6

 

Tunaweza kufanya nini ili kwamba nyumba zetu ziweze kumtumkia Bwana? Je, hatupaswi kujitahidi; kwanza, kuwazuia dhidi ya dhamba zote za nje-kulichukua JINA la Bwana bure na kufanya yasiyostahili kutendwa katika siku ya Bwana? Wale wanawakodi wanaweza kuzuiwa kwa mazungumzo ya mabishano au ushawishi, lakini klama watakuwa tayari; wanapaswa kuondolewa.

Mwenzi wako hawezi kuondolewa, isipokuwa uzinzi. Katika masuala mengine, nini kifanyike hasa wakati dhambi ni mazoea? Yote yanayofanyika, hufanyika kwa mifano, kwa sehemu, kupitia malumbano au ushawishi; kama yanayoweza kuelekezwa na mkristo mwenye busara. Kama uovu unaweza ukashindwa, lazima iwe kwa wema. Hatuwezi kumpinga shetani kwa silaha zake mwenyewe. Ikiwa uovu huu hauwezi kushindwa kwa wema, tumeitwa kuteswa katiak kupitia huo. Ikiwa Mungu auona wema mbele yake, na kuuondoa. Kwa sasa, endelea katika maombi ya kung’ang’ania kwa wakati sahihi. Anaweza kuliondoa jaribu na hulifnaya jaribu kuwa Baraka katika nafsi yako.

Wakati watoto wako wana umri mdogo, unaweza kuwazuia kufanya uovu kwa kuwashauri; kuwashawishi na kuwaonya, na kuwasahihisha pia. Pia kumbuka, njia hii inapswa kutumika kwa kuendelea - baada njia nyingine kuwa zimekwishafanyiwa kazi na kuabaini kuwa hazina matunda yaliyotarajiwa. Yote yafanyike kwa upole na kwa ukarimu. Vinginevyo, roho yako hupata hasara na mtoto hupata matokeo au faida kidogo. Usifikirie mwenyewe kuwa na busara kuliko Mungu. Anasema, mradi mwanao liko tumaini; wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake” (mithali 19:18).

 

Kristo ni yote

 

“Bali Kristo ni yote, na katika yote”

Wakolosai 3: 11

 

Tunajua kwamba Mungu ana uwezo wa kutoa neema ingawa hakuna njia katika uso nchi. Kwa maana hii tunaweza thibitisha, sambamba na Mungu, hakuna kitu kama hicho, njia tuiangaliayo, kuwa ana uwezo wa kutenda chochote kama apendavyo, kwa njia yoyote, au pasipo njia yoyote kabisa.

Tunajua zaidi, kwamba matumizi ya njia zote ambazo huweza kutupatanisha kwa sababu ya dhambi zetu. Ni damu ya kristo pekee ambayo kwa hiyo mwenye dhambi yeyote hupatanishwa na Mungu. Hakuna upatanisho mwingine kwa ajili ya dhambi zetu, au chemchemi kwa ajili ya dhambi; uchafu.

Kila mwamini katika kristo anashawishika kwa undani kwamba hakuna faida isipokuwa ndani yake. Hakuna faida yoyote katika  matendo yao: si katika kuomba, au kuchunguza maandiko, au kusikiliza neno la Mungu, au kula mkate ana kukinywea kile kikombe cha meza ya Bwana. Kama wale wanaosema.” Kristo ni njia pekee ya kupata neema”, Inamaanisha kwamba yeye ndiye pekee wa kusababisha neema, haiwezekani kushinda, ni kwa yeyote ambaye hujua neema ya Mungu. Kwa “Kristo”, kama Mtume aliyvyosema,”Ni yote katika yote”.

 

Siyo tu kusema maombi ya mtu

 

“Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jila lako?

Mathayo 7: 22

 

Bwana wetu alisema mara kadhaa kwamba, hakuna mtu ambaye hana ufalme wa Mungu ndani yake watakayeingia katika ufalme wa mbinguni. Hata hivyo, alijua vema kwamba wengi wasingeupokea usemi huu. Kwa hiyo anathibitisha: “Wengi (siyo mmoja, siyo wachache tu; siyo kitu cha juu juu) wataniambia katika siku hiyo”, siyo tu kwa kuomba sana; tumekusifu; hatujafanya uovu; lakini nini cha zaidi: “Tumefanya unabii kwa jina lako”. Tumesema mapenzi yako kwa wanaume na wanawake, tumewaonyesha wenye dhambi njia ya amani na utukufu. Na tunapofanya hivi “Kwa jina lako”, kwa mujibu wa kweli ya Injili yako. Katika au kwa jina lako, “Kwa nguvu ya neno lako na Roho wako”  hatukutoa pepo; na kwa jina lako (kwa nguvu zako, siyo zetu) hatukufanya miujiza mingi?

Lakini Yesu alisema, “na kisha nitawaambia kamwe sikuwajua ninyi”, sikuwajua ninyi kuwa watu wangu, kwa kuwa mioyo haikuwa sawa/ kukamilika kumwelekea Mungu. Hamkuwa wapole na wanyenyekevu; hamkuwa na upendo wa mungu; na watu wote. Hamkufanya upya katika sura ya Mungu; hamkuwa watakatifu kama jinsi nilivyo mtakatifu. “Ondokeni kwangu, ninyi” ambayo licha ya yote sheria yangu ni takatifu na pendo langu ni kamilifu. Umejenga juu ya mchanga.

 

Wema wangu wote, moyo wangu wote

 

“Fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu”

1 Wakorintho 10: 31

 

Kujiwekea hazina duniani kunakatazwa kabisa na Bwana wetu na kufananishwa na muuaji au mwasherati. Kwa kufanya hivyo, utakuwa unajiwekea hasira katika siku ya hasira (ghadhabu) na kufunulia kwa wenye haki siku ya hukumu ya Mungu.

Lakini, jaribu kufikiri kwamba isingekuwa inakatazwa? Je,  waweza kwa sababu za msingi, kutumia pesa kwa namna ambayo Mungu anaweza kukusamehe, badala ya kutumia katika namna ambayo hatukupa thawabu? Hatukuwa na thawabu mbinguni kwa kile ulichoweka; lakini pia utapata thawabu kwa kile ulichoweka mbinguni. Kila kiasi cha pesa unchoweka katika benki ya kidunia kinapotea, hakileti faida yoyote. Lakini kila kiasi cha pesa unachompa masikini kinawekwa katika akauni yako, katika benki ya mbinguni. Na italeta faida yenye utukufu, ikikusanywa katika umilele wote.

Ni nani aliye na ufahamu na hekima kwenu? Na akusaidie leo hii, akichagua katika mambo yote, njia iliyo bora zaidi.” Kwa uthabiti akitunza maamuzi sawasawa na kupumzika (kulala), sala, kazi, chakula, mazungumzo. Lakini vivyo hivyo katika kutumia kipawa muhimu na pesa. Moyo wako na uitikie katika wito wa Mungu, kuanzia sasa, Mungu awe msaada wangu, sitaweka hazina tena hapa duniani”. Nitaweka hazina mbinguni nitampa Mungu vitu vyake vyote, vyote vilivyo vyema na moyo wangu wote.

 

Kutimiza kusudi la Mungu

 

“Nimekuchagua katika tanuru ya mateso”

Isaya 44:10

 

Unapokuwa na uwezo juu ya moyo wa mwanadamu, Mungu hutiririsha chemchemi za moyo kama apendavyo. Kwa namna Fulani, huwasababisha wale awapendao kwenda nguvu hadi nguvu hata watakapofikia “utimilifu wa utakatifu”, kwa shida na kwa hali ya uzito. Lakini mambo kama haya hutokea kwa nadra sana. Kwa ujumla, Mungu huona mema ili kuwajaribu wanaume na wanawake waliokubaliwa ndani ya tanuru ya mateso.

Kwa hiyo, wingi wa majaribu na uzito huwapata wengi au wachache miongoni mwa watoto awapendao sana. Hakika, karibu watoto wote wa Mungu hupitia hii hatua, kwa kiwango cha juu au cha chini.

Bila mashaka, tunapaswa kukesha na kuomba na kujitahidi kwa kadiri tuwezavyo kuepuka kuanguka katika giza. Lakini hatuhitaji sana kujua namna ya kuepuka uzito kama namna ya kuboresha maisha yetu. Hiyo hali inapotokea tunapaswa kuwa waangalifu tunapomngoja Bwana ili uzito uweze kukamilisha kile kilichoruhusiwa - ili imani yetu iweze kuongozeka tumaini letu linapothibitika, hasira ya kibinadamu itakapoondolewa, na pendo lote hukamilika.

Tufanye kazi pamoja naye, kwa namna ambayo Bwana ameendelea kumkirimia, katika “kujitakasa katika uchafu, wa kimwili na kiroho”. Na kukua katika neema ya Bwana wetu yesu Kristo, mpaka tutakapopelekwa katika ufalme wake wa milele.

 

Ukristo halisi

 

“Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza”

Waebrania 11: 6

 

Baadhi ya wanaume na wanawake hujenga tumaini la wokovu wao katika hali ya kutokuwa na hatia. Je, wewe ni mmoja wao? Je, umejenga katika hali ya kuona kwamba hauna uhasama au ugomvi na mtu yeyote – hujamkosea mtu yeyote? Unajitaabisha tu! Unafanya mambo ambayo hayaongezi lolote kwako, kwani ndiyo sote tunavyopaswa kufanya. Husemi uongo, na unaishi vema. Na unadhamiri kumwelekea Mungu; wala haishi katika dhambi yoyote.

Yote ni mema pia, lakini hayo yote siyo wokovu. Unaweza kwenda au kufanya zaidi ya hapo na usiende mbinguni. Ikiwa hali hii inatoka katika kanuni sahihi, ni sehemu ndogo ya dini na kikristo. Lakini kama haitokani na kanuni sahihi, basi siyo sehemu ya dini kabisa. Kwa hiyo kuweka wokovu juu ya sehemu hiyo peke yake, bado utakuwa unajenga juu ya mchanga. Je, bado unaendelea zaidi? Je, unaongeza katika mtendo yako? Unaangalia njia zote za neema? Katika fursa zote angalia meza ya Bwana, fanya maombi ya mkusanyiko na ya faragha, fanya mara kwa mara kwa kadiri uwezavyo, unavyosikia, na chunguza maandiko na tafakari maandiko hayo?

Kweli, mambo haya yanapaswa kuwa yamefanyika. Hata hivyo, haya pia ni bure ikiwa yatafanyika bila imani, rehema na upendo wa Mungu, utakatifu wa moyo; mbingu kufunguka ndani ya nafsi kama kuna hivi, bado utakuwa umejenga juu ya mchanga.

 

Omba kabla migogoro

 

“Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye wewe na yeye peke yenu”.

 

Mathayo 18:

 

Njia kuu ya kawaida ya kufuata kanuni ya kwanza hapo juu ni bora kama wewe mwneyewe umeona au kusikia mkristo mwanamke ametenda dhambi isiyoweza kukanwa (Undeniable sin) - kiasi kwamba ni ngumu wewe kuwa na shaka juu ya ukweli wake hivyo sehemu yako ni dhahiri. Chukua nafsi ya kwanza kumwendea na kumwambia kosa lake kati yenu. Lazima kuwa na umakini mkubwa ili jambo lifanyike katika roho sahihi na katika namna sahihi. Maonyo yenye mafanikio hasa hutegemeana na roho ambayo maonyo hayo yametolewa. Omba kwa bidii ili kwamba yafanyike katika roho ya upole na unyenyekevu. Kwani mtu hawezi kurejeshwa pasipo roho ya upole (angalia Wagalatia 6; 1)

Angalia pia namna unavyoongea iwe sawasawa na injili ya Kristo. Epuka namna Fulani ya kutazama, ishara, sauti yenye kiburi au kutokuwa mnyenyekevu, kuwa na msimamo au majivuno, pamoja na kujali kwa usawa, epuka mshikano wa wenye hasira; kushutumu; au dalili ya kuumizwa, uchungu, au uchungu katika maelezo. Tumia pumzi na lugha tamu na upole pia, ambavyo vinatokana na upendo katika moyo. Hata hivyo utamu huu hauhitaji kukuzuia kusema kwa kumaanisha … Mungu kwa kadri ianvyobidi, tumia maneno matakatifu ya Mungu, kama jicho lake yeye ajaye kuwahukumu walio hai na wafu.

 

Kuomba katika Roho ya upole

 

“Mrejezeni mtu kama huyo kwa roho ya upole”

Wagalatia 6: 1

Kama wema umefanyika kwa kile kilichosemwa, ni Mungu anayefanya. Omba ili aulinde moyo wako, aongeze ufahamu wako, na auelekeze mwili wako katika maneno kama apendavyo katika kubariki. Kama akipinga kweli, hataweza kuletwe katika kuijua kweli hiyo, isipokuwa kwa upole. Hata hivyo ongea katika roho ya upendo wa dhati”, ambao maji mengi hayawezi kuuzimisha”. Kama upendo hauwezi kushindwa, unaweza kushinda vitu vyote, nani aweza kuelezea nguvu ya upendo?

Upendo unaweza kuinamisha shingo shupavu, jiwe kuwa nyama laini, lainisha, na kuchoma, na kuvunja moyo wa mtu mkaidi. Kama huna fursa ya kuongea na mtu; unaweza kufanya hivyo kwa kutumia mjumbe, rafiki wa karibu na mwenye busara na mnyofu ambaye hawezi kumficha. Kuongea wewe mwenyewe ni bora zaidi, lakini njia hii ni bora pia kuliko kutoongea kabisa (yaani kutumia rafiki wa karibu) kama huwezi kusema mwenyewe au kupata mjumbe mwaminifu (wakili wa siri), kilichobaki ni kuweka ujumbe huo katika maandishi. Kuna baadhi ya mazingira ambayo hufanya njia kuwa ndiyo hasa inayoweza kutumika katika kufikisha ujumbe.

Ikiwa mtu mwenyewe ni mwenye hasira ukamfikia kwa lugha laini (maandishi rahisi) katiak namna ambayo ataweza kuvumilia. Wengi huweza kusoma maneno yale yale ambayo wasingeweza kusikia moja kwa moja. Kwa kuongeza jina lako, ni karibu sawa na kuongea na mtu.

 

Kuongea (KUZUNGUMZA) na Bwana”

 

“Maana yote yawezekana kwa Mungu”

Marko 10: 32

 

Ni namna Fulani ya ujuzi wa jumla kwa wana wa Mungu kwamba bila kujali kutofautiana katika masuala Fulani. Fulani, hukubaliana na ujumla katika hili: ijapokuwa tunaweza”  kwa Roho, kufisha matendo ya mwili” na kumdhoofisha adui yetu siku kwa siku, hata hivyo hatuwezi kumwondoa. Kwa neema tuliyopewa siku ya wokovu hatuwezi kuviondoa. Ingawa tunaomba na kukesha kwa kadiri tuwezavyo, hatuwezi hata kujitakasa mioyo yetu na mioyo yetu na mikono yetu.

Kwa hakika kabisa, hatuwezi, mpaka inapompendeza Bwana wetu kusema / kuzungumza  na mioyo yetu. Tena, kuzungumza kwa mara ya pili, “uwe safi!” hivyo ni ukoma tu uliotakasika kisha ni shida ovu, nia ya mwili, imeharibiwa, na dhambi ya asili hauwezi kustahimili.

Katika hali hii, tunapokuwa tumetubu, hivyo tunaitwa “kuamini injili” na hili nalo linapaswa kueleweka kwa upekee, tofautiana ambapo tuliamini ili kuhesabiwa haki. Tunapaswa kuamini habari njema ya wokovu mkuu na mkamilifu ambao Mungu ameondoa. Amini kwamba yeye ambaye ni mng’ao wa utukufu wa baba yake, ana uwezo wa kuwaokoa wote wamjiao katika yeye. Ana uwezo wa kuokoa katika dhambi zote ambazo zimebaki ndani ya moyo, wako – na kukupa chochote unachopungukiwa. Hili haliwezekani kwa mwanadamu, lakini kwa Mungu yote yanawezekana.

 

Endelea kukesha na kuomba

 

“Na masikio yako yatasikia neno nyuma yako, likisema …. Njia ni hii, ifuateni”

Isaya 3: 21

 

Unaona mabadiliko na maendeleo au mabadiliko yasiyoweza kuhojiwa kutoka neema hadi dhambi. Hiyo huendelea, kutoka hatua hadi hatua: (1) Mbegu ya uepndo ya ki-ungu, imani ishindayo hubaki ndani ya aliyezaliwa na Mungu. “Hujilinda mwenyewe” kwa neema ya Mungu na hawezi kutenda dhambi”. (2) Jaribu linapoinuka; kama ni kutokea ulimwenguni, katika mwili au kwa shetani, haijalishi (3) Roho mtakatifu humpa tahadhari kuwa kwamba dhambi iko karibu na anapaswa kukesha katika sala. (4) Hukupa njia, kwa kiasi Fulani katika jaribu, ambalo sana limeanza kufuata mapenzi ya Mungu (yaani kilichoruhusiwa (5) Roho mtakatifu amehuzunishwa; imani yake imedhoofishwa na upendo wa Mungu umepoa (6) Roho mtakatifu anamwonya kwa bidii akisema, “Hii ndiyo njia; tembea katika hiyo” (7) Anageuka mbali na sauti ya Mungu na kusikiliza sauti ya kupendeza ya majaribu (8) shauku huanza na kuenea ndani ya nafsi yake mpaka imani na upendo unapotoweka.

Hatimaye huanza kutenda dhambi kwa dhahiri na nguvu inaondoka katika maisha yake. Ni ukweli usiohojiwa, kwamba aliyezaliwa na Mungu, hujilinda, huwa haishi au kutenda dhambi. Hata kama hata “Jilinda mwenyewe” anaweza kutenda dhambi za kila aina kwa uchu.

 

Amri mbili zilizo kuu

 

“Utampenda”

Marko 12: 30.

 

Kumpenda Bwana Mungu wako kwa moyo wako, akili nafsi nguvu ni tawi la kwanza la hakiya mkristo. Utajifurahisha katika Bwana Mungu, ukitafuta na kupata furaha timilifu katika yeye. Utasikia na kutimiza neno lake, “Mungu nipe moyo wako”. Na baada ya kumpa mtu wa ndani ili kutawala hapo bila ya kuvutana, unaweza kulia katika utimilifu wa moyo wako”, Nitakupenda, ee Bwana wangu, nguvu zangu. Bwana ni wangu ndio imara; mwokozi wangu; Mungu wangu, ambaye ninamtegemea.

Amri ya pili, tawi kuu la pili katika hali ya kikristo, ni kwa karibu na isiyotengana kabisa na ile ya kwanza”. Mpende jirani yako kama nafsi yako.”

“upendo” – ukumbatie kwa mapenzi mema, kwa bidii na pendo la dhati, shauku inayowaka ndani kuzuia au kukufunga na uovu na kuleta kila mema unapobidi. “Jirani yako” – siyo tu rafiki zako, washirika wenzako tu, au watu mnaofahamiana; siyo tu wenye nguvu (Neema) wanaokuheshimu, wanaokutendea mema, au kurudisha wema lakini kila mtu, siyo kuwatenga watu ambao hajawahi kuwaona au kuwajua kwa majina; siyo kwa kuwatenga watu unaowajua ka ubaya au wasio na shukurani, na wale ambao licha ya kukutumia.

Hata wale ambao utawapenda kama unavyo jipenda mwenyewe kwa kiu na furaha ile ile. Tumia umakini ule ule usiochoka kuhakikisha kwamba unawaponya na mambo ambayo yaweza kuwaumiza au kumjeruhi nafsi au miili yao. Huu ni upendo.

 

Kuthibitishwa katika milele yote

 

“Aidhihirishe bidii ile ile kwa utimilifu wa matumaini hata mwisho”

Waebrania 6: 11

 

Tunathibitisha kipawa cha Mungu ndani yetu kwa hisia za ndani, kwa kile ambacho ametuonyesha – hisia za pendo kuu na uwezo wa hali ya juu wa kuhisi (kutambua). Sasa tunaishi katika furaha na siyo katika hofu. Tunatazama mambo yenye kuleta furaha, hali, sifa, mambo yote ya dunia, kama yasiyokuwa na thamani, wa dhahiri, yasiyo kuwa na mfano wa vitu vya milele.

Je, unaweza kusema, ”wewe, Bwana na rehema katika hali yangu yakutokuwa na haki; makosa yangu hukuyakumbuka daima?” kisha, kwa muda ujao, tazama kwamba unaruka dhambi kama kutoka katika uso wa nyoka! Kwa jinsi gani jambo hilo huonekana ni dhambi iliyozidi mbele zako sasa!

Kwa upendo mwingine, kwa jinsi gani katika nuru unaweza kuona mapenzi ya Mungu yaliyo matakatifu na makamilifu! Sasa, kwa hiyo, fanya kazi ili yaweze kutimia katika maisha yako, kwa kupitia wewe, au kwa kuwa juu yako! Sasa kaza na uombe ili usijetenda dhambi tena, kwamba uone na kujiepusha na hata dhambi ndogo katika amri zake.

Jua linapoangaza katika giza, utaona vitu ambavyo hukuweza kuviona, kuanzia sasa jua la haki linawaka ndani ya moyo wako, na sasa unaweza kuona dhambi ambazo usingeweza kuziona hapo kwanza. Hivyo uwe na shauku zaidi ya kupokea nuru zaidi kila siku, zaidi ya maarifa na pendo la Mungu, zaidi ya Roho wa Kristo, zaidi ya uhai wake na zaidi ya nguvu za ufufuo. Sasa tumia vyote unavyopata. Kwa hiyo utazidi kuongezeka katika upendo mtakatifu mpaka imani itakapomezwa katika upeo na sheria ya upendo itakapothibitishwa katika umilele wote!

 

Kinyume na pendo la Mungu

 

“Wote niwapendao Mimi nawakemea… basi uwe na bidii, ukatubu”.

 

Ufunuo 3: 19

 

Mara au baada ya kuhesabiwa haki, mwamini anajisikia (utashi) – kufanya ambayo si kinyume na mapenzi ya Mungu. Sasa - (matakwa) ni sehemu muhimu sana ya siri katika mwili wa binadamu mwenye akili, hata ya Bwana wetu mwenyewe. Lakini ni mapenzi ya kibinadamu yalitiishwa katika mapenzi ya baba yake.

Suala ambalo hata waminio wa kweli katika Kristo ni kwamba kuyafuata mapenzi yao zaidi au kuyainua kiasi Fulani kuliko ya Mungu. Wanapamba dhidi utashi wa mapenzi yao. Kwa nguvu zao zote na kisha huendelea katika imani.

Lakini (utashi – ubinafsi) kama kilivyo kiburi ni vionyo vya sanamu. Yote yako tofauti na upendo wa Mungu, kama ilivyo kwa katika kupenda ulimwengu. Ni kweli mtu kutoka mautini na kuingia uzimani, hana shauku ya Mugnu zaidi. Hakika unaweza kusema, “Hakuna kingine katika ninacho tamam, zaidi yako”.

Lakini mara zote si hivyo. Kama hataendelea kukesha na kuomba, atajisikia tu kuependa ulimwengu, lakini tamaa huanza kuinuaka na kushambulia pendo la Mungu ndani yake. Hujisikia pambano la juu katika kupenda viumbe (ulimwengu) kuliko muumba – aliye viumba vitu vyote- iwe ni mme, wazazi, watoto, mke, rafiki wa karibu.

kiasi kwamba hujitoa kwenye shauku / tamaa za mambo ya kidunia na starehe zake, huelekea kumsahau Mungu. Na katika hili, hata wakristo wa kweli katika Kristo wanahitaji kutubu.

 

Kuwa mkrito kwa pamoja

 

“…pendo la Mugnu liemiminwa ndani ya mioyo yetu kwa njia ya Roho mtakatifu tuliyopewa”

Warumi 5: 6

 

Haitoshi tu kujitenga na uovu na kutenda mema katika fursa zote, pia haitoshi kutumia njia zote za neema kwa unyofu na shauku ya kumpenda Mungu.

Swali kubwa hubaki kwa kila mmoja wetu: Je, moyo wangu hulia kwamba yeye ni yote kwangu? Je, ninafuraha katika Mungu? Je, yeye (Mungu) ni shangwe yangu? Je haikuandikwa ndani ya moyo wangu kwamba wale wampendao Mungu huwapenda majirani zao?

Endelea mbele zaidi: Je, ninaamini kwamba Kristo alinipenda na akajitoa mwenyewe kwa ajili yangu? Je, nina imani katika damu yake? Je, ninaamini kwamba mwana kondoo ameniondoa dhambi zangu zote na kuzitupa kama jiwe katika kina cha bahari, na kunipa ukombozi kupitia damu yake, na hata ondole la dhambi? Je, Roho wake huishuhudia roho yangu kwamba Mimi ni mwana wa mungu?

Mtu asikushawishi kuacha dhawabu ya mwito mkuu. Lia mchana na usiku mbele zake ambaye, mlipokuwa hamna nguvu akafu kwa ajili ya waovu; mpaka utakapomjua unayemwamini kumfahamu kwamba mko pamoja kama wakaristo.

Kisha, kuhesabiwa haki bure kwa neema. Kwa ukombozi ulio katika Yesu, utakuwa na ujuzi wa Baraka ya Kristo na kujua pendo la Mungu lililomiminwa katika moyo kwa Roho tuliyopewa.

 

Kuzaliwa kutoka juu

 

“Mmezaliwa mara ya pili, si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele”

1 Petro 1: 23.

 

Haijalishi kama hukuishi maisha ya kujidhili na hukuishi maisha ya dhambi ya kudhamiria. Lazima uende mbele ya zaidi, au vinginevyo huwezi kuokolewa. Hata kama unafanya mema kwa kadiri uwezavyo na umefanikiwa kutumia nafsi ulizopata kutenda mema, hata hivyo hayo mema hayafuti au kubatili suala (kuzaliwa mara ya pili). Bado, unahitaji kuzaliwa mara ya pili.

Pasipo kuzaliwa mara ya pili, hakuna utakachofanya katika hali ya umaskini, ya dhambi na nafsi iliyochafuka. Unaweza kuhudhuria ibada kwa uaminifu na kushiriki meza ya Bwana, na kuomba sana kwa faragha; na kusikia jumbe nyingi za Neno la Mungu; unaweza kuwa umewahi kusoma vitabu vingi sana. Bado; unapaswa kuzaliwa mara ya pili” Hakuna hata kimoja kati ya hivi kinachoweza (chini ya jua) kukuokoa na Jehanamu, isipokuwa umezaliwa mara ya pili.

Kama bado hujapata badiliko hili ni ndani kupitia kazi ya Mungu; “haya yawe maombi ya kuendelea katika maisha yako”, Bwana, ongeza hili katika Baraka zako zote – Nizaliwe mara ya pili.

Usininyime hili; nizaliwe kutoka juu, ondoa kila kisichokupendeza - tabia mbaya, bahati, mbaya, marafiki wabaya, Afya mbaya – unipe hiki tu – kuzaliwa mara ya pili, kupokelewa miongoni mwa watoto wa Mungu. Nizaliwe na mbegu isiyoharibika kwa Neno la Mungu. Nikue kila siku katika neema, na katika maarifa ya Bwana na Mwokozi Yesu Kristo.

 

 

Swali la kushangaza

 

“Lakini kila na mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanyanywa”

Yakobo 1: 14

 

Wengi wenye mioyo minyoofu wamekuwa wakishangazwa na maswali. Je, dhambi hutangulia au hufuata baada ya kupoteza imani? Je, mtoto wa Mungu lazima atende dhambi kwanza  ndipo apoteze imani? Au hupoteza imani yake kwanza, kabla ya kutenda dhambi?”

Ninajibu: baadhi ya dhambi za kutotenda tuliyopewa kutenda, lazima hutangulia kupoteza imani-dhambi ya ndani. Lakini kupoteza imani lazima kutanguliwe na kutenda dhambi. Kwa kadiri mwamini anavyozidi kuchunguza moyo wake, ndivyo anavyoshuhudiwa hili. Kutenda kwa upendo huondoa dhambi ya ndani ya nje katika nafsi ya mtu anayekesha katika sala. Hata ikiwa tukiwa katika hali ya majaribu, hasa tunapokuwa katika dhambi ituzingayo kwa upesi.

Ikiwa jicho la upendo la nafsi linamtazama Mungu, jaribu hutoweka mara moja. Lakini kama sivyo tuko, kama mtume Yakobo asemavyo (Mstari wa 14), tunaondoshwa mbali na Mungu kwa tamaaa zetu na kukamatwa na kipawa cha starehe za muda tulizoahidiwa. Kisha hiyo tamaaa, hutunga mimba ndani yetu, huzaa dhambi, (Mstari 15). Kwa kuwa ni dhambi hiyo ndani, hudhoofisha na kisha kuharibu imani, tunakuwa tumekamatwa katika mtego wa Ibilisi, ili tuweze kutenda dhambi yoyote iliyo dhahiri. Kwa hiyo, kisha wakati wote, ili uweze kusikia na kutii sauti ya Mungu wakati wote.

 

Tiba: mimina moyo wako katika sala

 

“Jijaribuni wenyewe… jithibitisheni wenyewe”

2Wakorintho 13: 5

 

Je, umemlazimisha Mungu kuondoka katika maisha yako kwa kuruhusu hasira? Je, umewahi kuvunjika moyo kwa sababu ya maisha ya waovu? Au Umewahi kuwaonea wivu watenda mabaya? Je, umewahi kukwazwa na Kaka au Dada katika Bwana, ukiangalia uhalisi wa dhambi ya kufikirika - ili kutenda dhambi dhidi ya sheria na upendo, kwa kuugeuza moyo wako mbali mno? Mwangalie Bwana ili moyo wako uweze kufanywa upya - na kwamba ubaridi na ukatili huo uondoke, ili upendo, amani na furaha irejee, kwa moyo mkunjufu na roho ya msamaha.

Je, umejitoa katika tamaa za upumbavu? Katika aina yoyote au kwa kiasi Fulani cha kutokuwa mwadilifu,ufedhuli, pendo lisilo na uadilifu? Je, inawezekanaje upendo wa Mungu kuwa na nafsi ndani ya moyo wako mpaka utakapoweka vinyago mbali nawe? Haiwezekani kupona au kupata nuru ya Bwana ndani yako mpaka, “umeling’oa jicho lako la kuume,” na kulitupa mbali nawe. Ondoa vinyago vyote katika patakatifu pake, na mara utukufu wa Bwana utaonekana mara.

Labda ni kutokana na bidii, uvivu wa kiroho ambao umeiweka roho yako katika giza. Unandelea katika hali hiyo hiyo, katika shughuli za kawaida, na giza hilo limekuwa sehemu ya maisha yako.

Je, unastaajabu kwamba roho yako imekufa? Oo, jichochee mwenyewe mbele za Bwana. Jikung’ute mavumbi: pigana mieleka na Bwana ili upate Baraka kuu za ki-Mungu. Mimina moyo wako katika maombi! Endelea kwa uvumilivu  wote! Kesha! Uamke kutoka katika usingizi na uwe macho, ili usiwe tena na tena mateka mbali na nuru na uzima wa Mungu.

 

Ushikilie sana ujasiri wako

 

“Bali neno la Bwana huduma hata milele”

1 Petro 1: 25

 

Ni vigumu kujua kuliko kuelezea mapambano “vita” (mawazo) ambayo kwayo Shetani huleta majaribu kwa wale ambao wana njaa na kiu ya haki. Wanaona vema, kwa uwazi zaidi kwa upande mmoja, uovu uliokithiri wa mioyo yao. Kwa upande mwingine ni utakatifu usio na doa lolote ambao kwa huo waliitiwa.

Mara nyingi, wanaona hakuna roho iliyobaki ndnai yao. Wanaona uharibifu na jinsi walivyofungwa na Mungu, na jinsi walivyokuwa mbali na utukufu wa Mtakatifu, na wako tayari kuacha vyote, imani na tumaini. Hukaribia kutupa ujasiri ambapo “wanaweza mambo yote katika kristo awatiaye nguvu”. Hata hivyo kupitia kristo wanaweza kupokea ahadi.

Wakati shambulio hili lina ghafla linapokuja, shikilia sana, “najua mkombozi wangu yu hai, na nitasismama siku ya mwisho juu ya nchi”. Na sasa nina ukombozi katika damu yake, na ondoleo la dhambi”.

Hivyo, kujazwa na amani na fuzaha timilifu katika kumwamini, songa mbele katika imani ya kuwa na amani; na furaha katika kufanywa upya kwa nafsi katika sura yake aliyekuumba. Kwa sasa, mlilie Mungu ili upate thawabu ya mwito mkuu, na siyo kama shetani anavyowakilisha, lakini katika uzuri wa asili yake. Siyo kama kitu ambacho lazima, au utakwenda Jehanamu lakini kama kitu ambacho kinaweza kukuonyesha kuelekea mbinguni.

 

U-lazima wenye kudiriki

 

“Tukiangusha … kila kitu kilichoinuka… tukiteka nyara kila fikra… ipate kumtii Kristo”

2 Wakorintho 10: 5

 

Usahihi wa mtazamo wa asili ya toba na imani kwa waaminio unahitajika ili kuepuka madhara ya wazi ambayo hatuhitaji kuwa na badiliko lingine zaidi. Kwa kuwa wenye afya hawahitaji tabibu. Kama ndani tumefanywa wazima tayari, hakuna nafasi ya kutafuta uponyaji tena.

Vinginevyo, ule ushawishi wa Roho mtakatifu unaotuonyesha kwamba bado hatuja - kamilika, badohatushurutishi kupata ukombozi mkamilifu kwake aliye na uwezo wa kuokoa-kuishi kwamba anaweza kutusaidia:

Vunja nira za dhambi za mawazo na uiweke roho yangu huru ki ukamilifu! Siwezi kupumzika mpaka usafi uwemo moyoni, mpaka nimekaa ndani yako kabisa.

Usahihi wa mtazamo wa hii toba na hii imani, huenda sambamba na ushawishi wa Roho Mtakatifu kuhusu udhaifu wetu na hatia, ni lazima kabisa ili tuweze kuona uthamani wa kweli wa upatanisho katika damu. Tunahitaji ulazima wa kuona kushawishiwa au kushurutishwa na roho mtakatifu ili kujua au kufahamu kwamba tunahitaji hali hiyo ndani yetu mara baada ya kuhesabiwa haki kama ilivyokuwa hapo kwanza wakati tunashurutishwa na roho mtakatifu ili kuokoka ili kujua kuomba;

Anaishi (Mungu) juu ili tuweze kufanya maombezi, pendo lake la upatanisho na damu yake ya thamani, kusihi.

Hatimahe usahihi wa mtazamo wa toba na imani ya waaminio huleta ushawishi wa Roho Mtakatifu unaodhihirisha udhaifu wa kutoweza kuhifadhi cochote tulicopokea, ambao kwa huo tumeletwa kumhimidi Mungu il kila hali ya kuhamaki, mawazo, neno na tendo viletwe katika kumtii kristo.

 

Imani ilivyoongezwa kama njia

 

“Bwana Mungu akamwita Ibrahimu”

Mwanzo 3: 9

 

Ni hakika kwamba imani; hata katika ujumla wa neno lenyewe haikuwa na sehemu katika pepo (Paradiso). Ni uwezekano wa hali ya juu, kutoka katika kitabu cha Mwanzo, kwamba Adamu (kabla hajamwasi Mungu) alitembea na Mungu kwa hisia na siyo kwa imani.

“Kwa sababu hiyo macho yake yalikuwa yana nguvu na uwezo, Na (kama Tai awezavyo kutazama juu) aliweza kutazama uso wa Muumba kwa karibu kama jinsi malaika walivyoweza kufanya. Alikuwa anauwezo wa kuongea na Mungu uso kwa uso, yeye ambaye uso wake hatuwezi kuuona na kuishi naye katika hali ya ki-mwili; hivyoAdamu hakuhitaji imani ambayo kazi ni kutusaidia vema.

Kwa upande mwingine, hiyo ni hakika kwamba imani katika uhalisi wake haikuwa na nafsi kwao. Kwa mantiki hiyo, ni lazima kufikiria dhambi na ghadhabu ya Mungu dhidi ya wenye dhambi. Pasipo haya hakuna haja ya upatansiho kati ya mwenye dhambi na Mungu.

Kama kusingekuwa na haja ya upatanisho kabla ya anguko, hivyo kusingekuwa na nafsi ya imani katika upatanisho huo. Kwa sababu mwnadamu alikuwa safi mbali na doa la dhambi; yaani Mtakatifu kama Mungu alivyo Mtakatifu.

Na Upendo, mpaka hapo ulikuwa umejaa moyo wake, na kutawala hapa pasipo uasi. Lakini upendo ulikupokuwa umepotezwa na dhambi, imani iliongezwa, siyo kwa jinsi yake, lakini kama njia ya kuimarisha au kuthibitisha sheria ya upendo.

 
 

Ushirika na Mungu katika kuzaliwa upya

 

“Tuliumbwa katika Kristo”

Waefeso 2: 10

 

Tunapokuwa tumezaliwa mara ya pili ki-ungu, sasa tunaweza kusema tunaishi maisha sahihi. Mungu anakuwa ametuhuisha maisha ambayo ulimwengu hauyaelewi-na uhai wake umefichwa katika Kristo. Katika Mungu “Mungu anaendelea kupulizia pumzi yake katika nafsi yake, kama aina Fulani ya upumuaji wa kiroho, na nafsi nayo inapumua kumwelekea Mungu”.

Neema hushuka katika moyo wake, maombi na sifa hupanda kuelekea juu mbinguni: kwa ushiirika huu kati ya mtu na Mungu mwenyewe, kwa ushirika huu, kati ya Baba na mwana, uhai wa Mungu ndani ya mtu huendelea kuwepo. Mtoto wa Mungu hakua, mpaka atakapofikia utimilifu wa cheo cha kristo (Aghalia Waefeso 4:13).

Tunaona ya kuwa asili ya kuzaliwa upya ni kwamba badiliko kubwa ambalo hutokea wakati Mungu anatenda kazi ndnai ya  nafsi, wakati Mungu analeta uhai ndani yake, akiinua nafsi kutoka katika wafu (mauti) na kuileta katika uhai wa haki. Ni badiliko ambalo huleta ndani ya nafsi na Roho Mtakatifu wakati nafsi ikiumbwa upya ili kufanana na Mungu katika haki na utakatifu wa kweli (Angalia Waefeso 4:24).

Kuupenda ulimwengu kunabadilishwa na kumpenda Mungu; kiburi kuwa unyoofu, ukatili kuwa unyenyekevu; chuki, wivu, tamaaa za kidunia, nia ya kishetani hugeuzwa na kuwa nia iliyokuwa katika kristo Yesu. Hii ni asili ya kuzaliwa upya: “ kadhalika kwa mtu aliyezaliwa kwa Roho”.

 

Kuitwa na Mungu

 

“Usijivune, bali Uogope”

Warumi 11:20

 

Mungu huenda mbele yetu na Baraka za wema wake. Kwanza kabisa, anatupenda na kujidhihirisha ndani yetu. Tulipokuwa tungali mbali na neema yake alituita na kutuangazia nuru yake katika mioyo yetu. Lakini kama hatutampenda aliyetenda kwanza na kuisikia sauti yake, na kuyageuza macho yetu mbali naye, na kutokuruhusu nuru kuingia ndani yetu, na Roho wake wakati wote hushindana (Angalia Mwanzo 6:3). Kwa taratibu, huanza kuondoka na kutia giza ndan iyetu, isipokuwa roho zetu tuwasiliane naye tena; isipokuwa  tumerudisha pendo, sifa na maombi yasiyokoma, mawazo ya mioyo yetu, maneno yetu, na matendo yetu: mwili, nafsi na roho katika hali ya dhabihu takatifu na iliyokubalika (Angalia Warumi 12:1).

Tujifunze kufuata maelekezo hayo ya Mtume Mkuu, “Usinie makuu, lakini uogope”. Tuogope dhambi, kuliko mauti au Jehanamu. Na tuwe na hofu nyenye wivu, (japokuwa si kwa maumivu), ili tusije tukategemea moyo uliodanganyika. “yeye aliyesimama, aangalie asije akaanguka”. Hata yeye ambaye amesiamama imara katika neema ya Mungu, katika imani ishindayo ulimwngu anaweza kuangukia katika dhambi ya kutenda asiyopaswa kutenda na kuleta uharibifu wa imani”.

Kwa jinsi gani dhambi ya nje (inayoonekana) anavyopatanguvu ya kutawala maisha yako! Kesheni, kwamba mwombe bila kukoma wakati wote na kila mahali, huku ukiumimina moyo mbele ya Mungu! Hivyo unapaswa kuamini wkati wote, kupenda wakati wote, na kamwe kutotenda dhambi tena.

 

Uhai wa Mungu ndani ya roho

 

“Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika hayo yatakayotokea”

Luka 21 : 36

 

Kwa mara moja na kwa ulazima Fulani, uhai wa Mungu unamaanisha mwendelezo wa tendo la Mungu juu ya roho kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu na mwitikio wa roho ya mtu kwa Mungu kurudisha pendo, maombi na sifa zisizokoma.

Kuanzisha hapa, inaonekana kwa uwazi kwamba Mungu hataendelea kutenda lolote ndani ya roho, mpaka roho ya mtu inapoendelea kuwa na mawasiliano na Mungu. Ni rahisi kuelewa jinsi hawa watoto wa Mungu, Daudi, Barnabas, na Petro, wanaweza kufanya kitu kutokana na uimara wao, na hata hivyo kweli kuu ya Mungu, ilinenwa na Mtume Yohana, ibaki imara na bila kutikiswa. Hawakujilinda wenyewe, bali kwa neema ya Mungu. Hawakujilinda wenyewe, bali kwa neema ya Mungu, ambayo inatosha kwa kila mmoja. Kila mmoja huanguka, hatua kwa hatua, kwanza katika mambo ya kinyume, ndani ya moyo wa mtu, “bila kuchochea karama ya Mungu iliyo ndani yake,” bila “kukesha na kuomba”, bila “kukaza mwendo ili kupata thawabu ya mwito mkuu”.

 

Uzito wa nafsi

 

“Uko katika uzito”

1Petro 1: 6

 

Kuna uhusiano wa karibu katika ya giza katika ufahamu, na hali ya ukame na uzito wa nafsi, ambo ni wa kawaida miongoni mwa waaminio. Kufanana kwake ni kwa hali ya juu kiasi kwamba hali hizi hushikamana pamoja. Lakini haya si maneno yanayofanana; siyo mbali, tofauti yake ni kubwa na ya muhimu sana, kama jinsi ambavyo watoto wa Mungu wanahitaji kuelewa ili kuwazuia wasiteleze katika uzito ndani ya giza.

Aina ya watu ambao mtume petro alwaandikia walikuwa ni waaminio wakati huo anasema kwa uwezi (mstari 5) nanyi mnalindwa na nguvu za mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu tena (mstari 7) ametaja ili kwamba kujaribiwa kwa imani yetu na hivyo tena (mstari 9) anaongelea kupokea mwisho wa imani yenu yaani ya wakovu wa roho kwa hiyo ingawa walikuwa katika hali ya uzito lakini waliokuwa na imani iliyo hai.

Uzito wao haukuweza kuharibu imani. Hauwezi kuharibu amani ambayo haiwezi kutengwa na imani ya kweli na iliyo hai. Mtume anaomba (Mstari 2) siyo kuomba neema na amani iliyo tolewa, lakini iweze kuongozwa. Pia walikuwa wamejaa tumaini lililo hai. Kwa sababu, anasema, (Mstari 3) …. Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufukuka kwake Yesu kristo katika wafu; licha ya uzito wao, bado wana tumaini timilifu. Na wakafurahi (Mstari 8) kwa furaha isiyo neneka, yenye utukufu. Pamoja na uzito wao, huendelea na tumaini lililo hai furaha isiyoneneka!.

 

Changamoto ya mwisho

 

“Ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiye uliyenituma”

Yohana 17:  21

 

Oo, ili kwamba wote wanaolichukua jina la Kiristo waweze kuweka ouvu mbali nawe – kwa kuongea, kunong’ona usiruhusu hata kimoja kati ya hivi kutoka kinywani mwako! Angalia, usiseme neno ovu dhidi ya mwenzako, usiseme lolote isipokuwa lililo jema. Kama ungeweza kutofautishwa au kuwa mtu mashuhuri, na iwe kwa alama hii: “Hawamsengenyi mtu anapokuwa hayupo”. Kwa jinsi gani matokeo ya kujina mwenyewe, hata tukajaza haraka ndani ya mioyo yetu? Jinsi amani yetu inavyoweza kutiririka kama mto! Jinsi upendo wa Mungu unavyoweza kujaa tele ndani ya nafsi zetu huku tukithibitisha upendo wetu kwa Kaka na Dada zetu! Ni matokeo gani tutapata kwa hayo yote kwa umoja katika jina la Yesu Kristo! Jinsi upendo wa ndugu unaweza kuendelea kuongezeka ambapo kizuizi chake kilikwishatolewa.

Wala hii siyo yote. Ni matokeo gani haya yanaweza kuwa Jangwa, ulimwingu usiofikiria! Hivi karibuni wataona ndani yetu kile ambacho wasingeweza kukipata katika maelfu yao yote, na kulia, “Ona jinsi hawa wakristo wanavyopendana wao kwa wao”,

Kwa hii, Mungu atazidi kuishawishi dunia na kuwaandaa wao pia kwa ajili ya ufalme wake (Mungu). Kwa kuwa tunaweza kujifunza kutoka katika maneno hayo na ajabu ya ibada ya mwisho ya maombi ya Mungu wetu; “Nawaombea wale ambao wataniamini mimi, ambao wanaweza kuwa na umoja… ili kwamba ulimwengu upate kujua wewe ndiwe uliyenituma”.

Mungu, fanya hima muda ambao tunapendana kwa kweli na kwa ukweli, kama Yesu Kristo atupendavyo!