2024年7月4日 星期四

Maisha Yanayoongozwa Na Malengo (Siku Ya Ishirini na Tisa kwa Thelathini na Tano)

 

LENGO LA 4

ULIUMBWA KUMTUMIKIA MUNGU

Sisi ni watumishi wa Mungu tu … kila –mmoja wetu anafanya kazi

ile aliyopewa na Bwana kufanya. Mimi nilipanda mbegu,

Apolo akamwagilia maji, lakini Mungu ndiye aliyekuza mmea.

1 Wakorintho 3:5-6 (TEV)

Siku ya Ishirini na Tisa: Kupokea Jukumu Lako

Ni Mungu mwenyewe aliyetufanya tuwe kama tulivyo na akatupatia

maisha mapya kutoka kwa Yesu Kristo. Na tangu zamani sana

alipanga kwamba tuyatumie maisha haya kwa kuwasaidia wengine.

Waefeso 2:10 (LB)

Nimekutukuza ulimwenguni kwa kukamilisha kila kitu

cha jukumu ulilonipa kufanya.

Yohana 17:4 (Msg)

Uliwekwa duniani kutoa mchango wako. Hukuumbwa ili kutumia asilimali tu – kula, kupumua, na kuchukua nafasi. Mungu alikusanifu ili ufanye tofauti kwa maisha yako. Wakati vitabu vingi vinavyonunuliwa sana vinatoa ushauri juu ya “kupata” zaidi kutokana na maisha yako, hiyo siyo sababu Mungu alikuumba. Uliumbwa uongeze katika maisha ya duniani, siyo tu kuchukua kutoka duniani. Mungu anakutaka urudishe kitu fulani. Hili ndilo lengo la Mungu la nne kwa maisha yako, na linaitwa “huduma” yako. Biblia inatupatia mambo kwa kina zaidi.

Uliumbwa ili umtumikie Mungu. Biblia inasema, “Mungu ametuumba kwa ajili ya maisha ya kazi njema, ambazo ameziandaa ili tuzifanye.” Waefeso 2:10b Hizi “kazi njema” ni huduma zako. Unapowahudumia wengine katika njia yoyote, hakika unamtumikia Mungu (Wakolosai 3:23-24; Mathayo 25:34-45; Waefeso 6:7) na kutimiza moja ya malengo yako. Katika sura mbili zifuatazo utaona jinsi Mungu alivyokuumba kwa uangalifu kwa kusudi hili. Mungu alichomwambika Yeremia ni kweli kata kwako: “Kabla sijakuumba katika tumbo la mama yako, nilikuchkagua. Kabla hujazaliwa, nilikutenga kwa ajili ya kazi maalum.” Yeremia 1:5 (NCV) Uliwekwa katika sayari hii kwa ajili ya jukumu maalum.

Uliokolewa ili umtumikie Mungu. Biblia inasema, “Ni Yeye aliyetuokoa na akatuchagua kwa ajili ya kazi yake takatifu, siyo kwa sababu tunastahili lakini kwa sababu huo ulikuwa mpango wake.” 2 Timotheo 1:9 (LB) Mungu alikukomboa ili upate kufanya “kazi yake takatifu.” Huokolewi kwa huduma, lakini umeokolewa ili uhudumu. Katika ufalme wa Mungu, una sehemu, lengo, wajibu, na kazi ya kutimiza. Hii huyapa maisha yako umuhimu na thamani kubwa.

SIKU YA ISHIRINI NA TISA

KUPOKEA JUKUMU LAKO

Ilimgharimu Yesu Kristo maisha yake kununua wokovu wako. Biblia inatukumbusha, “Mungu alilipa gha rama kubwa sana kwa ajili yenu. Hivyo itumieni miili yenu kumtukuza Mungu.” 1Wakorintho 6:20 (CEV) Hatumtumikii Mungu kwa kuhukumiwa mioyoni, au kwa hofu au wajibu, lakini kwa furaha, na shukrani kubwa kwa alichotufanyia. Tuna deni la maisha yetu kwake. Kwa njia ya wokovu mambo yetu ya kale yamesamehewa, na maisha yetu ya sasa yamepewa maana, na hatima yetu iko salama. Kwa kuzingatia faida hizi kabambe Paulo alihitimisha kwa kusema, “Kwa sababu ya rehema kuu ya Mungu … jitoeni nafsi zenu kama dhabihu hai Mungu, iliyowekwa wakfu kwa utumishi wake.” Warumi 12:1 (TEV)

Mtume Yohana alifundisha kwamba huduma yetu ya upendo kwa wengine huonyesha kwamba kweli tumeokoka. Alisema, “Upendo wetu kwa wenzetu huthibitisha kwamba tumevuka kutoka mautini na kuingia uzimani.” 1 Yohana 3:14 (CEV) Kama sina upendo kwa wengine, sina upendo wa kuwatumika wengine, na ninajali tu mahitaji yangu, ni lazima nijiulize kama kweli Kristo yuko maishani mwangu. Moyo uliookolewa ni ule unaotaka kutumika.

Neno jingine linalohusu kumtumikia Mungu ambalo linaeleweka vibaya na watu wengi ni neno huduma (ministry). Watu wengi wanaposikia “huduma” wanafikiri juu ya wachungaji, mapadri, na watumishi wengine maalum makanisani, lakini Mungu anasema kila mshirika wa jamii yake ni mhudumu. Katika Biblia, maneno mtumishi na mhudumu yana maana moja, kama ilivyo kwa utumishi (service) na huduma (ministry). Kama wewe ni Mkristo, wewe ni mhudumu na unapotumika unahudumu.

Kama sina upendo kwa wengine, sina upendo wa kuwatumikia wengine, ni lazima nijiulize kama kweli Kristo yuko maishani mwangu.

Mama mkwe wake na Petro alipoponywa na Yasu, mara moja “aliinuka na kuanza kumhudumia Yesu.” Mathayo 8:15 (NCV) Kwa kutumia zawadi yake mpya ya afya. Hivyo ndivyo tunavyotakiwa kufanya. Tumeponywa ili tuwasaidie wengine. Tunabarikiwa ili tuwe Baraka. Tunaokolewa ili tutumike siyo kukaa na kusubiri mbingu.

Je, umewahi kujiuliza kwa nini Mungu hatuchukui mbinguni mara tu tunapookoka? Kwa nini anatuacha katika ulimwengu ulioanguka? Anatuacha hapa ili kutimiza malengo yake. Unapookoka Mungu hukusudia kukutumia kwa malengo yake. Mungu ana huduma kwa ajili yako katika kanisa lake na utume kwa ajili yako duniani.

Umeitwa kumtumikia Mungu. Wakati unakua, unaweza kuwa umefikiri kwamba “kuitwa” na Mungu ni kitu ambacho kiliwapata tu wamishenari, wachungaji, watawa, na watenda kazi wengine wa “kudumu” wa kanisa wenye uzoefu. Lakini Biblia inasema kila Mkristo ameitw kutumika. (Waefeso 4:4-14; angalia pia Warumi 1:6-7; 8:28-30; 1 Wakorintho 1:2, 9, 26; 7:17; Wafilipi 3:14; 1 Petro 2:9; 2Petro 1:3) Wito wako kwa wokovu ni pamoja na wito wako kwa huduma. Ni jambo lilelile. Bila kujali kazi yako, umeitwa kwenye huduma ya Kikristo ya kudumu. Mkristo “asiyetumika” yuko kinyume na wito wake.

Biblia inasema, “Alituokoa na kutuita ili tuwe watu wake, si kwa sababu ya matendo tuliyofanya, lakini kwa sababu ya lengo lake.” 2 Timotheo 1:9 (TEV) Petro anaongeza, “Mliitwa ili kuzitangaza sifa njema za Mungu aliyewaita.” 1 Petro 2:9 (GWT) Wakati wowote unapotumia uwezo uliopewa na Mungu kusaidia wengine, unatimiza wito wako.

Biblia inasema, “Sasa ninyi ni watu wake … ili tuweze kufaa katika utumishi wa Mungu.” Warumi 7:4 (TEV) Ni kwa muda gani wewe unafaa katika utumishi wa Mungu? Katika baadhi ya makanisa kule China, wanakaribisha waamini wapya kwa kusema, “Sasa Yesu ana macho mawili mapya ya kutazamia, masikio mapya ya kusikilizia, mikono mipya ya kusaidia, na moyo mpya wa kupenda watu wengine.”

Sababu moja kwa nini unahitaji kuwajibika katika jamii ya kanisa ni kutimiza wito wako wa kuhudumia waamini wengine kwa matendo. Biblia inasema, “Ninyi nyote pamoja ni mwili wa Kristo, na kila mmoja wenu ni kiungo pekee kinachohitajika katika mwili huo.” 1 Wakorintho 12:27 (NLT) Huduma yako inahitajika sana katika mwili wa Kristo – uliza kanisa lolote la mahali. Kila mmoja wetu anao wajibu wa kufanya, na kila wajibu ni wa muhimu. Hakuna huduma mdogo kwa Mungu; zote ni muhimu.

Vivyo hivyo, hakuna huduma zisizofaa kanisani. Nyingine zinaonekana na nyingine hazionekani, lakini zote ni za thamani. Huduma ndogo au zilizofichika, mara nyingi zina matokeo makubwa. Nyumbani mwangu, nuru ya muhimu sana siyo ile taa kubwa ya chumba cha kulia chakula lakini ni ile taa ndogo ya usiku ambayo hunisaidia nisijigonge kidole cha mguu ninapoamka usiku. Hakuna mlinganyo kati ya ukubwa na umuhimu. Kila huduma ni muhimu kwa sababu tunategemeana ili tufanye kazi.

Kunatokea nini pale sehemu moja ya mwili wako inaposhindwa kufanya kazi? Unaugua. Mwili wote unapata maumivu. Fikiri kama maini yako yangeamua kuishi yenyewe: “Nimechoka! Sitaki kuhudumia mwili huu tena! Nahitaji kufanya mambo yanayonifaa mimi! Viungo vingine vijaze nafasi yangu.” Kungetokea nini? Mwili wako ungekufa. Siku hizi makanisa maelfu yanakufa kwa sabau ya Wakristo ambao hawataki kutumika. Wanakaa kando kama watazamaji, na mwili unaugua.

Umeamriwa kutumika. Yesu hakukosea: “Nia yenu iwe kama yangu, kwa kuwa mimi Masihi, sikuja kutumikiwa kakini kutumika na kutoa uhai wangu.” Mathayo 20:28 (LB) Kwa Wakristo, utumishi si jambo la hiari, kitu cha kuwekwa kwenye ratiba kama tuna muda wa ziada. Ni kiini cha maisha ya Kikristo. Yesu alikuja “kutumika” na “kutoa” – na maneno haya mawili lazima yawe kigezo cha maisha yako hapa duniani. Kutumika na kutoa pamoja hufanya lengo la nne la Mungu kwa maisha yako. Mama Teresa alisema, “Kutoa kutakatifu kunahusu kufanya kazi ya Mungu kwa tabasamu.”

Kukua kiroho si mwisho wa yote. Tunakua ili tutoe.

Yesu alifundisha kwamba kukua kiroho si mwisho wa yote. Kukua ni kuhudumu! Tunakua ili tutoe. Haitoshi kuendelea kujifunza tu. Hatuna budi kutendea kazi yale tunayoyajua na kuyaamini. Kuvutia bila kuonyesha kwa matendo husababisha matatizo. Kujifunza bila huduma husababisha kudumaa kiroho. Mlinganyo wa kale kati ya Bahari ya Galilaya na Bahari ya Chumvi bado ni wa kweli hata leo. Galilaya ni ziwa lenye uhai kwa sababu huingiza na kutoa maji. Kinyume chake, hakuna kiumbe hai kinaishi katika bahari ya chumvi kwa sababu haitoi maji, hivyo imkedumaa.

Jambo la mwisho waamini wanalohitaji siku hizi ni kuenda kwenye mafunzo mengine ya Biblia. Wanajua mengi kuliko wanayotendea kazi. Wanachohitaji ni uzoefu wa kuhudumu ambao utawapa mazoezi ya misuli yao ya kiroho.

Kutumika ni kinyume cha hali yetu ya asili. Mara nyingi tuna ile hali ya “tutumikiwe” na siyo kutumika. Tunasema, “Natafuta kanisa linalohudumia mahitaji yangu na kunibariki,” siyo “Natafuta mahali pa kutumika na niwe Baraka.” Tunategemea wengine watutumikie, na siyo kinyume chake. Lakini tunapoendelea kukua katika Kristo, mwelekeo wa maisha yetu lazima uwe kuishi maisha ya utumishi. Mfuasi wa Yesu aliyekomaa huacha kuuliza, “Nani atatimiza mahitaji yangu?” na badala yake huanza kuuliza, “Nani nimsaidie mahitaji yake?” Je, wewe unauliza swali kama hilo?

JIANDAE KWA UMILELE

Mwishoni mwa maisha yako hapa duniani utasimama mbele za Mungu, na atakuthamini namna ulivyowatumikia wengine na maisha yako. Biblia inasema, “Kila mmoja wetu atatoa hesabu ya mambo yake binafsi mbele za Mungu.” Warumi 14:12 (NLT) Fikiri juu ya matokeo yake. Siku moja Mungu atalinganisha nguvu na wakati tulivyotumia kwa maisha yetu binafsi na vile tulivyotumia katika kuwatumikia wengine.

Kwa wakati huo, udhuru wetu wote kwa ajili ya ubinafsi wetu utakuwa hauna maana: “Nilikuwa na shughuli nyingi” au “Nilikuwa na kazi” au “Nilikuwa nafurahia, au nilikuwa najiandaa kustaafu.” Katika udhuru wote Mungu atajibu, “Pole, siyo jibu sahihi. Nilikuumba, nikakuokoa, na kukuita na kukuagiza kuishi maisha ya utumishi. Ni sehemu gani hukuelewa?” Biblia inawaonya wasioamini, “Atawamwagia hasira na ghadhabu yake wale wanaoishi kwa ajili ya nafsi zao tu,” Warumi 2:8 (NLT) lakini kwa Wakristo itamaanisha kupoteza thawabu za milele.

Tuko hai kabisa kama tunawasaidia wengine. Yesu alisema, “kama utakazia kuokoa maisha yako, utayapoteza. Ni wale tu wanaopoteza maisha yao kwa ajili yangu na Habaari Njema ndio wataelewa maana hasa ya kuishi.” Marko 8:35 (LB); angalia pia Mathayo 10:39; 16:25; Luka 9:24; 17:33 Ukweli huu ni wa muhimu sana kiasi cha kurudiwa mara tano katika Injili. Kama hutumiki, wewe unaishi tu, kwa sababu maisha yapo ili kuhudumu. Mungu anapenda ujifunze kupenda na kuwatumikia wengine na bila choyo.

HUDUMA NA UMUHIMU

Utumishi ni njia ya kupata umuhimu wa kweli.

Unatoa maisha yako kwa ajili ya kitu fulani. Hicho ni nini – kazi, michezo, mambo uyapendayo, kujulikana, utajiri? Hakuna kati ya haya litakalokuwa na umuhimu wa kudumu. Utumishi ni njia ya kupata umuhimu. Ni kupitia huduma ndipo tunagundua maana ya maisha yetu. Biblia inasema, “Kila mmoja wetu hupata maana na kazi kama sehemu ya mwile wake.” Warumi 12:5 (Msg) Tunapotumika pamoja katika jamii ya Mungu, maisha yetu hupata umuhimu wa milele. Paulo alisema, “Nataka ninyi mfikiri jinsi gani jambo hili huwafanya wa muhimu zaidi, siyo kidogo … kwa sababu ya kile mnachoshiriki.” 1 Wakorintho 12:14a, 19 (Msg) Mungu anapenda kukutumia kufanya mapadiliko ulimwengu zake. Anapenda kufanya kazi kupitia wewe. Kinachohitajika si urefu wa maisha yako, lakini kile unachotoa. Si muda gani umeishi, lakini uliishi vipi.

Kama huhusiki na huduma yoyote, umekuwa na udhuru gani? Ibrahimu alikuwa mzee, Yakobo hakuwa na usalama, lea hakuwa wa kukvutia, Yusufu alidhalilishwa, Musa alikuwa na kigugumizi, Gidioni alikuwa maskini, Samsoni alikuwa tegemezi, Rahabu alikuwa mzinzi, Daudi alizini na alikuwa na matatizo mengi ya kijamaa, Eliya alitaka kujiua, Yeremia alivunjwa moyo, Yona hakuwa tayari, Naomi alikukwa mjane, Yohana Mbatizaji hakuwa na matamshi mazuri, Petro alikuwa mwepesi wa hasira, Martha alikuwa mwenye hofu sana, mwanamke Msamaria alikuwa na ndoa kadhaa zilizovunjika Zakayo hakupendwa, Thomaso alikuwa mwenye mashaka, Paulo alikuwa na afya mbovu, na Timotheo alikuwa mwoga. Hiyo ni mifano ya sifa zisizofaa lakini Mungu aliwatumia kila mmoja katika huduma yake. Atakutumia wewe pia, ukiacha kutoa udhuru.

SIKU YA ISHIRINI NA TISA

KUFIKIRI JUU YA LENGO LANGU

Jambo la Kutafakari: Huduma siyo hiari.

Kifungu cha Kukumbuka:Maana sisi ni kazi ya mikono ya Mungu, tuliumbwa katika Kristo Yesu tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza tuyatende.” Waefeso 2:10 (NIV)

Swali la Kujiuliza: Je, ni jambo gani linanizuia nisikubali wito wa Mungu wa kumtumikia?

Siku ya Thelathini: Ulifinyangwa Kumtumikia Mungu

Mikono yako ilinifinyanga na kunitengeneza.

Ayubu 10:8 (NIV)

Watu niliowafinyanga kwa ajili yangu watatangaza sifa zangu.

Isaya 43:21 (MJB)

Ulifinyangwa ili umtumikie Mungu.

Mungu aliumba kila kiumbe katika sayari hii kwa utaalamu maalum. Wanyama wengine hukimbia, wengine huogelea, wengine huchimba mashimo na wengine huruka angani. Kila mmoja ana wajibu wa kufanya, Ndivyo livyo kwa wanadamu. Kila mmoja wetu alisanifiwa kipekee, au alifinyangwa ili kufanya vitu fulani.

Kabla wasanifu majengo hawajatoa michoro ya jengo jipya kwanza huuliza, “Lengo lake nini? Litatumiwaje?” Matumizi yaliyokusudiwa mara nyingi huwa kigezo cha sura ya jengo. Kabla Mungu hajakuumba aliamua wajibu utakaotimiza hapa duniani. Alipanga kabisa alivyotaka wewe umtumikie, na kisha akakufinyanga kwa ajili ya kazi hizo. Uko jinsi ulivyo kwa sababu ulifinyangwa kwa ajili ya huduma maalum.

Biblia inasema, “Sisi ni kazi ya mikono ya Mungu, tuliumbwa katika Kristo Yesu tutende matendo mema.” Waefeso 2:10 (NIV) Neno letu la Kiingereza ushairi (poem) linataokana na neno la Kiyunani linalotafsiriwa “kazi ya mikono.” Wewe ni kazi ya mikono ya ufundi wa Mungu. Wewe siyo matokeo ya vitu vilivyokusanywa pamoja bila kufikiri. Wewe umetokana na usanifu wa hali ya juu, wa asili.

Mungu hapotezi chochote.

Mungu kwa makusudi alikufinyanga ili umtumikie katika njia inayofanya huduma yako kuwa ya kipekee. Kwa uangalifu alichanganya DNA (viasili vya uhai) zilizokutengeneza. Daudi alimsifu Mungu kwa ajili ya kujali kwa kina: “Uliumba viungo vyote, sehemu za ndani ya mwili wangu na ukanishikamanisha pamoja katika tumbo la mama yangu. Asante kwa kuniumba kiajabu! Kazi ya mikono yako ni ya ajabu.” Zaburi 139:13-14 (NLT) Kama Ethel Waters alivyosema, “Mungu haumbi takataka.”

Mungu hakukufinyanga kabla ya kuzaliwa tu, alipanga kila siku ya maisha yako kusaidia mchakato wake wa kukufinyanga. Daudi anaendelea, “Kila siku ya maisha yangu iliandikwa kitabuni mwako. Kila wakat uliwekwa kabla hata siku moja haijawepo.” Zaburi 139:16 (NLT) Hii inamaanisha kwamba hakuna kdinachotokea maishani mwako bila kuwa na umuhimu. Mungu hutumia yote kukutengeneza kwa ajili ya huduma yako kwa wengine na pia kwa ajili ya huduma yako kwake.

Mungu hapotezi chochote. Asingeweza kukupa uwezo, utashi, vipawa karama, nafsi, uzoefu wa kimaisha, isipokuwa kwa makusudi ya utukufu wake. Kwa kuamsha na kuelewa vipengele hivi unaweza kugundua mapenzi ya Mungu kwa maisha yako.

Biblia inasema wewe ni “wa ajabu.” Wewe ni mchanganyiko wa vipengele vingi tofauti. Ili kukusaidia ukumbuke vipengele vitano nimetengeneza kielelezo rahisi – SHAPE. Katika sura hii na ile ifuatayo tutavitazama hivi vipengele vitano, na baada ya hapo, nitaeleza jinsi ya kugundua na kutumia umbo lako.

JINSI MUNGU ANAVYOKUUMBA KWA AJILI YA HUDUMA YAKO

Mungu anpotupatia jukumu, daima hutupatia zana zinazohitajika katika utekelezaji. Mchanganyiko huu unatiwa SHAPE yako:

Spiritual gifts   (Karama za kiroho)

Heart         (Moyo)

Abilities       (Akili)

Personality     (Nafsi)

Ezperience     (Uzoefu)

SHAPE: KUDHIHIRISHA KARAMA ZAKO ZA KIROHO

Mungu humpa kila mwamini karama za kiroho. (Wstumi 12:4-8; 1 Wakorintho 12; Waefeso 4:8-15; 1 Wakorintho 7:7) Hizi ni uwezo maalum kutoka kwa Mungu kwa ajili ya kumtumikia na hupewa kwa waamini tu. Biblia inasema, “Yeyote asiyekuwa na Roho hawezi kupokea vipawa vinavyotoka kwa Roho wa Mungu.” 1 Wakorinthoo 2:14 (TEV)

SIKU YA THELATHINI:

ULIFINYAN GWA UMTUMIKIE MUNGU

Huwezi kufanya chochote ili upate karama za rohoni, au uzistahili – ndiyo maana zinaitwa karama (zawadi)! Ni udhihirisho wa neema ya Mungu kwako. “Kristo kwa ukarimu ametugawia vipawa vyake.” Waefeso 4:7 (CEV) Wala hauchagui ni kipawa gani unataka, Mungu anaamua. Pauo alieleza, “Ni Roho peke yake anayegawa vipawa hivi. Yeye peke yake kuamua mani apate kipawa gani.”1 Wakorintho 12:11 (NLT)

Kwa sababu Mungu anapenda aina tofauti na anatutaka tuwe maalum, hakuna kipawa kimoja kinachopewa kwa kila mtu. (1 Wakorintho 12:29-30) Pia hakuna mtu mmoja anayepokea vipawa vyote. Kama ungekuwa navyo vyote, usingemhitaji mtu mwingine yeyote, na hili lingekwamisha moja ya malengo ya Mungu – kutufundisha kupendana na kutegemeana.

Vipawa vyako vya kiroho havikutolewa kwa ajili ya faida yako binafsi lakini kwa kuwafaidia wengine, kama vile watu wengine walipewa vipawa kwa ajili ya faida yako. Biblia inasema, “Kila mtu amepewa karama ya kiroho kama njia ya kulisaidia kanisa.” 1 Wakorintho 12:7 (NLT) Munguu alipanga hivyo ili tuhitajiane. Tunapotumia vipawa vyetu pamoja, sote tunafaidika. Kama wengine hawatumii karama zao, unadanganyika, na usipotumia karama zako, wao hudanganyika. Ndiyo maana tumeagizwa kugundua na kukuza vipawa vyetu vya rohoni. Je, umeshachukua muda kugundua vipawa vyako vya kiroho? Kipawa ambacho hakijafunuliwa hakina faida.

Tunaposahau kweli hizi za msingi kuhusu vipawa mara nyingi huleta matatizo kanisani. Matatizo mawili ya mara kwa mara ni “wivu wa karama” na “kutukuza kipawa.” Tatizo la kwanza hutokea tunapojilinganisha kipawa chetu na kile cha wengine, tunaacha kuridhika na kile Mungu alichotupa, na tunakuwa na uchungu au wivu kwa jinsi Mungu alichotupa, na tunakuwa na uchungu au wivu kwa jinsi Mungu anavyowatumia wengine. Tatizo la pili hutokea tunapotegemea kila mtu awe na kipawa kama chetu, afanye tulichoitwa kufanya, na ajihisi kama tunavyojihisi huu ya jambo hilo. Biblia inasema, “Kuna tofauti ya huduma katika kanisa, lakini ni Bwana mmoja tunayemtumikia.”1 Wakorintho 12:5 (NLT)

Wakati mwingine karama za rohoni zinakazwa kupita kiasi na kuacha vipengele vingine anavyotumia Mungu kukufinyanga kwa ajili ya huduma. Vipawa vyko hudhihirisha ufunguo mmoja wa kugundua mapenzi ya Mungu kwa huduma yako. Mungu anakufinyanga kwa njia nyingine nne.

SHAPE: KUSIKIKIZA MOYO WAKO

Biblia hutumia neno moyo kuelezea furushi la matakwa, matumaini, upendeleo, ndoto, na mapenzi uliyo nayo. Moyo yako huwakilisha asili ya msukumo wa mambo yako yote – unayopenda kufanya zaidi na unayoyajai zaidi. Hata siku hizi bado tunalitumia neno hili kwa maana ile ile tunaposema, “Nakupenda kwa moyo wangu wote.”

Biblia inasema, “Kama uso unavyoonekana sura yake katika maji, ndivyo moyo unavyomwonyesha mtu.” Mithali 27:19 (NLT) Moyo wako hukufunua wewe halisi ulivyo kikwali, sivyo matu wengine wanavyofikiri juu yako au jinsi mazingira yanavyokulazimisha uwe. Moyo wako huamua kwa nini useme mambo usemayo, kwa nini unahisi unavyohisi, na kwa nini unatenda unavyofanya.” (Mathayo 12:34; Mithali 4:23)

Kimaumbile kila mmoja wetu ana mapigo ya pekee ya moyo. Kama vile kila mmoja wetu alivyo na alama za pekee za kidole, macho, sauti, mioyo yetu pia hupiga kitofauti kidogo. Inashangaza kwamba katika mabilioni ya watu waliowahi kuishi, hakuna aliyewahi kuwa na mapigo sawa kabisa na ya kwako.

Vivyo hivyo, Mungu ametupatia “mapigo ya moyo” ya hisia ya kipekee ambayo hujitokeza tunapofikiri juu ya masomo, shughuli, na mazingira yanayotuvutia. Kwa njia ya asili tunajali mambo fulani na mengine hapana. Hivi ni vigezo kukuonyesha wapi unatakiwa utumike.

Neno jingine lenye maana ya moyo ni tamaa. Kuna mambo ambayo unakuwa na shauku kubwa nayo na mengine ambayo usingejali kabisa. Uzoefu mwingine hukuteka n kuchukua msimamo wako wakati mambo mengine hukufanya usiyatazame au hukuudhi kiasi cha kulia machozi. Haya hufunua hali ya moyo wako.

Ulipokuwa unakua, inawezekana uligundua kwamba ulipendelea masomo fulani ambayo hakuna mtu katika jamaa yenu aliyeyajali. Je, upendeleo huo ulitoka wapi? Ulitoka kwa Mungu. Mungu alikuwa na lengo kukupatia upendeleo huu wa kuzaliwa. Hisia zako ni ufunguo wa pili katika kuelewa kufinyangwa kwako kwa ajili ya huduma. Usidharau mambo unayopendelea. Angalia yanavyoweza kutumiwa kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Kuna sababu kwamba unapenda kufanya mambo haya.

Mara nyingi Biblia, inasema, “Kumtumikia Mungu kwa moyo wako wote.” (Kumbukumbu 11:13; 1 Samweli 12:20; Warumi 1:9; Waefeso 6:6) Mungu anapenda umtumikie kwa shauku, si wajibu. Mara chache watu hufanya vizuri katika kazi ambazo hawazifurahii au kuwa na shauku nazo. Mungu anakutaka kutumia matakwa yako ya asili kumtumikia. Yeye na wenzako. Sikiliza msukumo wa ndani kunaweza kukuongoza kwenye huduma Mungu anayokukusudia.

Unapofanya kitu unachopenda kufanya hakuna mtu anayehitajika kukuchochea.

Je, unafahamuje lini unamtumikia Mungu kutoka moyoni mwako? Alama ya kwanza ni shauku. Unapofanya kitu upendacho kufanya, hakuna mtu anayehitajika kukuchochea au kukupa changamoto au kukusimamia. Unafanya kwa furaha. Huhitaji pongezi wala malipo, kwa sababu unapenda kutumika kwa njia hii. Kinyume cha hapo pia ni kweli: Unapokuwa huna moyo na kile unachofanya, unavunjika moyo kwa urahisi.

Alama ya pili ya kumtumikia Mungu kutoka moyoni mwako ni ufanisi. Kila unapofanya kile Mungu alichokupangia upende kufanya, unakuwa na uwezo mkubwa nacho. Shauku huleta ukamilifu. Kama hujali kazi fulani, siyo rahisi kuifanya kwa ubora. Badala yake, wale wanaofanikiwa sana katika nyanja zote ni wale unaofanya kwa sababu ya shauku, siyo wajibu au faida.

Sote tumeshasikia watu wakisema, “Nilichukua kazi ninayoichukia ili nipate fedha nyingi, hivyo siku moja naweza kuiacha na kufanya kazi niipendayo.” Hilo ni kosa kubwa. Usipoteze maisha yako katika kazi isiyoshabihiana na moyo wako. Kumbuka, mambo makubwa maishani si vitu. Maana ni muhimu zaidi kuliko fedha. Mtu mmoja tajiri sana ulimwenguni aliwahi kusema, “Kuwa na mali chahe pamoja na kumcha Mungu ni bora kuliko maisha ya utajiri pamoja na taabu.” Mithali 15:16 (Msg)

Usiangalie u kupata “maisha mazuri, “kwa sababu maisha mazuri hayatoshi. Hakika hayatoshelezi. Unaweza kuwa na mali nyingi katika maisha na bado ukawa huna kitu cha kukiishia. Badala yake lenga kupata “maisha bora” – Kumtumikia Mungu katika njia ambayo inaonyesha moyo wako. Tafuta kile upendacho kufanya – ile Mungu alichokupa kufanya – na kisha kifanye kwa utukufu wake.

SIKU YA THELATHINI

KUFIKIRI JUU YA LENGO LANGU

Jambo la Kutafakari: Nilifinyangwa ili kumtumikia Mungu.

Kifungu cha Kukumbuka: Mungu hufanya kazi kupitia watu mbalimbali, lakini ni Mungu yule yule anayekamilisha malengo yake kwa kupitia hao wote. 1 Wakorintho 12:6 (Ph)

Swali la Kujiuliza: Je, ni katika njia gani naweza kujiona nikiwatumikia wengine kwa shauku na kupenda kufanya hivyo?

 Siku ya Thelathini na Moja: Kufahamu Umbo (SHAPE) Yako

Ulinumba kwanza ndani, kisha nje; Uliniumba tumboni mwa mama yangu.

Zaburi 139:13 (Msg)

Unaweza kuwa wewe tu.

Mungu alitutengeneza kila mmoja wetu ili kwamba kusiwe na mtu mwingine kama wewe duniani. Hakuna yeyote mwenye mchanganyiko wa viasili sawa kabisa na wa kwako vinavyokufanya uwe wa pekee. Maana yako ni kwama hakuna mwingine duniani anayeweza kutenda majukumu Mungu aliyokukusudia. Kama huwezi kutoa mchango wako wa pekee katika mwili wa Kristo, hautafanywa kabisa. Biblia inasema, “Kuna aina tofauti za karama za rohoni … njia tofauti za kuhudumu … na uwezo tofauti wa kutoa huduma.” 1 Wakorintho 12:4-6 (TEV) Katika sura iliyopita tuliona zile mbili za kwanza: karama zako za rohoni na moyo wako. Sasa tutaona sehemu iliyobaki ya umbo (SHAPE) yako kwa kumtumikia Mungu.

SHAPE: KUTUMIA UWEZO WAKO

Uwezo wako ni vipawa vya asili ulivyozaliwa navyo. Baadhi ya watu wana uwezo wa aili na maneno: walitoka tumboni wanaongea! Wengine wana uwezo wa asili wa michezo, wanafanya vizuri sana katika mazoezi ya viungo. Wengine ni wazuri katika hisabati, muziki, au ufundi.

Mungu alipotaka kutengeneza Hema ya Kukutania na vifaa vyote vya ibada, alitoa wasanii na wachongaji waliokuwa wamepata “ujuzi, uwezo, na maarifa katika aina zote za ufundi katika kufanya vifaa vya ufundi … na kufanya kazi za kila aina za ufundi wa mikono.” Kutoka 31:3-5 (NIV) Hata leo Mungu bado anatoa uwezo huu na zaidi ili watu wamtumikie.

Uwezo wetu wote hutoka kwa Mungu. Hata uwezo unaotumika kutenda dhambi unatoka kwaa Mungu; unatumiwa tu vibaya. Biblia inasema, “Mungu ametupatia kila mmoja wetu uwezo wa kutenda vyema.” Warumi 12:6a (NLT) Kwa kuwa uwezo wa asili unatoka kwa Mungu, ni wa muhimu sawa na karama zako za kiroho. Tofauti pekee ni kwamba uwezo wa asili ni wa kuzaliwa.

Udhuru mmojawapo wa ule unatolewa na wengi kwa kutotumika ni “sina uwezo wowote wa kutoa.” Hii inachekesha. Una makumi, labda mamia ya vipawa ambavyo havijulikani, havijatumika, ambavyo vimelala ndani yako. Utafiti mwingi umeonyesha kwamba mtu wa kawaida ana ujuzi wa vipawa tofauti vipatavyo 500 hadi 700 – kuliko unavyofahamu.

Kwa mfano, ubongo wako unaweza kutunza habari trilioni 100. Akili yako inaweza kumudu maamuzi 1,500 kwa sekunde, kama ilivyo wakati mfumo wako wa kuyeyusha chakula unafanya kazi. Pua yako inaweza kunusa kiasi cha 10,000 harufu tofauti. Mguso wako unaweza kutambua 1/25,000 ya unene wa inchi moja, na ulimi wako unaweza kuonja sehemu moja ya kwinini katika sehemu milioni mbili za maji. Wewe ni mkusanyiko wa vipawa mbali mbali vya maana. Ni kiumbe cha ajiabu cha Mungu. Sehemu ya wajibu wa kanisa ni kutambua na kuruhusu uwezo wako ili kumtumikia Mungu.

Kila uwezo unaweza kutumia kwa utukufu wa Mungu. Paulo alisema, “Kila mlifanyalo, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.” 1 Wakorintho 10:31 (NIV) Biblia imejaa mifano ya uwezo tofauti ambao Mungu aliutumia kwa utukufu wake. Hapa kuna mfano wa vipawa vilivyotajwa katika maandiko: Uwezo wa sanaa, uwezo wa ujenzi, uongozi, uokaji, kutengeneza meli, utengenezaji wa vyakula vitamu, mdahalo, ubunifu, kutia dawa maiti, kutarizi, kuchora kulima, uvuvi, bustani, kuongoza, kutawala, ufundi Uashi, muziki, kutengeneza silaha, ufumaji, kutia rangi, kupanda mbegu, falsafa, uwezo wa mitambo, uvumbuzi, useremala, ubaharia, uuzaji, uaskari, ushonaji, kufundisha, kuandika fasihi na mashairi. Biblia inasema, “kuna uwezo tofauti wa kutoa huduma, lakini Mungu yule mmoja hutoa uwezo kwa wote kwa ajili ya huduma yao maalum.” 1 Wakorintho 12:6 (NIV) Mungu ana nafasi katika kanisa lake ambapo kipawa chako chaweza kung’ara na unaweza kufanya tofauti. Ni juu yako kutafuta nafasi hiyo.

Ninachoweza kukifanya Mungu anapenda nifanye.

Mungu huwapa uwezo watu wengine uwezo wa kupata pesa nyingi. Musa aliwaambia Waisraeli, “Mkumbuke Bwana Mungu wako, Kwa kuwa ndiye akupaye uwezo wa kupata mali.” Kumbukumbu 8:18 (NIV) Watu wenye uwezo huu ni wazuri katika kufanya biashara, kufanya mikataba au kuuza, na kupata faida. Kama una uwezo huu wa biashara, utumie kwa utukufu wa Mungu. Namna gani? Kwanza, tambua uwezo wako ulitoka kwa Mungu na umpe sifa. Pili tumia biashara yako kusaidia hitaji la wengine na kushiriki imani yako na wasioamini. Tatu, rudisha walau zaka (asilimia 10) ya faida kwa Mungu kama tendo la ibada. Kumbukubu 14:23; (LB); Malaki 3:8-11. Mwisho, fanya lengo la kuwa Mjenzi Ufalme kulio kuwa Mjenga utajiri. Nitaeleza hili katika sura ya 34.

Ninachoweza kufanya, Mungu ananitaka nifanye. Wewe ni mtu pekee duniani unayeweza kutumia uwezo wako. Hakuna mwingine awezaye kufanya jukumu lako, kwa sababu hawana umbo la pekee ambalo Mungu amekupatia wewe. Biblia inasema kwamba Mungu hukupatia “Vyote unavyohitaji ili kufanya mapenzi yake.” Waebrania 13:21 (LB) Ili kugundua mapenzi ya Mungu kwa maisha yako, huna budi kuchunguza kwa makini una uwezo mkubwa katika kitu gani.

Kama Mungu hakukupa uwezo wa kuimba hataweza kukutegemea uwe mwimbaji mashuhuri. Mungu kamwe hatakutaka utoe maisha yako kwa kazi ambayo huna kipawa nayo.

Upande mwingine, uwezo uli nao ni kigezo thabiti cha kile Mungu anachopenda ufanye na maisha yako. Ni vigezo vya kutambua mapenzi ya Mungu kwako. Kama wewe una uwezo wa mitindo, au kutayarisha watu, au kuchora, au kupanga mipango, ni vyema kudhani kwamba mpango wa Mungu kwa maisha yako unahusisha kipawa hicho kwa namna fulani. Mungu hapotezi vipawa; anaoanisha miito yetu na vipawa vyetu.

Uwezo wako haukutolewa ili kukuwezesha kuishi tu; Mungu alikupatia kwa ajili ya huduma yako. Petro alisema, “Mungu amempa kila mmoja wenuu uwezo wa pekee; hakikisheni mnautumia kuksaidiana, mkiwashirikisha wengine aina mbalimbali za baraka za Mungu.” 1 petro 4:10 (LB)

Katika dakika hii ya kuandika, watu wapatao 7,000 wanatumia vipawa vyao kwa huduma katika Kanisa la Saddleback, wakitoa huduma ya kila namna unayoweza kuifikiri: kukarabati magari yaliyotolewa ili kuwapa wahitaji, kutafuta bei nzuri kwa manunuzi ya kanisa; kusawazisha ardhi, kuweka sawa mafaili, kusanifu sanaa, vipindi, majengo; kusaidia katika afya; kuandaa chakula; kutunga nyimbo; kufundisha muziki; kuandika mapendekezo ya misaada, kufundisha timu, kutafiti ujumbe au kuzitafsiri na mamia ya ujuzi mbalimbali. Washirika wapya wanaelezwa, “kama una uwezo katika kitu chochote, unapaswa kukifanya kwa kanisa lako.

SHAPE: KUTUMIA NAFSI YAKO

Hatuelewi jinsi kila – mmoja wetu alivyo wa pekee hasa. Viasili vya DNA vinaweza kuungana kwa njia zisizohesabika. Kiasi hicho ni uwezo wa sehemu 10 kwa 2,400,000,000. Kiwango hicho ni uthibitisho kwamba haiwezekani kupata mtu mwingine aliye kama wewe kila hali. Kama kila sifuri ungeiondoa kwa kuweka upana wa inchi moja, ungehitaji kipande cha karatasi cha urefu wa maili 37,000!

Ili kuweka jambo hili katika mwelekeo, wanasayansi wamebuni kwamba viasili vyote (particles) katika ulimwengu labda viko chini ya 10 na sifuri 76 nyuma yake, chini ya uwezekano wa DNA yako. Upekee wako ni ukweli wa kisayansi wa maisha. Mungu alipokuumba, alivunja kichongeo. Kwa hiyo hapakuwepo kamwe, na hapatakuwa na mtu yeyote anayefanana na wewe kila kitu.

Ni wazi kwamba Mungu anapenda aina tofauti – angalia tu kukuzunguka! Alituumba kila mmoja wetu kwa mchanganyiko pekee wa viasili vinavyounda nafsi. Mungu aliumba watu wakimya na wasemaji. Aliumba wanaopenda hali ya aina moja na wale wanaopenda hali tofauti tofauti. Aliumba wengine kuwa watu wa kufikiri na wengine wa hisia. Watu wengine hufanya kazi vizuri zaidi wanapopewa majukumu peke yao wakati wengine hufanya vizuri katika kikundi. Biblia inasema, “Mungu hufanya kazi kupitia watu tofauti kwa njia tofauti, lakini ni Mungu yule mmoja anayetimiza lengo lake kupitia wote hao.” 1 Wakorintho 12:6 (Ph)

Biblia hutupa uthibitisho mwingi kwamba Mungu hutumia watu wa aina zote. Petro alikuwa mcheshi (sanguine). Paulo alikuwa mtu makali (choleric). Yeremia alikuwa mwenye huzuni (melancholy). Unapotazama tofauti za nafsi za watu katika wale wanafunzi kumi na wawili ni rahisi kuona kwa nini wakati mwingine walikuwa na migongano baina yao.

Hakuna hulka (temperament) inayofaa au isiyofaa kwa huduma. Tunahitaji aina zote za nafsi ili kuliweka sawa kanisa na kulipatia ladha. Ulimwengu ungekuwa wa kuchosha sana kama sisi sote tungekuwa vanila tupu. Kwa bahati, watu huja na zaidi ya ladha thelathini na moja.

Hulka yako itakuwa na mvuto wa jinsi na wapi utatumia tabia zako za rohoni na vipawa. Kwa mfano, watu wawili wanaweza kuwa na kipawa cha aina moja cha uinjilisti, lakini kama mmoja ni mkimya na mwingine ni msemaji, kipawa hicho kitadhihirishwa kwa njia tofauti.

Unahisi vizuri unapofanya kile Mungu alikuumba ukifanye.

Mafundi seremala wanajua kwamba ni rahisi kufanya kazi kwa kufuata mwelekeo wa chembechembe kuliko kwenda kinyume nazo. Vivyo hivyo, unapolazimisha kuhudumu kwa njia ambayo ni kinyume cha tabia ya nafsi yako, husababisha ugumu na huzuni, huhitaji nguvu za ziada na hutoa matokeo hafifu kuliko yaliyotarajiwa. Ndiyo maana kuigiza huduma ya mtu mwingine hakusaidii. Huna tabia za nafsi zao. Zaidi ya hapo, Mungu alikuumba uwe wewe! Unaweza kujifunza kutoka mifano ya wengine, lakini lazima mchuje yale unayojifunza kupitia umbo lako. Siku hizi kuna vitabu vingi na zana nyingi zinazoweza kukusaidia kuelewa hali ya nafsi yako (personality) ili ukweze kuamua namna ya kuitumia kwa ajili ya Mungu.

Kama kioo chenye rangi, hulka zetu tofauti huonyesha mwana wa Mungu katika rangi mbali mbali na mifumo tofauti. Hii huibariki jamii ya Mungu kwa kina na kwa namna mbali mbali. Pia hutubariki sisi binafsi. Unapohudumu kulingana na nafsi aliyokupa Mungu, unapata utoshelevu, kuridhika, na mafanikio.

SHAPE: KUTUMIA UZOEFU WAKO

Umefinyangwa na uzoefu mbalimbai katika maisha yako, uzoefu huo mwingi ulikuwa zaidi ya uwezo wako. Mungu aliuruhusu kwa lengo lake la kukufinyanga. (Warumi 8:28-29) Katika kutengeneza umbo lako la kumtumikia Mungu, unahitaji kuchunguza walau aina sita za uzoefu kutoka maisha yako yaliyopita.

l  Uzoefu wa kijamaa: ulijifunza nini ulipokuwa unakua katika jamaa yako?

l  Uzoefu wa kielimu: Ni masomo gani uliyapendelea ulipokuwa shuleni?

l  Uzoefu wa kazi: Ni kazi gani umefanya kwa ufanisi zaidi na kuzifurahia?

l  Uzoefu wa kiroho: Ni nyakati gani zimekuwa za maana sana na Mungu?

l  Uzoefu wa kihuduma: Umemtumikiaje Mungu siku za nyuma?

l  Uzoefu wa maumivu: Matatizo gani, maumivu, mwiba, na majaribu yamekupa mafundisho?

Ni kipengele hiki cha mwisho, uzoefu wa maumivu, ambacho Mungu hutumia zaidi katika kukuanda kwa huduma. Mungu kamwe hapotezi maumivu yoyote! Hakika huduma yako kubwa itatoka kwenye maumivu yako makubwa. Nani angeweza kuhudumia vyema, wazazi wa mtoto mwenye udhaifu wa upungufu wa kimaumbile kuliko jamaa nyingine yenye mtoto aliye na tatizo kama hilo? Nani anaweza kumsaidia nyema mlevi kuliko mtu aliyeshinda pepo la ulevi akapata uhuru? Nani anaweza kumsaidia mwanamke aliyeachwa na mumewe kwa sababu ana mke nje kuliko mwanamke aliyepitia tatizo la aina hiyo?

Ili Mungu atumie uzoefu wako wa maumivu lazima uwe tayari kushirikisha wengine.

Mungu kwa makusudi hukuruhusu upite katika hali inayoleta maumivu ili kukuandaa kwa ajili ya kuwahudumia wengine. Biblia inasema, “Yeye hutufariji katika taabu zetu zote ili tuweze nasi kuwafariji wengine. Wengine wanapokuwa katika taabu, tutaweza kuwapa faraja ile ile Mungu aliyotupatia.” 2 Wakorintho 1:4 (NLT)

Kama kweli unatamani kutumiwa na Mungu, lazima uelewe ukweli huu muhimu: Uzoefu ule uliouchukia sana au hata kujilaumu katika maisha – ule uliotaka kuficha na kusahau – ndio uzoefu Mungu anapenda kutumia kuwasaidia wengine. Ndiyo huduma yako!

Ili Mungu atumie uzoefu wa maumivu uwe radhi kushirikisha wengine, Acha kuficha, na lazima ukubali makosa yako, kushindwa, na hofu zako. Kufanya hivi labda kutakuwa ni huduma yako kubwa zaidi. Watu daima hujengwa tunapowashirikisha jinsi neema ya Mungu ilivyotusaidia katika udhaifu kuliko tunapojisifia kufaulu kwetu.

Paulo alifahamu ukweli huu, hivyo alikuwa mwaminifu kuhusu kupambana kwake na udhaifu. Alikiri wazi: “Nafikiri lazima mafahamu, ndugu wapendwa kuhusu wakati mgumu tulioupata huko Asia. Kwa kweli tulilemewa kupita kiasi; tukaogopa kwamba hatutaweza kuishi tena. Tulihisi tulipangiwa kufa na tukaona jinsi tulivyokuwa hatuna nguvu za kujisaidia wenyewe, lakini ilikuwa vyema, kwa kuwa tulimkabidhi Mungu kila kitu, ambaye pekee angeweza kutuokoa, kwa kuwa anaweza kufufua hata wafu. Na kweli alitusaidia na kutuokoa kutoka kwenye kifo kibaya; ndiyo, na tunamtegemea afanye hivyo tena na tena.” 2 Wakorintho 1:8-10 (LB)

Kama Paulo angeficha uzoefu wake wa mashaka na udhaifu, mamilioni ya watu wasingefaidika leo. Ni ule uzoefu unaoshirikisha ndio tu unaweza kusaidia wengine. Aldous Huxley alisema, “Uzoefu si mambo yanayokupata, ni kile unachofanya na yale yanayokupata.” Utafanya nini na yale uliyoyapitia? Usipoteze maumivu yako; tumia hali hiyo kusaidia wengine.

Kama tulivyoona hizi njia tano Mungu anazotumia kukupa umbo la utumishi, natumaini una shukrani za kina kwa mwenyezi Mungu na mawazo sahihi ya jinsi alivyokuandaa kwa lengo la kumtumikia. Ukitumia SHAPE yako ni siri ya mafanikio na utoshelevu katika huduma. (Kwa msaada zaidi unaweza kuagiza kandaza Dalasa la 301, Kugundua Umbo Lako Kwa Ajili ya Huduma, ambazo hujumlisha nyezo ya kugundua Umbo.) Utakuwa na ufanisi ukitumia karama zako za rohoni na vipawa katika eneo la upendeleo wa moyo wako, na katika njia ambayo hudhihirisha vyema nafsi yako na uzoefu wako. Ukifanya kinachokulingana, utafaulu sana.

SIKU YA THELATHINI NA MOJA

KUFIKIRI JUU YA LENGO LANGU

Jambo la Kutafakari: Hakuna mwingine yeyote anayeweza kuwa mimi.

Kifungu cha Kukumbuka:Mungu amempatia kila mmoja wenu uwezo wa pekee, hakikisheni mnautumia kusaidiana, mkiwashirikisha wengine aina mbalimbali za baraka za Mungu.” 1 Petro 4:10 (LB)

Swali la Kujiuliza: Je, ni uwezo gani niliopewa na Mungu au uzoefu gani wa binafsi ninaweza kulipa kanisa langu?

Siku ya Thelathini na Mbile: Kutumia Alichokupa Mungu

Kwa kuwa tuko katika ufumo wa viungo vya mwili wa Kristo vilivyotengenezwa vizuri sana

na kufanya kazi kiajabu, hebu tusonge mbele na tuwe tulivyoumbwa tuwe.

Warumi 12:5 (Msg)

Vile ulivyo ni zawadi ya Mungu kwako; unachofanya na

nafsi yako ni zawadi yako kwa Mungu.

Mithali ya Kidenishi.

Mungu anastahili kilicho bora toka kwako.

Alikufinyanga kwa lengo, na Mungu anakutegemea utumie vyema kile ulichopewa. Hataki uwe na hofu au kuona wivu kwa ajili ya vipawa usivyo navyo. Badala yake anapenda uviangalie kwa makini vipawa alivyokupatia kutumia.

Ukijaribu kumtumikia Mungu kwa njia ambazo kwanza hukuumbwa kutumia kwazo, ni kama kulazimisha kipande cha mraba kuingiza katika tundu la mviringo. Inavunja moyo na matokeo yake ni duni. Pia hupoteza muda wako, kipawa na nguvu zako. Njia bora ya kutumia maisha yako ni kumtumikia Mungu kutokana na maumbile yako. Ili kufanya hivyo lazima ugundue umbo lako, ujifunze kulikubali na kulifurahia na kisha uliendeleze hadi kiwango chake cha juu.

GUNDUA SHAPE YAKO

Biblia inasema, “Msifanye mambo bila kufikiri lakini jaribuni kufahamu na kufanya lolote ambalo Bwana anawataka kufanya.” Waefeso 5:17 (LB) Usiache siku nyingine ipite. Anza kutafuta na kubainisha Mungu anapenda uwe nani na utende nini.

Anza kwa kutathmini karama na uwezo wako. Chukua muda mrefu, kwa uaminifu angalia mambo unayofanya vizuri na yale usiyofanya vizuri. Paulo alishauri, “Jaribuni kutumia akili katika kupima uwezo wenu.” Warumi 12:3b (Ph) Fanya orodha. Waulize watu wengine kwa maoni yao ya kweli. Waambie unatafuta ukweli, na wala sio kutafuta sifa. Karama za rohoni na vipawa vya asili daima huthibitishwa na wengine. Kama unafikiri umepewa kipawa cha kuwa mwalimu su mwimbaji na hakuna mwingine anayekubali, jiulize, kama unataka kujua iwapo una kipawa cha uongozi, wewe angalia tu juu ya bega lako! Kama hakuna anayekufuata basi wewe si kiongozi.

Jiulize maswali kama haya: Je, nimeona tunda gani maishani mwangu ambalo watu wengine walilithibitisha? Ni wapi nimeshafanikiwa? Vipimo vya karama za rohoni na rekodi za vipawa vyaweza kuwa na manufaa fulani, lakini vina mipaka katika matumizi yake. Kwanza, vimewekwa katika viwango, hivyo haviangalii upekee wako kama mtu. Pili hakuna ufafanuzi wa karamaa za rohoni katika Biblia, hivyo ufafanuzi wowote ni maamuzi ya binafsi na mara nyingi hutokana na msimamo wa kidhehebu. Tatizo jingine ni kwamba kadiri unavyokua katika imani, ndivyo unavyoweza kudhihirisha tabia za karama kadha wa kadha. Unaweza kuwa unatumika au unafundisha, au unatoa kwa ukarimu kutokana na kukua kwako badala ya kwamba ni karama yako ya rohoni.

Hivyo njia bora ya kugundua karama na uwezo wako ni kufanyia majaribio maeneo mbalimbali ya huduma. Ningeweza kuchukua vipimo vya karama na uwezo mia moja nilipokuwa kijana na kamwe nisingegundua kwamba nina karama ya kufundisha kwa sababu nilikuwa sijafanya kazi hiyo! Ni pale tu nilipoanza kupokea nafasi za kuhutubu ndipo nilianza kuona matokeo, kupokea uthibitisho toka kwa wengine, na nikaelewa “Mungu amenipa kipawa katika kazi hii!”

Hutaelewa kamwe una uwezo katika jambo gani mpaka umejaribu.

Vitabu vingi hurudisha nyuma mchakato wa ugunduzi. Husema, “Gundua karama yako ya Kiroho na kisha utaelewa huduma gani unatakiwa kuwa nayo.” Hii hufanya kazi kinyume kabisa. Wewe anza kutumika, ukijaribia kwa huduma tofauti, na kisha utagundua vipawa vyako. Mpaka ujihusishe na kutumika, huwezi ukafahamu wewe una uwezo katika jambo gani.

Una makumi ya vipawa vilivyofichika ambavyo hujui unavyo kwa sababu hujavijaribu kamwe. Hivyo nakutia moyo ujaribu kufanya mambo ambayo hujajaribu kabla. Usijali wewe una umri gani, nakusihi kamwe kufanya majaribio. Nimekutana na waatu wengi waliogundua vipawa vyao wakiwa katika umri wa miaka sabini hadi themanini. Namfahamu mwanamke mwenye umri wa miaka tisini na zaidi ambaye hukimbia na kushinda mbio za kilomita 10 na hakugundua kwamba ana uwezo kwenye mbio mpaka alipokuwa na umri wa miaka sabini na nane!

Usijaribu kutafuta kipawa chako kabla ya kujitoa kutumika mahali fulani. Anza tu kutumika. Unagundua vipawa vyako kwa kuingia katika huduma. Jaribu kufundisha, au kuongoza au kupanga mipango au kucheza chombo cha muziki au kufanya kazi na vijana. Hutaelewa kamwe una uwezo katika kitu gani mpaka umejaribu. Kama hupati matokeo mazuri, sema ni “jaribio” siyo kushindwa. Hatimaye utaelewa una uwezo katika jambo gani.

Angalia moyo wako na hulka yako. Paulo alishauri, “Fanyeni uchunguzi makini wa ninyi ni nani na kazi mliyopewa, na kisha mzame katika hilo.” Wagalatia 6:4b (Msg) Tena, inasaidia kupata maelezo kutoka wale wanaokufahamu zaidi. Jiulize maswali: Je, nafurahia kufanya nini zaidi? Ni lini najisikia kuwa hai kabisa? Je, nafanya nini ninapokuwa nimepoteza muda? Je, Napenda mambo ya kila siku au mambo tofauti? Je, napenda kufanya na wengine au peke yangu? Je, mimi ni msemaji au mtu mkimya? Je, mimi ni mwenye kufikiri au mwenye kufuata hisia? Je, nafurahia nini zaidi – ushindani au ushirika?

Chunguza uzoefu wako na upate masomo uliyojifunza. Chunguza maisha yako na ufikiri yalivyokufinyanga. Musa aliwaambia Waisraeli, “Kumbukeni leo mliyojifunza kuhusu Bwana kwa uzoefu wenu naye. “ Kumbukumbu 11:2 (TEV) Uzoefu ukisahaulika hauna faida; hili ni somo zuri la kutunza kumbukumbu za kiroho. Paulo alipata wasiwasi kwamba waamini na Galatia wangepoteza uzoefu wa maumivu waliyoyapata. Alisema, “Je hayo yote yaliyowapata yamepotea? Sidhani!” Wagalatia 3:4 (NCV)

Ni mara chache tunaona lengo zuri la Mungu katika maumivu au kushindwa au maudhi yanapokuwa yanatokea. Yesu alipomwosha Petro miguu alisema, “Nifanyalo sasa wewe huelewi, lakini baadaye utaelewa.” Yohana 13:7 (NIV) Ni baada ya muda kupita ndipo tunaelewa jinsi Mungu alivyoruhusu baya kwa ajili ya mema.

Kupata masomo kutoka katika uzoefu wako huchukua muda. Napendekeza kwamba uchukue juma zima kwa ajili ya mapumziko ya kutathmini maisha yako, ambapo utatulia na kuona vile Mungu amefanya kazi katika maeneo mbalimbali ya maisha yako na kuangalia anavyotaka kutumia masomo hayo kusaidia wengine. Kuna zana zinazoweza kukusaidia kufanya jambo hili. (Wasiliana na www.puposedrivenlife.com)

KUBALI NA UFURAHIE SHAPE YAKO

Kwa kuwa Mungu anajua nini kinafaa kwako, ni vyema upokee kwa shukrani jinsi alivyokutengeneza. Biblia inasema, “Una haki gani, wewe binadamu, kumhoji Mungu? Chungu hakina haki ya kusema kwa mfinyanzi: Kwa nini ulinifinyanga katika umbo hili? Hakika mfinyanzi anaweza kufanya apendavyo kwa udongo.” Warumi 9:20-21 (JB)

SHAPE yako ilikusudiwa na Mungu kwa lengo lake, hivyo usilichukie wala kulikataa. Badala ya kujaribu kujiumba upya na kuwa kama mtu mwingine, unpaswa kushangilia kwa umbo Mungu alilokupa wewe tu. “Kristo amempatia kila mmoja wetu uwezo wa aina fulani – chochote anachotaka tuwe nacho kutoka stoo yake iliyojaa vipawa.” Waefeso 4:7 (LB)

Sehemu ya kukubali umbo lako ni kutambua mipaka yako. Hakuna aliye na uwezo katika vyote, na hakuna aliyeitwa awe kila kitu. Sote tuna majukumu maalam. Paulo alielewa kwamba wito wake haukuwa kufanya kila kitu au kumfurahisha kila mtu lakini kukazania huduma maalum tu Mungu aliyomwandaa kuifanya. (Wagalatia 2:7-8) Alisema, “Lengo letu ni kukaa katika mipaka ya mpango wa Mungu kwa ajili yetu.” 2 Wakorintho 10:13 (NLT)

Neno mipaka humaanisha ukweli kwamba Mungu ametupa kila mmoja wetu uwanja wa huduma. Umbo lako huwa kigezo cha eneo la huduma yako. Tunapojaribu kupanua zaidi huduma yetu kuvuka umbo la Mungu alilotuandalia, tunapata taabu. Kama ilivyo kwa kila mkimbiaji anavyopewa mstari wa kufuata katika kukimbia, ni lazima sisi binafsi, “Kukimbia kwa uvumilivu mbio ambazo Mungu ameweka mbele yetu.” Waebrania 12:1 (LB) Usimwonee wivu mkimbiaji mwingine katika mstari wa karibu nawe; wewe kazania kumaliza mwendo wako.

Mungu anapenda ufurahie

 kutumia umbo alilokupatia.

Mungu anapenda ufurahie kutumia umbo alilokupatia. Biblia inasema, “Hakikisha unafanya wajibu wako, kwani ndipo utakapofurahia utoshelevu wa nafsi yako kwa kufanya kazi yako vyema, na hutahitaji kujilinganisha na mtu mwingine.” Wagalatia 6:4 (NLT) Shetani atajaribu kukuibia furaha yako ya huduma kwa njia kadhaa: Kwa kujaribu ujilinganishe huduma yako na wengine, na kukujaribu ufananishe huduma yako na matarajio ya watu wengine. Yote haya ni mitego mibaya sana ambayo itakuondoa Katika mwelekeo wa utumishi Mungu aliokukuksudia. Unapoteza furaha katika huduma, anza kwa kuangalia moja ya majaribu haya kuwa ndiyo sababu.

Biblia hutuonya tusijilinganishe kamwe na wengine: “Fanya kazi yako vyema, na kisha utakuwa na kitu cha kujivunia. Lakini usijilinganishe na wengine.” Wagalatia 6:4 (CEV) Kuna sababu mbili kwa nini usijilinganishe umbo lako, huduma, au matokeo ya huduma yako na mtu mwingine. Kwanza, wakati wote utampata mtu anayeonekana kufanya vizuri zaidi yako na utavunjika moyo. Au wakati wote utapata mtu anayeonefana kutokufanya vizuri kama wewe na utajaa majivuno. Tabia mojawapo itakuondoa katika huduma na kukuibia faraha yako.

Paulo alisema ni upumbavu kujilinganisha na watu wengine. Alisema, “Sisi hatujaribu kujifananisha au kujilinganisha nafsi zetu na wale wanaojipendekeza. Wanapojipima

SIKU YA THELATHINI NA MBILI:

KUTUMIA ALICHOKUPA MUNGU

wao kwa wao na kujilinganisha wao kwa wao, hawana hekima.” 2 Wakorintho 10:12 (NIV) Tafsiri ya The Message inasema, “Katika kulinganisha huku na kuweka katika makundi na kushindana, wanalikosa lengo kabisa.” 2 Wakorintho 10:12b (Msg)

Utakuta kwamba watu wasioelewa umbo lako la huduma watakulaumu na kukutaka ufuatishe yale wanayofikiri unapaswa kufanya. Wapuuze. Paulo mara nyingi alipambana na wapinzani ambao hawakuelewa huduma yake na hivyo kuipinga. Jibu lake daima lilikuwa lile lile: Epuka kujilinganisha, pinga kukukza mambo, natafuta tu kusifiwa na Mungu. (1 Wakorintho 10:12-18)

Moja ya sababu Paulo alitumiwa sana na Mungu ni kwamba alikataa kugeuzwa na mwelekeo na lawama au kwa kulinganisha huduma yake na wengine au kuvutwa na mijadala isiyo na faida kuhusu huduma yake. Kama John Bunyan alivyosema, “Kama maisha yangu hayana matunda haijalishi nani ananisifu, na kama maisha yangu yana matunda, haijalishi ni nani anayenilaumu.”

ENDELEZA UMBO LAKO

Mfano wa Yesu wa talanta ni kielelezo kwamba Mungu anatutazamia tutumie vizuri anachotupatia. Tunatakiwa kukuza karama na vipawa vyetu, kuipasha moto mioyo yetu, kukua katika tabia na nafsi zetu, na kupanua uzoefu wetu ili tuweze kuongezeka kiufanisi katika huduma. Paulo aliwaambia Wafilipi “endeleeni kukua katika maarifa na ufahamu wenu, “ Wafilipi 1:9 (NLT) na alimkumbusha Timotheo, “Washa upya karama ya Mungu iliyomo ndani yako.” 2 Timotheo 1:6 (NASB)

Kama hufanyi mazoezi ya misuli yako, hudhoofika na kupoteza nguvu. Vivyo hivyo, kama hutumii uwezo na ujuzi Mungu aliokupatia, utaupoteza. Yesu alifundisha mfano wa talanta ili kutoa kielelezo cha ukweli huu. Akimtaja yule mtumishi ambaye alishindwa kutumia talanta yake moja, bwana alisema, “Mnyang’anyeni ile talanta na mpatieni yule aliye na talanta kumi.” Mathayo 25:28 (NIV) Ukishindwa kutumia ulichopewa utapoteza chote. Tumia uwezo ulionao na Mungu atauongeza. Paulo alimwambia Timotheo, “Hakikisha unatumia vipawa ulivyopewa na Mungu … Tumia vipawa hivi katika kazi.” 1 Timotheo 4:14-15 (LB)

Karama yoyote uliyo nayo yaweza kukuzwa na kuongezwa kwa kuifanyia kazi. Kwa mfano, hakuna anayepata kipawa cha kufundisha kikiwa kimekamilika. Lakini kwa kujifunza, kupata maoni ya wengine, na mazoezi, mwalimu “mzuri” anaweza kuwa mwalimu bora, na kadiri muda unavyopita, anakua na kufikia mwalimu aliyefuzu. Usikae na kipawa kilichoendelezwa nusu. Jitanue na ujifunze kadiri uwezavyo. “Uwe na bidii kwa ajili ya Mungu, kazi ambayo hutaionea aibu.” 2 Timotheo 2:15 (Msg) Tumia vizuri kila nafasi ya mafunzo ili kuendeleza SHAPE yako na kunoa ujuzi wako wa utumishi.

Mbinguni tutamtumikia Mungu milele. Sasa hivi, tunaweza kujiandaa kwa ajili ya huduma hivyo ya milele kwa kufanya mazoezi hapa duniani. Kama wana michezo wanapojiandaa kwa ajili ya olimpiki, tunadumu kujiandaa kwa ajili ya siku ile kuu, “Wanafanya hivyo kwa ajili ya taji la dhahabu ambalo hupata kutu na kuchakaa. Ninyi mnaitafuta taji ya dhahabu ambayo ni ya milele.” 1 Wakorintho 9:25 (Msg)

Tunajiandaa kwa ajili ya majukumu na thawabu za milele.

 

SIKU YA THELATHINI NA MBILI

KUFIKIRI JUU YA LENGO LANGU

Jambo la Kutafakati: Mungu anastahili kilicho bora kutoka kwangu.

Kifungu cha Kukumbuka: “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, na anayetumia Neno la kweli kwa halali.” 2 Timotheo 2:15

Swali la Kujiuliza: Je nawezaje kutumia kwa ufanisi zadi kile Mungu alichonipa?

Siku ya Thelathini na Tatu: Jinsi Watumishi Halisi Wanavyotenda

Yeyote anayetaka kuwa mkuu lazima awe mtumishi.

Marko 10:43 (Msg)

Unaweza kusema wao ni nani kwa yale wayatendayo.

Mathayo 7:16 (CEV)

Tunamtumikia Mungu kwa kuwatumikia wengine.

Ulimwengu hufafanua ukuu kwa kuzingatia mamlaka, mali, heshima, na nafasi. Kama unaweza kudai kutumikiwa na wengine, umefika. Katika mila yetu watu wa magharibi ya kujitumikia binafsi na ule umimi kwanza, kutenda kama utumishi si jambo la kawaida.

Yesu, lakini, aliupima ukuu kwa kigezo cha utumishi, na sio nafasi uliyo nayo. Mungu anaona ukuu wako kwa watu wangapi unaowatumikia, na siyo watu wangapi wanaokutumikia. Hii ni tofauti kabisa na kipimo cha kidunia na hivyo ni vigumu kwetu kuelewa na kutenda. Wanafunzi wa Yesu walishindania juu ya nani atachukua nafasi ya juu, na miaka 2,000 baadaye, viongozi wa kikristo bado wanapigania nafasi na kujulikana katika kanisa, madhehebu na huduma shiriki za kanisa.

Maelfu ya vitabu yameandikwa kuhusu uongozi, lakini vichache kuhusu utumishi. Kila mtu anapenda kuongoza, hakuna yeyote anayetaka kuwa mtumishi. Ni bora tuwe majenerali kuliko kuwa askari wa kawaida. Hata wakristo wanapenda kuwa “viongozi – watumishi” siyo watumishi tu. Lakini kuwa kama Yesu ni kuwa mtumishi. Ndivyo alivyojiita mwenyewe.

Wakati kujua umbo lako ni muhimu kwa kumtumikia Mungu, kuwa na moyo wa utumishi ni muhimu zaidi. Kumbuka, Mungu alikufinyanga kwa ajili ya utumishi, siyo kwa ajili ya ubinafsi. Bila moyo wa utumishi utajaribiwa kutumia umbo lako kwa mapato ya binafsi. Pia utajaribiwa kulitumia kama udhuru wa kukwepa kutimiza mahitaji fulani.

Umbo lako hudhihirisha huduma yako lakini moyo wako wa utumishi hudhihirisha kukomaa kwako.

Mara nyingi Mungu hujaribu mioyo yetu kwa kututaka tutumike katika njia ambazo hatujafinyangwa. Kama ukiona mtu ameanguka shimoni, Mungu anakutazamia umsaidie, siyo kusema, “Sina kipawa cha rehema au huduma.” Unaweza kuwa huna karama ya kazi fulani lakini unatakiwa uifanye kazi hiyo kama hakuna alivye kipawa hicho karibu Huduma yako ya kwanza ni ile uliyofinyangiwa, lakini huduma ya pili ni pale unapohitajika.

SHAPE yako hudhihirisha huduma yako, lakini moyo wako wa utumishi hudhihirisha kukumaa kwako. Hakuna kipawa maalum kinachohitajika kubaki baada ya mkutano na kuokota takataka au kupanga viti. Kila mtu anaweza kuwa mtumishi, kinachohitajika ni tabia.

Kuna uwezekano wa kutumika kanisani kwa maisha yote bila kuwahi kuwa mtumishi. Lazima uwe na moyo wa utumishi. Je, unawezaje kujua kama una moyo wa utumishi? Yesu alisema “Unaweza kusema wao ni nani kwa yale wayatendayo.” Mathayo 7:16 (CEV)

Watumishi halisi huwa tayari kutumika. Watumishi hawajazi nafasi zao na mambo mengine yanayoweza kuzuia upatikanaji wao. Wanapenda kuwa tayari wanapoitwa kutumika. Kama askari, mtumwa lazima awe tayari kuwajibika: “Hakuna askari anayepigana vitu ajitiaye katika shughuli za maisha ya kila siku, ili ampendeze yeye aliyempa kazi ya uaskari.” 2 Timotheo 2:4 (NASB) Kama unatumika pale tu inapokufaa, wewe si mtumishi halisi. Watumishi halisi hufanya kinachohitajika, hata kwa wakati usiofaa.

Je, uko tayari kwa Mungu wakati wote? Je, unaweza kuvuruga mipango yako bila wewe kukasirika? Kama mtumishi, hutakiwi kuchagua lini au wapi utatumika. Kuwa mtumishi maana yake ni kuacha kutawala ratiba na kumruhusu Mungu kuingilia kati anapohitaji.

Kama unajikumbusha kila mwanzoni mwa siku kwamba wewe ni mtumishi wa Mungu, kuingilia ratiba yako hakutakuvunja moyo, kwa sababu agenda yako itakuwa chochote Mungu anachotaka kuleta maishani mwako. Watumishi huona vurugu kama hizo kuwa ni nafasi za kimungu za utumishi na wanafurahia kutoa huduma.

Watumishi halisi hujali mahitaji. Watumishi wanatafuta njia za kusaidia wengine wakati wote. Wanapoona hitaji, wanachukua nafasi hiyo kulitimiza, kama tu Biblia inavyotuagiza: “Kila tunapokuwa na nafasi, tutende mema kwa kila mtu, hasa kwa jamii ya wanaoamini.” Wagalatia 6:10 (GWT) Mungu anapomweka mtu mwenye mahitaji mbele yako, anakupa nafasi ya kukua katika utumishi. Tambua kwamba Mungu anasema mahitaji ya jamii ya kanisa lako yapewe kipaumbele, siyo kuyaweka chini katika orodha ya “mambo ya kufanya.”

Tunapoteza nafasi nyingi za kutumika kwa sababu tunakosa hali ya kujali na hiari. Nafasi kubwa za kutumika hazidumu kwa muda mrefu. Zinapita kasi, wakati mwingine hazirudi tena. Unaweze kupata nafasi moja tu ya kumtumikia mtu huyo, hivyo tumia nafasi hiyo, “Usiwaambie jirani zako kusubiri mpaka kesho kama unaweza kuwasaidia sasa.” Mithali 3:28 (TEV)

John Wesley alikuwa mtumishi mzuri wa Mungu Msemo wake ulikuwa “Fanya mema yote unayoweza, kwa njia zote unazoweza, katika sehemu zozote unazoweza, ili mradi unaweza.” Huo ndio ukubwa. Unaweza kuanza kwa kutafuta kazi ndogo ndogo ambazo hakuna mtu anapenda kufanya. Fanya vitu hivi vidogo kama vile vikubwa, kwa sababu Mungu anatazama.

Watumishi halisi hufanya vizuri zaidi na kile walichonacho. Watumishi hawatoi udhuru, au kusubiri mazingira ya kufaa. Watumishi hawasemi, “Siku fulani” au “Kwa wakati mwafaka.” Wao hufanya kile kinachohitajika kufanywa. Biblia inasema, “Kama utasubiri hali kamilifu, kamwe hutafanya chochote.” Mhubiri 11:4 (NLT) Mungu anakutazamia ufanye unachoweza, na kile uliho nacho, popote ulipo. Huduma nusu ni bora kuliko nia kamilifu.

Sababu moja kwa nini watu hawatumiki ni kwamba wanaogopa kwamba wao si wema vya kutosha kutumika. Wameamini uongo kwamba Mungu anahitaji tu wale mabingwa. Makanisa mengi yamechochea imani hii kwa kufanya “ubora” Mungu, kitu ambacho huwafanya watu wenye kipawa cha kawaida kutokuwa tayari kushiriki.

Unaweza kuwa umesikia inasemwa, “Kama haiwezi kufanywa kwa ubora, usifanye.” Yesu hakusema hivyo! Ukweli ni kwamba, karibu kila tunachofanya hufanywa kwa kiwango cha chini – ndivyo tunavyojifunza. Katikka Kanisa la Saddleback, tunayo kanuni ya “inatosha”: Haihitaji iwe kamilifu ili Mungu aitumie na kuibariki. Ni bora tuwe na maelfu ya watu wa kawaida wakitumika kuliko kuwa na kanisa kamilifu linaloongozwa na watu bora wachache.

Watumishi halisi hufanya kazi zote kwa kujitoa sawa sawa. Chochote wanachofanya, watumishi “hufanya kwa moyo wao wote.” (Wakolosai 3:23) Ukubwa wa kazi si kitu cha msingi. Jambo kuu, ni je, inahitaji kufanyika?

Hutaweza kufikia hali katika maisha ambayo utakuwa wa muhimu sana kabisa kiasi cha kutosaidia kazi ndogo ndogo. Mungu hawezi kukutenga kutoka katika majukumu hayo. Ni sehemu muhimu ya mtaala wa tabia yako. Biblia inasema, “Kama unadhani wewe ni wa muhimu sana huwezi kumsaidia mtu mwenye mahitaji, unajidanganya mwenyewe tu. Wewe si kitu kabisa.” Wagalatia 6:3 (NLT) Ni katika huduma hizi ndogo ndogo ndipo tunakua na kufanana na Kristo.

Yesu alichagua kufanya kazi za chini ambazo kila mtu aliziepuka: kuosha miguu, kusaidia watoto, kuandaa chakula cha asubuhi, kutumikia wakoma, hakuwa na kitu cha chini yake, kwa sababu alikuja kutumika. Haikuwa badala ya ukuu wake kwamba alifanya haya, lakini kwa sababu yake, na anatutarajia tufuate mfano wake. (Yohana 13:15)

Kazi ndogo ndogo mara nyingi huonyesha moyo mkubwa. Moyo wako wa kitumishi unaonekana katika matendo madogo ambayo wengine hawafikiri kuyatenda, kama vile Paulo alivyokusanya kuni kwa ajili ya moto wa kuwapa joto wote baada ya kuvunjikiwa na meli. (Matendo 28:3) Alikuwa amechoka kama wengine, lakini alifanya kile mtu alikihitaji. Hakuna kazi iliyo chini yako unapokuwa na moyo ya kiutumishi.

Nafasi kubwa mara nyingi hujificha kwenye kazi ndogo. Mambo madogo maishani huwa msingi wa ukubwa. Usitafute nafasi kubwa za kumtumikia Mungu. Wewe fanya tu hizo kazi ndogo ndogo, na Mungu atakupangia chochote anachokutaka ufanye. Lakini kabla ya kufanya mambo yasiyo ya kawaida, jaribu kufanya katika njia za kawaida. (Luka 16:10-12)

Nafasi kubwa mara nyingi hujificha kwenye kazi ndogo.

Daima kutakuwa na watu zaidi wanaotaka kufanya mambo “makuu” kwa ajili ya Mungu kuliko watu walio radhi kufanya mambo madogo. Mbio za kuwa kiongozi zimejaa watu, lakini kiwanja kiko tupu kwa wale walio tayari kuwa watumishi. Wakati mwingine unawatumikia walio juu wenye madaraka, na wakati mwingine unawatumikia walio chini wenye uhitaji. Kwa njia yote, unakuza moyo wa utumishi unapokuwa tayari kufanya chochote kinachohitajika.

Watumishi halisi ni waminifu kwa huduma yao. Watumishi humaliza kazi yao, hutimiza majukumu yao, hutunza ahadi zao, na humaliza wanachokifanya. Hawaachi kazi nusu, na hawaachi wanapovunjwa moyo. Ni wa kuaminika na kutegemewa.

Uaminifu umekuwa sifa nadra. (Zaburi 12:1; Mithali 20:6; Wafilipi 2:19-22) Watu wengi hawajui maana ya ahadi. Wanaweka ahadi kienyeji tu, wanazivunja kwa sababu ndogo tu bila kujali wala kuhuzunika. Kila wiki, makanisa na mashirika mengine huwa na dharura kwa sababu watu waliojitolea hwakuandaa, hawakuonekana, au hata hawakutoa taarifa kwamba hawangekuja.

Je, unaweza kuwajibishwa na wengine? Je, kuna ahadi unazotakiwa kutunza, nadhiri unazohitaji kutimiza, au ahadi unazotakiwa kuziheshimu? Hiki ni kipimo. Mungu anapima uaminifu wako. Kama utashinda mtihani huo, unakuwa katika kundi zuri: Ibrahimu, Musa, Samweli, Daudi, Danieli, Timotheo, na Paulo wote waliitwa watumishi waaminifu wa Mungu. Bora zaidi, Mungu amekuahidi tuzo mbinguni kwa sababu ya uaminifu. Hebu fikiri utakavyokuwa siku moja Mungu akikuambia, “Vyema, mtumishi wangu mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu katika kiasi hiki kidogo, sasa nitakupa majukumu makubwa zaidi. Hebu tusherehekee pamoja!” Mathayo 25:23 (NLT)

Hakika watumishi waaminifu hawastaafu. Hutumika kwa uaminifu maadam wako hasi. Unaweza kustaafu kazini kwako, lakini hutastaafu kumtumikia Mungu.

Watumishi halisi hawatafuti kujilikana. Watumishi hawajitangazi wala kutaka kujulikana. Badala ya kutenda kwa kujionyesha au kuvaa kuonyesha mafanikio, wao, “huvaa vazi la unyenyekevu, ili kutumikiana.” 1 Petro 5:5 (TEV) Wakishukuriwa kwa huduma yao, huipokea kwa unyenyekevu lakini hawaruhusu sifa kupita kiasi ziwaondoe kwenye utumishi wao.

Paulo aliweka wazi aina ya huduma inayoonekana ya kiroho lakini hakika ni maagizo na kujionyesha, tendo la kutafuta kujulikana. Aliita “huduma ya jicho” Waefeso 6:6 (KJV); Wakolosai 3:22 (KJV) – kutumik ili tuwavvutie watu wajue jinsi tulivyo wa kiroho. Hii ilikuwa dhamabi ya Mafarisayo. Waligeuza kusaidia wengine, utoaji, hata sala kuwa kitu cha maonyesho kwa wengine. Yesu alichukia tabia hii na akaonya, “unapofanya tendo jema, usijaribu kujionyesha. Ukifanya hivyo, hutapata thawabu kutoka kwa Baba yako wa mbinguni.” Mathayo 6:1 (CEV)

Kujitangaza na utumishi havichangamani. Watumishi halisi hawatumiki ili wasifiwe na wengine. Wanaishi ili watazamwe na mmoja. Kama Paulo alivyosema, “Kama ningelikuwa najaribu kufurahisha watu, nisingekuwa mtumishi wa Kristo.” Wagalatia 1:10 (NIV)

Huwezi kuwapata watumishi wa kweli wakitafuta kujulikana, ni dhahiri kabisa, wao huepuka hali hiyo inapowezekana. Wanaridhika na kutumika kimya kimya katika vivuli. Yusufu ni mfano madhubuti. Hakutafuta kujulikana, lakini alitumika kimya kwa Potifa, kifungoni, na kwa mwoka mikate na mnyweshaji wa Farao. Na Mungu alibariki moyo huo. Farao alipomwinua katika nafasi ya juu, Yusufu bado alidumu na moyo wa utumishi, hata kwa ndugu zake waliomsaliti.

Kwa bahati mbaya, viongozi wengi siku hizi huanza kama watumishi lakini huishia kuwa watu maarufu sana. Huchukuliwa na sifa, hawajui kwamba kuwa kwenye nuru kali hupofusha.

Unaweza kuwa unatumika kwenye mazingira ya kutojulikana katika maeneo madogo, ukijihisi kutojulikana wala kupewa shukrani. Sikiliza: Mungu alikuweka ulipo kwa malengo. Amezihesabu vywele zote za kichwa chako, na anafahamu anwani yako. Ni vyema ukae hapo mpaka akuhamishe. Atakujulisha kama anakuhitaji sehemu nyingine. Huduma yako ni ya muhimu katika ufalme wa Mungu. “Kristo … anapoonekana tena katika dunia hii, utaonekana pia – wewe halisi, wewe uliyetukuka, Kwa sasa, ridhika na hali yako ya unyonge.” Wakolosai 3:4 (Msg)

Kuna orodha za watu mashuhuri (Halls of Fame) 750 katika Marekani na vitabu 450 vya “Nani ni Nani” lakini huwezi kupata watumishi halisi katika haya. Kujulikana hakuna maana kwa watumishi kwa sababu wanajua tofauti na umuhimu wa watu. Unavyo viungo kadhaa vyenye sifa mwilini mwako ambavyo ungeishi hata bila kuwa navyo. Ni viungo vilivyofichika vya mwili wako ambavyo ni muhimu sana. Ndivyo ulivyo hata kwa mwili wa Kristo. Huduma ya muhimu sana ni ile isiyoonekana. 1 Wakorintho 15:58 (Msg)

SIKU YA THELATHINI NA TATU:

JINSI WATUMISHI HALISI WANAVYOTENDA

Mbinguni Mungu atatoa thawabu kwa baadhi ya watumishi wasiojulikana – watu ambao hatujawasikia hapa duniani, walifundisha watoto wenye matatizo ya akili, walisafisha wazee wenye tatizo la kibofu cha mkojo, walihudumia wagonjwa wa ukimwi, na wakatumika katika maelfu ya njia nyingine.

Kwa kujua hili usivunjike moyo pale unapojua huduma yako haijulikani au hupati shukrani yoyote. Endelea kumtumikia Mungu! “Jiingizeni katika kazi ya Bwana mkiwe na hakika kwamba hakuna mnachotenda kwa ajili yake ni kupoteza muda na nguvu.” 1 Wakorintho 15:58 (Msg) Hata huduma ndogo inatambuliwa na Mungu na itatunzwa. Kumbuka maneno ya Yesu: “Iwapa kama wawakilishi wangu, mtampatia hata kikombe cha maji ya baridi mtoto mdogo, hakika mtapewa thawabu.” Mathayo 10:42 (LB)

SIKU YA THELATHINI NA TATU

KUFIKIRI JUU YA LENGO LANGU

Jambo la Kutafakari: Nametumikia Mungu kwa kuwatumikia watu wengine.

Kifungu cha Kukumbuka: “Kama mkimpatia kikombe cha maji ya baridi mmoja wa wadogo hawa wa wafuasi wangu, hakika mtapata dhawabu:” Mathayo 10:42 (NLT)

Swali la Kujiuliza: Je, ni sifa gani kati ya zile sita za mtumishi halisi inanipa changamoto kubwa?

Siku ya Thelathini na Nne: Kufikiri Kama Mtumishi

Mtumishi wango Kalebu anafikiri tofauti na ananifuata kikamilifu.

Hesabu 14:24 (NCV)

Jifikirini wenyewe kama vile Kristo Yesu alivyojifikiria mwenyewe.

Wafilipi 2:5 (Msg)

Huduma huanzia akilini.

Kuwa mtumishi kunahitaji badiliko la akili, kubadilika katika nia yako. Mungu huchunguza sababu ya kufanya kitu Fulani, lakinsi siyo kitu tunachofanya. Nia ni ya muhimu sana kulio mafanikio yetu. Mfalme Amazia alipoteza kibali kwa Mungu kwa sababu “Alifanya kilichokuwa sawa machoni pa Bwana, lakini si kwa moyo wa kweli.” 2 Nyakati 25:2 (NRSV) Watumishi wa Mungu humtumikia Mungu wakiwa na mawazo yenye mwelekeo wa aina tano:

Watumishi hufikiri zaidi kuhusu wengine na siyo wao wenyewe. Watumishi huangalia watu wengine na siyo wao binafsi. Huu ni unyenyekevu wa kweli; siyo kujifikiria kuwa thamani yetu ni ndogo, lakini kujifikiria juu ya nafsi zetu kidogo. Wao hujisahau nafsi zao. Paulo alisema “Jisalimisheni nafsi zenu vya kutosha kuweza kutoa msaada kwa wengine.” Wafilipi 2:4 (Msg) Hii ndiyo maana ya “kupoteza maisha yako” – Kujisahau ili kutumikia wengine. Tunapoacha kukazia mahitaji yetu binafsi, tunaanza kuyafahamu mahitaji yaliyopo katika mazingira yetu.

Yesu “alijitoa kwa kuchukua hali ya mtumwa” Wafilipi 2:7 (GWT). Ni lini kwa mara ya mwisho ulijitoa nafsi yako kwa faida ya mtu mwingine? Huwezi kuwa mtumishi kama umejaa nafsi yako mwenyewe. Ni pale tu tunapojisahau nafsi zetu ndipo tunafanya vitu vinavyostahili kukumbukwa.

Watumishi halisi hawajaribu kumtumikia Mungu kwa malengo yao. Wanamruhusu Mungu awatumie kwa malengo yake.

Kwa bahati mbaya sehemu kubwa ya huduma yetu mara nyingi ni kujitumikia nafsi zetu. Tunatumika ili wengine watupende, au watutamani, au kutimiza malengo yetu. Hivyo ni kuvuta watu kwa hila wala siyo huduma. Muda wote tunajifikiri wenyewe na jinsi tulivyo wa thamani na wa ajabu. Watu wengine hujaribu kutumia huduma kama chombo cha kufanyia mapatano na Mungu. “Mungu nitakufanyia hiki, kama utanifanyia kitu fulani.” Watumishi halisi hawajaribu kumtumikia Mungu kwa malengo yao. Wanamruhusu Mungu awatumie kwa malengo yake.

Sifa ya kujisahau nafsi yako, kama uaminifu, ni nadra sana. Katika watu wote Paulo alijua Timotheo alikuwa mfano pekee ambao angetaja. (Wafilipi 2:20-21) Kufikiri kama mtumishi ni vigumu kwa sababu hutoa changamoto kwa tatizo la msingi la maisha yangu: kwa asili mimi ni mwenye ubinafsi. Najifikiri zaidi ndiyo maana unyenyekevu ni pambano la kila siku, somo la kujifunza tena na tena. Nafasi za kuwa mtumishi hunisonga mara kumi nyingi kwa siku, ambapo ninapewa uchaguzi wa kuamua kutimiza mahihaji yangu au kutimiza mahitaji ya wengine.

Tunaweza kupima moyo wetu wa utumishi kwa namna tunapoitikia pale wengine wanavyotutendea kama watumishi. Je, unajibuje watu wanapokutumia tu, wakijifanya wakubwa wako, au wanakutendea kama mtu mdogo sana kwao? Biblia inasema, “Kama mtu atataka kukutumia isivyo haki, basi tumia nafasi hiyo kuonyesha maisha ya mtumishi.” Mathayo 5:41 (Msg)

Watumishi hufikiri kama mawakili na sio wamiliki. Watumishi wanakumbuka kwamba Mungu anamiliki vyote. Katika Biblia, wakili alikuwa mtu aliyeamini na kukabidhiwa kutunza mali. Yusufu alikuwa mtumishi wa aina hiyo kama mfungwa huko Misri. Potifa alimkabidhi Yusufu nyumba yake. Mtunza gereza alimkabidhi Yusufu gereza lake. Hatimaye Farao alimkabidhi taifa zima. Utumishi na uwakili huenda pamoja. 1Wakorintho 4:1 (NJB) Kwa kuwa Mungu anatutegemea kuwa waaminifu katika yote mawili. Biblia inasema, “Kitu kimoja kinachotakiwa kwa watumishi kama hao ni kwamba wawe waaminifu kwa bwana wao.” 1 Wakorintho 4:2 (TEV) Je unatunzaje raslimali Mungu aliyokukabidhi?

Ili uwe mtumishi halisi unatakiwa kutatua tatizo la fedha Katika maisha yako. Yesu alisema “Hakuna mtumishi anayeweza kutumikia mabwana wawili … Huwezi kutumikia Mungu na fedha.” Luka 16:13 (NIV) Hakusema, “Hamtakiwi,” lakini alisema “Hamuwezi.” Haiwezekani. Kuishi kwa ajili ya huduma na kwa ajili ya fedha ni malengo mawili tofauti kabisa. Je, ni lipi utachagua? Kama wewe ni mtumishi wa Mungu huwezi kujipa kazi ya pili. Muda wako wote ni wa Mungu. Anakazia uaminifu mkamilifu, siyo uaminifu nusu.

Fedha zina uwezo mkubwa wa kuchukua nafasi ya Mungu katika maisha yako. Watu wengi wanapotoshwa njia ya utumishi kwa tamaa ya mali kuliko kitu kingine chochote. Wanasema, “Baada ya kufanikiwa mipango yangu ya fedha, nitamtumikia Mungu.” Huo ni uamuzi wa kipumbavu ambao utawapa majuto milele. Yesu akiwa Bwana wako, fedha hukutumikia, lakini fedha zikiwa Bwana wako, unakuwa mtumwa wa fedha. Utajiri kwa hakika si dhambi lakini kushindwa kuutumia kwa utukufu wa Mungu ni dhambi. Watumishi wa Mungu mara nyingi wanajali zaidi huduma kuliko fedha.

Biblia iko wazi: Mungu hutumia fedha kujaribu uaminifu wako kama mtumishi. Ndiyo maana Yesu alizungumzia sana kuhusu fedha kuliko hata alivyozungumzia mbingu au kuzimu alisema, “Kama hamjawa waaminifu katika mali ya dunia, nani atawaamini na kuwakabidhi utajiri wa kweli? Luka 16:11 (NIV) Unavyotumia fedha zako huwa na matokeo makubwa kwa kiasi ambacho Mungu anaweza kubariki maisha yako.

Katika sura ya 31, nilitaja aina mbili za watu: Wajenga Ufalme na Wajenga Utajiri. Wote wana kipawa cha kufanya mradi wao kukua, kwa mikataba na mauzo na kupata faida. Wajenga Utajiri huendelea kujirundikia mali hata wapate mali nyingi kiasi gani, lakini Wajenga Ufalme hubadili kanuni hiyo. Bado hujaribu kutengeneza fedha kwa kadiri ya uwezo wao, lakini wanafanya hayo ili wazitoe. Wanatumia utajiri huo kufanya kazi ya kanisa, na huduma yake kwa ulimwengu.

Katika kanisa la Saddleback, tuna kikundi cha mameneja na wamiliki wa miradi ya biashara ambao wanajitahidi kuzalisha kwa uwezo wao ili waweze kutoa kwa kadiri ya uwezo wao katika kuendeleza ufalme wa Mungu. Nakutia moyo uongee na Mchungaji wako ili kuanzisha kikundi cha kujenga ufalme kanisani mwenu. Kwa msaada angalia nyongeza ya 2.

SIKU YA THELATHINI NA NNE:

KUFIKIRI KAMA MTUMISHI

Watumishi hufikiri juu ya kazi yao, na siyo wanachofanya wengine. Hawajilinganishi, hawalaumu, na hawashindani na watumishi wengine au huduma nyingine. Wanajishughulisha zaidi na kazi waliyopewa na Mungu.

Ushindani kati ya watumishi wa Mungu haufai kwa sababu nyingi: Sote tuko timu moja; lengo letu ni kufanya Mungu aonekane mwema, siyo sisi wenyewe; tumepewa majukumu tofauti; na sisi sote tumefinyagwa kipekee. Paulo alisema, “Hatutajilinganisha sisi kwa sisi kana kwamba wengine wetu ni wema na wengine ni wabaya. Tuna mambo mazuri ya kufanya katika maisha yetu. Kila mmoja wetu ni wa asili.” Wagalatia 5:26 (Msg)

Hakuna nafasi ya wivu kati ya watumishi. Unapokuwa unatumika kwa bidii, huna muda muda wa kulaumu. Muda unaotumika kulaumu ungetumika vyema kwa kuhudumu. Martha alipolalamika kwa Yesu kwamba Mariamu alikuwa hasaidii kazi, alipoteza moyo wake wa utumishi. Watumishi halisi hawalalamiki dhidi ya kutotendewa haki, hawajihurumii, wala hawawachukii wale wasiotumika. Wao humwamini Mungu wakidumu katika kutumika.

Siyo kazi yetu kutathmini watumishi wengine wa Bwana. Biblia inasema, “Wewe ni nani kumuhukumu mtumishi wa mtu mwingine? Bwana ataamua iwapo mtumishi wake amefaulu.” Warumi 14:4 (GWT) Pia si kazi yetu kujitetea dhidi ya lawama, Mwachie Bwana wako ashughulikie. Fuata mfano wa Musa, aliyeonyesha unyenyekevu wa kweli alipokabiriwa na upinzani; kama alivyofanya Nehemia, ambaye aliwajibu wapinzani wake kuwa, “Kazi yangu ni ya muhimu sana hivyo siwezi kuacha sasa … niwatembelee.” Nehemia 6:3 (CEV)

Ukitumika kama Yesu, tegemea kulaumiwa. Ulimwengu, hata kanisa, hawaelewi Mungu anathamini nini. Moja ya matendo mazuri ya upendo aliyotendewa Yesu lililaumiwa na wanafunzi wake. Mariamu alichukua kitu cha thamani alichokuwa nacho, manukato ya thamani, na akammiminia Yesu. Huduma yake kubwa ilikuwa “Kupoteza” kwa maoni ya wanafunzi, lakini Yesu aliita “tendo la maana.” Mathayo 26:10 (Msg) Na hilo ndilo lilitakiwa. Huduma yako kwa Kristo haipotei kamwe hata kama watu wengine watasemaje.

Watumishi huweka msingi wa utambulisho wao kwa Kristo. Kwa sababu wanakumbuka kwamba wanapendwa na kukubaliwa kwa neema. Watumishi hawahitaji kuthibitisha uthamani wao. Kwa moyo hukubali kazi ambazo watu wenye hofu wangesema ni kazi zilizo “chini sana kwao”. Moja ya mifano madhubuti ya kutumika kwa kujiamini ni tendo la Yesu kuosha miguu ya wafuasi wake. Kuosha miguu ilikuwa sawa na kijana anayesafisha viatu mitaani, kazi isiyo na heshima. Lakini Yesu alijua alikuwa nani, kwa hiyo kazi haikutishia utu wake. Biblia inasema, “Yesu alijua kwamba Baba ameweka vitu vyote chini ya uwezo wake, na kwamba alikuwa ametoka kwa Mungu … hivyo aliinuka kutoka kwenye chakula, akachukua vazi lake la juu, na akajifunga kitambaa kiunoni.” Yohana 13:3-4 (NIV)

Kama unataka kuwa mtumishi lazima upate kitambulisho cha utu wako katika Kristo. Ni watu wenye amani ndio wanaweza kutumika. Watu wenye mashaka daima wana hofu ya jinsi wanavyoonekana kwa wengine. Wanaogopa kuonekana udhaifu wao na hivyo kujificha kwenye tabaka la majivuno na maigizo. Kadiri ulivyo na mashaka, ndivyo utakavyotaka na watu wakutumikie, na ndivyo utahitaji zaidi kukubalika kwao.

Henri Nouwen alisema, “Ili kuwaa na huduma kwa watu wengi lazima tuwafie; yaani, tuache kupima umuhimu na thamani yetu kwa kipimo cha wengine … Ndipo tunakuwa huru wa wenye huruma.” Unapoweka msingi wa uthamani na utambulisho wako kwa uhusiano wako na Kristo, unawekwa huru mbali na matazamio ya wengine, na hiyo hukupa uhuru wa kuwatumikia vyema zaidi.

Watumishi hawahitaji kufunika kuta zao kwa vyeti vyao kuthibitisha kazi zao. Hawasisitizi kuitwa kwa vyeo vyao, na hawavai mavazi ya ukubwa. Watumishi hawaoni umuhimu wa alama za wadhifa, na hawapimi uthamani wao kulingana na walichofanya. Paulo alisema, “Unaweza kujisifia mwenyewe, lakini kibali pekee ni kutoka kwa Bwana.” 2 Wakorintho 10:18 (CEV)

Kama kuna mtu yeyote aliyekuwa na nafasi ya maisha ya kujitukuza ni Yakobo, ndugu yake na Yesu. Alikuwa na sifa ya kukaa pamoja na yesu kama kaka yake. Lakini katika utangulizi wa waraka wake, anajitaja tu kama, “Mtumishi wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo.” Yakobo 1:1 Kadiri unavyokuwa karibu na Yesu, ndivyo unavyopunguza kujitukuza.

Kadiri unavyokuwa karibu na Yesu ndivyo unavyopunguza kujitukuza

Watumishi hufikiri huduma kama nafasi, na siyo wajibu. Wanafurahia kusaidia watu na kusaidia mahitaji, na kufanya huduma. Wao “humtumikia Mungu kwa furaha,” (Zaburi 100:2) kwa nini wanatumika kwa furaha? Kwa sababu wanampenda Bwana, wanamshukuru kwa neema yake, wanajua kutumika ndilo lengo kuu la maisha, na wanajua Mungu ameahidi thawabu. Yesu aliahidi, “Baba atamheshimu na kumzawadia yeyote anayenitumikia.” Yohana 1:26 (Msg) Paulo alisema, “Hatasahau kazi yenu ngumu kwa ajili yake na jinsi mlivyoonyesha upendo wenu kwake kwa kuwahudumia wakristo wengine.” Waebrania 6:10 (NLT)

SIKU YA THELATHINI NA NNE

KUFIKIRA JUU YA LENGO LANGU

Jambo la Kutafakari: Ili kuwa mtumishi lazima nifikiri kama mtumishi.

Kifungu cha kukumbuka: “Nia yenu iwe sawa ni ile ya Yesu Kristo.” Wafilipi 2:5 (NIV)

Swali la kujiuliza: Je, ninaangalia sana kutumikiwa au kutafuta njia za kutumikia wengine?

Siku ya Thelathini na Tano: Nguvu Ya Mungu Katika Udhaifu Wako

Sisi tu dhaifu … lackini kwa nguvu za Mungu tutaishi naye ili kuwatumikia.

2 Wakorintho 13:4 (NIV)

Mimi niko pamoja nawe; hiyo inakutosha. Nguvu yangu

 hudhihirika vyema katika watu dhaifu.

2 Wakorintho 12:9 a (LB)

Mungu hupenda kutumia watu dhaifu.

Kila mtu ana udhaifu. Kusema ukweli, una lundo la makosa na mapungufu: ya kimwili, kihisia, kiakili, na kiroho. Unaweza pia kuwa na mazingira yaliyo zaidi ya uwezo wako yanayokudhoofisha, kama vile mapungufu ya kifedha au mahusiano. Jambo la muhimu ni kile unachokifanya na hali hizi. Mara nyingi tunakana udhaifu wetu, tunatetea, tunatoa udhuru, tunaficha, na kuchukia. Hii humzuia Mungu kutumia udhaifu huo kama upendavyo.

Mungu ana mtazamo tofauti kwa udhaifu wako. Anasema, “Mawazo yangu na njia zangu ziko juu kuliko zenu.” Isaya 55:9 (CEV) Hivyo mara nyingi yeye hutenda kinyume kabisa na mategemeo yetu. Tunafikiri Mungu hupenda tu kutumia nguvu zetu, lakini pia anapenda kutumia udhaifu wetu kwa ajili ya utukufu wake.

Biblia inasema, “Mungu kwa makusudi alichagua … kilicho dhaifu machoni pa ulimwengu ili kuviaibisha vyeye nguvu.” 1 Wakorintho 1:27 (TEV) Madhaifu yako siyo bahati mbaya. Mungu aliyaruhusu kwa makusudi kabisa, kwa lengo la kudhihirisha nguvu zake kupitia wewe.

Mungu kamwe hajapendezwa na nguvu na utoshelevu wa binafsi. Hakika, anavutwa na watu dhaifu, wenye kukubali hivyo. Yesu alihesabu utambuzi wa uhitaji wetu kuwa kama, “mashini wa rohoni.” Huu ndio msimamo wa kwanza anaoubariki. (Mathayo 5:3)

Biblia imejaa mifano ya namna Mungu anavyopenda kutumia watu wa kawaida wenye mapungufu kufanya mambo yasiyo ya kawaida bila kujali udhaifu wao. Kama Mungu angetumia tu watu wakamilifu, hakuna ambacho kingetendeka, kwa sababu hakuna mmoja wetu asiye na mapungufu. Kwamba Mungu anatumia watu wenye mapungufu ni habari ya kututia moyo sisi sote.

Udhaifu, au “mwiba” kama Paulo alivyouita, (2 Wakorintho 12:7) siyo dhambi au uovu au tabia mbaya unayoweza kuibadili, mfano, ulafi, au kukosa uaminifu. Udhaifu ni upungufu wowote uliorithi au huna uwezo wa kuubadili. Unaweza kuwa upungufu wa kimwili, kama ulemavu, ugonjwa usiopona au nguvu kidogo. Waweza kuwa upungufu wa kihisia, kama vile kovu la hofu kuu, tumbukumbu inayoumiza, udhaifu wa nafsi, au mwelekeo wa kurithi. Au waweza kuwa upungufu wa kipawa au akili. Sote si watu wenye akili nyingi au kipawa.

Kama Mungu angetumia tu watu wakamilifu hakuna ambacho kingetendeka.

Unapofikiri mapungufu katika maisha yako, unaweza kujaribiwa kusema, “Mungu kamwe asingeweza kunitumia.” Lakini Mungu hafungwi na mapungufu yetu. Kusema kweli anafurahia kuweka nguvu zake nyingi katika vyombo vya kawaida. Biblia inasema, “Sisi ni kama vyombo vya udongo ambamo ametunza hazina yake nguvu halisi hutoka kwa Mungu na siyo kutoka kwetu.” 2 Wakorintho 4:7 (CEV) Kama chombo cha udongo, tunaweza kuvunjika na tuna mapungufu. Lakini Mungu atatutumia kama tukimruhusu kupitia udhaifu wetu. Ili iweze kutokea, tunatakiwa kufuata mfano wa Paulo.

Kiri udhaifu wako. Ukikubali upungufu wako. Acha kujifanya una kila kitu. Uwe mkweli kwako mwenyewe. Badala ya kuishi kwa kukana na kutoa udhuru, chukua muda kuainisha udhaifu wako. Unaweza kufanya orodha yake.

Ukiri mkubwa wa aina mbili katika Agano Jipya unaelezea unachohitaji ili kuishi maisha ya utoshelevu. Ukiri wa kwanza ulitolewa na Petro, alimwambia Yesu “Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” Mathayo 16:16 (NIV) Ukiri wa pili ni ule wa Paulo alipowaeleza kundi lililotaka kumwabudu kama Mungu, “Sisi ni wanadamu tu kama ninyi.” Matendo 14:15 (NCV) Kama unataka Mungu akutumie, lazima ujue Mungu ni nani na ujue wewe ni nani. Wakristo wengi, hasa viongozi, husahau ukweli huu wa pili: sisi ni binadamu tu! Kama italazimu ufikwe na tatizo ili ukubali ukweli huu, Mungu hatasita kuliruhusu, kwa sababu anakupenda.

Ridhika na udhaifu wako. Paulo anasema, “Nafurahi kujisifia udhaifu wangu, ili kwamba nguvu ya Kristo ifanye kazi kupitia mimi. Kwa kuwa nafahamu yote ni kwa ajili ya Kristo. Nimeridhika kabisa na udhaifu wangu.” 2 Korintho 12:9-10a (NLT) Mwanzoni hili halileti maana. Tunataka kuwekwa huru kutoka udhaifu wetu. Haturidhiki nao! Lakini kuridhika ni udhihirisho wa imani katika wema wa Mungu. Ni kusema, “Mungu naamini unanipenda na unajua nini kinanifaa zaidi.”

Paulo anatupatia sababu kadhaa za kuridhika na udhaifu wetu wa kuzaliwa nao. Kwanza, zinatufanya tumtegemee Mungu. Akirejea kwenye udhaifu wake mwenyewe ambao Mungu alikataa kumwondolea, Paulo alisema, “Nina furaha sana juu ya mwiba … kwa kuwa ninapokuwa dhaifu ndipo nina nguvu … nikiwa na kidogo ndipo ninapomtegemea zaidi.” 2 Wakorintho 12:10 (LB) Unapojihisi dhaifu, Mungu anakukumbusha kumtegemea.

Udhaifu watu pia huzuia majivuno. Hutufanya wanyenyekevu. Paulo anasema, “Ili nisiwe na kiburi, nilipewa zawadi ya udhaifu. Ili kunifanya kila wakati nijue mipaka yangu.” 2 Wakorintho 12:7 (Msg) Mara nyingi Mungu huambatanisha udhaifu mkubwa na uwezo mkubwa ili kudhibiti ubinafsi wetu. Upungufu unaweza kufanya kazi kama kizuizi cha kutufanya tusiende kasi zaidi na kumtangulia Mungu.

Gidioni alipotayarisha jeshi la watu 32,000 ili kupigana na Wamidiani Mungu alilipunguza mpaka watu 300 tu, akifanya maajabu ya watu 450 kwa mtu mmja walipoenda kupigana na jeshi la watu 135,000. Ilionekana kuwa kujiletea janga kubwa, lakini Mungu alifanya hivyo ili Israel wajue kwamba ilikuwa ni nguvu za Mungu, siyo nguvu zao wenyewe zilizowaokoa.

Huduma yako bora zaidi itatokana na maumivu yako ya kina.

Udhaifu wetu pia huchochea ushirika baina ya waamini. Wakati nguvu huleta roho ya kujitegemea (sihitaji mtu yeyote), mapungufu yetu hutuonyesha jinsi tunavyohitajiana. Tunaposokota pamoja nyuzi dhaifu za maisha yetu, Kamba yenye nguvu nyingi inatengenezwa. Vance Havner alitoa mfano, “Wakristo kama vile kipande kidogo cha theluji ni hafifu, lakini kama vikishikamana vinazuia msafara wa magari.”

Zaidi ya yote, udhaifu wetu huongeza uwezo wetu wa huruma na huduma. Tunaweza kuwa na huruma zaidi na kujali udhaifu wa wengine. Mungu anakutaka uwe na huduma kama ya yesu duniani. Maana yake watu wengine watapata uponyaji katika vidonda vyako. Ujumbe wako mkubwa katika maisha na huduma yako bora zaidi itatokana na maumivu yako ya kina. Mambo yanayokuudhi na kuyaonea haya zaidi, na usiyapende kuyasema, ndiyo sana Mungu anazoweza kutumia kwa nguvu sana kuponya wengine.

Mmishenari mkubwa Hudson Taylor alisema, “Watu maarufu wote wa Mungu walikuwa watu wadhaifu.” Udhaifu wa Musa ulikuwa hasira, ilimsababisha kumwua Mmisri, kupiga mwamba uliotakiwa kuusemesha, na kuvunja mbao za amri kumi. Lakini Mungu alimgeuza Musa kuwa “mtu mpole kuliko wote duniani.” (Hesabu 12:3)

Udhaifu wa Gidioni ulikuwa kutokujiamini na hali ya hofu kuu. Lakini Mungu alimgeuza kuwa “mtu shujaa.” Wamuzi 6:12 (KJV) Udhaifu wa Ibrahimu ulikuwa uoga. Si mara moja, mara mbili alidai mke wake alikuwa dada yake ili ajilinde. Lakini Mungu alimgeuza Ibrahimu na kuwa “Baba wa walio na imani.” Warumi 4:11 (NLT) Petro mwenye haraka na asiye na msimamo alkuwa “mwamba.” Mathayo 16:18 (TEV) Daudi mzinzi alikuwa “mtu aupendezaye moyo wangu.” Matendo 13:22 (NLT) Na Yohana mmoja wa watoto wa ngurumo wenye majivuno, akawa “Mtume wa upendo.”

Orodha inaweza kuendelea. “Ingelihitaji muda mrefu kutoa imani ya … Baraka, Samsoni, Yefta, Daudi, Samweli, na manabii wote … udhaifu wao uligeuzwa kuwa nguvu.” Waebrania 11:32-34 (NLT) Mungu ni bingwa wa kugeuza udhaifu kuwa nguvu. Anapenda kuchukua udhaifu wako mkubwa na augeuze.

Shirikisha udhaifu wako kwa uaminifu. Huduma huanza na udhaifu. Kadiri unavyoacha kujilinda, ukavua vazi la bandia, na ukashirikisha wengine vita vyako, ndipo Mungu ataweza kukutumia kuwatumikia wengine. Paulo alitoa kielelezo cha udhaifu wake katika nyaraka zake.

l  Kushindwa kwake: “ninapotaka kutenda mema nashindwa, ninapojaribu nisitende mabaya nayatenda.” Warumi 7:19 (NLT)

l  Hisi zake: “nimewaambia hisia zangu zote.” 2 Wakorintho 6:11 (EB)

l  Mambo ya kuvunja moyo: “tulivunjwa moyo kiasi cha kushindwa kabisa, na tukafikiri tusingeweza kuishi kabisa.” 2 Wakorintho 1:8 (NLT)

l  Hofu zake: “nilipokuja kwenu, nilikuwa mdhaifu na mwenye hofu na kutetemeka.” 1 Wakorintho 2:3 (NCV)

Kwa kweli ni hatari. Laweza kuwa jambo la kuogofya kupunguza ulinzi wako na kuweka wazi maisha yako kwa watu wengine. Unapofunua kushindwa kwako, hisia, mambo ya kukuvunja moyo, na hofu, unajiweka katika hali ya kukataliwa. Lakini faida zake zinastahili hatari hiyo. Udhaifu huleta uhuru kihisia. Kujiweka wazi huleta ahueni ya moyo, huondoa hofu zako, na ni hatua ya kwanza katika kupata uhuru.

Tumeona kwamba Mungu “huwapa neema wanyenyekevu,” lakini wengi hawaelewi vyema unyenyekevu. Unyenyekevu siyo kujiweka chini au kukana nguvu zako; badala yake, ni kuwa wazi kuhusu udhaifu wako. Kadiri unavyokuwa wazi ndivyo unavyopata neema ya Mungu zaidi. Pia utapokea neema kutoka kwa wengine. Kukubali udhaifu ni sifa ya kudumu; kwa asili tunavutwa na watu wanyenyekevu. Maigizo hufukuza lakini uhalisi huvuta, na kukubali udhaifu ni mlango wa uhusiano wa karibu.

Siku ya Thelathini na Tano: Nguvu Ya Mungu Katika Udhaifu Wako

Sisi tu dhaifu … lackini kwa nguvu za Mungu tutaishi naye ili kuwatumikia.

2 Wakorintho 13:4 (NIV)

Mimi niko pamoja nawe; hiyo inakutosha. Nguvu yangu

 hudhihirika vyema katika watu dhaifu.

2 Wakorintho 12:9 a (LB)

Mungu hupenda kutumia watu dhaifu.

Kila mtu ana udhaifu. Kusema ukweli, una lundo la makosa na mapungufu: ya kimwili, kihisia, kiakili, na kiroho. Unaweza pia kuwa na mazingira yaliyo zaidi ya uwezo wako yanayokudhoofisha, kama vile mapungufu ya kifedha au mahusiano. Jambo la muhimu ni kile unachokifanya na hali hizi. Mara nyingi tunakana udhaifu wetu, tunatetea, tunatoa udhuru, tunaficha, na kuchukia. Hii humzuia Mungu kutumia udhaifu huo kama upendavyo.

Mungu ana mtazamo tofauti kwa udhaifu wako. Anasema, “Mawazo yangu na njia zangu ziko juu kuliko zenu.” Isaya 55:9 (CEV) Hivyo mara nyingi yeye hutenda kinyume kabisa na mategemeo yetu. Tunafikiri Mungu hupenda tu kutumia nguvu zetu, lakini pia anapenda kutumia udhaifu wetu kwa ajili ya utukufu wake.

Biblia inasema, “Mungu kwa makusudi alichagua … kilicho dhaifu machoni pa ulimwengu ili kuviaibisha vyeye nguvu.” 1 Wakorintho 1:27 (TEV) Madhaifu yako siyo bahati mbaya. Mungu aliyaruhusu kwa makusudi kabisa, kwa lengo la kudhihirisha nguvu zake kupitia wewe.

Mungu kamwe hajapendezwa na nguvu na utoshelevu wa binafsi. Hakika, anavutwa na watu dhaifu, wenye kukubali hivyo. Yesu alihesabu utambuzi wa uhitaji wetu kuwa kama, “mashini wa rohoni.” Huu ndio msimamo wa kwanza anaoubariki. (Mathayo 5:3)

Biblia imejaa mifano ya namna Mungu anavyopenda kutumia watu wa kawaida wenye mapungufu kufanya mambo yasiyo ya kawaida bila kujali udhaifu wao. Kama Mungu angetumia tu watu wakamilifu, hakuna ambacho kingetendeka, kwa sababu hakuna mmoja wetu asiye na mapungufu. Kwamba Mungu anatumia watu wenye mapungufu ni habari ya kututia moyo sisi sote.

Udhaifu, au “mwiba” kama Paulo alivyouita, (2 Wakorintho 12:7) siyo dhambi au uovu au tabia mbaya unayoweza kuibadili, mfano, ulafi, au kukosa uaminifu. Udhaifu ni upungufu wowote uliorithi au huna uwezo wa kuubadili. Unaweza kuwa upungufu wa kimwili, kama ulemavu, ugonjwa usiopona au nguvu kidogo. Waweza kuwa upungufu wa kihisia, kama vile kovu la hofu kuu, tumbukumbu inayoumiza, udhaifu wa nafsi, au mwelekeo wa kurithi. Au waweza kuwa upungufu wa kipawa au akili. Sote si watu wenye akili nyingi au kipawa.

Kama Mungu angetumia tu watu wakamilifu hakuna ambacho kingetendeka.

Unapofikiri mapungufu katika maisha yako, unaweza kujaribiwa kusema, “Mungu kamwe asingeweza kunitumia.” Lakini Mungu hafungwi na mapungufu yetu. Kusema kweli anafurahia kuweka nguvu zake nyingi katika vyombo vya kawaida. Biblia inasema, “Sisi ni kama vyombo vya udongo ambamo ametunza hazina yake nguvu halisi hutoka kwa Mungu na siyo kutoka kwetu.” 2 Wakorintho 4:7 (CEV) Kama chombo cha udongo, tunaweza kuvunjika na tuna mapungufu. Lakini Mungu atatutumia kama tukimruhusu kupitia udhaifu wetu. Ili iweze kutokea, tunatakiwa kufuata mfano wa Paulo.

Kiri udhaifu wako. Ukikubali upungufu wako. Acha kujifanya una kila kitu. Uwe mkweli kwako mwenyewe. Badala ya kuishi kwa kukana na kutoa udhuru, chukua muda kuainisha udhaifu wako. Unaweza kufanya orodha yake.

Ukiri mkubwa wa aina mbili katika Agano Jipya unaelezea unachohitaji ili kuishi maisha ya utoshelevu. Ukiri wa kwanza ulitolewa na Petro, alimwambia Yesu “Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” Mathayo 16:16 (NIV) Ukiri wa pili ni ule wa Paulo alipowaeleza kundi lililotaka kumwabudu kama Mungu, “Sisi ni wanadamu tu kama ninyi.” Matendo 14:15 (NCV) Kama unataka Mungu akutumie, lazima ujue Mungu ni nani na ujue wewe ni nani. Wakristo wengi, hasa viongozi, husahau ukweli huu wa pili: sisi ni binadamu tu! Kama italazimu ufikwe na tatizo ili ukubali ukweli huu, Mungu hatasita kuliruhusu, kwa sababu anakupenda.

Ridhika na udhaifu wako. Paulo anasema, “Nafurahi kujisifia udhaifu wangu, ili kwamba nguvu ya Kristo ifanye kazi kupitia mimi. Kwa kuwa nafahamu yote ni kwa ajili ya Kristo. Nimeridhika kabisa na udhaifu wangu.” 2 Korintho 12:9-10a (NLT) Mwanzoni hili halileti maana. Tunataka kuwekwa huru kutoka udhaifu wetu. Haturidhiki nao! Lakini kuridhika ni udhihirisho wa imani katika wema wa Mungu. Ni kusema, “Mungu naamini unanipenda na unajua nini kinanifaa zaidi.”

Paulo anatupatia sababu kadhaa za kuridhika na udhaifu wetu wa kuzaliwa nao. Kwanza, zinatufanya tumtegemee Mungu. Akirejea kwenye udhaifu wake mwenyewe ambao Mungu alikataa kumwondolea, Paulo alisema, “Nina furaha sana juu ya mwiba … kwa kuwa ninapokuwa dhaifu ndipo nina nguvu … nikiwa na kidogo ndipo ninapomtegemea zaidi.” 2 Wakorintho 12:10 (LB) Unapojihisi dhaifu, Mungu anakukumbusha kumtegemea.

Udhaifu watu pia huzuia majivuno. Hutufanya wanyenyekevu. Paulo anasema, “Ili nisiwe na kiburi, nilipewa zawadi ya udhaifu. Ili kunifanya kila wakati nijue mipaka yangu.” 2 Wakorintho 12:7 (Msg) Mara nyingi Mungu huambatanisha udhaifu mkubwa na uwezo mkubwa ili kudhibiti ubinafsi wetu. Upungufu unaweza kufanya kazi kama kizuizi cha kutufanya tusiende kasi zaidi na kumtangulia Mungu.

Gidioni alipotayarisha jeshi la watu 32,000 ili kupigana na Wamidiani Mungu alilipunguza mpaka watu 300 tu, akifanya maajabu ya watu 450 kwa mtu mmja walipoenda kupigana na jeshi la watu 135,000. Ilionekana kuwa kujiletea janga kubwa, lakini Mungu alifanya hivyo ili Israel wajue kwamba ilikuwa ni nguvu za Mungu, siyo nguvu zao wenyewe zilizowaokoa.

Huduma yako bora zaidi itatokana na maumivu yako ya kina.

Udhaifu wetu pia huchochea ushirika baina ya waamini. Wakati nguvu huleta roho ya kujitegemea (sihitaji mtu yeyote), mapungufu yetu hutuonyesha jinsi tunavyohitajiana. Tunaposokota pamoja nyuzi dhaifu za maisha yetu, Kamba yenye nguvu nyingi inatengenezwa. Vance Havner alitoa mfano, “Wakristo kama vile kipande kidogo cha theluji ni hafifu, lakini kama vikishikamana vinazuia msafara wa magari.”

Zaidi ya yote, udhaifu wetu huongeza uwezo wetu wa huruma na huduma. Tunaweza kuwa na huruma zaidi na kujali udhaifu wa wengine. Mungu anakutaka uwe na huduma kama ya yesu duniani. Maana yake watu wengine watapata uponyaji katika vidonda vyako. Ujumbe wako mkubwa katika maisha na huduma yako bora zaidi itatokana na maumivu yako ya kina. Mambo yanayokuudhi na kuyaonea haya zaidi, na usiyapende kuyasema, ndiyo sana Mungu anazoweza kutumia kwa nguvu sana kuponya wengine.

Mmishenari mkubwa Hudson Taylor alisema, “Watu maarufu wote wa Mungu walikuwa watu wadhaifu.” Udhaifu wa Musa ulikuwa hasira, ilimsababisha kumwua Mmisri, kupiga mwamba uliotakiwa kuusemesha, na kuvunja mbao za amri kumi. Lakini Mungu alimgeuza Musa kuwa “mtu mpole kuliko wote duniani.” (Hesabu 12:3)

Udhaifu wa Gidioni ulikuwa kutokujiamini na hali ya hofu kuu. Lakini Mungu alimgeuza kuwa “mtu shujaa.” Wamuzi 6:12 (KJV) Udhaifu wa Ibrahimu ulikuwa uoga. Si mara moja, mara mbili alidai mke wake alikuwa dada yake ili ajilinde. Lakini Mungu alimgeuza Ibrahimu na kuwa “Baba wa walio na imani.” Warumi 4:11 (NLT) Petro mwenye haraka na asiye na msimamo alkuwa “mwamba.” Mathayo 16:18 (TEV) Daudi mzinzi alikuwa “mtu aupendezaye moyo wangu.” Matendo 13:22 (NLT) Na Yohana mmoja wa watoto wa ngurumo wenye majivuno, akawa “Mtume wa upendo.”

Orodha inaweza kuendelea. “Ingelihitaji muda mrefu kutoa imani ya … Baraka, Samsoni, Yefta, Daudi, Samweli, na manabii wote … udhaifu wao uligeuzwa kuwa nguvu.” Waebrania 11:32-34 (NLT) Mungu ni bingwa wa kugeuza udhaifu kuwa nguvu. Anapenda kuchukua udhaifu wako mkubwa na augeuze.

Shirikisha udhaifu wako kwa uaminifu. Huduma huanza na udhaifu. Kadiri unavyoacha kujilinda, ukavua vazi la bandia, na ukashirikisha wengine vita vyako, ndipo Mungu ataweza kukutumia kuwatumikia wengine. Paulo alitoa kielelezo cha udhaifu wake katika nyaraka zake.

l  Kushindwa kwake: “ninapotaka kutenda mema nashindwa, ninapojaribu nisitende mabaya nayatenda.” Warumi 7:19 (NLT)

l  Hisi zake: “nimewaambia hisia zangu zote.” 2 Wakorintho 6:11 (EB)

l  Mambo ya kuvunja moyo: “tulivunjwa moyo kiasi cha kushindwa kabisa, na tukafikiri tusingeweza kuishi kabisa.” 2 Wakorintho 1:8 (NLT)

l  Hofu zake: “nilipokuja kwenu, nilikuwa mdhaifu na mwenye hofu na kutetemeka.” 1 Wakorintho 2:3 (NCV)

Kwa kweli ni hatari. Laweza kuwa jambo la kuogofya kupunguza ulinzi wako na kuweka wazi maisha yako kwa watu wengine. Unapofunua kushindwa kwako, hisia, mambo ya kukuvunja moyo, na hofu, unajiweka katika hali ya kukataliwa. Lakini faida zake zinastahili hatari hiyo. Udhaifu huleta uhuru kihisia. Kujiweka wazi huleta ahueni ya moyo, huondoa hofu zako, na ni hatua ya kwanza katika kupata uhuru.

Tumeona kwamba Mungu “huwapa neema wanyenyekevu,” lakini wengi hawaelewi vyema unyenyekevu. Unyenyekevu siyo kujiweka chini au kukana nguvu zako; badala yake, ni kuwa wazi kuhusu udhaifu wako. Kadiri unavyokuwa wazi ndivyo unavyopata neema ya Mungu zaidi. Pia utapokea neema kutoka kwa wengine. Kukubali udhaifu ni sifa ya kudumu; kwa asili tunavutwa na watu wanyenyekevu. Maigizo hufukuza lakini uhalisi huvuta, na kukubali udhaifu ni mlango wa uhusiano wa karibu.

SIKU YA THELATHINI NA TANO:

NGUVU YA MUNGU KATIKA UDHAIFU WAKO

Ndiyo maana Mungu anapenda kutumia pia udhaifu wako, na sio tu nguvu zako. Kama watu wote wanaona nguvu zako tu wanakatishawa tamaa kufikiri, “Sawa, heri yake,lakini kamwe mimi sitaweza kufanya hivyo,” Lakini wakiona Mungu anakutumia pamoja kwamba wewe ni dhaifu huwatia nguvu na kufikiri “Labda Mungu anaweza kunitumia hata mimi!” Nguvu zetu hujenga ushindani lakini udhaifu wetu hujenga ushirika wa jamii.

Katika maisha yako ufikie kuamua kama unataka kuwapendeza watu au kuwavutia watu. Unaweza kuwapendeza watu kutoka kwa mbali lakini ni vizuri uwe karibu nao ili uwavute. Na unapofanya hivyo, wataweza kuyaona mapungufu yako Hiyo ni sawa tu. Sifa muhimu sana kwa uongozi siyo ukamilifu, lakini ni kuaminika. Watu lazima waweze kukuamini au hawatakuamini. Je, unajengaje uaminifu? Siyo kwa kuigiza kuwa mkamilifu, lakini kwa kuwa mkweli.

Jisifie udhaifu wako. Paulo anasema “Nitajisifia tu jinsi nilivyo dhaifu na jinsi Mungu alivyo mkuu kuweza kutumia udhaifu huo kwa utukufu wake.” 2 Wakorintho 12:5b (LB) Badala ya kujitumainia mwenyewe kama mtu asiyeweza kushindwa kitu, jione mwenyewe kama kumbukumbu ya neema. Shetani anapotaja udhaifu wako, mkubalie na ujaze moyo wako na sifa kwa Yesu ambaye “anaelewa kila udhaifu wetu.” Waebrania 4:1a (CEV) Na kwa Roho Mtakatifu ambaye “hutusaidia udhaifu wetu.” Warumi 8:26a (NIV)

Wakati mwingine, lakini, Mungu hugeuza nguvu kuwa udhaifu ili atutumie zaidi. Yakobo alikuwa mwenye hila aliyetumia maisha yake kwa kufanya hila na kukimbia matokeo yake. Usiku mmoja alipambana na Mungu na kusema “Sitakuacha uende hadi unibariki. “Mungu alisema, “Sawa.” Lakini hapa alikamata paja la Yakobo na kulitegua mfupa. Maana yake ni nini?

Mungu alikamata nguvu za Yakobo (msuli wa paja ndio wenye nguvu kuliko zote mwilini) na kuugeuza katika udhaifu. Tangu siku hiyo na kuendelea, yakobo alitembea kwa kuchechemea hivyo asingeweza kukimbia na kutoroka tena. Ilimfundisha kumtegemea Mungu apende au asipende. Ukitaka Mungu akubariki na akutumie sana, lazima uwe tayari kutembea kwa kuchechemea maisha yako yaliyobaki, kwa sababu Mungu hutumia watu dhaifu.

SIKU YA THELATHINI NA TANO

KUFIKIRA JUU YA LENGO LANGU

Jambo la Kutafakati: Mungu hutenda kazi vyema ninapokubali udhaifu wangu.

Kifungu cha Kukumbuka:Neema yangu yakutosha, nguvu zangu hukamilika katika udhaifu.” 2 Wakorintho 2:9a (NIV)

Swali la kujiuliza: Je, nazuia nguvu ya Mungu katika maisha yangu kwa kujaribu kuficha udhaifu wangu? Je, nahitaji kuwa mkweli katika jambo gani ili kuwasaidia wengine?

 

 

 

 

 

 

 

 

沒有留言:

張貼留言