2011年2月21日 星期一

Mimi Nipo Hapa Duniani Kwa Kitu Gani?

Mwandishi: Rick Warren

Mkalimani:  Apostle Joshua Kuhanda



na

Erick C Nzowa




Africans Send Internationals (ASI)


Mchapishaji: Mch. Rebecca Sun



Yote Huanza na Mungu
Siyo kuhusu wewe. Kusudi la maisha yako ni mbali zaidi ya kutimiza matakwa yako binafsi,kuwa na amani yako,au hata kuwa na furaha yako. Ni zaidi ya familia yako, zaidi ya kazi au ajira yako au hata ndoto zako na matamanio yako. Kama unataka kujua kwanini uliwekwa katika sayari hii, lazima uanze na Mungu. Umezaliwa kwa kusudi lake (Mungu) na kwa ajili ya kusudi lake.

Utafutaji wa kusudi la maisha kumekuwa fumbo au chemsha bongo kwa watu kwa maelfu ya miaka. Hii ni kwa sababu, Tumekuwa tukianzia katika chanzo kisicho kabisa – sisi wenyewe. Tunajiuliza maswali ya ubinafsi au umimi maswali kama, “Nataka kuja kuwa nani? Je, nifanye katika maisha yangu? Je, malengo yangu ni yapi? Matamanio yangu ni yapi? Ndoto yangu ya baadaye ni ipi?

Lakini kujitizama sisi wenyewe hakutakuja kufunua kusudi la maisha yetu. Biblia inasema “Ni Mungu ayaelekezaye maisha ya viumbe vyake, maisha ya kila mmoja wetu yapo katika nguvu zake.” (Ayubu 12:10)

Tofauti kabisa na vitabu vingi maarufu,mikanda ya sinema na warsha vinavyo kuambia; huwezi kugundua maana ya maisha yako kwa kuangalia ndani yako mwenyewe. Unaweza kuwa umeshajaribu kufanya hivyo.Hukujiumba mwenyewe kwa hiyo hakuwa njia unayoweza kujiambia mwenyewe kwa sababu gani. Wewe uliumbwa! Kama nikikupatia kitu kilichoundwa ambacho hujawahi kukiona kabla, huwezi kujua kusudi lake, wala kitu chenyewe hakiwezi kukuambia isipokuwa Muumbaji pekee au mmiliki ndiyo awaweza kufunua kusudi lake.

Wakati mmoja nilipotea katika milima. Niliposimama kwaajili ya kuuliza uelekeo katika dira, nikaambiwa “huwezi kufika pale kutokea hapa.” Lazima uanze upande mwingine wa mlima” Vivyohivyo (Kwanyia hiyo hiyo), huwezi kufika katika kusudi la maisha yako kwa kuanza kwa kujitizama wewe mwenyewe. Lazima uanze na Mungu, muumbaji wako. Upo kwa sababu tu ni mapenzi yake uwepo. Umeumbwa na Mungu kwa ajili ya Mungu – na mpaka uelewe hilo, la sivyo maisha yako hayatakuwa na maana. Ni kwa Mungu pekee tunagundua asili yetu, tunapofanana uthamani wetu, kusudi letu, umuhimu wetu na hatima yetu. Njia yoyote nyingine inatuongoza katika mwisho mfu au mwisho wa kifo.

Watu wengi wanajaribu kumtumia Mungu kwa ajili ya kijihakikishia weyewe. Wanataka Mungu awe mtu anayetimiza au anayefanya matakwa yao binafsi. Lakini hiyo ni kinyume cha asili na inapelekea kushindwa. Ulitengenezwa kwa ajili ya Mungu, na sio vinginevyo, na maisha ni kumwacha Mungu akutumie kwa kusudi lake, na siyo kumtumia yeye kwa makusudi yako mwenyewe. Biblia inasema.” - (Warumi 8:6)

Nimesoma vitabu vingi ambavyo vinaeleza njia za kugundua kusudi la maisha yangu. Vyote vinaweza kugawanywa kama vitabu vya “msaada-binafsi” kwa sabau vinalianzia somo katika mawazo au wazo la ubinafsi. Vitabu vya “msaada-binafsi” mara kwa mara vinatoa makadirio sawa ya hatua za kutafuta kusudi lako la maisha: fikiria ndoto zako. Angalia wewe ni mzuri katika kitu gani. Bainisha uthamani wako. Weka malengo kusudia. Amini waweza kuyafikia. Uwe na nidhamu. Usikate tamaa.

Bila shaka, hayo mapendekezo yote ni mazuri namaranyingi yanapelekea mafanikio makubwa. Waweza kufanikiwa katika kufikia malengo kama utaweka akili yako katika hayo. Lakini kuwa aliyefanikiwa na kutimiza makusudi ya maisha yako havifanani kabisa, siyo kitu kimoja. Unaweza kuyafikia malengo yako yote, na kuwa aliyefanikiwa kwa vipimo vya dunia na bado ukakosa kusudi ambalo Mungu amekuambia wewe. Unahitaji zaidi ya ushauri wa msaada-binafsi. Yesu Kristo wakati mmoja alisema, “kujisaidia mwenyewe siyo msaada kabisa-(Mathayo 16:25) Ili kujitoa mwenyewe ndio njia, njia yangu, ndiyo njia yako, kujua wewe ni nani (Ukweli juu ya maisha yako). Hiki kitabu siyo tu kujua kipawa chako, kufikia ndoto zako, au kupanga maisha yako. Sio kukupa ratiba juu ya ulicho nacho. Ni kuhusu lengo lako, ukijua lengo lako hapa duniani itatupunguzia mzigo maishani mwetu na kututazamisha maishani mwetu kwa Mungu na jinsi anavyo taka sisi tuwe. Jinsi gani utatambua kusudi uliloitiwa hapa duniani? Una uchaguzi wa vitu viwili. Uchaguzi (Njia ya kwanza ni) “kubahatisha” au “Ubahatishaji”. Hivi ndivyo maisha siku zote mtu anaposema “nina malengo ……….” na pia wanasema, “haya ndiyo malengo yangu nadhani.” Kwa miaka elfu na elfu, wanafilosofia wengi wameongelea na kukisia juu ya jambo hili la maisha. Mwana Falsafa ni somo muhimu na lina matumizi yake, lakini linapofika suala zima la maisha, hata wale wana Falsafa wenyewe wanabahatisha juu ya jambo hili.

Profesa wa Falsafa Dr. hugh Moorhead aliwahoji wana Falsafa 250 mashuhuri wa wanasayansi na Wahadhiri maarufu na kukuta majibu ya swali kuhusu maisha yanakatisha tamaa hata walio wenye hekima na upole walishindwa. Lakini aliwauliza, Je, nigetambua kusudi la mimi kuwepo hapa duniani?

Hakika, njia nzuri ya kukisia hilo swali ni kujua kusudi letu la maisha na maana yake. “Njia rahisi ya kugundua kusudi la maisha ni “kumuliza muumba wa hivyo vitu ajielezee-(1Wakorintho 2:7)” Njia hii itakusadia kujitambua na kutambua kusudi la kuishi hapa duniani. Ni kutafuta na kujua Mungu anasema nini juu ya maisha yako kwenye Biblia. “Ufunuo huushinda ukisiaji kila siku.

Mungu hakutuacha gizani kamwe, tuhangaike na kubahatisha tu maisha. Na hii inatuonyesha sababu kuu tano za kusudi la maisha yetu kwenye Biblia. Inatuambia kuhusu kwanini tunaishi, jinsi gani maisha yanakwenda, nini cha kukiepuka na nini cha kutegemea kwa baadaye.

Mungu siyo tu ni mwanzo wa maisha yako; Mungu ni “chanzo” cha maisha yako. Ili kutambua kusudi la maisha yako unatakiwa kusoma “neno lake”, siyo tu makisio toka kwa watu mahiri, unatakiwa kujenga maisha yako kwa kukubali kubadilishwa na neno la kweli daima, siyo tu kwa wana falsafa au kwa vipindi vya mahojiano au semina za mafanikio, Biblia inasoma “Ni kwa Yesu tu ndipo tunapojua sisi ni akina nani na kusudi la kuishi kwetu-(Waefeso 1:11)! Mstari huu unatuembia vitu vitatu kuhusu kusudi letu.

1.  “unatambua kusudi la maisha yako na utambulisho wako kupitia uhusiano wako na Yesu Kristo.” Kama hufahamu nitakuelezea.

2.  “Mungu alikufikiria muda mrefu hata kabla hujamfikiria yeye.” Alipanga maisha yako kabla wewe hujakuwepo, bila mchango mwenzi wako, tabia zako, na kila sehemu ya maisha yako, lakini huwezi kuchagua kusudi lako.

3. “Kusudi la maisha yako latosha kuwa kubwa ulimwengu” (Kusudi la kiulimwengu) kwamba Mungu amekuumba udumu. Ndio kusudi la kitabu.

Pointi ya kushikilia:

Kama Mungu asingalikuwepo, kila kitu kingekuwa ni bahati mbaya, kusingekuwa na kusudi la wewe kuishi. Yote yanaanza na Mungu.

Maswali
Ø       Uliwahi kuwa na wasiwasi kuhusu, au kuhisi kuchanganyikiwa, kuhusiana na kusudi la maisha yako?
Ø       Je, umegundua nini kuhusu kusudi la wewe kuishi, ambalo kwa sasa halijaanza kutokea?
Ø       Kwanini unafikiri watu hujaribu kutambua kusudi la wao kuishi bila kumjua Mungu, muumba wao?
Kama umekwisha kujibu haya maswali au kutaka kuja
 Tembelea Tovuti yetu www.purposedrivenlife.com
Haupo Kwa Bahati Mbaya

Haupo kwa Bahati mbaya, na kuzaliwa kwako hapa duniani hakukuwa kwa bahati mbaya, wazazi wako hawakukupangia, lakini haimaanishi kuwa Mungu naye hakushiriki kukupangia wewe. Yeye hufanya hata pale kwenye udhaifu wa ki binadamu na makosa yake. Hakushangazwa na kuzaliwa kwako ila alikutarajia huko kuzaliwa kwako kwa nia nzuri tu.

Sio kwamba ni hatima, wala kwa pendekezo wala kwa bahati au kwa kujikuta tu unapumua pumzi mpaka sasa. “Unaishi kwa sababu Mungu anataka akutengeneze! Biblia inasema.” “Mungu atalitimiza kusudi lake kwa ajili Yangu.” - (Zaburi 138:8)

Mungu amekuchora na anajua kila sehemu ya mwili wako alivyoiweka. Yeye ndiye aliyechagua rangi yako, ya ngozi yako, na nywele zako, na kila wasifu wako. Amekutengeneza mwili wako kama vile alivyotaka. Vile vile amekukadiria kipawa cha tofauti ndani yako uweza kuwa na Upekee (Utofauti) wako mwenyewe utakaoumiliki. Bibilia imesema, “Ndiwe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu, unajua kila mfupa wa mwili wangu, unajua ni jinsi gani tabia zangu zilivyo,  jinsi nilivyotengenezwa toka kwenye utupu kuwa mwenye kitu. - (Zaburi 138;15)

Kwa sababu Mungu amekuumba kwa kusudi, pia ameamua lini wewe utazaliwa na kwa muda gani utaishi. Amepanga siku za maisha yako kwa kiwango cha juu, akijua muda wako wa kuzaliwa na kufa. Biblia inasema, “Nalikujua tangu tumboni mwa  mama yako na kupanga kila siku ya maisha yako hata kabla hujaishi. Kila siku unarekodiwa kwenye kitabu chake”. - (Zaburi 139:16)

Na Mungu pia alipanga wapi utazaliwa na wapi utaishi kwa kusudi lake kutimia ndani yako. Sura yako na utaifa wako haukua kwa bahati mbaya. Mungu hakuacha hata maelezo yoyote kuhusu wewe Biblia inasema “kutoka kwa mtu mmoja(adam) aliyaumba mataifa, ……….”-(Matendo 17:26). Na kila mmoja amemuandalia wakati wake, na kila mtu atakapoishi. Hakuna shida yoyote itakayotokea  kwenye maisha yako. Yote ni ili kusudi lake litimie.

Kitu cha kushangaza, Mungu aliamua ni kwa jinsi gani utakavyoumbwa haijalishi ni mazingira gani utapitia au umepitia wakati wa kuzaliwa au wazazi wako watakuwa kina nani? Mungu ana mpango katika kukuumba wewe haijalishi kwamba wazazi wako ni wazuri au wabaya au watofauti.

Watoto wengine wametupwa na wazazi wao, lakini Mungu hajawatupa. Kusudi la Mungu lilichukua makosa ya wanadamu, na dhambi zao daima (kifo cha Yesu). Hii haimaanishi kuwa Mungu husababisha dhambi au uovu (Ubaya) – Yeye si tabia yake lakini ni kwamba Mungu anafanya hivi ili tuokolewe kwa faida yake na yetu pia.

Kwa hiyo mbali na tukio la kuzaliwa kwako, unaweza kusherehekea kwamba Mungu amekuumba.

Kila mmea na kila mnyama alivipanga Mungu kwa kusudi lake, Na kila mtu aliumbwa kwa kusudi la Mungu. Wewe ni “mapenzi yake kwako”. Biblia inasema “kabla ya kuambwa kwa misingi ya ulimwengu na alitujua, alitutazama sisi akiangalia ahadi na mapenzi yake kwako. - (Waefeso 1:4)”

Mungu alikufikiria wewe kabla ya kuumba ulimwengu.Mungu aliutengeneza ulimwengu kwa sababu yako, pamoja na mazingira yake. Biblia inasema “Mungu ameamua kutupa sisi maisha kupitia neno lake  kweli,ili kwamba tuwe watu wa muhimu kuliko vitu vyote alivyoviumba”_(Yakobo 1:18). Hivi ndivyo ambavyo Mungu anakupenda na kukuthamini.

Mungu hayupo kinyemelanyemela, amepanga kila kitu kwa kusudi kubwa. Jinsi ambavyo wanafizikia, wataalamu wa viumbe hai, na wana sayansi wengine wanajifunza kuhusu dunia, na tunavyozidi kufahamu juu ya huu utofauti wetu na umuhimu wetu hapa duniani, Biblia inasema “Mungu aliumba dunia ………… hakuiumba tu ili iwe na utupu, aliiumba ikaliwa na watu. - (Isaiah 45:18)”

Kwanini Mungu alifanya haya yote? Kwanini alijisumbua kupitia njia hii ya uumbaji kwa ajili yetu? Hii ni kwa sababu yeye ni Mungu wa upendo. Upendo huu ni mgumu kwa kufikirika, lakini ndiyo upendo unaotakiwa, umeumbwa kuwa kiumbe cha Mungu chenye upendo. Huu ni ukweli kuhusu maisha yako na ndiyo unaokujenga.

Biblia inatuambia, “Mungu ni Pendo-(1Yohana 3:2)” Haijaandika kuwa Mungu ana upendo. Yeye mwenyewae ni Pendo! Upendo ni tabia ya Mungu. Sasa Mungu ni mkamilifu na mkamilifu kama alivyo, kwa hiyo hakuwa na haja ya kukuumba wewe ili kudhihirisha pendo lake kwako Mungu amesema, “Nalikujua kabla ya kukuumba, nalikulinda kabla ya kuzaliwa kwako, hata utakapokuwa mzee, sitabadilika, hata kama nywele zako zimebadilika rangi, nitakujali. Nimekuumba mimi mwenyewe na mimi mwenyewe nitakujali.

Kama kungekuwa hamna Mungu, wote tungekuwa ni “Bahati mbaya.” Kusingekuwa na kosa au wema, uzuri au ubaya au tumaini hapa duniani. Maisha yasingekuwa na maana na kifo ndiyo mwisho wa yoke.

Lakini una Mungu ambaye amekutengeneza kwa kusudi, na maisha yako yanakuwa na maana! Tunatambua kwamba maana na kusudi letu pekee kumfanya Mungu kama angalizo lefu. “Njia pekee ya sisi kujielewa ni kuwa jinsi Mungu alivyo na nini anachotufanyia.”
Nukuu ya Kuchukua
“Wewe hukuwepo kwa bahati mbaya.”
Maswali ya Kujiusisha
Ø   Kuna tukio gani la maisha ambalo unahisi kweli, wewe upo kwa kusudi hapa duniani?

Ø   Umewahi kujisikia au kuhisi kiundani: Upendo wa Mungu kwako kiundani?

Ø   Je, maisha yako yangekuwaje kama ungekuwa unaishi kila siku na ujasiri kuwa Mungu anakupenda sana na ana kusudi kwa maisha yako unayopitia?

Kwa mawasiliano zaidi ya maswali.
Ni kitu gani Kinakuendesha Maishani mwako.

Kila mtu anaendeshwa na kitu maishani mwake. Kamusi zinaelezea ile neno kuendeshwa kama “kukutawala, kukupelekesha au kukupelekea.” Kama unaendesha gari, ndege au meli, lazima ulitawale, na wakati huo huo unaliongoza wewe mwenyewe kupitia usukani. Nini Usukani wa maisha yako au nini kinakupelekesha maishani?

Sasa unaweza kuwa unapelekeshwa na tatizo, presha au madeni. Labda unapelekeshwa na kumbukumbu ya kimaumivu, uwoga unakufuatilia, au roho ya kutojiamini kuna mamia ya majanga, mawazoni mwako na hisia zako zinazoweza kuendesha maisha yako. Hapa kuna vitu tano mahimu:

1.   Wengi wanaendeshwa na majuto:
Wanakesha muda mwingi kujutia waliyoyafanya na kukimbia makosa yao wakijutia,wakificha aibu yao, majuto huwaendesha watu kwa kumbukumbu ya mambo.Majuto huwaendesha watu kwa kumbukumbu ya mambo waliyoyafanya. Wanaruhusu kumbukumbu zao za matukio waliyoyafanya kutawala kesho yao. Na pia kwa ghafla yanawatesa mno na kujilaumu wenyewe na kusababisha kujizuia wenyewe katika kusonga mbele; katika biblia tunamuona kaini alimuua mdogo wake, kwa hiyo ‘majuto’ yake, yalimufarakanisha yeye na Mungu na Mungu akasema “Utakuwa mtu wa mahangaiko duniani.” Hii inaashiria wengi wanamahangaiko leo bila kujua kusudi la maisha yao.

Sisi ni matokeo ya jana yetu, ‘lakini si wafungwa wa hiyo jana yetu. (jana yako isikutawale wewe). Kusudi la Mungu kwenye maisha yako .” haliwezi kuzuiwa na jana yako. Yeye alimbadilisha Muuaji aitwae Musa (Kutoka 2:12) kuwa “kiongozi mwenye moyo,” mtu mwenye uwoga aitwae Gideon kuwa “shujaa shupavu” (waamuzi 6, 7, 8). Na pia anaweza kufanya mambo ya ajabu na makuu kwako na maisha yako yote. Yeye huwapa watu mwanzo mzuri Biblia inatuambia “jinsi gani ilivyo furaha wenye dhambi wakiwa wamesamahewa ……… jinsi gani uponyaji ulivyo kwa wale waliotubu dhambi zao na Mungu amefuta rekodi za makosa yao.”
2.   Watu Wengi wanaendeshwa na “Maudhi”

Wanashikilia sana “Machungu” yao na kuyaweka moyoni bila kuyatoa. Badala ya kutoa machungu (Maumivu, maudhi,hasira kwa njia ya msamaha, wanayaacha yawachukue na kuyapa nafasi kutawala akili zao. Maudhi mengine yanawapeleksha watu kiasi kwamba “wanakuja juu” na kuchochea hasira zaidi wakati wengine “wanakurupuka” na kulipuka kwa wengine. Maudhi (uchungu) ni maumivu sana (kuweka vitu moyoni). Pia kwa mtu unamchukia, wakati huo aliyewaudhi ni mwingine amesahau na anaendelea na maisha yake, wewe unakazana tu kukumbuka yaliyopita, wakilea maumivu yao.

Sikiliza: Wale walikupa maumiivu siku za nyuma hawawezi kuendelea kukuumiza ‘sasa’. Endapo utaachilia maumivu. Yaliyopita yamepita! Hakuna kitakachoweza kubadilisha ya kale. Unajiumiza bure na hasira zako. Sasa, kwa faida yako, jifunze toka kwenye hayo, na pia yaachilie. Neno la Mungu lasema: “Kujiunganisha kujitabisha na kifo cha hasira ni ujinga usiyo na maana hata kidogo.”
3.  Wengi wanaendeshwa na “Mashaka”.

Haya mashaka yanaweza kutokana na matukio yakutisha na matarajio ya ki miujiza, ukikua katika kutawaliwa kwa hali ya juu. Ukiachilia mbali sababu, watu wenye kuendeshwa na mashaka wanakosa fursa nyingi za ki maisha kwa sababu ya mashaka yao. Badala yake wanaepuka hizo gharama na kujaribu kujilinda wasipate shida zaidi.

Self Mashaka ni “kufungwa kibinafsi” kiasi cha kutengua mbali na vile ambavyo Mungu Anataka uwe. Njia pekee ya kushinda mashaka ni kujipanga sawa sawa ukiwa na silaha ya “Imani na Upendo.” Biblia inatuambia “Upendo uliotengenezwa vizuri unaondosha mashaka. Kutokana na kwamba mashaka yanajongea kwenye kifo, Mashaka juu ya hukumu haijatengenezwa na upendo.”
4.  Watu Wanapelekeshwa na Vitu.

Mfano, vitu kama anasa na maisha ya starehe yanakuwa ni tamaa ya kumiliki vitu na ndiyo linalokuwa lengo lao la ki maisha. Hizi tamaa na mambo ya kutokuridhika yanatokana na Imani potofu ambayo inasema ukiwa na vitu vingi ndipo furaha inapokuja, ndipo raha ya maisha na ulinzi mzuri. Lakini haya mawazo yote ni ya uwongo. Umiliki wa vitu siku zote huleta furaha ya kitambo tu. Hii ni kwa sababu vitu hua havibadiliki, hivyo huchosha na baadaye utahitaji vitu vingine vipya, vikubwa na vilivyo bora zaidi kimuonekano.

Pia kuna Imani Potafu nyingine inayosema ukiwa na vingi ndiyo utakuwa mtu muhimu sana duniani. Kujithamini mwenyewe na kuthamini watu ni vitu viwili tofauti. Uthamani wako hautegemei tu vitu vyenye uthamani mkubwa. Mungu anasema utu una uthamani kubwa. Mungu anasema vitu vya muhimu sana kwenye maisha yako sio vitu vyenyewe!

Imani potofu fulani inasema,“Ninapokuwa na hela itanilinda sana. Si kweli, utajiri ni kitu kinachaweza kupotea ghafla au hata kuibiwa. Lakini ulinzi mzuri utapatikana tu kwenye kitu ambacho huanzi poteza wala kupokonya ni “Uhusiano wako na Mungu.”
5.  Wengi Wanaendeshwa na Matakwa ya        Kimadai.

Wana ruhusu matarajio yao wazazi wao au watoto wao au wachumba zao na kuwalinda na kuwaongoza katika maisha yao.

Ukweli ni kwamba siku zote wanaofuata makundi hupotezwa na hilo kundi. Sijui nini funguo za mafaniko,lakini funguo moja ya kushindwa ni kujaribu kumwomba kila mmoja kuwa unatawaliwa na mawazo ya watu ni inaweza ikakugharimu kumhonga  Mungu na kusudi lake juu ya maisha yako. Yesu alisema. “Hakuna mtu anayewatumikia mabwana wawili.”

Kuna vitu vingine vinavyoweza kuendesha maisha yako, lakini yote hupelekea mwisho mbaya, ni shida zisizo na muhimu, nguvu zisizotumika, na maisha yasiyokamili.

Hapo ni dhahiri kuwa hakuna kitu zaidi ya kujua kusudi la Mungu maishani mwakeo. Bila kusudi au engo, maisha ni mwendo usio na maana, shughuli kubwa bila dira, na matukio mengi yasiyo na sababu. Bila kusudi au lengo, maisha ni jambo la kawaida lisilo na maana.

Yafuatayo ni mambo matano (5) muhimu yatakayo kufanya ujue faida ya kutambua kusudi wewe kuwepo hapa duniani.

(1)   Kujua kusudita lako kunakupa maana ya maisha yako

Tumeumbwa tuwe na maana katika maisha yetu. Hii ndiyo maana watu wanatumia njia za kisasa, wakati maisha yanapokuwa na maana; unaweza kustahimili kila kitu, bila maana ya maisha hakuna unachoweza kustahimili.

Bila Mungu, maisha hayana kusudi, na bila kusudi, maisha hayana maana, na bila maana maisha hayana umuhimu, au tumaini. Ndani ya Biblia, watu wengi wameelezea huu kukata tamaa. Isaya alilalamika “Nimefanya kazi bila kusudi lolote, nimetumia nguvu nyingi daima na bila faida.” Ayubu naye amesema.” Maisha yangu yanaendeshwa siku hadi siku baada ya siku isiyo na tumaini.” Na nimekata tamaa, nimechoka kuishi. Maisha yangu hayana maana. Hasara kubwa hapa sio kifo ila ni maisha bila kusudi.

Kijana mmoja katika umri wake wa miaka ishirini aliandika, Najisikia kushindwa kwa sababu nafanya jitihada kuwa mtu fulani, lakini sijui chochote kuhusa huyo mtu. Ninachojua ni namna tu ya kuweza kukifikia hiko cheo. Siku moja, kama nikilitambua kusudi langu, nitajisikia kuwa nina uhai wa maisha.”

Tumaini ni kama kibebeo cha maisha kama vile tuonavyo hewa kwa maji. Unahitaji sana tumaini ili kuliishia hilo. Daktari aitwaye Bemie amegundua kuwa mmoja wa wagonjwa wake wa saratani, wanaenda kuruhusiwa “Je, unataka kuwa mmoja wa mamia?” Wengi waliokuwa wanafikiria ki maisha na wanaangalia kusudi walisema ‘ndiyo’, baadaye walipona. Tumaini huja kutokana na kusudi.

Kama unajisikia kukata tamaa, shikilia hilo tumaini! Mabadiliko mazuri yanakwenda kutokea katika maisha yako kama ulivyoamua kuliishi hilo husudi. Mungu amesema “Najua mawazo ninayowawazia …..-(Yeremia 29:11)” Ni mawazo mazuri wala si mabaya. Kuwapa ninyi tumaini siku za mwisho.” Unaweza kujisikia kuwa unakumbana na magumu na vipingamizi vingi, lakini biblia inatuambia “Mungu ….. anaweza kufanya vitu ambavyo hata sis tusivyoviwaza wala kuviomba, kuvihitaji, kuvifikiri au hata tumaini.”

(2)  Kujua kusudi lako hurahisisha maisha yako
Hii itakwambia nini fanya na nini usifanye maishani kusudi lako linakuwa msingi na kipimo cha maisha yako, nini ufanye (kitu gain ufanye au vitu gain usifanye). Lazima ujiulize. Je hii shughuli itanisaidia nitimize moja ya kusudi la Mungu maishani mwangu?

Bila Kusudi sahili maishani mwako huna msingi ulio bora ambao utakuwekaa maamuzi yaliyosahihi.Unagawa muda wako, na kutumia rasiliamali zako. Utahitaji kufanya maamuzi kutemgemea hali ulizo nazo, uzito wa hali halisi na jinsi unavyojisikia kwa wakati huo. Watu wengi wanafanya vitu wakitumia nguvu nyingi sana ndiyo inayo wasababishia msongo wa mawazo, uchovu na mafarakano ya moyo.

Hawezakani kufanya kila kitu ambacho watu wanataka ufanye. Una muda wa kutosha kufanya mapenzi ya Mungu Kama huwezi kulifanya hilo, maana yake unafanya kuliko vile Mungu alivyokusudia ufanye au kiukweli ukawa unapote za muda wako kwa njia nyingine. Maisha yenye kuendeshwa na kusudi ndio yana yorahisisha kuishi kwako. Pia hupelekea kwenye utulivu na amani ya mawazo (akili) yako-(Isaya 26:3) “Wewe Mungu hunipa utupae amani kikamilifu kwa hao wanaoweka kusudi lao imara na wanaoweka tumaini kwako.

(3)  Kujua kusudi lako hukutazamisha kimaisha
Inakupa umakini katika jitihada na nguvu yako kwa jambo lililo la umuhimu. Unakuwa Imara katika kufanya uchaguzi.

Ni kawaida ya wanadamu kusumbuliwa na vitu vidogovidogo.

Bila “kusudi” lililo sahihi bado tu utakuwa unabadilisha mwelekeo, kazi zako, mahusiano yako, kanisa na vitu vingine.

Nguvu ya kutazama kwa umakini huonekana katika mwanga uliozagaa.Una nguvu kidogo au hauna athari, lakini hukazia sana bidii ukiutazama kwa umakini kama vile kioo cha kukuza. Mionzi ya jua inaweza kutazamwa kwa umakini jinsi inavyoweza kuunguza karatasi ikiwekwa juu yake, hii ni zaidi unapokuwa na mionzi mikali inayokata hata chuma.

Hakuna kitu cha muhimu kama maisha yaliyo na mtazamo makini. Wanawake na wanaume wengi waliofanikiwa kutengeneza historia ni wale walioweka malengo ya kimtazamo kwa umakini na wakafanikiwa mmoja wa viongozi mashuhuri kwenye Biblia aitwaye Mtume Paulo anasema “ninatizamia kwa nguvu zangu zote kwa kitu hiki kimoja, nayachuchumilia ya mbele nikisahau ya nyuma nikitazama ile ahadi yangu.” Je wewe umefanya hivyo.

Kama unataka maisha yako yawe na athari kubwa, Yawe na mtazamo! Usihangaike. Usijaribu kufanya kila kitu, fanya kwa kiasi. Hebu jaribu kupunguza kila shughuli uzipendezo na fanya kila kitu chakuleta faida maishani mwako. “Usichanganye kazi na walishaji, unaweza ukawa bize bila malengo yoyote, lakini yote haya ya nini? “Hebu na tulitazamiea hilo lengo letu, kwasisi tunaotaka kila kitu ambavyo Mungu anatupatia sisi.

Ukijua kusudi, malengo yako yanakutia wewe nguvu maishani mwake

Lengo siku zote huzaa uvumilivu. Hakuna kinachachochea kama jinsi unapokuwa na maengo yanayoeleweka kwa upande mwingine, uvumilivu hupotea pale unapokosa lengo. Kwa kawaida ni kazi isiyo na maana. Sio kujitesa kwa kazi kubwa, ambayo ina kuchosha na hata kukumaliza nguvu hata kuondosha furaha yako.

George benard Shaw ameandika kuwa “Hii ndio furaha ya kweli katika maisha – kujitambua wewe na kusudi lako hapa Duniani, kuachana na ubinafsi na hasira pia hata malalamishi; kiasi kwamba hata ufanyeje Dunia hii haiwezi kukupa hiyo furaha.”
Kujua Kusudi Lako hakusaidia na KuKuandaa Kwa Uzima

Watu wengi wanatumia muda wao mwingi kutafuta umaarufu na vitu vinavyowaongezea muda hapa Duniani. Wanataka kukumbukwa wakiwa wamekufa hapa Duniani. Wakati huo, kitakachokuwa kinasumbua sio tu watu wanasema nini juu yako, ila Mungu anasemaje juu yao, watu wanashindwa kuelewa kwamba maendeleo ni vitu vinavyopita tu (vya muda), rekodi zimevunjwa, na mchango wao umesahauliwa.

Ukiishi maisha ya kutafuta umaarufu hapa duniani ni malengo yasiyo na maono. Hukuwa hapa duniani ili ukumbukwe. “Umewekwa hapa duniani kuandaliwa kwa ajili ya uzima.
Kwanza: “Umelifanyia nini jina la mwanangu Yesu Kristo?” Mungu hatakuuliza historia ya kanisa,dini yako au maisha yako ya wokovu. Kitu kimoja kinachojalisha,  Ulipompokea Yesu kristo, umemkubali kwa mambo aliyokutendea na umejifunza namna ya kumpenda na kumuamini yeye?. Yesu amesema, “Mimi ndimi njia, kweli, and uzima, mtu haji kwa Baba isipokuwa kwa mimi-(Yohana 14:6). Mungu anataka tujifunze kumjua, kumpenda na kumuamini mwana wake Yesu, ambaye ametumiwa duniani ili kuonyesha njia; kuwa Mungu ni nani na kutusamehe na kutuokoa.

Pili: “Umeyafanyia nini maisha yako?” Umefanyia nini na maisha ambayo Mungu amekupa vipawa - vipawa vyote ambavyo Mungu amekupa – fani yako, fursa, nguvu; uhusiano, na rasilimali zako? Je, ulivitumia hivyo kwa ajili yako, au ulivitumia kwa kusudi la Mungu kwenye maisha yako? Jiandae kwa haya maswali mawili kupitia kitabu hiki,  swali hili linategemea, Umetumia muda wako hapa duniani kuandaa maisha yako ya uzima?.Je uko na Mungu au umejitenga naye. Swali: la pili, una malengo gani katika kuingia uzimani. –Wajibu wako na malipo yako mbinguni. Mpaka kufika mwisho wa kitabu hiki utaweza kuyajibu maswali haya yote mawili.
Maswali ya Kujihusisha

Ø  Ukiuliza familia na marafiki zako nini kinawapalekesha maisha yao, unafikiri watakwambia nini?

Ø  Unafikiri kwanini watu hawapendi kuweka malengo yao?

Ø  Ni Tabia gani, maumivu au mashaka yanayo kutenga we we na Mungu wako na kusudi lake kwako?

Tembelea tovuti yete: WWW.purposedrivenlife.com.
Umeumbwa Udumu Milele
Haya maisha sio t undo yaliyopo maisha hapa duniani ni mazoezi tu ya maisha yenyewe halisi ya baadaye. Una uwezo kutumia muda mwingi kuishi maisha yasiyozaa au maisha ya kifo au ukaishi maisha ya uzima. Dunia ni eneo la ukumbi wa mazoezi, na pia ni kama shule ya awali. Majaribio ya maisha yako kuingia uzimani ni sehemu ya mazoezi ya nguvu kabla ya mchezo wenyewe; au sehemu ya mazoezi ya viungo kabla mwendo haujaanza. “Haya ni maandalizi ya maisha yajayo.”

Zaidi ya yote, utaishi walau miaka mia moja hapa duniani, lakini utaishi zaidi daima kwenye uzima (mbinguni). Muda wako hapa duniani, ni kama bwana Thomas Browne anavyosema “Muda wako hapa duniani ni kama mabano kuingia uzimani.” Umeumbwa udumu milele.

Biblia inasema, “Mungu ameandaa uzima kwenye moyo wa mwanadamu-9Mhubiri 3:11)” Una tabia za kiungu ndani yako, za kudumu kwa muda mrefu bila kifo. Hii ni kwa sababu Mungu amekuumba, kila mmoja wetu lazima afe, kifo wakafi mwingine kinakuwa sio halisi na sio cha haki. Sababu kwanini tunafikiria kuishi na kudumu daima ni kwamba Mungu ametuunganisha fahamu zetu ili tuwena hayo mawazo.

Siku moja moyo wako utaacha kudunda. Hiyo ndiyo itakuwa siku yako ya mwisho hapa duniani, mwili na muda wako kuishi. lakini hautakuwa mwisho wako wewe. Mwili wako wa duniani hapa ni wa muda mfupi tu, lakini wakili pekee ni Roho yako. Wito wa Mungu kupitia neno lake ni mwili wako wa duniani kama “hema” yake. Pia ameifananisha kama “nyumba” Biblia inasema “Wakati hema hili tumeweka makazi yetu – miili yetu hapa duniani – inachakaa, Mungu atakuwa na nyumba yake nyingine mbinguni kwetu sis kuishi ndani yake (ametuandalia makao mapya) ambayo hudumu daima milele.”

Maisha hapa duniani hayatupi nafasi yoyote ya kuchagua, lakini maisha ya mbinguni yanatupa nafasi mbili 1) “Mahusiano yako na Mungu hapa duniani, yatategemea na ndio yanayotazamia uhusiano wako na yeye huko mbinguni.” Kama unajifunza kumpenda na kumwamini mwana wa Mungu (Yesu). Utahakikishiwa kuishi naye daima milele Mbinguni. Kwa upande mwingine ukimkataa yeye na pendo lake, msamaha na wokovu, hautaufurahia na hutaingia Mbinguni.

Professa mashuhuri wa Oxford na mwandishi wake C.S Lewis amesema - Kuna watu wa aina mbili: kuna wale wanaosema kwa Mungu, “Mapenzi yako yatimie” na wale wanaosema kwa Mungu. “Haya basi, fanya unavyojua mwenyewe”. Ki ukweli ni kwamba watu wengi wamechagua kuishi bila Mungu hapa duniani.

Wakati unapokuwa umeelewa vya kutosha kwamba hakuna maisha, wakati huu na sasa, na unapokuja kuelewa kuwa maisha haya ni maandalizi ya maisha mapya ya mbinguni, utaanza kuishi maisha ya tofauti (Misingi ya kimaisha). Utaanza kuishi katika mwanga wa uzima, na utaanza kujali mahusiano na watu, kila kazi, kila matatizo. Ghafla kila zoezi kazi, lengo na hata matatizo ambayo yanaonekana hayana muhimu kutokea. Unavyozidi kuwa karibu na Mungu ndivyo unavyoona matatizo yako yanapungua.

Ukiishi katika mwangaza wa uzima, uthamani wako unabadilika. Unatumia maisha yako na pesa zako kwa umakini. Unakuwa na nafasi nzuri ya mahusiano na kitabia unabadilika badala ya kuwa na umaarufu (Kujisifu) utajiri,mafanikio au hata kustarehe. Vitu unavyovipa kipaumbele ndivyo vinavyonukuliwa na Mungu mambo unayoya tanguliza kama mitindo au kujithaminisha mwenyewe hayajalishi sana kama unavyojitoa katika kazi ya Mungu.
Kama muda wako hapa duniani ulikuwa tu kwa ajili yako mwenyewe. Nakushauri uyaache haraka iwezekanavyo unasahau kuwa mwema na kusahau hata maadili yako na pia unaweza hata usijue makosa ya matendo yako utakuwa mtu mbinafsi, kimawazo na hautakuwa mtu mwenye faida. Lakini hii haina maana kwamba – kifo si mwisha wako. Kifo siyo hatima yako, lakini ni mabadiliko yako kuelekea uzimani kila tendo maishani mwetu lina athari kubwa katika maisha ya uzima.
Kitu au umbile lililoathiriwa na rika moja ni kuishi bila kuona mbele ili kufanya maisha yako yote, (kuwa na maisha safi). Ni maisha ya baadaye toka sasa! Uzima sio tu kuona mambo ya chini ya Dunia. Je, maisha yanafanana vipi tukiwa mbinguni (uzimani) na Baba yetu?. Kwa uwazi, nawaambia ubongo wetu hauwezi kukamata na kuweka kichwani huo ukuu alionao na maajabu huko mbinguni. Ni kama unajaribu kumuonyesha sisimizi mtandao wa Internet. Hakiwezakani hicho kitu. Bibli inasema “Hakuna mwanadamu aliyesikia wala kuwahi kufikiri, Jinsi gani ukuu wa Mungu ulivyo na hata sasa umeandaliwa kwa wanaomuamini na kumpenda Mungu-(1 Wakorintho 2:9)”
Hata hivyo Mungu ametupa vidokezo vya Mbinguni toka kwenye Neno lake (Biblia). Tunajua kuwa mpaka sasa Mungu anatuandalia makao mapya huko juu mbinguni tutakutana na wenzetu waliopata machungu na mateso, wakiwa wametunukiwa na zawadi ya uaminifu wao hapa Duniani, na wameacha kufanya kazi zao na kufanya ya Mungu. Ila tunafurahia ushirika na Mungu usio na mwisho, unadumu milele. Siku moja Yesu alisema “Njooni ninyi mliobarikiwa na baba yangu, njooni mrithi ufalme ambao mmeendaliwa tokea kuumbwa kwa ulimwengo. - (Mathayo 25:34)”
Mungu anakusidi maishani mwako hapa duniani, lakini haishii tu hapa, mipango yake inahusisha mpaka kufikia karne zote utakazoishi hapa duniani. “Ni fursa ya kimaishi hii” Mungu anatupa fursa ya kimaisha. Biblia inasema “Mipando ya Mungu ni kudumu. Kusudi lake ladumu daima. - (Zaburi 33:11)”
Muda pekee ambao watu wanafikiri kuhusu uzima ni wakati wa msiba, na pia ghafla inafifia maazo yaliyofungwa, wengi wanachochea mawazo, yaliyo ya kipumbavu (Ujinga). Unaweza ukaona ni vibaya kuweza juu ya kifo, lakini kwa kifupi ni vibaya kuwa na mawazo ya kutokufa na sio kuangaia ambalo haliepukiki. (lisilozuilika) Ni mjinga peke yake ndie anayepitia maisha hayo ya kuto kujiandaa kwa kitu ambacho tunajua ni lazima kitokee tu unahitaji kufikiri juu ya uzima, na sio kingine.
Kama jinsi ambavyo ulivyodumu miezi 9 tumboni mwa mama yako. Haikuwa mwisho ila kukuandaa wewe kwa maisha yajayo. Kwa hiyo huu uhusiano na Mungu kupitia Yesu ni njia kuelekea Mbinguni. Itakuwa ni saa ya mwisho wewe kuishi hapa duniani, lakini hautakuwa mwisho wako wewe. Itakuwa ni sikukuu yako ya kuzaliwa kwenye uzima wa milele. Biblia inasema “Huu ulimwengu sio wetu, tunasonga mbele kuelekea uzimani (nyumbani kwetu) Mbinguni-(11 Wakorintho 5:6).
Kipimo cha uzima, muda wako hapa duniani ni unavyopepesa tu macho yako, lakini matokeo ndiyo yatakayodumu daima. Matendo ya maisha yetu tuishiyo ndiyo hatima yetu kwa maisha mengine. Lazima tutambue kwamba kila wakati tunapotumia au tunavyoishi katika miili ya duniani ni muda tuliokwisha utumia hapa duniani ndio ambavyo tunapoteza mbingu yetu na Yesu kristo.
Miaka ya nyuma kulikuwa na msemo unaowafariji watu kuishi kila siku kama “Siki ya kwanza ya kila siku maishani mwako.” Kwa kifupi, itakuwa hekima zaidi kama kila siku tuishi kana kwamba ni siku ya mwisho ya maisha yako. Ni kila siku yatupasa kuishi maisha ya aina hii kwamba kila siku tujiandae kwa siku ya mwisho.
Pointi ya Kushikilia
“Maisha Siyo Kitu cha Kila Siku”
Maswali ya Kujikumbusha
Ø  Kwanini unafikiri Mungu ametuumba ili tudumu?
Ø  Kwanini unatumia muda mwingi kuwa na wasiwasi na kitu ambacho hakidumu na cha muda mfupi katika maandalizi yako. Kwenda uzimani, ambayo yanadumu daima?
Ø  Unafanya nini sasa hivi kwa ajili ya uzima wa milele (Maandalizi yako)?
Kama unahitaji pitia au kujibu maswali, tembelea Tovuti yetu www.purposedrivelife.com.

Kuona Maisha kuko na Mtazamo wa Kimungu
Jinsi unavyoona maisha yako ndivyo unavyoumba maisha yako. Jinsi unavyoyafafanua maisha yako ndivyo unavyoikusudia hatima ya maisha yako. Twasira yako ndiyo itakavyo kushawishi wewe namna ya kuwekeza muda wako, namna ya kutumia pesa yako, kutumia vipaji vyako na mahusiano yako.
Njia bora mojawapo yakuwaelewa wengine ni kuwauliza “Unaonaje maisha yako?. Utatambua majibu yao kuwa ni tofauti na ulivyouliza swali lako. Nimeambiwa kuwa maisha “ni mduara”, ni eneo la madini, ni bahari, ni msamiati, ni huzuni, ni safari na wengine wanasema maisha ngoma ya kucheza. Watu wamesema, “Maisha ni mzunguko.” Wakati mwingine upo juu, wakati mwingine upo chini na mduara unaendelea au maisha ni kama baiskeli yenye gia lakini hatuitumii hizo gia “maishani ni kama karata za kucheza.” Unatakiwa kucheza huo mchezo.”
Kama nakuuliza twasira ya maisha, ni tafsiri ipi ina kuja kichwani? Hiyo twasira ndiyo mabadiliko yako. Ni ule mtazama wa kimaisha ambao unao au unaushikilia, kwa kufahamu au kutokufahamu ndani ya akili yako. Ni mchoro (muonekano) jinsi gani maisha yanafanya kazi na unatarajia nini kutoka kwenye hicho. Watu wanaelezea maisha yao ya mzunguko kwenye nguo, mawe ya thamani, magari nywele, michoro nakadhalika.
Hayo maisha ya mabadiliko yasiyoelezeka yanakuvuta (athiri) maisha yako kuliko unavyofikiri. Inatazamia matarajio yako, malengo yako, na vipaumbele vyako kwa mfano, ukitazama maisha kama pati, ujue kwamba msingi wa mawazo yako ni “Kustarehe”. Kama unaona maisha ni mashindano, ujue tu kuwa utathamini mwendo wako na kutumia muda wako vizuri. Kama utatazama maisha yako kama marathon. (mashindano ya kukimbia, unathamini “kudumu.” Kama unaona maisha ni vita au mchezo, kushinda ndio kitu cha muhimu sana kwako je nini mtazama wa maisha yako?
Umewahi kujiuliza nini mzunguko wa maisha yako? Unaweza kukitoa hicho toka kwa wazazi wako, kutoka kwa rafiki zako, kutoka kwenye runinga au sinema unazoangalia au magazeti unayosoma, au kutoka kwenye vyazo vingine. Lakini ili kutimiza kusudi la Mungu, ambalo amekuitia, unahitaji kupambana na changamoto za hekima na kuzibadilisha na maisha ya mabadiliko ya kimungu. Biblia inasema “msiipende Dunia na mambo yaliyo ndani yake, lakini acha Mungu mwenyewe akubadilishe ndani yako, kwa mabadiliko ya akili (fahamu) zako. Ndipo utakapajua mapenzi ya Mungu.”
Biblia inatoa mabadiliko ya aina 3 ambayo yanatufundisha sisi mtazamo wa ki Mungu maishani. Maisha ni Jaribio, maisha ni uaminifu, na maisha ni utendakazi wa muda mfupi. Mawazo haya ni msingi wa kusudi lako la ki maisha. Tutaangalia milango miwili ya mwanzo na mlango wa tatu unaofuata.
Maisha hapa Duniani ni majaribio, Maisha haya ni kitendawili inapatikana katika habari za Biblia,  Mungu aliendelea Kujaribu tabia za watu, Imani, utii, upendo, uadilifu na upole. Maneno kama hukumu, majaribu, utakaso na majaribio yametokea kama mara 200 kwenye neno la Mungu. Mungu alimjaribu Ibrahimu kwa kumwambia amtoe mwanae wa pekee Isaka. Mungu alimjaribu Yakobo katika kuendelea kufanya kazi miaka mingi kwa ajili ya Raheli ili awe mkewe. Biblia pia inatupa mifano mingi ya watu ambao wamepitia majaribu ya kibinafsi ya tabia zao kama Yusufu, Lutu, Esta, na Danieli.
Tabia zinaboreshwa na kudhihirishwa kwa njia ya Jaribio, na maisha siku zote ni Jaribio “Siku zote unajaribiwa.” Mungu siku zote huangalia jinsi fani unavyokabiri watu, shida mafanikio, magonjwa malumbano, kujilaumu na pia hali ya hewa. Anaangalia hata matendo madogo madogo kama vile unafungua mlango kwa wengine, unapookota takataka au unapokuwa mpole kwa mfanyakazi wako.
Hatujui jaribio lolote ambalo Mungu atatupa, lakini tunaweza tabiri baadhi yao, kulingana na Biblia. Utajaribiwa kwa mabadiliko makubwa, kwa ahadi zisizotimia, kwa matatizo yasiyo tatuliwa, kwa maombi yasiyojaribiwa, kwa makosa yasiyostahili kwangu na hata kwa majanga mbalimbali. Katika maisha yangu nimetambua kwamba Mungu anaijaribu Imani yangu kwa jinsi ninavyokabili mali na hujaribu upendo nilionao kupitia watu.
Jaribio kuu kwa na la muhimu ni jinsi unavyotenda (unavyokuwa) unaposikia uwepo wa Mungu kwenye maisha yako. Wakati mwingine Mungu kwa makusudi anarudi nyuma na pengine hatusikii huwa uwepo. Mfalme aitwaye Hezekia aligundua jaribu lake Biblia inasema Mungu aliondoka na kumwacha Hezekia ili kuujaribu moyo wake ili kujua nini kipo moyoni mwaka Hezekiah amefaidi sana kuwa na ushirika wa karibu na Mungu, lakini tunaona Mungu alimwacha peke yake kujaribu tabia yake, kuudhihirisha udhaifu wake. Na kumuandaa kwa majukumu mengine Zaidi.
Ukishaelewa kuwa maisha ni Jaribio, utatambua kwamba hakuna kitakachokushinda maishani kwa kuboresha tabia yako. Kila siku ni siku ya muhimu kwako na kila sekunde ni hatua ya ukuaji kukuzamisha ndani ya hiyo tabia yako (moyoni mwako) Kuendeleza upendo wako au kumtegemea sana Mungu. Majaribu mengine yanatia moyo lakini mengine hayaelekei. lakini yote yana lengo kukupa uzima wa milele.
Habari njema ni kwamba Mungu anataka wewe ufaulu mitihani (majaribio) Yote ya maisha yako. Kwa hiyo usiruhusu hayo majaribu kuzidi hiyo neema aliyokupa ili kuyakabili hayo majaribu. Biblia inasema, “Mungu huiweka ahadi yake, na yeye haruhusu ujaribiwe kupita uwezavyo, kusimama imara; katika muda ambao wewe upo kwenye majaribu, atakupa nguvu ya kuyashinda, na kwa hiyo atakupa mlango wa kutokea.”
Kila wakati unapopitia majaribu, Mungu analitambua na kuandaa mpango wa kukuzawadia uzima wa milele. Biblia inasema, “heri wanaoshinda majaribio wanapokuwa wanajaribiwa. Wanapofanikiwa kupita hiyo majaribu, watapokea taji la uzima ambayo Mungu ameahidi kwao wampendeo.”
Maisha hapa duniani ni uaminifu. Hii ni Safari ya pili ya ki maisha tunayoipata kwenye Biblia. Nguvu zetu, ki muda, fursa, uhusiano na maliasili,  vyote ni zawadi toka kwa Mungu.Mungu ametujua kuwa tunamjali. Sisi ni watumishi au maneneja wa kila tunachopewa na Mungu (mawakili). Elimu ya utumishi inaanzia pale tunapotambua kwamba Mungu ni mmiliki wa kila kitu na kila mtu hapa duniani. Biblia inasema, “Dunia na vyote vijazavyo ni mali yake, nchi na vyote vijazavyo ni vyake.”
Hatutamilika kitu chochote kipindi hiki tupo hapa duniani. Mungu tu anatukopesha wakati tupo hapa duniani. Ni mali ya Mungu hata kabla hujawepo hapa duniani, na Mungu atamkopesha mtu mwingine baada ya wewe kufa utavifaidi kwa muda tu.
Mungu alimuumba Adam na Hawa, aliamini uumbaji wake unaweza kutunzwa na hao Adam na hawa, ndiyo maana akawapatia hizo mali. Biblia inasema, “Mungu aliwabariki na akasema, zaeni mkaongezeke, ili kwamba kizazi chenu kiishi katika ulimwengu huu na kutawala. Ninawakabidhi hivi vitu.”
Kazi ya kwanza ambayo Mungu anampa mwanadamu ni kutunza (kumilika na kutawala) uumbaji wake duniani kazi hii haikubatilishwa. Ni sehemu ya kusudi letu leo. Kila tunachokifurahia ambacho Mungu ameweka mkononi mwetu. Biblia inatuambia, “Una nini ambacho Mungu hajakupatia?.
Miaka imepita, wana ndoa fulani marafiki walituachia mimi na mke wangu tutumie ufukwe mzuri mbele ya nyumba yao huko Hawaii kwa ajili ya likizo yetu. Ilituletea uzoefu ambao ulituzidi maarifa, (ulitufundisha) na tulifurahia mno kwa shukrani. Tuliambiwa “Tuitumie hiyo fukwe kama ya kwetu.” Kwa hiyo tulifanya hivyo! Tuliogelea kwenye bwawa la kuogelea,na kuchukua chakula toka kwenye Jokofu,na kutumia mataulo kuogea na ndoo, na hata kulala!. Lakini tulijua saa zote hivi vitu tulivyopewa kwa muda, havikua vyetu, kwa hiyo tuliviangalia kwa umakini. Tulifurahia kuvitumia vitu kwa umakini. Tulifurahia kuvitumia vitu kwa faida yetu bila sisi wenyewe kuvimiliki.
Akili zetu za kibinadamu zinasema “kama sikimilika, Sina haja ya kukijali.” Lakini Mungu anataka tuishi kwenye viwango vya juu.” Kwa sababu Mungu anamiliki uumbaji, natakiwa kuwa nacho makini sana kwa uwezo wangu wote. Biblia inasema, “Wale walioaminiwa kwa vitu vya themani sana wanatakiwa waonyeshe jinsi gani walivyo waaminifu.” Yesu mwenyewe amesema maisha siku zote ni uaminifu na pia ametaja habari nyingi kuhusu uwajibikaji wetu kwa Mungu. Katika habari ya talanta, mfanyabiashara aliweka imani yake kwa mfanyakazi wakati akiwa ameondoka. Akiwa amerudi, anapiga mahesabu ya kila wajibu uliofanyiwa kazi na kuwapa thawabu kwa kazi walioifanya mmiliki atasema, “Kazi njema, wakili mwaninifu! Umekuwa mwaminifu kwa mambo madogo, nitakuweka kwenye mambo makubwa. Njoo ufurahi pamoja na Bwana wako.”
Siku ya mwisho hapa duniani utahesabiwa au utatoa hesabu ya maisha yako na baada ya hapo utazawadiwa kulingana na wema ulioutenda na nini Mungu amekupa. “Hii inamaana kwa kila kitu unachofanya, hata kama kitu kidogo, kina matokeo yake.” Ukifanya kila kitu kwa uaminifu.Mungu ana ahidi kukupatia vitu vitatu kwenye ufalme wake. Kwanza, utapokea “Uthibitisho” toka kwa Mungu mwenyewe: atasema, “Kazi njema!  Hongera sana!” Kingine utapokea “Kupandishwa cheo” na atakuweka kwenye majukumu makubwa zaidi kwenye uzima.” “Nitakuweka katika mambo makubwa” Mwisho utaheshimiwa kwa kufanyiwa “Sherehe”. “Njoo ufurahi na Bwana wako.”
Watu wengi wanashindwa tambua kwamba pesa ni vyote, Jaribio na pia ni “Uaminifu” toka kwa Mungu. Mungu anatumia uchumi wetu kutufundisha kumtegemea yeye. Na watu wengi, hela ni jaribu lao kubwa. Mungu huangalia jinsi gani tunatumia pesa kujaribu uaminifu wetu. Yesu alisema, “Kama hatutakuwa waaminifu kwa mali za dunia, nani atakuamini katika mali za utajiri wa mbingu?”
Hili ni jambo la muhimu sana, watu wengi hawapo makini katika hili Mungu anasema kuna uhusiano wa moja kwa moja jinsi ninavyotumia mali zangu na maisha ya kiroho! Jinsi ninavyotunza utajiri wa duniani ndivyo inavyotazamiwa na Mungu kwa jinsi gani atakavyo kupa Baraka za Rohoni (Utajiri wa kweli). Labda nikuulize: Jinsi gani ambavyo unalinda pesa zako kuzuia Mungu asifanye zaidi maishani mwako? Je Mungu anaweza kukuamini na Baraka zake za Rohoni?
Yesu alisema kuwa kila mmoja amepewa kwa kipimo, na kipimo hicho kitadaiwa, na kwa yale aliyepewa kipimo cha kutosha, kipimo hicho kitadaiwa.” Maisha ni jaribio na uaminifu, na kipimo ambacho Mungu anakupa ndicho kipimo ambacho anategemea zaidi toka kwako.
Pointi ya Kushikilia
Maisha ni Jaribu na pia uaminifu.

Maswali ya Kujiuliza
Ø   Umechora vipi maisha yako?
Ø   Unaweza kufikiri jinsi gani ulivyopitia wakati unajaribu ukaona kuwa Mungu alikuwa anakujaribu?
Ø  Kama ulikuwa unaanza kuiishi kweli kwamba kila kitu unachomiliki umekopeshwa na Mungu, ungejisikiaje kuhusu umiliki wa vitu?
Tembelea Tovuti yetu www.purposedrivenlife.com
Maisha ni Wajibu wa Muda Mfupi
Maisha duniani ni wajibu wa muda mfupi. Biblia imejaa mtindowa usemaji ulinganishao bila kutumia vilinganishi (sitiari) ambao unafundisha kuhusu ufupi, muda kidogo au asili ya maisha yasiyo dumu hapa duniani.
Maisha yanatafsiriwa kama ukungu au umande kama kitu kikimbiacho haraka sana, kama hewa au pumzi na pia kama moshi. Biblia inasema “kwa huwa tumezaliwa kama jana… . Siku zetu duniani zatoweka kama kivuli.” (Ayubu 8: 9)
Kufanya matumizi mazuri ya maisha yako, lazima kamwe usisahau kweli hizi mbili: Kwanza; kulinganisha na umilele, maisha ni mafupi sana. Pili, dunia ni makao ya muda mfupi tu. Hutakuwa hapa muda mrefu, kwa hiyo usijishikize sana. Muombe Mungu akusaidie uyaone maisha ya hapa duniani kama yeye ayaonavyo. Daudi amesema, “Bwana nisaidie kuzitambua siku zangu za kuishi hapa duniani zilivyo chache. Nisaidie kujua kwamba nipo hapa kwa kitambo tu.” (Zaburi 39: 4)
Kwa kurudia rudia Neno la Mungu limefananisha maisha ya duniani na kuishi kwa muda mfupi katika nchi ya ugenini. Hapa siyo nyumbani kwako pa kudumu au hatima yako ya mwisho. Unapita tu, umetembelea tu dunia. Biblia inatumia maneno kama aliye mgeni, msafiri, mhamiaji, ngeni usiyejulikana hapa, mtembeleaji na msafiri ukaaji wetu mfupi duniani. Daudi amesema, “mimi ni mgeni hapa duniani.” (Zaburi 119: 19) Na mtume Petro ameelezea, “Kama mnamwita Mungu baba, uishini muda wenu kama wakaaji wa kitambo tu duniani.”
Katika California ambako ninaishi, watu wengi wameenda au wakuja kutoka sehemu nyingine za dunia kuja kufanya kazi hapa, lakini wanatunza uraia wa nchi zao za nyumbani. Wanahitaji kubeba kadi ya mgeni kitambulisho cha mgeni kiitwacho “Kadi ya kijani” au “green card”, ambayo inawaruhusu wafanye kazi hapa hata kama wao siyo raia wan chi hiyo.
Kwa kweli, wote tunatakiwa tubebe kadi zetu za kijani za kiroho kwa kutambulisha uraia wetu ni mbinguni. Mungu anasema kwamba watoto wake wanatakiwa wafikirie kwa tofauti kuhusu maisha mbali na wale wasioamini wanaavyofanya.
“Yote wanayofikiria ni maisha haya ya duniani. Lakini sisi ni raia mbinguni ambako Yesu Kristo anaishi.” Waamini halisi wanaelewa kwamba kuna mambo zaidi katika maisha zaidi ya miaka michache tunayoishi kutika sayari hii.
Utambulisho wako ni umilele na nyumbani kwako ni mbinguni. Mara utakapo ukamata kikamilifu ukweli huu, utaacha kuwa na wasi wasi juu ya “kuwa na vyote” hapa duniani. Mungu yuko wazi sana kuhusu hatari ya kuishi kwa ajili ya “hapa na sasa” na kufuata desturi za uthamani, kipaumbele na kuyapa umuhimu wa kwanza aina ya maisha ya dunia inayotuzunguka. Pindi tunapotamani na kujaribu kujihusisha na tamaduni zetu, Mungu anaiita hiyo hali kuwa ni ukahaba wa kiroho. Biblia inasema, “Mna mdanganya Mungu kwa maana kila mnachohitaji ni njia zenu wenyewe, mnatamani na kujihusisha na dunia kwa kila nafasi mnayopata, mnaishia kuwa adui wa Mungu na njia zake.”  (Yakobo 4: 4)
Fikiri kama ungeombwa na nchi yako uwe balozi wake katika maadui wa taifa lenu. Labda ungehitaji kujifunza lugha mpya na ungehitaji kufuata itikadi ua taratibu na tamaduni tofauti ili uwe mpole uweze kutimiza kusudi hilo. Kama balozi usingeweza kujitenga na adui. Ili utimize kusudi lazima utatakiwa kuwasiliana na kuhusiana nao.
Lakini fikiri kama ungejesikia faraja katika nchi hii ya ugeni na umeipenda zaidi ya nchi yako ya nyumbani. Bidii yako waminifu wako na kujitoa kwako kutabadilika. Wajibu wako kama balozi utakuwa umeridhia umeafiki. Badala ya kuwa mwakilishi wa nchi yako utakuwa anaanza kufanya kama adui. Hivyo utakuwa msaliti.
Biblia inasema “sisi ni mabalozi wa Kristo.” Katika hali ya kusikitisha hata watu anaojifikiria kuwa ni wafuasi wa Yesu Kristo mara kwa mara wanasahau ukweli huu wa kiroho. Kipuuzi, wamehitimisha kwamba kwa sababu wanaishi duniani sasa hivi kwa hiyo ni nyumbani kwao kwa kudumu. La hasha, Mtume Petro anasema, “Marafiki, dunia hii siyo nyumbani kwenu, kwa hiyo msijifanyie tamaa nayo, msiitamani na kuto thamini nafsi zenu.” (1 Petro 2: 11)
Mungu anatuonya tusijihusishe sana na manibo ya dunia yanayotuzunguka, kwa sababu vyote ni vya muda tu. Tunaambiwa “Wale wanaohusiana mara kwa mara na vitu au mambo ya dunia wanatumia vizuri au wanafanya hivyo kwa wema kila ya kujiungamanisha navyo.Dunia hii na vyote vilivyomo vinapita” (1 Wakorintho 7: 31)
Kulinganisha na miongo bila (Miaka) mingine, Maisha hayajawahi kuwa rahisi katika dunia. Daima tumekuwa tukijifurahisha, kuburudisha na kujridhisha tu. Pamoja na vivutio vyote na hali zote za kuburudisha na kufurahisha zilizopo leo, ni rahisi kusahaulika kwamba njia ya kukupa furaha siyo jinsi maisha yalivyo!. Pale tunapokumbuka kwamba maisha ni jaribio, ni kipimo cha uaminifu, na ni wajibu wa muda mfupi kwa maandalizi ya umilele na tukayafanya kwa ajili ya wema huu. Tunajiandaa kwa kitu kilicho bora zaidi “Lakini vitu tuvionavyo leo, vinapotea kesho bali vitu visivyoonekana vyadumu milele.” (2 Wakorintho 4:18)
Ukweli wa kwamba dunia ni sio makao yetu ya milele unaelezea kwanini tuna pata hali za ugumu, huzuni na kukataliwa hapa duniani. (Yohana 16: 33) Pia inaelezea kwa nini baadhi ya ahadi za Mungu hazitimii, na baadhi ya maombi hayajibiwi na baadhi ya hali zinaoneka kuwa sinjema. Huu sio mwisho wa habari.
Ili kutufanya sisi tusishikwe sana na dunia, Mungu ana ana ruhusu kiwango muhimu cha kutoridhika na kutotosheka katika maisha. Uhitaji ambao hautakuja kukamilika katika upande huu wa umilele hatuna furaha kamilifu hapa kwa sababu hatutakiwi au hatupaswi kuwepo! Sio nyumbani kwetu kwa mwisho; tuliumbwa kwa kitu kingine cha kushangaza zaidi.
Samaki kamwe wasingeweza kuishi kwa furaha katika nchi au ardhi kwa sababu wameumbwa kwa ajili ya maji. Tai asingeweza kamwe kutosheka kama asingeruhusiwa kuruka, kuchukuliwa na upepo. Hautatosheka kamwe ki ukamilifu hapa duniani kwa sababu umeumbwa kwa kitu zaidi ya hapa.
Utakuwa na nyakati nyingi za furaha hapa duniani, Lakini ni sawa na hakuna kitu kulinganisha na kile Mungu alichokiandaa kwa ajili yako.
Kutambua kwamba maisha ya duniani ni wajibu wa muda ufupi tu lazima kuwe na viwango vya thamani. Viwango vya umilele na sio vya muda mfupi. Ndiyo vinatakiwa kuwa vigezo vya maamuzi yako. Kama C.S Lewis alivyotambau, “Yote yasiyo ya milele ni milele isiyo na faida.” Biblia inasema, “Hatuyaangalii yale yanayoonekana, bali kwa yale yasiyoonekana. Kwa kuwa yanayoonekana ni ya muda mfupi, lakini yasiyoonekana ni ya milele. (2 Wakorintho 4: 18)
Ni kosa kuu  kudhania malengo ya Mungu katika maisha yako ni mafanikio ya mali au kufanikiwa katika umaarufu kama dunia inavyodhani. Uzima tele hauhusiani na chochote na kuongezeka kwa mali, wala uaminifu wa Mungu haikupi kigezo cha kufanikiwa ili kuupata umilele. Mungu anapendelea Zaidi au anavutiwa zaidi na tabia yako kuliko kutarijika. Anavutiwa zaidi na matokeo yako kuliko kuyafanya maisha kuwa marahisi kwako. Kumbuka maisha ni jaribio.
Mtume Paulo alikuwa mwaminifu kwa Mungu, lakini bado aliishia magerezani. Yohana mbatizaji alikuwa ni mwaminifu kwa Mungu lakini aliondolewa kichwa kwa sababu hiyo!. Mamilioni ya watu waaminifu wamefi dini (wameteseka sana), wamepoteza kila kitu, au wamefika mwisho wa maisha bila ya kitu chochote chakuonesha katika ulimwengu huu (Katika macho ya ulimwengu). Lakini mwisho wa maisha sio mwisho!
Katika macho ya Mungu, mashujaa wakubwa siyo wale waliopata, mafanikio, waliositawi, na wenye nguvu katika maisha hapa. Lakini wale wayafanyayo maisha kama ni wajibu wa muda mfupi na kutukuka kwa uaminifu, wakitarajia ahadi zao za milele.

Maswali ya kuzingatia
Ø   Ikiwa kitu pekee kitakachodumu katika milele yote ni uhusiano wako na Mungu, Je, thamani ya utu wako ni nini, thamani ya vipaumbele vyako, thamni ya mali yako, na muda wako?

Ø  Ikiwa Mungu yuko makini na tabia yako kuliko utulivu wako, Je, kweli hii inawezaje kubadilisha jinsi unavyopaswa kuyaangalia na kuitikia katika matatizo.

Ø  Je, unamfahamu yeyote ambaye amekwisha kwenda mbinguni?. Sambamba na kile ulichokwisha soma, Unafikiri wanataka kukuambia nini, kama wangeweza?

Kama unataka kujua zaidi kuhusu maswali haya, Unaweza kusafu katika tovuti yetu. www.purposedrivenlife.com.
Sababu ya kila kitu
Yote ni kwa ajili ya Mungu.Si kwa sababu uliumbwa na Mungu tu, bali kwa ajili yake pia. Hatima ya ulimwengu na vyote viujazavyo ni kuonyesha utukufu wake.Ni sababu ya kila kitu katika ulimwengu, pamoja na wewe pia.Mungu aliyaumba yote kwa ajili ya utukufu wake.Kama kusingekuwa na kitu chochote, basi utukufu usingekuwa dhahiri. Je, utukufu wa Mungu ni nini? Ni jinsi au namna Mungu alivyo.Ni asili ya vyote alivyoviumba, Ni tabia yake, na uweza wake.

Je, utukufu wa Mungu uko wapi? Jaribu kutazama vitu vinavyokuzunguka.Karibu kila kitu alichokiumba kinaonyesha utukufu wake kwa namna yake.Tunauona utukufu kila mahali, kuanzia vitu vidogo sana na hata vitu vinavyoonekana kwa macho, kama nyota, dhoruba na majira yake.Uumbaji huonyesha utukufu wa Muumba.Unaweza kujifunza mengi kuhusu tabia za Mungu kwa kuangalia mambo yanayokuzunguka. Kupitia asili, tunajifunza kwamba Mungu ni mkuu na mwenye uweza, na kwamba anafurahia utofauti wa uumbaji wake, na hupenda uzuri wake, na jinsi hekima iliyotumika katika uumbaji huo.Biblia inasema, “Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu” - (Zaburi 19:1)

Je, unaweza kujua Mungu ana fanana namna gani? Katika historia yote, Mungu amekuwa akifunua utukufu wake kwa watu kwa jinsi tofauti.Lakini picha halisi ya jinsi Mungu alivyo inaonekana kupitia mwanaye, Yesu Kristo.Biblia inasema, “Mungu, ambaye alisema zamani na Baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi…..Yeye kwa kuwa ni mn’gao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu”-Waebrania 1:1-3)

   Yesu Kristo alisema, “Mimi ni nuru ya ulimwengu”  -  (Yohana 8:12).

Kwa sababu ya Yesu kristo, tumekuwa nuruni kama Yesu Kristo alivyo.Biblia inasema, “Mwanawe na mwangaza wa utukufu wake”-(Waebrania 1:3).Kuna upeo wa hali ya juu sana katika kumjua Mungu, ambao pasipo Yesu Kristo kuja dunia tusingeweza kumjua Mungu.hivyo Yesu Kristo alikuja ili tuufahamu utukufu wa Mungu kikamilifu.Biblia inasema, “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli” - Yohana 1:14.

Kama binadamu tulioumbwa na Mungu, tunaamuriwa kutambua utukufu wa Mungu, heshima, kusifu utukufu wake, na maisha yetu kuangaza utukufu wake na kuishi kwa ajili ya utukufu wake.-(1 Nyakati 16:26).Kwa nini? Bwana anastahili.Tuna deni la kumpa utukufu na heshima kwa kadiri anavyostahili.biblia inasema, “Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; na kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa”  -  (Ufunuo 4:11).

Katika ulimwengu wote, ni viumbe wawili tu ndiyo walioshindwa kuleta utukufu kwa Mungu: Malaika walioanguka (mapepo) na sisi (wanadamu). Kutokumpa Mungu utukufu anaostahili inaitwa “DHAMBI”.Dhambi zote, kwa asili yake ni kushindwa kumpa Mungu utukufu anaostahili.Ni kupenda kitu kingine zaidi kuliko kumpenda Mungu. Kukataa kumpa Mungu utukufu ni kuwa na kiburi cha uzima, na ni dhambi iliyomfanya Ibilisi kutupwa kutoka mbinguni na sisi pia. Katika namna tofauti kidogo tumeishi kwa ajili ya utukufu au fahari yetu wenyewe na siyo kwa ajili ya Mungu. Biblia inasema, “Wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu” - (Warumi 3:23).

Hakuna mwandamu aliyempa Mungu utukufu wote kama anavyostahili kutoka katika maisha yetu.Hii ni dhambi mbaya na kubwa ambayo tunaweza kutenda kinyume na Mungu.Kwa upande mwingine, tukiishi kwa ajili ya utukufu wake, ni mafanikio makubwa ambayo tunaweza kuyapata hapa duniani.Mungu anasema, “Kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemuumba kwa ajili ya utukufu wangu; mimi nimemuumba, mimi nimemfanya” - (Isaya 43:7). Hivyo kuleta utukufu kwa Mungu inapaswa kuwa lengo au shabaha ya kwanza kwa kila mtu katika maisha.

Yesu alimwambia Mungu katika mbingu, “Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia kwa kuwa; wao si wa ulimwengu, kama mimi ni sivyo wa ulimwengu” - (Yohana 17:14).Alimpa Mungu heshima kwa kutimiza kusudi lake hapa duniani. Vivyo hivyo tunampa heshima Mungu kwa jinsi hiyo.Kila kitu kinapotimiza kusudi lake hapa duniani hurudisha utukufu kwa Mungu.Ndege wa angani huleta utukufu kwa Mungu kwa kuruka, kutengeneza kiota na kufanya yote kama Mungu alivyowakusudia.Hata sisimi huleta utukufu kwa kutimiza kusudi la kuishi kwao.Mungu aliwaumba mchwa kuwa mchwa na alikuumba wewe kama aulivyo.Dada Irenaeus said, “Utukufu wa Mungu kwa binadamu ni kuishi katika ukamilifu wote kama Mungu alivyomkusudia.

Kitabu kiitwacho, “Maisha yanayoendeshwa na kusudi” kinaeleza kwa kina juu ya jinsi unavyoweza kutimiza kusudi katika maisha yako. Na tumaini utapata nakala moja na kusoma. Lakini huu hapa ni muhtathari wa kuhusu makusudi matano katika maisha:

Unaleta utukufu kwa Mungu kwa kumjua na kumpenda zaidi:

Kusudi la kwanza kwako linaitwa kuabudu.Ni wajibu wako namba moja hapa duniani. “Baadhi ya watu wamekosa kitu muhimu sana katika maisha-hawamjui Mungu”.Unaweza kujua mambo mengi, lakini kama humjui Mungu binafsi, unakuwa umekosa sababu ya kwanza ambayo kwayo uliumbwa.

Kuabudu ni zaidi ya kuhudhuria ibada katika makanisa.Kuabudu ni mtindo wa maisha ya kumfurahia Mungu, kumpenda Mungu, kujitoa wenyewe ili kutumika kwa ajili ya kusudi lake.Tunamwabudu Mungu kwa kumfurahia! C.S. Lewis anasema, “Katika kutuamuru sisi kumwabudu, Mungu anatualika ili tumfurahie.Mungu anataka kuabudu kwetu kuchochewe na upendo, shukurani, na furaha na siyo uwajibikaji pekee.Unapotumia maisha yako kwa ajili ya utukufu wa Mungu, kila unachokifanya huwa ni tendo la ki ibada.Biblia inasema,-(Warumi 6:13).Hutaweza kutimiza makusudi manne mpaka umeanza na kusudi la kwanza.
Unaleta utukufu kwa Mungu kwa kujifunza kuwapenda wengine ndani ya familia ya Mungu:

Kusudi la pili linaitwa “Ushirika”, na ni matayarisho kwa ajili ya u milele kule ambako wale waliompokea Yesu Kristo watakuwea na ushirika wa pamoja. Unapoyakabidhi maisha yako kwa Yesu Kristo, Unakuwa umefanyika sehemu ya familia ya Mungu.Maisha ambayo Mungu anatarajia uyaishi siyo kumwamini tu, bali ni ‘kila kilicho katika usimamizi wako kama wakili.Kwa nini? Kwa sababu kujifunza kumpenda ni moja ya mafundisho ambayo anataka ujifunze kabla ya kukupeleka katika u milele. Mtume Yohana anasema, “Upendano wa ndugu, huthibitisha kwamba, tumepita kutoka mautini mpaka uzimani”. Mtume Paulo anasema, “Pendaneni ninyi kwa ninyi kama kristo alivyowapenda ninyi; na Mungu atatukuzwa” - (Warumi 15:7).

Wajibu wako wa pili ni kupenda wengine kama Mungu anavyowapenda, kwa sababu Mungu ni pendo na anataka tuwe kama yeye.Ndiyo maana kuunganika na kanisa la mahali pamoja ni muhimu sana kama kiongozi wa kiroho.Huwezi kutimiza kusudi la pili wewe mwenyewe.Alituuumba ili tutegemeane.Yesu alisema kwamba kupendana sisi kwa sisi ni uthibitisho kuwa ni wanafunzi wa Yesu kristo.
Unaleta utukufu kwa Mungu kwa kufanana naye:

Mara tunapozaliwa kwa jinsi ya kiroho kwa kuwa sehemu ya familia ya Mungu kupitia kujitoa kwa Yesu Kristo, Mungu anataka tukue hata kufikia kumjua yeye zaidi.Je, hiyo hatua huonekana namna gani. Kukua au kuwa wakomavu kiroho ni kuwa kama Yesu zaidi kwa jinsi tunavyofikiri, tunavyohisi, na hata kutenda kwetu.Kwa kadiri unavyozidi kufanana na Kristo kitabia, ndivyo unavyoleta utukufu kwa Mungu.Biblia inasema, “Kwa kadiri Roho wa kristo atendavyo kazi ndani yetu, tunafanana naye na kuangaza utukufu wake zaidi”-(Wafilipi 1:11). Mungu hutumia zana tofauti-kama vile baadhi ya watu, Biblia, mazingira, na wakati-ili kuimarisha na kukuandaa kwa ajili ya umilele.
Unamletea Mungu utukufu kwa kuwatumikia wengine:
Tena, hili ni zoezi la u umilele.Tunakwenda mbinguni kufurahia utumishi mbele za Mungu, hivyo moja ya sababu za kukuweka hapa duniani ni kukupa muda wa kufanya matayarisho zaidi. Bila shaka, njia pekee ya kumtumikia Mungu usiyemwona ni kuwatumikia wale unaowaona.Ndiyo maana Mungu amekupa vipawa Fulani Fulani.Uliumbwa na Mungu kwa namna ya vipawa, ujuzi, na uwezo wa namna mbalimbali ili kumtumikia Mungu kwa kuwatumikia wengine. Na Biblia inaita hili kusudi la tano kama HUDUMA.

Mungu hakukupa uwezo huo kwa kusudi binafsi.Uwezo huo ulipewa ili uwanufaishe watu wengine.Biblia innasema, “kila mmoja wetu kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu…..”-(1Petro 4:10-11).
Unaleta utukufu kwa Mungu kwa kuwaambia wengine kuhusu Yesu Kristo:
Mungu hataki pendo na kusudi lake lifichwe tu.Mara tunapofahamu kweli, anataka tuwashirikishe wengine.Ni upendeleo wa ajabu sana, kuwasaidia wengine kujua kusudi la Mungu na kuwaandaa kwa ajili ya hatima ya milele. Biblia inasema katika 2 wakorintho 4:15.

Kuishi maisha yako yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu itakubidi ufanye mabadiliko katika muda wako, mahusiano yako, na kila kitu.Na wakati mwingine itakulazimu kufanya maamuzi magumu badala ya maamuzi rahisi.Hata Yesu Kristo mwenyewe alipambana na hali hii ya kufanya maamuzi magumu.Akijua ya kuwa anapaswa kusulubiwa, alilia - (Yohana 12:27).

Yesu alisimama katika barabara.Je, alitimiza kusudi na kumletea Mungu utukufu au hakuwa na furaha na kuishi maisha ya raha nay a kujitegemea na kujistarehesha?.Je,utaishi kwa ajili ya malengo yako tu, kwa ajili ya kujifariji, na maisha ya starehe, au utaishi maisha kwa ajili ya utukufu wako mwenyewe, ukijua kwamba ametuahidi thawabu?.Biblia inasema, (Yohana 12:25).

Suala hili ni la muhimu kulifakari. Unakwenda kuishi kwa ajili ya nani-kwa ajili ya Mungu?. Unaweza kusitasita, kustaajabu kama utakuwa na nguvu za kuishi kwa ajili ya Mungu.Usiwe na wasiwasi! Mungu atakupa unachohitaji ikiwa utafanya uchaguzi wa kuishi kwa ajili yake.Biblia inasema (2Petro 2:3).

Pia usidhani kuwa unahitaji kujibu maswali yote ili uweze kuwa na sifa ya kuishi kwa ajili ya Mungu.Utakuwa na maswali maisha yako yote.Nimekuwa mkristo kwa zaidi ya miaka 40 na bado nimekuwa na maswali ninaposoma Biblia. Lakini hayo maswali hayakunizuia kuufurahia uhusiano wangu na Mungu.Sihitaji kufahamu jinsi mlipuko wa mafuta ndani ya injini ili kunufaika na kutembea kwa gari.Sihitaji kujua mfumo wa uyeyushaji wa chakula tumboni ili kufurahia nyama ninayokula.Vivyo hivyo, ningempokea Yesu Kristo hata kama ningekuwa na maswali na mashaka hayo.Ungempokea pia.

Hivi sasa, Mungu anakualika kwa ajili ya utukufu wake ili utimize kusudi ambalo alikukusudia.Hii ndiyo njia pekee ya kuishi.Kila kitu hapa kipo ili kiendelee kuishi kama kilvyo kusudiwa.Maisha halisi huanza mtu anapoyakabidhi maisha yake kwa Yesu Kristo.Kama una uhakika kwamba hujafanya uamuzi huu, unahitaji kumpokea na kumwamini.Biblia inaahidi (Yohana 1:12).

Kwanza:Amini kwamba Mungu anakupenda na amekuumba kwa ajili ya kusudi lake.Amini kuwa siyo ajali kwako kumwamini Mungu.Amini kuwa uliumbwa ili uishi milele.Amini kwamba Mungu amekuchagua ili uwe na uhusiano na Yesu Kristo, ambaye alikufa msalabani kwa ajili yako.Amini kwamba, haijalishi umetenda dhambi gani, yeye yuko hapo kukusamehe.Mwambie akusamehe, na kukusaidia kubadilika.Anaweza kabisa.

Pili:Mpokee katika maisha yako kwa kumruhusu awe Bwana (Meneja, Bosi, na anayetawala maisha yako), na mwokozi(ili kufa na kulipa gharama ya kila kitu kibaya ulichofanya).Hivyo pokea msamaha kwa ajili ya dhambi zako.Pokea kusudi na pendo lake.Pokea nguvu ili uweze kuliishi kusudi lake hapa duniani.Biblia inasema - (Yohana 3:16).

Hivi sasa, bila kujali unasoma kitabu hiki ukiwa wapi, Ninakualika uinamishe kichwa chako katika hali ya ukimya na uombe kwa unyenyekevu maombi ambayo yatabadilisha maisha:
“Yesu, Ninakuamini na kukupokea.Nashukuru kwa kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu.Kwa jinsi nijuavyo, naomba uingie maishani mwangu na unisaidie kukufahamu wewe zaidi, na kukutegemea wewe”.Amina.

Ikiwa umemaanisha sala hii, Pongezi! Karibu ndani ya familia ya Mungu! Sasa uko tayari kuanza kuishi katika kusudi la Mungu kwa ajili ya maisha yako.Nakusihi umwambie mwingine kuhusu hili badiliko ndani yako. Unaweza tembelea tovuti yetu: www. Purposedrivenlife.com, au email info@purposedrivenlife.com, Unaweza kunijulisha unaendeleaje.

Pointi za kutafakari
Je, unakwenda kuishi kwa ajili kwa ajili ya nani, kwa ajili yako au kwa ajili ya Mungu?
Maswali ya kutafakari
Ø   Je, ulisali sala hapo juu?

Ø   Kama hujayatoa maisha yako kwa Yesu kristo, Je, unangoja nini?

Ø  Je, waweza kuwaambia wengine habari za Yesu Kristo na kuanza kuishi maisha yanayoendeshwa na kusudi la Mungu? Andika majina yao na kasha waambie siku ya leo.

Kama unataka kujua zaidi kuhusu maswali haya, Unaweza kusafu katika tovuti yetu. www.purposedrivenlife.com.