2010年11月2日 星期二

Nitakuaje na Uhakika wa Imani Yangu?

Mwandishi: Nicky Gumbel


Wakalimani: Erick Nzowa and Apostle 
                                  Joshua


Kaka Erick Nzowa


Apostle Joshua, alisimama kushoto


Mchapishaji: Mch. Rebecca Sun with 
                      Africans Send Internationals
                      (ASI)


Mch. Rebecca Sun




Nilipokuwa na miaka kumi na Nane, “Maisha yangu hayakwenda kama nilivyotarajia Nilikuwa ndio namalizia mwaka wangu wa kwanza chuoni. Nilikuwa nafidia mambo ya ujana, starehe za kila aina na kila fursa ya kimaisha niliitumia vizuri kwa starehe. Ukristo na mimi tulikuwa si marafiki. Nilifikiri maisha ya Ukristo (Ulokole) ni maisha ya uchovu na yanaboa. Nilifiri maisha hayo ya ulokole nikwamba, Mungu ataninyima Starehe na raha za kimaisha na kufanya hizo kazi za kichovu.

Kwa upande mwingine nilichukulia mambo ya ulokole ni ya kweli, lakini huwa ni baada ya kifo, ndo ntaokoka. Ghafla baada ya hapo nikajikuta nampa Yesu maisha baada ya kujua ukweli.Nilichoshindwa kutambua kwenye wokovu ni kuhusu uhusiano wetu na Mungu. Ni kwamba Mungu anatupenda sana na anatarajia kitu kizuri, toka kwetu.

Nilikuwa nikitumia kitabu cha mwandishi Fulani aitwae C.S. lewis kiitwacho “mshangao uletwao na furaha.” Nilianza kuwa na uhusiano mzuri sana na Mungu, pitia kitabu hiki.Ndipo nilipoanza kuwa na uhusiano mzuri na kuona raha iliyo ndani ya wokovu. Kama mtume Paulo alivyoandika kwamba aliye ndani ya Kristo amekua kiumbe kipya na maisha ni mapya. (2 Korintho 5:17) Paulo anaongelea: Mifano miwili hapa:

Hapo awali nilikata tama, sasa ninatumaini kuu. Ninaweza kusamehe sasa, wakati zamani nilikuwa nina hasira na mgumu…. . Mungu yu hai kwangu sasa, najisikia kulindwa na mkamilifu na sijisikii kuwa mpweke, upweke nilionao sasa unaisha, Mungu anainitosheleza na kunijaza.

Nilijisikia kumkumbatia kila mtu mtaani. Siwezi kuacha kuomba, kiasi kwamba mpaka naachwa na basi kituoni. Mazoea ni jambo la tofauti sana. Wengine hufahamu kitu mazoea ni nini na utofauti wake. Kwa wengine ni kitu kidogo kidogo. Kinachojalisha sio tu uzoefu, kama tumo ndani ya Yesu hakika tu wana wa Mungu. Ni mwanzo wa mahusiano mazuri na Mungu. Kama mtume alivyosema, (Yohana 1:12) “Wote waliompokea aliwapa uweza wa kuwa wana.”

Mzazi Bora ni yule anayehakikisha ana uhusiano wa karibu na mwanea. Ndivyo kama kwetu Sisi tuliookolewa na Mungu, Mungu anahakikisha tuna mahusiano mazuri naye. Wengi walio wakristo hawana uhakika na maisha yao kuwa wao ni wakristo au lah!

Niliuliza baadhi ya wakristo katika kazi mbalimbali na kujaza dondoo zangu nilizowapa. Swali mojawapo nililouliza ni : “Je unaweza kujieleza, wewe ni mkristo toka ulipo okoka?” Baadhi yao walinijibu hivi:

     Kuna ahadi nyingi kuu kwenye Biblia. Kuna mstari unaonisaidia kwenye Biblia, na hasa nilipoanza maisha yangu ya Wokovu ni ule unaotoka kitabu cha mwisho wa Biblia. Katika maono Yohana aliona Yesu anaongea na makanisa saba tofauti. kwa kanisa la Laodikia Yesu anasema.” Mimi Hapa! Nasimama nikibisha hodi, ye yote anayesikia sauti yangu. Nakunifungulia mlango, nitaingia na kula pamoja nae, naye pamoja nami.” (Ufunuo 3:20)
“Ndio! Lakini pasipo na mazoea ya kumuhusisha Mungu.”

Mwingine “Kiasi fulani”
Mwingine “Nafikiri Kidogo”
Mwingine “Sina uhakika”
Mwingine “Kwa kiwango Fulani.”
Mwingine “Ish.”
Mwingine “Hapana mi ni Nusu mkristo (Baridi na moto)”

Katika “agano Jipya” tunahakikishiwa kuwa inawezekana sisi kujiamini na wokovu wetu na kwamba tuna uzima wa milele. Mtume Yohana anaandika “Nimewaandikia ninyi: ninyi mnaoliamini jina la mwana wa Mungu ili kwamba mjue mnao uzima wa milele.” (Waraka wa kwanza Yohana wa kwanza 5:13)

Kama Jinsi miguu mitatu ya kamera inavyoishikiria kamera, uhakika na uhusiano na Mungu wetu kuwa anasimama na sisi. Sawasawa tukiwa kama msingi pamoja naye, na pia tukijua kazi za Utatu Mtakatifu, (yaani Mungu Baba, mwana na Roho). Ahadi ambayo baba wa mbinguni ametupa. Pitia neno lake, kwa kupitia mwana wake kujitoa pale msalabani na kwa uhakika wa kutupa Roho Mtakatifu ndani ya mioyo yetu. Hivi vinaweza kuelezwa kwenye vichwa vya habari vitatu “visemavyo”     NENO LA MUNGU, KAZI ZA YESU NA USHUHUDA WA ROHO WA MUNGU.

NENO LA MUNGU
Kama tungetegemea sana hisia zetu, Tusingekuwa na uhakika kuhusu chochote maishani mwetu. “Hisia zetu huenda juu na kushuka Chini.” Kutegemea na mambo tuyawazayo ni mengi. Kama hali ya hewa au kama tunakula mlo kwa siku huwa vinabadilikabadilika.Tena mara nyingi hutuangusha. Lakini neno la Mungu halibadiliki kamwe na pia kuwa lipo dhahili.


Yesu ni nuru ya ulimwengu,akisimama kwenye moyo ambao una michongoma na magugu mengi yaliyokwishakua.Huyu ni moyo wa mtu mkaidi ndani ya maisha yake,lakini Yesu akiendelea kubisha hodi moyoni mwake ili afunguliwe. Anataka kuja ndani awe Sehemu ya maisha ya huyo mtu.Inawezekana ni wewe,basi usisite.Kwa maneno mengine tunahitaji kumfungulia Yesu aingie maishani mwetu.

Yesu huwa halazimishi njia zake kuingia ndani yako. Hutoa nafasi ya uhuru wako kuchagua. Ni juu yako kuchagua au kutochagua kufungua mlango wa moyo wako. Kama tukimfungulia yeye ana ahidi kuwa, “Nitakuja na kula pamoja naye, naye pamoja na nami.” Kula pamoja ni ishara ya Urafiki ambao Yesu humpa Kila anayemfungulia mlango wa mioyo yao na hukaa na kuishi pamoja naye.

Tunapomualika Yesu aje ndani yetu, anahaidi kutotuacha. Anasema kwa wanafunzi wake “Nipo pamoja nanyi daima.” (Mathayo 28:20) Tunaweza tusiwe na mawasiliano uso kwa uso, lakini yeye yupo pamoja nasi.Kama unafanya kazi na rafiki yako ndani ya chumba, mnaweza msiongee naye mara kwa mara. Lakini utatambua kuwa yupo pamoja nawe kwa uwepo wake. (utahisi uwapo wake upo nawe). Yeye yupo pamoja nasi.

Hii ahadi ya Yesu kuwa karibu nasi inafanana na ahadi nyingine kuu katika agano jipya.

      Yesu anaahidi kuwapa wanaomtafuta uzima wa milele (Yohana 10:28) Kama tunavyoona “uzima wa milele” katika kitabu cha agano jipya ni husiano na Mungu kupitia Yesu Kristo (Yohana 17:3). Yanaanzia wakati huu unapoishi ujazo wa uzima ambao. Yesu alikuja na kutupa uzima. (Yohana 10:10) Sio tu kwenye maisha haya na hata maisha yajayo yaani uzima wa milele.




Kuna maana nyingi sana unapokuwa unaongelea maisha ya Imani– Ni pamoja na“Kuwa mkristo aliyeokoka”, “kumpa yesu kristo maisha yako”, kumpokea Kristo. “Kumwalika Kristo”, “Kumuamini Kristo ni kumfungulia Yesu mlango wa moyo wako, yana tofauti nyingi haya maneno. Yote haya yanaelezea uhalisi kwamba Yesu anapoingia maishani mwetu kwa Roho. Mtakatifu, kama anovyotueleza kwenye mstari hapo juu.(ufunuo 3:20)

Yesu ni nuru ya ulimwengu,akisimama kwenye moyo ambao una michongoma na magugu mengi yaliyokwishakua.Huyu ni moyo wa mtu mkaidi ndani ya maisha yake,lakini Yesu akiendelea kubisha hodi moyoni mwake ili afunguliwe. Anataka kuja ndani awe Sehemu ya maisha ya huyo mtu.Inawezekana ni wewe,basi usisite.Kwa maneno mengine tunahitaji kumfungulia Yesu aingie maishani mwetu.

Yesu huwa halazimishi njia zake kuingia ndani yako. Hutoa nafasi ya uhuru wako kuchagua. Ni juu yako kuchagua au kutochagua kufungua mlango wa moyo wako. Kama tukimfungulia yeye ana ahidi kuwa, “Nitakuja na kula pamoja naye, naye pamoja na nami.” Kula pamoja ni ishara ya Urafiki ambao Yesu humpa Kila anayemfungulia mlango wa mioyo yao na hukaa na kuishi pamoja naye.

Tunapomualika Yesu aje ndani yetu, anahaidi kutotuacha. Anasema kwa wanafunzi wake “Nipo pamoja nanyi daima.” (Mathayo 28:20) Tunaweza tusiwe na mawasiliano uso kwa uso, lakini yeye yupo pamoja nasi.Kama unafanya kazi na rafiki yako ndani ya chumba, mnaweza msiongee naye mara kwa mara. Lakini utatambua kuwa yupo pamoja nawe kwa uwepo wake. (utahisi uwapo wake upo nawe). Yeye yupo pamoja nasi.

Hii ahadi ya Yesu kuwa karibu nasi inafanana na ahadi nyingine kuu katika agano jipya. 

       Yesu anaahidi kuwapa wanaomtafuta uzima wa milele (Yohana 10:28) Kama tunavyoona “uzima wa milele” katika kitabu cha agano jipya ni husiano na Mungu kupitia Yesu Kristo (Yohana 17:3). Yanaanzia wakati huu unapoishi ujazo wa uzima ambao. Yesu alikuja na kutupa uzima. (Yohana 10:10) Sio tu kwenye maisha haya na hata maisha yajayo yaani uzima wa milele.


Kufufuka kwa Yesu toka mautini, una maana nyingi sana:

1.  Kwanza, unatuhakikishia ushindi dhidi ya maisha ya kale kupitia kifo cha Yesu Kristo msalaba. Ufufuo siyo badala ya kushindwa bali ni tangazo la ushindi!

2 Pili unashuhudia kuwa “leo” yetu Yesu yu hai maishani mwetu (ndani yetu). Nguvu yake ipo pamoja nasi, inatupa uzima katika utimilifu wake wote.

3. Tatu, unashuhudia “kesho yetu” huu uhai tulio nao hauna mwisho, kuna uhai baada ya kifo histona ina maana au inajirudia, Inaelekea kuwa kwenye kilele cha utukufu.

       Siku moja Yesu atarudi duniani kuleta au kuanzisha mbingu mpya na nchi mpya (ufunuo 21:1). Na wale ambao wamo ndani ya Kristo watakuwa pamoja naa Daima (1 wathethelonike 4:17). Kutakuwa hakuna kulio huko, hakuna maumivu huko, hakuna majaribu tena, hakutakuwa dhambi. Tena hakuna mateso, hakuna kutenganishwa na wapendwa wetu (1 Korintho 13:12). Tutapewa miili yenye uzima ya ufufuo na isiyo na maumivu. Tutabadilishwa na kufanana naye Yesu Kristo (1 Yohana 3:2). Mbingu itakuwa ni sehemu yenye wingi wa furaha isiyo na mwisho.


KAZI YA YESU

Nilipokuwa chuoni, nilipitia kitabu kiitwacho “mbingu, sasa ninakuja”. Hapo mwanzoni, kama wengi wetu leo, nilifikiri kuwa haya ni madai ya kujigamba. Ingekuwa Kujigamba kuwa na ujasiri. Kutegemea na ujasiri wetu wenyewe. Kama watu wangekuwa waningia mbinguni kwa “Matendo mema” tumaini la kwenda mbinguni lisingekuwepo ndani yangu kabisa.

     Habari ya ajabu kuingia mbinguni ni kwamba hakutegemei na matendo yangu mema (yaani kuingia mbinguni hakutegemei mtu mwenyewe abaki anatenda mema), Inategemea na kile Yesu amenifanya maishani mwangu; Haitegemei na ninachofanya au juhudi zangu lakini kazi yake pale msalabani “Kitu alichofanya Yesu msalabani ndicho kilichotupa sisi uzima wa milele kama karama (Tiketi ya kwenda Mbinguni) (Yohana10:28; Warumi 6:23b) Hatuimiliki zawadi hii, Ila twaipokea kwa shukurani.

Japokuwa uzima wa milele ni bure, sio rahisi Ilimgharimu Yesu maisha yake kuyatoa kwetu. Tunapokea kipaji (zawadi) cha toba na Imani. Neno la “Toba” linamaanisha kubadilisha mawazo yetu. Kama tunataka kupokea kipaji hiki, tunahitaji kuweka vitu vyote kando ambavyo tunajua ni vibaya.

Hii ni vitu vinavyotuagusha na kutupeleka mautini(Warumi 6:23) Tunavyo jaribu kuviweka kando Biblia inatuambia kuwa ni “Toba” (Kubadili mawazo yetu). C.S. Lewis anaeleza kwamba “Kukubali, kujisalimisha kuomba msamaha, kutambua kuwa haikuwa njia sahihi na kuanza maisha mapya tena, ndiyo njia pekee inayosisitizwa kupitia”)

Imani ni nini? John Patton(182-907) (mtafsiri wa kitabu cha Yohana anasema “Imani ni kumtwisha na kumuachia kila mzigo tuliona Yesu kristo na alichotufanyia msalabani.

Jean –Francois Gravelet (1824-1907) anasema kuwa “Imani sio tu maneno au darasa, bali inahusisha kuchukua hatua makini ya kuweka imani yetu kwa Yesu.

Kama tukiikubali hii karama toka kwa Mungu na tusiwe wasiri juu ya jambo hili (Warumi 10:9-10) na tukilitambua jambo hili na watu wa Mungu(Ebrania 11:25) Siyo suala kwamba tunamiliki huu wokovu kwa kutubu kwetu, Imani na kukubaliwa kwetu na jamii; lakini hivi ni vyanzo tu ambavyo kwa hivyo twapokea kipawa hiki bure. Ambacho hakitokani na sisi ila Yesu.

Yote hayo yameanza na upendo wa Mungu kwetu “kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanae wa pekee, ili kila amwaminie asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16) Sisi sote tulistahili kupotea. Mungu katika pendo lake kwetu, aliona kuwa tumejiingiza kwenye uchafu ambao tumejiingiza, akaamua kumtoa mwanae wa pekee.

      Kwa upande mwingine, Yesu hakuwahi kufanya kosa lolote. Aliishi maisha ya ukamilifu. Hakukuwa na kikwazo kati yake na baba wa mbinguni. Pale msalabani, Mungu alihamisha makosa yetu, kwa Baba Yesu pale msalabani. Ndio maana Yesu alilia sana pale msalabani. “Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha“ (Marko 15:34); baada ya hapo alikufa sio kwa sababu alikuwa mwovu, ila kwa sababu yetu sisi.
Na hili jambo ndio limeondoa kikwazo kati yetu na Mungu, kwa wote wanaokubaliana na kuamini jambo hili. Lazima tuwe na uhakiki kuwa hakuna hukumu kwetu tunaamini jina hili la Yesu. Kama Mtume Paulo asemavyo “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu“ (Warumi 8:1) Hapa, sasa hii ni sababu ya pili inavyotuhakikishia kuwa tuna uzima wa milele kwasababu Yesu amefanya na kufanikisha mpango wa Mungu pale msalabani kufa kwa ajili yetu.

USHUHUDA WA ROHO MTAKATIFU

Mtu anapokuwa Mkristo (Ameokoka) Roho wa Mungu anakuja na kukaa na kuishi ndani yake, kuna vitu vikuu viwili vya kuangalia katika kazi za Roho wa Mungu ambavyo vitatusaidia kutambua Imani yetu ndani ya kristo.

Kwanza, hutubadilisha utu wetu wa ndani hutupa tabia na asilia ya Yesu ndani yetu. Hii huitwa “Tunda la Roho” Upendo, furaha, Amani, Uvumilivu, utu wema, uaminifu, upole na Saburi. (Wagalatia 5:22-23) Wakati Roho Mtakatifu anatujilia ndani yetu matunda haya huanza kukua.

Kutakuwa na mabadiliko ndani ya tabia zetu za kale, lakini si mabadiliko ya papo kwa papo.

Hali kadharika, mabadiliko haya yakiwa yanatokea, pia mabadiliko haya kwenye mahusiano yetu, kati ya Mungu na wandamu wengine. Tunaboresha pendo jipya kwa Mungu – Baba, mwana na Roho mtakatifu.

Mfano, unaposikia jina la Yesu kuna mabadiliko ya kihisia. Kabla ya kufanyika mkristo (Aliyeokoka). Nilikuwa nikisikiliza Redio na kuangalia Runinga na kusikia somo linalomhusu Yesu.

Nilikubali kumfuata kutokana na kwamba mtazamo wangu kwake ulibadilika Ghafla, Hii ni ishara ndogo ya upendo wangu kwake.

     Pia mtazamo wetu kwa wengine pia hubadilika. Ghafla, wakristo wengine pia hubadilika, Ghafla wakristo wengine wanashagaa kuona nyuso zinabadilika huko wanapokuwa kwenye mitaa na vituoni kabla ya wao kuwa na mapenzi na Yesu, sasa wanapenda kujua na kujali kiundani zaidi watu waliopotea na wenye huzuni. Niliona moja ya tofauti kubwa niliyonayo ni mtazamo, nilikuwa nikiwatenga wakristo wote wenye Imani lakini baadaye nilibadilika nakuwaona kuwa ni wazuri tu kama wakristo wangine. Nikaanza kuwa na urafiki nao wote ambao sikuwajua.
Vilevile mabadiliko ambayo tunaweza kuyaona maishani mwetu, ni kuwa Roho mtakatifu hutuonyesha ni jinsi gani Mungu alivyo. Hutufunulia na kutushuhudia kuwa sisi ni watoto wa Mungu. (Warumi 8:15-16)

Nina watoto watatu. Katika mawazo yangu, watoto wengi, huwa wanafanya kazi na kusoma siku za masomo! Ushauri mkubwa nawapatia, wasiwe wanasoma kwa biidii sana (kupata kiasi)! Chochote kinachosemwa na waalimu juu ya matokeo ya watoto wangu shule nasema wao wanaakili mno.Nilikumbuka nikiangalia matokeo ya binti yangu wa miaka 13, ambayo kwangu niliona nafuu, lakini yeye hakuridhika nayo.

Alikuwa akisema, Alipaswa kufanya vema zaidi katika somo la ki faransa na masomo mengineni.Mimi naona wewe bado ni bora. Pia hata nisingejali kama matokeo yangekuwa mabaya nakupenda sana binti yangu.

Nilipokuwa namwambia haya, ghafla nikasikia moyoni mwangu Mungu ananiambia, ‘Hivi ndivyo na mimi ninavyokupenda” Upendo wa Mungu kwetu ni mkuu mno kuliko ule wa mzazi kwa watoto wake. Siku zote nafikiria kufanya zaidi kitu kizuri, kwamba kwa kila kitu niwe mzuri lakini nafeli na kufeli tena na tena. Lakini bado Mungu hunikubali na ananipenda zaidi kwasababu tu ananipenda. Huu ni mfano wa ushuhuda wa Roho mtakatifu.
Njia ya tatu ambayo tunahakikishiwa na Roho mtakatifu uhusiano wetu na Mungu, na kuwa tumesamehewa na kuwa na uzima wa milele. Tunajua kwa sababu Roho wa Mungu hutushuhudia pamoja nasi vyote vinavyoendelea ndani yetu na kubadilisha kwa Roho na kuwa wana wa Mungu na kurithi uzima wa milele.
      Sio kwamba hatuna uhakika ni kile ambacho Mungu ametuahidi, kile ambacho yesu ametufilia, na kazi ya roho wa Mungu ndani ya maisha yetu. Na kwa sababu tumepewa kipaumbele kuwa watoto wa Mungu, tunapata ujasiri kuhusiana na uhusiano wetu na Baba wa Mbinguni, na kujua msamaha wake kwetu na kuwa na uhakika kuwa tuna uzima wa milele.
Maombi hayo utakayokwenda kufanya yatakusaidia kuwa na uhusiano bora na Mungu kama huna uhakika na maisha yako ya wokovu.

MAOMBI
Baba wa mbinguni, Samahani kwa vitu (mambo) nilivyofanya; nimekosa (Chukua muda wa kutubu kwa kila jambo ulifanya) Naomba msamaha. Nageuka mbali na kuweka kando kila ninachofikiria kuwa ni kibaya.

Asante kwa kuwa umemtuma mwana wa pekee Yesu Kristo afe kwa ajili yangu msalabani ili nisamehewe nitamtafuta na kumueshimu Mungu.

Asante kwa kunipa zawadi ya msamaha na Roho Mtakatifu. Sasa napokea karama hii.

    Naomba uje maishani mwangu kwa Roho Mtakatifu awe ndani yangu daima. Kwa jina la Mwana wako mpendwa Yesu Kristo, Bwana wetu, Amen!

Asante Sana! Karibuni Tena!