2024年7月3日 星期三

Maisha Yanayoongozwa Na Malengo (Siku Ya Moja kwa Kumi na Mbili)




Niko Duniani kwa Kusudi Gani?

Maisha yanayotegemea vitu ni maisha mfu, kama kisiki; maisha

yanayomtegemea Mungu ni mti unaostawi sana.

Mithali 11:28 (Msg)

Wamebarikiwa wanaomtumaini Bwana…

Ni kama miti iliyopandwa kandokando ya mto,

Yenye mizizi ifikayo chini kwenye maji. Miti kama hiyo

Haisumbuliwi na joto wala miezi ya ukame. Majani yake

Hukaa mabichi na hudumu kuzaa matunda mazuri.

Yeremia 17:7-8 (NLT)

Siku ya Kwanza

Yote Huanza Na Mungu

Kwa kila jambo, hakika kwa kila kitu, kiicho juu na kiicho

chini, kinachoonekana na kisichoonekana,….

Kila kitu kilianza katika yeye na hupata

Kusudi lake katika yeye.

Wakolosai 1:16 (Mag)

Bila kukubali kuwa kuna Mungu, swali kuhusu

Kusudi la maisha halina maana.

Bertrand Russel, mpagani asiyeamini kuwa kuna Mungu

Siyo kuhusu Wewe.

Kusudi la maisha yako liko juu Zaidi ya utoshelevu wako binafsi, Amani yako, au hata furaha yako. Ni kubwa Zaidi ya jamaa yako, kazi yako, hata kuliko ndoto na matazamio ya mbele uliyo nayo. Kama unataka kujua kwa nini uliwekwa hapa duiani, lazima uanze na Mungu. Ulizaliwa na kusudi lake na kwa kusudi lake.

Kutafuta maana ya maisha kumewatatiza watu wengi kwa maelfu ya miaka. Hivi ni kwa sababu tunaanza na mwanzo mbaya – sisi wenyewe. Tunauliza maswali ya ubinaafsi kama, Je, nataka kuwa nani? Je, nifanye nini na maisha yangu? Je malengo yangu ni yapi, matarajio yangu, na ndoto zangu kwa ajili ya siku zijazo? Lakini kule kutafuta majibu ya maswali haya kutoka ndani yetu hakutatudhihirishia kusudi la maisha yetu. Biblia husema, “Mungu ndiye huongoza maisha ya viumbe yake; maisha ya kila mtu yako katika uwezo wake. Ayubu 12:10 (TEV)

文字方塊: Kujiangalia sisi wenyewe
Hakutaweza kudhihirisha kusudi la maisha yetu.Tofauti na mafundisho ya vitabu vingi vya siku hizi, sinema, na semina huwezi kugundua kusudi la maisha yako kwa kujichunguza ndani yako. Labda umekwisha kujaribu hivyo. Hukujiumba mwenyewe, hivyo hakuna njia yoyote unaweza kujieleza kwa nini uliumbwa. Kama nikikupatia chombo kilichovumbuliwa na hujawahi kukiona kabla huwezi kujua kusudi lake, na hata chombo hicho chenyewe hakiwezi kukueleza.

Wakati fulani nilipotea mlimani. Niliposimama kuuliza njia iendayo kwenye kituo, nilielezwa, “Huwezi kufika huko kutokea hapa. Ni lazima uanzie upande mwingine wa mlima.” Vivyo hivyo, huwezi kufika kwenye kusudi la maisha yako kwa kuanzia kujitazama mwenyewe. Ni lazima uanze na Mungu, Muumba wako. Unaishi kwa sababu tu Mungu anapenda uishi. Wewe uliumbwa na Mungu – na kwa ajili ya Mungu – na mpaka ufahamu hivyo, maisha hayatakuwa na maana yoyote. Ni katika Mungu peke yake nidipo tunaweza kuvumbua asili yetu, utambullisho wetu, umuhimu wetu, kusudi letu, umaana wetu, na mwisho wa maisha yetu kwa ujumla. Njia nyingine yoyote hugonga ukuta.

Watu Wengi hujaribu kumtumikia Mungu katika kujithibitishia nafsi zao wenyewe, lakini hivyo ni kinyume cha asili na mwisho wake ni kushindwa. Uliumbwa kwa ajili ya Mungu, na siyo kinyume, na maana ya maisha ni kumruhusu Mungu, akutumie kwa malengo yake, siyo wewe umtumie Mungu kwa malengo yako. Biblia husema, “kuendekeza nafsi yako katika mambo haya, huleta mauti, lakini kumtazama Mungu hutuongoza mahali pa uwazi na maisha buru.” Warumi 8:6 (Msg)

Nimesoma vitabu vingi ambavyo hupendekeza njia za kugundua kusudi la maisha yangu. Vyote naweza kuviweka katika kundi la “jisaidie-mwenyewe” kwa sababu vinalishughulikia somo hili katika mtazamo wa ubinafsi (kujitazama mwenyewe). Vitabu vya jisaidie-mwenyewe, hata vile vya Kikristo, mara nyingi vinatoa hatua zile zile zinazoweza kutabirika katika kutafuta kusudi la maisha yako: Angalia ndoto zako. Changanua mambo unayoyathamini (values). Weka malengo. Tambua kipawa chako. Uwe na malengo ya juu. Shughulikia hayo. Jiweke wakfu. Amini unaweza kuyatimiza malengo yako. Wahusishe wengine. Usikate tamaa.

Kwa hakika, maelezo haya huleta mafanikio makubwa mara kwa mara. Mara nyingi utafanikiwa kufikia lengo lako unapoweka moyo wako hapo. Lakini kuwa na mafanikio na kutosheleza kusudi la maisha yako siyo kitu kimoja kabisa! Unaweza kufikia malengo yako yote binafsi, ukawa na mafanikio makubwa kwa jinsi ya viwango vya dunia hii, na bado ukakosa kusudi zima alilokuumbia Mungu. Unahitaji Zaidi ya ushauri wa jisaidie-mwenyewe. Biblia inasema, “kujisaidia mwenyewe si msaada kabisa. Kujitoa nafsi yako ndiyo njia, njia yangu, katika kuipata nafsi yako, nafsi yako halisi. Mathayo 16:25 (Msg)

Hiki siyo kitabu cha jisaidie-mwenyewe. Siyo kuhusu namna ya kupata kazi sahihi, kufanikiwa ndoto zako, au kupanga kuhusu maisha yako. Siyo kuhusu namna ya kuongeza shughuli katika ratiba yako iliyojaa. Hakika kitakufundisha namna ya kufanya mambo machache – kwa kuangalia mambo yaliyo ya muhimu zaidi. Kitabu hiki kinaeleza namna ya kuwa vile Mungu alivyokuumba uwe.

文字方塊: Uliumbwa na Mungu na kwa ajili ya Mangu – na mpaka utambue hivyomaisha hayatakuwa na maana yoyote.Sasa je, ni kwa jinsi gani unaweza kuvumbua kusudi uliloumbiwa? Una njia mbili tu. Njia ya kwanza ni kukisia. Hii ndiyo njia ambayo watu wengi huichagua. Hubahatisha, kukisia, wakaandika nadharia. Watu wnaposema, “Mara nyingi nimedhania maisha ni….,” wana maana kwamba “Hili ndilo kisio bora ninaloweza kulifanya.”

Kwa maelfu ya miaka, wanafalsafa wenye akili wamejadili kuhusu maana ya maisha. Falsafa ni somo muhimu na lina umuhimu wake; lakini habari ya kutambua kusudi la maisha, hata wanafalsafa wenye hekima kuu hubahatisha tu.

Dr. Hugh Moorhead, mwalimu wa falsafa katika Chua kikuu cha Northeastern Illinois, aliwaandikia wanafalsafa maarufu, wanasayansi, waandishi, na wenye akili ulimwenguni, wapatao 250, akawauliza swali, “Nini maana ya maisha?” Kisha alichapisha majibu hayo katika kitabu.Baadhi yao walitoa makisio yao bora, wengine walikubali Kwamba walijitengenezea lengo la maisha, na baadhi yao walikuwa waungwana wakakubali kuwa hawakufahamu chochote. Kwa hakika, baadhi ya watu hawa maarufu wenye akili walimwandikia Profesa Moorhead kuwaandikia tena na kuwaarifu kama alivumbua kusudi la maisha! (Chicago: Chicago review Press, 1988)

文字方塊: SIKU YA KWANZA
YOTE
HUANZI NA
MUNGUKwa bahati nzuri, kuna njia nyingine Zaidi ya ile ya kukisia kuhusu maana na kusudi la maisha. Njia hii ni ufunuo.

 Tunaweza kupata kile Mungu alichokifunua kuhusu maisha katika neno lake. Njia rahisi ya kugundua kusudi la chombo chochote kipya ni kuuliza aliyekitengeneza. Ukweli huu unawiana na kugundua kusudi la maisha yako: Muulize Mungu. Mungu hajatuacha tutangetange katika giza na kubahatisha. Amefunua wazi makusudi yake matano kwa ajili ya maisha yetu katika Biblia. Hiki ni kitabu cha maelezo kwetu, kutueleza kwa nini tuko hai, maisha huendaje, nini cha kuepuka, na kitu gani kitatokea hapo siku za usoni. Biblia hutuelezea mambo ambayo kitabu cha jisaidie-mwenyewe au falsafa hakiwezi kuyajua. Biblia husema, “Hekima ya Mungu… huenda ndani sana katika makusudi yake… siyo ujumbe mpya, lakini ni wa zamani – kile ambacho Mungu alikusudia kuwa njia ya kuleta mema ndani yetu.” 1Wakorintho 2L7 (Msg)

Mungu siyo tu mwanzo wa maisha yako, Yeye ni asili yake. Ili kugundua kusudi la maisha yako lazima ugeukie neno la Mungu, siyo hekima ya ulimwengu. Unapaswa kujenga maisha yako kwenye msingi wa kweli wa milele, siyo katika saikolojia, hamasa ya mafanikio, au hadithi za kuhamasisha. Biblia inasema, “Katika Kristo tunatambua sisi ni nani na tunaishi kwa ajili gani. Mwanzoni tulipokuwa hatujasikia habari za Kristo na kutupa matumaini, Yeye aliweka jicho laske kwetu, alikuwa na mipango juu yetu ya maisha ya utukufu, ambayo ni sehemu ya mpango uliokamilika anaotekeleza katika kila kitu na kila mtu.” Waefeso 1:11 (Msg) Kifungu hiki hutupatia utambuzi wa aina tatu kuhusu kusudi lake:

1.         Unavumbua wewe ni nani na kusudi lako kwa kuwa na uhusiano na Yesu Kristo. Kama huna uhusiano kama huo, baadaye nitaeleza namna ya kuuanzisha.

2.         Mungu alikuwa akifikiri juu yako tangu zamani kabla hujawaza chochote juu yake. Kusudi lake kwa maisha yako limekuwepo kabla ya kutungwa mimba yako. Alipanga kabla hujakuwepo, bila mchango wako! Unaweza kuchagua aina ya kazi, mwenzi wa ndoa, mambo uyapendayo na mengine mengi kuhusu maisha yako, lakini huchagua kusudi lako.

3.         Kusudi la maisha yako linawiana na kusudi kubwa la uumbaji wa Mungu ambalo Mungu ameliweka kwa umilele. Kitabu hiki kipo kwa ajili yako.

Andrei Bitov, mwandishi wa Kirusi wa vitabu vya hadithi, alikulia katika mazingira ya utawala wa Kikomunisti ambayo hayakubali kuwa kuna Mungu. Lakini Mungu alipata usikivu wa mtu huyu siku moja ya huzuni. Anakumbuka, “Katika mwaka wangu wa ishirini na saba, nilipokuwa katika treni linalopita chini ya ardhi katika mji wa Leningrad (sasa St. Petersburg) nililemewa na kukata tamaa kiasi kwamba maisha yalionekana kukoma mara moja, yakiwa bila matumaini yoyote ya mbele wala maana yoyote kabisa. Ghafla, bila mtu yeyote kuhusika, maneno haya yalionekana: Bila Mungu maisha hayana maana. Nikayarudia kwa mshangao, nilitoka katika treni huyo na kutembea katika nuru ya Mungu. (Boston: Little, Brown, 1991)

文字方塊: SIKU YA KWANZA: KUFIKIRI JUU YA MAISHA YANGU
Jambo la kutafakari: Siyo kuhusu mimi
Kifungu cha Kukumbuka: “Kila kitu kilianza katika Yeye na hupata kusudi lake katika Yeye.” Wakolosai 1:16 (Msg)
Swali la Kujiuliza: Pamoja na matangazo yote yanayonizunguka, je, nawezaje kujikumbusha kuwa maisha hakika ni kuishi kwa ajili ya Mungu?Unaweza kuwa umejisikia uko gizani kuhusu kusudi la maisha yako. Hongera, uko karibu kuingia nuruni.

 

 

 

 

 

Siku ya pili

Wewe Si Bahati Mbaya

Mimi ni Muumba wako. Ulikuwa katika uangalizi

Wangu hata kabla hujazaliwa

Isaya 44:2a (CEV)

Mungu hachezi bahati nasibu.

Albert Einstein

Wewe si bahati mbaya.

Kuzaliwa kwako hakukutrokana na makossa wala bahati mbaya, na maisha yako si matokeo ya bahati tu ya asili. Wazazi wako wanaweza kuwa hawakupanga kukuzaa lakini Mungu alipanga.Hajashangazwa hata kidogo na kuzaliwa kwako. Kwa kweli alitegemea uzaliwe.

Hapo zamani kabla hujatungwa mimba na wazazi wako, ulitungwa katika mawazo ya Mungu. Alikufikiri kwanza. Si jambo baya, wala bahati au tukio la bila kutegemewa kwamba wewe unapumua kwa wakati huu. Uko hai kwa sababu Mungu alitaka kukuumba! Biblia inasema. “Bwana atatimiza kusudi lake kwangu.” Zaburi 138:8

Mungu alitoa maagizo ya kila kipengele cha mwili wako. Kwa kusudi kabisa alichagua taifa lako, rangi ya ngozi na nywele zako na kila kiungo chako. Alilitengeneza umbile lako kama alivyopenda. Pia alikupangia vipawa vya kuzaliwa navyo na namna ya hulka yako binafsi. Biblia inasema, “Unanijua ndani nan je, unajua kila mfupa katika mwili wangu; unajua jinsi nilivyotengenezwa, kidgo kidogo, nilivyotokana na vitu visivyokuwepo nilikuwa mtu halisi.” Zaburi 139:15 (Msg)

Kwa kuwa Mungu alikuumba akiwa na sababu, pia aliamua ni lini uzaliwe na uishi kwa muda gani. Alipanga siku za maisha yako kabla, akachagua muda maalum wa kuzaliwa na kufa kwako. Biblia inasema, “Uliniona kabla sijazaliwa na ukapanga kila siku ya maisha yangu kabla sijaanza kupumua. Kila siku iliandikwa katika kitabu chako.” Zaburi 139:16 (LB)

Mungu pia alipanga wapi uzaliwe na wapi uishi kwa ajili ya kusudi lake. Rangi na utaifa wako si wa bahati mbaya. Mungu hakuacha kipengele chochote cha maisha yako kitokee kwa bahati. Alipanga yote kwa ajili ya kusudi lake. Biblia inasema, “Kutoka katika mtu mmoja alifanya kila taifa … na aliwapangia nyakati na mipaka ya makazi yao.” Matendo 17:26 (NIV) Hakuna chochote katika maisha yako kinachoamriwa tu. Kuna kusudi katika yote.

Cha kustaajabisha Zaidi, Mungu aliamua utakavyozaliwa. Bila kujali mazingira uliyozaliwa au wazazi wako ni nani, Mungu alikuwa na mpango alipokuumba. Haijalishi kama wazazi wako walikuwa wema au wabaya au wasiojali. Mungu alijua kwamba watu hao wawili walikuwa na viini sahihi vya uzazi kuweza kutengeneza kama wewe mwenye sura aliyokuwa nayo akilini mwake. Walikuwa na viini vya uzazi (DNA) Mungu alivyovitaka ili kukutengeneza wewe.

文字方塊: Hapo zamani kabla hujawa Katika tumbo la mama yako ulikuwa katika mawazo ya MunguIngawa kuna wazazi haramu, hakuna watoto haramu. Watoto wengi hawakuwa katika mpango wa wazazi wao lakini si kwamba hawakupangwa na Mungu. Kusudi la Mungu lilipitia katika kosa au hata dhambi ya watu.

Mungu kamwe hafanyi jambo lolote kwa kubahatisha na wala hafanyi makossa. Analo kusudi kwa kila anachokiumba. Kila mmea na kila mnyama alikusudiwa na Mungu, na kila mtu alibuniwa kwa malengo maalum. Nia ya Mungu kukuumba ilikuwa ni upendo wake. Biblia inasema, “Hapo zamani kabla Mungu hajaweka misingi ya ulimwengu alitujua, na kutuweka kuwa washiriki wakuu wa pendo lake.” Waefeso 1:4a (Msg)

Mungu alikuwa anakufikiri hata kabla hajiaumba ulimwengu. Bila shaka ndiyo maana aliuumba ulimwengu. Mungu alibuni mazingira ya sayari hii dunia, yafae kwa sisi kuishi. Sisi ndio kitovu cha mwelekeo wa upendo wake na wa thamani kuliko viumbe vyake vyote. Biblia inasema, “Mungu aliamua kutupa uzima kwa njia ya neno la kweli ili tuwe wa muhimu sana kuliko vitu vyote alivyoviumba.” Yakobo 1:18 (NCV) Hivi ndivyo Mungu anavyokupenda na kukuthamini.

Mungu habahatishi; alipanga kwa usahihi mkubwa. Kadri wanasayansi wanavyojifunza kuhusu ulimwengu, ndivyo tunatambua jinsi ulivyotengenezwa kwa namna ya pekee utufae kuishi; ukawekewa utaratibu na mipango halisi ambayo humwezesha binadamu kuishi.

Dr. Michael Denton mtaalam maarufu katika utafiti wa kibaiolojia (molecular genetics) katika chuo kikuu cha Otango huko New Zealand, amehitimisha akisema, “Ushahidi wote uliokwishapatikana katika sayansi za kibaiolojia unaunga mkono … kwamba ulimwengu umebuniwa kwa ujumla ukiwa na lengo na kusudi kuu la kuhifadhi uhai na binadamu, kila kitu kina maana na maelezo yanayolenga ukweli huu. (New York, Free Press, 1998) Biblia ilisema jambo hilo hilo maelfu ya miaka iliyopita. “Mungu aliumba nchi … Hakuiumba ikae ukiwa lakini aliiumba ikaliwe. Isaya 45:18 (GWT)

Kwa nini Mungu alifanya haya yote? Kwa nini alijisumbua kuumba ulimwengu kwa ajili yetu? Kwa sababu yeye ni Mungu wa upendo. Upendo wa namna hii ni vigumu kuufahamu, lakini ni wa hakika na wa kuaminika. Uliumbwa kama kiumbe maalum cha kupokea upendo wa Mungu! Mungu alikuumba ili akupende. Huu ni ukweli wa kuimarisha maisha yako.

Biblia hutuambia, “Mungu ni upendo.” (1 Yohana 4:8) Haisemi kuwa Mungu ana upendo. Yeye ni upendo! Upendo ndio kiini cha tabia ya Mungu. Kuna upendo 文字方塊: SIKU YA PILI:
WEWE 
SI BAHATI 
MBAYAmkamilifu katika ushirika wa Utatu wa Mungu, hivyo Mungu hakuhitaji akuumbe wewe. Hakuwa mpweke. Lakini alitaka kukuumba ili aonyeshe upendo wake. Mungu anasema, “Nimekushika mikononi tangu ulipozaliwa; nimekutunza tangu siku ile ulipozaliwa. Hata ukiwa mzee, mimi nitakuwa yule yule. Hata nywele zako zikigeuka na kuwa nyeupe, nitakutunza. Nilikuumba na nitakutunza. Isaya 46:3-4 (NCV)

Kama Mungu asingekuwepo, sisi sote tungekuwa tumetokea kwa bahati tu, matokeo ya mwendo wa viumbe vya angani. Ungeweza kuacha kusoma kitabu kiki kwa sababu maisha hayangekuwa na maana yoyote. Kusingekuwa na mema wala mabaya, wala matumaini baada ya miaka michache ya kuishi hapa duniani.

Lakini kuna Mungu aliyekuumba kwa kusudi, na maisha yako yana umuhimu mkubwa! Tunavumbua maana na kusudi hilo tunapomfanya Mungu kuwa kiini cha maisha yetu. Ujumbe wa Warumi 12:3 unasema, “Njia pekee sahihi ya sisi kujitambua ni kwa vile Mungu alivyo na kwa yale Mungu anayotutendea.”

Ushairi wa Russell Kelfer unatoa muhtasari wa ukweli huu:

Wewe ni wewe kwa kusudi.

Wewe ni sehemu ya mpango wa ajabu.

Wewe ni wa thamani na chombo maalum kikamilifu.

Unaitwa mtu mwanamume au mwanamke maalum wa Mungu.

Unaonekana kama unatafuta sababu.

Mungu wetu hakukosea.

Alikufinyanga vizuri tumboni,

Wewe uko vile alivyopenda kukuumba.

Wazazi ulionao ndio aliowachagua,

Na haijalishi unajisikiaje,

Waliumbwa kwa kusudi la Mungu,

Na wanao muhuri wa Bwana.

Hapana, ile taabu uliyoipata haikuwa rahisi.

Na Mungu alilia kwa kuwa ili kuufinyanga moyo wako.

Ili kwamba ukue katika sura yake.

Wewe ni wewe kwa kusudi,

Umetengenezwa kwa fimbo ya Bwana.

Wewe ni wewe, mpendwa,

Kwa sababu kuna Mungu! (Russell Kelfer, Kimetumiwa kwa ruhusa)

 

 


文字方塊: SIKU YA PILI: KUFIKIRI JUU YA MAISHA YANGU
Jambo la Kutafakari: “Mimi ni Muumba wako ulikuwa katika uangalizi wangu hata kabla hujazaliwa.” Isaya 44:2b (CEV)
Swali la Kujiuliza: Najua kwamba Mungu aliniumba kwa namna ya pekee. Je, ni maeneo gani ya hulka yangu, mazingira yangu, au sura yangu, au sura yangu ninahangaika kuyakubali?
 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


Siku ya Tatu: Je, Nini Huongoza Maisha Yako?

Nilichunguza na kuona kuwa nia kubwa ya mafanikio

ni ule msukumo wa husuda na wivu!

Mhubiri 4:4 ( LB)

Mtu asiye na lengo ni kama meli bila

usukani – mtu aliyepotea, mtu bure, kabwela.

Thomas Carlyle

Maisha ya kila mtu yanaongozwa na kitu fulani.

Kamusi nyingi hugaganua neno ongoza (drive) kama “Kuongoza, kutawala, kuelekeza.” Unapokuwa unaongoza gari, msumari, au mpira wa gofu, unachokifanya ni kuongoza, kutawala na kuelekeza kwa wakati hua. Je, ni nguvu gani inayoongoza maisha yako?

Sasa hivi unaweza kuongozwa na tatizo, msukumo fulani, au tarehe ya mwisho kwa kitu fulani. Unaweza kuongozwa na kumbukumbu ya jambo fulani linaloumiza, hofu mbaya, au Imani ya ndani. Kuna mamia ya hali mbalimbali, mambo muhimu, na hisia ambavyo vyaweza kukuongoza. Hapa kuna mambo matano ambayo ni ya kawaida kwa wengi.

Watu wengi huongozwa na hatia. Watu hawa hutumia muda wa maisha yote wakiepuka lawama na kuficha aibu. Watu wanaoongozwa na hatia wanaonewa sana na kumbukumbu. Wanaruhusu mambo yaliyopita kutawala mambo yao ya usoni.

Wanajiadhibu bila kujua kwa kuharibu mafanikio yao. Kaini alipotenda dhambi, hatia yake ilimtenga na Mungu, na Mungu akasema, “Utakuwa mtangatangaji asiyetulia katika nchi.” Mwanzo 4:12 (NIV) Hii inawaeleza jinsi watu wengi walivyo siku hizi – wanatagatanga katika maisha bila lengo.

Sisi ni matokeo ya muda uliopita lakini hatupaswi kuwa wafungwa wa muda hua. Kusudi la Mungu halifungwi na muda wako uliopita. Alimbadilisha muuaji Musa na kuwa kiongozi mzuri: akambadilisha Gidioni aliyekuwa mwoga akawa shujaa na hodari; anaweza kufanya mambo ya ajabu na maisha yako yaliyobaki. Mungu ni mtaalam wa kuwapa watu mwanzo mpya. Biblia inasema,”Wana furaha kubwa wale waliosamehewa hatia yao! ….. Wana Amani wale waliotuby dhambi zao na Mungu amefuta mashtaka yako.” Zaburi 32:1 (LB)

Watu wengi wanaongozwa na chuki na hasira. Wanashikilia maumivu (machungu) bila kuyaacha. Badala ya kutoka katika maumivu kwa kusamehe, wanaendelea kuyakumbuka katika mawazo yao tena na tena. Baadhi ya watu wanaoongozwa na chuki hutunza ndani uchungu wao, na wengine huwalipukia watu wengine. Hali zoe hizi si nzuri na hazisaidii maishani.

Chuki mara nyingi huleta maumivu kwako kuliko yule unayemchukia. Mtu aliyekukosea anaweza kuwa amesahau lile kosa na anaendelea na maisha yake vizuri, wewe unaendelea kuumia na kuhangaika na yaliyopita.

Sikiza: Wale waliokuumiza wakati uliopita hawawezi huendelea kufanya hivyo sasa isipokuwa kama utaendelea kutunza uchungu. Yaliyopita yamepita! Hakuna kitakachoyabadilisha. Unajiumiza tu na uchungu wako. Kwa ajili yako, jifunze kutokana na hilo na kisha achana nalo. Biblia inasema, “Kuwa na hofu kiasi cha kufa kwa sababu ya uchungu ni upumbavu, ni kitu cha kipumbavu kukifanya.” Ayubu 5:2 (TEV).

Watu wengi wanaongozwa na woga. Woga wao unaweza kutokana na jambo baya sana lililowapata, matarajio yasiyotekelezeka, kukulia katika jamaa isiyo na uhuru, au hata maumbile ya asili. Bila kujali sababu, watu wanaoongozwa na woga mara nyingi hupitwa na nafasi kubwa kwa sababu wanaogopa kuchukua hatua. Badala yake wanajitahidi kuwa salama, wakiepuka kupata hasara na hivyo hujaribu kulinda hadhi yao.

Woga ni kifungo ambacho mtu hujifunga mwenyewe na chaweza kukuzuia kuwa mtu yule ambaye Mungu anapenda uwe. Unatakiwa kutoka humo kwa silaha ya Imani na upendo. Biblia inasema, “Upendo halisi huiondoa hofu kwa kuwa hofu hulemaza, maisha ya hofu – hofu ya kifo, hofu ya hukumu – ni maisha ambayo hayajakamilika katika upendo.” 1 Yohana 4:18 (Msg)

Watu wengi wanaongozwa na mali. Tamaa yao ya kupata vitu linakuwa ndilo lengo la maisha yao yote. Msukumo huu wa kutaka Zaidi kila siku una misingi yako katika udanganyifu wa kuwa nikiwa na vingi nitakuwa na furaha Zaidi, nitakuwa wa muhimu, na nitakuwa salama; lakini mawazo yote haya matatu si ya kweli. Mali huleta furaha ya muda mfupi. Kwa kuwa vitu havibadiliki, hivyo vinatuchosha na tunataka vipya, vikubwa, na bora Zaidi.

Kuna Imani pia kwamba kama nitapata mali nyingi nitakuwa wa muhimu. Umuhimu wako na umuhimu unaotegemea ulivyo navyo ni vitu viwili tofauti. Thamani yako haitegemei mali zako, Mungu anasema kitu cha muhimu maishani mwako si vitu!

文字方塊: Hakuna kitu cha muhimu
Kama kuja makusudi ya 
Mungu kwa maisha yako, na hakuna badala yake.Imani ya watu wengi kuhusu fedha ni kwamba kuwa nazo nyingi kutanipa usalama. Haziwezi. Utajiri unaweza kupotezwa mara moja kwa sababu zisizozuilika. Usalama halisi unaweza kupatikana katika kile ambacho huwezi kunyang’anywa yaaani uhusiano wako na Mungu.

Watu wengi wanaongozwa na kutaka sifa. Wanaruhusu matarajio ya wazazi, waume au wake, watoto, waalimu au rafiki zao kutawala maisha yao. Watu wazima wengi bado wanajaribu kupata sfa kwa wazazi wao ambao hawajafurahi kamwe. Wengine wanasukumwa na vikundi vya marafiki, wanahofu wenzao watawafikiriaje. Kwa bahati mbaya, wale wafuatao kundi hupotelea ndani yake.

Sijui funguo zote za mafanikio, lakini ufunguo mmoja wa kushindwa ni kujaribu kumpendeza kila mtu. Kutawaliwa na maoni ya watu wengine ni nijia wazi ya kukosa makusudi ya Mungu katika maisha yako. Yesu alisema, “Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili.” Mathayo 6:24 (NLT)

Kuna nguvu nyingine zinazoweza kuongoza maisha yako lakini zote mwisho wako ni mfu: kutotumia vipawa ulivyo navyo, mahangaiko ya moyo, na maisha yasiyo ya utoshelevu.

Safari hii siku 40 itakuonyesha jinsi ya kuishi maisha yanayoongozwa na malengo – maisha yanaoongozwa, kutawaliwa , na kuelekezwa na makusudi ya Mungu. Hakuna kitu cha muhimu Zaidi kama kujua malengo ya Mungu kwa maisha yako, na hakuna mbadala kwa hilo – siyo mafanikio, utajiri, kujulikana, au anasa. Bila malengo, maisha ni mwendo usio na maana, shughuli bila mwelekeo, na matukio bila sababu. Bila malengo, Maisha ni kitu duni, kidogo sana, kisicho na umuhimu wowote.

FAIDA ZA KUISHI KWA MALENGO

Kuna faida kuu tano za kuishi misha yenye kuongozwa na malengo:

Kujua lengo lako hukupa maana ya maisha yako. Tuliumbwa tuwe na maana. Ndio maana watu hujaribu njia za udanganyifu kama unajimu na mazingaombwe ili kuigundua. Maisha yanapokuwa na maana unaweza kuchukuliana na chochote; bila hiyo hakuna kinachobebeka.

Kijana mmoja katika umri wa miaka 20 hivi aliandika, “najisikia kama mtu aliyeshindwa kwa sababu najaribu kuwa kitu fulani, na hata sijui kitu hicho ni nini. Ninachojua ni kuendelea tu. Siku fulani kama nitagundua lengo langu, nitajisikia sasa naanza kuishi.

文字方塊: Siku ya Tatu:
NINI HUONGOZA MAISHA YAKO?Bila Mungu maisha hayana lengo, na bila lengo maisha hayana maana. Bila maana maisha hayana umuhimu wala thamani au matumaini. Katika Biblia, watu wengi walionyesha hali hii ya kukosa matumaini. Isaya alinung’unika akisema. “Nimefanya kazi bila malengo; nimetumia nguvu zangu bure kabisa.” Isaya 49:4 (NIV) Ayubu alisema, “Maisha yangu yamejikongoja – siku baada ya siku bila matumaini.” Ayubu 7:6 (LB) na “Nakata tamaa; nimechoka na kuishi. Niacheni. Maisha yangu hayana maana yoyote. Ayubu 7:16 (TEV) Jambo baya kuliko yote siyo kifo, lakini maisha yasiyo na malengo.

Kuwa na tumaini ni muhimu kwa maisha yako kama vile hewa na maji. Unahitaji tumaini ili kukabili mambo ya maisha. Dr. Bernie Siegel aligundua kuwa angeweza kutabiri ni mgonjwa gani kati ya wagonjwa wake wa kansa angeweza kufa kwa kuulize; “Je, unapenda kuishi mpaka miaka mia moja?” Wale wenye hali ya kina ya malengo katika masha walijibu ndiyo na hao ndio walioishi. Tumaini hutokana na kuwa na malengo.

Kama umewahi kujisikia kutokuwa na tumaini, tulia, mabadiliko makubwa yatatokea maishani maishani mwako mara utakapoanza kuishi maisha yenye malengo. Mungu anasema, “Najua yale ninayoyapanga kwa ajili yenu … nina mipango mizuri kwa ajili yenu, sio mipango ya kuwaumiza. Nitawapatia tumaini na mustakabali wa maana.” Yeremia 29:11 (NCV) Unajihisi unakabiliana na hali isiyowezekana, lakini Biblia inasema, “Mungu … anaweza kufanya Zaidi ya yale tunayoweza kuyaomba au kuyaota – anafanya mambo ya juu Zaidi kuliko sala zetu, nia zetu, mawazo yetu, au matumaini.” Waefeso 3:20 (LB)

Kujua lengo lako hurahisisha maisha yako. Hii hukuwezesha kuelewa ni nini ufanye na nini usifanye. Lengo lako linakuwa ndicho kigezo cha kutathmini kazi gani ni muhimu na zipi siyo. Unajiuliza, “Je, kazi hii inanisaidia kutimiza moja ya malengo ya Mungu kwa maisha yangu?”

Bila kuwa na malengo Dhahiri huna msingi wa kufanyia maamuzi, kupanga muda, na kutumia rasilimali zako. Utajaribu kuganya maamuzi kwa kuzingatia mazingira, msukumo, na hali yako kimawazo wakati huo. Watu wasiojua lengo lao hujaribu kufanya mambo mengi – na hiyo husababisha msongo (stress), uchovu, na migongano.

Haiwezekani kufanya kila kitu watu wanachotaka ufanye. Una muda wa kutosha tu kufanya mapenzi ya Mungu. Kama huwezi kufanya Zaidi ya Mungu alivyokukusudia kufanya (au labda, unatumia muda wako mwingi kutazama runinga). Kuishi kwa kuongozwa na malengo hutuwezesha kuishi maisha rahisi na yenye ratiba iliyopangwa kwa busara. Biblia inasema, “Maisha ya kuigiza na kujionyesha ni maisha ya ubatili; maisha ya uwazi na yaliyo rahisi ni maisha ya utoshelevu.” Mithali 13:7 (Msg) Maisha yanayoongozwa na malengo pia huleta Amani moyoni. “Wewe BWANA unawapa Amani kamili wale wanaotunza malengo yao kwa uthabiti na kuweka tumaini lao kwako.” Isaya 26:3 (TEV)

Kujua lengo lako hukupa mwelekeo wa maisha yako. Hukuwezesha kukusanya pamoja juhudi na nguvu zako kufanya kilicho cha muhimu. Unakuwa na ufanisi katika kuchagua kilicho cha muhimu.

Ni hali ya binadamu kukanganywa na mambo madogo madogo. Tunacheza mchezo wa Trivial Pursuit katika maisha yetu. Henry David Thoreau alisema kuwa watu huishi maisha ya “kukata tama sana,” lakini siku hizi maelezo mazuri yaweza kuwa ni kutokuwa na mwelekeo. Watu wengi wako kama gurudumu lizungukalo upesi (gyroscope) bila kwenda popote.

Bila kuwa na malengo Dhahiri, utadumu katika kubadili mwelekeo, kazi, mahusiano, makanisa, na mengineyo – ukitegemea kuwa kila badiliko litajaza utupu ulio moyoni mwako, unafikiri, Labda sasa mambo yatakuwa tofauti, lakini tatizo lako halisi linabaki – kutokuwa na mwelekeo na malengo.

Biblia inasema, “Msiishi pasipo uangalifu, bila kufikiri. Hakikisheni Bwana wenu anapenda nini.” Waefeso 5:17 (Msg)

Nguvu ya kuwa na mwelekeo inaweza kuonekana kwenye nuru. Nuru hafifu ina nguvu kidogo, lakini unaweza kuifanya nuru hivyo kuwa na nguvu kwa kukusanya pamoja mwanga huo. Kwa kutumia kipande cha kioo kikuzacho, mionzi ya jua yaweza kukusanywa na kuchoma moto nyasi au karatasi. Mwanga huo unapokusanywa pamoja kwa namna fulani unaweza kukata hata chuma.

Hakuna kitu chenye nguvu kama maisha yenye mwelekeo, ukiyaishi kwa malengo. Wanaume na wanawake waliofanya tofauti kubwa katika historia ni watu waliokuwa na mwelekeo. Mathalani, Mtume Paulo kwa sehemu kubwa alieneza Ukristo katika Himaya ya Rumi. Siri yake ilikuwa maisha yenye mwelekeo. Alisema, “Ninaelekeza nguvu zangu zote katika kitu kimoja: Nikiyasahau yaliyopita na ninatazama yale valiyo mbele yangu.” Wafilipi 3:13 (NLT)

Kama unataka maisha yako yawe na mvuto mbubwa, yape mwelekeo! Acha kufanya mambo juu juu tu. Acha kufanya mambo yote. Fanya machache. Ondo ahata zile shughuli nzuri na ufanye kile cha muhimu Zaidi. Usichanganye shughuli na ufanisi wa kuzalisha. Unaweza kuwa na shughuli nyingi bila malengo, lakini kuna faida gani? Paulo anasema, “Na tudumu kuwa na mwelekeo wa lengo hilo, sisi ambao tunataka kila kitu alichonacho Mungu kwa ajili yetu.” Wafilipi 3:15 (Msg)

Kujua lengo lako huhamasisha maisha yako. Lengo wakati wote huzaa bidi ya moyo. Hakuna kinachotia nguvu kama lengo Dhahiri. Kwa upande mwingine, shauku hupungua unapokuwa huna malengo. Kuamka toka kitandani tu inakuwa mzigo. Mara nyingi hatuchoshwi na kufanya kazi za ziada, bali kazi isiyokuwa na maana ndiyo hutuchosha sana na kutuchukulia furaha yetu yote.

George Bernard Shaw aliandika, “Hii ndiyo furaha ya kweli ya maisha: kutumiwa kwa ajili ya lengo unalolifahamu kuwa ni kubwa; ikiwa ni nguvu ya asili badala ya pupa za maumivu madogo madogo na manung’uniko, ukilalamika kuwa ulimwengu hauwezi kujitoa na kukupa furaha.”

文字方塊: Hukuwekwa duniani ili
Ukumbukwe. Uliwekwa hapa
Kujiandaa kwa ajili ya umilele.Kujua lengo lako hukuandaa kwa ajili ya maisha ya milele. Watu wengi wanatumia nguvu nyingi katika kujaribu kufanya historia duniani. Wanapenda wakumbukwe watakapokuwa wametoka duniani. Lakini cha muhimu Zaidi si kile watu watacholsema juu yako, bali kile Mungu anasema. Kitu kile Mungu anasema. Kitu ambacho watu hushindwa kufahamu ni kwamba mafanikio yote mwishowe hupitwa, na rekodi huvunjwa, heshima hufifia, na sifa za watu husahaulika. Katika chuo, malengo ya James Dobson yalikuwa awe bingwa wa shule yao katika mpira wa tenesi. Alijisikia vizuri sana pale kombe la ushindi wake lilipowekwa katika schemu ya makombe ya shule ya ushindi. Miaka kadhaa baada ya mtu mmoja alimtumia lile kombe. Walikuwa wameliokota kwenye pipa la takataka wakati shule ilipofanyiwa matengezo. James akasema, “kadiri muda wa kutosha unapopita vikombe vyako vya ushindi vitatupwa na mtu mwingine!” Wafilipi 3:15 (MSg)

Kuishi ukitengeneza historia ya kuacha duniani ni lengo la mtu asiyeona mbali. BMatumizi ya busara ya muda ni kujenga urithi wa milele. Hukuwekwa duniani ili ukumbukwe. Uliwekwa hapa kujiandaa kwa ajili ya umilele

Siku moja utasimama mbele za Mungu na atakagua maisha yako, mtihani wa mwisho, kabla ya kuingia katika umilele. Biblia inasema, “Kumbuka kila mmoja wetu binafsi atasimama mbele za kiti cha hukumu cha Mungu … ndiyo, kila mmoja atapaswa kutoa hesabu binafsi kwa Mungu.” Warumi 14: 10b, 12 (NLT) Kwa bahati, Mungu anatutaka tushinde jaribio hilo, hivyo ametupa maswali mapema kabisa. Kutoka katika Biblia tunaweza kuona kuwa Mungu atatuuliza maswali muhimu mawili:

Kwanza, “Je, ulifanya nini kuhusu mwanangu Yesu Kristo?”Mungu hatauliza kuhusu maisha yako ya nyuma ya kidini au maoni kuhusu mafundisho ya Imani Jambo la pekee ambalo litakuwa la muhimuni, Je, ulipokea kile Yesu alikufanyia , na je, ulijifunza kumpenda na kumtumaini? Yesu alisema “Mimi ndimi njia na ukweli wa uzima. Hakuna mtu awezaye kuja kwa Baba isipokuwa kwa njia ya mimi.” Yohana 14:6 (NIV)

Pili, “Je, ulifanya nini na kile nilichokupa?” ulifanya nini na vipawa vyote, nafasi mbalimbali, nguvu, mahusiano, na raslimali alizokupa Mungu? Je, ulivitumia mwenyewe tu, au ulivitumia kwa malengo Mungu aliyokuumbia? Kukuandaa kwa ajili ya maswali haya mawili ndilo kusudi la kitabu hiki. Swali la kwanza litaamua ni wapi utaishi milele. Swali la pili litaamua utafanya nini katika umilele. Mwisho wa kitabu hiki utakuwa tayari kujibu maswali yote mawili.

 


文字方塊: SIKU YA TATU: KUFIKIRI JUU YA MAISHA YANGU
Jambo la Kutafakari: Kuishi kwa malengo ni njia ielekeayo kwenye amani.
Kifungu cha Kukumbuka: “Wewe, BWANA, unawapa amani wale wanaotunza malengo yao kwa uthabiti na kuweka tumaini la kwako.” Isaya 26:3 (TEV)
Swali Kujiuliza: Je, jamaa na rafiki zangu wangesema ni kitu gani kinaongoza maisha yangu? Je, nataka iweje?
 

 

 

 

 

 

 

 


Siku ya Nne: Umeumbwa Kuishi Milele

Mungu… amepanda umilele ndani ya moyo wa mwanadamu.

Mhubiri 3:11 (NLT)

Hakika Mungu asingeweza kuumba kiumbe kama binadamu na aishi kwa siku moja! Hash ahata kidogo, mtu aliumbwa aishi milele.

Abraham Lincoln

Maisha haya si mwisho wa kila kitu.

Maisha duniani ni kama vazi la mazoezi tu kabla ya kitu halisi. Utatumia muda mwingi Zaidi katika ule upande mwingine baada ya kifo – yaani katika umilele kuliko hapa duniani. Duniani ni jukwaa la maonyesho yako ya milele. Ni kazi ya mazoezi kabla ya mchezo halisi; matayarisho kabla ya shindano halisi la mbio. Maisha haya ni maandalizi ya yale yajayo.

Kwa kiwango cha juu sana, unaweza kuishi miaka mia moja duniani, lakini utaishi siku zote katika umilele. Maisha yako duniani ni, kama bwana Thomas browne alivyosema, “ni alama ndogo sana katika umilele.” Uliumbwa ili uishi milele.

Biblia inasema, “Mungu… amepanda umilele katika moyo wa binadamu.” (NLT) Mhubiri 3:11Ndani yako kuna hali ya kuzaliwa nayo ambayo inatamani kuishi tu bila kufa. Hii ni kwa sababu Mungu alikubuni katika sura yake, uishi milele. Ingawa tunajua kwamba kila mtu mwishowe hufa kifo wakati wote huonekana si cha kawaida na ni kibaya Sababu inayotufanya tujisikie kuishi milele ni kwamba Mungu amefungamanisha hali hiyo na ubongo wetu!

Siku moja moyo wako utaacha kupiga. Huo utakuwa mwisho wa mwili wako na wakati wako hapa duniani. Mwili wako wa duniani ni makazi ya muda ya roho yako. Biblia huita mwili wako wa duniani “hema,” lakini inauita mwili wako wa baadaye “nyumba”. Biblia inasema, “wakati hemahili tunaloishi – mwili wetu hapa duniani – likiharibiwa, Mungu anayo nyumba mbinguni ya sisi kuishi, makazi ambayo Yeye mwenyewe ameandaa, yadumuyo milele”. 2 Wakorintho 5:1 (TEV)

Wakati maisha duniani yana uchaguzi mwingi, umilele hutoa mambo mawili tu: mbingu au kuzimu. Mahusiano yako na Mungu duniani yataamua uhusiano wako naye katika umilele. Ukijifunza kumpenda na kumtumikia Mwana wa Mungu, Yesu, utakaribishwa kuishi naye milele. Vinginevyo, kama utakataa upendo wake, msamaha, na wokovu wake, basi utatengwa milele kutoka uso wa Mungu.

C.S Lewis alisema, “Kuna aina mbili za watu: wale wasemao Mungu ‘mapenzi yako yafanyike’ na wale ambao Mungu huwaambia ‘haya basi, fanyeni mjuavyo wenyewe.’” Inasikitisha sana, watu wengi watalazimika kuishi katika hali ya kutengwa na Mungu milele yote kwa kuwa walichangua kuishi bila Mungu hapa duniani.

文字方塊: Maisha haya ya maandalizi yay ale yajayo.Utakapotambua bayana kwamba kuna Zaidi katika maisha kuliko maisha haya katika dunia, na kufahamu kuwa maisha ni maandaalizi tu ya umilele, utaanza kuishi kitofauti. Utaanza kuishi katika nuru ya umilele na hiyo itaonekana katika jinsi unavyohusiana na watu wengine, unavyofanya kazi, na unavyokuwa katika mazingira mbalimbali. Ghafla, shughuli nyingi, malengo n ahata matatizo mengi yaliyokuwa yakionekana ya muhimu yataanza kuonekana mambo madogo madogo yasiyohitaji uyashughulikie. Kadiri unavyoishi karibu na Mungu, Ndivyo kila kitu huonekana kidogo.

Unatumia muda na pesa zako kwa busara. Unaweka umuhimu wa juu katika mahusiano na tabia badala ya kutafuta kujulikana na utajiri au mambo makuu au hata michezo. Mpangilio wa mambo yako muhimu unabadilika. Kufuatisha mambo ya kisasa kama mitindo na mengineyo hayana maana tena. Paulo alisema, “Hapo nyuma nilidhani mambo haya yote yalikuwa ya muhimu, lakini sasa nayaona kuwa bure kwa sababu ya kile Kristo amefanya.” Wafilipi 3:7 (NLT)

文字方塊: Unapoishi katika nuru ya umilele, mambo ya muhimu kwako hubadilika.Iwapo muda wako duniani ungekuwa ndiyo kila kitu kwa maisha yako, basi ningekushauri uanze kuutumia ipasavyo mara moja. Ungeweza kusahau kuwa mwema wala mwadilifu, na wala usingehofu chochote kama matokeo ya matendo yako. Ungeweza kuzama katika mambo ya kuifurahisha nafsi yako kwa sababu matendo yako yasingekuwa na madhara ya kudumu. Lakini – hii inafanya tofauti – kifo siyo mwisho wako! Kifo ni hali ya mpito kuelekea katika umilele, hivyo kuna matokeo ya kila unachokifanya duniani. Kila tendo la maishani mwetu hugusa nyuzi ambaxo hutikisa katika umilele.

Jambo baya kabisa katika maisha ya siku hizi ni kuwa na mtazamo mfupi kimawazo. Ili kutumia vizuri maisha yako unapaswa kuwa na maono ya umilele katika akili zako na kutunza uthamani wako moyoni mwako. Kuna mengi Zaidi katika maisha kuliko ya hapa na ya sasa tu! Leo ni kama ncha ndogo ya mwamba wa barafu ichomozayo baharini. Umilele ni kama ile sehemu nyingine isiyooneka iliyo ndani ya bahari.

Je, itakuwaje katika umilele na Mungu? Kusema wazi, uwezo wa ubongo wetu hauwezi kuelewa ajabu na ukuu wa tovuti (internet) kwa sisimizi. Ni upuuzi. Hayajagunduliwa maneno ambayo labda yangeweza kueleza hali ilivyo katika umilele. Biblia inasema, “Hakuna mtu was kawaida amewahi kuona, kusikia n ahata kufikiri mambo ya ajabu Mungu aliyowaandalia wale wampendeo.” 1 Korintho 2:9 (LB)

文字方塊: SIKU YA NNE:
UMEUMBWA A UISHI MILELELakini, Mungu ametudokeza kuhusu mambo ya milele katika Neno lake. Tunajua kwamba sasa hivi Mungu anatuandalia makao ya milele. Mbinguni tutakutana na wapendwa ambao ni waamini, tutakutana na wapendwa ambao ni waamini, mateso, tutapewa tuzo kwa uaminifu hapa duniani, na tutapewa kazi nyingine ambayo tutaifurahia kuifanya kwetu. Hatutalala mawinguni tukizingirwa na nuru kichwani huku tukicheza vinubi! Tutafurahia ushirika wa kudumu pamoja na Mungu, na atatufurahia milele. Siku moja Yeu atasema, “Njooni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa kwa ulimwengu.” Mathayo 25:34 (NIV)

C.S. Lewis aliliweka wazo la umilele katika ukurasa wa mwisho wa kitabu chake dkiitwacho Chronicles of Narnia, ambayo ni sehemu ya vitabu vyake saba vyenye mfululizo wa hadithi za watoto: “Kwetu huu ni mwisho wa hadithi zote… Lakini kwao ulikuwa ni mwanzo wa hadithi ya kweli. Maisha yao yote hapa duniani … yalikuwa ni ukurasa wa jalada na jina la kitabu; sasa hatimaye walikuwa wanaanza Sura ya kwanza ya ile Hadithi Kuu, ambayo hakuna mtu hapa duniani amewahi kuisoma, ambayo inaendelea milele na ambayo kila sura ni bora Zaidi kuliko iliyotangulia.” C.S. lewis, Vita ya Mwisho (New York: Collier Books, 1970), 184.

Mungu ana malengo kwa maisha yako duniani, lakini hayakomei hapa. Mpango wake unahusisha Zaidi ya miongo michache ya miaka utakayoishi katika sayari hii. Ni Zaidi ya “nafasi njema sana maishani;” Mungu hukupatia nafasi iliyo juu Zaidi kuliko maisha yako ya hapa. Biblia inasema “Mipango yake (Mungu) yadumu milele; makusudi yake niya milele.” Zaburi 33:11 (TEV)

Muda pekee ambao watu hufikiri juu ya umilele ni ule wakati wa msiba, na hata hivyo hufikiri juu juu tu bila ufahamu wa kutosha. Unaweza kudhani kuwa ni jambo baya kuongelea mambo ya kifo, kwa kweli, si vema kuishi kwa kukikana kifo, kitu ambacho ni lazima kitokee. Mhubiri 7:2 (CEV) Ni mpumbavu tu ndiye aweza kuishi pasipo maandalizi kwa ajili ya kile sisi tunajua hatimaye kitatokea. Unahitaji kufikiri Zaidi kuhusu umilele, na siyo kidogo.

Kama ilivyokuwa katika ile miezi tisa uliyoitumia katika tumbo la mama yako kwamba haikuwa mwisho wa yote, lakini maandalizi kwa ajili ya maisha, hivyo maisha haya ni maandalizi kwa yajayo. Kama una uhusiano na Mungu kwa njia ya Yesu, huhitaji kuogopa kifo. Ni mlango wa kuingia umilele. Hivyo itakuwa saa yako ya mwisho wako. Badala ya kuwa mwisho wa maisha yako, itakuwa siku ya kuzaliwa katika maisha ya umilele. Biblia inasema, “ulimwengu huu si nyumbani, tunatazamia makao yetu ya kudumu mbinguni.” Hebrews 13:14 (LB)

Maisha yetu hapa duniani, yakilinganishwa na yale ya milele, ni kama kufumba na kufumbua jicho, na matokeo yake yatadumu milele. Matendo ya maisha haya ni mwamuzi wa maisha yajayo. Tunatakiwa “kufahamu kwamba muda tuishipo katika miili hii ya duniani ni muda wa kukaa mbali na makao yetu ya milele huko mbinguni na Yesu.” 2 Wakorintho 5:6 (LB) Miaka iliyopita kulikuwa na msemo uliopendwa na uliwahimiza watu kuishi kila siku kama “siku ya kwanza ya maisha yako yote.” Hakika, ingekuwa busara kuishi kila siku kama vile ilikuwa siku ya mwisho wa maisha yako. Matthew Henry alisema, “Yapasa iwe wajibu wa kila siku kujiandaa kwa ajili ya sku ya mwisho.”


文字方塊: SIKU YA NNE: KUFIKIRI JUU YA MAISHA YANGU
Jambo la Kutafakari: Kuna Zaidi katika maisha maisha kuliko ya hapa nay a sasa.
Kifungu cha Kukumbuka: “Ulimwengu huu unapita, na tamaa zake zote. Lakini kama ukifanya mapenzi ya Mungu, utaishi milele.” 1Yohana 2:17 (NLT)
Swali la Kujiuliza: Kwa kuwa niliumbwa niishi milele, je, ni kitu gani napaswa kuacha kukifanya na ni kitu gani napaswa kuanza kukifanya?
 

 

 

 

 

 

 

 


Siku ya Tano: Kuyaona Maisha Katika Mtazamo Wa Mungu

Maisha yako ni kitu gani?

Yakobo 4:14 (NIV)

Hatuoni vitu kama vilivyo, tunaviona kama tulivyo.

Anais Nin

Jinsi uyaonavyo maisha yako huumba maisha yako.

Jinsi unavyoelewa maana ya maisha huamua juu ya hatima yako. Mtazamo wako utakuwa na mvuto juu ya matumizi ya muda wako, pesa zako, vipawa na jinsi unavyothamini mahusiano.

Njia mojawapo ya kuwaelewa watu wengine ni kuwauliza, “Unayaonaje maisha yako?” Utagundua kwamba kuna majibu mengi kwa swali hilo sawa na watu uliowauliza. Nimeshaelezwa kuwa maisha ni tamasha, machimbo ya madini, reli ndogo ya michezo, fumbo, wimbo, safari, na mchezo wa dansi. Watu wamesema, “maisha ni karamu au ulevi: mara unaanguka, wakati mwingine unazunguka tu” au “maisha ni baiskeli yenye mwendo mkali tusiyoweza kutumia gia zake” au “maisha ni kama mchezo wa karata.”

Kama ningekuuliza unayaoonaje maisha, je, picha gani ingekujia akilini mwako? Hiyo sura ndiyo mfano wako wa maisha. Ni mtazamo wa maisha ulio nao, kwa kufahamu au kutokufahamu, akilini mwako. Ni maelezo yako jinsi maisha yanavyofanya kazi ya yale unayotazamia kuyapata. Mara nyingi watu hudhihirisha mfano wa maisha yao kwa njia ya mavazi, mapambo, magari, nywele, maandishi makubwa, au hata mikwaruzo katika miili yao.

Mfano wa maisha yako ambao hautamkwi kwa maneno una mvuto kwa maisha yako kuliko unavyofahamu. Huwa na mvuto kwa matarajio yako, mambo yako ya muhimu (values), mahusiano yako, malengo na vipaumbele vyako. Mathalani kama unadhani maisha ni sherehe, jambo muhimu maishani mwako litakuwa kujifurahisha. Kama unafikiri maisha ni mbio, utathamini mwendo mkali na labda utakuwa mtu mwenye haraka wakati wote. Kama unaona maisha kuwa riadha, utathamini uvumilivu. Kama utaona maisha kuwa vita au mashindano, basi ushindi litakuwa jambo la muhimu kwako.

文字方塊: SIKU YA TANO:
KUYAONA MAISHA KWA MTAZAMO WA MUNGUJe, mtazamo wako wa maisha ni upi? Unaweza kuwa umejenga maisha yako kwenye mfano wa maisha usio sahihi. Ili kutimiza malengo aliyokuumbia Mungu, basi utapaswa kuipa changamoto hekima yako ya kawaida na badala yake utumie kielezo cha kibiblia kuhusu maisha. Biblia inasema, “Msijifananishe na kanuni za ulimwengu huu, lakini mpeni Mungu nafasi awabadilishe utu wa ndani kwa kuwabadilisha kabisa nia zenu. Kisha mtaweza kuyajua mapenzi ya Mungu.” Warumi 12:2 (TEV)

Biblia hutoa mifano mitatu ambayo hutufundisha mtazamo wa Mungu wa maisha ni jaribu, maisha ni dhamana, na maisha ni jukumu la muda mfupi. Mawazo haya ni ya msingi kwa maisha yanayoongozwa na malengo. Tutayatazama mawazo mawili katika sura hii na lile la tatu katika sura inayofuata.

Maisha duniani ni Jaribu. Kielelezo hiki cha maisha kinaonekana ktika hadithi ya Biblia yote. Wakati wote Mungu huijaribu tabia ya watu, Imani yao, utii, upendo, ukamilifu na uaminifu wao. Maneno kama majaribu, kusafisha, na kujaribu hupatikana mara 200 katika Biblia. Mungu alimjaribu Ibrahimu kwa kumwambia amtoe sadaka mwanae Isaka. Mungu alimjaribu Yakobo alipopaswa kufanya kazi miaka ya ziada ili kumpata Raheli kama mkewe.

Adamu na Hawa walishindwa jaribio lao katika Bustani va Edeni, na Daudi alishindwa majaribu yake kutoka kwa Mungu mara kadhaa. Lakini Biblia pia hutupa mifano mingi ya watu walioshinda majaribu makubwa mfano Yusufu, Ruthu, Esta na Daniel.

Majaribu hukuza tabia na kuiweka wazi, na maisha yote ni majaribu. Siku zote unajaribiwa. Mungu siku zote anatazama unavyoenenda kwa watu, matatizo, mafanikio, migongano, magonjwa, mambo ya kukatisha tamaa, hata hali ya hewa! Mungu anaangalia hata matendo rahisi sana kama vile unapowafungulia mlango wengine, unapookota kipande cha takataka, au unapoonyesha upole kwa karani au mhudumu.

文字方塊: Majaribu hukuza tabia na kwiweka wazi, na maisha yote ni majaribu.Hatuyajui majaribu yote ambayo Mungu anatupa lakini tunaweza kutabiri baadhi yake, kwa kuzingatia Biblia. Utajaribiwa kwa mabadiliko makubwa, kucheleweshwa ahadi, matatizo magumu, sala zisizojibiwa, lawama zisizostahili, na hata mikasa isiyo na sababu. Katika maisha yangu nimetambua kwa Mungu anajaribu Imani yangu kupitia matatizo, anajaribu tumaini langu kwa njia ya mali, na anajaribu upendo wangu kwa njia ya watu.

Jaribu la muhimu sana ni jinsi unavyotenda unapoacha kuhisi uwepo wa Mungu katika maisha yako. Wakati mwingine Mungu hujiondoa kwa makusudi, na hatuoni uwepo wake. Mfalme aitwaye Hezekia alipatwa na jaribu hili. Biblia inasema, “Mungu alimwacha Hezekia ili kumjaribu na aweze kuona kile kilichokuwa ndani ya moyo wake hasa.” 2 Mambo ya Nyakati 32:31 (NLT) Hezekia alikuwa amefaidi ushirika wa karibu na Mungu, lakini kwa wakati wa muhimu sana Mungu alimwasha peke yake ili ampime tabia yake, adhihirishe udhaifu wake, na amwandae kwa majukumu Zaidi.

Ukielewa kuwa maisha ni jaribu, unatambua kuwa hakuna kitu kidogo katika maisha yako. Hata tukioa dogo sana lina maana kubwa katika kukuza tabia yako. Kila siku ni siku ya muhimu, na kila dakika ni wasaa wa kukua kitabia, kuonyesha upendo, au kumtegemea Mungu. Majaribu mengine hata huyatambui. Lakini yote yana matokeo ya milele.

Habari njema ni kwamba Mungu anakutaka ushinde mtihani huo wa maisha, kwa hiyo haruhusu majaribu unayoyapata kuwa makubwa kuliko neema anayokupatia katika kukabili majaribu hayo. Biblia inasema, “Mungu hutunza abadi yako, na hatawaacha mjaribiwe kupita uwezo wenu wa kutahimili; mnapokuwa katika majaribu, atawapa nguvu za kuvumilia na mlango wa kutokea.” 1 Wakorintho 10:13 (TEV)

Kila unaposhinda jaribu, Mungu hutambua na kupanga kukupa tuzo la milele. Yakobo anasema, “Heri wanaostahimili wanapojaribiwa. Wakishinda jaribu hilo, watapokea taji ya uzima ambayo Mungu ameawaahidi wampendao.” Yakobo 1:12 (GWT)

Maisha duniani ni dhamana. Huu ni mfano wa pili wa kibiblia kuhusu maisha. Muda wetu duniani na nguvu zetu, akili, nafsi, mahusiano, na mali zetu zote ni zawadi toka kwa Mungu ambazo ametukabidhi tuvitunze na kuvitumia vizuri. Sisi ni mawakili wa yale Mungu anasema, “Ulimwengu na vyote vilivyomo ni mali ya BWANA; dunia na wote waishio humo ni mali yake.” Zaburi 24:1 (TEV)

Hakika hatumiliki chochote kwa wakati wetu mfupi wa kuishi duniani. Mungu hutukopesha dunia tunapoishi hapa. Ilikuwa mali ya Mungu kabla hujaja, na Mungu atamkopesha mtu mwingine ukifa. Unaifurahia kwa muda mfupi tu.

Mungu alipowaumba Adamu na Hawa, aliwakabidhi uangalizi wa uumbaji wake na akawaweka kuwa wadhamini wa uumbaji wamali yake. Biblia inasema, “Mungu aliwabariki akasema, ‘mkawe na watoto wengi, iliwazaliwa wenu waishi duniani kote na kuitawala. Nawaweka kuwa waangalizi.’” Mwanzo 1:28 (TEV)

Kazi ya kwanza ambayo Mungu aliwapa wanadamu ni kuangalia na kutunza “vitu” vya Mungu duniani. Wajibu huu haujaondolewa kamwe. Ni sehemu ya malengo yetu leo. Kila kitu tunachokifurahia yapasa tukione kama dhamana ambayo Mungu ameiweka mikononi mwetu. Biblia inasema, “Mna kitu gani ambacho Mungu hakuwapa” Na iwapo kila mlicho nacho kinatoka kwa Mungu kwa nini basi mjivune kama vile mmefanikiwa kwa nguvu zenu wenyewe?” 1 Wakorintho 4:7b (NLT)

Miaka mingi iliyopita, jamaa moja walituruhusu kutumia nyumba yao nzuri mbele ya pwani kule Hawaii kwa ajili ya mapumziko. Ilikuwa ni jambo ambalo tusingemudu gharama zake, lakini tulifurahia kweli. Tuliambiwa, “Itumieni kama vile ni yenu,” Hivyo ndivyo tulivyofanya! Tuliogelea katika bwawa, tukala chakula kilichokuwa jokofuni, tukatumia vitambaa vya kuogea na vyombo, n ahata tukarukia vitandani kucheza! Lakini tulifahamu wazi kwamba nyumba hii haikuwa yetu, hivyo tulikuwa waangalifu kwa kila kitu. Tulifaidi kutumia nyumba ambayo haikuwa yetu.

Mila zetu husema, “Kama si mali yako, huhitaji kuitunza.” Lakini Wakristo wanaishi kwa maadili ya kiwango cha juu: “Kwa kuwa ni mali ya Mungu, ni lazima niitunze kwa uangalifu wa hali ya juu.” Biblia inasema, “Wale ambao wameaminiwa kwa kitu cha thamani waonyeshe kweli wanastahili heshima hiyo’”

文字方塊: Kadiri Mungu anavyokupa vingi, ndivyo anavyokutaka uwajibike Zaidi.yo.” 1 Korintho 4:2 (NCV) Yesu mara kwa mara alionyesha kuwa maisha ni dhamana na alitoa mifano mingi kufundisha wajibu huu kwa Mungu. Katika ule mfano wa talanta, Mathayo 25:14-19 nfanya biashara aliposafiri. Aliporudi alitathmini kazi ya kila mtumishi na kumpa ujira sawasawa na kazi yake. Yule tajiri anasema, “Vema, mtumishi mwema na mwaminifu! Umekuwa mwaminifu katika vichache; nitakuweka uwe mwangalizi wa vitu vingi. Njoo ushiriki hatika furaha ya bwana wako.” Mathayo 25:21 (NIV)

Mwisho wa maisha yako duniani utatathminiwa kulingana na ulivyotumia yale Mungu aliyokukabidhi. Hii ina maana mambo yote unayoyafanya, hata yale mambo madogo madogo ya kila siku, yana matokeo ya umilele. Kama utaona mambo yote kuwa dhamana, Mungu anaahidi zawadi tatu katika maisha ya milele. Kwanza, utapewa uthibitisho. Atasema, “kazi nzuri! Umefanya vema!” Kisha utapandishwa daraja na utapewa jukumu kubwa katika umilele: “Nitakuweka uwe mwangalizi wa vitu vingi.” Na mwisho utakaribishwa katika karamu: “Njoo ushiriki katika furaha ya bwana wako.”

Watu wengi wanashindwa kufahamu kuwa pesa ni jaribu na dhamana toka kwa Mungu. Mungu anatumia pesa kutufundisha kumtegemea; na kwa watu wengi fedha ni jaribu kuu kupita yote. Mungu anaagalia jinsi tunavyotumia pesa ili kupima jinsi gani tunaaminika. Biblia inasema, “Kama hamuaminiki kwa utajiri wa duniani, je, ni nani atakayewaamini kwa utajiri wa kweli mbinguni?” Luka 16: 11 (NLT)

Huu ni ukweli wa muhimu sana. Mungu anasema kuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya ninavyotumia pesa zangu na hali yangu ya kiroho. Jinsi ninavyotawala pesa zangu (“utajiri wa dunia”) ni kigezo cha kiasi gani Mungu anaweza kunikabidhi Baraka za rohoni, (“utajiri wa kweli”). Hebu Nikuulize: je, namna unavyotumia fedha zako yaweza kumzuia Mungu kufanya mambo zaidi maishani mwako? Je, unaweza kuaminiwa katika utajiri wa kirobo?

Yesu alisema, “kutoka kila mtu aliyepewa vingi, vitatakiwa vingi; na kutoka aliyekabidhiwa Zaidi; ataulizwa vingi Zaidi.” Luka 12:48b (NIV) Maisha ni jaribu na dhamana. Na kadiri Mungu anavyokupa Zaidi, ndivyo anakutaka uwajibike Zaidi.


文字方塊: SIKU YA TANO: KUFIKIRI JUU YA MAISHA YANGU
Jambo la Kutafakari: Maisha ni jaribu na dhamana.
Kifungu cha Kukumbaka: “Isipokuwa mmekuwa waaminifu katika mambo madogo, hamwezi kuwa waaminifu katika mambo makubwa.” Luka 16:10a (NLT)
Swali la Kujiuliza: Kumetokea nini kwangu hivi karibuni ambacho sasa najua lilikuwa jaribu toka kwa Mungu? Je, Mungu amenikabidhi mambo gani makubwa sana.
 

 

 

 

 

 

 

 


Siku ya Sita: Maisha ni Jukumu La Muda Mfupi

Bwana nikumbushe jinsi muda wangu wa kukaa hapa duniani ulivyo mfupi. Nikumbushe kuwa siku zangu zimehesabiwa, na kwamba maisha yangu yanatoweka kwa haraka.

Zaburi 39:4 (NLT)

Niko duniani kwa muda mfupi tu.

Zaburi 119:19 (TEV)

Maisha duniani ni jukumu la muda mfupi.

Bfiblia imejaa mifano ambayo hutufundisha kuhusu maisha yetu duniani yalivyo mafupi na yasiyodumu. Maisha yanaelezwa kama ukungu, mkimbiaji, pumzi, na mvuke. Biblia husema, “Kwa kuwa tulizaliwa jana tu … Maisha yetu duniani yanapita kama kivuli.” Ayubu 8:9 (NLT)

Ili kutumia vizuri maisha yako hupaswi kusahau ukweli wa aina mbili: Kwanza, yakilinganishwa na umilele, maisha ni mafupi sana. Pili, dunia ni makazi ya muda tu. Huwezi kukaa hapa kwa muda mrefu, hivyo usijishikamanishe sana nayo. Mwombe Mungu akusaidie kuyaona maisha ya duniani kama anavyoyaona yeye mwenyewe. Daudi aliomba, “Bwana nisaidie nitambue jinsi muda wangu wa kukaa duniani utakavyokuwa mfupi. Nisaidie kujua kwamba niko hapa kwa muda tu.” Zaburi 39:4 (LB)

Biblia imerudia sana kulinganisha maisha hapa duniani kama kuishi nchi ya ugenini. Haya si makazi yako ya kudumu, au hatima yako ya mwisho. Unapita tu, unatembea tu duniani. Biblia inatumia maneno kama vile mgeni, msafiri, na mtoka nchi ya mbali, katika kueleza ufupi wa maisha yetu duniani. Daudi alisema, “Mimi ni mgeni hapa duniani.” Zaburi 119:19 (NLT) na Petro akasema, “Kama mnamwita Mungu Baba yenu, muishi kama wakazi wa muda mfupi hapa duniani.” 1 Petro 1:17 (GWT)

Kule California, ambako runaishi, watu wengi wamehamia toka schemu nyingine za dunia ili kupata kazi hapa, lakini wanatunza uraia wao wa nchi zao. Hapa wanatakiwa kuwa na kitambulisho cha mgeni (kiitwacho “kadi ya kijani”), ambacho huwaruhusu kufanya kazi hapa hata kama si raia wa hapa. Wakristo lazima wachukue kadi za kijani za kiroho ili kutambulisha kwamba uraia wetu uko mbinguni. Mungu anasema watoto wake wanapaswa kufikiri tofauti na wasioamini kuhusu maisha. “Wao wanachokifikiri ni maisha haya duniani. Lakini sisi ni raia wa mbinguni, ambako Bwana Yesu Kristo anaishi.” Wafilipi 3:19-20 (NLT) Waamini wa kweli wanafahamu wazi kwamba kuna mambo mengi ya maisha kuliko hii miaka michache tunayoishi hapa duniani.

文字方塊: Kitambulisho chako kiko katika umilele, nan chi yako ni mbinguni.Kitambulisho chako kiko katika umilele, na nchi yako ni mbinguni. Unapofahamu ukweli huu, utaacha kuwa na wasiwasi wa “kupata kila kitu “hapa duniani. Mungu yuko wazi kabisa kuhusu habari za kuishi kwa ajili ya hapa na sasa tu huku ukijifananisha na watu wa dunia hii katika kipaumbele na mtindo wa maisha. Tunapochezacheza na majaribu ya dunia hii, Mungu anaita hali hivyo uzinzi wa kiroho. Biblia inasema, “Mnajidanganya mbele za Mungu. Iwapa mnachotaka ni mambo yenu tu, kuchezacheza na ulimwengu kwa kila nafasi mnayopata mwisho wenu ni kuwa maadui wa Mungu na njia yake.” Yokobo 4:4 (Msg)

Hebu fikiri kama ungeombwa na nchi yako uwe balozi katika taifa adui yenu. Labda ungelazimika kujifunza lugha mpya na mila na desturi zao uweze kukubalika na kukamilisha huduma yako. Kama balozi hungeweza kuitenga na adui zako. Ili kukamilisha kazi yako, ungelazimika kuwa na mawasiliano na uhusiano nao.

Lakini fikiri kama ungefurahia maisha katika nchi hii ya ugeni, ukaipenda kuliko nchi yako. Uaminifu na kujitoa kwako bingeweza kubadilika. Wajibu wako kama balozi ungeingia dosari. Badala ya kuiwakilisha nchi yako, ungeanza kufanya mambo kama adui. Ungekuwa msaliti.

文字方塊: SIKU YA SITA:
MAISHA NI JUKUMU LA MUDA MFUPIBiblia inasema, “Sisi ni mabalozi wa Kristo.” 2 Korintho 5:20 (NLT) Cha kusikitisha, Wakristo wengi wamemsaliti mfalme wao na ufalme wake. Katika hali ya upumbavu wameamua kwamba, kwa sababu wanaishi duniani, basi hapa ndiko nyumbani kwao. Biblia iko wazi: “Rafiki, hii dunia si nyumbani kwenu, hivyo msidanganywe na dunia. Msifuate tamaa zenu na kuleta hasara kwa nafsi zenu.” 1 petro 2:11 (Msg) Mungu anatuonya tusijishikamanishe sana na vitu vinavyotuzunguka kwa kuwa si vya kudumu. Tunaambiwa, “Wale wanaowasiliana mara kwa mara na vitu vya dunia hii wavitumie vizuri bila kujishikamanisha navyo, kwa kuwa ulimwengu huu na vyote vilivyomo vitapita.” 1 Wakorintho 7:31 (NLT)

Ikilinganishwa na karne zingine, maisha yamekuwa si mepesi kwa sehemu kubwa ya ulimwengu wa magharibi. Wakati wote tunafurahishwa na tunapewa huduma. Kwa mivuto ya hali ya juu, na vyombo vy mawasiliano vyenye kutia upofu, na mambo mengi ya anasa yaliyopo siku hizi, ni rahisi kusahau kwamba maisha si kutafuta raha tu. Ni pale tu tunapokumbuka kuwa maisha ni majaribu, dhamana, na jukumu la muda mfupi ndipo mvuto wa mambo ya anasa utakapokosa nguvu maishani mwetu. Tunajiandaa kwa jambo jingine ambalo ni bora Zaidi. “Mambo tunayoyaona sasa yapo leo, na kutoweka kesho. Lakini mambo tusiyoyaona sasa yatadumu milele.” 2 Wakorintho 4:18b (Msg)

Ukweli kwamba dunia si makazi yetu ya kudumu huelezea kwa nini, kama wafuasi wa Kristo, tunapatwa na magumu, huzuni, na kukataliwa duniani. (Yahana 16:33; 16:20; 15:18-19) Ukweli huu pia hueleza kwa nini baadhi ya ahadi za Mungu huonekana kutotimizwa, baadhi ya sala hazijajibiwa, na baadhi ya mazingira kuonekana kutokuwa ya haki. Huu si mwisho wa mambo.

文字方塊: Dunia si makazi yetu ya kudumu; tuliumbwa kwa ajili ya kitu bora Zaidi.Ili kutufanya tusijifungamanishe na ulimwengu sana, Mungu hurubusu tusikie hali fulani ya kutokuridhirisha na kutosheka katika maisha – hitaji ambalo haliwezi kutoshelezwa kamwe hapa duniani. Hatuna furaha kabisa hapa kwa sababu hatutakiwi! Dunia si makazi yetu ya milele, tuliumbwa kwa ajili ya kitu bora zaidi.

Samaki hawezi kuwa na furaha kuishi nchi kavu, kwa sababu ameumbwa kwa ajili ya kuishi majini. Tai asingefurahi kama hangeruhusiwa kupaa angani. Hatuwezi kamwe kujisikia kutosheka kabisa hapa duniani, kwa sababu uliumbwa kwa ajili ya mambo mengine Zaidi. Utakuwa na vipindi vya furaha hapa, lakini hakuna cha kufanana na kile Mungu amepanga kwa ajili yako.

Kwa kutambua kwamba maisha duniani ni jukumu la muda mfupi tu ni lazima kubadili kabisa mambo unayoyaona ya muhimu maishani mwako. Mambo ya milele, yasiyo ya muda mfupi, yapasa yawe vigezo vya maamuzi yako. Kama C.S. Lewis alivyosema, “Kila kisicho cha milele hakifai milele.” Biblia inasema, “Tunakaza macho yetu si kwa kile kinachoonekana, lakini kwa kisichoonekana. Kwa kuwa kila kinachoonekana ni cha muda, na kisichoonekana ni cha milele.” 2 Korintho 4:18 (NIV)

Ni kosa kubwa kudhani kuwa mpango wa Mungu kwa ajili ya maisha yako ni mafanikio ya mali au mafanikio ya siku hizi, kama ulimwengu unavyoyaona. Maisha tele hayana uhusiano na mali tele, na uaminifu kwa Mungu hautuhakikishii kuwa na mafanikio ya kazi au huduma, usitazamie taji zisizodumu. 1 Petro 2:11 (GWT)

Paulo alikuwa mwaminifu lakini alijikuta gerezani. Yohana Mbatizaji alikuwa mwaminifu lakini alikatwa kichwa. Mamilioni ya watu waaminifu wameuawa, wamepoteza kila walichokuwa nacho, au maisha yao yamekoma wakiwa hawana kitu. Lakini mwisho wa maisha haya si mwisho!

Katika macho ya Mungu, mashujaa wa Imani sio wale waliopata mali, wenye mafanikio na nguvu katika maisha haya, lakini ni wale wanaoyaona maisha kama jukumu la muda mfupi na kutumika kwa uaminifu, wakitumaini kupokea thawabu yao katika umilele. Biblia husema kuhusu jambo hili, “Watu hawa wote wakafa katika Imani. Hawakupata vitu vile Mungu alivyowaahidi watu wake, lakini waliviona kwa mbali vikija wakashangilia. Walisema walikuwa kama wangeni na wapitaji hapa duniani … Walisubiri nchi bora- nchi ya mbinguni. Hivyo Mungu haoni hayakuitwa Mungu wao, kwa sababu amewatayarishia mji.” Waebrania 11:13, 16 (NCV) Maisha yako duniani si historia timilifu ya maisha yako. Unahitaji kusubiri mpaka mbinguni kwa ajili ya utimilifu wa maisha yako yote. Unahitaji Imani kuishi duniani kama mgeni.

Hadithi ya zamani inayosemwa mara nyingi ya mmishonari aliyekuwa anamaliza kazi yake na kurudi nyumbani Marekani alikuwa katika meli moja na Rais wa Marekani. Kundi kubwa la watu lililokuwa linashangilia, bendi ya jeshi, zuria jekundu, bendera na watangazaji walimkaribisha Rais nyumbani, lakini mmishonari alitoka polepole katika meli na kwenda zake bila Mungu. Kisha Mungu kwa upole alimkumbusha, “Lakini mwanangu, hujafika nyumbani bado.”

Hutakuwa mbinguni nukta mbili kabla hujapiga kelele ukisema, “Kwa nini niliweka umuhimu mkubwa kwa vitu ambavyo vilikuwa vya muda mfupi sana? Nilikuwa nafikiri nini? Kwa nini nilipoteza muda mwingi sana, nguvu nyingi, na kujali sana vitu ambavyo si vya kudumu?”

Maisha yanapokuwa magumu, unapokuwa umelemewa na mashaka, au unapojiuliza kama kumwishia Kristo kweli kunahitajika, kumbuka kuwa hujafika nyumbani bado. Wakati wa kufa hutatoka nyumbani bali utakwenda nyumbani.


文字方塊: SIKU YA SITA: KUFIKIRI JUU YA MAISHA YANGU
Jambo la kutafakari: Ulimwengu huu si nyumbani.
Kifungu cha Kukumbuka: “Hivyo tunakaza macho yetu si kwa mambo yanayookena, lakini kwa yale yasiyoonekna. Kwa kuwa yale yanayoonekana ni ya muda mfupi, lakini yale yasiyoonekana ni ya milele.” 2 Wakorintho 4:18 (NIV)
Swali la Kujiuliza: Je, ukweli kwamba maisha ya hapa duniani ni ya muda mfupi unawezaje kubadili ninavyoishi sasa hivi?
 

 

 

 

 

 

 

 


Siku ya Saba: Sababu Ya Kila Kitu

Kila kitu kimetoka kwa Mungu tu.

Ila kitu huishi kwa nguvu zake,

na kila kitu kipo kwa ajili ya utukufu wake.

Warumi 11:36 (LB)

BWANA amefanya kila kitu kwa ajili ya utukufu wake.

Mithali 16:4 (NLTo)

Kila kitu ni kwa ajili yake.

Lengo la ulimwengu mzima ni kuonyesha utukufu wa Mungu. Ni sababu ya kila kitu kilichopo, hii ni pamoja na wewe. Mungu aliumba vyote kwa ajili ya utukufu wake. Bila utukufu wa Mungu, kusingekuwepo chochote.

Utukufu wa Mungu ni nini? Ni Mungu alivyo. Ni kiini cha hali yake, uzito wa umuhimu wake,mng’ao wa ukuu wake, udhihirisho wa nguvu zake, na hali ya uwepo wake. Utukufu wa Mungu ni udhihirisho wa wema wake na sifa zake zote za milele.

Utukufu wa Mungu uko wapi? Tazama kuzunguka pande zote. Kila alichokiumba kinadhihirisha utukufu wake kwa namna fulani. Tunauona kila mahali, kuanzia viumbe vidogo vyenye uhai hadi mfumo mkubwa wa nyota, tangu kutua kwa jua na nyota hadi tufani na majira. Uumbaji unafunua utukufu wa muumba wetu. Kwa uumbaji wa asili tunajifunza kuwa Mungu ni mwenye nguvu, kwamba anafurahia vitu viwe tofauti tofauti, anapenda uzuri, ni wa mipango, na ana hekima na ubunifu. Biblia inasema, “Mbingu zinatangaza utukufu wa Mungu.” Zaburi 19:1 (NIV)

Katika historia yote, Mungu amedhihirisha utukufu wake kwa watu katika mazingira mbali mbali. Alijjifunua kwanza katika Bustani ya Edeni, kisha kwa Musa, 文字方塊: Kuishi kwa ajili ya utukufu wa Mungu ndilo jambo kubwa tunaloweza kulifanya kwa maisha yetu.na halafu katika Hema ya Kukutania na hekaluni, na kisha kwa njia ya Yesu, na sasa kupitia Kanisa. (Mwanzo 3:8; Kutoka 33:18-23; 40:33-38; 1 Wafalme 7:51; 8:10-13; Yohana 1:14; Waefeso 2:21-22; 2 Wakorintho 4:6-7) Utukufu wake ulionekana kama moto ulao, wingu, ngurumo, moshi, namwanga mkali. (Kutoka 24:17; 40:33-38, Zaburi 29:1; Isaya 6:3-4; 60:1; Luka 2:9) Mbinguni, utukufu wa Mungu hutoa mwanga wote unaohitajika. Biblia inasema, “Ule mji hauhitaji jua wala mwezi ili kutoa mwanga kwa kuwa utukufu wa Mungu huuangazia.” Ufunuo 21:23 (NIV)

Utukufu wa Mungu unaonekana vizuri Zaidi katika Yesu Kristo. Yeye, nuru ya ulimwengu, hudhihirisha hali ya Mungu. Kwa sababu ya Yesu, hatuko tena gizani kuhusu jinsi Mungu alivyo. Biblia inasema, “Mwana ni mng’ao wa utukufu wa Mungu.” Waebrania 1:3 (NIV), 2 Korintho 4:6 (LB) Yesu alikuja duniani ili tumfahamu Mungu vyema. “Neno akawa mwanadamu na akaishi katikati yetu. Tuliuona utukufu wake … utukufu uliojaa neema na kweli.” Yohan 1:14 (GWT)

Utukufu wa asili wa Mungu ni ule alionao kwa sababu yeye ni Mungu. Ni hali yake ya asili. Hatuwezi kuongeza chochote Kwenye utukufu huu, kama ambavyo haiwezekani kwetu kulifanya jua ling’ae Zaidi. Lakini tumeamriwa kuutambua utukufu wa Mungu, kuuheshimu utukufu wake, kuutangaza, kuusifu, kuuonyesha, na kuishi kwa utukufu wake. (Mambo ya Nyakati 16:24; Zaburi 29:1; 66:2; 96:7; 2 Wakorintho 3;18) Kwa nini? Kwa sababu Mungu anastahili. Tunawiwa kila namna ya heshima tunayoweza kumpa. Kwa kuwa Mungu aliumba vitu vyote, anastahili utukufu wote. Biblia inasema, “Unastahili, Ee Bwana Mungu wetu, kupokea utukufu, heshima na nguvu. Kwa kuwa uliumba kila kitu.” Ufunuo 4:11a (NLT)

Katika ulimwengu mzima, ni viumbe viwili tu, katika viumbe vyake vyote, waliishashindwa kuleta utukufu kwake: malaika walioanguka (mapepo) na sisi (Watu).

Dhambi yote, katika mzizi wake, ni kushindwa kumpa Mungu utukufu. Ni kupenda kitu kingine Zaidi ya Mungu. Kukataa kuleta utukufu kwa Mungu ni uasi wenye majivuno, na ni dhambi iliyomsababisha Shetani kuanguka na kuanguka kwetu pia. Kwa njia mbalimbali sisi sote tumeishi kwa ajili ya utukufu wetu, siyo utukufu wa Mungu. Biblia inasema, “Wote wefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” Warumi 3:23 (NIV)

Hakuna hata mmoja wetu ambaye amempa Mungu utukufu wote anaostahili katika maisha yetu. Hii ndiyo dhambi mbaya na kosa kubwa kufanya. Kwa upande mwingine, kuishi kwa ajili ya Mungu ni jambo kubwa tunaloweza kufanya katika maisha yetu Mungu anasema, “Wao ni watu wangu, na niliwaumba waniletee utukufu,” Isaya 43:7 (TEV) kwa hiyo ni lazima liwe lengo letu kuu maishani.

JE, NAWEZAJE KULETA UTUKUFU KWA MUNGU

文字方塊: Kila kitu katika uumbaji kinapotimiza lengo lake, huleta utukufu kwa Mungu.Yesu alimwambia Baba yake, “Nimeleta utukufu kwa jina lako hapa duniani kwa kufanya kila kitu ulichoniambia nifanye.” Yohana 17:4 (NLT) Yesu alimheshimu Mungu kwa kutimiza lengo lake hapa duniani.

Tunamheshimu Mungu kwa njia hiyo hiyo. Kila kitu katika uumbaji kinapotimiza lengo lake, huleta utukufu wa Mungu. Ndege huleta utukufu kwa Mungu kwa kuruka juu, kwa kuimba, kutengeneza viota, na kufanya kazi nyingine ambazo Mungu aliwapangia. Hata sisimizi wadogo huleta utukufu kwa Mungu pale wanapotimiza lengo la kuumbwa kwao. Mungu aliumba sisimizi ili wawe sisimizi, na alikuumba wewe uwe wewe. Mtakatifu Irenaeus alisema, “Utukufu wa Mungu ni binadamu mkamilifu aliye hai!”

Kuna njia nyingi za kuleta utukufu kwa Mungu, lakini zaweza kuwekwa katika muhtasari wa malengo matano ya Mungu kwa ajili ya maisha yako. Tunatumia sehemu iliyobaki ya kitabu hiki kuyaangalia kwa kina, lakini hapa tunatoa kwa ufupi:

Tunamletea Mungu utukufu kwa kumwabudu. Kuabudu ni wajibu wetu wa kwanza kwa Mungu. Tunamwabudu kwa kumfurahia C. W. Lewis alisema, “Katika kutuamuru tumwabudu, Mungu anatualika tumfurahie,” Mungu anapenda kuabudu kwetu kuchochewe na upendo, shukrani, na kufurahia, na siyo wajibu.

John Piper anasema, Mungu anatukuzwa Zaidi ndani yetu tunapokuwa tumetoshelezwa sana katika Yeye.”

Kuabudu ni Zaidi ya kusifu, kuimba na kumwomba Mungu. Kuabudu ni mtindo wa maisha wa kumfurahia Mungu, kumpenda, na kujitoa tutumiwe kwa ajili ya malengo yake. Unapotumia maisha yako kwa ajili ya utukufu wa Mungu, Kila unachokifanya chaweza kuwa tendo la ibada. Biblia inasema, “Tumia mwili wote kama chombo cha kufanya yaliyo sahihi kwa ajili ya utukufu wa Mungu.” Warumi 6:13b (NLT)

Tunaleta utukufu kwa Mungu kwa kuwapenda waamini wengine. Ulipozaliwa mara ya pili, ulikuwa sehemu ya jamii ya Mungu. Kumfuata Kristo siyo tu kuamini, ni pamoja na kuwa sehemu ya jamii ya Mungu, na kuipenda. Yohana aliandika, “Upendo wetu kwa ndugu unathibitisha kwamba tumetoka mautini na kwenda uzimani.” 1 Yohana 3:14 (CEB) Paulo alisema, “Pokeaneni kila mmoja na mwenzake kama vile Kristo alivyowapokea; ndipo Mungu atatukuzwa.” Warumi 15:7 (NLT)

Ni wajibu wako kujifunza kupenda kama Mungu apendavyo, kwa sababu Mungu ni upendo, na hii humletea heshima. Yesu alisema, “Kama nilivyowapenda, pendaneni vivyo hiyo. Kwa njia hii watu wote watajua kwamba ninyi ni wanafunzi wangu, kama mkipendana.” Yohana 13:34-35 (NIV)

Tunaleta utukufu kwa Mungu kwa kuwa kama Kristo. Mara tunapozaliwa katika jamii ya Mungu, anatutaka tukue kiroho. Hiyo inaonekanaje? Kukua kiroho ni kuwa kama Kristo katika namna tunavyofikiri, tunavyohisi, na kutenda. Kadiri unavyokua katika tabia ya Kristo, ndivyo unamletea utukufu Zaidi. Biblia inasema, “Kadiri Roho wa Bwana anavyotenda kazi ndani yetu, tufanane naye zaidi na Zaidi na tunaonyesha utukufu wake Zaidi.” 2 Wakorintho 3:18 (NLT)

Mungu alikupa maisha mapya na asili mpya ulipompokea Kristo. Sasa, kwa maisha yako yaliyobaki hapa duniani, Mungu anapenda kuendeleza kazi ya kukubadili tabia. Biblia inasema, “Mjazwe siku zote na tunda la wokovu wenu – yale mambo mazuri yanayotolewa maishani mwenu na Yesu Kristo – Kwa kuwa hili litaleta utukufu mwingi na sifa kwa Mungu.” Wafilip 1:11 (NLT); Yohana 15:8 (GWT)

Tunaleta utukufu kwa Mungu kwa kuwatumikia wengine kwa vipawa vyetu. Kila mmoja wetu alibuniwa kwa namna ya pekee na Mungu. Jinsi ulivyosokotwa si bahati mbaya. Mungu hakukupa uwezo ulio nao kwa ajili ya matumizi ya kichoyo. Ulipewa ili kuwafaidi wengine, kama vile wengine walivyopewa uwezo mbalimbali ili kukufaidi wewe. Bibla inasema, “Mungu amewapa karama kila mmoja wenu kutoka katika karama zake mbalimbali. Zitumieni vizuri ili ukarimu wa Mungu ububujike kupitia ninyi … Je, umeitwa kusaidia wengine? Fanya hivyo kwa nguvu zote unazojaliwa na Mungu. Kisha Mungu atapewa utukufu.” 1 Petro 4:10-11 (NLT); 2 Wakorintho 8;19 (NLT)

Tunaleta utukufu kwa Mungu kwa kuwaelezea wengine habari zake. Mungu hapendi upendo wake na malengo yake yawe siri. Mara tunapofahamu ukweli, anategemea tuwashirikishe wengine. Hii ni heshima kubwa – kuwatambulisha wengine kwa Yesu, kuwasaidia wagundue lengo lao, na kuwaandaa kwa ajili ya hatima yao ya millele. Biblia inasema, “Kadiri neema ya Mungu inavyoleta watu wengi Zaidi kwa Kristo, … Mungu atapokea utukufu Zaidi na Zaidi.” 2 Korintho 4:15

JE, TUNAISHI KWA AJILI YA NINI?

Ili kuishi maisha yako yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu unahitaji kubadili vipaumbele vyako, ratiba yako, mahusiano yako, na kila kitu. Wakati mwingine itamaanisha kuchagua njia ngumu badala ya ile nyepesi. Hata Yesu alihangaika na jambo hili. Akijua alikuwa karibu kusulubiwa, alilia akisema, “Nafsi yangu inahangaika; na nisemeje, ‘Baba uniokoe kutika saa hii’? Lakini kwa ajili ya lengo hili nimefika saa hii. Baba, litukuze jina lako.” Yohana 12:27-28 (NASB)

Yesu alisimama katika njia panda barabarani. Je, atatimiza lengo lake na kuleta utukufu kwa Mungu, au atanyong’onyea na kuishi maisha ya raha yenye ubinafsi? Unakabiliwa na uchaguzi wa aina hiyo. Je, utaishi kwa ajili ya malengo yako mwenyewe, ya kujifurahisha, au utaishi maisha yako yaliyosalia kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ukijua kwamba ameahidi zawadi na milele? Biblia inasema, “Yeyote anayeyashika maisha kama yalivyo huyaharibu maisha hayo. Lakini ukiyaacha, … utayapata milele, ya kweli nay a milele.” Yohana 12:25 (Msg)

Ni wakati wa kutengeneza jambo hili. Utaishi kwaajili ya nani – nafsi yako au Mungu? Unaweza kusita au kushangaa kama utakuwa na nguvu za kuishi kwa ajili ya Mungu. Usihofu. Mungu atakupa unachohitaji kama utafanya uchaguzi wa kuishi kwaajili yake. Biblia inasema, “Kila kitu kinachoenda katika maisha ya kumpendeza Mungu kimepewa kwetu kimiujiza kwa kumjua binafsi na kwa ukaribu, yeye aliyetukaribisha kwa Mungu.” 2Petro 1:3 (Msg)

Sasa hivi, Mungu anakukaribisha uishi kwa ajili ya utukufu wake kwa kutimiza kusudi alilokuumbia. Ndiyo njia ya pekee ya kweli kuishi. Vingine ni kuwepo tu. Maisha ya kweli huanza kwa kujiweka wakfu kikamilifu kwa Yesu Kristo. Kama huna hakika umefanya hivi unachohitaji kufanya ni kupokea na kuamini. Biblia inaahidi, “Kwa wote waliompokea, wale walioliamini jina lake, aliwapa haki ya kuwa watoto wa Mungu.” Yohana 1:12 (NIV) Je, unaweza kupokea zawadi ya Mungu?

文字方塊: Yesu atakupa kila kitu unachohitaji ili kumwishiaKwanza, uamini. Amini Mungu anakupenda na alikuumba kwa lengo au malengo yake. Amini wewe si bahati mbaya. Amini uliumbwa kuishi milele. Amini Mungu amekuchagua uwe na uhusiano na Yesu, aliyekufia msalabani. Amini kwamba haijalishi umeshafanya nini, Mungu anapenda kukusamehe.

Pili, pokea. Mpokee Yesu maishani mwako kama Bwana na mwokozi wako. Pokea msamaha wa dhambi zako. Pokea Roho wake Mtakatifu, ambaye atakupa nguvu za kutimiza lengo la maisha yako. Biblia inasema, “Yeyote ampokeaye na kumwamini Mwana hupata yote, uzima mtimilifu na wa milele.” Yohana 3:36 (Msg) Popote unaposoma maneno haya nakualika uinamishe kichwa chako, na taratibu Sali sala hii itakayobadili umilele wako: “Yesu nakuamini, na ninakupokea.” Endelea.

Kama kweli ulimaanisha sala hiyo kutoka moyoni, hongera! Karibu katika jamii ya Mungu! Sasa uko tayari kugundua na kuanza kuishi malengo ya Mungu kwa ajili ya maisha yako. Nakushauri umweleze mtu mwingine juu ya jambo hili. Utahitaji msaada. Kama utanitumia barua pepe (Nyongeza ya 2), nitakutumia kijitabu kidogo nilichoandika kiitwacho Hatua za Mwanzo Katika Kukua Kiroho.


文字方塊: SIKU YA SABA: KUFIKIRI JUU YA LENGO LANGU
Jambo la Kutafakari: Yote ni kwa ajili yake.
Kifungu cha kukumbuka: “Kwa kuwa kila kitu chatoka kwa Mungu. Kila kitu kinaishi kwa uwezo wake, na kila kitu kipo kwa ajili ya utukufu wake.” Warumi 11:26 (LB)
Swali la Kujiuliza: Je, ni wapi katika maisha yangu ya kila siku naweza kuuona utukufu wa Mungu Zaidi?
 

 

 

 

 

 

 

 


Lengo La I


文字方塊:
 

 

 

 

 


ULIKUSUDIWA KWA AJILI YA FURAHA YA MUNGU

Kwa kuwa Mungu amewapanda kama mti imara wenye

kuneemeka kwa ajili ya utukufu wake

Isaya 61: 3 (LB)

 

Siku ya Nane: Ulikusudiwa Kwa Ajili Ya Furaha Ya Mungu

Uliumba Kila kitu, na ni kwa furaha yako kwanba vipo na viliumbwa.

Ufunuo 4:11 (NLT)

Bwana huwafurahia watu wake

Zaburi 149:4a (TEV)

Ulikusudiwa kwa furaha ya Mungu.

Wakati ulipozaliwa duniani, Mungu alikuwepo hapa kama shahidi asiyeonekana, akifurahia kuzaliwa kwako. Alikutaka uwe hai, na kufika kwako kulimpa furaha kubwa. Mungu hakuhitaji kukuumba, lakini alichagua kukuumba kwa ajili ya furaha yake mwenyewe. Upo kwa sababu ya faida yake, utukufu wake, na furaha yake. Kuleta furaha kwa Mungu na kumburudisha, ni lengo la kwanza kwa maisha yako. Unapoelewa kikamilifu ukweli huu hutakuwa na tatizo kamwe la kujisikia hufai. Ni uthibitisho wa uthamani wako. Kama wewe ni wa muhimu hivyo kwa Mungu, na anakuthamini kiasi cha kukutunza ukae naye milele, ni uthamani gani mkubwa ungekuwa nao? Wewe ni mtoto wa Mungu, na unaleta furaha kwa Mungu kuliko chochote kingine alichokiumba. Biblia inasema, “kwa sababu ya upendo wake Mungu ameamua kwamba kupitia Yesu Kristo atatufanya watoto wake – hii ilikuwa furaha yake na kusudi lake. Waefeso 1:5 (TEV)
Moja ya zawadi kubwa Mungu aliyokupatia ni uwezo wa kufurahia.


Alikuunganisha kwa milango mitano ya fahamu na hisia ili uweze kupata furaha hiyo. Anapenda ufurahie maisha, siyo tu kuyavumilia. Sababu ya wewe kuweza kufurahia ni kwamba Mungu alikuumba kwa mfano wake.

Mara nyingi tunasahau kwamba Mungu ana hisia pia. Huhisi mambo kwa kina. Biblia inatuambia kwamba Mungu huhuzunika, hupata wevu na hasira, na husikia huruma, sikitiko, pia furaha, shangwe, na utoshelevu. Mungu hupenda, kufurahia, hupata burudiko, hushangilia, na hata kucheka! Mwanzo 6:6; Kutoka 20:5; Kumbukumbu 32:36; Waamuzi 2:20; 1 Wafalme 10:9; 1 Mambo ya Nyakati 16:27; Zaburi 2:4; 5:5; 18:19; 35:27; 37:23; 103:13; 104:31; Ezekiel 5:13; 1 Yohana 4:16.

Kuleta furaha kwa Mungu huitwa “kuabudu.” Biblia inasema, “Mungu anapenezwa na wale tu wanaomwabudu na kutumaini pendo lake. Zaburi 147:11 (CEV)

Chochote ufanyacho kinacholeta furaha kwa Mungu ni tendo la ibada. Kama almasi, kuabudu kuna nyuso nyingi, lakini katika sehemu hii tutaangalia mambo ya msingi kuhusu kuabudu.

Wataalamu wa mambo ya wanadamu na mila zao wamegundua kwamba kuabudu ni jambo lililo ndani ya wanadamu wote, Mungu amelifunga ndani ya utu wetu wa ndani – hitaji lililojengwa ndani yetu kutuunganisha na Mungu.Kuabudu ni hali ya asili yetu kama vile kula na kupumua. Tukishindwa kuabudu, mara nyingi tunatafuta njia mbadala, hata ikibidi sisi wenyewe. Sababu ya Mungu kutuumba na hamu hii ni kwamba anapenda wamwabuduo! Yesu alisema, “Baba anatafuta waabuduo.” Isaya 29:13 (NIV)

文字方塊: Jambo lolote unalolifanya na linaleta furaha kwa Mungu ni tendo la kuabudu.Kutegemeana na mazingira ya nyuma ya kidini, unaweza kuhitaji kupanua ufahamu wako kuhusu “kuabudu.” Unaweza kufikiri ibada za kanisani zenye nyimbo, sala, na kusikiliza mahubiri. Au unaweza kufikiri desturi mbalimbali, mishumaa, na meza ya Bwana. Au unaweza kufikiri uponyaji, miujiza, na hali ya kuwa katika msisimko wa kiroho. Kuabudu kunaweza kuhusisha mambo yote haya, lakini kubudu ni zaidi sana kuliko mambo haya. Kuabudu ni maisha.

文字方塊: Kuabudu ni Zaidi sana kuliko uimbaji.Kuabudu ni Zaidi sana kuliko kuimba. Kwa watu wengi, kuabudu ni sawa na uimbaji. Wanasema, “Kanisani kwetu tunaabudu kwanza, kisha mafundisho. “ Huku ni kutokujua ukubwa. Kila tendo la huduma ya kanisa ni ibada: sala, kusoma maandiko, kuimba, toba, ukimya, kutulia, kusikiliza mahubiri, kuandika mahubiri, sadaka, ubatizo, meza ya Bwana, ahadi mbalimbali, na hata kuwasalimu waabuduo wengine.

Kwa hakika, kuabudu hutangulia uimbaji. Adamu aliabudu katika Bustani ya Edeni, lakini uimbaji haujatajwa mpaka Mwanzo 4:21 kwa kuzaliwa kwa Yubali. Kama kuabudu kungekua uimbaji tu, basi wale wote wasio na kipawa cha kuimba wasingeabudu. Kuabudu ni Zaidi sana kuliko uimbaji.

Kibaya Zaidi, kuabudu mara nyingi kumefananishwa na mtindo fulani wa uimbaji: “Kwanza tuliimba utenzi, kisha wimbo wa sifa na kuabudu.” Au “Napenda nyimbo za haraka za sifa lakini nafurahia Zaidi nyimbo za pole pole za kuabudu.” Kwa matumizi haya, kama wimbo unaimbwa kwa haraka au kwa sauti ya juu, au unatumia zana za shaba, basi unadhaniwa ni wa “sifa.” Lakini ukiwa wa pole pole na wa taratibu wenye mguso wa karibu, labda ukifuatana na gitaa, huo ni wa kuabudu. Hayo ni matumizi mabaya ya neno “kuabudu.”

Kuabudu hakuhusiani na namna (mtindo) au sauti au mwendo wa wimbo. Mungu anapenda aina zote za uimbaji kwa kuwa zote alizibuni yeye – za haraka na polepole, za juu na za chini, za kale na mpya. Labda wewe huzipendi kabisa, lakini Mungu anazipenda! Kama zinatolewa kwa ajili ya Mungu katika roho na kweli, ni   tendo la kuabudu.

Wakristo mara nyingi hawakubaliani kuhusu mtindo wa uimbaji unaotumiwa katika kuabudu, wakitetea mtindo wanaoupendelea wao kuwa ndio wa kibiblia au unaomheshimu Mungu. Lakini hakuna mtindo wa kibiblia! Hakuna nota za muziki katika Biblia; wala siku hizi hatuna zana za uimbaji zilizotumika wakati wa Biblia.

Kusema kweli, mtindo wa uimbaji unaoupenda Zaidi unasema sana kuhusu wewe – mazingira yako na hali ya utu wako – kuliko kuhusu Mungu. Aina fulani ya uimbaji wa jamii fulani ya watu yaweza kusikika kama kelele kwa watu wa jamii nyingine. Lakini Mungu anapenda aina mbalimbali na anazifurahia zote.    

文字方塊: SIKU YA NANE:
ULIKUSUDIWA KWA FURAHA YA MUNGU.Hakuna kitu kama muziki wa “Kikristo,” kuna mashairi tu ya Kikristo. Maneno ndiyo hufanya wimbo kuwa mtakatifu, siyo sauti. Hakuna sauti za kiroho kama ningeimba wimbo bila maneno, huna jinsi ya kujua kama ni wimbo wa “Kikristo”.

Kuabudu si kwa ajili ya faida yako. Kama mchungaji, napokea ujumbe usemao “Nilipenda ibada ya leo. Nimepata mengi.” Huku ni kutokuelewa tena maana ya neno kuabudu. Si kwa ajili yetu! Tunaabudu kwa ajili ya faida ya Mungu. Tunapoabudu, lengo letu ni kuleta furaha kwa Mungu, si kwetu wenyewe. Nia yetu ni kuleta utukufu na furaha kwa Muumba wetu.

Kama ukisema, “sikupata chochote katika kuabudu leo” Uliabudu na sababu zisizo za haki. Kuabudu sio kwako wewe. Ni kwa Mungu. Kwa kweli, Ibada za “Kuabudu” kwingi pia huwa na aina za ushirika, mafundisho mema, na uinjilisti na pia kuna faida za kuabudu, lakini hatuabudu kwa kujifurahisha wenyewe. Nia yetu ni kuleta utukufu na raha kwa Muumba wetu.

Katika Isaya 29 Mungu analalamika juu ya ibada ambayo ni nusu nusu na ya kinafiki. Watu walikuwa wakitoa sala za ovyo ovyo, sifa zisizotoka moyoni, maneno matupu, na mapokeo ya ibada yaliyotungwa na watu bila hata kufikiri maana yake. Moyo wa Mungu hauguswi na desturi katika ibada, lakini kwa nia ya ndani na kwa moyo wote. Biblia inasema, “Watu hawa huja karibu yangu kwa vinywa vyao na huniheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami. Kuniabudu kwao ni sheria zinazofundishwa na wanadamu tu.” Zaburi 105:4 (TEV)

Kuabudu siyo sehemu ya maisha yako tu; ni maisha yako. Kuabudu si        tu huduma za kanisani. Tunaagizwa “kumwabudu kila wakati.” Zaburi 113:3 (LB) na “kumsifu tangu maawio hadi machweo.” Zaburi 119:147; 5:3; 63:6; 119:62 Katika Biblia watu walimtukuza Mungu kazini, nyumbani, vitani, gerezani, hata vitandani. Sifa iwe ni kazi yako ya kwanza unapofumbua macho asuhuhi na iwe kazi unapofumba macho usiku. Zaburi 34:1 (GWT) Daudi alisema, “Nitamshukuru Bwana wakati wote. Kinywa change kitamtukuza daima.” 1 Wakorintho 10:31 (NIV)

Kila shughuli yaweza kugeuzwa na kuwa tendo la ibada unapoifanya kwa ajili ya sifa, utukufu, na furaha ya Mungu. Biblia inasema, “Hivyo mlapo au mnywapo au chochote mkifanyacho, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.” Wakolosai 3:21 (NIV) Martin Luther alisema, “Mfanyakazi wa nyumbani anaweza kukamua ng’ombe wa maziwa kwa utukufu wa Mungu.”

Je, yawezekanaje kufanya kila kitu kwa utukufu wa Mungu? Kwa kufanya kila kitu kana kwamba unamfanyia Yesu na huku ukifanya mazungumzo naye unapoendelea na kazi hiyo. Biblia inasema, “Kila mkifanyacho, kifanyeni kwa moyo wenu wote, kama kumtumikia Bwana, siyo watu.” Warumi 12:1 (Msg)

Hii ndiyo siri ya maisha ya kuabudu, kufanya kila kitu kana kwamba unamfanyia Yesu. Tafsiri ya ujumbe inasema, “Yachukueni maisha yenu ya kawaida, ya kila siku, kulala kwenu, kula, kwenda kazini, na mizunguko yenu ya maisha - na myaweke mbele za Mungu kama sadaka.” Warumi 12:1 (Msg) Kazi inakuwa ibada unapoiweka wakfu kwa Mungu na ukaifanya na utambuzi wa uwepo wake.

Nilipompenda kwa mara ya kwanza mke wangu, nilimfikiria daima: nilipokua kifungua kinywa, nilipoendesha kwenda shuleni, nilipokuwa darasani, nilipokuwa kwenye msitari sokoni – sikuacha kumfikiria mwanamke huyu! Mara nyingi nilijisemea peke yangu kuhusu huyu mwanamke na nikafikiri mambo yote niliyoyapenda kwake. Hii ilinisaidia kujisikia kuwa karibu na Kay ingawa tuliishi maili mamia kadhaa mbali na tulikuwa katika vyuo tofauti. Kwa kumfikiria daima, nilidumu katika pendo lake. Hivi ndivyo kuabudu halisi kulivyo – kumpenda Yesu.


文字方塊: SIKU YA NANE
KUFIKIRI JUU YA LENGO LANGU
Jambo la Kutafakari: Nilikusudiwa kwa ajili ya furaha ya Mungu.
Kifungu cha Kukumbuka: “BWANA huwafurahia watu wake.” Zaburi 149:4a
Swali la kujiuliza: Je, ni kazi gani ya kawaida ninayoweza kuanza kuifanya kana kwamba naifanya kwa ajili ya Yesu moja kwa moja?
 

 

 

 

 

 

Siku ya Tisa: Nini Humfanya Mungu Kutabasamu?

BWANA anatabasamu kwa ajili yako…

Hesabu 6:25 (NLT)

Tabasamu kwa ajili ya yangu, mtumishi wako,

nifundishe njia sahili ya kusihi.

Zaburi 119:135 (Msg)

Tabasamu la Mungu ni lengo la maisha yako.

Kwa kuwa kumfurahisha Mungu ndilo lengo lako la kwanza la maisha yako, kazi yako ya muhimu Zaidi ni kugundua namna ya kutekeleza jambo hilo. Biblia inasema, “Tafuteni ni nini kinachompendeza Kristo, na kisha fanyeni hicho” Waefeso 5:10 (Msg) Kwa bahati nzuri, Biblia hutupa mfano Dhahiri wa maisha yampendezayo Mungu. Jina la mtu huyo alikuwa Nuhu.

Wakati wa Nuhu, ulimwengu wote ulikuwa umeharibika kwa kukosa uadilifu. Kila mtu aliishi kwa kujifurahisha mwenyewe na siyo Mungu. Mungu hakuweza kupata mtu yeyote duniani aliyetafuta kumpendeza, hivyo alihuzunika na akajilaumu kwa nini alimuumba mwanadamu. Mungu alikasirishwa sana na binadamu kiasi cha kufikiri kumfutilia mbali kabisa. Lakini kulikuwa na mtu mmoja aliyemfanya Mungu kutabasamu. Biblia inasema, “Nuhu alimfurahisha Bwana.” Mwanzo 6:8 (LB)

Mungu alisema, “Mtu huyu ananiletea furaha. Hunifanya nitabasamu. Nitaanza upya na jamaa yake.” Kwa sababu Nuhu alileta furaha kwa Mungu, ndiyo maana mimi na wewe tupo leo. Kutokana na maisha yake tunajifunza matendo ya ibada yanayomfanaya Mungu atabasamu.

Mungu hutabasamu tunapompenda kuliko vyote. Nuhu alimpenda Mungu kuliko kitu chochote duniani, hata kama hapakuwa na mwingine yeyote aliyefanya hivyo! Biblia inatuambia kwamba kwa maisha yake yote, “Nuhu siku zote alifuata mapenzi ya Mungu na kufurahia uhusiano wa karibu naye.” Mwanzo 6:9 (NLT)

Hiki ndicho Mungu anachokitaka kwako kuliko vyote: Uhusiano! Ni ukweli wa ajabu duniani – kwamba Muumba wetu anapenda kuwa na ushirika na sisi. Mungu alikuumba ili akupende, na anatamani na wewe umpende. Anasema, “Sitaki dhabihu zenu – nataka upendo wenu; Sitaki sadaka zenu – nataka mnifahamu.” Hosea 6:6 (LB)

Je unaweza kuona nia ya Mungu katika kifungu hiki? Mungu anakupenda kwa kina na anatamani umpende. Anatamani umjue na utumie muda pamoja naye. Ndigyo maana kujifunza kumpenda Mungu na kupendwa naye linapaswa liwe lengo lako kubwa la maisha. Hakuna kinachokaribia lengo hili katika umuhimu. Yesu aliliita amri kuu kupita zote. Alisema, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri kuu naya kwanza.” Mathayo 22:37-38 (NIV)

文字方塊: Mungu anachotaka zaidi kwako ni uhsiano.Mungu hutabasamu tunapomwamini kabisa. Sababu ya pili Nuhu alimpendeza Mungu ni kwamba alimtumaini Mungu, hata pale ambapo hapakuleta maana yoyote. Biblia inasema, “Kwa imani, Nuhu alijenga meli katikati ya nchi kavu. Alionywa juu ya jambo ambalo hakuliona, na akatenda kama alivyoagizwa …. Matokeo yake, Nuhu akawa karibu sana na Mungu.” Waebrania 11:6 (NIV)

Jaribu kukisia tukio hili: siku moja Mungu anakuja kwa Nuhu kumwambia, “Nimekatishwa tamaa na wandamu. Dunia nzima, isipokuwa wewe, hakuna anayenifikiria. Lakini Nuhu, ninapokuangalia, naanza kutabasamu. Nimefurahishwa na maisha yako, hivyo nakwenda kuugharikisha ulimwengu mzima na kuanza upya na jamaa yako. Nakutaka ujenge meli kubwa ambayo itawaokoa ninyi pamoja na wanyama.”

Kulikuwa na matatizo matatu ambayo yangemfanya Nuhu kuwa na mashaka. Kwanza, Nuhu alikuwa hajaona mvua, kwa sababu kabla ya gharika, Mungu alinyeshea ardhi kutoka chini kwenda juu. Mwanzo 2: 5-6 Pili, Nuhu aliishi mamia ya maili kutoka bahari ya karibu. Hata kama angejifunza kutengeneza meli, angeipelekaje majini? Tatu kulikuwa na tatizo la kuwapata wanyama wote hao na kuwatunza. Lakini Nuhu hakulalamika wala kutoa udhuru. Alimtumaini Mungu kabisa, na hicho kilimfanya Mungu kutabasamu.

Kumwamini Mungu kabisa maana yake ni kuwa na Imani kwamba yeye anajua kilicho bora kwa maisha yako. Unamtengemea kuwa atatimiza ahadi zake, atakusaidia katika matatizo, na afanye yasiyowezekana inapobidi. Biblia inasema, “Anawafurahisha wale wanaomheshimu; wale wanaoamini upendo wake wa daima.” Zaburi 147:11 (TEV)

Iimchukua Nuhu miaka 120 kujenga safina. Nahisi alikabiliwa na siku nyingi za kukatisha tamaa. Bila dalili yoyote ya mvua mwaka hadi mwaka, alichekwa na kudharauliwa kama “Mtu punguani anayefikiri Mungu anasema naye.” Nafikiri watoto wa Nuhu waliudhiwa mara nyingi na lile meli kubwa lilipojengwa uwanjani mwao. Lakini Nuhu alidumu kumwamini Mungu.

Je, ni eneo gani la maisha yako unahitaji kumwamini Mungu kabisa? Kuamini ni tendo la kuabudu. Kama vile wazazi wanavyofurahi watoto wao wanapoamini pendo na hekima yao, Imani yako humfanya Mungu afurahi. Biblia inasema, “Pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu.” Waebrania 11:6 (NIV)

Mungu hutabasamu tunapomtii kwa moyo wote. Ili kuokoa wanyama wa aina zote duniani kutoka kwenye gharika la dunia nzima kulihitaji uangalifu mkubwa katika utekelezfaji na maelekezo ya kina. Kila kitu kilipaswa kifanywe kama Mungu alivyoagiza. Mungu hakusema, “Nuhu jenga safina yoyote unayopenda.” Alitoa maelekezo ya kina kuhusu ukubwa, umbo, na vifaa vya kujengea safina pamoja na idadi mbalimbali ya wanyama wa kuletwa ndani ya safina. Biblia hutuelezea juu ya mwitikio wa Nuhu: “Hivyo Nuhu alifanya kila kitu kama Mungu alivyomwagiza.” Mwanzo 6:22 (NLT); Waebrania 11:7b (NCV)

Angalia ambavyo Nuhu alitii kabisa (Hakuacha agizo hata moja), na alitii kama alivyoagizwa (kwa namna na wakati Mungu alivyotaka ifanyike). Hii ni kwa moyo wote. Haishangazi kwamba Mungu alitabasamu kwa Nuhu.

Kama Mungu angekueleza ujenge meli kubwa, hufikiri kwamba ungekuwa na mswali kadhaa, upinzani, au kusita? Nuhu hakuwa hivyo. Alimtii Mungu kwa moyo wote. Hii ina maana kufanya yale yote Mungu anavyosema bila kusubiri au kusita. Hupaswi kuahirisha kwa kusema, “nitaliombea jambo hili”. Fanya bila kuchelewa. Kila mzazi anafahamu kwamba kuchelewa kutii ni kutokuwa na utii (uasi kamili).

文字方塊: Kumwamini Mungu kabisa maana yake ni kuwa na Imani ya kwamba yeye anajua kilicho bora kwa maisha yakoMungu hahitaji kutoa sababu au kujieleza kwako kwa alivyokuagiza kufanya. Kufahamu kunawezi kusubiri, lakini huwezi kungoja kutii. Utii wa mara moja unakufundisha kuhusu Mungu kuliko majadiliano ya Biblia kwa maisha yako yote. Hakika huwezi kuelewa baadhi ya maagizo mpaka uyatii kwanza. Utii hufungua ufahamu.

Mara nyingi tunajaribu kumpa Mungu nusu utii. Tunataka kuchagua maagizo ya kutii tuna fanya orodha ya maagizo tunayopenda kutii na tunayaacha yale tunayodhani hayafai, magumu, ya gharama, au hayakubaliki na wengi. Nitahudhuria kanisani lakini sitatoa fungu la kumi. Nitasoma Biblia yangu lakini sitamsamehe mtu aliyenikosea. Lakini kutii nusu ni kutotii.

Kutii kwa moyo wote kunafanywa kwa furaha, na moyo wa kupenda. Biblia inasema, “Mtii BWANA kwa furaha.” Zaburi 100:2 (LB) Hii ndiyo ilikuwa nia ya Daudi: “Niambie cha kufanya nami nitatenda, Bwana. Kwa siku zote nitakazoishi nitakutii kwa moyo wote.” Zaburi 119:33 (LB)

Yakobo, akiwaeleza Wakristo, alisema, “Tunampendeza Mungu kwa yale tuyafanyayo na siyo tu kwa yale tuyaaminiyo.” Yakobo 2:24 (CEV) Neno la Mungu liko wazi kwamba mtu huwezi kupata wokovu kwa nguva zako. Hupatikana tu kwa neema, si nguvu zako. Lakini kama mtoto wa Mungu unavyoweza kuleta furaha kwa Baba yako wa mbinguni kwa kutii.

Tendo lolote la utii ni tendi la kuabudu pia. Kwa nini utii ni jambo linalopendeza sana kwa Mungu? Kwa sababu hii huthibitisha kweli unampenda Mungu. Yesu alisema, “Kama mnanipenda, mtatii amri zangu.” Yohana 14:15 (TEV)

Mungu hutabasamu tunapomsifu na kumshukuru daima. Ni vitu vichache hufurahisha kuliko kupokea sifa na shukrani toka kwa mtu mwingine. Mungu hupenda jambo hili pia. Yeye hutabasamu tunapoonyesha ibada na shukrani kwake.

Maisha ya Nuhu yalileta furaha kwa Mungu kwa sababu aliishi na moyo wa sifa na shukrani. Tendo la kwanza la Nuhu baada ya gharika lilikuwa kuonyesha shukrani kwa Mungu kwa kutoa dhabihu. Biblia inasema, “Kisha Nuhu alijenga madhabahu kwa ajili ya BWAMA ….. na akatoa sadaka ya kuteketezwa juu yake.” Zaburi 116:17 (KJV)

Kwa sababu ya sadaka ya Yesu, hatutoi sadaka za wanyama kama alivyofanya Nuhu. Badala yake tunaambiwa kumtolea Mungu “dhabihuza sifa” Waebrania 13:15 (KJV) na “dhabihu za shukrani.” Zaburi 116:17 (KJV)

Tunamsifu Mungu kwa vile alivyo, na tunamshukuru kwa yale anayoyafanya. Daudi alisema, “Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo na kumtukuza kwa shukrani. Hili litampendeza Bwana.” Zaburi 69:30-31 (NIV)

Jambo la ajabu hutokea tunapotoa sifa na shukrani kwa Mungu. Tunapompa Mungu furaha, mioyo yetu inajawa na furaha!

Mama yangu alipenda kunipikia. Hata baada ya kumwoa Kay, tulipowatembelea wazazi, mama alituandalia karamu safi sana. Moja ya mambo yaliyomfurahisha maishani ilikuwa ni kutuona sisi watoto wake tukila na kufurahia chakula alichokiandaa. Kadiri tulivyofurahia, ndivyo furaha yake ilivyoongezeka.

Lakini sisi pia tulifurahia kumpendeza mama kwa kuonyesha kukifurahia chakula chake. Ilifanyika kwa pande zote mbili. Nilipokula ule mlo safi, nilikisifia na kumsifu mama pia. Nilikusudia si kukifurahia chakula tu, lakini kumfurahisha mama pia. Kila mmoja alikuwa na furaha.

Kuabudu kunahusisha pande mbili pia. Tunafurahia kile Mungu ametutendea, na tunapoonyesha furaha hiyo kwa Mungu, humletea furaha – lakini pia huongeza furaha yetu. Kitabu cha Zaburi kinasema, “Wenye haki wanafuraha, na wanashangilia katika uwepo wake; wanafuraha na wanapiga kelele za shangwe.” Zaburi 68:3(TEV)

Mungu hutabasamu tunapotumia uwezo wetu. Baada ya gharika, Mungu alimpa Nuhu maagizo rahisi: “Zaeni mkaongezeke na mkaijaze nchi …. Kila kilicho hai na kiendacho katika nchi kitakuwa chakula chenu. Kama nilivyowapa mimea, sasa nawapa kila kitu.” Mwanzo 9:1-3 (NIV)

Mungu alisema, “Ni wakati wa kuendelea na maisha yenu! Fanyeni mambo niliyowaambia wanadamu kufanya. Lala na mwenzi wa ndoa. Zaeni watoto. Mtunze jamaa. Pandeni mazao na kula chakula. Iweni wanadamu! Ndivyo nilivyowaumba muwe!”

Unaweza kuhisi kwamba muda pekee anaokufurahia Mungu ni pale unapofanya mambo ya “kiroho” – kama kusoma Biblia, kwenda kanisani, kusali, au kuwaeleza watu wengine Imani yako. Na unaweza kufikiri kwamba Mungu hahusiki na mambo mengine ya maisha yako. Hakika, Mungu anafurahi kuona 文字方塊: Bwana hufurahia kuona kila jambo katika maisha yako.kila jambo katika maisha yako, iwe kazini, kucheza, kupumzika, au kula. Hakosi kuhusika na chochote kile unachokifanya. Biblia inatuambia, “Hatua za wenye haki zinaongozwa na BWANA. Hupendezwa kila jambo katika maisha yao.” Zaburi 37:23 (NLT)

Kila kazi ya binadamu, isipokuwa dhambi, yaweza kufanywa kwa ajili ya furaha ya Mungu hasa kama kukuona ukitumia karama na uwezo aliokupa. Unaweza kuosha vyombo, kurekebisha mtambo, uza kitu, andika ratiba ya kompyuta, kuuza zao, na lea jamaa kwa utukufu wa Mungu.

Kama mzazi aonaye furaha kwa mwanae, Mungu hufurahia sana akikuona ukivitumia vipawa na uwezo aliokupa. Kwa makusudi alitupa vipawa mbalimbali kwa ajili ya furaha yake. Wengine amewafanya wakimbiaji na wengine watafiti. Unaweza kuwa umepewa kipawa cha ufundi au hisabati au muziki au maelfu ya vipawa vingine. Vipawa vyote hivi vinaweza kuleta tabasamu kwenye uso wa Mungu. Biblia inasema, “Amemuumba kila mtu kwa zamu; sasa anaangalia kila kitu tunachokifanya.” Zaburi 33:15 (Msg)

文字方塊: SIKU YA TISA:
NINI KINAMFANYA MUNGU ATABASAMUMtu huwezi kuleta furaha au utukufu kwa Mungu kwa kuficha vipawa vyako au kwa kujaribu kuwa mwingine. Unamletea furaha pale tu unapokuwa wewe. Wakati wowote unapokataa sehemu yoyote uliyonayo, unakataa hekima ya Mungu na utawala wake katika kukuumba. Mungu anasema, “Huna haki ya kubishana na Muumba wako. Wewe ni chombo cha udongo wa mfinyanzi kilichotengenezwa na mfinyanzi. Udongo hauulizi, ‘Kwa nini umenitengeneza namna hii?’” Isaya 45:9 (CEV)

Katika filamu iitwayo Chariots of Fire, mkimbiaji wa Olimpiki aitwaye Eric Liddell anasema, “Mungu aliniumba kwa malengo, lakini aliniumba mwepesi na ninapokimbia, nahisi furaha ya Mungu.” Baadaye anasema, “kuacha kukimbia ingekuwa kumsaiti.” Hakuna vipawa visivyo vya kiroho, labda vinavyotumiwa vibaya. Anza kutumia vipawa ulivyo navyo kwa ajili ya furaha ya Mungu.

Mungu pia hufurahi anapokuona unafurahia uumbaji wake. Alikupa macho ili ufurahie uzuri, masikio ufurahie sauti, pua yako na ulimi uweze kufurahia harufu na kuonja, na mishipa ya fahamu chini ya ngozi yako ili ufurahie mguso. Kila tendo la kufurahia huwa tendo la kuabudu unapomshukuru Mungu kwa ajili yake. Kwa kweli, Biblia inasema, “Mungu … Kwa ukarimu hutupatia kila kitu ili tufurahie.” 1 Timotheo 6:17 (TEV)

Mungu anafurahia hata kukuona umelala! Watoto wangu walipokuwa wadogo, nakumbuka utoshelevu wa kina nilioupata kwa kuona wamelala. Wakati mwingine siku hiyo ilikuwa imejaa matatizo na kutotii, lakini wakiwa wamelala walionekana wametosheka, salama, na wenye amani, na nilikumbushwa kiasi gani ninavyowapenda.

Watoto wangu hawakuhitaji kufanya chochote ili niwapende. Nilikuwa na furaha ile kuwaona tu wakipumua, kwa sababu niliwapenda sana. Kadiri vifua vyao vidogo vilivyopanda na kutelemka, nilitabasamu, na wakati mwingine machozi ya furaha yalijaza macho yangu. Unapokuwa umelala, Mungu hukutazama kwa upendo kwasababu ulitokana na mawazo yake. Anakupenda kama vile ni wewe peke yako dunia nzima hakuna mtu. 

Wazazi hawahitaji watoto wao kuwa wakamilifu, au kupevuka, ili kuwafurahia. Wanawafurahia katika kila hatua ya kukua kwao. Vivyo hivyo, Mungu hasubiri wewe ufikie kupevuka kabla ya kuanza kukupenda. Anakupenda na anakufurahia katika kila hatua ya kukua kwako kiroho.

Inawezekana umewahi kuwa na walimu au wazazi wasiofurahia katika kukua kwako. Tafadhali usifikiri Mungu naye yuko hivyo juu yako. Anajua huna uwezo wa kuwa mkamilifu au bila dhambi. Biblia inasema, “Anajua bila shaka sisi tumetengenezwa na nini. Anajua moyoni mwake kuwa sisis tu mavumbi.” Zaburi 103:14 (GWT)

Mungu anachokitazama ni nia ya moyo wako: Je, kumpendeza yeye ndiyo nia yako kubwa? Hili ndilo lilikuwa lengo la Paulo maishani: “Zaidi ya chochote kile, walakini, tunataka kumpendeza Yeye, iwe katika maskani yetu hapa au kule.         2 Wakorintho 5:9 (TEV) Unapoishi katika nuru ya umilele, mtazamo wako unabadilika kutoka “Ni kiasi gani cha furaha ninakipata maishani?” kwenda “Je, Mungu anapata kiasi gani cha furaha kutoka maishani mwangu?”

Mungu anatafuta watu kama Nuhu katika karne hii ya ishirini na moja – watu walio tayari kuishi kwa ajili ya furaha ya Mungu. Biblia inasema, “Mungu anatazama chini kutoka mbinguni ili aone kama kuna watu wenye hekima, wanaotaka kumpendeza Mungu.” Zaburi 14:2 (LB)

Je, utafanya kumpendeza Mungu liwe lengo lako la maisha? Hakuna chochote ambacho Mungu hawezi kumfanyia mtu ambaye amejitosheleza kabisa kutimiza lengo hili.


文字方塊: SIKU YA TISA
KUFIKIRI JUU YA LENGO LANGU
Jambo la Kutafakari: Mungu hutabasamu ninapomwamini.
Kifungu cha Kukumbuka: “Bwana anawafurahia wale wanaomwabudu na kuliamini pendo lake.” Zaburi 147:11 (CEV)
Swali la Kujiuliza: Kwa kuwa Mungu anajua kilicho bora, je ni katika maeneo gani ya maisha yangu nahitaji kumwamini zaidi?
 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Siku ya Kumi: Kiini Cha Kuabudu

Jikabidhini kwa Mungu …

Jisalimisheni utu wenu kwake ili mpate kutumiwa kwa malengo ya haki.

Warumi 6:13 (NLT)

Kiini cha kuabudu ni kujisalimisha.

Ni neno lisilotumiwa sana, halipendwi kama vile neno kunyenyekea. Lina maana ya kupoteza, na hakuna mtu yeyote anapenda kupoteza. Kujisalimisha kunaonyesha picha isiyopendeza ya kukubalika kushindwa katika vita, kupoteza katika michezo, au kukubali kushindwa na mpinzani mwenye nguvu zaidi. Neno hili linatumiwa mara nyingi katika hali isiyokubalika. Wahalifu waliotekwa hujisalimisha kwa mamlaka.

Katika mila ya leo ya ushindani tunafundishwa kutokuacha au kutokukubali tu – hivyo hatusikii sana kuhusu kujisalimisha. Kama kushinda ndiyo kila kitu, basi kujisalimisha hakupo. Labda tuongelee kushinda, kufanikiwa, kuzidi nguvu na kushinda vita kuliko kujitoa, kunyenyekea, kutii, na kujisalimisha. Lakini kujisalimisha ni kiini cha kuabudu. Ni mwitikio wa asili wa huruma na upendo wa ajabu wa Mungu.Tunajitoa nafsis zetu kwake, si kwa hofu au kwa kuwa ni wajibu, lakini kwa upendo, “kwa sababu alitupenda kwanza.” 1 Yohana 4:9-10, 19

Baada ya kutumia sura kumi na moja za kitabu cha Warumi kuelezea neema kuu ya Mungu wetu, Paulo anatusihi tujisalimishe maisha yetu yote kwa Mungu kwa kuabudu. “Hivyo basi ,ndugu zangu, kwa sababu ya rehema kuu ya Mungu Kwetu … Jitoeni nafsi zenu kama dhabihu hai kwa Mungu, ilivyowekwa wakfu kwa utumishi wake na yenye kumpendeza. Hii ndiyo ibada ya kweli mnayopaswa kutoa.” Warumi 12:1 (TEV)

Ibada ya kweli yenye kuleta furaha kwa Mungu hutokea unapojitoa kikamilifu kwa Mungu. Angalia neno la kwanza na la mwisho katika kifungu hicho yanafanana: kutoa.

Kujitoa kwa Mungu ndiyo kuabudu hasa.

Kujitoa nafsi yako kwa Mungu ndiyo kuabudu hasa

Tendo hili la kujisalimisha binafsi linaitwa kwa majina mengi: kujiweka wakfu, kumfanya Yesu Bwana wako, kuchukua msalaba wako, kuifisha nafsi, kujitoa kwa Roho mtakatifu. Cha muhimu hapa ni kwamba ulitende, siyo linaitwaje. Mungu anapenda maisha yako – yote kabisa. Asilimia tisini na tano haitoshi.

Kuna vizuizi vitatu ambavyo huzuia kujisalimisha kwetu kikamilifu kwa Mungu. Hatuelewi kiasi gani Mungu anatupenda, tunataka kutawala maisha yetu wenyewe, na tunashindwa kuelewa maana ya kujisalimisha.

Je, naweza kumwamini Mungu? Imani ni jambo muhimu katika kujisalimisha. Huwezi kujisalimisha kwa Mungu mpaka uwe unamwamini, lakini huwezi kumwamini Mungu mpaka umfahamu vyema. Hofu hutuzuia kujisalimisha, lakini upendo huondoa hofu yote. Kadiri unavyotambua jinsi Mungu anavyokupenda, ndivyo kujisalimisha kunavyokuwa rahisi.

Je unajuaje Mungu anakupenda? Anakupa ushahidi mwingi: Mungu anasema anakupenda; hautoki kwenye uangalizi wake kamwe; Zaburi 145:9 hautoki kwenye uangalizi wake kamwe; Zaburi 139:3 yeye anayaangalia mambo yote ya maisha yako; Mathayo 10:30 alikupa uwezo wa kufurahia aina zote za viburudisho; 1 Timotheo 6:17b ana mpango mzuri kwa ajili ya maisha yako; Yeremia 29:11 yeye hukusamehe; Zaburi 86:5 na kwa upendo anakuvumilia; Zaburi 145:8 Mungu anakupenda kiasi kisichopimika kuliko unavyoweza kufikiri.

Uthibitisho wa ukweli huu ni dhabihu ya mwana wa Mungu kwa ajili yako. “Mungu aliuthibitisha upendo wake kwetu kwa vile tulipokuwa tungali wenye dhambi Kristo alitufia.” Warumi 5:8 (NRSV) Kama unataka kufahamu uthamani wako mbele za Mungu, mwangalie Yesu Kristo na mikono yake iliyowambwa msalabani, akisema“nakupenda sana! Bora nife kuliko kukukosa.”

Mungu siyo kiongozi katili wa msafara wa watumwa au mchokozi anayetumia mabavu kutulazimisha tumtii. Hajaribu kuvunja utashi wetu, lakini hutusihi ili tujitoe wenyewe kwake kwa kupenda. Mungu ni mpendwa na mkombozi, na kujisalimisha kwake huleta uhuru, siyo utumwa. Tunapojisalimisha kwa Yesu kikamilifu, tunagundua kwamba yeye si mtawala wa imla, lakini ni mwokozi; siyo bwana mkubwa, lakini ndugu; si mtawala wa imla, lakini rafiki.

Kukubali mipaka yetu. Kikwazo kingine cha kujisalimisha kikamilifu ni majivuno yetu. Hatukubali kwamba sisi ni viumbe tu na kwamba hatuna utawala na kwamba hatuna utawala juu ya kila kitu. Hili ni jaribu kila zamani; mtakuwa kama Mungu, Mwanzo 3:5 tamaa hiyo ya kuwa na utawala juu ya kila kitu ni chanzo cha matatizo mengi katika maisha yetu. Maisha ni mapambano, lakini jambo ambalo watu wengi hawaelewi ni kwamba mapambano yetu kama yale ya Yakobo hakika ni mapambano na Mungu! Tunataka kuwa sawa na Mungu, na haitawezena sisi kushinda pambano hilo.

SIKU YA KUMI:

MOYO WA KUABUDU

A.W. Tower alisema, “Sababu kwa nini watu wengi bado wanasumbuka, bado wanatafuta, bado wanafanya maendeleo kidogo ni kwa vile bado hawajafikia mwisho wao wenyewe. Bado tunajaribu kuamuru na kuingilia kazi ya Mungu ndani yetu.”

Sisi sio Mungu na hatutakuwa kamwe. Sisi ni wanadamu. Ni pale tunapojaribu kuwa Mungu ndipo tunaishia kuwa kama Shetani kabisa, ambaye alitamani jambo hilo hilo.

Tunakubali ubinadamu wetu kiakili lakini siyo kihisia. Tunapokabiliwa na mapungufu yetu, ndipo tunaonyesha uchungu, hasira na chuki. Tunataka kuwa warefu (au wafupi), wenye akili, wenye nguvu, wenye vipawa, warembo, na matajiri. Tunataka kuwa na kila kitu na kufanya kila kitu na tunakata tamaa inaposhindikana. Kisha tunatambua kwamba Mungu aliwapa watu wengine vipawa ambavyo sisi hatuna, na hivyo tunapatwa husuda, wivu, na kujisikitikia.

Maana ya kujisalimisha. Kujisalimisha kwa Mungu si kujiuzulu na kukaa tu kusubiri, au kuamini kuwa yote yameandikwa binadamu hana hiari, au kuwa na udhuru na wivu. Siyo kukubali hali hiyo hiyo uliyo nayo. Inaweza kumaanisha kinyume cha haya; kujitoa sadaka maisha yako au kuteseka ili kubadilisha yanayohitajika kubadilishwa. Mara nyingi Mungu huwaita watu waliojisalimisha kwake kupiga vita kwa jina lake. Kujisalimisha sio kwa uoga au mazulia. Vivyo hivyo haimaanishi kuacha kutumia akili katika kufikiri. Mungu asingependaa kupoteza akili alizokupa! Mungu hapendi watu wawe kama mitambo (robots) ili kumtumikia. Kujisalimisha siyo kukomesha utu wako. Badala ya kukomesha utu wako, kujisalimisha hutia nguvu. C. S. Lewis alisema, “Kadiri tunavyomruhusu Mungu atutawale ndivyo tunavyozidi kuwa sisi wenyewe – kwa sababu yeye ndiye aliyetuumba. Alibuni namna mbalimbali za watu wote tofauti ambao mimi na wewe tulikusudiwa kuwa .… Ni pale ninapomgeukia Kristo, ninapojikabidhi nafsi yangu kwake, ndipo ninapokuwa na ule utu wangu halisi.”

Kujisalimisha kunadhihirika vyema katika utii. Unasema “ndivyo, Bwana” Kwa chochote anachokueleza. Kusema “hapana, Bwana” ni kutamka kinyume. Hatuwezi kumwita Yesu Bwana na wakati huo huo hatutaki kumtii. Baada ya usiku kucha bila kupata samaki, Simioni alionyesha kujisalimisha pale Yesu alipomwambia kujaribu tena: “Bwana tumefanya kazi kwa bidi usiku wote na hatujakamata samaki yeyote. Lakini kwa sababu umesema, nitatia nyavu majini.” Luka 5:5 (NIV) Watu waliojisalimisha hutii neno la Mungu hata kama linaonekana kutokuwa na maana.

Jambo jingine katika kujisalimisha ni Imani. Ibrahimu alifuata maelekezo ya Mungu bila kujua alikokuwa akienda. Hana alisubiri wakati wa Mungu bila kujua ni lini. Mariamu alitarajia muujiza bila kufahamu utatendekaje. Yusufu aliamini lengo la Mungu bila kujua kwa nini mazingira yalikuwa hivyo. Kila mmoja wa watu hawa alikuwa amejisalimisha kwa Mungu kwelikweli.

Utafahamu umejisalimisha kwa Mungu unapomtegemea Mungu akutengenezee mambo yako badala ya kujaribu kuwafanyia hila wengine, ukapitisha jambo lako, na mwisho ukatawala mazingira hayo. Unamwachia Mungu afanye, huhitaji wakati wote kuwa “mwangalizi”. Biblia inasema, “Jisalimishe nafsi yako kwa Bwana, na umsubiri kwa uvumilivu.” Zaburi 37:7a (GWT) baada ya kujaribu sana, umwamini zaidi. Pia unafahamu kwamba unajisalimisha unapokua huchukizwi na lawama na kukimbilia kujitetea. Mioyo iliyojisalimisha huonyesha mahusiano mazuri na wengine. Huwatupilii mbali wengine, hudai haki zako, na hutumikii nafsi yako kama umejisalimisha.

Eneo gumusana kwa watu wengi kujisalimisha ni pesa zao. Wengi wamefikiri, “Nataka kuishi kwa ajili ya Mungu lakini pia nataka kupata pesa nyingi ili niishi kwa raha baadaye nipumzike.” Kupumzika siyo lengo la maisha ya kujisalimisha, kwa sababu huku ni kushindana na Mungu kwa sababu ya kuweka mkazo kwanza kwa maisha yetu. Yesu alisema, “Huwezi kutumikia Mungu na pesa” Mathayo 6:24 na kwamba “Popote hazina yako ilipo ndipo na moyo wako uko.” Mathayo 6:21

Kielelezo kikubwa cha kujisalimisha ni Yesu. Usiku ule kabla ya mateso Yesu alijisalimisha kwa mpango wa mpango wa Mungu. Alisali, “Baba Kila kitu kinawezekana kwako. Tafadhali niondolee kikombe hiki cha mateso. Lakini nataka mapenzi yako, siyo yangu.” Marko 14:36 (NLT)

Kujisalimisha kunadhihirika vyema katika utii na Imani.

Yesu hakuomba, “Baba, kama unaweza kuniondolea maumivu haya, tafadhali fanya hivyo.” Alikuwa tayari amethibitisha kuwa Mungu ana uwezo kufanya lolote! Badala yake aliomba, “Mungu, kama inapendeza kwako kuniondolea mateso haya, tafadhali fanya hivyo. Lakini kama yanatimiza kusudi lako, ndivyo ninavyotaka pia.”

Kujisalimisha halisi husema, “Baba, kama tatizo hili, maumivu, ugonjwa, au hali yoyote inahitajika kutimiza lengo lako na utukufu kwako katika maisha yangu au ya mwingine, tafadhali usiliondoe.” Kiwango hiki cha ukomavu hakiji kwa urahisi. Kwa upande wa Yesu, aliugua sana kuhusu mpango wa Mungu kiasi cha kutoa jasho la damu. Kwa upande wetu, ni vita kali dhidi ya asili yetu ya ubinafsi.

Baraka za kujisalimisha. Biblia iko wazi kabisa kuhusu unavyoweza kufaidika unapojisalimisha kikamilifu kwa Mungu. Kwanza, unapata amani: “Acha kugombana na Mungu! Ukikubaliana naye, utapata amani hatimaye, na mambo yatakunyookea.” Ayubu 22:21 (NLT) Pili, unapata uhuru: “Jitoeni nafsi zenu kuzifuata njia za Mungu na uhuru hautatoka kamwe … Amri zake zinawaweka huru kuishi kwa uwazi katika uhuru wake!” Warumi 6:17 (Msg) Tatu, unapata nguvu za Mungu katika maisha yako. Majaribu makali na matatizo mazito yanaweza kushindwa na Kristo kama atakabidhiwa.

Joshua alipoviendea vita vile vikubwa maishani mwake, Yoshua 5:13-15 alikutana na Mungu, akamsujudia, na akasalimisha mipango yake. Kujisalimisha huko kulileta ushindi mkubwa pale Yeriko. Hiki ni kitendawili: Ushindi huja kwa kujisalimisha, kujisalimisha hakukudhoofishi wewe; kunakutia nguvu. Jisalimishe kwa Mungu, hauhitaji kuogopa au kujisalimisha kwa chochote kile. William Booth, mwanzilishi wa Jeshi la wokovu, alisema, “ukuu wa nguvu za ubinadamu unapimwa kwa kiwango chake cha kujisalimisha.”

Watu waliojisalimisha ndio Mungu anaowatumia. Mungu alimchagua Mariamu kuwa mama wa Yesu, siyo kwa sababu alikuwa na kipawa, utajiri au uzuri wa umbile, lakini kwa sababu alikuwa amejitoa kikamilifu kwake. Malaika wa Bwana alipomwelezea mpango mgumu wa Mungu, alijibu kwa upole, “Mimi ni mjakazi wa Bwana, na niko tayari kupokea chochote anachotaka.” Luka 1:38 (NLT) Hakuna kitu kikubwa kama maisha ya kujisalimisha katika mikono ya Mungu. “Hivyo zikabidhini nafsi zenu kikamilifu katika mikono ya mungu.” Yakobo 4:7a (NCV)

Kujisalimisha sio njia bora ya kuishi. Ndiyo njia ya pekee ya kuishi. Hakuna nyingine inayoleta ufanisi.

Njia bora ya kuishi. Kila mtu hatimaye hujisalimisha kwa mtu au kitu Fulani. Kama sio kwa Mungu, utajisalimisha kwa matarajio au maoni ya watu wengine, au pesa, chuki, hofu, au kwa kiburi chako au tamaa mbaya, au ubinafsi. Ulibuniwa kumwabudu Mungu – na kama utashindwa kumwabudu, utatengeneza vitu vingine (sanamu) ili uvipe maisha yako. Unao uhuru wa kuchagua usalimishe maisha yako, lakini hauko huru na mtokeo ya uchuguzi huo. E. Stanly Jones alisema, “kama hutajisalimisha kwa Kristo, utajisalimisha kwa machafuko.”

Kujisalimisha si nijia bora ya kuishi; ni njia pekee ya kuishi. Hakuna kitu kingine cha kukufanikisha. Njia nyingine zote hukuongoza kwenye kukukatisha tamaa, na kuiangamiza nafsi. Tafsiri ya King James huita kujisalimisha “ ibada yenu yenye maana.” Warumi 12:1 (KJV) Tafsiri nyingine inasema, njia yenye maana zaidi ya kumtumikia Mungu.” Warumi 12:1 (CEV) Kusalimisha maisha yako si hisia za kipumbavu lakini nitendola akili na busara ambalo unaweza kulifanya kwa ajili ya maisha yako. Ndiyo maana Paulo alisema, “Ni lengo letu kwamba tumpendeze yeye.” 2 Korintho 5:9 (NIV) Nyakati zako za busara zitakuwa zile ambazo unasema ndiyo kwa Mungu.

Wakati mwingine huchukua miaka, lakini hatimaye unagundua kwamba kizuizi kikubwa kwa baraka zaMungu maishani mwako sio watu wengine, ni wewe mwenyewe – matakwa yako binafsi, kiburi cha hali ya juu, na matarajio yako. Huwezi kutimiza lengo la Mungu kwa maisha yako huku ukikazania malengo yako binafsi.

Kama Mungu ataenda kufanya kazi ya kina ndani yako, itaanza hivyo. Kwa hiyo mpe yote Mungu: kushindwa kwako hapo nyuma, matatizo yako ya sasa, matarajio yako ya mbele, hofu zako, ndoto, udhaifu, tabia, maumivu, na madhara yoyote uliyo nayo. Mweke Yesu katika kiti cha dereva wa maisha yako na uondoe mikono yako toka kwenye usukani. Usiopope; hakuna chochote katika uongozi wake kinaweza kupoteza dira. Chini ya uongozi kwa Kristo unaweza kumudu chochote. Utakuwa kama Paulo, “Niko tayari kwa lolote na kuwa sawa na chochote kwa njia yayeye anayetia nguvu ndani yangu, yaani, ninajitosheleza katika utoshelevu wa Kristo.” Wafilipi 4:13 (Amp)

Kujisalimisha kwa Paulo kulitokea katika njia ya Dameski alipoangushuwa chini na mwanga mkali uliompofusha. Kwa watu wengine, Mungu anapata mwitikio wetu bila kutumia njia ya ajabu sana. Pamoja na hayo, kujisalimisha siyo tukio la wakati mmoja tu. Paulo alisema, “Nakufa kila siku.”1 Wakorintho 15:31 Kuna wakati wa kujisalimisha, na kuna tendo la kujisalimisha, ambalo ni la muda-hadi-muda na maisha zote. Tatizo la sadaka iliyo hai ni kwamba inaweza kutambaa na kutoka madhabahuni, hivyo unaweza kutakiwa kujisalimisha hata mara hamsini kwa siku. Ni lazima ufanye jambo hili kuwa tabia yako ya kila siku. Yesu alisema, “Kama watu wanapenda kunifuata ni lazima waache mambo wanayoyapenda. Lazima wawe tayari kuacha maisha yao kila siku na kunifuata.” Luka 9:23 (NCV)

Ngoja nikuonye: unapoamua kuishi maisha ya kujisalimisha kikamilifu, uamuzi huo utapimwa. Wakati mwingine itamaanisha kufanya mambo yasiyostahili, ya gharama, au yanayoonekana hayawezekani. Mara nyingi itamaanisha kufanya kinyume cha unavyojisikia kufanya.

Mmoja wa viongozi wakuu wa Kikristo wa karne ya ishirini alikuwa Bill Bright, mwanzilishi wa Campus Crusade for Christ. Kwa kupitia watumishi wa shirika hili duniani pote, kipeperushi cha sheria nne za kiroho, na filamu ya Yesu (iliyoonwa na watu zaidi ya billioni nne), zaidi ya watu milioni 150 wamekuja kwa Yesu na watatumia umilele mbinguni.

Siku moja nilimuuliza Bill, “Kwa nini Mungu anakutumia na kubariki maisha yako kiasi kikubwa hivyo? Alisema, “Nilipokuwa kijana mdogo, nilifanya mkataba na Mungu. Niliandika na kutia sahihi ya jina langu chini yake. Mkatabahuo ulisema, ‘Tangu siku ya leo na kuendelea, mimi ni mtumwa wa Kristo.’”

Je, umewahi kusaini mkataba kama huo na Mungu? Au bado unabishana na kupambana na Mungu juu ya haki yake kufanya lolote apendalo kwa maisha yako? Sasa ni wakati wako kujisalimisha – kwa neema ya Mungu, upendo na hekima yake.

SIKU YAKUMI

KUFIKIRIA JUU YA LENGO LANGU

Jambo la kutafakari: Kiini cha kuabudu ni kujisalimisha.

Kifungu cha Kukumbuka: Jisalimisheni utu wenu wote kwake ili mpate kutumiwa kwa malengo ya haki.        Warumi 6:13b (TEV)

Swali la Kujiuliza: Je, ni eneo gani la maisha yangu bado sijamkabidhi Mungu?

 

 

 

 

 

 

Siku ya Kumi na moja: Kuwa Marafiki Wakubwa Na Mungu

Kwa kuwa tulirejeshwa tena katika urafiki na Mungu kwa kifo cha

Mwana wake tulipokuwa tungali adui zake, bila shaka tutaokolewa

Kutoka hukumu ya milele kwa uzima wake.

Warumi 5:10 (NLT)

Mungu anapenda kuwa rafiki yako mkubwa. Uhusiano wako na Mungu una vipengele vingi mbalimbali: Mungu ni Muumbaji na Mtengenezaji wako, Bwana na Mtawala, Hakimu, Mkombozi, Baba, Mwokozi, na zaidi. (Zaburi 95:6; 136:3; Yohana 13:13; Yuda 1:4; 1 Yohana 3:1; Isaya 33:22; 47:4; Zaburi 89:26). Lakini ukweli wa kushtua ni huu: Mungu mwenyewe anatamani kuwa rafiki yako!

Katika Edeni tunaona uhusiano halisi aliotaka kuwa nao nasi: Adamu na Hawa walifurahia uhusiano wa karibu na Mungu.. Hapakuwa na desturi za ibada wala dini – ulikuwa ni uhusiano rahisi wa upendo kati ya Mungu na watu aliowaumba. Haukuwa na kizuizi cha hatia wala hofu, Adamu na Hawa walipendezwa na Mungu, naye aliwafurahia.

Tuliumbwa ili kuishi katika uwepo wa Mungu daima, lakini baada ya anguko, uhusiano huo mkamilifu ulipotea. Watu wachache tu katika Agano la kale walikuwa na upendeleo wa urafiki na Mungu. Musa na Ibrahimu waliitwa “marafiki wa Mungu” Daudi aliitwa “mtu aliyeupendeza moyo wa Mungu”, na Ayubu, Henoko, na Nuhu walikuwa na urafiki wa karibu na Mungu. (Kutoka 33:11, 17 2Mambo ya Nyakati 20:7; Isaya 33:22; 47:4; Zaburi 89:26). Lakini hofu ya Mungu, siyo urafiki, lilikuwa ni jambo la kawaida katika Agano la Kale.

SIKU YA KUMI NA MOJA

KUWA RAFIKI WAKUBWA WA MUNGU

Kisha Yesu alibadilisha mambo. Alipolipa kwa ajili ya dhambi zetu msalabani,pazia la hekaluni ambalo lilionyesha kutengwa kwetu na Mungu lilipasuka toka juu hadi chini, hii ikiwa ni kuonyesha kwamba sasa haki ya kumwendea Mungu moja kwa moja ilikuwa tena imepatikana.

Tofauti na makuhani wa Agano la Kale ambao walipaswa kutumia masaa kujiandaa kukutana naye, sisi sasa tunaweza kumwendea Mungu saa yoyote. Biblia inasema, “Sasa tunaweza kushangilia katika uhusiano wetu wa ajabu mpya na Mungu – yote hii ikiwa ni kwa sababu yayale aliyofanya Bwana wetu Yesu Kristo kwa ajili yetu kwa kutufanya rafiki wa Mungu.” Warumi 5:11 (NLT)

Urafiki na Mungu unawezekana tu kwa sababu ya neema ya Mungu na sadaka ya Yesu. “Yote haya yamefanywa na Mungu ambaye kwa njia ya Yesus Kristo alitubadilisha kutoka maadui na kuwa marafiki zake.” 2 Wakorintho 5:18a (TEV). Wimbo wa zamani unasema, “Yesu kwetu ni rafiki,” lakini kwa kweli Mungu anatualika tufurahie urafiki na uhusiano na nafsi zotetatu za utatu: Baba(1 Yohana 1:3), Mwana (1Wakorintho 1:9), na Roho Mtakatifu (2Korintho 13:14).

Yesu alisema, “Siwaiti tena watumwa, kwa sababu mtumwa hajui kazi za Bwana wake. Badala yake, ninawaita rafiki, kwa kuwa kila nilichojifunza kwa Baba yangu nimewajulisha.” Yohana 15:15(NIV) Nenorafiki, katika kifungu hikihalimaanishi urafiki wa juu juu lakini ule wa karibu sana, uhusiano wa kuaminika. Neno hilo hilo linatumika kumaanisha msimamizi wa ndoa katika harusi (Yohana 3:29) na watu wa karibu sana na mfalme, rafiki wa kuaminika. Katika nyua za kifalme, watumishi lazima wawe mbali na mfalme, lakini wale marafiki wa karibu yake huwa na ukaribu, humwendea moja kwa moja, na kufahamu taarifa nyeti.

Kwamba Mungu angependa niwe rafiki yake wa karibu ni vigumu kuelewa, lakini Biblia inasema, “Yeye ni Mungu ambaye anatamani uhusiano wake na ninyi.” Kutoka 34:14 (NLT)

Mungu anatamani sana kwamba tumjue kwa ukaribu sana. Kwa hakika, Mungu aliubuni ulimwengu na kuipanga historia, ikiwa ni pamoja na maisha yetu, ili kwamba tuweze kuwa marafiki zake. Biblia inasema, “Aliumba wanadamu wote na akaifanya nchi iweze kukalika, akaweka muda na nafasi vya kutosha kwa kuishi ili tumtafute Mungu, na sio tu tutangatanga gizani lakini tupate kumwona hakika.” Matendo 17:26-27 (Msg)

Kumjua na kumpenda Mungu ni upendeleo mkubwa kwetu, na kujulikana na kupendwa na Mungu ni furaha kubwa kwa Mungu. Mungu anasema, “Kama kuna watu wanaotaka kujisifu, basi wajisifu kwamba wananijua na kunifahamu …. Haya ndio mambo yanifurahishayo.”Yeremia 9:24 (TEV)

Si rahisi kuelewa jinsi uhusiano wa karibu unawezekana kati ya Mungu muweza wa yote, asiyeonekana, mkamilifu na mwanadamu ambaye ni kiumbe kidogo na tena mwenye dhambi. Ni rahisi kuelewa uhusiano wa Bwana na mtumishi au muumba na kiumbe au hata uhusiano wa Baba na mtoto. Lakini ina maana gani Mungu anaponitaka niwe rafiki zake? Kwa kuyachunguza maisha ya marafiki za Mungu katika Biblia, tunajifunza siri sita za urafiki na Mungu. Katika surahii, utaona sura mbili na zile nne tutaziangalia katika sura ifuatayo.

KUWA RAFIKI MKUBWA WA MUGU

Kwa njia ya mazungumzo ya daima. Huwezi kamwe kuwa na uhusiano wa karibu na Mungu kwa kuhudhuria Kanisani mara moja tu kwa wiki au hata kwa kuwa na muda wa kutulia mbele za Mungu kila siku. Urafiki unajengeka kwa kumshirikisha mambo yako yote ya maisha.

Kumjua na kumpenda Mungu ni upendeleo mkubwa kwetu, na kujulikana na kupendwa na Mungu ni furaha kubwa kwa Mungu.

Kwa kweli, ni muhimu kuwa na muda kila siku wa kujitoa mbele za Mungu, (Angalia, “Jinsi ya kuwa na wakati wa kimya Wenye Manufaa” ndani ya kanuni za kujisomea Biblia Binafsi, Rick Warren, 1981, kutoka www.pastors.com) Lakini unahitaji zaidi ya muda huo wa kwenye ratiba yako. Anahitaji kuhusishwa katika kila kazi, kila mazungumzo, kila tatizo, na hata kila wazo. Unaweza kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja naye kwa siku nzima, ukiongea naye kuhusu kila unachofanya au kufikiri kwa muda huo. “Kuomba bila kukoma” (1 Wathesalonike 5:17) maana yake ni kuzungumza na Mungu wakati ukiwa dukani, unaendesha gari, au unafanya kazi yoyote ya kila siku.

Watu wengi hudhani “kuwa na mudana Mungu” humaanisha kuwa peke yako na Mungu. Ni kweli, kama Yesu alivyotoa kielelezo, unahitaji muda peke yako na Mungu, lakini huo ni sehemu tu ya masaa yako ya kukesha. Kila kitu unachofanya chaweza kuwa “muda pamoja na Mungu” kama akikaribishwa kushiriki na wewe ukautambua uwepo wake.

Kitabu cha kisasa kinachohusu kujifunza kukuza mazungumzo ya daima na Mungu kinaitwa “Kujizoeza Uwepo wa Mungu”. Kiliandikwa katika karne ya kumi na saba na Brother Lawrence, mpishi katika nyumba ya watawa Ufaransa. Brother Lawrence aliweza kugeuza hata maeneo ya kawaida na shughuli ndogo ndogo, kama vile kupika na kuosha vyombo, kuwa matendo ya sifa na ushirika na Mungu. Ufunguo wa urafiki na Mungu, alisema, siyo kubadili unachofanya, lakini kubadili nia ya ndani kuhusu unachofanya, kili unachofanya kwa ajili yako sasa unakifanya kwa ajili ya Mungu, iwe ni kula, kuoga, kufanya kazi, kupumzika, au kutupa taka.

Siku hizi tunajisikia lazima “tutoke” katika kazi zetu za kila siku ili kumwabudu Mungu, lakini hiyo ni kwa sababu hatujajifunza kujizoeza uwepo wake wakati wote. Brother Lawrence aliona jambo hili kwa rahisi la kumwabudu Mungu kwa kazi za kawaida maishani; hakuhitaji kwenda mahali maalum kwa ajili ya mambo ya kiroho.

Hili ndilo kusudi la Mungu. Kule Edeni, kuabudu halikuwa tukio la kuhudhuria, lakini hali ya daima; Adamu na hawa walikuwa na ushirika wa daima na Mungu. Kwa sababu Mungu yu pamoja nawe wakati wote, hakuna sehemu iliyo karibu naye kuliko hapo ulipo sasa hivi. Biblia ina sema, “Anatawala kila kitu na yuko kila mahali na yuko ndani katika kila kitu.” Waefeso 4:6b (NCV)

Wazo jingine la msaada toka kwa Brother Lawrence lilikuwa kusali sala fupi za kimazungumzo daima mara kwa mara katika siku badala ya kujaribu kusali kwa muda mrefu sala ngumu. Ili kuwa na mwelekeo mmoja na kuepuka mawazo mbali mbali, alisema, “sikushauri kutumia maneno mengi katika sala, kwa kuwa maneno mengi mara nyingi ni chanzo cha kutangatanga.” Brother Lawrence, Mazoezi ya uwepo wa Mungu (Grand Rapids: Revell/Spire Books, 1967), Barua ya Nane. Katika kipindi hiki ambacho hakuna muda wa kutulia, ushauri huu uliotolewa miaka 450 unaonekana kuwa wa muhimu na wa kufaa sana.

Kila kitu unachofanya chaweza kuwa “muda na Mungu” kama akikaribishwa kushiriki na wewe ukatambua uwepowake.

Biblia inatuambia, “kusali bila kukoma.” 1 Wathesalonike 5:17 (Msg) Je, inawezekana vipi kufanya hivi? Njia moja wapo ni kutumia “sala za pumzi” katika siku nzima, kama wakristo wengi wamefanya kwa karne nyingi. Unachagua sentensi fupi au maneno machache yanayoweza kurudiwa mbele za Yesu kwa pumzi moja: “Uko nami.”“Napokea neema yako.”“Nakutegemea.”“Kwangu kuishi ni Kristo.”“Hutaniacha kamwe.”“Wewe ni Mungu wangu.” Sali sentensi hii fupi mara kwa mara ikae moyoni mwako. Hakikisha kwamba nia yako ni kumheshimu Mungu na siyo kumtawala.

Kujizoeza uwepo wa Mungu ni ujuzi, tabia ambayo unaweza kuijenga. Kama vile wanamuziki wanavyofanya mazoezi kila siku ili waimbe muziki mzuri kwa wepesi, ni lazima ujilazimishe kufikiri juu ya Mungu kwa Nyakati mbali mbali katika siku nzima. Ni lazima ufundishe akili yako kumkumbuka Mungu.

Mwanzoni itakubidi utengeneze vitu vya kukukumbusha daima kwamba Mungu yupo pamoja nawe kwa wakati huo. Anza kwa kuweka vitu vinavyoonekana ili kukukumbusha. Unaweza kuweka ukutani maandishi yanayosema, “Mungu yuko nami na yupo kwa ajili yangu sasa hivi.” Watawa wabenedictine hutumia kengele ya saa kuwakumbusha kutulia na kusali “sala ya kila saa.” Kama una saa au simu ya mkononi yenye kengele, unaweza kufanya hivyo hivyo. Mara nyingine unahisi uwepo wa Mungu; wakati mwingine hutaweza.

Kama unatafuta kuhisi uwepo wake kwa kupitia haya yote, basi umekosa maana halisi. Hatumsifu Mungu ili tujisikie vizuri, lakini tutende mema. Lengo lako siyo hisia, lakini ufahamu wa wakati wote wa ukweli kwamba Mungu yupo wakati wote. Haya ndiyo maisha ya kuabudu.

Kwa njia ya kutafakari daima. Njia ya pili ya kujenga urafiki na Mungu ni kwa kufikiri juu ya neno lake siku nzima. Hii huitwa kutafakari, na Biblia hutushauri kutafakari kuhusu Mungu ni nani, amefanya nini, na amesema nini. (Zaburi 23:4; 143:5; 145:5; Yoshua 1:8; Zaburi 1:2).

Haiwezekani kuwa rafikiwa Mungubila kufahamu asemayo. Huwezi kumpenda Mungu mpaka umjue, na huwezi kumjua bila kujua neno lake. Biblia inasema Mungu “Alijifunua kwa Samueli kwa kupitia neno lake.” (1 Samueli 3:21) Mungu bado anatumia njia hiyo siku hizi.

Ingawa huwezi ukatumia siku nzima kusoma Biblia, unaweza kufikiri juu yake siku nzima, ukikumbuka vifungu ulivyosoma au kukariri na kuanza kuvitafakari akilini mwako.

Kutafakari ni jambo ambalo watu wengi hawalielewi na kudhani kuwa ni jambo fulani la kiibada lililo gumu na la siri fulani ambalo hufanywa na watawa wajitengao wa watu. Lakini kutafakari ni kufikiri kwa mwelekeo mmoja – ujuzi ambao mtu yeyote anaweza kujifunza na kuutumia popote.

Unapofikiri juu ya tatizo tena na tena katika akili yako, hiyo ni hofu. Unapofikiri juu ya neno la Mungu tena na tena, huko ni kutafakari. Kama unajua namna ya kuhofu, tayari unajua namna ya kutafakari! Unatakiwa kubadili mwelekeo wako kutoka kwenye matatizo yako na kwenda kwenye vifungu vya Biblia. Kadiri unapotafakari neno la Mungu, ndivyo na hofu yako inavyopungua.

Sababu iliyomfanya Mungu awaone Ayubu na Daudi kuwa rafiki zake wa karibu ni kwamba walithamini neno la Mungu kuliko chochote kile, na walilitafakari daima siku nzima. Ayubu alikiri, “Nimeyatunza maneno ya kinywa chake kuliko mkate wangu wa kila siku.” Ayubu 23:12 (NIV) Daudi alisema, “Jinsi gani ninavyoipenda sheria yako! Naitafakari mchana kutwa.” Zaburi 119:27 (NIV) “Nayatafakari daima. Siwezi kuacha kuyafikiri.” Zaburi 77:12 (NLT)

Marafiki hushirikishana siri, na Mungu atakushirikisha siri zake kama utajenga tabia ya kutafakari neno la lake siku nzima. Mungu alimwambia Ibrahimu siri zake, na alifanya hivyo pia kwa Daudi, Paulo, wanafunzi wake, na marafiki wengine. (Mwanzo 18:17; Danieli 2:19; 1 Wakorintho 2:7-10).

Unaposoma Biblia yako au ukasikiliza mahubiri au kanda, usisahau na kuondoka. Jenga tabia ya kutathmini ukweli akilini mwako, ufikiri tena na tena. Kadiri unapotumia muda mwingi kutathmini Mungu alichosema, ndipo utakapoelewa zaidi “siri” za maisha haya ambazo watu wengi hawana. Biblia inasema, “Urafiki na Mungu ni kwa ajili ya wale wanaomheshimu. Ni hao tu ndio anaowashirikisha siri za ahadi zake.” Zaburi 25:14 (LB)

Siku ya Kumi naMbili: Kukuza Urafiki Wako Na Mungu

Yeye hufanya urafiki na watauwa

Mithali 3:32 (NLT)

Mkaribieni Mungu, naye Mungu atawakaribia ninyi.

Yakobo 4:8 (NLT)

Unakuwa karibu na Mungu kulingana na unavyochagua kuwa.

Kama urafiki mwingine wowote, ni lazima ujitahidi kuukuza urafiki wako na Mungu. Haiwezi kutokea tu kwa bahati, inahitaji nia, muda na nguvu. Kama unataka uhusiano wa kina na Mungu lazima ujifunze kumshirikisha wazi hisia zako, kumwamini anapokutaka ufanye kitu fulani, jifunze kujali mambo anayoyajali, na utamani urafiki wake kuliko kitu kinginecho.

Lazima nichague kuwa mwaminifu kwa Mungu. Tofali la kwanza la kujenga urafiki wa kina na Mungu ni uaminifu wa kweli kuhusu makosa na hisia zako. Mungu hakutegemei wewe kuwa mkamilifu, lakini anasisitiza uaminifu wa kweli. Hakuna rafiki yoyote wa Mungu katika Biblia aliyekuwa mkamilifu. Kama ukamilifu kingekuwa kigezo cha kuwa rafiki wa Mungu, haingewezekana kwetu kuwa rafiki zake, lakini kwa sababu ya neema ya Mungu, Yesu bado ni “rafiki wa wenye dhambi.” Mathayo 11:19

Katika Biblia marafiki wa Mungu walikuwa waaminifu kuhusu hisia zao, mara nyingi walilalamika, walikisia, walilaumu, na kubishana na Mungu wao. Mungu hata hivyo hakuonekana kuudhiwa na uwazi huu, badala yake alichochea hali hiyo.

Mungu alimruhusu Ibrahimu kuuliza kutoa changamoto kuhusu maangamizi ya mji wa Sodoma, Ibrahimu alijadili na Mungu kuhusu kilichotakiwa ili kutokuangamiza mji, akajadili na Mungu toka watu hamsini mpaka watu kumi. Mungu pia alimsikiliza kwa uvumilivu Daudi katika lawama zake nyingi za kumnyima haki, kusalitiwa na kuachwa. Mungu hakumuua Yeremia alipodai kuwa Mungu amemfanyia ujanja. Ayubu aliruhusiwa kutoa uchungu wake katika mateso na hatimaye Mungu alimtetea kwa kuwa mwaminifu, na akawakemea rafiki za Ayubu kwa kutokuwa wakweli. Mungu aliwaambia, “Hamkuwa waaminifu kwangu wala juu yangu – sivyo rafiki yangu alivyofanya … Rafiki yangu Ayubu sasa atawaombea na nitapokea maombi yake.” Ayubu 42:7 (Msg)

Katika mfano mmoja wa ajabu wa urafiki ulio wazi (Kutoka 33:1-17), Mungu alionyesha kuchukizwa kwake kabisa na uasi wa Israeli. Alimwmbia Musa kwamba angeitunza ahadi yake ya kuwapatia Israeli nchi ya ahadi, lakini asingeweza kuendelea nao zaidi jangwani! Mungu alikuwa amechoshwa, na alimjulisha wazi Musa alivyokuwa anajisikia.

Mungu hategemei wewe kuwa mkamilifu lakini anasisitiza uaminifu wa kweli.

Musa akizungumza kama “rafiki” wa Mungu alijibu: “Tazama unaniambia kuongoza watu hawa lakini hunijulishi nani utamtuma kwenda nami … kama mimi ni wa muhimu kwako, basi nijulishe mipango yako … kama uwepo wako hautatuongoza, basi simamisha safari hii sasa hivi! Je nitajuaje uko pamoja na mimi katika hili, mimi pomoja wa watu wako? Je utaenda nasi au la? … Mungu akamwambia Musa, ‘Vyema. Kama unavyosema; hili pia nitalifanya, kwa kuwa nakujua vyema na wewe ni mtu wa muhimusana kwangu.’”Kutoka 33:12-17 (Msg)

Je, Mungu anaweza kuchukuliana na uaminifu wako wa kina na wa wazi? Bila shaka! Urafiki wa kweli umejengwa kwenye uwazi. Kile kinachoweza kuonekana kama ufidhuli Mungu anauona kuwa ukweli. Mungu husikiliza maneno ya uwazi ya rafiki zake; anachoshwa na maneno yale yale ya kiunyenyekevu ya kidini. Kuwa rafiki wa Mungu ni lazima uwe mwaminifu kwa Mungu, ukimshirikisha hisia zako kikweli, siyo unavyodhani unapaswa kuhisi au kusema.

Uchungu ni kikwazo kikubwa cha urafiki na Mungu.

Wakati mwingine inabidi kutubu hasira na chuki vilivyofichika dhidi ya Mungu kwa maeneo fulani ya maisha yako uliyofikiri umedanganywa au kukatishwa tamaa. Mpaka tutakapopevuka kufikia kuelewa vile Mungu hutumia kila kitu kutupa mema maishani mwetu, tutaendelea kutunza chuki dhidi ya Mungu kuhusu sura zetu, mazingira yetu ya nyuma, maombi ambayo hayakujibiwa, maumivu ya nyuma, na mambo mengine ambayo tungeyabadilisha kama tungekuwa Mungu. Watu mara nyingi humlaumu Mungu kwa maumivu yanayosababishwa na watu wengine. Hii inatengeneza kile William Backus anaita “ufa uliofichika kati yako na Mungu.”

Uchungu ni kikwazo kikubwa cha urafiki na Mungu: kwa nini nitamani kuwa rafiki wa Mungu kama aliruhusu jambo hili? Dawa, kwa kweli, ni kuelewa kwamba Mungu siku zote hutenda yote ili kukupa mema. Hata kama inaumiza na huelewi jambo hilo. Lakini kuachilia chuki na kudhihirisha hisia zako ni hatua ya kwanza kuelekea uponyaji. Kama watu wengi wa Biblia walivyofanya, mwambie Mungu wazi unavyojisikia. Fikiria Ayubu (Ayubu 7:17-21), Asafu (Zaburi 83:13), Yeremia (Yeremia 20:7), Naomi (Ruth 1:20).

Ili kutupa mwongozo dhahiri kuhusu uaminifu, Mungu alitupa kitabu cha zaburi – kitabu cha ibada, kilichojaa makelele, kupayukapayuka, mashaka, hofu, chuki, shauku zenye kujaa shukrani, sifa na kauli za imani. Kila aina ya hisia imo katika Zaburi. Unaposoma toba za Daudi na wengine, elewa kwamba hivi ndivyo Mungu anapenda umwabudu – usizuie chochote unavyojihisi. Unaweza kusali kama Daudi, “Natoa manung’uniko yangu mbele zake na kumwambia mateso yangu yote. Kwa kuwa mimezidiwa.” Zaburi 142:2 (NLT)

Inatia moyo kwamba marafiki wote wa Mungu – Musa, Daudi, Ibrahimu, Ayubu na wengine – walikabiliwa na mashaka. Lakini badala ya kuigiza kwa namna ya kidini tu, walisema wazi na hadharani. Kuelezea mashaka yako wakati mwingine ni hatua ya kwanza kuelekea kiwango kingine cha uhusiano na Mungu.

Ni lazima nichague kumtii Mungu katika Imani. Kila wakati unapoamini hekima ya Mungu na kufanya kila analosema, hata pale unapokuwa huelewi, unakuza urafiki wako na Mungu. Mara nyingi hatufikiri utii kama sifa ya urafiki; huo ni kwa ajili ya uhusiano na mzazi, mkubwa wa kazi, siyo kwa rafiki. Lakini, Yesu aliweka wazi kwamba utii ni kigezo cha uhusiano na Mungu. Alisema, “Ninyi ni rafiki zangu kama mtafanya ninayowaamuru.” Yohana 15:14 (NIV)

SIKU YA KUMI NA MBILI:

KUKUZA URAFIKI NA MUNGU

Katika sura iliyopita nilisema kwamba neno alilolitumia Yesu alipotuita “rafiki” laweza kumaanisha “marafiki wa mfalme,” katika baraza la kifalme. Wakati hawa marafiki wana upendeleo maalum, walikuwa bado chini ya mfalme na walipaswa kutii amri zake. Sisi ni marafiki na Mungu, lakini sisi siyo sawa na Yeye. Yeye ni kiongozi wetu atupendaye, na tunamfuata.

Tunamtii Mungu, si kama wajibu au kwa hofu au kwa kushurutishwa, lakini kwa sababu tunampenda na tunaamini kwamba anajua kile kilicho bora kwetu. Tunataka kumfuata Kristo kwa shukrani kwa yote aliyotufanyia, na tunapomfuata kwa karibu, ndipo urafiki wetu naye unakuwa wa kina zaidi.

Wasioamini mara niyingi hudhani kwamba Wakristo hutii kwa sababu ni wajibu, au kuogopa lawama, au kuogopa hukumu, lakini ukweli ni kinyume cha hayo. Kwa sababu tumesamehewa na kuwekwa huru, tunatii kwa upendo – na utii wetu hutuletea furaha kubwa! Yesu alisema, “Nimewapenda kama vile Baba alivyonipenda. Kaeni katika pendo langu. Mnaponitii mnakaa katika pendo langu, kama ninavyomtii Baba yangu na kukaa katika pendo lake. Nimewaambia haya ili mjazwe na furaha yangu. Ndiyo, furaha yenu itafurika!” Yohana 15:9-11 (NLT)

Angalia jinsi ambavyo Yesu anatutazamia kufanya yale tu aliyoteda kwa Baba yake. Uhusiano wake na Baba yake ni Kielelezo kwa uhusiano wetu naye. Yesu alifanya chochote Baba alichomwagiza kufanya – kwa upendo.

Urafiki wa kweli si wa kukaa tu ni wa vitendo. Yesu anapotuagiza kuwapenda wengine, kusaidia wahitaji, kuwagawia wengine mali zetu, kuwa na maisha safi, kusamehe, na kuleta wengine kwake, upendo hutuchochea kutii mara moja.

Mara nyingi tunapewa changamoto la kumfanyia Mungu “mambo makubwa.” Ni bayana kwamba Mungu anafurahishwa zaidi tunapotenda mambo madogo madogo kwa ajili yake kutokana na utii wa upendo. Yawezekana kuwa hayonekani kwa wengine, lakini Mungu anayaona na kuyahesabu kuwa matendo ya kuabudu.

Nafasi kubwa inaweza kutokea mara moja katika maisha, lakini nafasi ndogo ndogo zinatuzunguka kila siku. Hata katika matendo madogo kama vile kusema kweli, kuonyesha wema, kuwatia moyo wengine, tunaleta tabasamu katika uso wa Mungu. Mungu anathamini matendo rahisi tu ya utii kuliko sala zetu, sifa na sadaka. Biblia inatuambia, “Kinachompendeza Mungu zaidi ni nini? Je, ni dhabihu za kutekezwa na sadaka au kutii sauti yake? Nibora kutii kuliko sadaka.” 1 Samweli 15:22 (NCV)

Yesu alianza huduma yake ya hadharani katika umri wa miaka thelathini kwa kubatizwa na Yohana. Katika tukio hilo Mungu alizungumza kutoka mbinguni, “Huyu ni mwanangu mpendwa na ninapendezwa naye.” Mathayo 3:17 (NLT) Je, Yesu alikuwa anafanya nini kwa miaka thelathini ambacho kilimfurahisha Mungu? Bablia haisemi kitu huhusu miaka hiyo iliyofichika, isipokuwa kwa maneno machache katika Luka 2:51: “Alirudi Nazareti nao na akaishi kwa kuwatii” (Msg). Miaka thelathini ya kumpendeza Mungu ilijumuishwa katika maneno: “Akaishi kwa kuwatii.

Ni lazima nichague kuthamini mambo Mungu anayoyathamini. Hivyo ndivyo marafiki hufanya – wanajali kile ambacho ni cha muhimu kwa mwenzake. Unapozidi kuwa rafiki wa Mungu, ndivyo utakavyozidi kujali mambo anayoyajali, kusikitika kwa mambo anayosikitikia, na kufurahia mambo yanayomletea furaha.

Paulo ni mfano wa hili. Mjadala wa Mungu ndio ulikuwa mjadala wake, na shauku ya Mungu ilikuwa shauku yake; “Jambo linalonilemea moyo ni kwamba ninawajali ninyi sana – hii ni shauku ya Mungu ikiwaka ndani yangu!” 2 Wakorintho 11:2 (Msg) Daudi alijisikia namna hiyo hiyo: “Shauku ya nyumba yako inawaka ndani yangu, hivyo wanaokutukana wananitukana na mimi pia.” Zaburi 69:9 (NLT)

Je, Mungu anajali nini zaidi? Ukombozi wa watu wake. Anapenda watoto wake wote waliopotea warudi! Hiyo ndiyo sababu kuu ya Yesu kuja duniani. Jambo la thamani sana kwenye moyo wa Mungu ni kifo cha mwanae. Jambo la pili la thamani ni pale watoto wake wanaposhirikisha wengine habari hizo. Kuwa rafiki wa Mungu ni lazima uwajali watu wote wanaokuzunguka ambao Mungu anawajali. Marafiki wa Mungu wanawaeleza rafiki zao kuhusu Mungu.

Unapozidi kuwa fafiki wa Mungu nidivyo utakavyozidi kujali mambo anayoyajali.

Ni lazima nitamani urafiki na Mungu kuliko kitu chochote. Zaburi zimejaa mifano mingi ya shauku hii. Daudi alikuwa na shauku kubwa ya kumjua Mungu kuliko vitu vyote; alitumia maneno kama vile kutamani, kuwa na shauku, kuwa na kiu, kuwa na njaa. Alimhitaji Mungu. Alisema, “Jambo ninalolitafuta zaidi ni ule upendeleo wa kutafakari hekaluni mwake, kuishi katika uwepo wake siku zote za maisha yangu. Niufurahie ukamilifu na utukufu wake usiopimika.” Zaburi 63:3 (LB)Katika zaburi nyingine alisema, “Upendo wako wamaanisha zaidi ya uzima kwangu.” Zaburi 63:3 (CEV)

Shauku ya Yakobo kwa ajili ya baraka za Mungu katika maisha yake ilikuwa kubwa sana kiasi kwamba alipigana na Mungu usiku kucha, “Sitakuachaia uende mpaka unibariki.” Mwanzo 32:26 (NIV) Sehemu ya kushangaza ya hadithi hiyo ni kwamba, Mungu mweza yote alimruhusu Yakobo ashinde! Mungu haudhiwi tunaposhindana naye, kwa sababu pambano hilo huhitaji kugusana ana kwa ana na hutuleta karibu naye. Pia ni kazi yenye shauku, na Mungu anapenda hivyo tunapokuwa na shauku naye.

Paulo ni mtu mwingine aliyekuwa na shauku ya kuwa na urafiki na Mungu. Hakuna kilichokuwa na maana kwake; Hili ndilo lilikuwa jambo la kwanza kwake, mwelekeo mzima, na lengo kuu la maisha yake. Ndiyo maana Mungu alimtumia Paulo kwa kiwango kikubwa sana. Tafsiri ya Biblia iitwayo Amplified huueleza vizuri msukumo wa shauku ya Paulo, “Lengo langu kubwa ni kwamba nimjue yeye – ili hatua kwa hatua nimjue kwa kina na kwa karibu sana, nikitambua na kuelewa na kufahamu maajabu yanafsi yake kwa kina na kwa uwazi.” Filipi 3:10 (Amp)

Ukweli ni kwamba – unakuwa karibu na Mungu kulingaza unavyochagua. Urafiki wa karibu na Mungu ni uchaguzi, si bahati tu. Ni lazima uutafute kwa makusudi. Je, kweli unauhitaji urafiki huu – kuliko chochote kile? Je, kuna faida gani kwako? Je, kuna faida kuacha mengine? Je, unastahili kutia bidii kujenga tabia na ujuzi unaohitajika?

Yawezekana ulikuwa na shauku ya Mungu siku zilizopita lakini umepoteza haja hiyo. Hilo lilikua tatizo la Wakristo kule Efeso – walikuwa wameacha upendo wao wa kwanza. Walifanya mambo yote sahihi, kwa kutimizawajibu, na siyo kwa upendo. Kama umekuwa katika hali ya hisia tu kiroho, usishangae Mungu akiruhusu maumivu katika maisha yako.

Maumivu ni kichocheo cha shauku – hututia nguvu kwa kuchochea badiliko ambalo kwa kawaida hatunalo. C.S. Lewis alisema, “Maumivu ni kipaza sauti cha Mungu.” Ni njia ya Mungu ya kutuamsha katika usingizi wa kiroho. Matatizo yako si adhabu; ni miito ya kukuamsha kutoka kwa Mungu wa upendo. Mungu hajakukasirikia; anasumbuka kwa ajili yako, atafanya kila awezalo ili kukurudisha katika ushirika naye. Lakini kuna njia rahisi ya kuwasha upya shauku yako kwa ajili ya Mungu: Anza kumwomba Mungu akupatie, na endelea kumwomba mpaka umepata. Omba hivi kwa siku nzima: “Mpendwa Yesu, zaidi ya chochote kile, nataka kukujua wewe kwa ukaribu sana. “Mungu aliwaambia mateka wa babeli, “Mtanitafuta kwa bidii na mtamani jambo hilo kuliko chochote kile, nitahakikisha hamkatishwi tamaa.” Yeremia 29:13 (Msg)

UHUSIANO MUHIMU ZAIDI KWAKO

SIKU YA KUMI NA MBILI

KUFIKIA JUU YA LENGO LANGU

Jambo la Kutafakari: Ninakuwa karibu na Mungu kulingana na ninavyochagua.

Kaifungu cha Kumbukumbu:Mkaribieni Mungu na Munguatawakaribieni.” Yakobu 4:8a (NLT)

Swali la kujiuliza: Je, ni mambo gani ninayoweza kuchagua kuyafanya leo ili niweze kuwa karibu na Mungu?

Hakuna chochote – hakuna kabisa – kilicho cha muhimu kuliko kukuza uhusiano na Mungu. Ni uhusiano utakaodumu milele. Paulo alimwambia Timotheo, “baadhi ya watu hawa wanakikosa kitu cha muhimu sana katika maisha – hawamjui Mungu.” 1Timotheo 6:21a (LB) Je, umekuwa ukikosa kitu cha muhimu zaidi maishani? Unaweza kufanya kitu fulani kuanzia sasa. Kumbuka ni uchaguzi wako. Unakuwa pamoja na Mungu kulingana na unavyochagua.

 

 

 

 

 

 

SIKU YA KUMI NA MOJA

KUFIKIRI JUU YA LENGO LANGU

Jambo la kutafakari: Mungu aapenda kuwa rafiki yangu mkubwa.

Kifungu cha Kukumbuka:Urafiki na Mungu ni kwa ajili ya wale wanaomheshimu.” Zaburi 25:14a (LB)

Swali la Kujiuliza: Je, naweza kufanya nini ili kujikumbusha kuhusu Mungu na kusema naye mara kwa mara siku nzima?


Siku ya Kumi naMbili: Kukuza Urafiki Wako Na Mungu

Yeye hufanya urafiki na watauwa

Mithali 3:32 (NLT)

Mkaribieni Mungu, naye Mungu atawakaribia ninyi.

Yakobo 4:8 (NLT)

Unakuwa karibu na Mungu kulingana na unavyochagua kuwa.

Kama urafiki mwingine wowote, ni lazima ujitahidi kuukuza urafiki wako na Mungu. Haiwezi kutokea tu kwa bahati, inahitaji nia, muda na nguvu. Kama unataka uhusiano wa kina na Mungu lazima ujifunze kumshirikisha wazi hisia zako, kumwamini anapokutaka ufanye kitu fulani, jifunze kujali mambo anayoyajali, na utamani urafiki wake kuliko kitu kinginecho.

Lazima nichague kuwa mwaminifu kwa Mungu. Tofali la kwanza la kujenga urafiki wa kina na Mungu ni uaminifu wa kweli kuhusu makosa na hisia zako. Mungu hakutegemei wewe kuwa mkamilifu, lakini anasisitiza uaminifu wa kweli. Hakuna rafiki yoyote wa Mungu katika Biblia aliyekuwa mkamilifu. Kama ukamilifu kingekuwa kigezo cha kuwa rafiki wa Mungu, haingewezekana kwetu kuwa rafiki zake, lakini kwa sababu ya neema ya Mungu, Yesu bado ni “rafiki wa wenye dhambi.” Mathayo 11:19

Katika Biblia marafiki wa Mungu walikuwa waaminifu kuhusu hisia zao, mara nyingi walilalamika, walikisia, walilaumu, na kubishana na Mungu wao. Mungu hata hivyo hakuonekana kuudhiwa na uwazi huu, badala yake alichochea hali hiyo.

Mungu alimruhusu Ibrahimu kuuliza kutoa changamoto kuhusu maangamizi ya mji wa Sodoma, Ibrahimu alijadili na Mungu kuhusu kilichotakiwa ili kutokuangamiza mji, akajadili na Mungu toka watu hamsini mpaka watu kumi. Mungu pia alimsikiliza kwa uvumilivu Daudi katika lawama zake nyingi za kumnyima haki, kusalitiwa na kuachwa. Mungu hakumuua Yeremia alipodai kuwa Mungu amemfanyia ujanja. Ayubu aliruhusiwa kutoa uchungu wake katika mateso na hatimaye Mungu alimtetea kwa kuwa mwaminifu, na akawakemea rafiki za Ayubu kwa kutokuwa wakweli. Mungu aliwaambia, “Hamkuwa waaminifu kwangu wala juu yangu – sivyo rafiki yangu alivyofanya … Rafiki yangu Ayubu sasa atawaombea na nitapokea maombi yake.” Ayubu 42:7 (Msg)

Katika mfano mmoja wa ajabu wa urafiki ulio wazi (Kutoka 33:1-17), Mungu alionyesha kuchukizwa kwake kabisa na uasi wa Israeli. Alimwmbia Musa kwamba angeitunza ahadi yake ya kuwapatia Israeli nchi ya ahadi, lakini asingeweza kuendelea nao zaidi jangwani! Mungu alikuwa amechoshwa, na alimjulisha wazi Musa alivyokuwa anajisikia.

Mungu hategemei wewe kuwa mkamilifu lakini anasisitiza uaminifu wa kweli.

Musa akizungumza kama “rafiki” wa Mungu alijibu: “Tazama unaniambia kuongoza watu hawa lakini hunijulishi nani utamtuma kwenda nami … kama mimi ni wa muhimu kwako, basi nijulishe mipango yako … kama uwepo wako hautatuongoza, basi simamisha safari hii sasa hivi! Je nitajuaje uko pamoja na mimi katika hili, mimi pomoja wa watu wako? Je utaenda nasi au la? … Mungu akamwambia Musa, ‘Vyema. Kama unavyosema; hili pia nitalifanya, kwa kuwa nakujua vyema na wewe ni mtu wa muhimusana kwangu.’”Kutoka 33:12-17 (Msg)

Je, Mungu anaweza kuchukuliana na uaminifu wako wa kina na wa wazi? Bila shaka! Urafiki wa kweli umejengwa kwenye uwazi. Kile kinachoweza kuonekana kama ufidhuli Mungu anauona kuwa ukweli. Mungu husikiliza maneno ya uwazi ya rafiki zake; anachoshwa na maneno yale yale ya kiunyenyekevu ya kidini. Kuwa rafiki wa Mungu ni lazima uwe mwaminifu kwa Mungu, ukimshirikisha hisia zako kikweli, siyo unavyodhani unapaswa kuhisi au kusema.

Uchungu ni kikwazo kikubwa cha urafiki na Mungu.

Wakati mwingine inabidi kutubu hasira na chuki vilivyofichika dhidi ya Mungu kwa maeneo fulani ya maisha yako uliyofikiri umedanganywa au kukatishwa tamaa. Mpaka tutakapopevuka kufikia kuelewa vile Mungu hutumia kila kitu kutupa mema maishani mwetu, tutaendelea kutunza chuki dhidi ya Mungu kuhusu sura zetu, mazingira yetu ya nyuma, maombi ambayo hayakujibiwa, maumivu ya nyuma, na mambo mengine ambayo tungeyabadilisha kama tungekuwa Mungu. Watu mara nyingi humlaumu Mungu kwa maumivu yanayosababishwa na watu wengine. Hii inatengeneza kile William Backus anaita “ufa uliofichika kati yako na Mungu.”

Uchungu ni kikwazo kikubwa cha urafiki na Mungu: kwa nini nitamani kuwa rafiki wa Mungu kama aliruhusu jambo hili? Dawa, kwa kweli, ni kuelewa kwamba Mungu siku zote hutenda yote ili kukupa mema. Hata kama inaumiza na huelewi jambo hilo. Lakini kuachilia chuki na kudhihirisha hisia zako ni hatua ya kwanza kuelekea uponyaji. Kama watu wengi wa Biblia walivyofanya, mwambie Mungu wazi unavyojisikia. Fikiria Ayubu (Ayubu 7:17-21), Asafu (Zaburi 83:13), Yeremia (Yeremia 20:7), Naomi (Ruth 1:20).

Ili kutupa mwongozo dhahiri kuhusu uaminifu, Mungu alitupa kitabu cha zaburi – kitabu cha ibada, kilichojaa makelele, kupayukapayuka, mashaka, hofu, chuki, shauku zenye kujaa shukrani, sifa na kauli za imani. Kila aina ya hisia imo katika Zaburi. Unaposoma toba za Daudi na wengine, elewa kwamba hivi ndivyo Mungu anapenda umwabudu – usizuie chochote unavyojihisi. Unaweza kusali kama Daudi, “Natoa manung’uniko yangu mbele zake na kumwambia mateso yangu yote. Kwa kuwa mimezidiwa.” Zaburi 142:2 (NLT)

Inatia moyo kwamba marafiki wote wa Mungu – Musa, Daudi, Ibrahimu, Ayubu na wengine – walikabiliwa na mashaka. Lakini badala ya kuigiza kwa namna ya kidini tu, walisema wazi na hadharani. Kuelezea mashaka yako wakati mwingine ni hatua ya kwanza kuelekea kiwango kingine cha uhusiano na Mungu.

Ni lazima nichague kumtii Mungu katika Imani. Kila wakati unapoamini hekima ya Mungu na kufanya kila analosema, hata pale unapokuwa huelewi, unakuza urafiki wako na Mungu. Mara nyingi hatufikiri utii kama sifa ya urafiki; huo ni kwa ajili ya uhusiano na mzazi, mkubwa wa kazi, siyo kwa rafiki. Lakini, Yesu aliweka wazi kwamba utii ni kigezo cha uhusiano na Mungu. Alisema, “Ninyi ni rafiki zangu kama mtafanya ninayowaamuru.” Yohana 15:14 (NIV)

SIKU YA KUMI NA MBILI:

KUKUZA URAFIKI NA MUNGU

Katika sura iliyopita nilisema kwamba neno alilolitumia Yesu alipotuita “rafiki” laweza kumaanisha “marafiki wa mfalme,” katika baraza la kifalme. Wakati hawa marafiki wana upendeleo maalum, walikuwa bado chini ya mfalme na walipaswa kutii amri zake. Sisi ni marafiki na Mungu, lakini sisi siyo sawa na Yeye. Yeye ni kiongozi wetu atupendaye, na tunamfuata.

Tunamtii Mungu, si kama wajibu au kwa hofu au kwa kushurutishwa, lakini kwa sababu tunampenda na tunaamini kwamba anajua kile kilicho bora kwetu. Tunataka kumfuata Kristo kwa shukrani kwa yote aliyotufanyia, na tunapomfuata kwa karibu, ndipo urafiki wetu naye unakuwa wa kina zaidi.

Wasioamini mara niyingi hudhani kwamba Wakristo hutii kwa sababu ni wajibu, au kuogopa lawama, au kuogopa hukumu, lakini ukweli ni kinyume cha hayo. Kwa sababu tumesamehewa na kuwekwa huru, tunatii kwa upendo – na utii wetu hutuletea furaha kubwa! Yesu alisema, “Nimewapenda kama vile Baba alivyonipenda. Kaeni katika pendo langu. Mnaponitii mnakaa katika pendo langu, kama ninavyomtii Baba yangu na kukaa katika pendo lake. Nimewaambia haya ili mjazwe na furaha yangu. Ndiyo, furaha yenu itafurika!” Yohana 15:9-11 (NLT)

Angalia jinsi ambavyo Yesu anatutazamia kufanya yale tu aliyoteda kwa Baba yake. Uhusiano wake na Baba yake ni Kielelezo kwa uhusiano wetu naye. Yesu alifanya chochote Baba alichomwagiza kufanya – kwa upendo.

Urafiki wa kweli si wa kukaa tu ni wa vitendo. Yesu anapotuagiza kuwapenda wengine, kusaidia wahitaji, kuwagawia wengine mali zetu, kuwa na maisha safi, kusamehe, na kuleta wengine kwake, upendo hutuchochea kutii mara moja.

Mara nyingi tunapewa changamoto la kumfanyia Mungu “mambo makubwa.” Ni bayana kwamba Mungu anafurahishwa zaidi tunapotenda mambo madogo madogo kwa ajili yake kutokana na utii wa upendo. Yawezekana kuwa hayonekani kwa wengine, lakini Mungu anayaona na kuyahesabu kuwa matendo ya kuabudu.

Nafasi kubwa inaweza kutokea mara moja katika maisha, lakini nafasi ndogo ndogo zinatuzunguka kila siku. Hata katika matendo madogo kama vile kusema kweli, kuonyesha wema, kuwatia moyo wengine, tunaleta tabasamu katika uso wa Mungu. Mungu anathamini matendo rahisi tu ya utii kuliko sala zetu, sifa na sadaka. Biblia inatuambia, “Kinachompendeza Mungu zaidi ni nini? Je, ni dhabihu za kutekezwa na sadaka au kutii sauti yake? Nibora kutii kuliko sadaka.” 1 Samweli 15:22 (NCV)

Yesu alianza huduma yake ya hadharani katika umri wa miaka thelathini kwa kubatizwa na Yohana. Katika tukio hilo Mungu alizungumza kutoka mbinguni, “Huyu ni mwanangu mpendwa na ninapendezwa naye.” Mathayo 3:17 (NLT) Je, Yesu alikuwa anafanya nini kwa miaka thelathini ambacho kilimfurahisha Mungu? Bablia haisemi kitu huhusu miaka hiyo iliyofichika, isipokuwa kwa maneno machache katika Luka 2:51: “Alirudi Nazareti nao na akaishi kwa kuwatii” (Msg). Miaka thelathini ya kumpendeza Mungu ilijumuishwa katika maneno: “Akaishi kwa kuwatii.

Ni lazima nichague kuthamini mambo Mungu anayoyathamini. Hivyo ndivyo marafiki hufanya – wanajali kile ambacho ni cha muhimu kwa mwenzake. Unapozidi kuwa rafiki wa Mungu, ndivyo utakavyozidi kujali mambo anayoyajali, kusikitika kwa mambo anayosikitikia, na kufurahia mambo yanayomletea furaha.

Paulo ni mfano wa hili. Mjadala wa Mungu ndio ulikuwa mjadala wake, na shauku ya Mungu ilikuwa shauku yake; “Jambo linalonilemea moyo ni kwamba ninawajali ninyi sana – hii ni shauku ya Mungu ikiwaka ndani yangu!” 2 Wakorintho 11:2 (Msg) Daudi alijisikia namna hiyo hiyo: “Shauku ya nyumba yako inawaka ndani yangu, hivyo wanaokutukana wananitukana na mimi pia.” Zaburi 69:9 (NLT)

Je, Mungu anajali nini zaidi? Ukombozi wa watu wake. Anapenda watoto wake wote waliopotea warudi! Hiyo ndiyo sababu kuu ya Yesu kuja duniani. Jambo la thamani sana kwenye moyo wa Mungu ni kifo cha mwanae. Jambo la pili la thamani ni pale watoto wake wanaposhirikisha wengine habari hizo. Kuwa rafiki wa Mungu ni lazima uwajali watu wote wanaokuzunguka ambao Mungu anawajali. Marafiki wa Mungu wanawaeleza rafiki zao kuhusu Mungu.

Unapozidi kuwa fafiki wa Mungu nidivyo utakavyozidi kujali mambo anayoyajali.

Ni lazima nitamani urafiki na Mungu kuliko kitu chochote. Zaburi zimejaa mifano mingi ya shauku hii. Daudi alikuwa na shauku kubwa ya kumjua Mungu kuliko vitu vyote; alitumia maneno kama vile kutamani, kuwa na shauku, kuwa na kiu, kuwa na njaa. Alimhitaji Mungu. Alisema, “Jambo ninalolitafuta zaidi ni ule upendeleo wa kutafakari hekaluni mwake, kuishi katika uwepo wake siku zote za maisha yangu. Niufurahie ukamilifu na utukufu wake usiopimika.” Zaburi 63:3 (LB)Katika zaburi nyingine alisema, “Upendo wako wamaanisha zaidi ya uzima kwangu.” Zaburi 63:3 (CEV)

Shauku ya Yakobo kwa ajili ya baraka za Mungu katika maisha yake ilikuwa kubwa sana kiasi kwamba alipigana na Mungu usiku kucha, “Sitakuachaia uende mpaka unibariki.” Mwanzo 32:26 (NIV) Sehemu ya kushangaza ya hadithi hiyo ni kwamba, Mungu mweza yote alimruhusu Yakobo ashinde! Mungu haudhiwi tunaposhindana naye, kwa sababu pambano hilo huhitaji kugusana ana kwa ana na hutuleta karibu naye. Pia ni kazi yenye shauku, na Mungu anapenda hivyo tunapokuwa na shauku naye.

Paulo ni mtu mwingine aliyekuwa na shauku ya kuwa na urafiki na Mungu. Hakuna kilichokuwa na maana kwake; Hili ndilo lilikuwa jambo la kwanza kwake, mwelekeo mzima, na lengo kuu la maisha yake. Ndiyo maana Mungu alimtumia Paulo kwa kiwango kikubwa sana. Tafsiri ya Biblia iitwayo Amplified huueleza vizuri msukumo wa shauku ya Paulo, “Lengo langu kubwa ni kwamba nimjue yeye – ili hatua kwa hatua nimjue kwa kina na kwa karibu sana, nikitambua na kuelewa na kufahamu maajabu yanafsi yake kwa kina na kwa uwazi.” Filipi 3:10 (Amp)

Ukweli ni kwamba – unakuwa karibu na Mungu kulingaza unavyochagua. Urafiki wa karibu na Mungu ni uchaguzi, si bahati tu. Ni lazima uutafute kwa makusudi. Je, kweli unauhitaji urafiki huu – kuliko chochote kile? Je, kuna faida gani kwako? Je, kuna faida kuacha mengine? Je, unastahili kutia bidii kujenga tabia na ujuzi unaohitajika?

Yawezekana ulikuwa na shauku ya Mungu siku zilizopita lakini umepoteza haja hiyo. Hilo lilikua tatizo la Wakristo kule Efeso – walikuwa wameacha upendo wao wa kwanza. Walifanya mambo yote sahihi, kwa kutimizawajibu, na siyo kwa upendo. Kama umekuwa katika hali ya hisia tu kiroho, usishangae Mungu akiruhusu maumivu katika maisha yako.

Maumivu ni kichocheo cha shauku – hututia nguvu kwa kuchochea badiliko ambalo kwa kawaida hatunalo. C.S. Lewis alisema, “Maumivu ni kipaza sauti cha Mungu.” Ni njia ya Mungu ya kutuamsha katika usingizi wa kiroho. Matatizo yako si adhabu; ni miito ya kukuamsha kutoka kwa Mungu wa upendo. Mungu hajakukasirikia; anasumbuka kwa ajili yako, atafanya kila awezalo ili kukurudisha katika ushirika naye. Lakini kuna njia rahisi ya kuwasha upya shauku yako kwa ajili ya Mungu: Anza kumwomba Mungu akupatie, na endelea kumwomba mpaka umepata. Omba hivi kwa siku nzima: “Mpendwa Yesu, zaidi ya chochote kile, nataka kukujua wewe kwa ukaribu sana. “Mungu aliwaambia mateka wa babeli, “Mtanitafuta kwa bidii na mtamani jambo hilo kuliko chochote kile, nitahakikisha hamkatishwi tamaa.” Yeremia 29:13 (Msg)

UHUSIANO MUHIMU ZAIDI KWAKO

SIKU YA KUMI NA MBILI

KUFIKIA JUU YA LENGO LANGU

Jambo la Kutafakari: Ninakuwa karibu na Mungu kulingana na ninavyochagua.

Kaifungu cha Kumbukumbu:Mkaribieni Mungu na Munguatawakaribieni.” Yakobu 4:8a (NLT)

Swali la kujiuliza: Je, ni mambo gani ninayoweza kuchagua kuyafanya leo ili niweze kuwa karibu na Mungu?










Hakuna chochote – hakuna kabisa – kilicho cha muhimu kuliko kukuza uhusiano na Mungu. Ni uhusiano utakaodumu milele. Paulo alimwambia Timotheo, “baadhi ya watu hawa wanakikosa kitu cha muhimu sana katika maisha – hawamjui Mungu.” 1Timotheo 6:21a (LB) Je, umekuwa ukikosa kitu cha muhimu zaidi maishani? Unaweza kufanya kitu fulani kuanzia sasa. Kumbuka ni uchaguzi wako. Unakuwa pamoja na Mungu kulingana na unavyochagua.

 

 

 

 

 

 

Katika sura inayofuata tutaona siri nyingine nne za kukuza urafiki na Mungu, lakini usisubiri mpaka kesho. Anza leo kwa kujizoeza kuzungumza na Mungu daima na kutafakari mara kwa mara Neno lake. Sala hukupa nafsi ya kuzungumza kwa Mungu; kutafakari humpa Mungu kuzungumza kwako. Yote mawili ni muhimu kwa wewe kuwa rafiki wa Mungu.


 

 

 

 

 

 

 






沒有留言:

張貼留言