2024年7月4日 星期四

Maisha Yanayoongozwa Na Malengo (Siku Ya Thelathini na Sita kwa Siku ya Arobaini)

 LENGO LA 5

ULIUMBA KWA AJILI YA UTUME

Tunda la mwenye haki ni mti wa uzima, na mwenye

kuvuta roho za watu ana hekima.

Mithali 11:30 (NIV)

Siku ya Thelathini na sita: Aliumba kwa Ajili ya Utume

Kama ulivyonituma ulimwenguni, vivyo hivyo na

mimi ninawatuma hawa ulimwenguni.

Yohana 17:18 (Msg)

Jambo la muhimu sana ni kwamba niikamilishe huduma yangu,

kazi ambayo Bwana Yesu alinipatia.

Matendo 20:24 (NCV)

Uliumba kwa ajili ya utume.

Mungu anatenda kazi kuniani, na atataka uungane naye. Jukumu hili linaitwa utume wako. Mungu anakutaka uwe na huduma katika mwili wa Kwa Kristo kwa waamini, Wakolosai 1:25 (NCV) na utume wako ambao ni huduma yako kwa wasioamini. Kutimiza utume wako katika ulimwengu ni lengo la tano la Mungu kwa maisha yako.

Utume wa maisha yako ni wa kushirikiana na pia ni maalum. Sehemu moja ni ule wajibu wa kushirikiana na kila Mkristo mwingine, na sehemu nyingine ni wajibu maalum kwa ajili yako. Tutaangalia sehemu hizi mbili katika sura zinazofuata.

Neno la kiingereza utume (mission) kutoka katika neno la Kilatini lenye maana “kutuma.” Kuwa Mkristo ni pamoja na kutumwa ulimwenguni kama mwakilishi wa Yesu Kristo. Yesu alisema, “Kama Baba alivyonituma mimi nami nawatuma ninyi.” 2 Yohana 20:21 (NIV)

Yesu Kristo alielewa bayana utume wa maisha yake duniani. Akiwa na umri wa miaka kumi na mbili alisema “Imenipasa kuwa katika kazi ya Baba yangu.” Luka 2:49 (KJV) Kwa miaka kumi na moja baadaye, alisema, “Imekwisha.” (Yohana 19:30) Kama vyuma viwili vinavyoshika vitabu pamoja kwenye shelfu, kauli hizi mbili hutengeneza mwelekeo mzuri wa maisha yanayoogozwa na malengo. Yesu alikamilisha utume Baba aliompa.

Utume aliokuwa nao Yesu hapa duniani sasa ni utume wetu kwa sababu sisi ni mwili wa Kristo. Alichokifanya katika mwili weke kama binadamu tunatakiwa kukiendeleza sisi kama mwili wake wa kiroho, kanisa. Utume huo ni upi? Kuwatambulisha watu kwa Mungu! Biblia inasema, “Kristo alitubadilisha kutoka maadui na kuwa rafiki zake na akatupatia kazi ya kuwafanya wengine wawe rafiki zake pia.” 2 Wakorintho 5:18 (TEV)

Mungu anapenda kuwakomboa wanadamu kutoka kwa shetani na awapatanishe na nafsi yake mwenyewe ili tuweze kutimiza yale malengo matano aliyotuambia: kumpenda, kuwa sehemu ya jamii yake, kufanana naye, kumtumikia, na kuwambia wengine habari zake. Tukishakuwa hivi, Mungu hututumia kuwafikia wengine. Anatuokoa na kisha anatutuma huko nje. Biblia inasema, “Tumetumwa ili tuseme kwa ajili ya Kristo.” 2 Wakorintho 5:20 (NCV) Sisi ni wajumbe wa upendo wa Mungu na malengo yake kwa ulimwengu.

UMUHIMU WA UTUME WAKO

Kutimiza utume wa maisha yako hapa duniani ni sehemu muhimu ya kuishi kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Biblia hutoa sababu kadhaa kwa nini utume wako ni wa muhimu.

SIKU YA THELATHINI NA SITA:

ALIUMBA KWA AJILI YA UTUME

Utume wako ni mwendelezo wa utume wa Yesu hapa duniani. Kama wafuasi wake, tunapaswa kuendeleza kile alichoanzisha Yesu. Yesu hatuiti tu kuja kwake, lakini kwenda kwa ajili yake. Utume wako ni wa muhimu sana kiasi kwamba Yesu aliuzungumzia mara tano, katika njia tofauti tano, katika vitabu vitano tofauti. (Mathayo 28:19-20; Marko 16:15; Luka 24:47; Yohana 20:21; Matendo 1:8) Ni kama vile alikuwa anasema, “hakika nataka ninyi mwelewe jambo hili!” Soma maagizo haya matano ya Yesu na utajifunza kwa kina kuhusu utume wako duniani –kuhusu lini, wapi, kwa nini, na vipi.

Yesu hatuiti tu kuja kwake, lakini kwenda kwa ajili yake

Katika Agizo Kuu Yesu alisema, “Nendeni kwa watu wa mataifa yote naa mkawafanye kuwa wanafunzi wangu. Wabatizeni kwa jina la Baba, la Mwana, na la Roho Mtakatifu, na wafundisheni kufanya kila kitu nilichowaambia.” Mathayo 28:19-20 (CEV) Agizo hili alipewa kila mfuasi wa Yesu, siyo la wachungaji na wamishenari peke yao. Hili ni agizo lako kutoka kwa Yesu, na si la hiari. Haya maneno ya Yesu siyo Pendekezo Kuu. Kama wewe ni sehemu ya jamii ya Mungu, utume wako ni wa lazima. Kuupuza itakuwa kutotii.

Yawezekana ulikuwa hujui kwamba Mungu anakuwajibisha kwa watu wasiomwamini wanaokuzunguka. Biblia inasema, “Ni lazima uwaonye ili waishi. Kama hutasema nao ili kuwaonya waovu kuacha njia zao mbaya, watakufa katika dhambi zao. Lakini nitakuwajibisha kwa kifo chao.” Ezekieli 3:18 (NCV) Wewe ni Mkristo pekee ambaye baadhi ya watu watakufahamu, na utume wako ni kuwaambia habari za Yesu.

Utume wako ni upendeleo wa ajabu. Ingawa ni wajibu mkubwa, pia ni heshima kubwa kutumiwa na Mungu. Paulo alisema, “Mungu ametupatia upendeleo wa kumsihi kila mmoja aje katika neema yake na apatanishwe naye.” 2 Wakorintho 5:18 (LB) Utume wako unahusisha upendeleo wa aina mbili: kumtumikia Mungu na kumwakilisha. Tunakuwa na ubia na Mungu katika kujenga ufalme wake. Paulo anatuita, “watenda kazi pamoja” na anasema “Sisi tu watenda kazi pamoja na Mungu.” 2 Korintho 6:1 (NCV)

Yesu ametutayarishia wokovu, ametuweka katika jamii yake, ametupa Roho wake, na kisha akatufanya wawakilishi wake ulimwenguni. Huu ni upendo wa ajabu! Biblia inasema, “Sisi ni wawakilishi wa Kristo. Mungu anatutumia kuwasihi wanaume na wanawake kuacha tofauti zao na waingie katika kazi ya Mungu ya kusawazisha mambo kati yao. Tunasema kwa ajili ya Kristo mwenyewe sasa: Iweni marafiki wa Mungu.” 2 Wakorintho 5:20 (Msg)

Kuwaambia wengine wanavyoweza kupata uzima wa milele ndiyo jambo kubwa unaloweza kuwatendea. Kama jirani yako angeugua kanza au AIDS na ukawa unafahamu tiba, lingekuwa kosa kubwa kutomfahamisha habari hizo za kuokoa maisha. Ni kosa pia kuficha njia ya msamaha, lengo, amani na uzima wa milele. Tuna habari kuu kuliko zote duniani, na kushirikisha wengine ndiyo wema mkubwa kuliko wote unaoweza kumfanyia mtu.

Tatizo moja walilonalo Wakristo wa muda mrefu ni kwamba wanasahau jinsi walivyokuwa hawana matumaini walipoishi bila Yesu. Lazima tukumbuke kwamba haijalishi watu wanaonekana kutosheka na kufanikiwa kiasi gani, bila Yesu hawana matumaini na wamepotea na pia wanaelekea katika kutengwa na Mungu milele. Biblia inasema, “Yesu ndiye pekee mwenye uwezo wa kuokoa watu.” Matendo 4:12 (NCV) Kila mtu anamhitaji Yesu.

Agizo Kuu alipewa kila mfuasi wa Yesu.

Utume wako una umuhimu wa milele. Utakuwa na matokeo makubwa kwa hatima ya milele ya watu wengine, hivyo ni wa muhimu kuliko kazi nyingine yoyote, mafanikio yoyote, au lengo lolote utakalolifikia katika maisha yako hapa duniani. Matokeo ya utume wako yatadumu milele; matokeo ya kazi yako hayawezi. Hakuna chochote unachofanya kitalingana na kuwasaidia watu wafanye uhusiano wa milele na Mungu.

Ndiyo maana lazima tuwe na juhudi kubwa katika utume wetu. Yesu alisema, “Sisi sote lazima tutekeleze haraka kazi tulizopewa na yeye aliye mkubwa, kwa sababu kuna wakati mchache uliobaki kabla usiku kuja na kazi yote kukoma.” Yohana 9:4 (NLT) Saa inakwenda na maisha yako ya utume yanapita, hivyo usichelewe siku nyingine. Anza utume wako wa kuwafikia wengine sasa! Tutakuwa na muda wa milele wa kufurahi na wale wote tuliowaleta kwa Yesu, lakini tuna muda mfupi tu wa maisha yetu ili kuwafikia.

Hii haimaanishi uache kazi yako ili uwe mwinjilisti wa kudumu. Mungu anakutaka uwashilikishe watu wengine walio nawe Habari Njema. Kama mwanafunzi, mama, mwalimu wa shule, mfanya biashara, au meneja, au chochote unachofanya, unatakiwa daima kutafuta watu Mungu anaowaweka mbele yako upate kuwashirikisha Injili.

Utume wako hukupatia umuhimu wa maisha yako. William James alisema, “Mtumizi bora ya maisha ni kuyatumia kwa kufanya kitu kitakachodumu kuliko maisha yako.” Ukweli ni kwamba, ni ufalme wa Mungu tu ndio utadumu milele. Kila kitu kingine hatimaye kitatoweka. Ndiyo maana tunatakiwa kuishi maisha yanayoongozwa na malengo – maisha ya kuabudu, kuwa na ushirika, kukua kiroho, huduma, na utume wetu duniani. Matokeo ya shughuli hizi yatadumu – milele!

Kama utashindwa kutimiza utume uliopewa na Mungu hapa duniani, utakuwa umepoteza maisha Mungu aliyokupa. Paulo anasema, “Maisha yangu si kitu isipokuwa nikiyatumia kwa kufanya kazi niliyopewa na Bwana. Yesu – kazi ya kuwaeleza wengine habari njema kuhusu wema na upendo wa ajabu wa Mungu.” Matendo 20:24 (NLT) Kuna watu katika sayari hii ambao ni wewe tu unayeweza kuwafikia kwa sababu ya mahali unapoishi na jinsi Mungu anavyokufinyanga. Iwapo mtu mwingine atakuwa mbinguni kwa sababu yako, maisha yako yatakuwa yamefanya tofauti ya milele. Anza kuangaza katika maeneo ya utume wako binafsi na usali, “Mungu, nani umemweka katika maisha yangu ili nimweleze kuhusu Yesu?”

Ratiba ya Mungu ya kuhitimisha historia inashikamana na ukamilishaji wa agizo tulilopewa. Siku hizi kuna hamu kubwa ya kujua kuhusu kurudi kwa Yesu mara ya pili na mwisho wa ulimwengu. Je, itakuwa lini? Kabla Yesu hajapaa mbinguni wanafunzi walimuuliza swali hili hili na jibu lake lilikuwa wazi. Alisema, “Si wajibu wenu kujua nyakati au tarehe Baba aliyopanga kwa mamlaka yake. Lakini mtapokea nguvu Roho Mtakatifu atakapokuja juu yenu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yersalemu na Uyahudi yote, na Samaria yote na mwisho wa ulimwengu.” Matendo 1:7-8 (NIV)

Wanafunzi walipotaka kuongea juu ya unabii, Yesu kwa haraka aligeukia uinjilisti aliwataka wakazanie utume wao ulimwenguni. Alisema akimaanisha, “Mambo ya kina kuhusu kurudi kwangu hayawahusu. Jambo la muhimu kwenu ni utume niliowapa. Kazanieni hilo!”

Ni rahisi kutiwa wasiwasi, kwa sababu Shetani angependa wewe ufanye kitu

chochote kuliko kushirikisha wengine imani yako.

Kukisia juu ya muda halisi wa kurudi kwa Yesu ni upuuzi, kwa sababu Yesu alisema, “hakuna anayejua kuhusu siku wala saa hiyo, wala hata malaika wa mbinguni, wala Mwana, lakini Baba yake pekee.” Mathayo 24:36 (NIV) Kwa kuwa Yesu alisema hakuna ajuaye siku wala saa, kwa nini wewe ujaribu kuibashiri? Tunachokijua kwa hakika ni kwamba: Yesu hatarudi mpaka kila mmoja Mungu anayemtaka asikie habari njema awe amesikia. Yesu alisema, “Habari njema ya ufalme wa Mungu itahubiriwa katika ulimwengu wote, kwa kila taifa. Ndipo ule mwisho utakuja.” Mathayo 24:14 (NCV) Kama unataka Yesu arudi haraka tia bidii kutimiza utume wako, siyo kubashiri unabii.

Ni rahisi kutiwa wasiwasi, kwa sababu shetani angependa wewe ufanye kitu chochote kuliko kushirikisha watu wengine Imani yako. Atakuruhusu ufanye aina zote za mambo mema ili mradi hakuna mtu yeyote utakayempeleka mbinguni. Lakini mara utakapokuwa na bidii katika utume wako, tegemea Ibilisi kukutupia kila aina ya mambo yatakayokuachisha kazi hiyo. Inapotokea hivyo, kumbuka maneno ya Yesu: “Mtu yeyote anayekubali kuachishwa kazi ninayompangia hafai kwa ufalme wa Mungu.” Luka 9:62 (LB)

GHARAMA YA KUTIMIZA UTUME WAKO

Ili utimize utume wako itakulazimu uache ajenda zako na ukubali majadala wa Mungu kwa ajili ya maisha yako. Huwezi tu kung’ang’ania mambo mengine yote ambayo ungependa kufanya katika maisha yako. Lazima useme, kama Yesu, “Baba, … nataka mapenzi yako, siyo mapenzi yangu.” Luka 22:42 (NLT) Unampatia Mungu haki zako, matazamio yako, ndoto, mipango, na matakwa yako. Acha kuomba sala za kibinafsi kama vile “Mungu bariki ninachotaka kukifanya.” Badala yake Sali hivi, “Mungu nisaidie nifanye kile unachokibariki!” Unamkabidhi Mungu karatasi tupu yenye jina lako chini na unamwambia ajaze kwa kina sehemu iliyabaki. Biblia inasema, “Jikabidhini nafsi zenu zote kwa Mungu – kila sehemu ya utu wenu … mpate kuwa vyombo mikononi mwa Mungu kwa ajili ya kutumiwa kwa malengo yake mema.” Warumi 6:13b (LB)

Kama utajitoa kutimiza utume wako katika maisha bila kujali gharama, utapata Baraka za Mungu kwa njia ambazo watu wachache huzipata. Hakuna kitu ambacho Mungu hawezi kufanya kwa ajili ya mtu ambaye amejitoa kutumikia ufalme wa Mungu. Yesu alisema, “Mungu atawapa yote mnayohitaji kila siku kama mtamwishia na kufanya ufalme waa Mungu kuwa jambo la kwanza kwenu.” Mathayo 6:33 (NLT)

MMOJA ZAIDI KWA AJILI YA YESU

Baba yangu alikuwa mtumishi kwa zaidi ya miaka hamsini, akitumika zaidi katika makanisa madogo ya shambani. Alikuwa mhubiri wa kawaida, lakini alikuwa mtu mwenye utume. Shughuli aliyopenda zaidi ilikuwa kupeleka vikundi vya kujitolea ng’ambo kujenga majengo ya kanisa kwa makanisa madogo. Katika maisha yake, Baba alijenga zaidi ya makanisa 150 duniani kote.

Mwaka 1999, baba yangu alikufa kwa kansa. Juma la mwisho la maisha yake ugonjwa ulimfanya akae macho katika hali ya kujitambua nusu kwa kadiri ya masaa ishirini na nne kwa siku. Alipoota, aliweza kusema kwa sauti mambo aliyoyaota. Nikiwa kando ya kitanda chake, nilijifunza mengi kuhusu baba yangu kwa kusikiliza ndoto zake. Alizungumzia mradi wa kanisa moja baada ya jingine.

Usiku mmoja karibu na mwisho, wakati mke wangu, mpwa wangu wa kike, na mimi tulikuwa kando yake, baba ghafla alipata nguvu na kujaribu kutoka kitandani. Ni kweli, alikuwa dhaifu sana, na mke wangu alisisitiza alale tu. Lakini yeye alikazania kutoka kitandani, hivyo mke wangu baadaye aliuliza, “Jimmy unajaribu kufanya nini? Alijibu, “Niokoe mmoja zaidi kwa ajili ya Yesu! Niokoe mmoja zaidi kwa ajili ya Yesu! Niokoe mmoja zaidi kwa ajili wa Yesu!” Alianza kurudia maneno hayo tena na tena.

Kwa muda wa saa moja iliyofuatia, alisema maneno haya labda mara mia moja. “Niokoe mmoja zaidi kwa ajili ya Yesu!”Nikiwa nimekaa kando ya kitanda chake na machozi yakinichuruzika mashaavuni, niliinamisha kichwa change kumshukuru Mungu kwa imani ya baba yangu. Wakati kuo baba yangu alinyoosha mkono wake dhaifu na kuniwekea kichwa na kusema, kama vile akiniagiza, “Okoa mmoja zaidi kwa ajili ya Yesu! Okoa mmoja zaidi kwa ajili ya Yesu! Okoa mmoja zaidi kwa ajili ya Yesu!”

Ninakusudia kufanya jambo hili kuwa ndiyo mwongozo wa maisha yangu yaliyobaki. Nakualika kulichukua kama mwelekeo wa maisha yako pia, kua kuwa hakuna kingine kitakachoweza kufanya tofauti kubwa katika umilele. Kama unataka kutumiwa na Mungu, lazima ujali kile Mungu anachokijali; anachokijali zaidi ni ukombozi wa watu aliowaumba. Anapenda watoto wake waliopotea wapatikane! Hakuna kitu cha muhimu zaidi kwa Mungu; msalaba unathibitisha hilo. Naomba kwamba daima utakuwa ukitafuta kumfikia “mmoja zaidi kwa ajili ya Yesu” ili kwamba utakaposimama mbele za Mungu siku moja, uweze kusema, “Utume umekamilika!”

Siku ya Thelathini na Saba: Kushirikisha Wengine Ujumbe

Wa Maisha yako

Wale unaomwamini Mwana wa Mungu wana ushuhuda wa Mungu udani yao.

1 Yohana 5:10 (GWT)

Maisha yenu yanatangaza Neno la Bwana … Habari za imani yenu katika Mungu zimeenea.

Hata hatuhitaji kusema chochote zaidi – ninyi ndio ule ujumbe!

1 Thesalonike 1:8 (Msg)

Mungu amekupa ujumbe wa maisha ili kushirikisha wengine.

Unapomwamini, pia unakuwa mjumbe wa Mungu. Mungu anapenda kusema na ulimwengu kupitia wewe. Paulo alisema, “Tunasema ukwali mbele za Mungu, kama wajumbe wa Mungu.” 2 Wakorintho 2:17b (NCV)

Unaweza kuhisi huna kitu cha kusema kwa watu, lakini huyo ni Ibilisi akijaribu kukunyamazisha. Una akiba kubwa ya uzoefu ambao Mungu anapenda kuutumia kuwaleta wengine katika jamii yake. Biblia inasema, “Wale wanaomwamini Mwana wa Mungu wana ushuhuda wa Mungu ndani yao.” 1 Yohana 5:10a (GWT) Ujumbe wa maisha yako unazo sehemu nne:

l  Ushuhuda wako. Hadithi kuhusu ulivyoanza uhusiano wako na Yesu.

l  Masomo ya maishani mwako: Masomo muhimu zaidi ambayo Mungu amekufundisha.

l  Shanuku yako ya utauwa: mambo ambayo Mungu amekuwezesha kuyathamini zaidi.

l  Habari Njema: Ujumbe wa Wokovu.

Kuhadithia hujenga daraja la uhusiano ambalo Yesu anaweza kulipitia toka moyoni mwako hadi kwa wengine.

Ujumbe wa Maisha yako ni pamoja na ushuhuda wako. Ushuhuda wako ni hadithi kuhusu jinsi Kristo alivyobadilisha maisha yako. Petro anatuambia kwamba tulichaguliwa na Mungu “Kufanya kazi yake na kusema kwa ajili yake, kuwatangazia wengine tofauti ya usiku na mchana aliyowafanyia ninyi.” 1 Petro 2:9 (Msg) Hiki ndicho kiini cha ushuhuda – ni kushirikisha wengine uzoefu wako kuhusu Bwana. Katika mahakama, shahidi hatakiwi kubishana kwenye kesi, kuthibitisha ukweli, au kukazia hukumu, hiyo ni kazi ya wanasheria. Mashahidi hutoa tu maelezo ya kilichotokea kwao au walichokiona.

Yesu alisema “Mtakuwa mashahidi wangu,” Matendo 1:8 (NIV) siyo “Mtakuwa wanasheria wangu.” Anakutaka ushirikishe wengine hadithi yako. Kushirkisha wengine ushuhuda wako ni sehemu muhimu ya utume wako hapa duniani kwa sababu ni wa pekee. Kama hutawashirikisha watu wengine, utaupoteza milele. Unaweza usiwe mtaalamu wa Biblia, lakini una mamlaka kwa maisha yako, na ni vigumu kupingana na uzoefu wa mtu binafsi. Kwa kweli, ushuhuda wako binafsi una nguvu kuliko hotuba ya mahubiri, kwa sababu wasioamini huwaona wachungaji kama wataalamu wa kuuza biashara, lakini wanakuona kama “mteja aliyetosheka,” hivyo wanakupa umuhimu zaidi.

Hadithi za binafsi pia ni rahisi kuzifuata kuliko kanuni, na watu hufurahi kuzisikiliza. Zinateka mawazo yetu, na tunazikumbuka kwa muda mrefu. Wasioamini labda wangepoteza hamu ya kusikia kama ungeanza kunukuu wanatheologia, lakini wana shauku ya asili kuhusu uzoefu ambao hawajausikia. Kuhadithia hujenga daraja la uhusiano ambalo Yesu anaweza kulipitia toka moyoni mwako hadi kwa wengine.

Faida nyingine ya ushuhuda wako ni kwamba uko juu ya utetezi wa kiakili. Watu wengi ambao hawawezi kukubali mamlaka ya Biblia watasikiliza ushuhuda wa mtu mnyonge. Ndiyo maana kwa nyakati kita tofauti Paulo alitumia ushuhuda wake Kuhubiri Injili badala ya kunukuu maandiko. (Matendo 22 to 26)

Biblia inasema, “Muwe tayari siku zote kumjibu yeyote atakewauliza kuelezea tumaini mlilo nalo ndani yenu, lakini fanyeni hivyo kwa upole na heshima.” 1 Petro 3:15-16 (TEV) Njia bora ya “kuwa tayari” ni kuandika ushuhuda wako na kisha kukariri mambo makuu. Ugawanye katika sehemu nne:

1.         Maisha yangu yalivyokuwa kabla sijakutana na Yesu.

2.         Nilivyotambua kwamba nilimhitaji Yesu.

3.         Jinsi nilivyomkabadhi maisha yangu Yesu.

4.         Tofauti aliyoifanya Yesu Katika maisha yangu.

Ni kweli kwamba unazo shuhuda nyingine nyingu mbali na ushuhuda wako wa wokovu. Unayo hadithi ya kila uzoefu ambamo Mungu amekusaidia. Fanya orodha ya matatizo yote, mazingira magumu ambayo Mungu amekupitisha. Kisha uwe makini kutumia hadithi ambayo rafiki yako asiyeamini itaweza kumsaidia zaidi. Mazingira tofauti huhitaji shuhuda tofauti pia.

Ujumbe wa Maisha yako ni pamoja na masomo ya maishani mwako. Sehemu ya pili ya ujumbe wa maisha yako ni ukweli kwamba Mungu amekufundisha kwa ule uzoefu pamoja naye. Kuna masomo na ufahamu uliojifunza kuhusu Mungu, mahusiano, matatizo, majaribu, na mambo mengine ya maisha Daudi aliomba, “Mungu nifundishe masomo ya maaisha ili niweze kudumu katika njia.” Zaburi 119:33 (Msg) Inasikitisha, hatujifunzi kutokana na mambo mengi yanayotupata. Kuhusu Waisraeli, Biblia inasema, “Mungu aliwaokoa tena na tena, lakini hawakujifunza – mpaka hatimaye dhambi zao ziliwaagamiza.” Zaburi 106:43 (Msg) Labda umeshakutana na watu kama hao.

Wakati ni busara kujifunza kutokana na uzoefu, ni busara zadi kujifunza kutokana na uzoefu wa wengine. Hakuna muda wa kutosha kujifunza kila kitu katika maisha kwa kujaribu na kukosea. Lazima tujifunze kutoka masomo ya kila mmoja wetu. Biblia inasema, “Maonyo yanayotolewa na mtu mwenye uzoefu kwa mtu aliye tayari kusikiliza ni ya thamani zaidi kuliko … pambo lililotengenezwa kwa dhahabu.” Mithali 25:12 (TEV)

Wakati ni busara kujifunza kutokana na uzoefu, ni busara zaidi kujifunza kutokana na uzoefu wa wengine.

Orodhesha masomo makubwa ya maisha ambayo umejifunza ili uweze kuwashirikisha wengine. Tunatakiwa kushukuru kwa kuwa Sulemani alifanya hivyo, na hii ilitupatia vitabu vya Mithali na Mhubiri, ambavyo vimejawa mafundisho ya maisha ya kila siku. Fikiri ni matatizo mangapi tungeyaepuka kama tungejifunza kutoka katika mafundisho maisha ya kila mmoja wetu.

Watu waliokomaa hujijengea tabia ya kupata mafundisho kutokana na uzoefu wa kila siku. Nakusihi ufanye orodha ya masomo kutokana na uzoefu wa kila siku. Nakusihi ufanye orodha ya masomo kutokana na uzoefu wa maishani mwako. Hapa kuna maswali kadhaa yanayoweza kukufanya ukumbuke na kuanza kuandika: (Zaburi 51; Filipi 4:11-13; 2 Wakorintho 1:4-10; Zaburi 40; Zaburi 119:71; Mwanzo 50:20.)

l  Mungu alinifundisha nini kutokana na kushindwa?

l  Mungu amenifundisha nini kutokana na kukosa fedha?

l  Mungu amenifundisha nini kutokana na maumivu au huzuni?

l  Mungu amenifundisha nini kupitia kusubiri?

l  Mungu ameifundisha nini kupitia ugonjwa?

l  Mungu amenifundisha nini kupitia kuvunjwa moyo?

l  Nimejifunza nini kutoka kwa jamaa yangu, kanisa langu, mahusiano yangu, makundi yangu madogo, nawatu wanaonilaumu?

Ujumbe wa Maisha yako ni pamoja na kushirikisha wengine shauku yako ya kimungu. Mungu ni mwenye shauku kubwa. Kwa shauku kubwa anapenda vitu fulani na kwa shauku kubwa anachukia vitu vingine. Unapokuza ukaribu naye, atakupa shauku ya kitu fulani anachokijali kwa kina ili uwe msemaji wake duniani. Yaweza kuwa shauku juu ya tatizo, lengo, kanuni, au kundi la watu. Chochote kile, utahisi kusukumwa kukizungumzia na kufanya chochote unachoweza ili kufanya tofauti.

Huwezi kujizuia kuzungumza kile unachokijali zaidi. Yesu alisema, “Moyo wa mtu ni kiini cha kauli zake.” Mathayo 12:34 (LB) Mifano miwili ni Daudi, aliyesema, “Wivu wangu kwa Mungu na nyumba yake vinawaka moto ndani yangu,” Zaburi 69:9 (LB) na Yeremia alisema, “Ujumbe wako unawake ndani ya moyo wangu na katika mifupa yangu, na siwezi kunyamaza.” Yeremia 20:9 (CEV)

Mungu huwapa watu fulani shauku ya kimungu ili kuwa watetezi wa jambo fulani. Mara nyingi ni tatizo ambalo wao binafsi wanalipata kama vile kudhalilishwa, ulevi, kutokuzaa, huzuni, ugonjwa, au ugumu wowote ule. Wakati mwingine Mungu huwapatia watu shauku ya kutetea kikundi cha watu wengine ambao hawawezi kujsemea: Watoto wali tumboni, wanaoteswa, masikini, wafungwa, wanaonyanyaswa, watu ambao hawakubahatika, na wale wanaonyimwa haki. Biblia imejaa maagizo ya kuwatetea wasi na utetezi.

Mungu hutupatia Shauku tofauti ili kwamba kila kitu anachotaka Kitendeke duniani kipate kutendeka.

Mungu hutumia watu wenye shauku ili kuendeleza ufalme wake. Anaweza kukupatia shauku ya kimungu ya kuanzisha makanisa mapya, kuimarisha jamii, kuwapa fedha watafsiri wa Biblia, au kufundisha viongozi wa Kikristo. Unaweza kupewa shauku ya kimungu ya kuwafikia na Injili kikundi cha watu fulani: Wafanya biashara, vijana, wanafunzi wa kimataifa wa kubadilishana, wamama vijana, au wale wenye kupenda mambo fulani au michezo. Kama ukimwomba Mungu atakupa mzigo moyoni mwako wa nchi maalum au kundi la watu fulani ambalo linahitaji ushuhuda mzito wa Kikristo.

Mungu hutupatia shauku tofauti ili kwamba kila kitu anachotaka kitendeke duniani kipate kutendeka. Usitegemee kila mtu kuwa na shauku juu ya shauku yako. Badala yake, lazima tusikilize na kuthamini ujumbe wa maisha ya kila mmoja wetu kwa sababu hakuna awezaye kusema yote. Usipuuze shauku ya kimungu ya mtu mwingine. Biblia inasema, “Ni vyema kuwa na shauku kubwa, maadam ni kwa lengo jema.” Wagalatia 4:18 (NIV)

Ujumbe wa Maisha yako ni pamoja na Habari Njema. Habari Njema ni nini? “Habari Njema huonyesha jinsi Mungu anavyowafanya watu wapatane naye – hiyo huanza na kumalizika kwa imani.” Warumi 1:17 (NCV) “Kwa kuwa Mungu alikuwa katika Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie tena watu dhambi. Hii ndiyo habari njema ya ajabu aliyotupatia tumaambie wengine.” 2 Wakorintho 5:19 (NLT) Habari njema ni kwamba tunapoamini neema ya Mungu kutuokoa kupitia kile alichofanya Yesu, dhambi zetu zinasamehewa, tunapata lengo la maisha, na tunaahidiwa makazi yajayo mbinguni.

Kuna mamia ya vitabu vizuri vinavyoeleza namna ya kushirikisha wengine Habari Njema. Naweza kutoa orodha ya vitabu ambavyo vimenisaidia (angalia nyongeza ya 2). Lakini mafunzo yote ya ulimwenguni hayawezi kukuchochea kumshuhudia Kristo mpaka utie moyoni kweli nane zilizokwishazungumziwa katika sura zilizopita. Cha muhimu zaidi, ni lazima ujifunze kuwapenda watu waliopotea kama Mungu anavyowapenda.

Mungu kamwe hakuumba mtu asiyempenda. Kila mtu ni wa thamani kwake. Yesu aliponyoosha na kufungua mikono yake msalabani, alikuwa anasema, “Nawapenda ninyi kiasi hiki!” Biblia inasema, “Kwa kuwa upendo wa Kristo unatubidisha, kwa kuwa tumehakikishiwa kwamba mtu mmoja alikufa kwa ajili ya wote.” 2 Wakorintho 5:14 (NIV) Unapojihisi kupoa juu ya utume wako duniani, tumia muda fulani kufikiri juu ya kile Yesu alikufanyia msalabani.

Ni lazima tujali juu ya wasioamini kwa sababu Mungu anawajali. Upendo hauturuhusu kuhiari. Biblia inasema, “Hakuna hofu katika pendo; pendo kamilifu huondoa hofu yote.” 1 Yohana 4:18 (TEV) Mzazi atakimbilia ndani ya jengo linaloungua ili amwokoe mtoto kwa sababu upendo wake kwa mtoto huyo ni mkuu kuliko hofu yake. Kama u mwoga kuwashirikisha Habari Njema wanaokuzunguka, mwombe Mungu akujaze moyo wako kwa upendo wake kwa ajili yao.

Biblia inasema, “Mungu hapendi mtu yeyote apotee, lakini anapenda watu wote wahadili mioyo na maisha yao.” 2 Petro 3:9 (NCV) Ukiwa unafahamu mtu mmoja ambaye hamfahamu Kristo, ni lazima udumu kuwaombea ukiwatumikia katika upendo na kuwaambia Habari Njema. Na kama kuna mtu yeyote katika jamii yenu ambaye hajaingia katika jamii ya Mungu, kanisa lenu lazima lidumu kuwafikia watu kama hao. Kanisa ambalo halitaki kukua linasema kwa ulimwengu, “Mnaweza kwenda kuzimu.”

Je, unataka kufanya nini ili kwamba wale watu unaowajua waweze kwenda mbinguni? Waalike kanisani? Waambie hadithi yako? Uwape kitabu hiki? Uwapelekee chakula? Uwaombee kila siku mpaka waokoke? Kiwanja chako cha utume kinakuzunguka. Usikose nafasi ambayo Mungu anakupatia. Biblia inasema, “Tumieni nafsi zenu vizuri kuwaambia wengine Habari Njema. Iweni na busara katika mahusiano yenu yote nao.” Wakolosai 4:5 (LB)

Je, kuna mtu yeyote atakayeingia mbinguni kwa sababu yako? Je, kuna mtu yeyote mbinguni atakayeweza kukuambia, “Nataka kukushukuru. Niko hapa kwa sababu ulinijali sana ukaniambia Habari Njema?” Fikiri furaha ya kusalimiana na watu uliowasaidia wafike huko. Wokovu wa milele wa nafsi moja ni muhimu kuliko chochote utakachoweza kufanikiwa kukifanya maishani. Ni watu tu ndio wataishi milele.

Katika kitabu hiki umejifunza malengo matano ya Mungu kwa maisha yako duniani. Alikuumba ili uwe mshirika katika jamii yake, kielelezo cha tabia yake, mtu anayetukuza utukufu wake, mtumishi wa neema yake, na mjumbe wa Habari zake Njema. Katika malengo haya matano, lile la tano linaweza tu kutendwa hapa dunianni. Yale mengine manne utaendelea kuyafanya milele kwa namna fulani. Ndiyo maana kutangaza Habari Njema ni muhimu sana; una muda mfupi tu wa kushirikisha wengine ujumbe wa maisha yako na kutimiza utume wako.

SIKU YA THELATHINI NA SABA

KUFIKIRI JUU YA LENGO LANGU

Jambo la Kutafakari: Mungu anapenda kusema kitu kwa ulimwengu kupitia mimi.

Kifungu cha Kukumbuka:Kuweni tayari kumjibu kila mtu atakayewauliza kueleza juu ya tumaini mlilonalo ndani yenu, lakini fanyeni hivyo kwa pole na heshima.” 1 Petro 3:15-16 (TEV)

Swali la kujiuliza: Ninapotafakari juu ya hadithi yangu binafsi, je, Mungu anapenda mimi nimshirikishe nani hadithi yangu?

 Siku ya Thelathini na Nane: Kuwa Mkristo Wa Tabaka

la Ulimwengu Wote

Yesu aliwaambia wafuasi wake, “Nendeni kila mahali ulimwenguni na mkamwambie

kila mmoja Habari Njema.”

Marko 16:15 (NCV)

Tutume ulimwenguni kote na habari za nguvu zako za kuokoa na

mpango wako wa mile kwa wanadamu wote.

Zaburi 67:2 (LB)

Agizo kuu ni Agizo lako.

Una uchaguzi wa kufanya. Utakuwa Mkristo wa tabaka la ulimwengu wote au utakuwa Mkristo wa kidunia. Kitabu cha Paulo Borthwick wazo la umisheni (Colorado Springs: NavPress, 1987) na Jinsi ya kuwa Mkristo wa Tabaka Zote za Dunia (Waynesboro GA: Authentic media, 1999) lazima visomwe na kila mkristo.

Wakristo wa kidunia humtazama Mungu kwanza kwa ajili ya kukidhi haja zao binafsi. Wanapenda kuhudhuria mikutano na semina za kujenga, lakini hutawakuta katika mkutano wa umisheni kwa sababu hawaupendelei. Maombi yao yanajali mahitaji yao binafsi, baraka na furaha yao. Ni ile imani ya “mimi kwanza.”: Je, Mungu anawezaje kufanya maisha yangu kuwa na furaha? Wanapenda kumtumia Mungu kwa malengo yao badala ya wao kutumiwa kwa malengo yake.

Kinyume cha hapo, Wakristo wa tabaka la ulimwengu mzima wanajua waliokolewa ili watumike na kutayarishwa kwa ajili ya utume. Wako tayari kupokea jukumu la mtu binafsi na wanafuharia upendeleo huo wa kutumiwa na Mungu. Wakristo wa tabaka la ulimwengu wote ndio watu pekee walio hai kikamilifu katika sayari hii. Furaha yao, uhakika na hamasa yao vinaambukiza kwa sababu wanajua wanafanya tofauti. Wanaamka asubuhi wakitazamia Mungu kufanya kazi kuwapitia katika njia mpya. Je, unataka kuwa Mkristo wa aina gani?

Mungu anakualika kushiriki katika tendo kubwa kuliko yote, la aina yake na la muhimu sana katika historia – ufalme wake. Historia ni habari inayomhusu (His story). Anajenga jamii yake kwa umilele. Hakuna chochote kilicho cha muhimu wala hakuna kitakachodumu siku zote. Kutoka katika kitabu cha Ufunuo tunajua kwamba umisheni wa Mungu kwa dunia nzima utakamilika. Siku moja Agizo Kuu litakuwa utimilifu mkuu. Kundi kubwa la watu mbinguni kutoka “Kila jamii, kila kabila, taifa na lugha” Ufunuo 7:9 (CEV) siku moja watasimama mbele ya Yesu Kristo kumwabudu. Kuhusika kama Mkristo wa tabaka la dunia yote itakuruhusu kuonja hali kidogo itakavyokuwa mbinguni.

Yesu alipowaambia wafuasi wake “Kwenda kila mahali ulimwenguni na kusema Habari Njema kwa kila mtu,” hicho kikundi kidogo cha wafuasi maskini wa Mashariki ya Kati walishikwa na mshangao mkubwa. Je, walitakiwa kutembea au kupanda wanyama waendao pole pole? Huo ndio usafiri waliokuwa nao, na hapakuwa na meli za kukatisha baharini, hivyo kulikuwa na vizuizi vya wazi ili kuweza kwenda katika ulimwengu mzima.

Siku hizi tuna ndege, meli, treni, mabasi na magari. Umekuwa ni ulimwengu mdogo, na unazidi kuwa mdogo kila siku. Unaweza kupaa na kuvuka bahari kwa masaa tu na ukafika nyumbani kama unataka. Nafasi sasa iko wazi kwa Wakristo wa kawaida kujihusisha na umisheni wa kimataifa kwa muda mfupi. Kila pembe ya ulimwengu iko wazi kwa ajili yako – wewe waulize wasafirishaji. Hakuna sababu ya kutoeneza Habari Njema.

Sasa, na mtandao wa intaneti, ulimwengu umekuwa mdogo kabisa. Pamoja na simu na faksi, Mkristo yeyote aliye na nafasi ya intaneti anaweza kuwasiliana binafsi na watu wa kila nchi duniani. Ulimwengu mzima uko katika ncha ya vidole vyako!

Hata maeneo ya mashambani kabisa yanapata barua-pepe, sasa unaweza kufanya mazungumzo ya uinjilisti na watu walio katika ulimwengu wa upendo mwingine, bila kuondoka nyumbani kwako! Haijawahi kuwa rahisi katika historia kutimiza agizo la kwenda katika ulimwengu wote. Vikwazo vikubwa siyo tena umbali, gharama au usafiri. Kikwazo pekee ni jinsi tunavyofikiri. Kuwa Mkristo wa tabaka la ulimwengu wote ni lazima kufanya mabadiliko ya akili. Mtazamo na msimamo wako lazima vibadilike.

JINSI YA KUFIKIRI KAMA MKRISTO WA TABAKA LA ULIMWENGU WOTE

Badilika kutoka kufikiri ubinafsi na uanze kufikiri kuzingatia wengine. Biblia inasema, “Rafiki zangu acheni kufikiri kama watoto. Fikirini kama watu wazima.” 1 Wakorintho 14:20 (CEV) Hii ni hatua ya kwanza ili kuwa Mkristo wa tabaka la ulimwengu wote. Watoto tu ndio hujifikiri wenyewe, watu wazima hufikiri juu ya watu wengine. Mungu anaagiza, “Usifikiri kuhusu mambo yako tu, lakini jail mambo ya wengine pia.” Wafilipi 2:4 (NLT)

Bila shaka, hili ni badiliko gumu la akili, kwa sababu tu watu wa ubinafsi kwa asili na karibu matangazo yote hutuchochea kujifikiri wenyewe. Njia pekee ya kufanya badiliko hili kubwa ni kwa kumtegemea Mungu muda wote. Kwa bahati nzuri hatuachi tuhangaike peke yetu.

Haijawahi kuwa rahisi katika historia kutimiza agizo lako la kwenda katika ulimwengu wote

Mungu ametupatia Roho wake. Ndiyo maana hatufikiri sawasawa na watu wa ulimwengu huu wanavyofikiri.”1 Wakorintho 2:12 (CEV)

Anza kumwomba Roho Mtakatifu akusaidie katika kufikiri mahitaji ya kiroho ya wale wasioamini kila unaposema nao. Kwa mazoezi unaweza kukuza tabia ya kusali kimya “sala ya moyoni” kwa wale unaokutana nao. Sema, “Baba, nisaidie nielewe ni kitu gani kinachomzuia mtu huyu asikujue wewe.”

Kazi yako ni kuelewa wengine wako wapi katika safari yao ya kiroho na kisha ufanye chochote kinachoweza kuwaleta hatua moja karibu na kumjua Yesu. Unaweza kujifunza namna ya kufanya hivi kwa kuiga mtazamo wa Paul, aliyesema, “Sifikirii juu ya kile kingnifaa mimi lakini juu ya kile kinachoweza kuwafaa watu wengine ili kwamba waokolewe.”1 Wakorintho 10:33 (GWT)

Hama kutoka kufikiri kienyeji, na uanze kufikiri kiulimwengu mzima. Mungu ni Mungu wa ulimwengu mzima. “Mungu aliupenda sana ulimwengu…” Yohana 3:16 (KJV) Tangu mwanzo Mungu amewataka watu na jamii kutoka kila taifa aliowaumba. Biblia inasema, “Kutoka mtu mmoja Mungu aliumba mataifa yote wanaoshi duniani na akaamua majira na mahali kila taifaa litakapokuwa. Mungu amefanya haya yote, ili kwamba tumtafute na kuweza kumpata.” Matendo 17:26-27 (CEV)

SIKU YA THELATHINI NA NANE:

KUWA MKRISTO WA TABAKA LA ULIMWENGU WOTE

Sehemu kubwa ya watu duniani wanafikiri kiulimwengu mzima. Njia kuu za mawasiliano na makampuni ya biashara yote ni ya kimataifa. Maisha yetu yanazidi kufungamana na ya wale mataifa mengine tunaposhirikiana mitindo, burudani, muziki, michezo, hata chakula cha kubeba. Labda nguo nyingi unazovaa na chakula ulichokula leo vilitengenezwa nchi nyingine. Tumefungamanishwa kuliko tunavyoweza kuelewa.

Hizi ni siku zinazopendeza kuwa hai. Kuna Wakristo wengi duniani sasa kuliko siku zozote zilizopita. Paulo alikuwa sahihi; “Habari hii Njema iliyowafikia ninyi inakwenda nje katika ulimwengu wote. Inabadilisha maisha kila mahali, kama tu ilivyowabadilisha maisha yenu.” Wakosai 1:6 (NLT)

Njia ya kuanza kufikiri kiulimwengu mzima ni kuanza kuombea nchi maalum. Wakristo wa tabaka la ulimwengu wote huombea ulimwengu. Huchukua ramani na kuanza kuombea mataifa kwa majina. Biblia inasema, “Kama ukiniomba nitakupa mataifa; watu wote duniani watakuwa wako.” Zaburi 2:8 (NCV)

Maombi ni silaha ya muhimu sana kwa utume wako duniani. Watu wanaweza kukataa upendo wetu, au kutupilia mbali ujumbe wetu, lakini hawawezi kuzuia maombi yetu. Kama kombora la kutoka bara moja kwenda bara jingine, unaweza kulenga maombi kwa moyo wa mtu hata kama uko umbali futi kumi au maili 10,000.

Je, uombee nini? Biblia hutuambia kuomba kwa ajili ya nafasi za kushuhudia, Wakolosai 4:3 (NIV) ujasiri wa kusema, Waefeso 6:19 (Msg) kwa wale watakaoamini, Yohana 17:20 (NIV) kwa ajili ya kuenea haraka ujumbe, (2 Wathesalonike 3:1) na kwa ajili ya watenda kazi zaidi. (Mathayo 9:38) Maombi hukufanya mshirika pamoja na wengine wote duniani kote.

Watu wanaweza kukataa upendo wetu, au kutupilia mbali ujumbe wetu lakini hawawezi kuzuia maombi yetu

Waombee pia wamishenari na yeyote yule anayejihusisha na uvunaji kiulimwengu mzima. Paulo aliwaeleza washirika wake wa kusali, “Pia mnashiriki katika kutusaidia mnapotuombea.” 2 Wakorintho 1:11 (GWT) Kama ungependa mapendekezo kwa ajili ya kuomba kwa ufahamu kwa ajili ya ulimwengu na watendakazi wakristo, angalia nyongeza ya 2.

Njia Nyingine ya kukuza kufikiri kiulimwengu mzima ni kusoma na kusikiliza habari kwa “macho ya Agizo Kuu.” Popote palipo na badiliko au mgogoro, unaweza kuwa na hakika kwamba Mungu atatumia nafasi hiyo kuwaleta watu kwake. Watu wana uwezekano mkubwa wa kumpokea Mungu wanapokuwa katika matatizo au katika mpito. Kwa sababu kasi ya mabadiliko inaongezeka katika ulimwengu wetu, watu wengi wako wazi kupokea Habari Njema sasa kuliko wakati mwingine wowote uliopita.

Njia bora ya kuelekea kufikiri kiulimwengu mzima ni kuinuka tu na kwenda katika umishenari wa muda mfupi katika nchi nyingine! Hakuna mbadala wa uzoefu wa moja kwa moja katika mila ya kingeni. Acha kusoma na kujadili utume wako, wewe anza kuutekeleza tu! Nakushauri ujaribu kuogelea katika kina kirefu. Katika Matendo 1:8 Yesu alitupatia kielelezo cha namna ya kuhusika, “Mtamweleza kila mtu habari zangu katika Yerusalemu, katika Uyahudi, katika Samaria, na kila mahali ulimwenguni.” Matendo 1:8 (CEV) Wafuasi wake walitakiwa wahubiri katika jamii ya watu wao (Yerusalemu), katika nchi yao (Uyahudi), katika mila nyingine (Samaria), na katika mataifa mengine (kila mahali ulimwenguni). Kumbuka agizo letu linatokea kwa wakati mmoja, siyo moja baada ya jingine. Wakati si kila mtu ana kipawa cha umishenari, kila Mkristo ameitwa kuwa na utume katika makundi yote manne. Je, wewe ni Mkristo wa Matendo 1:8?

Jiwekee lengo la kushiriki katika mradi wa utume katika vikundi vyote hivi vinne. Nakusihi uweke akiba na kufanya lolote linalowezekana ili ushiriki katika safari fupi za kimeshenari nje haraka iwezekanavyo. Karibu kila shirika la umisheni linaweza kukusaidia kufanya hivyo. Hii itakuza moyo wako, itapanua maono yako, na kukukuza imani yako, itakuza kwa kina huruma yako, na kukujaza furaha ambayo hujawahi kuwa nayo. Yaweza kuwa ni wakati wa kufanya mabadiliko makubwa katika maisha yako.

Acha kufikiri “hapa na sasa” anza kufikiri mambo ya milele. Ili kutumia vizuri muda wako duniani, lazima uwe na mtazamo wa umilele. Hii itakusaidia kuepuka kuweka kipaumbele katika mambo madogo na itakusaidia kutofuatisha mambo ya dharura na mambo ya kiini (au mambo ya mwisho wa yote). Paulo alisema, “Tunakaza macho yetu si kwa yale yanayoonekana – bali kwa yasiyoonekana. Kwa kuwa yanayaonekana ni mambo ya muda tu, lakini yasiyoonekana ni ya milele.” 2 Wakorintho 7:31 (Msg)

Mambo mengi tunayopoteza nguvu nyingi kuyafanya si ajabu hayatadumu hata mwaka mmoja tangu sasa, hayafai kwa umilele. Usiuze maisha yako kwa mambo ya muda tu. Yesu alisema, “Mtu yeyote atakayepotoshwa kutoka katika kazi ninayompangia hafai kwa ufalme wa Mungu.” Luka 9:62 (LB) Paulo akaonya, “Jishughulisheni mara chache iwezekanavyo na mambo yanayotokana na ulimwengu. Ulimwengu huu kama mnnavyouona unatoweka.” 1 Wakorintho 7:31 (Msg)

“Huwezi kwendaa nayo” – lakini biblia inasema unaweza kuituma mbele yako kwa kuwekeza kwa watu wanaokwenda huko!

Je, unaruhusu kitu gani kusimama katika njia ya utume wako? Ni nini kinachokuzuia kuwa Mkristo wa tabaka la ulimwengu wote? Chochote kiwacho, kiache. “Na tuvue kitu chochote kinachopunguza mwendo wetu au kuturudisha nyuma.” Waebrania 12:1 (LB)

Yesu alituambia, “Jiwekeeni akiba zenu mbinguni.” Mathayo 6:20-21 (CEV) Je, tunawezaje kufanya hivi? Katika moja ya misemo yake ambayo hueleweka vibaya, Yesu alisema, “Nawaambieni, tumieni mali ya dunia kujipatia marafiki, ili kwamba itakapokuwa imetoweka mtakaribishwa katika makao ya milele.” Luka 16:9 (NIV)

Yesu hakumaanisha wewe “kununua” marafiki kwa fedha. Aichomaanisha ni kuwa unapaswa kutumia fedha Mungu anazokupa kuleta watu kwa Yesu. Kisha watakuwa marafiki milele ambao watakukaribisha wewe utakapofika mbinguni! Ni uwekezaji mzuri wa kifedha ambao unaweza kuufanya.

Labda umewahi kusikia msemo “Huwezi kwenda nayo” – lakini Biblia inasema unaweza kuituma mbele yako kwa kuwekeza kwa watu wanaokwenda huko! Biblia inasema, “Kwa kufahamu hivi watakuwa wanajiwekea hazina ya kweli kwa ajili yao mbinguni – ni uwekezaji pekee ulio salama milele! Na pia wataishi maisha ya Kikristo yenye matunda hapa duniani.” 1 Timotheo 6:19 (LB)

Acha kufikiri udhuru na anza kufikiri njia za ubunifu ili kutimiza agizo lako. Kama una utayari, siku zote kuna njia ya kufanya hii kazi, na kuna mashirika yatakayokusaidia. Hapa kuna baadhi ya udhuru unaotolewa mara kwa mara:

l  Mimi nazungumza Kiingereza tu.” Hakika hii ni faida kwa nchi nyingi ambako mamilioni ya watu wanapenda kujifunza Kiingereza na wana shauku kukizungumza.

l  Sina chochote cha kutoa.” Ndiyo, unacho. Kila uwezo na uzoefu katika kufinyangwa kwako waweza kutumika mahali fulani.

l  Mimi ni mzee sana (au ni mdogo saana).” Mashirika mengi ya umisheni yana miradi ya muda mfupi.

Hata kama Sara alidai kuwa mzee sana na asingeweza kutumiwa na Mungu au Yeremia alidai kuwa mtoto sana, Mungu alikataa udhuru wao. “Usiseme hivyo, Bwana akajibu, ‘kwa kuwa ni lazima uende popote nitakapokutuma na kusema chochote nitakachokuambia. Na usiwaogope watu, kwa kuwa nitakuwa pamoja nawe na nitakuangalia.’” Yeremia 1:7-8 (NLT)

Labda umeamini kwamba ulihitaji “wito” maalum kutoka kwa Mungu, na umekuwa unasubiri hisia za kimiujiza au tendo lolote la miujiza. Lakini Mungu tayari ameshasema wito wake mara nyingi. Sote tumeitwa kutimiza malengo matano ya Mungu kwa ajili ya maisha yetu: kuabudu, kuwa na ushirika, kukua na kukfanana ya Yesu, kutumika, na kuwa katika utume na Mungu duniani. Mungu hapendi kutumia baadhi ya watu tu; anapenda kuwatumia watu wake wote. Sote tumeitwa kuwa katika utume wa Mungu. Anapenda kanisa lake lote kuchukua Injili yake yote katika ulimwengu wote. Marko 8:35 (LB)

Wakristo wengi wamekosa mpango wa Mungu kwa sababu kamwe hawajawahi hata kumuuliza Mungu kama alitaka kutumika kama wamishenari mahali fulani. Ikiwa ni kwa hofu au kutokujua, moja kwa moja wamefumba akili zao kuhusu uwezekano wa kutukmika kama wamishenari wa kukaa katika eneo la mila tofauti. Kama unajaribiwa kusema hapana, unatakiwa kuchunguza njia zote tofauti na uwezekano wowote uliopo sasa (itakushangaza), na unapaswa kumwomba na kumuuliza Mungu anachotaka kutoka kwako kwa miaka yako ya mbele. Maelfu ya wamishenari wakazi wanatakiwa mno katika kipindi hiki cha kihistoria wakati milango mingi inafunguka kuliko ilivyowahi kutokea.

Iwapo unataka kuwa kama Yesu, ni lazima uwe na moyo kwa ajili ya ulimwengu mzima. Huwezi kutoshelezwa na jamaa yako na rafiki zako tu kuona wakija kwa Yesu. Kuna zaidi ya watu bilioni 6 katika ulimwengu, na Yesu anapenda watoto wake wote waliopotea wapatikane. Yesu alisema, “Ni wale tu wanaotoa maisha yao kwa ajili yangu na kwa ajili ya Habari Njema ndio watakaojua maana hasa ya kuishi.” Agizo Kuu ni Agizo lako, na kufanya sehemu yako ndiyo siri ya kuishi maisha yenye maana.

SIKU YA THELATHINI NA NANE

KUFIKIRI JUU YA LENGO LANGU

Jambo la Kutafakari: Agizo Kuu ni Agizo langu.

Kifungu cha Kukumbuka:Tutume ulimwenguni na habari za nguvu zako za kuokoa na mpango wako wa milele kwa wanadamu wote.” Zaburi 67:2 (LB)

Swali la Kujiuliza: Je, ni hatua gani ninazoweza kuchukua ili kujiandaa kwenda katika umisheni wa muda mfupi mwaka ujao?

Siku ya Thelathini na Tisa: Kusawazisha Maisha Yako

Muishi maisha mkijua kuwajibika, si kama wale wasiojua

maana ya maisha lakini kama wanaofahamu.

Waefeso 5:15 (Ph)

Msiruhusu makosa ya watu waovu yawapeleke katika njia

iliyopotoka na kuwafanya kupoteza msimamo wenu.

2 Petro 3:17 (CEV)

Wamebarikiwa wenye maisha yaliyosawazishwa; wataishi muda mrefu kuliko kila mtu.

Moja ya matukio katika Michezo ya Olimpiki ni mchezo wa pantathloni. Mchezo huu una matukio matano: kupiga bunduki, kupigana kwa panga, kupanda farasi, kukimbia, na kuogelea. Mwana michezo wa pantathloni ana lengo la kufanikiwa katika maeneo yote matano, siyo tu katika moja au mawili.

Maisha yako ni kama mchezo wa pantathloni yenye malengo matano, ambayo lazima uyaweke katika usawa. Malengo haya yalitekelezwa na Wakristo wa kwanza katika Matendo 2, yameele zwa na Paulo, na Kristo alitoa kielelezo chake katika Yohana 17, lakini yameandikwa kwa muhtasari katika Amri Kuu na Agizo Kuu la Yesu. Kauli hizi mbili ni jumla ya yote yaliyo katika kitabu hiki – malengo matano ya Mungu kwa maisha yako.

1.         “Mpende Mungu kwa moyo wako wote”: Ulikusudiwa kwa ajili ya furaha ya Mungu, hivyo lengo lako ni kumpenda Mungu kwa njia ya kuabudu.

2.         “Mpende jirani yako kama nafsi yako”: Ulifinyangwa kwa ajili ya kumtumikia, hivyo lengo lako ni kuonyesha upendo kwa wengine kwa njia ya huduma.

3.         “Nendeni mkafanye wanafunzi”: Uliumbwa kwa ajili ya utume, hivyo lengo lako ni kuwashirikisha wengine ujumbe wa Mungu kwa njia ya uinjilisti.

4.         “Wabatizeni katika …”: Uliumbwa kwa ajili ya jamii ya Mungu, hivyo lengo lako ni kuwa mmoja wa watu wa kanisa lake kwa njia ya ushirika.

5.         “Wafundisheni kuyashika mambo yote …”: Uliumbwa ili ufanane na Kristo, hivyo lengo lako ni kukua kufikia utu uzima kwa njia ya mafundisho.

Kujitoa kwa kiwango kikubwa kutii Amri Kuu na Agizo Kuu kutakufanya Mkristo aliyefanikiwa.

Kujitoa kwa kiwango kikubwa kutii Amri Kuu na Agizo Kuu kutakufanya mkristo aliyefanikiwa.

Kutunza malengo haya matano katika usawa siyo rahisi. Sote hujaribu kukazia zaidi malengo tunayohisi kuwa na shauku zaidi nayo na hivyo kuyaacha yale mengine. Makanisa hufanya hivyo hivyo. Lakini unaweza kutunza maisha yako katika usawa na katika mwelekeo kwa kujiunga na kikundi kidogo kwa uwajibikaji, kwa kutathmini afya yako ya kiroho mara kwa mara, kwa kuweka ratiba ya maendeleo yako katika kitabu chako cha kumbukumbu, na kwa kuwapa watu yale mengine unayojifunza. Hizi ni kazi nne za muhimu kwa kuishi maisha yanayoongozwa na malengo. Kama una bidii katika kudumu katika mwelekeo huu, utahitaji kukuza tabia hizi.

Zungumza juu yake na rafiki wa kiroho au kikundi kidogo cha kiroho. Njia bora ya kuweka ndani ya moyo kanui za kitabu hiki ni kuzijadili na wengine katika kikundi kidogo. Biblia inasema, “Kama chuma kinavyonoa chuma kingine, ndivyo watu wanavyoweza kuinuana.” Mithli 27:17 (NCV) Tunajifunza vizuri zaidi katika jamii. Mawazo yetu yananolewa na imani zetu zitakuwa kwa kina kwa njia ya mazungumzo.

Ninakusihi sana ukusanye kikundi kidogo cha marafiki na mtengeneze Kikundi cha Kujisomea cha Maisha Yanayoongozwa na Malengo ili kuzipitia sura za kitabu hiki kila juma. Uliza “Kwa hiyo?” na “Sasa nini?” Je, jambo hili lina maana gani kwangu, kwa jamaa yangu, na kwa kanisa letu? Je, nitafanya nini juu ya hili? Paulo alisema, “Yatendeni yale mliyojifunza.” Wafilipi 4:9 (TEV) Katika nyongeza ya 1, nimeandaa orodha ya maswali ya kujadili kwa ajili ya vikundi vyenu vidogo au kwa matumizi ya shule ya Jumpapili.

Kikundi kidogo cha kujisomea kina faida nyingi ambazo kitabu tu hakiwezi kuzitoa. Unaweza kutoa na kupokea majibu kuhusu unachojifunza. Mnaweza kujadili mifano halisi ya maisha. Mnaweza kuombeana, kutiana moyo, na kusaidiana mara mnapoanza kutendea kazi malengo haya. Kumbuka, tumekusudiwa kukua pamoja, siyo kwa kutengana. Biblia inasema, “Tianeni moyo na kupeana nguvu kila mmoja.” 1 Wathesalonike 5:11 (NCV) Baada ya kupitia kitabu hiki chote kama kikundi, mnaweza kuamua kujifunza masomo mengine ya maisha yanayoongozwa na malengo ambayo yanapatikana kwa ajili ya madarasa au vikundi (tazama nyongeza ya 2).

Pia nakutia moyo kujifunza Biblia wewe binafsi. Nimetia katika rejea zaidi ya Maandiko elfu moja yaliyotumika katika kitabu hiki ili uyasome katika mazingira yake. Tafadhali soma nyongeza ya 3, ambayo inaeleza kwa nini kitabu hiki kinatumia tafsiri nyingi tofauti. Ili kuzifanya sura hizi ziwe na urefu unaofaa kwa kusomwa kwa siku moja, sikuweza kuelezea mazingira ya kila mistari iliyotumika. Lakini Biblia imekusudiwa kusomwa kwa kufuata aya (paragraphs), sura, au hata vitabu vyote. Kitabu change kiitwacho Njia za Kujifunza Biblia Wewe Binafsi kinaweza kukuonyesha jinsi ya kujifunza kwa hoja.

Jifanyie mwenyewe uchunguzi wa mara kwa mara wa kiroho. Njia bora ya kuweka katika usawa yale malengo matano katika maisha yako ni kujipima mwenyewe kwa vipindi. Mungu anathamini sana tabia ya kujitathmini binafsi. Angalau mara tano katika Maandiko tumeambiwa kujaribu na kupima afya yetu ya kiroho. Maombolezo 3:40 (NLT); 1 Wakorintho 11:28 (NLT); 31 (TEV) 13:5 (Msg); Wagalatia 6:4 (NIV). Biblia inasema, “Jiraribuni wenyewe ili kuhakikisha mko imara katika imani. Msijiendee tu bila kuwa makini. Jifanyieni wenyewe uchunguzi wa mara kwa mara … Pimeni. Mkianguka jaribio, fanyeni kitu juu ya hilo.” 2 Wakorintho 8:11 (LB)

SIKU YA THELATHINI NA TISA:

KUSAWAZI SHA MAISHA YAKO

Ili kutunza afya yako ya mwili, unahitaji kupimwa mara kwa mara na daktari anayeweza kukuangalia dalili muhimu – msukumo wa damu, joto, uzito na mengineyo. Kwa afya yako ya kiroho unahitaji kupima mara kwa mara dalili tano muhimu za kuabudu, ushirika, kukua tabia, huduma, na utume. Yeremia alishauri, “Hebu tujichunguze namna tunavyoishi na tuyatengeneze maisha yetu kwa uongozi wa Mungu.” Maombolezo 3:40 (Msg)

Katika kanisa la Saddleback tumetengeneza chombo rahisi cha kujitathmini mtu binasfsi ambacho kimesaidia maelfu ya watu wadumu katika lengo la Mungu. Kama utapenda kupata nakala ya chombo hiki cha kupima afya ya kiroho ya maisha yanayoongozwa na malengo, unaweza kunitumia barua pepe (tazama nyongeza ya 2). Utashangaa jinsi gani chombo hiki kidogo kitavyokusaidia uweke maisha yako katika usawa kiafya na katika kukua. Paulo alisihi, “Hebu lile wazo lenu la kupenda la pale mwanzoni liwe sawa na kutenda kwenu halisi sasa.” 2 Wakorintho 8:11 (LB)

Andika maendeleo yako katika kitabu chako cha kumbukumbu (journal). Njia bora ya kutia nguvu maendeleo yako katika kutimiza malengo ya Mungu kwa maisha yako ni kutunza ratiba ya mambo yako ya kiroho. Hiki siyo kitabu cha matukio, lakini ratiba ya masomo ya maisha ambayo hupendi kuyasahau. Biblia husema, “Ni muhimu kuyashika sana yale tuliyoyasikia ili tusije tukapotoka.” Waebrania 2:1 (Msg) Tunakumbuka kile tunachorekodi.

Kuandika husaidia kuchanganua kile Mungu anafanya maishani mwako. Dawson Trotman alizoea kusema. “Mawazo hujichanganua yenyewe yanapopita katika ncha za vidole vyako.” Biblia ina mifano kadhaa ya Mungu akiwaambia watu kutunza rekodi ya kiroho. Insema, “Kwa uongozi wa Mungu, Musa alitunza rekodi ya maandishi ya safari yao.” Hesabu 33:2 (NLT) Je, huna furaha kwamba Mungu alitii Agizo la Mungu la kutunza rekodi ya safari ya kiroho ya Waisraeli? Angekuwa mvivu, tungeibiwa masomo makubwa ya maisha katika kitabu cha Kutoka.

Ingawa haiwezekani kwamba rekodi yako ya kiroho itasomwa sana kama ile ya Musa, hata ile yako bado ni ya muhimu. Tafsiri mpya ya kimataifa ya Biblia (NIV) inasema, “Musa aliandika hatua za safari yao.” Maisha yako ni safari, na safari inastahili rekodi. Natumaini utaandika kuhusu hatua za safari yako ya kiroho katika kuishi maisha yanayoongozwa na malengo.

Usiandike tu yale mambo ya kupendeza. Kama Daudi alivyofanya, andika mashaka yako, hofu, na mashindano na Mungu. Masomo mengine makubwa hutokana na maumivu, na Biblia inasema Mungu hutunza rekodi ya machozi yetu. Zaburi 56:87 (TEV) Kila matatizo yanapotokea, kumbuka kwamba Mungu huyatumia kutimiza malengo yote matano katika maisha yako: Matatizo hukulazimisha kumwelekea Mungu, hukusogeza kwa wengine katika ushirika, hujenga tabia ya mfano wa Kristo, hukupatia huduma, na hukupatia ushuhuda. Kila tatizo linaongozwa na malengo.

Katikati ya hali ya maumivu, Mwandishi wa Zaburi alisema, “Andika kwa ajili ya kizazi kijacho mambo ambayo BWANA amefanya, ili kwamba watu ambao hawajazaliwa wapate kumtukuza.” Zaburi 102:18 (TEV) Unadaiwa na vizazi vijavyo kutunza ushuhuda wa jinsi Mungu alivyokusaidia upate kutimiza malengo yake duniani.

Wajulishe wengine yale unayoyajua. Kama unataka uendelee kukua, njia bora ya kujifunza zaidi ni kuwapatia wengine mambo ambayo tayari umejifunza. Mithali hutuambia, “Mtu anayewabariki wengine anabarikiwa sana, wale wanaosaidia wengine husaidiwa.“ Mithali 11:25 (Msg) Wale wanaowagawia wengine ufahamu hupokea zaidi toka kwa Mungu.

Unadaiwa na vizazi vijavyo kutunza ushuhuda wa jinsi Mungu alivyokusaidia upate kutimiza malengo yake duniani

Kwa kuwa sasa unaelewa lengo la maisha, ni wajibu wako kupeleka ujumbe kwa wengine. Mungu anakuita uwe mhudumu wake. Paulo alisema, “Sasa nataka uwaambie mambo haya wafuasi wanaoweza kuaminika kuwaambia wengine.“ 2 Timotheo 2:2b (CEV) Katika kitabu hiki nimekupatia mambo ambayo wengine walinifundisha kuhusu lengo la maisha; sasa ni wajibu wako kuwapatia wengine mambo uliojifunza.

Labda unajua aina ya watu ambao hawajui lengo la maisha. Washirikishe ukweli huu watoto wako, rafiki zako, jirani zako, na wale unaofanya kazi nao. Ukimpa kitabu hiki rafiki yako, ongeza maelezo yako binafsi kwenye ukurasa wa kuweka wakfa (dedication).

Kadiri unavyojua zaidi, ndivyo Mungu anavyokutegemea kutumia maarifa hayo kusaidia wengine. Yakobo alisema, “Mtu yeyote anayefahamu jambo sahihi la kufanya, lakini halifanyi, anatenda dhambi.” Yakobo 4:17 (NCV) Maarifa huongeza uwajibikaji. Lakini kuwapatia wengine malengo ya maisha ni zaidi ya wajibu, ni moja ya upendeleo mkubwa katika maisha. Fikiri ambavyo ulimwengu ungekuwa kama kila mmoja angejua lengo lake. Paulo alisema, “Iwapo utafundisha ukweli huu kwa wafuasi wenginel, utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu.” 1 Timotheo 4:6 (CEV)

YOTE NI KWA AJILI YA UTUKUFU WA MUNGU

Sababu ya kuwapatia wengine mambo tunayojifunza ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu na kukua kwa ufalme wake. Usiku ule kabla ya kuteswa msalabani, Yesu alitoa maelezo kwa Baba yake, “Nimekuletea utukufu duniani kwa kukamilisha kazi uliyonipa nifanye” Yohana 17:4 (NIV) Yesu aliposali maneno haya, alikuwa hajafa bado kwa ajili ya dhambi zetu, hivyo ni “kazi” gani alikuwa ameikamilisha? Kwa tukio hili alikuwa akitaja kitu kingine siyo kifo cha msalabani. Jibu liko katika yale aliyosema katika vifungu ishirini vinavyofuata vya sala yake. (Yohana 17: 6-26)

Yesu alimwambia Baba yake kile alichokuwa anakifanya kwa miaka mitatu iliyopita: kuwaandaa wafuasi wake kuishi kwa ajili ya malengo ya Mungu. Aliwasadia kumjua na kumpenda Mungu (kuabudu), aliwafundisha kupendana (ushirika), aliwapa Neno ili wakue kufikia utu uzima (mafundisho), aliwaonyesha namna ya kutumika (huduma), na aliwatuma nje kuwaeleza wengine (utume). Yesu alitoa kielelezo cha maisha yanayoongozwa na malengo, na aliwafundisha wengine pia namna ya kuishi hivyo. Hiyo ndiyo “kazi” iliyoleta utukufu kwa Mungu.

Leo Mungu anatuitia kazi hiyo hiyo. Hapendi tu tuishi maisha ya malengo yake, anatutaka pia tuwasaidie wengine wafanye vivyo hivyo. Mungu anapenda tuwatambulishe watu kwa Yesu, kuwaleta katika ushirika wake, kuwasaidia wakue kufikia utu uzima na wagundue nafasi yao katika huduma, na kisha kuwatuma nje kuwafikia wengine pia.

Hili ndilo kusudi zima la maisha yanayoongozwa na malengo. Bila kujali umri wako, maisha yako yaliyosalia yaweza kuwa yenye maana zaidi kuliko yaliyopita, na unaweza kuanza kuishi kwa malengo leo hii.

SIKU YA THELATHINI NA TISA

KUFIKIRI JUU YA LENGO LANGU

Jambo la Kutafakari: Wamebarikiwa wenye maisha yaliyosawazishwa.

Kifungu cha kukumbuka: Mwishi maisha mkijua kuwajibika, si kama wale wasiojua maana ya maisha, lakini kama wanaofahamu. Waefeso 5:15 (Ph)

Swali la Kujiuliza: Ni ipi kati ya zile kazi nne nitaanza kutenda ili nikae katika njia na kusawazisha malengo matano ya Mungu kwa maisha yangu?

 Siku ya Arobaini: Kuishi Kwa Malengo

Moyo wa binadamu una mipango mingi, lakini kusudi la Mungu ndilo hufanikiwa.

Mithali 19:21 (NIV)

Kwa kuwa Daudi … alitumikia kusudi la Mungu katika kizazi chake.

Matendo 13:36 (NASB)

Kuishi kwa malengo ndiyo njia pekee ya kuishi hasa. Vinginevyo ni kwa hai tu.

Watu wengi hufanya bidii katika mambo matatu ya msingi katika maisha. La kwanza ni utambulisho: “Mimi ni nani?” La pilii ni umuhimu: “Je, mimi nina maana?” La tatu ni mchango: “Nafasi yangu ni ipi katika maisha?” Majibu kwa maswali yote matatu yanapatikana katika malengo matano ya Mungu kwa ajili yako.

Katika chumba cha juu, Yesu alipokuwa alipokuwa anahitimisha siku yake ya mwisho ya huduma pamoja na wanafunzi wake, aliwaosha miguu kama kielelezo na alisema, “Kwa kuwa sasa mnajua mambo haya, mtabarikiwa kama mkiyatenda.” Yohana 13:17 (NIV) Unapofahamu kile Mungu anapenda ufanye, Baraka huja kwa kutenda jambo hilo. Tunapofikia mwisho wa safari yetu ya siku arobaini pamoja, na kuwa sasa unajua malengo ya Mungu kwa maisha yako, utabarikiwa kama utayatenda.

Hii labda ina maana utalazimika kuacha kutenda baadhi ya mambo. Kuna mambo mengi “mazuri” unayoweza kufanya na maisha yako, lakini malengo ya Mungu ni mambo ya muhimu matano ambayo lazima uyatende. Kwa bahati mbaya, ni rahisi kuchukuliwa na mengine na ukasahau mambo ya muhimu. Ni rahisi kuacha njia ya mambo ya muhimu zaidi na pole pole unakwenda mbali kabisa. Ili kuzuia hali hii isitokee, jitengenezee kauli ya lengo la maisha yako na uiangalie mara kwa mara.

KAULI YA KUSUDI LA MAISHANI NINI?

Ni kauli inayotoa kwa muhtasai malengo ya Mungu kwa maisha yako. Katika maneno yako mwenyewe unathibitisha kujitoa kwako kwa ajili ya malengo matano ya Mungu kwa maisha yako. Kauli ya kusudi la maisha si orodha ya malengo. Malengo (goals) ni ya muda mfupi; makusudi (purposes) ni ya milele. Biblia inasema, “Mipango yake yadumu milele; na makusudi yake ni ya milele.” Zaburi 33:11 (TEV)

Ni kauli inayoonyesha mwelekeo wa maisha yako. Kuandika kwenye karatasi malengo yako itakulazimisha kufikiri bayana kuhusu njia za maisha yako. Biblia inasema, “Fahamu unakoelekea, na utakaa mahali palipo imara.” Mithali 4:26 (CEV) Kauli ya kusudi la maisha haihitaji tu mambo unayokusudia kufanya na maisha yako, muda na pesa zako, lakini pia huashiria ni mambo gani hutayafanya. Mithali husema, “Mtu mwenye akili hulenga matendo ya busara, lakini mpumbavu huwa na mielekeo mingi.” Mithali 17:24 (TEV)

Ni kauli inayofafanua “mafanikio” kwa ajili yako. Hutaja unachokiamini kuwa cha muhimu, siyo kile ulimwengu unasema kuwa ni cha muhimu. Huchanganua mambo ya muhimu kwako. Paulo alisema, “Nataka ninyi muelewe kilicho cha muhimu hasa.” Wafilipi 1:10 (NLT)

Ni kauli inayochanganua majukumu yako. Utakuwa na majukumu tofauti katika hatua tofauti za maisha, lakini malengo yako kamwe kayatabadilika. Ni makubwa kuliko jukumu lolote utakalokuwa nalo.

Ni kauli inayoeleza umbo lako. Ni taswira ya njia za pekee Mungu alizokuumba umtumikie.

Chukua muda kuandika kauli ya kusudi la maisha yako. Usijaribu kuimaliza kwa kikao kimoja, na usilenge ukamilifu katika hatua ya kwanza ya kuandika; wewe andika tu mawazo yako. Ni rahisi kusahihisha kuliko kutengeneza. Yafuatayo ni maswali matano unayoweza kuyatumia unapoandika kauli yako.

MASWALI MAKUU MATANO YA MAISHA

Mungu anapokuwa katikati ya misha yako unaabudu. Anapokuwa hayupo unahofu.

Nini kitakuwa kiini cha maisha yangu? Hili ni swali la kuabudu. Je, nani utamwishia? Je, utajenga maisha yako kwenye nini? Unaweza kufanya kazi yako kuwa kiini cha maisha yako, au jamaa yako, michezo, fedha, burudani, na shughuli nyingine vyaweza kuwa kiini chako. Vitu hivi ni vizuri, lakini siyo kiini cha maisha yako. Hakuna kilicho imara kiasi cha kukushika pamoja mara maisha yako yakianza kuparaganyika. Unahitaji kiini kisichotikisika.

Mfalme Asa aliwaambia watu wa Yuda “kumfanya Miungu kiini cha maisha yao.” 2 Nyakaati 14:4 (Msg) Kwa kweli, chochote kilicho katikati ya maisha yako ni Mungu kwako. Ulipomkabidhi Yesu maisha yako, aliingia katikati lakini lazima udumu kumpa nafasi hiyo kwa njia ya ibada. Paulo anasema, “Naomba kwamba Kristo akae vizuri mioyoni mwenu.” Waefeso 3:17 (NLT)

Je, unafahamuje ni lini Mungu yuko katikati ya maisha yako? Mungu anapokuwa katikati, unaabudu. Na anapokuwa hayupo, una hofu. Hofu ni onyo kwamba Mungu amewekwa pembeni. Mara unapomrudisha katikati unapata amani tena. Biblia inasema, “Ufahamu wa utimilifu wa Mungu … utawajia na kuwapa amani. Inafurahisha ajabu kwa kinachotokea Kristo anapoondoa hofu na kukaa katikati ya maisha yenu.” Wafilipi 4:7 (Msg)

Je, maisha yangu yatakuwa na tabia gani? Hili ni swali la uanafunzi. Je, utakuwa mtu wa aina gani? Mungu anapenda zaidi wewe ulivyo kuliko yale unayoyatenda. Kumbuka, utachukuwa tabia yako katika umilele, lakini siyo kazi yako. Fanya orodha ya sifa za tabia unazotaka kuzikuwa katika maisha yako. Ungeweza kuanza na tunda la Roho (Wagalatia 5:22-23) au maneno ya Heri ya Yesu. (Mathayo 5:3-12)

SIKU YA AROBAINI

KUISHI KWA MALENGO

Petro alisema, “Msipoteze hata dakika moja katika kujenga juu ya kile mlichopewa, mkiikamilisha imani yenu kwa tabia yenu njema, ufahamu wa kiroho, kukesha, subira, utauwa, ukarimu, na upendo.” 2 Petro 1:5 (Msg) Usivunjike moyo na kukata tamaa unapojikwaa. Inachukua muda wa maisha yako yote kujenga tabia ya mfano wa Kristo. Paulo alimwambia Timotheo, “Angalia kwa makini tabia na mafundisho yako. Usipotoshwe. Wewe dumu katika hilo.” 1 Timotheo 4:16b (Msg)

Je, maisha yangu yatakuwa na mchango gani? Hili ni swali la utumishi. Je, huduma yako itakuwa ipi katika mwili ya Kristo? Kufahamu mseto wa karama zako za rohoni, moyo yako, vipawa, hulka, na uzoefu wako (SHAPE), majukumu gani yangekufaa katika jamii ya Mungu? Je, unawezaje kufanya tofauti? Je, kuna kundi maalum katika Mwili wa Kristo ambalo nimefinyangwa ili nilitumikie? Paulo alitaja faida mbili za ajabu unapotekeleza huduma yako: “Huduma hii mnayoifanya haikidhi tu mahitaji ya watu wa Mungu, lakini pia inaleta shukrani nyingi kwa Mungu.” 2 Wakoorintho 9:12 (TEV)

Ingawa umefinyangwa kuwatumikia wengine, hata Yesu hakutimiza mahitaji ya kila mtu alipokuwa duniani. Lazima uchague ni watu gani unaweza kuwasaidia vizuri zaidi, kulingana na SHAPE lako. Unahitaji kuuliza, “Nina hamu ya kumsaidia nani zaidi?” Yesu alisema, “Nimewatuma kwenda nje ili kuzaa matunda, matunda yatakayodumu.” Yohana 15:16a (NJB) Kila mmoja wetu anazaa matunda tofauti.

Je, mawasiliano ya maisha yangu ni yapi? Huu ni utume wako kwa wasioamini. Kauli ya utume wako ni sehemu ya kaulli ya kusudi la maisha yako. Hii ni pamoja na kujitoa kwako kushirikisha wengine ushuhuda wako na Habari Njema. Ni lazima pia uorodheshe masomo ya maisha na shauku ya kimungu unayohisi Mungu amekupa kuwashirikisha walimwengu. Unapoendelea kuku katika Kristo, Mungu anaweza kukupa kundi maalum la watu ili ulenge kuwafikia. Hakikisha unaongeza hili katika kauli yako.

Kama wewe ni mzazi, sehemu ya utume wako ni kukuza watoto wako katika kumjua Kristo, kuwasaidia wajue malengo yake kwa maisha yao, na kuwatuma katika utume wao duniani. Unaweza kuongeza kauli ya Yoshua katika kauli yako: “Kwa kuwa mimi na jamaa yangu, tutamtumikia BWANA.” Yoshua 24:15 (NLT)

Bila shaka, maisha yetu lazima yaunge mkono na kuthibitisha ule ujumbe tunaoutangaza. Kabla watu wengi wasioamini kuikubali Biblia kuwa ya kweli wanapenda kujua kwamba sisi ni wa kweli. Biblia inasema, “Hakikisheni mnaishi kwa namna ambayo huiletea heshima Habari Njema ya Yesu.”Wafilipi 11:27 (NCV)

Je ni jamii gani nitakayoshirikiana nayo katika maisha yangu? Hili ni swali juu ya ushirika. Ni jinsi gani utaonyesha kujitoa kwako kwa waamini wengine na kuwa na mwungano na jamii ya Mungu? Ni wapi ambapo utafanyia mazoezi amri za “ninyi kwa ninyi” na Wakristo wengine? Ni katika jamii ya kanisa gani utajiunga kama mshirika aliye hai? Kadiri unavyokomaa, ndivyo utakavyozidi kuupenda Mwili wa Kristo na kujitoa kwa ajili yake. Ndiyo maana Biblia husema, “Kristo alilipenda kanisa na akatoa maisha yake kwa ajili ya kanisa.” Waefeso 5:25 (TEV) Lazima uweke maelezo ya upendo wako kwa kanisa katika kauli yako.

Kabla watu wengi wasioamini kuikubali Biblia kuwa ya kweli wanapenda kujua kwamba sisi ni wa kweli.

Unapofikiria majibu yako kwa maswali haya, ambatanisha Maandiko yoyote yanayosema nawe katika kila moja ya malengo haya. Yako mengi katika kitabu hiki. Yaweza kukuchukua majuma au miezi kadhaa kuweza kuundaa kauli ya kusudi la maisha yako kama unavyopenda. Omba, fikiri juu yake, ongea na rafiki zako wa karibu, na tafakari Maandiko. Unaweza kuandika nakala kadhaa na kurekebisha kabla ya kufikia nakala ya mwisho. Hata hapo, labda utafanya mabadiliko madogo kadiri muda unapopita na Mungu akaendelea kukupa ufahamu zaidi katika hali yako mwenyewe. Kama ungependa kuona mifano kadiri kutoka watu wengine, wewe nitumie barua pepe (angalia nyongeza 2).

Kwa nyongeza juu ya kuandika kwa kina kauli ya kusudi la maisha, pia inasaidia kuwa na kauli fupi ambayo ni muhtasari wa malengo matano ya maisha yako kwa njia ambayo ni rahisi kukumbuka na inayokutia hamasa. Hivyo unaweza kujikumbusha kila siku. Sulemani alishauri, “Itakuwa vyema kutunza mambo haya akilini mwako ili uwe tayari kuyarudia.” Mithali 22:18 (NCV) Hapo kuna mifano mitano:

l  “Kusudi la maisha yangu ni kumwabudu Kristo kwa moyo wangu, kumtumikia kwa umbo langu nishiriki na jamii yake, nikue katika mfano wake kitabia, na kutimiza utume wake duniani ili apokee utukufu.”

l  “Kusudi la maisha yangu ni kuwa mshirika wa jamii ya Kristo, kielelezo cha tabia yake, mhudumu wa neema yake, mjumbe wa Neno lake, na mwinuaji wa utukufu wake.”

l  “Kusudi la maisha yangu ni kumpenda Kristo, kukua katika Kristo, kumtangaza Kristo, na kumtumikia Kristo kupitia kanisa lake, na kuongoza jamii yangu na wengine ili wafanye vivyo hivyo.”

l  “Kusudi la maisha yangu ni kujitoa kwa kina kutekeleza Agizo Kuu na Amri Kuu.”

l  Lengo langu kuu ni kufanana na Kristo; jamii yangu ni kanisa; huduma yangu ni _______________________; utume wangu ni ___________________; nia yangu ni utukufu kwa Mungu.”

Unaweza kushangaa, Je, vipi kuhusu mapenzi ya Mungu kwa kazi yangu au ndoa yangu, au wapi ninapotakiwa kuishi, au kwenda shule? Kusema ukweli haya ni mambo yanayochukua nafasi ya pili katika maisha yako, na kuna uwezekano mwingi ambao wote ungeweza kuwa katika mapenzi ya Mungu kwako. Cha muhimu zaidi kuliko vyote ni kwamba utimize malengo ya Mungu ya milele bila kujali wapi unaishi au kufanya kazi au nani utamwoa. Maamuzi hayo lazima yaunge mkono malengo yako. Biblia inasema, “Moyo wa binadamu una mipango mingi, lakini kusudi la Mungu ndilo hufanikiwa.” Mithali 19:21 (NIV) Eleza moyo wako kwenye malengo ya Mungu kwa maisha yako, siyo mipango yako, kwa kuwa hayo ndiyo yatadumu milele.

Niliwahi kusikia pendekezo kwamba unatengeneza kauli ya kusudi la maisha yako kwa kuzingatia mambo ambayo ungependa wengine waseme kwenye msiba wako. Hebu fikiri juu ya hotuba kamili ya kukusifia, kisha jenga kauli yako hapo. Kusema wazi, huo ni mpango mbaya. Mwisho wa maisha yako haitakuwa na maana sana watu wengine watasemaje juu yako. Kitu cha muhimu sana wakati huo ni kile atakachosema Mungu kuhusu wewe. Biblia inasema, “Lengo letu ni kumpendeza Mungu, siyo watu.” 1 Wathesalonike 2:4b (NLT)

Siku moja Mungu atapima majibu yako kwa maswali haya ya maisha. Je, ulimweka Yesu katikati ya maisha yajayo? Je, ulitoa maisha yako kuwatumikia wengine? Je, ulitangaza ujumbe wake na kutimiza utume wake? Je, uliipenda na kushiriki katika jamii yake? Haya ndiyo mambo pekee yatakayokuwa ya maana. Kama Paulo alivyosema, “Lengo letu ni kufikia mpango wa Mungu kwa ajili yetu.” 2 Wakorintho 10:13 (LB)

MUNGU ANAPENDA KUKUTUNIA

Kama miaka thelathini iliyopita, niligundua fungu dogo la maneno katika Matendo 13:36 ambalo lilibadili kabisa mwelekeo wa maisha yangu. Lilikuwa na maneno saba tu, lakini kama kwa muhuri wa chuma cha moto, maisha yangu yalitiwa alama ya kudumu kwa maneno haya: “Daudi alitumikia kusudi la Mungu katika kizazi chake. “ (Matendo 13:36a) Sasa nilielewa kwa nini Mungu alimwita Daudi “Mtu aupendezaye moyo wangu.” (Matendo 13:22) Daudi aliweka wakfu maisha yake kumtumikia Mungu duniani.

Hakuna maandishi ya kwenye kaburi yanayoweza kuzidi kauli hiyo! Hebu fikiri kama maneno hayo yatachongewa kwenye jiwe la kaburi lako: Kuwa ulitumikia kusudi la Mungu katika kizazi chako. Maombi yangu ni kwamba watu wataweza kusema hivyo nitakapokufa. Ni maombi yangu pia kwamba watu wataweza kusema hivyo utakapokufa Ndiyo maana nimekuandikia kitabu hiki.

Fungu la maneno haya mafupi ni ufafanuzi wa maisha sahihi. Unafanya mambo ya milele yasiyozuiliwa na wakati (malengo ya Mungu) katika njia ya kisasa na inayokubalika (katika kizazi chako). Hili ndilo kusudi zima la maisha yanyoongozwa na malengo. Kizazi kilichopita wala kijacho hakiwezi kumtumikia Mungu katika kizazi hiki. Sisi tu tunaweza. Kama Esta, Mungu alikuumba “Kwa ajili ya wakati kamam huu.” (Esta 4:14)

Mungu bado anatafuta watu wa kutumia. Biblia inasema, “Macho ya Bwana yanaangalia duniani kote ili kuwaimarisha wale wenye moyo uliojitoa kwa ajili yake.” 2 Nyakati 16:9 (NLT) Je, unaweza kuwa mtu anayeweza kutumiwa na Mungu kwa kusudi lake? Je, utatumikia kusudi la Mungu katika kizazi chako?

Unaweza kuanza kuishi kwa malengo leo.

Paulo aliishi maisha yenye kuongozwa na malengo. Alisema, “Nakimbia moja kwa moja kuelekea lengo nikiwa na kusudi kila hatua.” 1 Wakorintho 9:26 (NLT) Sababu yake ya pekee ya kuishi ilikuwa kutimiza malengo ya Mungu kwa ajili yake. Alisema, “Kwangu mimi, kuishi ni Kristo na kufa ni faida.” Wafilipi 1:21 (NIV) Paulo hakuogopa kuishi au kufa. Vyovyote, angeweza kutimiza malengo ya Mungu. Asingepoteza! Siku moja historia itafungwa, lakini umilele utaendelea siku zote. William Carey alisema, “Mbele kunang’aa kama zilivyo ahadi za Mungu. “Unapoona ugumu katika kutimiza malengo yako, usivunjike moyo. Kumbuka thawabu yako, ambayo itadumu milele. Biblia inasema, “Kwa kuwa taabu zetu zilizo nyepesi na za muda mfupi zinatutayarishia utukufu wa milele ambao hauwezi kulinganishwa na haya yote.” 2 Wakorintho 4:17 (NIV)

Fikiri itakavyokuwa siku moja, sisi sote tukisimama mbele za kiti cha enzi cha Mungu tukikabidhi maisha yetu kwa shukrani kubwa na sifa kwa Kristo. Kwa pamoja tutasema, “Unastahili, Ee Bwana! Ndiyo, Mungu wetu! Pokea Utukufu! Heshima! Nguvu! Uliumba vyote; viliumbwa kwa sababu ulitaka hivyo!” Ufunuo 4:11 (Msg)

Tutamtukuza Yeye kwa ajili ya mpango wake na tutaishi kwa kusudi lake milele!

SIKU YA AROBAINI

KUFIKIRI JUU YA LENGO LANGU

Jambo la Kutafakari: Kuishi kwa malengo ndiyo njia pekee ya kuishi hasa.

Kifungu cha Kukumbuka:Kwa kuwa Daudi … alitumikia kusudi la Mungu katika kizazi chake mwenyewe.” Matendo 13:36 (NSBS)

Swali la kujiuliza: Je, ni lini nitachukua muda kuandika majibu yangu kwa maswali matano makuu ya maisha? Je, lini nitaweka lengo langu katika maandishi?

SIKU YA THELAATHINI NA SITA

KUFIKIRIA JUU YA LENGO LANGU

Jambo la Kutafakari: Niliumba kwa ajili ya utume.

Kifungu cha Kukumbuka:Nendeni mkafanye wanafunzi wa mataifa yote, Mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, na kuwafundisha kutii kila kitu nilichowaagiza. Na hakika niko pamoja nanyi daima, mpaka mwisho wa wakati.” Mathayo 28:19-20 (NIV)

Swali la Kujiuliza: Je, ni hofu gani zinanizuia kutimiza utume alioniumba Mungu niufanye? Nini kinanizuia nisiwaambie wengine Habari Njema?