Siku
ya Kumi na Tatu: Ibada Impendezayo Mungu
Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho
yako yote na kwa akilizako zote na kwanguvu zako zote.
Marko 12:30 (NIV)
Mungu anakutaka wewe mzima.
Mungu hapendi sehemu tu ya maisha yako. Anapenda umpe moyo
wako wote,
roho yako yote,
akili zako zote,
na nguvu zako zote.
Mungu hafurahii kujitoa nusu, nusu utii, na mabaki ya muda na pesa zako. Anatamani
kujitoakwako kikamilifu, siyo sehemu ndogo tu za maisha yako.
Wakati Fulani, Mwanamke Msamaria alijaribu kuwa na mjadala
na Yesu kuhusu muda sahihi, mahali pa kuabudu, na namna ya kuabudu. Yesu
alijibu kwamba haya mambo ya nje hayana maana. Mahali unapoabudia si muhimu
kama kwa nini unaabudu na kiasi gani unajitoa unapomwabudu Mungu. Kuna njia
sahihi na isiyo sahihi katika kuabudu. Biblia inasema, “Tuwe na shukurani nakumwabudu Mungu katika njia
inayompendeza.” Waebrania 12:28 (TEV) Aina ya kuabudu inayompendeza Mungu
ina sifa nne:
Mungu
anafurahia kuabudu kwetu kunapokuwa sahihi.
Mara nyingi watu husema, “Napenda kumfikiri Mungu kama ….,” na kisha wanaeleza
mawazo yako kuhusu aina ya Mungu ambaye wangependa kumwabudu. Lakini hatuwezi
kujitengenezea sura ya Munguinayotupendeza au ya kisiasa nakuiabudu. Hiyo ni
ibada ya sanamu.
Ibada ya kumpendezea Munguni ya hisia za kina na
mafundisho ya Imani ya kina. Tutatumia moyo na vichwa vyetu pamoja. |
“Kuabudu katika kweli” maana yake ni kumwabudu Mungu kama kweli ilivyofunuliwa
katika Biblia.
Mungu
anafurahia kuabudu kwetu kunapokuwa halisi. Yesu
aliposema ni lazima “kuabudu katika roho,”
hakuwa akimaanisha Roho Mtakatifu, lakini roho yako. Ukiwa umeumbwa kwa mfano wa Mungu, wewe ni roho inayoishi
katika mwili, na Mungu alibuni roho yako iwasiliane naye. Kuabudu ni roho yako
inaitikia kwa Roho waMungu.
Yesu aliposema, “Mpende Mungu wako kwa
moyo na roho” alimaanisha kwamba
kuabudu lazima kuwe kweli na kuguse moyo. Si jambo la kusema tu maneno sahihi;
ni lazima umaanishe unachokisema. Sifa zisizotoka moyoni si sifa hata kidogo.
Hazifai na nikumtukana Mungu.
Tunapoabudu, Mungu haangalii maneno kwanza huangalia nia ya
moyo wetu. Biblia husema, “Mwanadamu huangalia
mwonekano wanje, lakini Bwana huangalia moyo.”1
Samweli 16:7b (NIV)
Kwa kuwa kuabudu kumehusisha kumfurahia Mungu, kunahusisha
hisia zako. Mungu alikupa hisia ili uweze kumwabudu na hisia za kina – lakini
hisia hizo lazima ziwe halisi na siyo za kuigiza. Mungu anachukia unafiki.
Hapendi kujionyesha, au kuigiza au sauti za ajabu ajabu. Anapenda upendo wetu
halisi. Tunaweza kumwabudu Mungu si kikamlifu lakini tunaweza kunaweza
kumwabudu
kiukweli.
Ukweli peke yake hautoshi; unaweza kuwa mkweli lakini katika
makosa. Ndio maana vyote viwili ukweli na roho vinahitajika. Kuabudu lazima
kuwe sahihi na kweli. Ibada ya kumpendeza Mungu ni ya hisia za kina na
mafundisho ya imani ya kina. Tunatumia moyo na vichwa vyetu pamoja.
Watu wengi siku hizi wanalinganisha mvuto wa muziki kwa
hisia na kule kuvutwa na Roho, lakini haya mawili si sawa. Kuabudu halisi
hutokea pale roho yako inamwitikia Mungu na siyo sauti ya muziki. Hakika nyimbo
nyingine zenye mguso wa hisia zetu za ndanihuzuiakuabudu kwa sababu hutuondoa
katika kumwelekea Mungu na badala yake tunaelekea kwenye hisia zetu. Kizuizi
kikubwa katika kuabudu ni wewe mwenyewe – mambo uyapendayo na hofu zako kuhusu
watu wengine wanakufikiriaje.
Njia bora ya kuabudu ni ile inayoonyesha kwa uhalisi
upendo wako kwa Mungu. |
Rafiki yangu Gary Thomas aligundua kwamba wakristo wengi
huonekana kuzama katika shimo la kuabudu-jambo la kila mara
lisilotosheleza-badala ya kuwa na urafiki uliochangamka na Mungu, kwa sababu
hujilazimisha kufuata taratibu za kujitoa au mitindo yakuabudu ambazo haziwiani
na jinsi Mungu alivyowaumba.
Gary alishangaa, kama Mungu alituumba
tofauti, yawezekanaje kila mtu atazamiwe kumpenda Mungu kwa njia moja? Aliposoma maandishi ya Kikristo ya siku hizi na kuwasaili
waamini waliokomaa, Gary aligundua kwamba Wakristo wanatumia njia nyingi
tofauti kwa miaka 2000 kufurahia uhusiano wa karibu na Mungu: Kukaa nje ya
nyumba, kujifunza, kuimba, kusoma, kucheza, kutengeneza Sanaa, kuwatumikia
wengine, kuwa pekee, kushirikiana na wengine, na kushiriki katika shughuli
mbalimbali.
Katika kitabu chaake, Njia
Takatifu, Gary anataja njia tisa ambazo kwanza watu humkaribia
Mungu: wapendao uumbaji wa asili (naturalists) wanasukumwa kumpenda Mungu nje ya majumba, katika
mazingira ya asili. Watu wenye mvuto wa milango ya fahamu (sensates)
humpenda Mungu kwa milango yao ya fahamu na hupenda ibada nzuri inayohusisha
kuona, kuonja, kunusa, kugusa, na siyo masikio yao tu. Watu wa desturi (traditionalists)
humwendea Mungu kwa kufuata njia za kanuni za kidini, liturujia, alama, na
mifano isiyobadilika. Watu wenye kujikana (ascetics) humpenda Mungu kwa kukabili uovu, kupigania haki, na
kuufanya ulimwengu uwe mahali bora. Waangalizi (caregivers) humpenda Mungu kwa kuwapenda wengine na kuwatimizia
mahitaji yao. Watu wenye shauku (enthusiasts) humpenda Mungu kwa sherehe. Watu
wa kutafakari (contemplatives) humpenda Mungu kwa njia ya kusujudu. Watu wenye akili
nyingi (intellectuals) humpenda Mungu kwa kujifunza kwa kili zao. (Gary Thomas, njia takatifu,
(Grand Rapids: Zondervan, 2000).
Hakuna “njia moja” inayofaa kwa watu wote kumwabudu na
kufanya urafiki na Mungu. Jambo moja ni bayana: Huwezi kuleta utukufu kwa Mungu
kwa kujaribu kuwa mtu Fulani ambaye hukukusudiwa kuwa. Mungu anakutaka uwe wewe
mwenyewe. “Hao ndio aina yawatu Baba anawatufuta: wale ambao husimama mbele za
Mungu katika hali rahisi yauhalisi wao katika kuabudu kwao. Yohana 4:23 (Msg)
Mungu
anafurahia ibada yetu inapokuwa na kutafakari. Amri
ya Yesu ya “Mpende Mungu kwa akili zako zote” imerudiwa mara nne katika Agano Jipya. Mungu hafurahii
nyimbo zisizo na kufikiri, kusali sala za harakaharaka bila kujali, au maneno
ya ovyo ya “Bwana asifiwe,” Kwa sababu hatuna neno jingine tunaloweza kusema
kwa wakati huo. Kama kuabudu hakuhitaji akii, basi hakuna maana yoyote. Ni
lazima utumie akili zako.
SIKU
YA KUMI NA TATU: IBADA IMPENDEZ AYO MUNGU |
Jaribu kumtumikia Mungu bila kutumia maneno kama Bwana asifiwe, haleluya, asante, au amina. Badala ya kusema, “Tunataka kukutukuza,” fanya orodha ya
maneno yanayofanana kama vile tamani, heshimu,
thamini, kucha, inua, na shukuru.
Pia uwe na uhalisi.
Kama mtu Fulani angekuja kwako na kurudiarudia, “Nakusifu!” mara kumi, labda
ungefikiri, kwa nini?
Ni bora ungepokea sifa mara mbili za kitu halisi kuliko ishirini za jumla. Hata
Mungu ni hivyo.
Wazo jingine ni kuorodhesha majina ya Mungu na kuyaangalia kwa
makini. Majina ya Mungu hayakuwekwa tu; yanatueleza kuhusu mambo mbalimbali
kuhusu tabia yake. Katika Agano la kale, Mungu alijifunua hatua kwa hatua kwa
kutambulisha majini yake mapya, na anatuagiza kulisifu jina lake. (Angalia
mlolongo 11 wa kanda kanda za majina ya Mungu, “Jinsi Mungu
Anavyokutana na Mahitaji Yako Ya Ndani,” na
Wachungaji wa Saddleback (1999), www.pastors.com
Mungu anapenda ibada yetu ya pamoja iwe ya kufikiri pia. Paulo
aliandika sura nzima kwa ajili ya jambo hili katika 1Wakorintho 14 na
anahitimisha hivi, “Kila kitu kifanyike kwa njia
inayokubalika na kwa utaratibu.”
1 Wakorintho 14:40 (NIV)
Sawa na hili, Mungu anasisitia kwamba ibada yetu ya pamoja ieleweke
kwa wasioamini wanapohudhuria mikusanyiko ya kuabudu. Paulo alisema, “Fikiri
wageni wamehudhuria katika ibada yenu, mnapomtukuza Mungu katika roho zenu.
Kama hawatawaelewa, watajuaje kusema “Amina”? Mnaweza kuwa mnamwabudu Mungu
katika njia nzuri, lakini hakuna hata mwingine atakayesaidika.” 1 Wakorintho 14:16-17 (NIV) Kuwajali wasioamini wanaotembelea
mikusanyiko yenu ya kuabudu ni amri ya kibiblia. Kutokujali amri hii ni kutotii
na kukosa upendo. Kwa maelezo ya kina kuhusu jambo hili angalia sura inayohusu “Kuabudu
Kunaweza Kuwa Ushuhuda”katika kitabu cha Kanisa Linaloongozwa
Na Malengo.
Mungu
anafurahia kuabudu kwetu kukiwa na matendo. Biblia
inasema, “Itoeni miili
yenu kama dhabihu iliyo hai, takatifu naya kumpendeza Mungu – hili ndilo tendo
lenu la kiroho la kuabudu.” Warumi 12:1 (NIV) Kwa nini Mungu
anapendaa mwili wako? Kwa nini hasemi, “Toa roho yako?” Kwa sababu bila mwili
wako huwezi kufanya chochote katika sayari hii. Mbinguni utapokea mwili mpya wa
kiwango cha juu, lakini unapokuwa hapa duniani, Mungu anasema, “nipe ulicho
nacho!” Anahitaji matendo katika kuabudu.
Umesikia watu wakisema, “Leo siwezi kuja katika ibada lakini nitakuwa
pamoja nanyi katika roho.” Unajua hiyo ina maana gani? Hakuna. Haina maana yoyote! Maadamu
bado uko duniani, roho yako yaweza kuwepo tu mwili wako ulipo. Kama mwili wako
haupo pale, basi hata roho yako haiko hapo.
Katika kuabudu tunatoa “miili yetu kama dhabihu iliyo hai.” Sasa
mara nyingi tunaunganisha wazo la “dhabihu” na kitu kilichokufa, lakini Mungu
anakutaka uwe dhabihu hai. Anapenda umwishie! Lakini, tatizo la sadaka hai ni
kwamba inaweza kutambaa kutoka madhabahuni, na mara nyingi tunafanya hivyo.
Tunaimba, “Twende mbele, Askari Wakristo,” siku ya Jumapili; na siku ya
Jumatatu tumetoroka jeshini.
Katika Agano la Kale Mungu alifurahia dhabihu nyingi za ibada kwa
vile zilikuwa kielelezo cha sadaka ya Yesu msalabani kwa ajili yetu. Sasa Mungu
anafurahishwa na sadaka mbali mbali za kuabudu, kama vile: shukurani, sifa,
unyenyekevu, toba, pesa, sala, kuwatumikia wengine, na kuwasaidia wahitaji.
Zaburi 5:14 (TEV); Waebrania 13:15 (CEV); Zaburi 51:17; 54:6 (NIV); Filipi 4:18
(NIV); Zaburi 141:2 (GWT); Waebrania 13:16; Marko 12:33 (Msg); Warumi 12:1
(TEV).
Kuabudu halisi kuna gharama. Daudi alijua hivi na akasema, “Sitamtolea
Bwana wangu sadaka ambazo hazikunigharimu chochote.”
2 Samweli 24:24 (TEV)
Jambo moja ambalo kuabudu hutugharimu ni ubinafsi wetu. Huwezi
kumwinua Mungu na ukajinua mwenyewe kwa wakati mmoja. Hauabudu ili uonekane na
wengine au kujipendezesha nafsi yako. Kwa makusudi kabisa unaacha kujielekea
nafsi yako.
Yesu aliposema, “Mpende Mungu wako kwa nguvu zako zote,”alionyesha kwamba kuabudu huchukua
bidi na nguvu. Mara nyingi si tendo rahisi na la kufurahia, na wakati mwingine
kuabudu ni tendo la kukusudia katika utashi-sadaka ya kupenda. Ibada
isiyotokkana na utashi wetu ni upuuzi tu.
Unapomsifu Mungu hata pale hujisikii, unapotoka kitandani ili kuabudu
ukiwa umechoka, au unapowasaidia wengine na wakati wewe mwenyewe uko hoi,
unatoa dhabihu ya kuabudu kwa Mungu. Hivyo humfurahisha Mungu sana.
Matt Redman, kiongozi wa kuabudu huko Uingereza, anaeleza jinsi
Mchungaji wake alivyofundisha Kanisani maana ya kuabudu. Kuonyesha kuwa kuabudu
ni zaidi ya muziki, aliondoa uimbaji katika ibada zote kwa muda fulani huku
wakijifunza kuabudu kwa njia nyingine. Mwisho wa muda huo, Matt alikuwa
ameandika wimbo wa kisasa uitwao “Moyo wa kuabudu”:
Nitakuletea zaidi ya wimbo,
Kwa sababu wewe huhitaji wimbo
peke zake.
Unachunguza ndani zaidi Kuliko mambo
yanayoonekana.
Unaona moyoni mwangu.
Matt Redman, Moyo wa kuabudu
(Kingsway’s Thankyou Music, 1997)
Kiini cha jambo ni jambo la kiini.
SIKU YA KUMI NA TATU KUFIKIRI JUU YA LENGO LANGU Jambo la Kutafakari: Mungu ananitaka mimi mzima. Kifungu cha Kukumbuka: “Mpende
Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako
zote na kwa nguvu zako zote.”Marko 12:30 (NIV) Swali la kujiuliza: Je, ni jambo gani linalomfurahisha
zaidi Mungu sasa hivi – ibada ya pamoja na wengine au ibada yangu binafsi?
Je, nitafanya nini kuhusu hili? Siku ya Kumi Na Nne:
Wakati Mungu Anapoonekana kuwa Mbali |
Mungu
amejificha kutoka kwa watu wake, Lakini namwamini na kuweka
tumaini
langu kwake.
Isaya 8:17 (TEV)
Mungu yupo haijalishi unajisikiaje.
Ni rahisi kumwabudu Mungu mambo yanapokuwa yanakuendea vizuri
maishani – anapokuwa amekupa chakula, marafiki, jamaa, afya, na hali ya
kupendeza. Lakini mazingira hayawi ya kupendeza siku zote. Je, unamwabudu Mungu
vipi basi? Unafanyaje wakati Mungu anapoonekana kuwa maili milioni moja mbali
nawe?
Kiwango cha kina sana cha kuabudu ni kumsifu Mungu hata katika
maumivu, kumshukuru Mungu wakati wa majaribu, kumwamini unapojaribiwa,
kujisalimisha huku unaumia, na kumpenda anapoonekana kuwa mbali.
Urafiki mara nyingi unajaribiwa kwa kutengana au ukimya; mnatengwa
kwa umbali wa mahali au kwa kutoongea. Katika urafiki wako na Mungu,
hutajisikia wakati wote kuwa karibu naye. Philip Yancey amesema kwa hekima
kwamba, “Uhusiano wowote huwa na nyakati za ukaribu na nyakati za kuwa mbali,
na katika uhusiano na Mungu, haijalishi ukaribu uliopo, kutakuwa na hali ya
kuwa karibu na kutokuwa karibu.” Philip Yancey, Kusoma Kwa Ajili
ya Mungu Asiyeonekana (Grand
Rapids: Zondervan, 2000), 242. Ndipo hapo kuabudu huwa kugumu.
Ili kukomaza urafiki wenu, Mungu ataujaribu kwa wakati unaoonekana
kama kutengana – nyakati unapojisikia kama amekuacha au amekusahau. Unamsikia
Mungu kama yupo maili milioni moja mbali nawe. St. John of the Cross aliziita
siku hizi za ukavu wa kirobo, mashaka, na kutengwa na Mungu kama “usiku wa giza
kwa roho.” Henri Nouwen aliziita nyakati hizi “huduma ya kutokuwepo.” A.W.
Tozer aliziita nyakati hizo “huduma ya usiku.” Wengine huziita “kiangazi cha
moyo.”
Mbali na Yesu, Daudi labda alikuwa na ukaribu kwa Mungu zaidi ya
mtu yeyote. Mungu alifurahia kumwita “mtu aupendezaye moyo wa Mungu.” 1 Samweli
13:14; 13:22 Lakini bado Daudi alilalamika juu ya Mungu kuwa mbali. “Bwana,
mbona umekaa kando na uko mbali sana? Kwa nini umejificha ninapokuhitaji sana?”Zaburi 10:1 (LB) “Kwa nini umeniacha? Kwanini uko mbali
hivyo?”“Kwa
nini hujali kilio changu kwa ajili ya msaada?”
Zaburi 22:1 (NLT) “Mbona umeniacha?” Zaburi 43:2 (TEV); Zaburi 44:23 (TEV); 74:11 (TEV).
Kwa kweli, Mungu hakuwa amemwacha Daudi, na hakuachi. Ameahidi
mara nyingi, “sitakuacha wala kukupungukia kamwe.” Kumbukumbu 31:8; Zaburi
37:28; Yohana 14:16-18; Ebrania 13:5. Lakini Mungu hajaahidi kwamba “siku zote
utahisi uwepo wangu.” Hakika, Mungu anasema wazi kwamba wakati mwingine
anaficha uso wake toka kwetu. Ayubu 23:8-10 (NLT) Kuna nyakati anapoonekana
kutokuwa katika matendo maishani mwako.
Floyd McClung hueleza nyakati hizo kama hivi: “Unaamka siku moja
asubuhi na hisia zako zote za kiroho zinatoweka. Unasali lakini hakuna
linalotokea. Unamkemea Shetani, lakini hakuna badiliko lolote. Unafanya mazoezi
ya kiroho … rafiki zako wanakuombea … unatubu kila dhambi unayoidhania, kisha
unazunguka kuomba msamaha kwa kila unayemfahamu. Unafunga … Bado hakuna kitu.
Unaanaza kushangaa giza hili la kiroho litakwisha lini. Siku? Wiki? Mwezi? Je,
kweli litakwisha? … inaonekana kama sala zako zinagonga dari. Katika kukata
tamaa kabisa, unalia “Nina tatizo gani?” Floyd McChung, Kupata kufanya na Mungu
(Ann Arbot, MI: Vine books 1992, 186.)
Mungu anasema wazi kwamba wakati mwingine anaficha
uso wake toka kwetu. |
Wakati Mungu anaonekana kuwa mbali, unajisikia kwamba
amekukasirikia au anakuadhibu kwa sababu ya dhambi Fulani. Ni kweli, dhambi
hututenganisha kutoka ushirika wa karibu na Mungu. Tunamhuzunisha Roho wa Mungu
na kuzimisha uhusiano wetu kwa kutotii, ugomvi na watu wengine, shughuli
nyingi, urafiki na dunia, na dhambi nyingine. Zaburi 51; Efeso 4:29-30; 1 Wathesalonike
5:19; Yeremia 2:32; 1 Wakorintho 8:12; Yakobo 4:4 (NLT).
Lakini mara nyingi hali hii ya kujisikia kuachwa au kutengwa na
Mungu haihusiani na dhambi. Ni kipimo cha Imani– jambo ambalo sote lazima
litupate: Je, utaendelea kumpenda, kumwamini, kumtii, na kumwabudu Mungu, hata
kama huhisi uwepo wake au ushahidi unaoonekana wa wazi maishani mwako?
Kosa linalofanywa na Wakristo wengi katika kuabudu siku hizi ni
kutafuta uzoefu badala ya kumtafuta Mungu. Wanatafuta hisia, na iwapo itatokea
wanaamini kuwa sasa wameabudu. Ni makosa! Kwa kweli, mara nyingi Mungu huondoa
hisia ili tusizitegemee. Kutafuta hisia, hata hisia ya ukaribu na Kristo, siyo
ibada.
Unapokuwa mkristo mchanga, Mungu hukupa hisia nyingi za
uthibitisho na mara nyingine anajibu sala nyingi za uchaga na ubinafsi – ili
ujue yupo. Lakini unapokua katika Imani, anakuachisha hali ya utegemezi.
Kosa linalofanywa na wakristo katika kuabudu siku
hizi ni kutafuta uzoefu badala ya kumtafuta Mungu. |
Ndiyo, anapenda wewe uhisi uwepo wake, lakini anajali sana umwamini zaidi kuliko unavyomhisi. Imani, na siyo hisia, ndiyo inayompendeza Mungu.
Nyakati zitakazokuza Imani yako ni pale maisha yako yanapoonekana
yanasambaa na Mungu hapatikani. Hii ilitokea kwa Ayubu. Kwa siku moja alipoteza
kila kitu – jamaa yake, miradi yake, afya yake, na kila alichokuwa nacho. Sura
thelathini za kukatisha tamaa, Mungu hakusema kitu!
Utamtukuzaje Mungu wakati huelewi kinachoendelea maishani mwako na
Mungu amenyamaza? Utakaaje katika uhusiano wakati wa shida bila mawasiliano?
Utawekaje macho yako katika Yesu yakiwa yamejawa na machozi?
Fanya alivyofanya Ayubu: “Kisha alianguka katika nchi akasujudu na
kusema:‘Nilitoka katika
tumbo la mama nchi, na nitaondoka nchi.
BWANA alitoa na
BWANA ametwaa; Jina la Bwana na libarikiwe.” Ayubu 1:20-21 (NIV)
Mwambie
Mungu ukweli unavyohisi. Mimina moyo wako kwa Mungu. Tua
mzigo wa hisia zako ulizonazo. Ayubu alifanya hivyo aliposema, “Siwezi
kunyamaza! Nimekasirika na nina uchungu. Ni lazima niseme!” Ayubu 7:11 (TEV) Alilia Mungu alipoonekana kuwa mbali: “Ee,
kwa siku ambazo nilikuwa katika kufanikisha, wakati urafiki wa karibu na Mungu
ulibariki nymba yangu.”
Ayubu 29:4 (NIV) Mungu atachukuliana na mashaka yako, hasira, woga, huzuni,
kuchanganyikiwa, na maswali yako.
Je, ulijua kwamba kukiri kwa Mungu hali yako ya kukata tamaa
yaweza kuwa ni maneno ya Imani? Akiwa anamwamini lakini akisikia kukata tamaa,
Daudi aliandika, “Naamini, hivyo nilisema, ‘Nimeangamizwa kabisa’” Zaburi
116:10 (NCV) Hii inaonekana kama kupingana: Namwamini Mungu lakini nimefutiliwa
Mbali! Uwazi wa Daudi hakika anafunua Imani ya kina: Kwanza, alimwamini Mungu.
Pili aliamini Mungu angesikia sala yake. Tatu, aliamini Mungu angemruhusu aseme
alivyojisikia nabado aendelee kumpenda.
Anglia
zaidi Mungu ni nani – asili yake isiyobadilika. Pamoja
na mazingira na jinsi unavyojihisi ng’ang’ania tabia ya Mungu isiyobadilika.
Jikumbushe yale unayojua kuwa ni ya kweli milele kuhusu Mungu: Yeye ni
mwema,ananipenda, yuko pamoja nami, anajua yanayonipata, anajali, anao mpango
mzuri kwa maisha yangu. V. Raymond Edman alisema, “Usitilie mashaka unapokuwa
gizani yale Mungu aliyokuambia nuruni.”
Maisha ya Ayubu yalipoharibiwa, na Mungu alikuwa kimya Ayubu bado
alikuwa na vitu vya kumsifia Mungu:
l Kwamba ni mwema na wa upendo. Ayubu 10:12
l Kwamba ni mwenye nguvu zote. Ayubu 42:2; 37:5; 28
l Kwamba anajua kila kitu katika maisha. Ayubu 23:10; 31:4
l Kwamba anatawala kila kitu. Ayubu 34:13
l Kwamba ataniokoa. Ayubu 19:25
Mwamini
Mungu katika kutunza ahadi zake. Nyakati za
ukavu wa kiroho lazima uwe na subira katika kuzitengemea ahadi za Mungu, siyo
hisia zako, na uelewe kwamba anakupeleka katika kiwango cha kina cha kukua
kiroho. Urafiki unaotegemea hisia ni wa juu juu tu.
Hivyo usisumbuliwe na usumbufu. Mazingira hayawezi kubadili asili
ya Mungu. Neema ya Mungu bado ni timilifu; bado yuko upande wako, hata
unapokuwa huna hisia hiyo. Katika mazingira magumu, Ayubu alilishika neno la
Mungu. Alisema, “Sijayaacha maagizo ya kinywa chake;
nimeyatunza maneno ya kinywa chake kuliko mkate wangu wa kila siku.” Ayubu 23:12 (NIV)
Imani hii katika Neno la Mungu ilimfanya Ayubu kukaa mwaminifu
ingawa hakuna alilolielewa. Imani yake ilikuwa imara katikati ya maumivu: “Mungu
anaweza kuniua, lakini bado nitamwamini.” Ayubu 13:15 (CEV)
Unapohisi kuachwa na Mungu bado endelea kumwamini bila kujali
hisia hizo, mwabudu kwa kina zaidi.
Kumbuka
yale Mungu ameshakutendea. Kama Mungu hajakufanyia chochote
kamwe, bado anastahili sifa zako daima maisha yako yote kwa sababu ya
alichokifanya Yesu msalabani. Mwana wa Mungu alikufia! Hii
ni sababu kubwa ya kuabudu.
Unapohisi kuachwa
na Mungu bado endelea kumwamini, mwabudu kwa kina zaidi. |
Kisha, akiwa karibu kuzimia kwa sababu ya kupoteza damu nyingi,
alilazimishwa kubeba msalaba kwenda mlimani, alipigwa misumari juu yake, na aliachwa
afe pole pole, kifo cha mateso ya kusulubishwa. Damu yake ya uhai ilipomwagika,
watu wenye maudhi walisimama na kumtukana huku wakimpa changamoto ya kuhoji
uhusiano wake na Mungu.
Akisha Yesu kuchukua dhambi ya binadamu na hukumu yake, Mungu
alitazama pembeni mwa sehemu hiyo ovu, na Yesu alilia katika hali ya kulemewa
sana, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? “Yesu angeweza kujiokoa
mwenyewe –lakini asingekuwa amekuokoa.
Maneno hayatoshi kueleza giza la wakati huo. Kwa nini Mungu
aliruhusu na kuvumilia mateso maovu kiasi hicho. Kwa nini? Hii ni ili wewe
uweze kuokolewa na kuzimu ya milele! Biblia inasema, “Kristo
hakuwa na dhambi, lakini kwa ajili yetu Mungu alimfanya ashiriki dhambi yetu
ili kwamba katika kushirikiana naye tuweze kushiriki haki ya Mungu.” 2 Wakorintho. 5:21 (TEV)
Yesu aliacha vyote ili wewe upate vyote. Alikufa ili wewe uishi
milele. Jambo hilo tu linatosha kukufanya umshukuru na kumsifu daima.
Usijiulize kamwe jambo la kushukuru.
SIKU YA KUMI NNE KUFIKIRI JUU YA LENGO LANGU Jambo la Kutafakari: Mungu ni halisi, haijalishi ninahisi vipi. Kifungu cha Kukumbuka:“Kwa kuwa
Mungu amesema, ‘Sitakuacha kamwe, sitakupungukia kamwe.’” Waebrania
13:5 (TEV) Swali la Kujiuliza: Je, nawezaje kudumu katika kuutazamia
uwepo wa Mungu, hasa anapoonekana kuwa mbali? |
Siku ya Kumi na
Tano: Uliumbwa kwa Ajili Ya Jamii Ya Mungu
Mungu
ndiye aliyeumba vitu vyote, na vitu vyote ni kwa ajili ya utukufu wake.
Alitaka
watoto wake wengi washiriki utukufu wake.
Waebrania 2:10a (NCV)
Oneni
jinsi gani Mungu anavyotupenda sana, Kwa kuwa anaturuhusu
tuitwe
watoto wake, Na kweli ndivyo tulivyo!
1 Yohana 3:1 (NLT)
Ulimbwa kwa ajili ya jamii ya Mungu. Mungu anapenda jamii, na alikuumba
uwe sehemu ya hiyo jamii. Hili ni lengo la pili la Mungu kwa maisha yako,
alilolipanga kabla hujazaliwa. Biblia nzima ni hadithi ya Mungu akijenga jamii
ya watu watakaompendeza, kumheshimu, na kutawala naye milele. Imeandikawa, “Mpango
wake usiobadilika umekuwa siku zote ni kutufanya kuwa wa jamii yake kutuleta
kwake kwa kupitia Yesu Kristo. Na jambo hili lilimpa furaha kubwa.” Waefeso 1:5 (NLT)
Kwa sababu Mungu ni upendo, anathamini mahusiano. Asili yake ni
uhusiano, na anajitambulisha katika hali ya kijamaa: Baba, Mwana, na Roho.
Utatu ni uhusiano wa Mungu kwake mwenyewe. Ni kielelezo kikamilifu cha umoja
katika uhusiano, na ni lazima tujifunze kutokana na kielelezo hicho.
Mungu daima ameishi katika uhusiano wa upendo yeye mwenyewe, hivyo
hajawahi kuwa na upweke. Hakuhitaji jamaa-alitamani kuwa nayo, na
kutushirikisha vyote alivyo navyo. Hili humpa Mungu furaha. Biblia inasema, “Ilikuwa
ni siku ya furaha kwake alipotupa sisi maisha yetu mapya, kwa njia ya ukweli wa
Neno lake, na tukawa, kama alivyokuwa, wazaliwa wa kwanza katika jamaa yake
mpya.” Yakobo 1:18 (LB)
Tunapoweka imani yetu kwa Kristo, Mungu anakuwa Baba yetu,
tunakuwa watoto wake, waamini wengine wanakuwa kaka na dada zetu, na kanisa
linakuwa jamii yetu ya kiroho. Jamii ya Mungu ni pamoja na waamini wa siku
zilizopita, na wakati huu, na ule ujao.
Kila binadamu aliumbwa
na Mungu, lakini si kila mmoja ni mtoto
wa Mungu. Njia pekee ya kuingia katika jamii ya Mungu ni kwa kuzaliwa mara ya
pili. Unakuwa mmoja wa jamii ya kibinadamu kwa kuzaliwa kwa mara ya kwanza,
lakini unakuwa katika jamii ya Mungu kwa kuzaliwa mara ya pili. Mungu, “ametupatia
upendeleo wa kuzaliwa kwa mara ya pili, ili kwamba sasa tuwe watu wa jamii ya
Mungu.” 1 Petro 1:3 (LB); Rumi 8:15-16 (TEV)
Mwaliko wa kuingia katika jamii ya Mungu ni kwa watu wote. (Marko
8:34; Matendo 2:21; Rumi 10:13; 2 Petro 3:9.) Lakini kuwa sharti moja: Imani
katika Yesu. Biblia inasema, “Ninyi nyote ni watoto wa Mungu kwa
njia ya imani katika Kristo Yesu.” Wagalatia
3:26 (NLT)
Jamii yako ya kiroho ni bora zaidi kuliko ya kimwili kwa sababu
itadumu milele Jamii zetu duniani ni zawadi nzuri kutoka kwa Mungu, lakini ni
za muda mfupi na ni rahisi kuvunjika, mara nyingi zinavunjwa na talaka,
kutengwa na umbali, kuzeeka, na kifo. Kwa upande mwingine, jamii yetu ya
kiroho-uhusiano wetu kwa waamini wengine-utadumu milele. Ni uhusiano imara
zaidi, wa kudumu kuliko ule wa damu. Kila Paulo alipotulia na kutafakari juu ya
kusudi la Mungu kwetu sote alijikuta akibubujika katika sifa: “Ninapofikiri
juu ya hekima na upeo wake napiga magoti yangu na kumwomba Baba wa jamii yote
kubwa ya Mungu-wengine wao wako mbinguni tayari na wengine hapa dumiani,” Wafeso 3:14-15 (LB)
FAIDA ZA KUWA KATIKA JAMII YA MUNGU
Mara ulipozaliwa katika jamii ya kiroho, ulipewa zawadi bora za
siku ya kuzaliwa ambazo ni: jina la jamaa, uhusiano wa karibu kijamaa, na
urithi wa kijamaa!” (1 Yohana 3:1; Rumi 8:29; Wagalatia 4:6-7; Rumi 5:2; 1
Wakorintho 3:23; Waefeso 3:12; 1 Petro 1:3-5; Warumi 8:17.) Biblia inasema, “Kwa
kuwa wewe ni mototo wake, kila ulicho nacho ni mali yake.” Wagalatia 4:7b (NLT)
Jamii yako ya kiroho ni bora kuliko ya kimwili
kwa sababu itadumu milele.
Agano jipya hutoa mkazo mkubwa kuhusu “urithi” wetu mkubwa.
Hutuambia, “Mungu wangu atawatimizieni mahitaji yenu yote
kulingana na utajiri wa utukufu wake katika Kristo Yesu.” Wafilipi 4:19 (NIV) Kama watoto wa Mungu tunashiriki baraka za kijamii.
Hapa duniani tumepewe “utajiri … neema yake … wema … subira …
utukufu … hekima … nguvu … na rhema.”
(Waefeso 1:7; Warumi 2:4; 9:23; 11:33; Waefeso 3:16; 2:4.) Lakini katika maisha
ya milele tutapata zaidi ya hapo.
Paulo alisema, “Nataka mtambue utajiri na utukufu wa
urithi aliowapatia watu wake.” Waefeso 1:18b (NLT) Je, urithi
huo una nini? Kwanza, tutakuwa na Mungu milele. (1 Wathesalonike 5:10; 4:17)
Pili, tutabadilishwa kabisa na kuwa kama Kristo. (1 Yohana 3:2; 2 Wakorintho
3:18) Tatu, tutawekwa huru kutoka maumivu yote, kifo na mateso. (Ufunuo 21:4) Nne,
tutapewa zawadi na kutunukiwa nafasi za huduma. (Marko 9:4; 10:30; 1 Wakorintho
3:8; Waebrania 10:35; Mathayo 25:21, 23) Tano, tutashiriki katika utukufu wa
Kristo. (Warumi 8:17; Kolosai 3:4; 2 Wathesalonike 2:14; 2 Timotheo 2:12; 1
Petro 5:1) Ni urithi wa ajabu: Wewe ni tajiri mno kuliko unavyodhani.
Biblia inasema, “Mungu amewatunzia urithi wa thamani
watoto wake. Umetunzwa mbinguni kwa ajili yenu, safi usio na taka, hauwezi
kubadilika wala kuoza.” 1 Petro 1:4 (NLT) Hii ina maana
kuwa urithi wako wa milele hauna kipimo cha thamani, ni safi, wa kudumu, na
unalindwa. Hakuna mtu anayeweza kukuondolea; hauwezi kuharibiwa na vita, uchumi
mbovu, au majanga ya asili. Urithi huu wa milele, siyo mapumziko ya uzeeni,
ndicho kiwe kitu unachokitazamia na kukifanyia kazi. Paulo alisema, “Kila
mfanyalo, fanyeni kwa moyo wote, kama kumfanyia kazi Bwana, na siyo watu, kwa
kuwa mnajua kwamba mtapokea urithi kutoka kwa Bwana kama zawadi.” Wakolosai 3:23-24a (NIV) Mapumziko ya uzeeni ni lengo la muda
mfupi. Ni lazima uishi katika mtazamo wa milele.
UBATIZO: KUJULIKANA KATIKA JAMII YA MUNGU
Jamaa bora hujivunia jamaa zao; wanajamaa hiyo hawaoni aibu
kujulikana kama wanajamaa hiyo. Lakini, nimekutana na waamini wengine ambao hawajajitambulisha
hadharani kuwa ni wanajamaa wa jamii ya kiroho kama Yesu alivyoagiza-kwa
kubatizwa.
SIKU YA KUMI NA TANO: ULIUMBWA KWA AJILI YA JAMII
YA MUNGU |
Kwa miaka mingi nilishangaa kwanini Agizo Kuu la Yesu linatoa
umuhimu sawa Kati ya ubatizo na wajibu wa uinjilisti na mafundisho. Kwa nini
ubatizo ni wa muhimu? Kisha nikatambua kuwa ni sababu ni kielelezo cha lengo la
pili la Mungu kwa maisha yako: Kuwa mshirika katika jamii ya Mungu la milele.
Ubatizo una maana kubwa. Ubatizo wako ni tangazo la imani yako,
kushiriki kuzikwa na kufufuka kwa Kristo, huonyesha kufa kwa utu wako wa kale,
na hutangaza maisha yako mapya katika Kristo. Pia ni sherehe ya wewe kuingizwa
Katika jamii ya Mungu.
Ubatizo wako ni tangazo la nje la ukweli wa kiroho. Huwakilisha
kilichotokea pale Mungu alipokuingiza katika jamii yake: “Wengine
wetu ni Wayahudi, wengine Mataifa, baadhi ni watumwa, na wengine huru. Lakini
sisi sote tumebatizwa katika mwili wa Kristo kwa Roho mmoja, na wote tumempokea
Roho huyo mmoja.” 1 Wakrintho 12:13 (NLT)
Ubatizo haukufanyi mwanajamaa wa jamii ya Mungu. Imani katika
Kristo tu ndiyo hufanya kazi hiyo. Ubatizo huonyesha kuwa wewe ni mmoja wa jamii ya Mungu.
Kama pete ya harusi ni ukumbusho unaoonekana wa mkataba wa ndani
uliofanywa moyoni mwako. Ni tendo la kuingizwa hatua nyingine (initiation),
siyo kitu cha kufanya unapokuwa umekomaa kiroho. Sharti pekee la kibiblia ni
kwamba unaamini. (Matendo 2:41; 8:12-13, 35-38)
Katika Agano Jipya, watu walibatizwa mara tu walipoamini. Siku ya
Pentekoste, watu 3,000 walibatizwa siku ile ile walipompokea Kristo. Penginepo,
towashi wa Kushi alibatizwa pale pale alipoongoka; Paulo na Sila waliwabatiza
mlinzi wa gereza pamoja na jamaa jake usiku. Hakuna kuchelewesha ubatizo katika
Agano jipya. Kama hujabatizwa kama kielelezo cha imani yako katika Kristo. Fanya
hivyo haraka iwezekanavyo, Kama Kristo alivyoagiza.
UPENDELEO MKUBWA KATIKA MAISHA
Kuingizwa katika
jamii ya Mungu ni heshima ya hadi ya juu na upendeleo mkubwa sana unaoweza
kuupata |
SIKU YA KUMI NA TANO KUFIKIRI
JUU YA LENGO LANGU Jambo la Kutafakari: Niliumbwa kwa ajili ya jamii ya Mungu. Kifungu cha Kukumbuka: “Mpango wake usiobadilika umekuwa siku zote
ni kutufanya kuwa watu wa jamii yake kwa kutuleta kwake kupitia Yesu Kristo.” Waefeso 1:5a (NLT) Swali la kujiuliza: Je? Naweza kuanza kuwatendea waamini
wengine kama watu wa jamii yangu mwenyewe? |
Haijalishi
ninachosema, ninachoamini, na ninachofanya,
Mimi
sina kitu kabisa kama sina upendo
1 Wakorintho 13:36 (Msg)
Upendo
maana yake ni kuishi kama Mungu alivyotuagiza tuishi.
Kama
mlivyosikia tangu mwanzo, amri yake ni hii,
muishi
maisha ya upendo.
2 Yohana 1:6 (NCV)
Maisha yanahusu upendo.
Kwa sababu Mungu ni upendo, somo
la muhimu analotaka wewe ujifunze hapa duniani ni jinsi ya kupenda. Ni katika
kupenda ndiyo tunafanana naye, hivyo upendo ni msingi wa kila amri
aliyotupatia: “Sheria yote inaweza
kujumlishwa katika amri moja: Wapende wengine kama unavyojipenda mwenyewe.” Wagalatia 5:14 (LB)
Kujifunza kupenda pasipo ubinafsi
siyo kazi rahisi. Ni kinyume cha hali yetu ya ubinafsi. Ndiyo maana tunapewa
muda wa maisha yetu yote kujifunza kupenda. Bila shaka, Mungu anatutaka
tumpende kila mtu, lakini hasa anatutaka tujifunze kuwapenda watu wengine katika
jamii yake. Kama tulivyokwishakuona, hili ni lengo la pili la maisha yako.
Petro anatuambia, “Onyesheni upendo maalum kwa watu wa
Mungu.” 1 Petro 2:17b (CEV) Paulo pia anatoa maelezo ya namna hiyo: “Tunapokuwa
na nafasi ya kumsaidia mtu yeyote, tufanye. Lakini tuwape kipaumbele wale walio
wa jamii ya waaminio.” Wagalatia 6:10 (NCV)
SIKU YA KUMI NA SITA KITU CHA MUHIMU |
Mbinguni tutaifurahi jamii ya
Mungu milele, lakini tunayo kazi kubwa ya kufanya hapa duniani ili kujiandaa
kwa kutupatia “Wajibu wa kijamii,” na wajibu mkubwa ni kupendana.
Mungu anakutaka uwe katika
ushirika wa karibu na wa mara kwa mara na waamini wengine ili uweze kukuza
ujuzi wako katika kupenda. Lazima uwe karibu na watu-watu wanaoudhi, wasio
wakamilifu, na wa kuvunja moyo. Kwa kushirikiana tunajifunza kweli muhimu tatu.
MATUMIZI MAZURI YA MAISHA NI UPENDO
Upendo lazima uwe kitu cha kwanza,
lengo kuu, na tamanio lako kuu maishani. Upendo si kipengele kizuri katika
maisha yako, ni sehemu ya muhimu kuliko zote katika maisha. Biblia inasema, “Upendo
na uwe lengo lenu kuu.” 1 Wakorintho 14:1a (LB)
Haitoshi kusema, “moja ya vitu
ninavyotaka maishani ni kuwa na upendo,” kama vile ni kitu cha kwanza katika
orodha ya vitu kumi. Uhusiano upewe kipaumbele katika maisha yako kuliko vyote.
Kwa nini?
Maisha bila upendo hayana thamani.
Paulo anatoa hoja hii: “Haijalishi
ninachosema, ninachoamini, mimi sina kitu kabisa kama sina upendo.” 1 Korintho 13:3 (Msg)
Mara nyingi tunatenda kama vile
uhusiano ni kitu tunachoweza kukibana na kukiingiza kwenye ratiba zetu.
Tunaongea juu ya kutafuta
muda kwa ajili ya watoto wetu au kutenga
muda kwa ajili ya watu wetu. Hiyo huonyesha kwamba uhusiano ni sehemu ya maisha
yetu pamoja na shughuli nyinginezo. Lakini Mungu anasema uhusiano ndiyo maisha
yalivyo.
Amri nne kati ya amri kumi
zinahusu uhusiano wetu na Mungu na zile sita zinahusu uhusiano wetu na wetu.
Lakini zote kumi zinahusu uhusiano. Baadaye Yesu alijumlisha na kuonyesha
kilicho cha muhimu zaidi sana kwa Mungu katika kauli mbili. Mpende Mungu na
wapende watu. Alisema, “Ni lazima umpende Mungu kwa moyo wako
wote ..’ Hii ndiyo amri ya kwanza na kuu kuliko zote. Ya pili nayo ni muhimu
sawa na hiyo: Mpende jirani yako kama nafsi yako. Amri nyingine zote na maagizo
yote ya manabii yanategemea amri hizi mbili.”
Mathayo 22:37-40 (NLT) Baada ya kujifunza kumpenda Mungu (kuabudu), kujifunza
kuwapenda wengine ni lengo la pili kwa maisha yako.
Uhusiano si mafanikio ya mali,
ndiyo kitu cha muhimu zaidi maishani. Sasa kwa nini tunaruhusu uhusiano uchukue
sehemu ndogo maishani? Ratiba zetu zinapokuwa zimejaa kupita kiasi, tunaanza
kupitapita juutu mambo ya uhusiano, tunapunguza muda, nguvu na usikivu kwa
matarajio ya uhusiano yalivyotakiwa. Jambo ambalo ni muhimu zaidi kwa Mungu
linaloondolewa na jambo la dharura.
Shughuli nyingi ni adui mkubwa wa
uhusiano. Tunachukuliwa na kutafuta maisha, kufanya kazi zetu, kulipa madeni,
kutekeleza malengo kama vile shughuli hizi ndizo lengo kuu la maisha. La hasha!
Lengo la maisha ni kujifunza kupenda-Mungu na watu. Maisha yasiyo na upendo ni
bure.
Upendo utadumu milele.
Sababu nyingine Mungu anayotupa ili tufunye upendo kitu cha kwanza ni kwamba
upendo ni wa milele: “Mambo haya matatu yatadumu milele:
Imani, tumaini, na upendo. Na lililo kubwa kuliko yote ni upendo.” 1 Wakorintho
13:13 (NCV)
Upendo huacha kumbukumbu. Jinsi
unavyowatendea watu wengine, siyo utajiri au mafanikio yako ndicho kitu
kinachodumu unachoweza kuacha duniani. Kama Mama Teresa alivyosema, “Sivyo
unavyotenda, lakini kiasi gani cha upendo unaweka katika tendo hilo ndilo jambo
la muhimu sana.” Upendo ni siri ya urithi wa kudumu.
Nimekuwa kando ya kitanda cha watu
wengi wanaokuwa katika kufa, wanaposimama pembezoni mwa umilele, na sijiasikia
yeyote akisema, “Nileteeni vyeti vyangu! Nataka kuviona mara moja tena.
Nionyesheni zawadi zangu, medali zangu, ile saa ya dhahabu niliyopewa.” Maisha
yanapokoma duniani, watu hawajizungushii vitu. Tunachotaka kituzunguke ni
watu-watu tuwapendao na tulio na uhusiano nao.
Katika dakika zetu za mwisho wote
tunang’amua kwamba maisha ni uhusiano. Hekima ni kujifunza ule ukweli mapema na
siyo baadye. Usingoje mpaka utakapokuwa katika kitanda cha kifo ili ufahamu
kuwa hakuna chenye thamani zaidi.
Tutatathminiwa katika upendo wetu.
Sababu ya tatu ya kufanya kujifunza kupenda liwe lengo la maisha yako ni Kwamba
ndicho kigezo kitakachotumika kututathmini katika umilele. Njia moja wapo Mungu
hutumia kupima upevu wa kiroho ni ile thamani ya uhusiano wako. Mbinguni Mungu
hatasema, “Niambie kuhusu taaluma yako, akaunti yako ya benki, na mambo
uyapendayo,” Badala yake ataangalia ulivyowatenda watu wengine, hasa wale wenye
mahitaji. (Mathayo 25:40) Yesu alisema njia yaa kumpenda ni kupenda jamii yake
na kuangalia mahitaji yao ya kila siku: “Nawaambieni
ukweli, kama mlivyowatendea wadogo hawa walio watu wa jamii ya Mungu,
mlinitendea mimi.” Mathayo 25:34-46 (NRSV)
Maisha ni uhusiano. |
Tukijua hili, napendekeza kwamba
unapoamka kila asubuhi, piga magoti kando ya kitanda chako, au kaa juu yake, na
usali hivi: “Mungu, hata kama nitafanya chochote, nataka kuhakikisha kwamb
natumia muda kukupenda wewe na kuwapenda watu wengine – kwa sababu hayo nidiyo
maisha. Sitaki kupoteza siku hii.” Kwa nini Mungu akupe siku nyingine kama
utaipoteza?
UDHIHIRISHO MZURI WA UPENDO NI MUDA
Umuhimu wa vitu unaweza kupimwa
kwa kiasi cha muda tunaoutumia kwa vitu hivyo. Ukitumia muda mwingi kwa kitu fulani,
ndivyo anaonyesha umuhimu wa kitu hicho kwako. Ukitaka kujua mambo ya muhimu
kwa mtu, angalia tu jinsi wanavyotumia muda wao.
Mudaa ni zawadi ya thamani sana
kwa sababu una kiasi maalum tu cha muda. Unaweza kutengeneza pesa nyingi,
lakini huwezi kutengeneza muda zaidi. Unapompa mtu fulani muda wako unampa
sehemu ya maisha yako ambayo hutaipata tena. Muda wako ni maisha yako. Ndiyo
maana zawadi kuwa unayoweza kumpa mtu ni muda wako.
Zawadi kubwa unayoweza
kumpa mtu ni upendo wako. |
Kiini cha upendo siyo tunavyofikiri
au kufanya au kuwapa watu wengine, lakini ni kiasi gani tunajitoa sisi wenyewe.
Wanaume hasa hawalewi jambo hili mara nyingi. Wengi wao wameniambia, “Siwaelewi
mke wangu na watoto wangu, nawapatia kila kitu wanachotaka. Wanaahitaji nini
Zaidi?” Wanakuhitaji wewe! Macho yako, masikio yako, muda wako, usikivu wako,
uwepo wako, kujali kwako-mudaa wako. Hakuna kinachoweza kuziba pengo hilo.
Zawadi ya upendo inayotamaniwa na
wengi siyo almasi au maua, au chokoleti. Watu wanahitaji uskivu
usiogawanyika. Upendo unamjali mtu mwingine kwa
makini kiasi kwamba unajisahau mwenyewe kwa muda huo. Usikivu husema “ninakujali
wewe sana kiasi cha kukupa mali yangu ya thamani sana-muda wangu.“ Kila
unapotoa muda wako, unatoa sadaka, na sadaka ni kiini cha upendo. Yesu alitoa
kielelezo cha jambo hili. “Mjawe upendo kwa wengine, mkifuata
kielelezo cha Kristo aliyewapenda na akajitoa nafsi yake kwa Mungu kama sadaka
ili kuondoa dhambi zenu.” Wafeso 5:2 (LB)
Unaweza kutoa bila upendo, lakini
huwezi kupenda bila kutoa. “Mungu aliupenda ulimwengu sana hata
akamtoa …” (Yohana 3:16a) Upendo humaanisha kuachilia-kutoa nivpendavyo,
furaha, malengo, usalama, pesa nguvu, au muda kwa faida ya mtu mwingine.
WAKATI MZURI WA KUPENDA NI SASA
Wakati mwingine kuahirisha
kunakubalika hasa kwa mambo madogo madogo. Lakini kwa sababu upendo ndicho kitu
cha muhimu zaidi, unahitaji kupewa nafasi ya kwanza. Biblia hukazia jambo hili
mara nyingi, “Tunapokuwa na nafasi, tuwatendee mema watu
wote.” Wagalatia 6:10 (NLT) “Kila unapoweza,
watendee wema wale wanaouhitaji. Efeso 5:16
(NCV) Usimwambie jirani yako asubiri mpaka kesho
kama unaweza kuwasaidia sana.” Mithali 3:27 (TEV)
Kwa nini sasa ndiyo muda mwafaka
wa kuonyesha upendo? Kwa sababu hujui utakuwa na muda mpaka lini. Mazingira
hubadilika. Watu hufa. Watoto hukua. Huna dhamana ya kesho. Kama unataka
kuonyesha upendo, ni bora ufanye sasa.
Ukijua kwamba siku moja utasimama
mbele za Mungu, hapa kuna maswali unayopaswa kujiuliza: Je, utazielezeaje zile
nyakati ambazo miradi au vitu ndivyo vilikuwa vitu vya muhimu zaidi kuliko
watu? Nani ambaye unahitaji kuanza kutumia muda zaidi naye? Je, ni kitu gani
unahitaji kukiondoa katika ratiba yako ili uweze kutimiza haya? Je, unahitaji
kutoa sadaka gani?
Matumizi mazuri ya maisha ni
upendo. Udhihirisho wa upendo ni muda. Wakati mzuri wa kupenda ni sasa.
SIKU
YA KUMI NA SITA KUFIKIRI JUU YA LENGO LANGU Jambo la Kutafakari: Maisha ni kupenda. Kifungu cha Kukumbuka: “Shria
yote imejumlishwa katika amri moja; mpende jirani yako kama nafsi yako.” Wagalatia 5:14 (NIV) Swali la Kujiuliza: Kusema ukweli, je uhusiano naupa nafasi
ya kwanza? Je, nawezaji kuhakikisha kwamba nafanya hivyo? |
Ninyi mumekuwa watu wa jamii ya Mungu,
raia wa taifa la
Mungu nanyi ni watu wa nyumbani mwa
Mungu pamoja na kila Mkristo.
Waefeso 2:19b
Jamii ya Mungu ni kanisa la Mungu
aliye hai,
Nguzo ya msingi wa ile kweli.
1 Timotheo 3:15b (GWT)
Umeitwa kuwa mshiriki, siyo tu
kuamini.
Hata katika mazingira makamilifu
yasiyo na dhambi ya Edeni, Mungu alisema, “Si vyema mtu kuwa
peke yake.” (Mwanzo 2:18) Tumeumbwa kuwa katika jamii, tukatengenezwa kuwa
na ushirika, na tukaumbwa tuwe jamii, na hakuna mmoja wetu anayeweza kutimiza
malengo ya Mungu peke yake.
Bilia haielewi chochote juu ya
watakatifu wanaoishi peke yao au watu wa rohoni wanaojitenga kutoka waamini
wengine na kujinyima ushirika na wengine. Biblia inasema tumewekwa
pamoja, tumeungwa pamoja, tumejengwa pamoja, tu warithi pamoja, na tutanyakuliwa pamoja. (1 Wakorintho 12:12-13; Waefeso 2:21,22; 3:6; 4:16;
Kolosai4:17.) Huko peke yako tena.
Wakati uhusiano wako kwa Kristo ni
kati yako na yeye, Mungu hakukusudia uwe wa binafsi. Katika jamii ya Mungu
umeunganishwa na kila mwamini mwingine, na kila mtu ni sehemu ya mwingine milele. Biblia inasema, “Katika Kristo sisi ambao ni wengi
tumekuwa mwili mmoja, na kila mmoja ni sehemu ya wengine wote.” Warumi 12:5 (NIV)
Kumfuata Kristo ni pamoja na kuwa
mshirika, siyo tu kuamini. Sisi ni viungo vya mwili wake-yaani kanisa. C.S.
Lewis alisema kuwa neon ushirika
(membership) lina asili ya Ukristo, lakini ulimwengu umeliondolea maana yake ya
asili Masoko hutoa punguzo la bei kwa “washirika” wake, na watangazaji hutumia
jina la mwanachama kutengeneza orodha ya usafirishaji. Katika kanisa ushirika
ni kuandikisha jina lako au Bila masharti au wajibu.
Kwa Paul, Kuwa “mshirika” wa
kanisa alimaanisha kuwa kiungo cha mwili ulio hai, hiungo muhimu,
kilichoshikamana na viungo vingine katika mwili wa Kristo. (Warumi 12:4-5; 1
Wakorintho 6:15; 12:12-27.) Tunahitaji kurudia na kutenda sawasawa na maana ya
kibiblia ya “ushirika.” Kanisa ni mwili, siyo jengo, kiumbe na siyo chama.
Tunagundua wajibu wetu katika maisha kwa njia ya
uhusiano na wengine. |
Kama kiungo kimeondolewa kwenye
mwili wake, kitasinyaa na kufa. Hakiwezi kuishi peke yake, na hata wewe huwezi.
Ukiwa umetengwa na kukatwa toka kwenye damu ya uhai ya kanisa la mahali, maisha
yako ya kiroho yatanyauka na hatimaye yatakoma. (Waefeso 4:16) Ndiyo maana
dalili ya kwanza ya kuanguka kiroho mara nyingi nikutohudhuria mara kwa mara
katika ibada na mikusanyiko mingine ya waamini. Tunapoacha kujali kuhusu
ushirika, kila kitu kingine huanza kuteleza pia.
Ushirika katika jamii ya Mungu ni
jambo la muhimu si la kudharau. Kanisa ni mjadala wa Mungu kwa ulimwengu. Yesu
alisema, “Nitalijenga kanisa langu, na nguvu za kuzimu
hazitalishinda.” Mathayo 16:18 (NLT) Kanisa
haliharibiwi na litadumu milele. Litakuwepo hata baada ya ulimwengu huu, ndivyo
ilivyo hata kwa wajibu wako ndani yake. Mtu anayesema “Sihitaji
kanisa,” ni mwenye majivuno au haelewi. “Kristo
alilipenda kanisa na akatoa maisha yake kwa ajili yake.” Waefeso 5:25 (GWT)
Kanisa litakuwepo hata baada ya ulimwengu huu, ndivyo
ilivyo hata kwa wajibu wako ndani yake. |
USHIRIKA WAKO WA MAHALI
Mara nyingi kila neon kanisa linapotumika katika Biblia linamaanisha kusanyiko la mahali
linaloonekana, isipokuwa tu kwa matumizi machache sana, humaanisha waamini wote
katika historia. Agano Jipya linaonyesha kuwa kila mwamini ni mshirika wa
kanisa la mahali. Wakristo pekee ambao hawakuwa washiriki wa kanisa la mahali
ni wale waliokuwa kwenye marudio ya kanisa ambao wameondolewa kwa sababu ya
dhambi za hadharani. (1 Wakorintho 5:1-13; Wagalatia 6:1-5.)
Biblia husema Mkristo ambaye hana
kanisa la nyumbani ni kama kiungo kisicho na mwili, kondoo asiye na kundi, au
mtoto asiye na jamaa. Ni hali isiyo ya kawaida. Biblia inasema, “Ninyi
ni watu wa nyumbani mwa Mungu pamoja na kila Mkristo mwingine.” Waefeso 2:19b (LB)
Mila ya leo ya ubinafsi na
kujitegemea imesaababisha kuwepo yatima wa kiroho wengi- “Wakristo wa majina”
wanaozunguka kutoka kanisa moja hadi jingine bila utambulisho, kuwajibika, wala
kujitoa. Wengi huamini eti mtu anaweza kuwa “mwamini mzuri” bila kujiunga (au
hata kuhudhuria) katika kanisa la mahali; lakini Mungu hatakubaliana nao
kabisa. Biblia hutoa sababu nyingi za maana kuhusu kuwa mshirika mwaminifu na
hai katika kanisa la mahali.
KWA NINI UNAHITAJI JAMII YA KANISA
Jamii ya kanisa hukutambulisha kama mwamini halisi. Siwezi kudai kuwa mimi namfuata Kristo kama mimi si mmoja wa
kikundi maalum cha wafuasi wake. Yesu alisema, “Upendo wenu kati
yenu utathibitisha kwa ulimwengu kwamba ninyi ni wafuasi wangu.” Yohana 13:35 (NLT)
Tunapokutanika katika upendo kama jamii
ya kanisa kutoka mazingira tofauti, rangi, au daraja za kijamii tofauti, ni
ushuhuda mkubwa kwa ulimwengu. Wagalatia 3:28 (Msg); Yohana 17:21. Wewe si
mwili wa Kristo peke yako. 1 Wakorintho 12:27 (NCV)
Jamii ya kanisa hukuondoa kutoka upweke wa ubinafsi. Kanisa la mahali ni darasa la kujifunza jinsi ya kuendelea katika
jamii ya Mungu. Ni mahali pa kujizoeza kutokuwa na uchoyo,upendo wenye huruma.
Kama mshiriki mtendaji unajifunza kuwajali wengine na kushiriki katika mambo
yao: “Kama kiungo kimoja cha mwili kitaugua, viungo
vingine vyote huugua pamoja nacho. Au kama kiungo kimoja cha mwili wetu
kitatukuzwa, viungo vingine vyote hushiriki heshima hiyo.” 1 Wakorintho 12:26 (NCV) Kaika kushiriki na waamini kwa
kawaida, wasio wakamilifu, ndipo tunajifunza ushirika halisi na uzoefu wa
ukweli wa Agano Jipya wa kuwa katika mshikamano na kutengemeana mmoja kwa
mwingine. (Waefeso 4:16; Warumi 12:4-5; Wakolosai 2:19, 1 Wakorintho 12:25.)
Ushirika wa kibiblia ni sisi
kushikamana kama tunavyoshikamana na Kristo. Mungu anatutegemea kutoa maisha
yetu kwaa ajili ya wenzetu. Wakristo wengi wanaofahamu Yohana 3:16 hawafahamu 1
Yohana 3:16. “Yesus Kristo alitoa maisha yake kwa ajili yetu.
Imetupasa na sisi kutoa maisha yetu kwa ajili ya wengine.” 1 Yohana 3:16 (NIV) Huu ni mfano wa upendo wa jujitoa sadaka
ambao Mungu anatutaka tuwaonyeshe waamini wengine-kuwapenda kama Kristo
anavyokupenda.
Jamii ya kanisa hukusaidia kukomaa kiroho. Huwezi kamwe kukomaa kwa kuhudhuria ibada tu na kuwa mtazamaji. Ni
katika kushriki kikamilifu katika maisha ya kanisa la mahali ndipo utajengwa
kiroho. Biblia inasema, “Kama kila kiungo kinafanya kazi yake
maalum, husaidia viungo vingine kukua, kiasi kwamba mwili wote unakuwa na afya
na kukua, na kuwa na upendo tele.” Waefeso
4:16b (NLT)
Zaidi ya mara hamsini katika Agano
Jipya maneno “kati yenu” au “mmoja kwa mwenzake” yametumiwa. Tumeagizwa kupendana mmoja kwa mwenzake, kuombeana, kutiana moyo, kuonyana,
kusalimiana, kutumikiana, kufundishana, kupokeana, kuheshimiana, kubebeana
mizigo, kusameheana, kunyenyekeana, kujitoa
mmoja kwa mwenzake na kazi nyinginezo za kutendeana. Huu ndio ushirika wa
kanisa la mahali. Je, unafanya majukumu haya na nani?
Inaweza kuonekana rahisi kuwa
mtakatifu kunapokuwa hakuna mtu yeyote karibu wa kukuvuruga mambo yako, lakini
huu ni utakatifu usio wa kweli na ambao haujajaribiwa. Kujitenga huleta
udanganyifu, ni rahisi kujidanganya kuwa tumepevuka iwapo hakuna watu wa kutupa
changamoto. Upevu wa kweli huonekana katika uhusiano.
Tunahitaji Zaidi ya Biblia ili
tukue; tunahitaji waumini wengine. Tunakua haraka na wenye nguvu kwa kujifunza
kutoka kwa wenzetu na kuwajibika kwa kila mmoja wetu. Wengine wanaposhirikisha
yale Mungu anawafundisha tunajifunza na kukua pia.
Mwili wa Kristo unakuhitaji. Mungu
ana jukumu maalum kwa ajili yako ulifanye katika jamii yake. Hili huitwa “huduma”
yako, na Mungu amekupa vipawa kwa ajili ya jukumu hili: “Karama
ya kiroho imetolewa kwa kila mmoja wetu kama njia ya kulisaidia kanisa lote.” 1 Wakorintho 12:7 (NLT)
Kanisa lako la mahali ndipo Mungu
alipkuandalia wewe ili ugundue, uendeleze, na kutumia vipawaa vyako. Unaweza
pia kuwa na huduma pana, lakini hiyo ni nyongeza kwa huduma yako katika kanisa
la mahali. Yesu hakuahidi kujenga huduma yako, aliahidi kujenga kanisa lake.
Utashiriki katika huduma ya Mungu kwa ulimwengu. Yesu alitembea hapa duniani; Mungu alitembea kupitia mwili halisi wa Kristo. Kanisa ni chombo cha Mungu duniani. Hatupaswi
kuonyesha upendo wa Mungu kwa kupendana sisi tu, lakini tunatakiwa kuupeleka
pamoja kwa ulimwengu nzima. Huu ni upendeleo mkubwa tuliopewa kwa pamoja. Kama
viungo katika mwili wa Kristo, sisi ni mikono yake, miguu yake, na moyo wake.
Anafanya kazi ulimwenguni kupitia sisi. Sisi kila mmoja ana mchango wake wa
kutoa. Paulo anatuambia, “Anatuumba kila mmoja wetu kwa njia ya
Kristo ili kujiunga naye katika kazi anayoifanya, kazi njema aliyotuandalia
tuifanye, kazi ambayo yatupasa tuifanye.”
Waefeso 2:10 (Msg)
Yesu
hakuahidi kuijenga huduma yako; aliahidi kujenga kanisaa lake. |
Faida nyingine kama hiyo ya kanisa
la mahali ni kwamba hutoa ulinzi wa kiroho wa viongozi wacha Mungu. Mungu
anawapa viongozi wachungaji jukumu la kulinda, kutunza, kupigania, na kuangilia
maslahi ya kundi lake. (Matendo 20:28-29; 1 Petro 5:1-4; Waebrania 13:7, 17.)
Tunaambiwa, “Kazi yao ni kuangalia nafsi zenu na wanajua
kuwa watatoa hesabu kwa Mungu.” Waebrania 13:17 (NLT)
Shetani hupenda waamini
waliojitenga, waliojiondoa kwenye uhai wa mwili, waliojitenga na jamii ya
Mungu, na wasiotoa hesabu kwa viongozi wa kiroho, kwa kuwa anajua hao hawana
kinga wala nguvu dhidi ya mbinu zake.
YOTE YAKO KANISANI
Katika kitabu change, Kanisa
Linaloongozwa Na Malengo, nimeelezea jinsi ambavyo kuwa
sehemu ya kanisa imara ni muhimu kwa kuishi maisha ya ushindi. Natumaini utasoma
kitabu hicho pia, kwa sababu kitakusaidia kuelewa jinsi Mungu alivyolibuni
kanisa lake ili likusaidie kutimiza yale malengo matano aliyo nayo kwa ajili ya
maisha yako. Alilitengeneza kanisa kukidhi mahitaji yako matano ya kina: lengo
la kuishi, watu wa kuishi nao, kanuni za kuishi, ukiri wa kuishi, na nguvu za
kuishi. Hakuna sehemu nyingine yoyote duniani unakoweza kupata faida zote hizi
tano sehemu moja.
Malengo ya Mungu kwa kanisa lake
yanafanana na malengo yake matano kwako. Kuabudu hukusaidia kumtazama
Mungu, ushirika hukusaidia kukabili matatizo ya maisha; mafundisho hukusaidia kuimarisha imani
yako; huduma hukusaidia kupata vipawa vyako; uinjilisti hukusaidia kutimiza wito
wako. Hakuna kingine duniani kilicho kama kanisa.
UCHAGUZI WAKO
Kila mtoto anapozaliwa, mara moja
yeye huwa ni sehemu ya jamaa ya watu wote duniani. Lakini pia mtoto huyo
anahitaji kuwa mshirika wa jamaa maalum ili kupata malezi ili akue na kustawi.
Jambo hili ni la kweli hata kiroho. Ulipozaliwa mara ya pili, mara moja
ulijiunga na jamii ya Mungu ya waamini wote, lakini unahitaji pia mahali
utakaposhiriki kama jamii ya Mungu.
Tofauti ya kuwa mhudhuria kanisani
na mshirika wa kanisa ni kule kujitoa. Wahudhuriaji ni watazamaji kutoka
pembeni; washirika huhusika na huduma. Wahudhuriaji ni watumiaji tu, washirika
ni watoaji. Wahudhuriaji hutaka faida ya kanisa bila kushiriki majukumu. Hawa
ni kama watu wawili wanaotaka kuishi pamoja bila kujitoa kufunga ndoa.
Kwa nini ni muhimu sana kujunga na
jamii ya kanisa la mahali? Kwa sababu inathibitisha kwamba umejitoa
kushirikiana na ndugu na dada kikweli, sio kwa nadharia. Mungu anakutaka upende
watu halisi,
sio watu wa mawazoni tu. Unaweza kutumia muda wote wa maisha yako ukitafuta
kanisa kamilifu, Lakini hutalipata. Umeitwa kupenda watu wasio wakamilifu na
wakosaji, kama Mungu anavyowapenda.
Katika Matendo ya Mitume, Wakristo
walikuwa makini katika kujitoa mmoja kwa mwenzake. Walikuwa wamejitoa kwa
ushirika. Biblia inasema, “Walidumu katika mafundisho ya mitume,
maisha ya pamoja, kula pamoja, na kusali.”
Matendo 2:42 (Msg) Mungu anakutarajia udumu katika kufanya mambo kama hayo siku
hizi.
Maisha ya Kikristo ni Zaidi ya kujitoa kwa Kristo, ni pamoja na
kujitoa kushiriki na Wakristo wengine. Wakristo kule Makedonia walilijua jambo
hili. Paulo alisema, “Kwanza walijitoa nafsi zao kwa Bwana, kisha, kwa mapenzi ya Mungu,
na walijitoa kwetu pia.” 2 Kakorintho 8:5 (TEV) Kujiunga
na ushirika wa kanisa la mahali ni hatua inayofuata baada ya kuwa Mwana wa
Mungu. Unakuwa mshirika wa kanisa kwa kujitoa kushiriki katika kikundi maalum
cha waamini. Uamuzi wa kwanza huleta wokovu, uamuzi wa pili huleta ushirika.
SIKU YA
KUMI NA SABA KUFIKIRI
JUU YA LENGO LANGU Jambo la Kutafakari: Nimeitwa kuwa mshirika siyo kuamini tu. Kifungu cha Kukumbuka: “Katika Kristo
sisi tulio wengi tunafanya mwili mmoja, na kila kiungo ni sehemu ya viungo
vingine.” Warumi 12: 5 (NIV) Swali la kujiuliza: Je kuhusika kwangu katika kanisa langu la
nyumbani kunadhihirisha kwamba naipenda na kujitoa kwa ajili ya jamii ya Mungu? |
Kila
mmoja wenu ni sehemu ya mwili wa Kristo, na
Mlichaguliwa
ili muishi pamoja kwa amani.
Wakolosai 3:15 (CEV)
Ni
ajiabu, na inapendeza sana, kwa watu wa Mungu
Kuishi
pamoja kwa umoja!
Zaburi 133:1
Maisha ni kushirikiana.
Mungu anatukusudia tushirikiane katika maisha. Biblia huita hali
hii ya kushirikiana ushirika (fellowship). Siku hizi, lakini neno hili
limepoteza maana yake ya kibiblia. “Ushirika” mara nyingi sasa humaanisha
mazungumzo ya kawaida, mahusiano, chakula, na burudani Swali, “Je, unashiriki
wapi?” humaanisha “Unahudhuria kanisa gani?” “Kaa baada ya ushirika,”
humaanisha “subiri vinywaji.”
Ushirika halisi ni Zaidi ya kuonekana tu katika ibada. Ni kushiriki
maisha pamoja. Ni pamoja na upendo usio na
choyo, kushirikishana kwa uaminifu, kutumika, kutoa kwa moyo, kufariji kwa
kuhurumiana, na amri nyinginezo zote za Agano Jipya za “mmoja kwa mwingine.”
Inapokuja kuhusu ushirika, ukubwa wa kikundi ni muhimu: kikundi
kidogo ni bora zaidi. Unaweza kuabudu na kundi, lakini
huwezi kushirikiana nalo. Mara kundi linapokuwa kubwa kuliko watu wapatao kumi,
wengine huanza kutoshiriki-hasa mtu mkimya-na watu wachache tu hutawala
kikundi.
Yesu alihudumu katika mazingira ya kikundi kidogo cha wanafunzi.
Angeweza kuchagua wengi, lakini alijua kuwa kumi na mbili ni kiwango cha juu
cha watu katika kikundi kidogo iwapo kila mmoja atatakiwa kushiriki.
Mwili wa Kristo. Kama mwili wako, ni mkusanyiko wa chembechembe
nyingi. Uhai wa mwili wa Kristo, kama mwili wako, uko katika chembechembe. Kwa
sababu hii, kila Mkristo anatakiwa kushiriki katika kikundi kidogo kanisani
mwake, chaweza kuwa kikundi kidogo cha nyumbani, darasa la Jumapili, au kikundi
cha kujisomea Biblia. Hapa ndipo ushirika halisi kutokea, si katika mikusanyiko
mikubwa. Kama unalifikiri kanisa lenu kama meli, basi vile vikundi vidogo ni
kama zile meli za kuokoa zilizofungwa hapo.
Mungu amefanya ahadi kubwa kuhusu vikundi vidogo vya waamini: “Kwa
kuwa wawili au watatu wakikusanyika kwa jina langu, niko hapo katikati yao.” Mathayo 18:20 (NASB) Kwa bahati mbaya, hata kuwa katika kikundi
kidogo hakutuhakikishii kwamba utapata ushirika halisi. Madarasa mengi ya shule
za Jumapili na vikundi vidogo vimezama kwenye taratibu za kawaida na hawana
habari kabisa na ushirika halisi ni upi. Je, tofauti ni ipi kati ya ushirika
halisi na ule wa kuigiza?
Katika
ushirika wa kweli watu hupata uhalisi. Ushirika
halisi si wa kuigiza, mazungumzo ya juu juu tu. Ni wa kweli, wa kutoka moyoni,
wakati mwingine mazungumzo ya kina. Hii hutokea wakati watu wanapokuwa
waaminifu juu ya wao ni ndani na nini kinatokea maishani mwao. Hushirikishana
mambo yanayo waumiza, hufunua hisia zao, hukiri kushindwa kwao, hufunua mashaka
yao, hukiri hofu zao, hukubali udhaifu wao, na kuomba msaada na maombi.
Uhalisi ni kinyume cha unachokikuta katika baadhi ya makanisa.
Badala ya mazingira ya uaminifu na unyenyekevu, kuna kuigiza, kujionyesha,
kufanya siasa, na upole wa nje tu lakini mazungumzo duni. Watu huvaa kifuniko
cha uso, wakijilinda na kutenda kama vile kila kitu ni shwari maishani mwao.
Hali za namna hii ni kifo cha ushirika wa kweli.
Ushirika wa kweli hutokea wakati watu wanapokuwa Waaminifu juu ya wao ni nani na nini kinatokea maishani mwao. |
Kwa kweli, kuwa mkweli huhitaji ujasiri na unyenyekevu. Humaanisha
kukabili hofu zetu za kuwekwa wazi, kukataliwa na kuumizwa tena. Kwa nini mtu
yeyote ajihatarishe hivyo? Kwa sababu ndiyo njia pekee ya kukua kiroho na kuwa
na hisia nzuri. Biblia husema, “Fanyeni jambo hili daima: ungamianeni
dhambi ninyi kwa ninyi na kuombeana ili muishi pamoja kwa amani na kuponywa.” Yakobo 5:16a (Msg) Tunakuwa tu kwa kujihatarisha, na hatari
kubwa zaidi ni kule kuwa wakweli kwetu wenyewe na kwa wengine.
Katika
ushirika wa kweli watu hutegemeana.
Kutegemeana (mutuality) ni maisha ya kutoa na kupokea. Ni Kutegemeana. Biblia
husema, “Mungu alivyoibuni miili yetu ni kielelezo cha
kuelewa maisha yetu pamoja kama kanisa: kila kiungo hutegemea kila kiungo
kingine.” 1 Wakorintho 12:25 (Msg) Kutegemeana ni kiini cha ushirika:
kujenga uhusiano wa kutendeana, kushirkiana wajibu, na kusaidiana. Paulo
alisema, “Nataka tusaidiane kila mmoja na mwenzake kwa
imani tuliyo nayo. Imani yenu itanisaidia, na Imani yangu itawasaidia.” Warumi 1:12 (NCV)
Sisi sote Imani yetu huwa imara pale watu wengine wanatembea nasi
na kututia moyo. Biblia inahimiza kila mtu kuwajibika kwa mwenzake, kutiana
moyo, kutumikiana, na kuheshimiana. Warumi 12:10 (NRSV) Zaidi ya mara hamsini
katika Agano Jipya tumeagizwa “kututendeana.” Biblia husema, “Fanyeni
bidii katika yale yanayoleta amani ya kujengana ninyi kwa ninyi.” Warumi 14:19 (NIV)
Hauwajibiki kwa kila mtu katika mwili wa Kristo, lakini
unawajibika kwao. Mungu anakutarajia kufanya uwezavyo kuwasaidia.
Katika
ushirika wa kweli watu hupata huruma (sympathy).
Huruma siyo kutoa ushauri au msaada wa haraka; huruma ni kuzama ndani na
kushiriki maumivu ya wengine. Huruma husema, “Naelewa unachopata, na unavyojihisi
siyo wenda wazimu au wehu.” Siku hizi watu wengine huita “kumwelewa mtu”
(empathy), lakini Biblia hutumia neno “huruma” (sympathy). Biblia husema, “Kama
watu watakatifu … muwe na huruma, wema, wanyenyekevu, wapole na wavumilivu.” Wakolosai 3:12 (GWT)
Huruma husaidia mahitaji mawili makuu ya binadamu: hitaji la kueleweka
na hitaji la hisia za mtu kukubalika. Kila wakati unapoelewa na kukubali hisia
za mtu mwingine unajenga ushirika. Tatizo ni kwamba, mara nyingi tunaharaka ya
kushughulikia mambo na hatuna muda na watu. Au tumechukuliwa sana na matatizo
yetu. Kujihurumia binafsi huondoa huruma kwa watu wengine.
Kuna viwango tofauti vya ushirika, na kila kiwango kinafaa kwa
wakati wake. Viwango rahisi vya ushirika ni ushirika wa
kushirikishana na ushirika wa kujifunza neno
la Mungu pamoja. Kiwango cha kina ni kile cha ushirika wa
kutumika, kama tunapohudumu pamoja katika safari za umisheni au miradi ya
rehema. Kiwango cha kina kuliko zote ni ushirika wa mateso, (Wafilipi 3:10; Waebrania 10:33-34) ambapo tunaingia katika
maumivu na huzuni za mwenzetu na kubebeana mizigo. Wakristo wanaoelewa kiwango
hiki vyema ni wale walio katika nchi za mateso, wakidharauliwa na kuuwawa kwa
ajili ya Imani yao.
Biblia inaagiza, “Shirikianeni katika matatizo na shida
za kila mmoja wenu, na kwa njia hii mpate kuitii sharia ya Kristo.” Wagalatia 6:2 (NLT) Ni katika wakati wa matatizo mazito, msiba,
na mashaka ndipo tunahitajiana sana. Mazingira yanapotugandamiza kiasi kwamba Imani
yetu inadhoofika, ndipo tunapowahitaji sana marafiki waamini. Tunahitaji
vikundi vidogo kuwa na Imani kwa ajili yetu ili kututia nguvu za kuendelea.
Katika kikundi kidogo, mwili wa Kristo ni dhahiri hata kama Mungu anaonekana
kuwa mbali. Hiki ndicho Ayubu alikihitaji mno wakati wa mateso yake. Alilia, “Mtu
aliyevunjika moyo anahitaji faraja wa rafiki zake, hata kama ataiacha hofu ya
Mwenyezi Mungu.” Ayubu 6:14 (NIV)
Katika
ushirika wa kweli watu hupata rhema (mercy).
Ushirika ni sehemu ya neema, ambapo makosa hayatunzwi bali kuondolewa. Ushirika
hutokea pale rehema inashinda hukumu.
Sote tunahitaji rehema, kwa kuwa sote tunajikwaa na kuanguka na
kuhitaji msaada ili kurudi katika njia. Tunahitaji kurehemiana na kuwa tayari
kupokea kutoka kwa wenzetu. Mungu anasema, “Watu wanapotenda
dhambi, wasameheni na huwatia moyo, ili wasikate tamaa.” 2 Wakorintho 2:7 (CEV)
SIKU YA KUMI NA NANE: MAISHA YA PAMOJA |
Rehema ya Mungu kwetu ni kichocheo cha kuonyesha rehema kwa
wengine. Kumbuka hautaelezwa kumsamehe mtu mwingine saidi ya alivyokusamehe
Mungu.
Unapoumizwa na mtu fulani, unao uchaguzi wa kufanya: Je, nitatumia
nguvu na hisia zangu kulipa kisasi
au kusuluhisha?
Huwezi kufanya yote mawili.
Watu wengi husita kuonyesha rehema kwa sababu hawaelewi tofauti ya
imani na msamaha. Kusamahe ni kuyaacha yaliyopita. Imani inahusika na tabia ya
mbele.
Kusamehe lazima kufanywe mara moja, bila kujali kama mtu ameomba
msamaha huo au la. Imani inajengeka kwa muda kitambo. Imani inahitaji
ufuatiliaji mrefu. Kama mtu atakuumiza mara nyingi, umeagizwa na Mungu
kuwasamahe mara moja, lakini hutazamiwi kuwaamini mara moja. Wala hutemegewi
kuwaruhusu kuendelea kukuumiza. Ni lazima wathibitishe kuwa wamegeuka kadiri
muda unavyopita. Mahali mwafaka pa kurejeza imani ni katika mazingira ya
kikundi kidogo cha kutiana nguvu ambacho hutia moyo na kuwajibishana.
Kuna faida nyingine nyingi utakazozipata kwa kujiunga na kikundi
kidogo kilichojitoa kuwa na ushirika wa kweli. Ni sehemu ya muhimu ya maisha
yako ya Kikristo ambayo hutakiwi kuyapuuza. Kwa Zaidi ya miaka 2,000 Wakristo
wamekuwa wakikusanyika kwenye vikungi vidogo vidogo vya ushirika. Kama hujawahi
kuwa katika kikundi au darasa la namna hii, kwa kweli hujui unachokikosa.
Katika sura inayofuata tutaona ni nini kinatakiwa ili kuweza
kuunda jumuiya kama hii na waamini wengine, lakini natumaini sura hii
imekujengea hamu ya kupata uhalisi, kutegemeana, huruma, na rehema katika
ushirika wa kweli. Uliumbwa kwa ajili ya jamii.
SIKU YA
KUMI NA NANE KUFIKIRI
JUU YA LENGO LANGU Jambo la Kutafakari: Nawahitaji wengine maishani mwangu. Kifungu cha Kukumbuka: “Saidianeni
katika shida na matatizo, ili muitimize sharia ya Kristo.” Wagalatia 6:2 (NLT) Swali la Kujiuliza: Je, ni hatua gani moja ninayoweza
kuchukua leo ili kujenga uhusiano na mwamini mwingine katika hali ya kweli
kutoka moyoni? |
Siku ya Kumi na Tisa: Kukuza Jamii
Mnaweza
kujenga jamii yenye afya na yenye kustawi, ambayo inaishi sawa mbele za Mungu
na kufurahia matunda yake iwapo mtafanya bidii kuwa na amani kati yenu,
mkiheshimiana.
Yakobo 3:18 (Msg)
Walijitoa
kupokea mafundisho ya mitume, kuishi kwa pamoja, wakila pamoja, na kusali
pamoja.
Matendo 2:42 (Msg)
Ushirika wa jamii huhitaji kujitoa.
Ni Roho Mtakatifu peke yake anayeweza kujenga ushirika wa kweli
kati ya waamini lakini huukuza kwa kuzingatia uchaguzi wetu nakujitoa kwetu.
Paulo anautaja wajibu huu wa aina mbili kwa kusema, “Mumeungwa
pamoja kwa amani kwa njia ya Roho Mtakatifu, hivyo fanyeni bidii katika kudumu
pamoja.” Waefeso 4:3 (NCV) Inahitajika nguvu ya Mungu na bidii yetu ili
kupata jamii ya Kikristo yenye upendo.
Kwa bahati mbaya, watu wengi hukua katika jamaa zenye uhusiano
duni, hivyo wanakuwa hawana ujuzi wa mahusiano unaotakiwa kwa ajili ya ushirika
halisi. Ni lazima wafundishwe jinsi ya kuhusiana na wengine katika jamii ya Mungu.
Inapendeza kwamba, Agano Jipya limejaa maelekezo ya namna ya kushirikiana
pamoja kimaisha. Paulo aliandika, “Nakuandikia mambo haya … ili ujue
inavyopaswa kuishi katika jamii ya Mungu, jamii hiyo ni kanisa.” 1 Timotheo 3:14-15 (NCV)
Kama umechoka na ushirika usio halisi na ungependa kujenga
ushirika wa kweli na jamii yenye upendo katika kikundi chako kidogo, shule ya
Jumapili, na kanisa, utahitaji kufanya maamuzi magumu na kuchukua hatua.
Kujenga
ushirika wa jamii huhitaji uaminifu. Utahitaji
kuwa mtu mwenye kujali ili useme ukweli katika upendo, hata wakati ambapo ungekaa
kimya na kupuuzia jambo fulani. Ingawa ni rahisi kunyamaza wakati wengine
karibu yetu wanaumizana au wengine wanatenda dhambi, huu siyo upendo. Watu
wengi hawana mtu anayewapenda kiasi cha kuwaeleza ukweli (hata kama inaumiza),
hivyo wanadumu katika njia za kujiangamiza. Mara nyingi tunajua kile
kinachostahili kusemwa kwa mtu fulani, lakini woga wetu hutuzuia kusema
chochote. Ushirika mbalimbali umevunjika kwa sababu ya hofu: Hapa kuwa na mtu
yeyote wa kusema kitu wakati maisha ya mshirika fulani yalikuwa hatarini.
Biblia inatuambia, “Semeni ukweli katika upendo.” (Waefeso 4:15) Kwa sababu hatuwezi kuwa na ushirika wa kijamii
bila unyofu. Suleimani alisema, “Jibu la uaminifu ni ishara ya urafiki
wa kweli.” Mithali 24:26 (TEV) Wakati mwingine itamaanisha kuonyesha
upendo kwa kumwendea moja kwa moja ndugu anayetenda dhambi au anayejaribiwa
kutenda dhambi, “Ndugu zangu wa kiume na wa kike, kama
mmoja wenu katika kikundi akitenda kosa, ninyi mlio wa kiroho lazima mwende kwa
mtu huyo na kumsaidia kwa upole apate kurejea.”Wagalatia
6:1-2 (NCV)
Ushirika mwingi wa kanisa na vikundi vidogo vidogo hubaki wa juu
juu tu kwa sababu watu wanaogopa migogoro. Kila kunapotokea jambo ambalo
linaweza kusababisha machafuko, mara moja linafunikwa ili kutunza amani ya
uongo. Tatizo halitatuliwi na kila mmoja anaishi katika hali ya kukata tamaa.
Kila mtu anajua juu ya tatizo hilo, lakini hakuna anayelizungumzia wazi. Hali
hii huumba mazingira mabaya ambamo siri na usengenyaji hujikita. Suluhisho la
Paulo lilikuwa wazi. “Hakuna tena uongo. Hakuna tena kuigiza. Mwambie jirani
yako ukweli. Katika mwili wa Kristo sisi sote tumeunganishwa pamoja pia.
Unapowadanganya wengine unajidanganya mwenyewe.” Waefeso 4:25 (Msg)
Migongano inapotatuliwa ipasavyo, tunaendelea kuwa
karibu zaidi mmoja kwa mwingine. |
Uwazi siyo kibali cha kusema chochote unachotaka, popote na saa
yoyote. Siyo ujeuri. Biblia hutuambia kuna wakati mwafaka na njia sahihi ya
kufanya killa kitu. Mhubiri 8:6 (TEV) Maneno ya bila kufikiri huacha vidonda
vya kudumu. Mungu anatuagiza na kusema pamoja katika kanisa kama wanajamii
wenye upendo: “Usitumie maneno makali unapomrekebisha ndugu
alivye mzee, lakini sema naye kama baba yako: Ongea na vijana kama vile ni
ndugu zako, akina mama wazee kama vile mama zako, na wasichana kama vile dada
zako.” 1 Timotheo 5:1-2 (GWT)
La kusikitisha, vikundi maelfu vimeharibiwa kwa kukosa uaminifu.
Paulo aliwakemea kanisa la Korintho kwa ukimya wao kwa kuruhusu zinaa katika
ushirika wao. Kwa kuwa hapakuwepo mtu jasiri wa kukemea hali hiyo, Paulo
alisema, “Hampaswi kutazama pembeni na kufikiri mambo
yatakwisha yenyewe. Liwekeni wazi na mlishughulikie … Bora uharibifu na
kuudhika kuliko hukumu … Malipita tu kama jambo dogo, lakini ni jambo ambalo …
hampaswi kutenda kama vile kila kitu kiko sawa wakati Mkristo mwenzenu ni mwovu
au amepotoka, hajali Mungu au ni jeuri kwa wenzake, analewa au ni mchoyo, na
mnyang’anyi. Huwezi kuyakubali haya tu, kuyafanya ati kama ni tabia
zinazokubaliwa. Sihusiki na walio nje, lakini je, hatuna wajibu kwa wale wa
jamii ya waamini?” 1 Wakorintho 5:3-12 (Msg)
Kujenga
ushirika wa jamii huhitaji unyenyekevu.
Kujiona kwa muhimu na kujikinai, na kiburi huharibu ushirika haraka sana kuliko
chochote. Kiburi hujenga ukuta kati ya watu; unyenyekevu hujenga daraja.
Unyenyekevu ni mafuta yanayolainisha na kuvuta mahusiano. Ndiyo maana Biblia
inasema, “Jivikeni unyenyekevu katika kuhusiana kwenu.” 1 Petro 5:5 (NIV) Vazi sahihi kwa ajili ya ushirika ni moyo wa
unyenyekevu.
Sehemu iliyobaki ya kifungu hicho husema, “… kwa
sababu Mungu huwapinga wenye kiburi lakini huwapa wanyenyekevu neema.” 1 Petro 5:5c (NIV) Hii ni sababu nyingine ya sisi kuwa
wanyenyekevu: Kiburi huzuia neema ya Mungu maishani mwetu, ambayo tunaihitaji
ili tukue, tubadilike, tuweze kuponya na kusaidia wengine. Tunapokea neema ya
Mungu kwa kukiri kwa unyenyekevu kuwa tunaihitaji. Biblia inasema, wakati
wowote tukiwa na kiburi, tunaishi tukipingana na Mungu! Hayo ni maisha ya Kipumbavu na ya hatari.
Unyenyekevu siyo kufikiri haufai;
ni kufikiri juu ya nafsi yako
kidogo |
Unyenyekevu siyo kufikiri hufai, ni kufikiri juu ya nafsi yako
kidogo. Unyenyekevu ni kufikiri juu ya wengine Zaidi. Watu wanyenyekevu wana
mwelekeo mkubwa sana katika kuwatumikia wengine; hawajifikirii nafsi zao.
SIKU YA KUMI NA TISA: KUKUZA JAMII |
Katika Kila kanisa na katika kila kikundi kidogo, kuna walau mtu
mmoja “mgumu,” mara nyingi ni Zaidi ya mmoja. Watu hawaa wanaweza kuwa na
kitaji maalum la kihisia, hofu ya ndani, tabia ya kuudhi, au ujuzi duni wa
kijamii. Ni lazima uwaone kama watu Wanaohitaji Neema ya Ziada.
Mungu aliwaweka watu hawa katikati yetu kwa faida yao na yetu pia.
Hutupatia nafasi ya kukua na kupima ushirika: Je, tutawapenda kama kaka na dada
zetu na kuwapa heshima?
Katika jamaa, kukubaliwa hakutegemei usafi, uzuri, au vipawa vya
mtu. Hutegemea ukweli kwamba sisi sote ni wamoja. Tunaitetea na kuilinda jamaa.
Mmoja wa jamaa anaweza kuwa mpumbavu kidogo, lakini yeye bado ni mmoja wetu.
Vivyo hivyo, Biblia husema, “Shirikianeni ninyi kwa ninyi kama
jamii yenye upendo. Mzidi sana katika huheshimiana.”
Warumi 12:10 (GWT)
Ukweli ni kwamba, sisi sote tuna mapungufu na tabia za kuchukiza.
Lakini ushirika huhusiani na kuiana. Msingi wa ushirika ni uhusiano wetu kwa
Mungu: Sisi ni jamii.
Ufunguo wa adabu ni kuelewa watu wanatokea wapi, utaelewa Zaidi.
Badala ya kufikiri ni mwendo gani bado wanatakiwa kwenda, fikiri wametoka
umbali gani na maumivu yao.
Sehemu nyingine ya adabu ni kuepuka kupuuza hofu za wengine. Ikiwa
wewe huogopi kitu fulani, si kwamba hiyo ndiyo hisia sahihi. Watu huwa katika
ushirika wa kweli wanapojua kuwa kuna usalama wa kutosha kushirikisha wengine
mashaka na hofu zao bila kuhukumiwa.
Ushirikiano wa kanisa ni muhimu Zaidi kuliko mtu
yoyote binafsi. |
Mungu anachukia usengeyaji, na hasa inapowekwa kama “maombi” kwa
ajili ya mtu mwingine. Mungu anasema, “Usengenyaji
huenezwa na watu waovu; huchochea matatizo na kuvunja urafiki.” Mithali 16:28 (TEV) Usengenyaji mara nyingi husababisha
mavumivu na matengano, na huharibu ushirika, na Mungu yuko wazi kabisa kwamba
lazima tuwakemee wale waletao matengano kati ya Wakristo. Tito 3:10 (NIV)
Wanaweza kukasirika au kuondoka kwenye kikundi au kanisani kama utawakemea
tabia yao inayoleta mgawanyiko, lakini ushirika wa kanisa ni muhimu Zaidi kuliko
mtu yeyote binafsi.
Kujenga
jamii huhitaji kufanywa mara nyingi.
Ni lazima
kukutana na kundi lako mara kwa mara ili kujenga ushirika halisi. Mahusiano
huhitaji muda. Biblia inatuambia, “tusiache kukuktanika pamoja, kama wengine
wanavyofanya. Badala yake, tutiane moyo.” Waebrania 10:25 (TEV) Tunatakiwa
kujenga tabia ya kukutana pamoja. Tabia ni jambo unalofanywa mara kwa mara,
siyo kwa muda fulani. Unapaswa kutumia muda na watu-muda mwingi-kujenga
uhusiano wa kina. Ndiyo maana ushirika katika makanisa mengi ni duni, hatutumii
muda wa kutosha pamoja, na muda tunaotumia mara nyingi ni kumsikiliza mtu mmoja
akiongea.
Jamii haijengwi kwa wakati unaokubalika (“tutakusanyika
nikijisikia”), lakini katika kweli kwamba naihitaji kwa ajili ya afya yangu
kiroho. Kama unataka kujenga ushirika wa kweli, itamaanisha kukutana hata pale
unapokuwa hujisikii kufanya hivyo, kwa sababu unaamini ni muhimu. Wakristo wa
kwanza walikutana kila siku! “Waliabudu pamoja hekaluni kila siku,
wakakusanyika katika vikundi vidogo nyumbani kwa ajili ya ushirika, na
wakashirikiana vyakula vyao kwa furaha kubwa na shukrani.” Matendo 2:46 (LB) Ushirika huhitaji kuwekeza muda.
Kama wewe ni mshirika wa kikundi kidogo au darasa, nakushauri
kufanya agano la kikundi ambalo lina sifa tisa za ushirika wa kibiblia:
Tunashirikisha hisia zetu halisi (uhalisi), kutiana moyo (kutegemeana), kutiana
nguvu (kuhurumiana), kutiana moyo (kutegemeana), kutiana nguvu (kuhurumiana),
Kusameheana (rehema), kusema ukweli katika upendo (uaminifu), kukiri udhaifu wetu
(unyenyekevu), kuheshimu tofauti zetu (adabu), hapana kutetana (kutunza siri),
na kuweka kipaumbele kwa kikundi (kukutana mara kwa mara).
Tunapoangalia orodha ya sifa hizo, ni wazi kwa nini ushirika
halisi ni vigumu kuupata. Maana yake ni kuacha ubinafsi wetu na kujitegemea ili
tuweze kufikia hali ya kutegemeana. Kushirikiana kuna faida kubwa kuliko
gharama, na kunatuandaa kwa ajili ya mbinguni.
SIKU YA KUMI NA TISA KUFIKIRI JUU YA LENGO LANGU Jambo la kutafakari: Ushirika wa kijamii huhitaji kujitoa. Kifungu cha kukumbuka: “Tunaelewa upendo ni kitu gani
tunapofahamu kwamba Kristo alitoa maisha yake kwa ajili yetu. Hii maana
yake ni kwamba inatupasa kutoa maisha yetu kwa ajili ya waamini wengine.” 1
Yohana 3:16 (GWT) Swali la kujiuliza: Je, nawezaje kusaidia leto kujenga sifa za
ushirika wa jamii ulio halisi katika kundi langu dogo na kanisa? |
Siku ya Ishirini:
Kurejeza Uhusiano Uliovunjika
Mungu
amerejesha uhusiano wetu naye kwa njia ya Kristo,
na
ametupatia sisi huduma hii ya kurejesha mahusiano.
2 Wakorintho 5:18 (GWT)
Uhusiano unastahili kurejeshwa.
Kwa kuwa maisha ni juu ya kujifunza kupenda, Mungu anatutaka
tuthamini uhusiano na kufanya bidii kuutunza badala ya kuutupilia mbali mara
kunapokuwepo kupishana, maumivu, au migogoro. Kwa kweli, Biblia inatuambia
kwamba Mungu ametupatia huduma ya kurejeza uhusiano. 2 Wakorintho 5:18 (GWT)
Kwa sababu sehemu kubwa ya Agano Jipya inatufundisha jinsi ya kuishi pamoja.
Paulo aliandika. “Kama mumepata chochote kwa kumfuata
Kristo, kama upendo wake umefanya badiliko lolote, kama kuwa katika ushirika wa
Roho Mtakatifu kuna maana yoyote kwenu, … kubalianeni, pendaneni, iweni na
urafiki wa kutoka moyoni.” Wafilipi 2:1-2 (Msg) Paulo
alifundisha kwamba uwezo wetu wa kuishi vyemaa na wengine ni alama ya ukomavu
wetu kiroho. Warumi 15:5 (Msg)
Kwa kuwa Kristo anapenda kanisa lake lijulikane kwa upendo wake wa
ndugu, (Yohana 13:35) basi kuvunjika kwa uhusiano ni ushuhuda wa aibu kwa
wasioamini. Ndiyo maana Paulo alikuwa amedhuzunishwa kwa washirika wa kanisa la
Korintho kugawanyika katika vikundi vilivyopigana vita na hata kupelekana
mahakamani. Aliwaandikia, “Aibu kwenu! Kwa hakika hakuna walau
mtu mmoja mwenye hekima katika ushirika wenu anayeweza kumaliza mgogoro katik
ya Wakristo wenzake.” 1 Wakorintho 6:5 (TEV)
Alishangazwa kwamba hapakuwepo yeyote kanisani aliyekuwa amekomaa kiroho kuweza
kutatua mgogoro kwa amani. Katika barua hiyo hiyo, alisema, “Nitalifanya
kuwa ni jambo la dharura kama niwezavyo: Ni lazima mpatane.” 1 Wakorintho 1:10 (Msg)
Kama unataka baraka za Mungu kwa maisha yako na unataka kujulikana
kama mtoto wa Mungu, ni lazima ujifunze kuwa mpatanishi. Yesu alisema, “Mungu
huwabariki wale wanaotafuta amani, kwa kuwa wataitwa watoto wa Mungu.” Mathayo 5:9 (NLT) Angalia Kristo hakusema, “wamebarikiwa
wapenda amani,” kwa sababu kila mtu
hupenda amani. Wala hakusema “wamebarikiwa walio na amani,” wala wasiosumbuliwa
na chochote. Yesu alisema, “wamebarikiwa wale waitafutao amani” –wale wanaofanya bidii kutatua migogoro. Watafuta amani ni
wachache kwa sababu upatanishi ni kazi ngumu.
Kwa sababu uliumbwa ili uwe sehemu ya jamii ya Mungu na lengo la
pili la maisha yako hapa duniani ni kujifunza jinsi ya kupenda na kuhusiana na
wengine, upatanishi ni moja ya ujuzi unaotakiwa kujifunza. Kwa bahati mbaya,
wengi wetu hatukufundishwa namna ya kutatua migogoro.
Kutafuta amani siyo kuepuka mgogoro, kukimbia mgogoro, kujifanya hakuna tatizo au kuogopa kuliongelea
tatizo huo ni woga kwa hakika. Yesu, mfalme wa amani, hakuogopa kamwe migogoro.
Mara nyingine aliuchochea ukatokea kwa faida ya wote. Wakati mwingine
tunatakiwa kuepuka migogoro, wakati mwingine kuisababisha, na wakati mwingine
tunahitaji kuitatua. Ndiyo maana tunapaswa kuomba uongozi wa Roho Mtakatifu
daima.
Kuleta amani siyo kuktuliza hasira. Mara nyingi unakubaliana, unakuwa kama jamvi, na unawaruhusu
wengine wakukanyage sivyo alivyokusudia Yesu. Alikataa kuacha mambo kama
yalivyo, na akachukua msimamo mbele za upinzani wa waovu.
JINSI YA KUREJESHA UHUSIANO
SIKU YA ISHIRINI: KUREJEZA
UHUSIANO ULIOVUNJI KA |
Kusema
na Mungu kabla ya kusema na mtu. Jadili
tatizo na Mungu. Kama utaomba kwa ajili ya mgogoro huo kabla ya kusengenya na
rafiki, mara nyingi utagundua kwamba Mungu anabadili moyo wako au anambadili
yule mwingine bila msaada wako. Mahusiano yako yote yangekuwa shwari kama
ungeyaombea zaidi.
Kama Daudi alivyofanya na zaburi zake, tumia sala kupata uhusiano
wa juu na Mungu. Mwambie Mungu mashaka yako. Mlilie. Hashangazwi wala
kukatishwa tamaa na hasira yako, maumivu, hofu, au hisia nyingine zozote. Hivyo
mwambie ukweli wa unavyojihisi.
Migogoro mingi chanzo chake ni uhitaji. Baadhi ya mahitaji haya
yanaweza kutimizwa tu na Mungu. Unapomtazamia mtu yeyote-rafiki, mume au mke,
mkuu wa kazi, au mwanajamaa-kutimiza hitaji ambalo linaweza tu kutimizwa na
Mungu, unajiweka katika hili ya kuvunjika moyo na uchungu. Hakuna
mtu yeyote anayeweza kutimiza mahitaji yako yote isipokuwaa Mungu.
Mtume Yakobo alisema kuwa migogoro yetu mingi inatokana na maisha
ya kutokusali, “Nini kinasababisha vita na ugomvi kati yenu? …
mnataka kitu lakini hampati … hampati kwa sababu hamwombi Mungu.” Yakobo 4:1-2 (NIV) Badala ya kumtazama Mungu tunawatazama watu
ili tupate furaha na tunakasirika wanaposhindwa kutusaidia. Mungu anasemaa, “mbona
huji kwangu kwanza?”
Kila
ara chukua hatua za kwanza. Si kitu kama wewe ni mkosaji au
umekosewa: Mungu anakutazamia kuchukua hatua za kwanza. Usisubiri kwa ajili ya
upande ule mwingine waendee kwanza. Kurejeza uhusiano uliovunjika ni muhimu,
Yesu aliagiza kwamba jambo hili lifanywe hata kabla ya kukusanyika katika
kikundi cha kuabudu. Alisema, “Kama ukiingia sehemu ya kuabudu na,
unataka kutoa sadaka, ukakumbuka ghafla kwamba rafiki yako ana neno dhidi yako,
acha sadaka yako, ondoka mara moja, nenda kwa rafiki huyo na kuweka mambo sawa.
Hapo ndipo unaweza kuja na kumtolea Mungu.”1
Petro 3:7; Methali 28:9
Ushirika unaposongwa au kuvunjika, panga mkutano wa upatanisho
mara moja. Usiahirishe, usitoe sababu wala kuahidi “nitalishughulikia siku fulani.”
Andaa mkutano wa uso kwa uso haraka iwezekanavyo. Kuchelewa huongeza chuki na
kufanya mambo kuwa mabaya zaidi. Katika migogoro, muda hauponyi kitu, husababisha
maumivu kuongezeka.
Kuchukua hatua haraka pia hukupunguzia maumivu ya kiroho. Biblia
husema dhambi, pamoja na mgogoro ambao haujatatuliwa,” pia hutufanya tuwe na
huzuni. Marafiki wa Ayubu walimkumbusha, “Kuhofu kiasi cha
kufa ukijaa uchungu ni upumbavu na kitu kisicho ch busara” na “unajiumiza nafsi
yako kwa hasira.” Ayubu 5:2 (TEV); 18:4 (TEV)
Kufanikiwa kwa mkutano wa kutafuta amani hutegemea uchaguzi wa
wakati na mahali mwafaka katika kukutana. Msikutane mmoja wenu akiwa amechoka
au ana haraka au atapata usumbufu fulani. Muda mzuri ni ule ambao nyote mko
tayari.
Wahurumie
katika hisia zao. Tumia masikio yako zaidi kuliko
mdomo wako. Kabla ya kujaribu kutatua mgogoro wowote ni lazima kwanza usikilize
hisia za watu. Paulo alishauri, “Yatafuteni mambo yanayowapendeza
wenzenu, siyo tu mambo yenu.” Wafilipi 2:4 (TEV) Neno “yatafuteni”
ni neno la kiyunani skopos,
kutokana nalo tunapata neno teleskopu na
mikroskopu.
Ina maana ya kuweka uangalifu wa karibu sana! Ziangalie sana hisia zao, sio ule
ukweli. Anza na huruma sio suluhisho.
Usijaribu kuwasema watu kulingana na wanavyohisi kwanza. Wewe
sikiliza tu na wamimine hisia zao bila kuhisi kujilinda. Tikisa kichwa
kuonyesha kuwa unawaelewa hata kama hukubaliani nao. Hisia haziko sahihi au za
busara – mara nyingi Hakika, uchungu hutufanya tufikiri na kutenda kipumbavu.
Daudi alikiri, “Fikra zangu zilipojaa uchungu na hisia zangu
zikaumizwa, nilikuwa mpumbavu kama mnyama.”
Zaburi 73:21-22 (TEV) Sisi sote hutenda kinyama tunapokuwa tumeumizwa.
Kinyume na hapa Biblia husema, “Hekima ya mtu
humpa subira, ni utukufu kwake kutohesabu makosa.”
Mithali 19:11 (NIV) Subira hutokana na hekima, na hekima huja kwa kusikiliza
maoni ya wengine. Kusikia husema, “Najali maoni yako, najali uhusiano wetu, na
wewe ni wa muhimu kwangu.” Mesemo huu ni wa Kweli: Watu hawajali mambo
tunayojajua mpaka wajue kwamba tunajali.
Ili kurejeza ushirika “Ni lazima tubebe ‘mzigo’ wa kujali
mashaka na hofu za wengine … Na tumfurahishe mwenzetu, na siyo nafsi zetu, na
kufanya yanayomfaa.” Wafumi 15:2 (LB) Ni kujitoa sadaka kumeza kwa uvumilivu
hasira za watu wengine, hasa kama jambo hilo si la kweli. Kumbuka, hivi ndivyo
Yesu alivyokutendea. Alivumilia hasira ya uongo na uonevu ili akuokoe: “Kristo hakufuatisha hisia zake … kama
maandiko yasemavyo: matusi yao wakutukanayo yaliniangukia.” Warumi 15:3 (NJB)
Kiri
sehemu yako ya mgogoro. Kama unamaanisha kibisa kuhusu
kurejeza uhusiano, unatakiwa uanze na kukiri makosa yako au dhambi. Yesu
alisema ni njia ya kuona mambo dhahiri: “Kwanza toa boriti
ndani ya jicho lako; kisha labda utaona vyema kuondoa kibanzi kwenye jicho la
rafiki yako.” Mathayo 7:5 (NLT)
Kwa kuwa sote tuna maeneo ya giza maishani, utahitaji kuuliza mtu
wa tatu asaidie kutathmini matendo yako kabla ya kukutana na mtu uliye na
mgogoro naye. Pia mwombe Mungu akuonyeshe ni kiasi gani cha tatizo ni kosa
lako. Uliza, “Je, mimi ni tatizo? Je, mimi si mkweli, sijali, au najali sana?”
Biblia inasema, “Kama tutasema kwamba hatuna dhambi,
tunajidanganya tu wenyewe.” 1 Yohana 1:8 (Msg)
Toba ni chombo chenye nguvu katika kuleta upatanisho. Mara nyingi
namna tunavyoshughulikia mgogoro huleta maumivu makubwa kuliko hata lile tatizo
la kwanza. Unapoanza kwa kukiri kinyenyekevu makosa yako, hupunguza makali ya
hasira ya yule mwingine na huondoa nguvu ya mashambulizi kwa kuwa walitegemea
utajitetea. Usitoe udhuru wala kuhamishia lawama kwa wengine; kwa uaminifu
kubali makosa yako katika mgogoro huo. Kubali kuwajibika kwa makosa yako na
uombe msamaha.
Shambulia
tatizo na siyo mtu. Huwezi kutatua tatio kama
umekusudia tu kuondoa lawama. Ni lazima uchague kati ya hayo mawili. Biblia
inasema, “Jawabu la upole hutuliza hasira, lakini ulimi
mkali huwasha hasira.” Mithali 15:1 (Msg) Hutaweza
kupitisha jambo lako kwa kuwa na hasira, hivyo chagua maneno yako kwa busara.
Jibu laini mara nyingi ni bora kuliko jeuri.
Katika kusuluhisha migogoro, unavyosema ni muhimu kama ulichosema.
Ukikisema kwa kukasirisha, litapokelewa kwa kujilinda. Mungu anatuambia, “Mtu
mwenye hekima, mkomavu anajulikana kwa ufahamu wake. Kadiri maneno yake
yanavyopendeza, ndivyo anavyokuwa na ushawishi mkubwa.” Mithali 16:21 (TEV) Kulaumu hakusaidii. Huwezi kuwa na
ushawishi kama wewe ni jeuri.
Wakati wa Vita Baridi, pande zote mbili walikubaliana kwamba
baadhi ya silaha zilikuwa za maangamizi sana hivyo zisitumiwe kamwe. Leo silaha
za kikemia na kibaiolojia zilizopigwa marufuku, na maghala ya silaha za nyuklia
yanapunguzwa na kuangamizwa. Kwa ajili ya ushrikiano, lazima uangamize ghala
lako la silaha za uhusiano, ambazo ni lawama, dharau, kulinganisha, kuwapa watu
majina, kututana, ubwana, na kutoa maneno makali. Paulo anajumlisha yote
akisema, “Msitumie maneno yanayodhuru, lakini maneno
yenye kusaidia, yenye kujenga na kutoa kila kinachohitajika, ili kwamba kile
msemacho kiwajenge wanaosikia.” Efeso 4:29 (TEV)
Onyesha
ushirikiano ipasavyo. Paulo alisema, “Fanyeni
kila mwezalo kwa upande wenu ili kuishi kwa amani na watu wote.” Warumi 12:18 (TEV) Amani siku zote ina gharama. Wakati mwingine
hugharimu majivuno yetu. Kwa ajili ya ushirika, jitahidi kujirekebisha,
ukubalike na wengine, na uonyeshe kujali mahitaji yao. (Warumi 12:10; Wafilipi
2:3) Ufafanuzi wa heri ya saba ya Yesu husema, “Mumebarikiwa kama
mkiwaonyesha watu namna ya kushirikiana badala ya kushindana au kugombana.
Ndipo mnapogundua ninyi ni akina nani, na nafasi yenu katika ufalme wa Mungu.” Mathayo 5:9 (Msg)
Upatanisho hulenga uhusiano Wakati usuluhisihi hulenga tatizo |
Tunaweza kurejeza uhusiano hata kama hatuwezi kuondoa tofauti
zetu. Wakristo mara nyingi wana mambo ambayo wanatofautiana kwa halali na wana
maoni tofauti ya kweli, lakini tunaweza kutokukubaliana kimaoni bila kukataana
sisi wenyewe. Almasi moja huonekana tofauti toka pande tofauti tofauti. Mungu
anatarajia umoja, siyo kufanana, na tunaweza kutembea mkono kwa mkono bila
kuonana jicho kwa jicho kwa kila kitu.
Hii haina maana kwamba basi uache kutafuta suluhu. Mnaweza
kuendelea kujadili na kuwa na kongamano-lakini mnafanya hivyo katika roho ya
amani. Upatanisho maana yake unasemehe yaliyopita na si lazima lile jambo.
Je, ni nani unahitaji kumwona baada ya kusoma sura hii? Je, unahitaji
kurejeza uhusiano na nani? Usichelewe dakika nyingine. Tulia sasa na uzungumze
na Mungu kuhusu mtu huyo. Sasa chukua simu na anza kuchukua hatua. Hatua hizi
saba ni rahisi, lakini si nyepesi. Huhitajiki juhudi kubwa kerejeza uhusiano.
Ndiyo maana Petro alisihi, “Jitahidini kuishi kwa amani baina yenu.” 1 Petro 3:11 (NLT) Ndiyo maana Mungu anawaita wapatanishi kuwa
ni watoto wake. Mathayo 5:9
SIKU YA ISHIRINI KUFIKIRI
JUU YA LENGO LANGU Jambo la Kutafakari: Uhusiano ni wa muhimu kuurejeza. Kifungu cha Kukumbuka: “Fanyeni kila mwezalo kwa upande wenu ili
kuishi kwa amani na watu wote.” Warumi 12:18 (TEV) Swali la Kujiuliza: Je, ni nani ninahitaji kurejeza uhusiano
naye leo? |
Siku ya Ishirini
na Moja: Kuhifadhi Kanisa Lako
Mmeunganishwa
pamoja kwa amani kwa njia ya Roho Mtakatifu, hivyo
fanyeni
kila bidii ili kuendelea pamoja katika hali hiyo.
Waefeso 4:3 (NCV)
Zaidi
ya yote, upendo uongoze maisha yenu, kwa nijia hiyo kanisa lote
litakaa
pamoja katika amani kamilifu.
Wakolosai 3:14 (LB)
Ni kazi yako kuutunza umoja wa kanisa lako.
Umoja wa kanisa ni muhimu jambo kiasi kwamba Agano Jipya limelipa
mkazo zaidi kuliko hata mbingu au kuzimu. Mungu anapenda sana tuwe na umoja na
amani baina yetu.
Umoja ndiyo uhai wa ushirika. Ukiuharibu, umeondoa moyo kwenye
mwili wa Kristo. Ni Kiini, na asili ya jinsi Mungu anavyotukusudia tuwe na
maisha ya pamoja katika kanisa lake. Mfano mzuri kwetu wa umoja ni Utatu. Baba,
mwana, na Roho Mtakatifu wameunganika kikamilifu katika umoja. Mungu mwenyewe
ni kielelezo cha juu katika upendo wa kujitoa sadaka, kuwajali wengine kwa unyenyekevu,
na umoja mkamilifu.
Kama vile kila mzazi, Baba yetu wa mbinguni kufurahi akituona
watoto wake pamoja katika amani. Katika saa yake ya mwisho, kabla ya kukamatwa,
Yesu aliomba kwa moyo kwa ajili ya umoja wetu. (Yohana 17:20-23) Umoja wetu
ndio ulichukua nafasi kubwa katika mawazo yake muda ule alipokuwa katika kuugua
moyoni.
Hakuna kitu cha thamani duniani
kama kanisa lake. |
Kukazia
mambo yanayotuhusu wote na siyo tofauti zetu.
Paulo anatuambia, “Tuyaangalie mambo yaletayo amani, na yale
yanayoleta tabia njema kwa kila mtu.”
Warumi 14:19 (NIV) Kama waamini tunashiriki Bwana mmoja, mwili mmoja, ubatizo
mmoja, na upendo mmoja. (Warumi 10:12; 12:4-5; 1 Wakorintho 1:10; 8;6; 12:13; Waefeso
4:4; 5:5; Wafilipi 2:2.) Tunashiriki wokovu ule ule, maisha yale yale, na
hatima moja-mambo haya ni ya muhimu sana kuliko tofauti zozote tunazoweza
kuzitaja. Haya ndiyo mambo, siyo tofauti zetu binafsi, tunayoweze kuyajadili
zaidi.
Ni lazima tukumbuke kwamba ni Mungu aliyechagua kutupatia hali
tofauti, mazingira tofauti, rangi, na mambo tuyapendayo, hivyo yatupasa
kuthamini na kuzifurahia tofauti hizo, sio tu kuzivumilia. Mungu anapenda umoja
siyo kufanana. Lakini kwa ajili ya umoja tusiruhusu tofauti zitugawe. Ni sharti
tuyatazame zaidi mambo ya muhimu. Kujifunza kupendana kama Kristo alivyotupenda
na kutimiza malengo ya Mungu matano kwa maisha ya kila mmoja wetu na kanisa
lake.
Migogoro ni dalili ya kwamba tumeanza kuyaagalia mambo yasiyo
muhimu, Biblia huyaita mambo hayo “mambo yanayotatiza.” (Warumi 14:1; 2 Timotheo 2:23) Tunapokazania hulka za watu,
matakwa, tafsiri, mitindo, na njia, migawanyiko hutokea mara nyingi. Lakini tunapoelekeza
nguvu zetu katika kupendana na kutimiza malengo ya Mungu, amani hutokea. Paulo
alisihi kwa ajili ya jambo hili, “Kuweni na umoja wa kweli ili kusiwe na
mgawanyiko kanisani. Nawasihi muwe na nia moja, mkishikamana katika wazo na
lengo.” 1 Wakorintho 1:10 (NLT)
Kuwa
na matazamio halisi. Ukishagundua Mungu anavyotaka
ushirika halisi
uwe, ni rahisi kuvunjwa moyo na bonde lililopo kati ya matarajio
na hali halisi kanisani mwako. Lakini lazima
tulipende kanisa kwa moyo bila kujali mapungufu yake. Kutamani hali ya
matarajio huku ukilaumu hali halisi iliyopo ni ushahidi wa uchanga. Kwa upande
mwingine, kuridhika na hali halisi badala ya kutia bidii kufikia matarajio ni
kujikinai. Kukua ni kuishi katika mvutano.
Lazima
tulipende kanisa bila
kujali mapungufu yake. |
Watu huvunjwa moyo na kanisa kwa sababu nyingi zinazoeleweka.
Orodha yaweza kuwa ndefu: migogoro, maumivu, unafiki, kutokujali, kuonekana
kutofaa, sharia na dhambi nyingine. Badala ya kushangaa, lazima tukumbuke
kwamba kanisa lina watu wenye dhambi, ikiwa ni pamoja na sisi. Kwa sababu tu
wenye dhambi tumeumizana, kwa makusudi au bila kukusudia. Lakini badala ya
kuliacha kanisa, tunapaswa kukaa na kutafuta utatuzi. Upatanisho, siyo
kukimbia, ni njia ya kuelekea ukomavu wa tabia na ushirika wa kina.
Kuliacha kanisa lako kwa dalili ya kwanza ya kuvunjwa moyo ni
dalili ya uchanga. Mungu ana mambo anayotaka kukufundisha, na wengine pia.
Zaidi, hakuna kanisa kamilifu la kikimbilia. Kila kanisa lina mapungufu na matatizo
yake. Si muda mrefu utavunjwa moyo tena.
Groucho Marx alijulikana kwa kusema asingetaka kuwa kwenye chama
chochote ambacho kingemwingiza ndani. Kama kanisa litakuwa kamili
kukutosheleza, basi ukamilifu huo huo utakuondoa kwenye ushirika, kwa sababu
wewe si mkamilifu!
Dietrich Bonhoeffer, Mchungaji wa kijerumani aliyeuawa kwa kupinga
utawala wa Nazi, aliandika kitabu cha ushirika kinachopendwa kitwacho, Maisha
ya Pamoja. Ndani yake anapendekeza kwamba kuvunjwa moyo na kanisa letu la
mahali ni jambo zuri kwa sababu huharibu matarajio yetu potofu juu ya
ukamilikfu. Mara tunapoacha ndoto hiyo ya kuwa kanisa lazima liwe kamilifu ili
tulipende, ndipo tunaacha kuigiza na tunaanza kukiri kuwa sote si wakamilifu na
tunahitaji neema. Huu ndiyo mwanzo wa ushirika halisi wa kijamii.
Kila kanisa linaweza kuweka ilani ikisema Hakuna mtu yeyote
anahitaji kutuma maomlbi. Hapa ni pahali tu pa watu waliokiri kuwa wenye
dhambi, wahitaji neema, na wanaotaka kukua.
Bonhoeffer alisema, “Yeye apendaye ndoto yake ya jamii kuliko
jamii ya Kikristo yenyewe huwa mharibifu wa jamii ya Kikristo … Kama hatutoi
shukrani kila siku kwa ajili ya ushrika wa Kikristo tulimowekwa, hata kama
hakuna mambo makubwa, hakuna utajiri, lakini udhaifu mwingi, Imani mdogo, na
magumu, na kama badala yake tunadumu kulalamika kwamba kila kitu ni duni na
hakifai, basi tunamzuia Mungu kukukza ushikrika wetu.” ( Marumi 14:13; Yakabo
4:11; Waefeso 4:29; Mathayo 5:9; Yakobo 5:9)
Chagua
kutia moyo badala ya kulaumu. Ni rahisi
kusimama kando na kuwashambulia wanaotumika kuliko kuhusika na kutoa mchango
wako. Mungu anatuonya tena na tena tusilaumu, tusijilinganishe, wala
tusihukumiane. Warumi 14:4 (CEV) Kama utalaumu anachofanya Mkristo mwingine kwa
Imani na uthabiti wa moyo, unaingilia kazi ya Mungu. “Una
haki gani kumhukumu mtumishi wa mtu mwingine? Ni Bwana wake tu anayeweza kuamua
kama wanafanya vyema.” Warumi 14:10 (Ph)
Paulo anaongeza kwamba hatupaswi kuhukumu au kudharau waamini
wengine ambao wanaamini tofauti nasi. “Kwa nini basi,
unalaumu matendo ya ndugu yako, kwa nini unamdhalilisha? Sote tutahukumiwa siku moja, si kwa kutumia
vigezo vyetu, lakini kwa vigezo vya Kristo.”
Ufunuo 12:10
Ninapomhukumu mwamini mwingine, mambo manne hutokea mara moja:
napoteza ushirika na Mungu, nadhihirisha majivuno na hofu zangu, najiweka
kuhukumiwa na Mungu, na ninaathiri ushirika wa kanisa. Roho ya kuhukumu ni
jambo la hatari.
SIKU YA ISHIRINI NA MOJA: KUHIFADHI
KANISA LAKO |
Kataa
kusikiliza masengenyo. Kusengenya ni kusema habari ambao
haikuhusu wala huhusiki kusuluhisha. Unajua kueneza usenganyaji ni kosa, lakini
usiusikilize, iwapo unataka kulinda kanisa lako. Kusikiliza masengenyo ni kama
kupokea mali ya wizi, na inakufanya uhukumiwe kwa kosa lilelile.
Mtu anapoanza kusengenya kwako chukua ujasiri kumweleza, “Tafadhali
acha, sihitaji kujua hili. Je umemweleza mhusika moja kwa moja jambo hili?”
Watu wanaosengenya kwako watakusengenya pia. Hawaaminiki. Ukisikiliza
masengenyo, Mungu anasema, wewe ni mleta matatizo. Mithali 17:4 (CEV) “Wasumbufu
husikiliza wasumbufu wenzao.” Yuda 1:19 (Msg) “Hawa ndio
wanaogawa makanisa, wakijifikiri wenyewe tu.”
Wagalatia 5:15 (Amp)
Ni huzuni kwamba katika kundi la Mungu, majeraha makubwa mara
nyingi hutokana na kondoo wengine, sio mbwa mwitu. Paulo alionya juu ya
Wakristo “wala nyama”. “Wanaokulana” na kuharibu ushirika. Mithali 20:19 (NRSV) Biblia inasema watu
wa aina hii waepukwe. “Masengenyo hufunua siri, hivyo
usishirikiane na msengenyaji.” Mithali 26:20 (LB) Njia ya haraka
ya kukomesha mgogoro kanisani au katika kikundi kidogo ni kuwaonya wazi kwa
upendo wale wasengenyaji waache kabisa. Sulemani alisema, “Moto
huzimika kwa kukosa mafuta, na ugomvi hutoweka usengenyaji unapokoma.” Mathayo 18:15-17a (Msg)
Tumia
njia ya Mungu ya kutatua migogoro. Kwa
nyongeza ya kanuni zilizotajwa katika sura iliyopita, Yesu alilipa kanisa njia
rahisi yenye hatua tatu: “Kama mwamini mwenzako atakosea, nenda
kamwambie-malizeni kati yenu wawili. Akisikia, umempata rafiki yako. Asipokusikiliza,
wachukue ndugu wawili au watatu pamoja nawe ili kutunza ushahidi halali, na
ujaribu tena. Asiposikiliza tena liambie kanisa.”
(Mathayo 18:17; 1 Wakorintho 5:5)
Wakati wa mgogoro, ni rahisi kulalamika kwa mtu wa tatu badala ya
kusema kijasiri ukweli katika upendo kwa mtu aliyekuudhi. Hii hufanya tatizo
kuwa baya zaidi. Badala yake, mwendee moja kwa moja mtu anayehusika.
Kumwendea mtu binafsi ndiyo hatua ya kwanza, na lazima ufanye
hivyo haraka iwezekanavyo. Kama hamwezi kuyamaliza ninyi wawili, hatua ya pili
ni kuchukua ndugu mmoja au wawili wasaidie kuthibitisha tatizo na kupatanisha
uhusiano. Je, utafanya nini kama mtu huyo bado jeuri? Yesu alisema chukua
tatizo hilo kwa kanisa. Kama mtu huyo bado hataki kusikiliza baada ya hapo,
unamwona mtu huyo kama yule asiyeamini. Waebrania 13:17 (Msg)
Waunge
mkono mchungaji na wazee wa kanisa. Hakuna
viongozi wakamilifu, lakini Mungu huwapa viongozi majukumu na mamlaka ya kutunza
umoja wa kanisa.
Kunapokuwepo migogoro baina ya watu hiyo si kazi ya kufurahia.
Wachungaji huwa na kazi ngumu ya kuwa wapatanishi kati ya washirika walioumizwa
au walio kwenye mgogoro. Pia wanapewa jukumu gumu la kujaribu kufanya kila mtu
afurahi, kazi ambayo hata Yesu hakuifanya!
Tunalinda
ushirika wa kuwaheshimu wale wanao tutumikia kwa kuongoza. |
Wachungaji siku moja watasimama mbele za Mungu na kutoa hesabu ya
jinsi walivyowaangalia vizuri. “Wao huwaangalia kama watu watakaotoa
hesabu.” (2 Timotheo 2:14,23-26; Waf 10-11.) Lakini wewe pia utatoa
hesabu ya jinsi ulivyowafuata viongozi wako.
Biblia inawapa wachungaji maagizo maalum ya namna ya kufanya na
watu waletao matengano katika ushirika. Wanapaswa kuepuka mabishano,
kuwafundisha kwa upole wale wapinzani huku wakiwaombea wabadilike, kuwaonya
wabishi, kusihi kuwa na amani na umoja, kuwakemea wanaodharau uongozi, na
kuwaondoa waletao matengano kanisani kama wakidharau maonyo mawili. 1
Wathesalonike 5:12-13a (Msg)
Tunalinda ushirika kwa kuwaheshimu wale wanaotutumikia kwa
kuongoza. Wachungaji na wazee wanahitaji maombi yetu, kutiwa moyo, kuwashukuru
na kuwapenda. Tumeamriwa, “Waheshimuni wale viongozi wanaofanya
kwa bidii kwa ajili yenu, ambao wamepewa jukumu la kuwasihi na kuwaongoza katika
utii wenu. Washukuruni na kuwapenda!”
1 Wakorintho 10:24 (NLT)
Nakupa changamoto la kupokea wajibu wako wa kulinda na kukuza
umoja wa kanisa lako. Weka juhudi zote kwa jambo hili, na Mungu atafurahi.
Haitakuwa rahisi daima. Wakati mwingine utatakiwa kufanya lililo bora kwa mwili
wa Kristo, si kwako, kuonyesha kipaumbele kwa wengine. Hiyo ni sababu moja ya
Mungu kutuweka katika jamii ya kanisa – kujifunza kutokuwa na ubinafsi. Katika
jamii tunajifunza kusema “sisi” badala ya “mimi” na “yetu” badala ya “yangu.”
Mungu anasema, “Usifikirie manufaa yako tu. Fikiri juu ya
Wakristo wengine na kile kinachowafaa.”
Mungu hubariki makanisa yaliyo na umoja. Katika kanisa la Saddleback,
kila mshirika husaini mkataba ambao pia unaahadi ya kuhifadhi umoja wa ushirika
wtu. Matokeo yake, kanisa halijawahi kuwa na mgogoro wa kugawa ushirika wetu.
Ilivyo muhimu, kwa kuwa ni ushirika wenye umoja, na upendo, watu wengi wanapenda kuwa sehemu yake! Katika miaka saba iliyopita kanisa limebatiza
zaidi ya waamini wapya 9,100. Mungu anapokuwa na kundi la waamini wachanga
anaotaka wazaliwe, anatafuta kanisa lenye joto zuri.
Je, wewe unafanya nini ili kulifanya kanisa lako liwe jamii yenye
uchangamfu wa upendo? Kuna watu wengi katika jamii yenu wanaotafuta upendo na
mahali pa kuwa washirika. Ukweli ni kwamba, kila mmoja anapenda na anahitaji
kupendwa, na watu wanapopata kanisa ambapo washirika wake wanapendana na
kujaliana kikweli, utalazimika kufunga mlango ili wasije maana nafasi
haitatosha.
SIKU YA ISHIRINI NA MOJA KUFIKIRI JUU YA LENGO LANGU Jambo la Kutafakari: Ni wajibu wangu kuhifadhi umoja wa kanisa
langu. Kifungu cha kukumbuka: “Tuyaangalie
mambo yanayoleta amani na kukua kwa ushirika wetu kwa pamoja.” Warumi 14:19 (Ph) Swali la Kujiuliza: Je, sasa hivi mimi ninafanya nini ili
kulinda umoja katika jamii ya kanisa langu? |
沒有留言:
張貼留言