LENGO LA 3
|
ULIUMBWA ILI UFANANE NA KRISTO
Mizizi
yenu ikue na kuzama udani ya Kristo na kupata lishe kutoka kwake. Hakikisheni
kwamba
mnaendelea kukua katika Bwana, na mpate kuwa na nguvu katika ile kweli.
Wakolosai 2:7 (LB)
Siku ya Ishirini na
Mbili: Uliumbwa Ili Ufanane na Kristo
Mungu
alijua alichokuwa anafanya tangu mwanzo. Aliamua tangu mwanzoni
kuyafanya
maisha ya wale wampendao yafanane na maisha ya mwana wake …
Tunaona
sura ya asili na iliyokusudiwa ya maisha yetu katika yeye.
Warumi 8:29 (Msg)
Tunamwangalia
mwana huyu na kuona lengo la asili la Mungu
katika
kila kilichoumbwa.
Wakolosai 1:15 (Msg)
Tuliumbwa ili tufanane na Kristo.
Tangu mwanzo, mpango wa Mungu umekuwa ni kukufanya wewe uwe kama
Mwana wake, Yesu Kristo. Hii ndiyo hatima yako na lengo la tatu la maisha yako.
Mungu alitangaza kusudi hili wakati wa uumbaji, “Kisha Mungu
akasema, ‘Na tufanye wanadamu katika sura na mfano wetu.’” Mwanzo 1:26 (NCV)
Katika uumbaji wake wote, ni binadamu tu ndio wameumbwa “katika
mfano wa Mungu.” Huu ni upendeleo mkubwa na hutupa heshima. Hatujui yote huhusu
kifungu hiki cha maneno, lakini tunajua baadhi ya vipengele: kama Mungu, sisi
ni viumbe vya kiroho-roho
zetu hazifi na zitaishi hata baada ya miili yetu ya duniani kufa; sisi tuna akili-tunaweza kufikiri kutatua matatizo; kama Mungu, tuna busara-tunaweza kutoa na kupokea upendo; na tuna hali
ya uadilifu-tunaweza kujua mema na mabaya,
ambayo kutufanya kutoa hesabu kwa Mungu.
Biblia inasema kwamba watu wote, sio waamini tu, wana sehemu ya
sura ya Mungu, ndiyo maana uuaji na utoaji mimba ni dhambi. (Mwanzo 9:6; Zaburi
139:13-16; Yakobo 3:9.) Lakini sura hii si kamilifu imeharibiwa na dhambi. Hivyo
Mungu alimtuma Kristo na kazi ya kuja kurejeza sura kamili ambayo tumeipoteza.
Je, sura na “mfano wa Mungu” kamili ukoje? Huonekana kama Kristo!
Biblia husema Yesu ni “Mfano halisi wa Mungu,” “Sura ya Mungu asiyeonekana,” na “Mwakilishi halisi wa nafsi yake.” 2 Wakorintho 4:4 (NLT); Wakolosai 1:15 (NLT)
Watu mara nyingi hutumia maneno, “Kama baba kama mwana” kumaanisha
kufanana katika jamaa. Watu wanapoona mfano wangu katika watoto wangu,
hunifurahisha. Mungu anapenda watoto wake kuwa na sura na mfano wake pia.
Biblia inasema, “Ninyi … mliumkbwa ili muwe kama Mungu,
wenye haki na watakatifu kweli.” Waefeso
4:24 (GWT)
Ngoja niwe wazi zaidi: Kamwe hutakuwa Mungu, au hata mungu. Uongo
huo wa kiburi ni jaribu la zamani la Shetani. Shetani aliwaahidi Adamu na Hawa
kwamba kama wangefuata ushauri wake, “Mtakuwa kama
miungu.” Mwanzo 3:5 (KJV) Dini nyingi na falsafa za wakati mpya (New
Age) bado wanaendeleza uongo huu wa kale kwamba sisi ni miungu au tunaweza kuwa
miungu.
Tamaa hii ya kuwa Mungu hujitokeza kila wakati tunapotaka kutawala
mazingira yetu, hatima yetu, na watu wanaotuzunguka. Lakini kama viumbe,
hatutakuwa muumba kamwe. Mungu hapendi wewe uwe Mungu; anakutaka uwe mcha Mungu
(godly)-ukichukua matakwa yake, nia na tabia zake. Biblia husema, “Vaeni
njia mpya ya maisha-maisha ya kimungu, maisha yaliyofanywa upya kutoka ndani na
kujitokeza katika tabia yenu kama Mungu anavyodhihirisha bayana tabia yake
ndani yenu.” Waefeso 4:22 (Msg)
Lengo la Mungu kwa maisha yako duniani siyo faraja, lakini kukuza
tabia. Anapenda ukue kiroho na uwe kama Kristo. Kuwa kama Kristo haimaanishi
kupoteza nafasi yako au uwe kama kiumbe kisicho na akili. Mungu alikuumba wa
kipekee, hivyo bila shaka hapendi kukuangamiza. Kufanana na Kristo ni kuhusu
kubadilisha tabia yako, siyo nafsi yako.
Lengo kuu la mungu kwa maisha yako siyo faraja lakini
kukuza tabia yako. |
Watu wengi huelewa vibaya ahadi ya Yesu ya “uzima tele” (Yahana
10:10) kama kumaanisha afya kamilifu, maisha ya raha, furaha daima, kutimiza
ndoto zako zote, na kupata nafuu mara moja kutoka matatizoni kwa njia ya Imani
na maombi. Kwa maneno mengine, wanategemea maisha ya Kikristo kuwa rahisi.
Wanategemea mbingu duniani.
Mtazamo huu wa ubinafsi humwona Mungu kama jinni ambaye yupo tu
kukutumikia kafika kutimiza tamaa zako. Lakini Mungu siyo mtumishi wako, na
kama utachukuliwa na wazo la kwamba maisha lazima yawe mepesi, basi utapotoka
vibaya sana au utaishi katika hali ya kukana ukweli.
Usisahau kwamba maisha si juu yako! Upo kwa sababu ya lengo la
Mungu, na si kinyume cha hapo. Kwa nini Mungu akupe mbingu duniani wakati ameandaa
kitu halisi kwa ajili yako katika umilele? Mungu hutupa muda wetu wa duniani
ili kujenga na kuimarisha tabia yetu kwa ajili ya mbinguni.
KAZI YA ROHO MTAKATIFU NDANI YAKO
Ni kazi ya Roho Mtakatifu ndani yako kukupa tabia ya Kristo ndani
yako. Biblia inasema, “Kama Roho wa Bwana anavyofanya kazi
ndani yetu, tunafanana naye zaidi na zaidi na kudhihirisha utukufu wake zaidi.” 2 Wakorintho 3:18b (NLT) Mchakato huu wa kutubadilisha ili tuwe
kama yesu unaitwa utakaso,
ni lengo la tatu la maisha yako duniani.
Huwezi kudhihirisha tabia Kristo kwa nguvu zako mwenyewe. Maazimio
ya mwaka mpya, nguvu ya utashi, na nia njema havitoshi. Ni Roho Mtakatifu peke
yake aliye na nguvu za kufanya mabadiliko anayotaka kufanya Mungu katika maisha
yetu. Biblia inasema, “Mungu anatenda kazi ndani yenu,
akiwapa nia ya kumtii na nguvu za kufanya kile kimpendezacho.” Wafilipi 2:13 (NLT)
Ukitaja “nguvu za Roho Mtakatifu,” watu wengi hufikiri juu ya
udhihirisho wa
SIKU YA ISHIRINI NA MBILI: ULIUMBWA ILI UFANANE NA KARISTO |
Sura ya Kristo haipatikani kwa kuigiza, lakini kwa kukaa ndani.
Tunamruhusu Kristo kuishi kupitia sisi. “Kwa kuwa siri ni
hii: Kristo anaishi ndani yesu.” Kolosai
1:27 (NLT) Je, hii inatokeaje katika maisha halisi? Kwa uchaguzi tunaoufanya.
Tunachagua kufanya kitu sahihi katika mazingira fulani na kisha tunamwamini
Roho Mtakatifu kutupatia nguvu zake, upendo, imani na hekima ya kutenda. Kwa
kuwa Roho wa Mungu anaishi ndani yetu, mambo haya yanapatikana siku zote kwa
kuyaomba.
Lazima
tushirikiane na kazi ya Roho Mtakatikfu.
Katika Biblia nzima tunaona ukweli muhimu ukionyeshwa tena na tena: Roho
Mtakatifu hutoa nguvu zake mara unapochukua hatua ya imani. Wakati Yoshua
alipokabiliwa na kizuizi kisichopitika, mafuriko ya mto Yordani yalitoweka
baada ya viongozi kukanyaga kwenye mkondo wa maji kwa utii na imani. (Yoshua
3:13-17) Utii hufungulia nguvu za Mungu.
Mungu anakusubiri utende kwanza. Usingoje uwe na nguvu au ujisikie
kujiamini. Songa mbele katika udhaifu wako, ukifanya kitu sahihi pamoja na hofu
zako na hisia zako. Hivyo ndivyo unavyoshirikiana na Roho Mtakatifu, na ndivyo
tabia yako inavyokua.
Biblia hulinganisha kukua kiroho na mbegu, jengo, na mtoto anayekua.
Kila kielelzo huhitaji kushiriki kimatendo: mbegu lazima zipandwe na kulimwa,
majengo lazima yajengwe-hayatokei tu-na watoto lazima wale na kufanya mazoezi
ili wakue.
Wakati bidii haina chochote kuhusu wokovu wako, ina kazi kubwa kwa
kukua kwako kiroho. Angalau mara nane katika Agano Jipya tumeambiwa “kutia
bidii” Luka 13:24; Warumi 14:19; Waefeso 4:3; (zote NIV); 2 Timotheo
2:15 (NCV) Waebrania 4:11; 12:4; 2 Petro 3:14 (zote NIV). Katika kukua kwenu na
kuwa katika mfano wa Kristo. Hakai tu na kusubiri itokee.
Paulo anaeleza katika Waefeso 4:22-24 wajibu wetu wa aina tatu
katika kuwa kama Kristo. Kwanza, lazima tuchague kuziacha tabia zetu za zamani.
“Kila kitu … kinachohusiana na maisha ya zamani
lazima kiachwe. Kimeoza kabisa, kiondoeni!”
Waefeso 4:22 (Msg)
Pili, lazima tubadili namna tunavyofikiri. “Roho
Mtakatifu abadili namna mnavyofikiri.”
Waefeso 4:23 (CEV) Biblia inseam “tunabadilishwa” kwa kufanywa upya nia zetu.
(Warumi 12:2) Neno la Kiyunani la kubadilishwa ni metamorphosis (limetumiwa
katika Warumi 12:2 na 2 Wakorintho 3:18), linatumiwa leo kuelekeza badiliko la ajiabu
analopitia kiwavi na kuwa kipepeo. Ni kielelezo kizuri kwa kile kinachotokea
kwetu kiroho tunapomruhusu Mungu kuongoza mawazo yetu: Tunabadilishwa toka
nadani kuja nje, tunavutia zaidi, na tunawekwa huru kuruka katika anga jipya.
Tabia
yako hasa ni jumla ya mazoea yako. |
Mungu
hutumia Neno lake, watu na mazingira kukufinyanga.
Mambo haya matatu ni ya muhimu katika kukuza tabia. Neno la Mungu hutupa kweli tunayoihitaji ili tukue, watu wa Mungu hutupa msaada tunaohitaji kukua, na mazingira
hutupa mazingira tunayohitaji kukfanyia mazoezi ya kufanana na Kristo.
Unaposoma na kulifanyia kazi Neno la Mungu, ushirikiane na waamini wengine, na
ujifunze kumtumaini Mungu katika mazingira magumu, na kuhakikishia utakuwa na
mfano wa Kristo. Tutaviangalia hivi kila kimoja katika sura zilizoko mbele.
Watu wengi hudhani ili kukua kiroho kinachohitajika ni kusoma
Biblia na maombi. Lakini baadhi ya mambo maishani hayatabadilishwa na kusoma
Biblia au maombi peke zake. Mungu hutumia watu. Hupenda kufanya kazi kupitia
watu zaidi kuliko miujiza, ili tutegemeane kwa ajili ya ushirika. Anapenda
tukue pamoja.
Katika dini nyingi, watu wanaofikiriwa kuwa wamekomaa kiroho na
watakatifu ni wale wanaojitenga na wengine na kwenda katika nyumba za watawa
milimani, ambako wanaishi bila kuchafuliwa na watu wengine. Lakini huu ni
uelewa potofu. Upevu wa kiroho siyo kujitenga na watu kutafuta mambo ya
binafsi! Huwezi kukua katika hali ya mfano wa Kristo katika upweke ni lazima
kuwa karibu na watu na kuwa na uhusiano nao. Unahitaji uwe mshirika wa kanisa
na jamii. Kwa nini? Kwa sababu kukua kiroho halisi ni juu ya kujifunza kupenda
kama Yesu, na huwezi kutenda kwa mfano wa Kristo bila kuwa na uhusiano na watu
wengine. Kumbuka, yote ni juu ya upendo-kumpenda Mungu na kuwapenda wengine.
Kuwa
kama Kristo ni mchakato mrefu wa kukua na wa polepole. Kukua kiroho si tendo la mara moja au linalotokea lenyewe tu; ni tendo
la taratibu, linalotokea hatua kwa hatua ambalo litachukua maisha yako yote.
Akizungumzia mchakato huu, Paulo alisema, “Jambo hili
litaendelea mpaka hapo sisi … tumepevuka kama Kristo alivyo, na tutakuwa kama
yeye kabisa.” Waefeso 4:13 (CEV)
Unafanya kazi katika kuendelea. Mageuzi yako ya kiroho katika
kukuza tabia ya Kristo yatachukua maisha yako yote, na hata hapo hayatakuwa
kamilifu hapa duniani.
Yatakamilika utakapofika mbinguni au pale Yesu akirudi. Kwa wakati
huo, kazi yoyote ambayo haijamalizika juu ya tabia yako itakamilishwa. Biblia
inasema kwamba tutakapomwona Yesu kikamilifu, tutakuwa wakamilifu kama Yeye: “Hatuwezi
hata kufikiri tutakavyokuwa Kristo atakaporudi. Lakini tunajua kwamba
atakapokuja tutakuwa kama Yeye. Kwa kuwa tutamwona halisi kama alivyo.” 1 Yohana 3:2 (NLT)
Mungu
anajali zaidi wewe ni nani kuliko unachofaanya. |
Mungu anajali zaidi wewe ni nani kuliko unachofanya. Sisi ni wanadamu, si watendaji.
Mungu anahusika zaidi kuhusu tabia yako kuliko kazi yako, kwa sababu utachukua
tabia yako hadi katika umilele, na siyo kazi yako.
Biblia inaonya, “Msijifananishe sawa sawa kabisa na
mila na desturi zenu bila kufikiri. Badala yake, mtazameni Mungu. Mtabadilishwa
kutoka ndani kuja nje … tofauti na mila inayowazunguka, kila wakati ikiwavuta
mrudi katika uchanga, Mungu anawaandaa vyema, akiwakuza kukfikia utu uzima.” Warumi 12:2 (Msg) Lazima ufanye maamuzi kupingana na mila ili
kuelekea hali ya kufanana na Kristo. Vinginevyo, nguvu nyingine kama ya
marafiki, wazazi, wafanyakazi, na mila vitajaribu kukufinyanga katika sura
yake.
Inasikitisha, ukipitia kwa haraka vitabu vingi vya Kikristo
vinavyopendwa na watu huonyesha kwamba waamini wengi wameacha kumwishia Mungu
kwa malengo makubwa na wamezamia mambo ya binafsi na kujenga hisia zao. Hiyo ni
kujipendezesha na siyo kumfuata Kristo. Yesu hakufa msalabani ili tuishi kwa
raha mstarehe duniani. Lengo lake ni la kina sana: anapenda kutufanya tufanane
naye kabla hajatuchukua mbinguni. Huu ni upendeleo mkubwa kwetu, ni wajibu watu
sasa, na hatima yetu huu.
SIKU YA ISHIRINI NA MBILI KUFIKIRI JUU YA LENGO LANGU Jambo la Kutafakari: Niliwekwa wakfu nifanane na Kristo. Kifungu cha Kukumbuka: “Kadiri Roho wa Bwana anavyofanya kazi
ndani yetu, tunakuwa kama Yeye zaidi na zaidi na tunadhihirisha utukufu
wake zaidi.” 2 Wakorintho 3:18b (NLT) Swali la Kujiuliza: Je, ni katika eneo gani la maisha yangu
nahitaji kuomba nguvu za Roho Mtakatifu ili niwe kama Kristo leo? |
Siku ya Ishirini
na Tatu: Jinsi Tunavyokua
Mungu
anapenda tukue … kama Kristo katika kila kitu.
Waefeso 4:15a (Msg)
Hatukukusudiwa
kukaa kama watoto.
Waefeso 4:14a (Ph)
Mungu anapenda ukue.
Lengo la Baba yako a mbinguni ni wewe ukue ufikie kiwango cha
tabia za Kristo. Inasikitisha, mamilioni ya Wakristo wanazeeka bila kukua
kiroho. Wamezama katika utoto wa kiroho, wakikaa katika mavazi ya kitoto.
Sababu ni kwamba hawana mpango na kukua.
Kukua kiroho si tendo linalotokea tu. Huhitaji kuchukua hatua za
maksudi. Lazima utake
kukua, uamue
kukua, fanya bidii
kukua na udumu
katika kukua. Kuwa mwanafunzi (discipleship) – mchakato wa kuwa kama Kristo –
daima huanza na uamuzi. Yesu anatuita, na sisi tunaitika: “Njoo
uwe mwanafunzi wangu, Yesu alimwambia. Hivyo Mathayo aliinuka na kumfuata.” Mathayo 9:9 (NLT)
Wanafunzi wa kwanza walipoamua kumfuata Yesu, hawakuelewa matokeo
yote ya uamuzi wao. Wao waliitikia tu mwaliko wa Yesu. Ndivyo unavyohitaji
kuanza: Amua kuwa mwanafunzi.
Hakuna kinachobadilisha maisha yako zaidi kuliko uamuzi
unaouchukua. Maamuzi yako yaweza kukuendeleza au kukuharibu, lakini kati ya
hayo, yataonyesha wewe ni nani. Niambie ni jambo gani umejitoa kwalo, nami
nitakuambia utakuwa nani miaka ishirini ijayo. Tunakuwa katika hali kulingana
na uchaguzi tuliojitoa kuuishia.
Ni katika kujitoa huku kwamba watu wengi hulikosa lengo la Mungu
kwa maisha yao. Watu wengi wanaogopa kujitoa kwa ajili ya kitu chochote, hivyo wao
hujiendea kiholela katika maisha. Watu wengine hujitoa nusu kufuata mambo yanayopingana
maishani, jambo ambalo husababisha maisha ya huzuni na uvuguvugu. Watu wengine
hujitoa kikamilifu kwa mambo ya ulimwengu, kama vile kuwa tajiri au kujulikana,
na mwisho wake ni kukatishwa tamaa pamoja na uchungu mwingi. Kila uchaguzi una
matokeo ya milele, hivyo bora uchague kwa busara. Petro anaonya, “Kwa
kuwa kila kitu kinachotuzunguka kitayeyuka na kutoweka, basi mnatakiwa kuishi
maisha matakatifu yenye kumcha Mungu!”
2 Petro 3:11 (NLT)
Tunakuwa katika hali kulingana na uchaguzi tuliojitoa
kuuishia. |
Kifungu hiki huonyesha pande mbili za kukua kiroho: “kuutumikia” na “atendaye.” “Kuutumikia”
ni wajibu wako, na “atendaye”
ni wajibu wa Mungu. Kukua kiroho ni kazi ya kushirikiana wewe na Roho
Mtakatifu. Roho wa Mungu hufanya kazi pamoja nasi, siyo tu ndani yetu.
SIKU YA ISHIRINI NA TATU: JINSI TUNAVYOK UA |
Unapocheza mchezo wa mafumbo (puzzle), tayari unavyo vipande
vyote-kazi yako ni kuviunganisha. Wakulima hufanya kazi shambani siyo kupata
ardhi, lakini kuendeleza kile tayari wanacho. Mungu amekupa wewe maisha mapya;
sasa una wajibu wa kuyaendeleza “Kwa hofu na kutetemeka.” Maana yake ni kuchukua kwa makini ukuaji wako wa kiroho! Watu
wanapoacha kujali kukua kwao kiroho, inaonyesha hawaeliwi matokeo yake ya
milele (kama tulivyoona katika sura ya 4 na 5)
Kubadilisha
mwongozo wako. Ili kubadili maisha yako, lazima
ubadili unavyofikiri. Nyuma ya kila ufanyalo kuna wazo lako. Kila tabia
hutokana na imani, na kila tendo linachochewa na msimamo. Mungu alifunua ukweli
huu miaka elfu iliyopita kabla ya wanasaikolojia kuelewa: “Angalia
unavyofikiri; maisha yako yanafinyangwa na mawazo yako.” Mithali 4:23 (TEV)
Hebu fikiri kwamba umepanda mtumbwi wa kazi ziwani ukienda bila
nahodha ila umefungiwa mashine kwenda mashariki. Ukiamua kuugeuza mtumbwi huu
kuelekea magharibi, una njia mbili unazoweza kutumia kubadili uelekeo wa
mtumbwi huu. Njia ya kwanza ni kushika usukani na kutumia nguvu kuugeuza
kuelekea upande mwingine kutoka kwenye mwelekeo wa kwanza. Kwa nguvu ya utashi
unaweza kuishinda ile mashine inayojipeleka tu, lakini utasikia kizuizi wakati
wote. Mikono yako inaweza kuchoka, unaweza kuuachia usukani, na mtumbwi mara
moja unaweza kuelekea mashariki, njia ambayo ilipangwa ndani yake.
Hivi ndivyo hutokea unapojaribu kubadili maisha yako kwa nguvu na
nia yako; unasema, “Nitajilazimisha kula chakula kidog … kufanya mazoezi … ache kutokuwa na mipango
na kuchelewa chelewa.” Ndiyo, nguvu ya utashi inaweza kutoa matokeo ya muda
mfupi, lakini hujenga usumbufu wa daima ndani yako kwa sababu hujashughulikia
mzizi wa tatizo. Badiliko haliwi la asili kwako, hivyo mwisho unakata tamaa,
unarudia mlo wako, na unaacha mazoezi. Mara moja unarudia kawaida yako ya
nyuma.
Kuna njia bora na rahisi: badili mwongozo wako-jinsi unavyofikiri.
Biblia inasema, “Mruhusuni Mungu awabadili na kuwafanya
mtu mpya kwa kubadili jinsi mnavyofikiri.”
Warumi 12:2b (NLT) Hatua yako ya kwanza katika kukua kiroho ni kubadili
unavyofikiri. Mabadiliko daima huanzia katika akili. Unavyofikiri huchochea
unavyohisi, na unavyohisi huwa na mvuto wa unavyotenda. Paulo alisema, “Lazima
kuwe na kufanywa upya kirobo kwa fikra na nia zenu.”
Waefeso 4:23 (NLT)
Kuwa kama Kristo lazima ukuze nia ya Kristo ndani yako. Agano
Jipya huita tendo hilo la akili toba,
ambalo kwa kiyunani maana yake ni “kubadili nia yako.” Unatubu mara unapobadili
namna unavyofikiri kwa kuanza kufikiri Mungu anavyofikiri-kuhusu wewe, dhambi
Mungu, watu wengine, maisha, hatima yako, na kila kitu. Unachukua mtazamo wa
Kristo.
Tumeagizwa “kufikiri kama Kristo alivyofikiri.” Wafilipi 2:5 (CEV) Kuna sehemu mbili za kufanya hili. Nusu ya
kwanza ya badiliko hili la kiakili ni kuacha kufikiri mawazo ya kichanga,
ambayo ni ubinafsi na kutafuta mambo ya binafsi. Biblia inasema, “Acheni
kufikiri kama watoto, kuhusu maovu iweni watoto lakini katika kufikiri kwenu
iweni watu wazima.” 1 Wakorintho 14:20 (NIV) Watoto
wachanga kwa asili ni wenye ubinafsi kabisa. Wanajifikiri wao tu na mahitaji
yao. Hawawezi kutoa, wanawena tu kupokea. Huko ni kufikiri kwa mtu mchanga. Kwa
bahati mbaya, watu wengi hawakui kupita kiwango hicho cha kufikiri. Biblia
inasema kuwa kufikiri katika ubinafsi ni asili ya matendo ya dhambi, “wale
wanaoishi kwa kufuata nia zao za dhambi hufikiri vitu vile tu ambavyo nafsi zao
zenye dhambi zinataka.” Warumi 8:5 (NCV)
Nusu ya pili ya kufikiri ni kuanza kufikiri ki-utu uzima, ambayo
ni kuwaangalia wengine na siyo wewe. Katika sura yake kuu ya upendo, Paulo
alihitimisha kusema kwamba kuwafikiri wengine ni alama ya ukomavu: “Nilipokuwa
mtoto niliongea kama mtoto, niliamua kama mtoto. Nilipokuwa mtu mzima, niliacha
mambo ya kitoto.” 1 Wakorintho 13:11 (NIV)
Siku hizi watu wengi hudhani upevu wa kiroho unapimwa kwa kiasi
cha habari ya Biblia na mafundisho uliyo nayo. Wakati ufahamu ni moja ya vipimo
vya ukomavu, siyo mwisho. Maisha ya Kikristo ni zaidi ya mafundisho, na imani
yetu; ni pamoja na mwenendo na tabia. Matendo yetu lazima yafanane na
mafundisho yetu, na imani yetu lazima iwe msingi wa mwenendo wetu wa mfano wa
Kristo.
Ukristo siyo dini au falsafa, lakini ni uhusiano na mtindo wa
maisha. Kiini cha mtindo huu wa maisha ni kufikiri juu ya wengine, kama Yesu
alivyofanya, badala ya nafsi zetu. Biblia inasema, “Tufikirie yaliyo
mema kwao na kujaribu kuwasaidia kwa kufanya yale yanayowapendeza. Hata Kristo
hakujaribu kujipendeza nafsi yake.” Warumi
15:2-3a (CEV)
Kuwajili wengine ni icha ya kufanana na Kristo na uthibitisho imara wa kukua kiroho. Namna hii ya kufikiri siyo ya siyo ya asili, ni kinyume cha desturi, ni ngumu na nadra. Mungu ashukuriwe tuna msaada: “Mungu umetupatia Roho wake. Ndiyo maana hatufikiri kama watu wa ulimwengu huu wanavyofikiri.” 1 Wakorintho 2:12a (CEV) Katika sura chache zifuatazo tutaangalia zana anazotumia Roho Mtakatifu kutusaidia kukua.
SIKU YA ISHIRINI NA TATU KUFIKIRI JUU YA LENGO LANGU Jambo la Kutafakari: Hujachelewa kamwe kuanza kukua. Kifungu cha Kukumbuka: “Mruhusuni
Mungu awabadili ndani kwa kuwabadili kabisa nia zenu. Kisha mtaweza kujua
mapenzi ya Mungu – yaliyo mema na yenye kumpendeza na kamili.” Warumi 12:2b (TEV) Swali la Kujiuliza: Je, ni eneo gani moja ambao nahitaji
kuacha kufikiri nionavyo tu na kuanza kufikiri kwa njia ya Mungu? Siku ya Ishirini
na Nne: Kubadilishwa na Kweli |
Watu
wanahitaji zaidi ya mkate kwa ajili ya maisha yao; Lazima wale
kila
Neno kutoka kwa Mungu.
Mathayo 4:4 (NLT)
Neno
la neema … la Mungu laweza kuwafanya muwe apendavyo na
Kuwapatieni
kila kitu mnachoweza kuhitaji.
Matendo 20:32 (Msg)
Ukweli unatubadili.
Kukua kiroho ni mchakato wa kuondoa uongo na kuweka ukweli Yesu
aliomba, “Uwatakase kwa ile kweli, Neno lako ndiyo kweli.” Yohana 17:17 (NIV) Utakaso unahitaji ufunuo. Roho Mtakatifu
hutumia Neno la Mungu kutanya tufanane na Mwana wa Mungu. Kuwa kama Yesu, ni
lazima tujaze maisha yetu na Neno lake. Biblia inasema, “Kwa
njia na Neno tumewekwa pamoja na kutayarishwa kwa ajili ya kazi alizonazo Mungu
kwe ajili yetu.” 1 Timotheo 3:17 (Msg)
Neno la Mungu si kama neno lolote lile. Liko hai. (Waebrania 4:12;
Matendo 7:38; 1 Petro 1:23.) Yesu alisema, “Maneno niliyosema
kwenu ni roho na ni uzima.” Yohana 6:63 (NASB) Mungu
anaposema, mambo hubadilika. Kila kitu kinachozunguka-viumbe vyote-vinaishi kwa
sababu “Mungu alisema.” Aliposema vyote vikawa. Bila Neno la Mungu usingeweza
kuwa hai. Yakobo anasema, “Mungu aliamua kutupa uzima kwa njia ya
Neno la kweli ili tuwe watu wa muhimu zaidi katika vyote alivyoumba.” Yokobo 1:18 (NCV)
Roho wa Mungu hutumia neno la mungu kutufanya
tufanane na mwana wa Mungu |
Neno la Mungu ni lishe ya kiroho ni unayohitaji ili utimize lengo
lako. Biblia inaitwa maziwa yetu, mkate, chakula kigumu, na matunda matamu. (1
Petro 2:2; Mathayo 4:4; 1 Wakorintho 3:2; Zaburi 119:103.) Chakula hiki ni
chakula cha Roho kwa ajili ya nguvu za kiroho na kukua kiroho. Petro anashauri,
“Tamanini maziwa safi ya kiroho, ili kwamba kwa
hayo mpate kukua katika wokovu wenu.”
1 Petro 2:2 (NIV)
KUKAA KATIKA NENO LA MUNGU
Siku hizi kuna Biblia nyingi zimepigwa chapa kuliko hapo nyuma,
lakini Biblia kwenye shelfu haina faida yoyote. Mamilioni ya waamini wamepatwa
na ugonjwa wa kiroho wa kutokula, wanafufa kwa njaa ya kiroho. Kuwa mwanafunzi
wa Yesu mwenye afya, kujilisha Neno la Mungu lazima liwe jambo lako kuu katika
maisha. Yesu aliliita “Kukaa.”
Alisema, “Mkikaa katika Neno langu, basi ninyi ni
wanafunzi wangu kweli.” Yohana 8:31 (NASB, 1978
edition) Katika maisha ya kila siku, kukaa katika Neno la Mungu ni pamoja na
mambo matatu:
Ni
lazima nikubali mamlaka yake. Biblia lazima iwe ndicho kipimo
chenye mamlaka kwa maisha yangu: dira ya maisha yangu, ushauri ninaousikiliza
kwa kufanya maamuzi yangu, na kigezo ninachotumia kutathmini kila kitu. Biblia
lazima iwe na kauli ya mwanzo na ya mwisho katika maisha yangu.
Matatizo mengi hutupata kwa sababu tunaweka msingi wa maamuzi yetu
kwenye mamlaka zisizoaminika: Mila (“kila mtu anafanya”), desturi (“tumefanya
hivi siku zote”), fikra (“inaonekana kuwa na maana”) au hisia (“nilihisi vizuri”).
Haya yote manne yameharibiwa na Anguko. Tunachohitaji ni kipimo kikamilifu
ambacho hakitatuongoza kimakosa. Ni neno la Mungu tu ndilo linafikia kiwango
hicho. Sulemani anatukumbusha, “Kila Neno la Mungu halina kasoro,” Mithali 30:5 (NIV) na Paulo anasema, “Kila
kitu katika maandiko ni Neno la Mungu. Lote linafaa kwa mafundisho na kusaidia
watu na kwa kuwa sahihisha na kuwaonyesha namna ya kuishi.” 2 Timothy 3:16 (CEV)
Miaka ya mwanzoni ya huduma yake, Billy Graham alipitia kipindi
ambapo alihangaishwa na mashaka juu ya usahihi na mamlaka ya Biblia. Usiku
mmoja wa mbalamwezi alipiga magoti kwa machozi na kumwambia Mungu kwamba,
pamoja na vifungu vilivyomchanganya na kutokuvielewa, tangu hapo na kuendelea
ataiamini Biblia kama mamlaka pekee kwa maisha yake na huduma. Tangu siku hiyo
na kuendelea, maisha Billy yalibarikiwa na nguvu zisizo za kawaida na utendaji
bora.
Uamuzi wa muhimu sana unaoweza kuufanya leo ni kuamua ni nini
kitakuwa mamlaka ya mwisho kwa maisha yako. Amua kwamba bila kujali mila yako,
desturi, fikra, au hisia, unachagua Biblia kuwa mamlaka yako ya mwisho. Azimia
kujiuliza kwanza, “Je, Biblia inasemaje?” katika kufanya uamuzi. Amua kwamba
Mungu anaposema kufanya kitu fulani, utaliamini Neno la Mungu na kulitenda hata
kama linaleta maana au la hujisikii kulifanya. Chukua maneno ya Paulo kuwa
uthibitisho wa imani yako: “Naamini kila kitu kinachokubaliana na
sharia na kile kilichoandikwa katika manabii.”
Matendo 24:14 (NIV)
Ni
lazima nijae ukweli wa Biblia. Haitoshi tu
kuamini mamlaka ya Biblia, ni lazima nijaze akili yangu na kweli yake ili
kwamba Roho Mtakatifu anibadilishe na kweli hiyo. Kuna njia tano za kufanya:
unaweza kulipokea, kulisoma, kulitafiti, kulikumbuka, na kulitafakari.
Kwanza unalipokea
Neno la Mungu unapolisikia na kulipokea kwa nia wazi ya kupokea. Mfano wa
mpanzi ni kielelezo cha namna ya kupokea kwetu kunavyowezesha Neno la Mungu
kuwa na mizizi ndani yetu na kuzaa matunda au la. Yesu alitaja misimamo mitatu
isiyo ya kupokea-nia iliyofungwa (udongo mgumu), nia ya kuigiza (udongo usio na
rutuba) na nia iliyopotoka (udongo wenye magugu)-na kisha alisema, “Angalieni
sana jinsi mnavyosikia.” Luka 8:18 (NIV)
Mara unapohisi kwamba hujifunzi chochote kutoka na mahubiri au
mafundisho ya mwalimu wa Biblia, angalia msimamo wako, hasa kuhusu kiburi, kwa
sababu Mungu anaweza kusema hata kupitia mwalimu anayechosha sana unapokuwa
mnyenyekevu na mwenye kupokea. Yakobo anashauri, “Katika roho ya
unyenyekevu (upole, kiasi) pokeeni na kulikaribisha Neno ambalo limepandwa na
kuota mizizi moyoni mwenu lina nguvu ya kuokoa nafsi zenu.” Yakobo 1:21b (Amp)
Pili, sehemu kubwa ya historia ya miaka 2000 ya kanisa, ni mapadri
ndio walisoma
Biblia moja kwa moja, lakini sasa mabilioni yetu tunayo mikononi. Pamoja na
hayo, waamini wengi ni waaminifu kusoma gazeti la kila siku kuliko Biblia yao.
Haishangazi kwamba hatukui. Hatuwezi kutazama televisheni
kwa masaa matatu, na kisha tusome Biblia kwa dakika tatu halafu tutegemee
kukua.
Watu wengi wanaodai kuiamini Biblia “kutoka ukurasa hadi ukurasa”
hawajawahi kuisoma ukurasa kwa ukurasa. Lakini kama utaisoma Biblia dakika kumi
na tano kila siku, utaisomo yate katika mwaka mmoja. Kama utatenga dakika
thelathini za televisheni kila siku na badala yake usome Biblia, utaisoma
Biblia mara mbili kwa mwaka.
Kusoma Biblia kila siku itakuweka katika mazingira ya kuisikia
sauti ya Mungu. Ndiyo maana Mungu aliwaagiza wafalme wa Israeli kutunza nakala
ya Neno lake daima karibu nao: “Analazimika kulitunza Neno karibu naye
wakati wote na kulisoma kila siku ya maisha yao.”
Kumbukumbu 17:19a (NCV) Lakini usilitunze tu karibu yako; lisome mara kwa mara!
Dhana rahisi inayoweza kusadia kufanya jambo hili ni kuwa na mpango wa kila
siku wa kusoma Biblia. Mpango huu utakuzuia kurukia kurasa mbalimbali bila
mpango na kuacha sehemu nyingi. Kama ungependa nakala yako ya mpango wa kila
siku wa kusoma Biblia angalia nyongeza ya 2.
Tatu, kutafiti,
au kujifunza Biblia ni njia nyingine ya kukaa katika Neno. Tofauti kati ya
kusoma na kujifunza Biblia ni kuongezeka kwa kazi nyingine mbili: kuuliza
maswali ya kifungu na kuandika mambo uliyojifunza.Hujajifunza Biblia mpaka
umeandika mawazo yako chini katika karatasi au kompyuta.
Nafasi hainiruhusu kueleza njia tofauti za kujifunza Biblia. Kuna
vitabu kadhaa juu ya kujifunza Biblia , pamoja na kile nilichoandika miaka
ishirini iliyopita. (Rick Warren, Mbinu 12 za kujifunza Biblia Binafsi. Kitabu hiki kimetafsiriwa katika lugha sita. Hupatikana www.pastors.com) Siri ya kujisomea Biblia vizuri ni kuuliza maswali sahihi tu.
Njia tofauti hutumia maswali tofauti. Utagundua zaidi kama ukitulia na kuuliza
maswali kama nani? Nini? Wapi? Kwa nini? Na vipi? Biblia inseam, “Watu
wenye furaha kweli ni wale wanaojifunza sharia kamilifu ya Mungu ambayo
kuwaweka watu huru, na wanaendelea kujifunza. Hawasahau walichojifunza, lakini
wanatii mafundisho ya Mungu yanavyosema. Wale wanaofanya hivi watakuwa na
furaha.” Yokobo 1:25 (NCV)
Njia ya nne ya kukaa katika Neno la Mungu ni kwa kulikumbuka. Uwezo wako wa kukumbuka ni kipawa toka kwa Munkgu. Unaweza
kufikiri huna kumbukumbu nzuri, lakini ukweli ni kwamba, una mamilioni ya
mawazo, kweli na mifano ambayo umekariri. Unakumbuka kilicho muhimu kwako. Kama Neno la Mungu ni muhimu utachukua muda kulikumbuka.
Kuna faida nyingi za kukariri vifungu vya Biblia. Itakusaidia
kushinda majaribu, kufanya maamuzi ya busara, kupunguza mahangaiko ya moyo,
kujenga kujiamini, kutoa ushauri mzuri, na kushirikisha imani yako kwa wengine.
(Zaburi 119:105; 119:49-50; Yeremia 15:16; Mithali 22:18; 1 Petro 3:15.)
Kumbukumbu yako ni kama msuli. Kadiri unavyoitumia zaidi, ndivyo
inakuwa na nguvu, na kukariri Maandiko kutakuwa rahisi. Unaweza kuanza kwa
kuchagua vifungu vichache vya Biblia kutoka kitabu hiki ambavyo vimekugusa na
kuviandika kwenye kadi ndogo unayoweza kubeba. Kisha virudie kwa sauti siku nzima. Unaweza kukariri Maandiko popote: kazini au mazoezini
au ukiendesha gari, ukisubiri au wakati wa kulala. Funguo tatu za kukariri
Maandiko ni kurudia, kurudia, na kurudia tena! Biblia inasema, “Kumbukeni
yale aliyofundisha Kristo na Neno lake liwajae maishani na kuwafanya wenye
hekima.” Kolosai 3:16a (LB)
Njia ya tano ya kukaa katika Neno la Mungu ni kulifikiri, Biblia huita “kutafakari.” Kwa wengi, wazo la kutafakari lina
maana ya kuacha kufikiri na kuacha akili yako ianze kutangatanga. Hii ni
kinyume kabisa na kutafakari Kibiblia. Kutafakari ni kufikiri kwa mwelekeo. Huhitaji juhudi kubwa. Unachagua kifungu, na kufikiri tena na
tena akilini mwako.
Kama nilivyotaja katika sura ya 11, kama unajua jinsi ya kuhofu,
tayari unajua namna ya kutafakari. Hofu ni kufikiri kwa mwelekeo katika jambo
lisilofaa. Kutafakari ni kufanya jambo hilo hilo, lakini kwa kuelekea Neno la
Mungu badala ya matatizo yako.
Hakuna tabia yoyote inayoweza kugeuza maisha yako zaidi na
kukufanya kama yesu kuliko kutafakari Neno la Mungu kila siku. Tunapochukua
muda kulitafakari Neno la Mungu, huku tukimfikiri Kristo kwa makini, “tunabadilishwa
na kuchukua mfano wake na utukufu unaozidi.”2
Korintho 3:18 (NIV)
Ukiangalia nyakati zote ambazo Mungu huzungumzia kutafakari katika
Biblia, utashangazwa na faida alizoahidi kwa wale wanaochukua muda kulitafakari
Neno lake siku nzima. Sababu moja wapo ya Mungu kumwita Daudi “mtu
aupendezaye moyo wangu” Matendo 13:22 (NIV) ni kwamba
Daudi alipenda kutafakari Neno la Mungu. Alisema, “Nayapenda
mafundisho yako! Nayafikiri mchana kutwa.”
Zaburi 119:97 (NCV) Kutafakari kwa makini ukweli wa Mungu ni ufunguo kwa maombi
kujibiwa na siri ya maisha yenye mafanikio. (Yohana 15:7; Yoshua 1:8; Zaburi
1:2-3.)
Ni
lazima niweke katika vitendo kanuni za Neno la Mungu. Kupokea, kusoma, kutafiti, kukumbuka na kutafakari Neno la Mungu
yote hayafai kama hatutendi yale tuliyopata. Lazima tuwe “watendaji
wa Neno.” Yokobo 1:22 (KJV) Hii ndiyo hatua ngumu zaidi ya zote, kwa
sababu Shetani huipiga vita kali. Hajali kama utaenda kwenye kujifunza Biblia
ili mradi chochote na kile ulichojifunza.
Kweli
itakuweka huru, lakini kwanza inaweza kukufanya uwe na huzuni! |
Sababu nyingine kwa nini tunaepuka utekelezaji kwa mtu binafsi ni
kwa sababu ni vigumu au hata kuleta maumivu. Kweli itakuweka huru, lakini
kwanza inaweza kukufanya uwe na huzuni! Neno la Mungu hufunua nia yetu ya
ndani, hudhihirisha makosa yetu, hukemea dhambi yetu, na kututegemea
kubadilika. Ni asili ya binadamu kupinga badiliko, hivyo kutekeleza Neno la
Mungu ni kazi ngumu. Ndiyo maana ni vigumu kujadili utekelezaji wako binafsi na
watu wengine.
Siwei nikakazia kupita kiasi umuhimu wa kuwa mmoja katika kikundi kidogo
cha kujifunza Biblia. Mara nyingi tunajifunza kweli nyingi kutoka kwa wengine
ambazo tusingejifunza kama tungekuwa peke yetu. Watu wengine watakusaidia
kufahamu mambo ambayo usingeyaona na kuweka katika matendo ile kweli ya Mungu.
Njia bora ya kuwa “mtendaji wa Neno” ni kuandika daima hatua za
kuchukua kutekeleza ulichojifunza kwa kusoma, kutafiti au kutafakari Neno la
Mungu. Kuza tabia ya kuandika kile unachokusudia kufanya. Hatua hii ya
utekelezaji lazima iwe ya binafsi
(ikuhusishe wewe), inayotekelezeka (kitu unachoweza kufanya), na inayothibitika (weka muda maalum). Kila hatua ya utekelezaji itahusisha uhusiano
wako na Mungu, au uhusiano wako na wengine, au tabia yako binafsi.
Kabla ya kusoma sura inyofuata tumia muda fulani kufikiri juu ya
swali hili: Je, Mungu amekueleza nini katika Neno lake ambacho hujaanza
kukifanya bado? Kisha andika chini maneno machache ya utekelezaji ambayo yatakusaidia
utende unachojua. Unaweza kumweleza rafiki ambaye atakuwajibisha. Kama D.L.
Moody alivyosema, “Biblia haikutolewa ili kuongeza ufahamu wetu bali
kubadilisha maisha yetu.”
SIKU YA ISHIRINI NA NNE KUFIKIRI JUU YA LENGO LANGU Jambo la Kutafakari: Kweli hunigeuza. Kifungu cha Kukumbuka: “Mkikaa katika
Neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli,
nayo hiyo kweli itawaweka huru.” Yohana
8:31-32 (KJV) Swali la Kujiuliza: Je, Mungu amenieleza nini katika Neno
lake ambacho sijaanza kukifanya bado? |
Siku ya Ishirini
na Tano: Kubadilishwa na Taabu
Maana
dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia
utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana.
2 Wakorintho 4:17 (NIV)
Ni
moto wa mateso ambao hutoa dhahabu ya utauwa.
Madame Guyon
Mungu ana lengo kwa kila tatizo.
Yeye hutumia mazingira kukuza tabia yetu kwa kweli. Yeye hutegemea
zaidi mazingira katika kutufanya tufanane na Kristo kuliko anavyotegemea
usomaji wetu wa Biblia. Sababu iko wazi: Unakabiliana na mazingira masaa
ishirini na nne kila siku.
Yesu alituonya kwamba tutakuwa na matatizo ulimwenguni. (Yohana
16:33) Hakuna aliye sugu kwa matatizo au amefunikwa asipatwe na mateso, wala
hakuna aliye huru mbali na matatizo katika maisha. Maisha ni mfululizo wa
matatizo. Kila unapotatua moja, jingine linasubiri kutokea. Si yote makubwa, lakini
yote yana maana kwa Mungu katika kukuza tabia yako. Petro anatuhakikishia
kwamba matatizo ni ya kawaida, “Msishangazwe wala kushtushwa mnapopitia
katika mnapopitia katika majaribu yenye moto mbele yenu, kwa kuwa hili si geni,
ni jambo la kawaida ambalo litawapata.”
1 Petro 4:12 (LB)
Mungu anatumia matatizo kukusogeza karibu yake. Biblia inasema, “Mungu
yuko katibu yao waliopondeka mioyo, huwaokoa wale waliopondeka rohoni.” Zaburi 34:18 (NLT) Wakati wako mzuri wa kuwa na ibada ya karibu
na Mungu unaweza kuwa siku zile za giza sana-moyo wako unapokuwa umepondeka,
unapohisi kuachwa, unapokuwa huna uchaguzi, maumivu yanapokuwa makubwa-na
unamgeukia Mungu peke yake. Ni wakati wa taabu ndipo tunajifunza kusali sala za
kweli na uaminifu kutoka moyoni. Tunapokuwa katika maumivu, hatuna nguvu za
sala za juu juu.
Wakati wako mzuri wa kuwa na ibada ya karibu na Mungu
unaweza kuwa siku zile za giza sana. |
Mungu angeweza kuzuia Yusufu asitiwa gerezani, (Mwanzo 39:20-22)
angezuia Danieli asitupwe kwenye shimo la simba, (Danieli 6:16-23) angezuia
Yeremia asitupwe katika shimo la matope, (Yeremia 38:6) angezuia Paulo
asivunjikiwe na jahazi mara tatu, (2 Wakorintho 11:25) na angewazuia vijana
watatu Waebrania wasitupwe katika tanuru la moto (Danieli 3:26) – lakini
hakufanya hivyo. Aliruhursu matatizo hayo kutokea, na matokeo yake kila mmoja
wao alimsogelea Mungu karibu zaidi.
Matatizo hutulazimisha kumtazama Mungu na kumtegemea badala ya
nafsi zetu wenyewe. Paulo alishuhudia kuhusu faida hii, “Tulihisi
tuliwekewa kufa na tuliona jinsi tulivyokuwa hatuna nguvu za kujisaidia
wenyewe; lakini ilikuwa vyema, kwa kuwa hapo tuliweka kila kitu mikononi mwa
Mungu, ambaye peke yake angeweza kutuokoa.”
2 Wakorintho 1:9 (LB) Kamwe hutajua kwamba unachohitaji ni Mungu tu mpaka pale
utakapojikuta umebaki na Mungu tu.
Bila kujali chanzo, hakuna tatizo lolote linaloweza kukupata bila
ruhusa ya Mungu. Kila kinachotokea kwa mtoto wa Mungu kinachujwa
na Baba, na amekusudia kukitumia kuleta mema ingawa Shetani na watu
wengine wanakusudia mabaya.
Kila kinachotokea kwako kina umuhimu wa kiroho |
KUELEWA
WARUMI 8:28-29
Hiki ni kifungu ambacho hunukuliwa na kueleweka vibaya katika
Biblia. Hakisemi, “Mungu husababisha kila kitu kufanya kazi kama ninavyopenda
mimi.” Hii si kweli. Wala hakisemi, “Mungu husababisha kila kitu kufanya kazi
ili kuleta maisha ya furaha duniani.” Hisi kweli pia. Kuna miisho ya huzuni
duniani.
Tunaishi katika ulimwengu ulioanguka. Ni mbinguni tu mdiko mambo
yanatendeka kikamilifu kama Mungu alivyokusudia. Ndiyo maana tumeelezwa kusali,
“Mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko
mbinguni.” Mathayo 6:10 (KJV) Ili kuelewa vyema Warumi 8:28-29 ni lazima
uangalie kwa makini kila fungu la maneno.
“Tunajua”: Tumaini letu wakati wa magumu hutegemei kufikiri chanya, kufikiri
kwa kutarajia, au kule kutegemea mazuri kwa kawaida. Huu ni uhakika uliojengwa
kwenye kweli ya kwamba Mungu anatawala kikamilifu ulimwengu na kwamba
anatupenda.
“Kwamba
Mungu husababisha.” Kana mbunifu nyuma ya kila kitu. Maisha
yako siyo matokeo ya bahati mbaya, ajali, au bahati nzuri. Kuna msanifu nyuma.
Historia ni hadithi yake.
Mungu anavuta nyuzi. Tunafanya makosa, lakini Mungu hakosei kamwe. Mungu hawezi kufanya kosa-kwa sababu yeye ni Mungu.
“Kila
kitu.” Mpango wa Mungu kwa maisha yako unahusisha yote yanayokutokea –
pamoja na makosa yako, dhambi zako, na maumivu yako. Pia ni pamoja na magonjwa,
madeni, majanga, talaka, kifo cha uwapendao. Mungu anaweza kuleta mema kutokana
na jambo ovu sana. Alifanya hivyo pale Kalvari.
“Kufanya
kazi pamoja”: Siyo kwa kipekee au kwa
kujitegemea. Matukio katika maisha yako hufanya kazi pamoja katika mpango wa Mungu Siyo matukio yaliyojitenga, lakini matukio
yanayotegemeana katika mchakato mzima wa kukufanya ufanane na Kristo. Ili
kutengeneza keki lazima utumie unga wa ngano, chumvi, yai bichi, sukari, na
mafuta. Kama kila kimoja kikiliwa peke yake hakina ladha nzuri au hata ni
kichungu. Lakini ukivioka pamoja vinakuwa chakula kitamu. Kama ukimpa Mungu
maono yako yote mabaya, matukio yasiyopendeza, atayaunganisha pamoja kuwa kitu
chema.
“Kwa
ajili ya mema”: Hii si kwamba kila kitu maishani
ni chema. Mengi yanayotokea katika ulimwengu ni maovu na mabaya, lakini Mungu
ni mtaalam wa kutoa mema kutokana na hayo. Katika ukoo wa Yesu Kristo, Mathayo
6:10 (KJV) wanawake wanne wameorodheshwa: Tamari, Ruthu, Rahabu, na Bethsheba.
Tamari alimhadaa baba mkwe wake. Rahabu alikuwa kahaba. Ruthu hakuwa Myahudi na
alivunja sheria kwa kuolewa na Myahudi. Bethsheba alitenda uzinzi na Daudi,
jambo lililoleteleza mauaji ya mume wake. Hizi hazikuwa ni sifa nzuri, lakini
Mungu alileta mema kutokana na mabaya, na Yesu akaja kupitia ukoo wao. Kusudi
la Mungu ni kubwa kuliko matatizo yetu, maumivu yetu na hata dhambi yetu.
“Ya
wale wampendao Mungu na wameitwa”: Ahadi
ya Mungu ni kwa watoto wa Mungu tu. Si kwa kila mmoja. Kila kitu hufanya kazi
pamoja kwa ubaya
kwa wale wanaoishi wakimpinga Mungu na kukazia kufuata njia zao.
“kulingana
na lengo lake.” Lengo hilo ni lipi? Ni kwamba
sisi “tufanane na Mwana wake.” Kila
kitu Mungu anachokiruhusu kutokea katika maisha yako kinaruhusiwa kwa kusudi
hilo!
KUJENGA TABIA YA MFANO WA KRISTO
Sisi ni kama lulu, tumechongwa kwa nyundo na tezo ya taabu nyingi.
Kama nyundo ya sonara haina nguvu sana kuweza kuondoa mikwaruzo, Mungu atatumia
nyundo nzito zaidi. Kama sisi ni jeuri zaidi, anatumia nyundo nzito ya
kunyanyuliwa na chombo maalum. Atatumia chochote kile.
Kila tatizo ni nafasi ya kujenga tabia, na kadiri linavyokuwa gumu
zaidi, ndivyo kunakuwa na matokeo makubwa katika kujenga msuli wa kiroho na
uadilifu. Paulo alisema, “Tunajua kwamba mateso haya yanaleta
subira. Na subira huleta tabia bora.”
Warumi 5:3-4 (NCV) Kile kinachotokea kwa maisha yako ya nje si cha muhimu sana
kama kile kinachotokea ndani yako. Mazingira yako ni ya muda mfupi, lakini
tabia yako itadumu milele.
Biblia hufananisha majarikbu na moto wa kusafisha madini ambao
huchoma takataka zote. Petro alisema, “Mateso haya huja
ili kuthibitisha kwamba imani yenu ni safi. Usafi huu wa imani ni bora sana
kuliko dhahabu.” 1 Petro 1:7a (NCV) Mfua fedha
aliulizwa, “Je, unafahamu vipi kwamba sasa fedha ni safi? Alijibu, “ninapoona
sura yangu ndani yake.” Unapokuwa umesafishwa kwa majaribu, watu wanaweza
kuiona sura ya Kristo ndani yako. Yakobo alisema, “Katika matatizo,
maisha yenu ya imani yanajitokeza nje na kuonyesha rangi yake halisi.” Yakobo 1:3 (Msg)
Kila kinachotokea kwa maisha yako ya nje si cha
muhimu kama kile kinachotokea ndani yako. |
KUPOKEA MATATIZO KAMA KRISTO
Matatizo hayaleti mara moja yale Mungu anakusudia. Watu wengi huwa
na uchungu, badala ya kufurahi, na kamwe hawakui. Unapaswa kuyapokea kama vile
Kristo angeyapokea.
Kumbuka
mpango wa Mungu ni mwema. Mungu anajua kilicho bora kwako na
anakutakia mema moyoni mwake. Mungu alimwambia Yeremia, “Mipango
niliyo nayo kwa ajili yenu ni mipango ya kuwapa mafanikio na wala si kuwapa
mabaya, mipango ya kuwapatia tumaini na hatima njema.” Yeremia 29:11 (NIV) Yusufu alielewa ukweli huu alipowaeleza
ndugu zake waliomuuza utumwani, “Ninyi mlinikusudia mabaya, lakini
Mungu aliyakusudia kwa mema.” Mwanzo 50:20 (NIV) Hezekia naye
alionyesha mtazamo huo huo alipopata tisho la kufo kwa ugonjwa: “Ilikuwa
ni kwa ajili ya faida yangu kwamba nilipatwa na wakati mgumu kama huo.” Isaiah 38:17 (CEV) Mungu akisema hapana unapoomba kupata nafuu,
kumbuka, “Mungu anafanya kilicho chema kwetu,
akitufundisha kuishi katika utakatifu wa Mungu ipasavyo.” Waebrania 12:10b (Msg)
Ni jambo la muhimu kwamba utazame mpango wa Mungu daima, si
maumivu wala matatizo yako. Hivi ndivyo Kristo alivyoweza kuvumilia maumivu ya
msalaba, na tunashauriwa kufuata kielelezo hiki: “Mtazameni Kristo,
kiongozi wetu na makufunzi wetu. Alikuwa tayari kufa kifo cha aibu msalabani
kwa sababu ya furaha aliyofahamu ataipata baada ya hapo.” Waebrania 12:2a (LB) Carrie ten Boom, aliyeteseka katika
magereza ya Nazi ya kifo, alieleza nguvu ya kuwa na mwelekeo: “Ukiutazama
ulimwengu, utafadhaishwa. Ukitazama ndani utahuzunika. Lakini ukimtazama
Kristo, utapata pumziko!” Mwelekeo wako utakuwa kigezo cha hisia zako. Siri ya
uvumilifu ni kukumbuka kwamba maumivu yako ni ya muda mfupi lakini zawadi yako
ni ya milele. Musa alivumilia maisha ya matatizo ya milele. “Kwa
kuwa aliyatazamia malipo.” Waebrania 11:26 (NIV) Paulo
alivumilia magumu vilevile. Alisema, “Mateso yetu ya
sasa ni madogo na hayatadumu kwa muda mrefu sana. Lakini yanatuletea utukufu
usiopimika ambao utadumu milele.” 2
Wakorintho 4:17 (NLT)
Usiwe mtu wa kufikiri kwa karibu. Kaza macho kwa matokeo ya
mwisho: “Kama tutashiriki utukufu wake, ni lazima pia
tushiriki mateso yake. Mateso tunayopata sasa si kitu chochote ukilinganisha na
utukufu atakaokupatia baadaye.” Warumi 8:17-18 (NLT)
Furahi
na kushukuru. Biblia inatuambia “Shukuruni
katika kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.” 1 Wathesalonike 5:18 (NIV) Inawezekanaje? Angalia, Mungu
anatuambia kushukuru “Katika kila jambo” siyo “Kwa kila jambo.” Mungu hategemei
wewe umshukuru kwa mabaya, kwa dhambi, kwa mateso, au kwa matokeo ya mambo haya
yenye maumivu katika ulimwengu. Badala yake, Mungu anakutaka umshukuru kwamba
atatumia matatizo yako kutimiza malengo yake.
SIKU YA ISHIRINI NA TANO: KUBADILIS HWA NA TAABU |
Tunaweza kufurahi pia katika kujua kwamba Mungu yuko pamoja nasi
katika maumivu hayo. Hatumtumikii Mungu aliye mbali na kujitenga ambaye anatupa
maneno ya juu juu tu kututia moyo akiwa amekaa pembeni! Badala zake yeye
huingia katika mateso yetu. Yesu alifanya hivyo kwa kuchukua ubinadamu wetu, na
Roho wake anafanya hivyo ndani yetu sasa. Mungu kamwe hatatuacha peke yetu.
Kataa
kukata tamaa. Uwr mvumilivu na udumu. Biblia
husema, “Mchakato huo na uendelee mpaka uvumilivu wenu
uimarishwe, na mpate kuwa watu wenye tabia iliyopevuka … bila mawaa ya udhaifu.” Yokobo 1:3-4 (Ph)
Kujenga tabia ni mchakato wa polepole. Kila tunapojaribu kuepuka
au kutoroka magumu katika maisha, tunakatisha mchakato huo, na kuchelewesha
kukua kwetu, na hakika mwisho wetu unakuwa na maumivu mabaya zaidi-hali ya
kutokufaa inayoambatana na kukana na kuepuka. Ukielewa matokeo ya milele ya
kukua kwa tabia yako, utasali mara chache sala za “Nifariji” (“Nisaidie njihisi vizuri”) na utasali mara nyingi sala za “Nifananaji.”
(“Tumia jambo hili kunifanya nifanane na wewe zaidi”)
Unafahamu kwamba unakua unapoanza kuona mkono wa Mungu katika
mazingira magumu, ya ajabu na yasiyo na maana maishani.
Kama unakabiliwa na matatizo sasa hivi, usiulize, “Kwa nini mimi?”
Badala yake uliza, “Mungu unataka nijifunze nini?” Kisha mwamini Mungu na dumu
katika kutenda yaliyo haki. “Mnahitaji kusimama imara, mkikaa
katika mpango wa mungu ili mpate kuwepo kwenye ahadi ya utimilifu.” Waebrania 10:36 (Msg) Usikate tamaa-kua!
SIKU YA
ISHIRINI NA TANO KUFIKIRI
JUU YA LENGO LANGU Jambo la Kutafakari: kuna kusudi nyuma ya kila tatizo. Kifungu cha Kukumbuka: “Nasi twajua
ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi kuwapatia mema wale wampendao,
wale walioitwa kwa kusudi lake.” Warumi
8:28 (NIV) Swali la Kujiuliza: Ni tatizo gani katika maisha yangu
limenisababisha kukua kwa kiwango kikubwa? |
Siku Ya Ishirini
Na Sita: Kukua Kwa Njia Ya Majaribu
Heri
mtu yule asiyetenda dhambi anapojaribiwa, kwa kuwa baada ya hapo atapokea
zawadi
ya taji la uzima ambayo Mungu amewaahidi wale wampendao.
Yakobo 1:12 (LB)
Majaribu
yangu yamekuwa ni shahada yangu ya juu
Katika
mambo ya Mungu.
Martin Luther.
Kila jaribu ni nafasi ya kutenda mema.
Katika kuelekea kukua kiroho, hata majaribu huwa ni jiwe la
kukanyaga badala ya jiwe la kukwaza unapotambua kwamba ni wakati mwingine wa
kutenda jema badala ya kutenda baya. Majaribu huleta uchaguzi. Wakati majaribu
ni silaha kuu ya Shetani ili kukuharibu, Mungu anapenda kuyatumia kukukuza.
Kila unapochagua kufanya jema badala ya dhambi, unakua katika tabia ya Kristo.
Kuelewa jambo hili, ni lazima kwanza uziainishe sifa za tabia ya
Kristo. Moja ya maelezo mafupi ya tabia yake ni tunda la Roho: “Roho
Mtakatifu anapotawala maisha yetu, atazaa tunda kama vile: Upendo, furaha,
amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi.” Wagalatia 5:22-23 (NLT)
Sifa hizi tisa ni upanuzi wa Amri Kuu na huonyesha picha nzuri ya
Yesu. Yesu ni mkamilifu
katika upendo, furaha, amani, uvumilivu na matunda mengine yote yalikuwa ndani
ya huyu mtu mmoja. Kuwa na tunda la Roho Mtakatifu ni kuwa kama Yesu.
Je, jinsi gani basi, Roho Mtakatifu anatoa matunda haya tisa
katika maisha yako? Je, utaamka siku moja na kukuta ghafla hizi sifa zimekuwa
ndaani yako? Hapana. Tunda daima hukua na kuiva polepole.
Mungu hukuza tunda la Roho katika maisha yako kwa
kukuruhusu upite katika mazingira ambayo unajaribiwa kutenda kinyume kabisa
cha sifa ya tunda la Roho. |
Kwa mfano Mungu hutufundisha upendo kwa watu wasiopendeka karibu yetu. Haihitaji tabia kupenda watu wanaopendeka na pia
wanaokupenda. Mungu hutufundisha furaha
halisi katikati ya huzuni tunapomgeukia. Raha (happiness) hutegemea mazingira
ya nje, lakini furaha (joy) hutegemea uhusiano wako na Mungu.
Mungu hukuza amani halisi ndani yetu, siyo kwa kufanya mambo
yatendeke kama tulivyopanga, lakini kwa kuruhusu nyakati za machafuko na
vurugu. Mtu anaweza kuwa na amani akitazama machweo ya jua yanayopendeza au
akistarehe mapumzikoni. Tunajifunza amani halisi kwa kuchagua kumwamini Mungu
katika mazingira ambayo tunajaribiwa kuhofu au kuogopa. Vivyo hivyo, uvumilivu unakuzwa katika mazingira ambayo tunalazimika kusubiri na
tunajaribiwa kukasirika.
Mungu hutumia mazingira ya kinyume cha kila tunda ili kutupa
uchaguzi. Huwezi kudai kuwa mwema kama hujajaribiwa kuwa mbaya. Huwezi kudai
kuwa mwaminifu kama hujawahi kupata nafasi ya kutokuwa mwaminifu. Uaminifu
unajengwa kwa kushinda jaribu la kutokuwa mwaminifu, unyenyekevu hukua
tunapokataa kuwa na majivuno; na uvumilivu hukua kila wakati unapokana jaribu
la kukata tamaa. Kila unaposhinda jaribu, unakuwa kama Kristo zaidi!
JINSI JARIBU LINAVYOFANYA KAZI
Inasaidia kufahamu kwamba Shetani anaweza kueleweka kabisa.
Ametumia mkakati ule ule na mbinu za zamani tangu uumbaji. Majaribu yote
hufuata mfumo ule ule. Ndiyo maana Paulo alisema, “Tunazifahamu hila
zake za uovu.” 2 Wakorintho 2:11 (NLT) Kutoka
Biblia tunajifunza kwamba jaribu hufuata mchakato wa hatua nne, ambao ndio
shetani aliutumia kwa Adamu na Hawa na kwa Yesu pia.
Katika hatua ya kwanza, shetani anaainisha tamaa ndani yako. Inaweza kuwa tamaa ya dhambi, kama tamaa ya kulipa
kisasi au kutawala wengine, au yaweza kuwa tamaa njema, kama vile tamaa ya
kupendwa na kuthaminiwa au kuhisi furaha. Jaribu huanza pale Shetani
anapopendekeza (kwa wazo) kwamba ufuate tamaa mbaya, au utimize ile tamaa njema
kwa njia mbaya au kwa wakati usio sahihi. Wakati wote jihadhari na njia mbaya
au kwa wakati usio sahihi. Wakati wote jihadhari na njia za mkato.Mara nyingi
ni majaribu! Shetani ananong’oneza, “Unastahili hicho! Kichukue sasa!
Kitafurahisha … au kitakufanya ujisikie vizuri.”
Tunadhani jaribu liko karibu nasi, lakini Mungu anasema linaanzia
ndani yetu. Kama usingekuwa na tamaa ya ndani, jaribu lisingekuvuta, jaribu
mara nyingi huanzia akilini mwako, siyo katika mazingira. Yesu alisema, “Kwa
kuwa kutoka ndani ndani ya moyo wa mtu, hutoka mawazo mabaya, zinaa, wizi,
uuaji, uzinzi uchoyo, ufisadi, uongo, tamaa mbaya, husuda, masingizio, kiburi,
na upumbavu. Mambo yote haya maovu hutoka ndani.”
Marko 7:21-23 (NLT) Yakobo hutuambia kwamba kuna “Jeshi zima la
tamaa mbaya ndani yako.” Yakobo 4:1 (LB)
Tunadhani jaribu liko karibi nasi lakini Mungu
anasema linaanzia ndani yetu. |
Hatua ya tatu ni udanganyifu. Shetani hawezi kusema ukweli na
anaitwa “Baba wa Uongo.”
(Yohana 8:44) Chochote atakachokuambia kitakuwa uongo au nusu ukweli tu.
Shetani hutoa uongo wake badala ya kile Mungu alichokwisha sema katika Neno
lake. Shetani anasema, “Hamtakufa, mtakuwa na hekima kama Mungu. Unaweza
kuchukua. Kakuna atakayefehamu. Itatatua tatizo lako. Zaidi ya hapo kila mmoja
anafanya jambo hili. Ni dhambi ndogo tu.” Lakini dhambi ndogo ni kama kuwa na
mimba ndogo: Baadaye itajitokeza tu.
Hatua ya nne ni kutokutii.
Hatimaye unatendea kazi yale mawazo ambayo umekuwa unaumba akilini mwako. Kile
kilichoanza kama wazo kinazaliwa katika tabia. Unatenda kile ambacho
kimekuvutia. Unaamini uongo wa Shetani na kuanguka katika mtego ambao yakobo
anaonya: “Tunajaribiwa pale tunapovutwa na kunaswa na
tamaa yetu mbaya. Kisha tamaa yetu mbaya huchukua mimba na kuzaa dhambi; na
dhambi inapokomaa, huzaa mauti. Msidanganyike, rafiki zangu wapendwa!” Yakobo 1:14-16 (TEV)
KUSHINDA MAJARIBU
Kuelewa jinsi jaribu linavyofanya kazi ni msaada mkubwa, lakini
kuna hatua maalum unazotakiwa kuchukua ili kushinda jaribio hilo.
Kataa
kutishwa. Wakristo wengi huogopa na kuvunjwa moyo kwa mawazo ya majaribu,
kuhisi hukumu, kwamba hawako “juu” ya majaribu. Wanahisi aibu kwa kujaribiwa.
Huu ni uelewa potofu kuhusu kukua kiroho. Kamwe hutakua kiasi cha kutojaribiwa.
Kwa maana nyingine yaone majaribu kama heshima. Shetani hawezi kuwajaribu
wale ambao tayari wanafanya matakwa yake maovu; wao ni wa kwake tayari. Jaribu
ni alama kwamba Shetani anakuchukia, siyo dalili ya udhaifu au kuwa mtu wa
dunia. Pia ni sehemu ya kawaida ya wanadamu na kuishi katika ulimwengu
ulioanguka. Usishangae wala kushitushwa, au kuvunjwa moyo. Ukubali hali halisi
kuhusu ulazima wa kujaribiwa; hutaweza kuepuka kujaribiwa kabisa. Biblia
inasema, “Mnapojaribiwa, … siyo “kama.” Paulo alishauri, “Kumbukeni kwamba majaribu yanayokuja
katika maisha yenu hayana tofauti na yale yanayowapata wengine.” 1 Wakorintho 10:13 (NLT)
Siyo dhambi kujaribiwa. Yesu alijaribiwa, lakini hakutenda dhambi.
(Waebrania 4:15) Jaribu huwa dhambi unapolikubali. Martin Luther alisema, “Huwezi
kuzuia ndege wasiruke juu ya kichwa chako lakini unaweza kuwazuia wasijenge
kiota kwenye nywele zako.” Huwezi kumzuia Ibilisi asilete mawazo kwako, lakini unaweza kuchagua kutoyatafakari na kuyatendea kazi.
Mfano, watu wengi hawajui tofauti ya mvuto wa kimwili au kusisimuka kingono, na tamaa mbaya (lust). Haviko sawa. Mungu alimuumba kila mmoja wetu na tamaa za tendo la ndoa, na hiyo ni vyema. Kuvutiwa na kusisimka ni mwitikio wa asili na wa kawaida na kwa uzuri wa mwili-mwitikio huo tulipewa na Mungu-wakati tamaa
Jaribu ni alama kwamba shetani anakuchukia, Siyo
dalili ya udhaifu au kuwa mtu wa dunia |
Kwa Kweli, kadiri unavyokua na kuwa karibu na Mungu, ndivyo
Shetani atazidi kukujaribu. Mara ulipoanza kuwa mtoto wa Mungu, Shetani
alikuwekea “mkataba.” Wewe ni adui yake, na anapanga namna ya kukuangusha.
Wakati mwingine unapokuwa unasali Shetani atakuchanganya au kuleta
mawazo machafu ili tu akuvuruge na kukuaibisha. Usitishwe wala kuaibishwa na
hili, lakini tambua kwamba Shetani anaogopa sala zako na atajaribu kila kitu
kuzizuia. Badala ya kujihukumu mwenyewe kwa kufikiri “Je, niliwezaje kufikiri
wazo hilo?” lione kama ni usumbufu kutoka kwa Shetani na mara moja mwelekee
Mungu.
Elewa
mfumo wako wa kujaribiwa na uwe tayari kwa huo.
Kuna hali fulani ambazo hukufanya uwe dhaifu zaidi kwa majaribu kuliko
nyingine. Mazingira mengine yatakufanya ujikwae mara moja ambapo mengine
hayakusumbui sana. Mazingira haya ni ya pekee kwa udhaifu wako, na unahitaji
kuyaainisha kwa sababu Shetani anayajua hakika! Anajua ni nini hukuweka tayari
kuanguka, na daima anafanya kazi ili kukuingiza katika mazingira hayo. Petro
anaonya, “Jihadharini. Shetani amejiweka tayari kuvamia,
na angependa kuwakamata kwa kuwashtukiza mkiwa usingizini.” 1 Petro 5:8 (Msg)
Jiulize mwenyewe, “Lini
ninajaribiwa kwa kiasi kikubwa?” Siku gani ya juma? Wakati gani wa siku?
Jiulize, “Ni wapi
ninajaribiwa zaidi?” Nyumbani? Kazini? Kwa jirani? Kwenye baa ya michezo?
Kwenye kiwanja cha ndege au hotelini nje ya mji?
Jiulize, “Nani yuko nami
ninapojaribiwa zaidi? Rafiki? Wafanyakazi wenzangu? Wageni? Ninapokuwa peke
yangu?” Pia jiulize, “Najisikiaje ninapokuwa nimejaribiwa zaidi?” Yaweza kuwa unapokuwa umechoka, uko mpweke,
au umechoshwa, umesongwa na mambo mengi. Inawezekana unapokuwa umeumizwa, au
umekasirika, au umehofu, au baada ya mafanikio makubwa, au umefaulu kiroho.
Unapaswa kutambua mfumo wako wa kajaribiwa na ujiandae kuepuka
mazingira hayo kadiri iwezekanavyo. Biblia inatuambia mara nyingi kujiandaa na
kuwa tayari kukabiliana na majaribu. (Mathayo 26:41; Waefeso 6:10-18; 1
Wathesalonike 5:10-18; 1 Petro 1:13; 4:7; 5:8.) Paulo alisema, “Msimpe
Ibilisi nafasi.” Waefeso 4:27 (TEV) Kupanga kwa
busara hupunguza majaribu. Fuata ushauri wa Mikthali: “Panga
kwa uangalifu kile Unachokifanya … Epuka uovu na uende kwa unyoofu. Usiende
hatua moja nje na njia sahihi.” Mithali 4:26-27 (TEV) “Watu
wa Mungu huepuka njia za uovu, na wanajilinda kwa kuangalia wanakokwenda.” Mithali 16:17 (CEV)
Omba
msaada wa Mungu. Mbingu ziko tayari masaa ishirini
na nne kupokea mwito wa hali ya hatari. Mungu anapenda umwombe msaada katika
kushinda majaribu. Anasema, “Ukaniite wakati wa mateso. Nitakuokoa
na utaniheshimu.” Zaburi 50:15 (GWT)
SIKU YA ISHIRINI NA SITA: KUKUA KWA NJIA YA MAJARIBU |
Biblia inatuhakikishia kwamba kilio chetu kitasikilizwa kwa sababu
Yesu anatuhurumia katika kuhangaika kwetu. Alipatwa na majaribu kama yetu. “Yeye
anaelewa udhaifu wetu, kwa kuwa alipitia majaribu kama tunayopata sisi, lakini
hakutenda dhambi.” Waebraniaa 4:15 (NLT)
Kama Mungu anasubiri kutusaidia ili tushinde majaribu, kwa nini
hatumgeukii mara nyingi? Kusema wazi, wakati mwingine hatuhitaji kusaidiwa! Tunataka
kuingia katika jaribu ingawa tunajua ni vibaya. Na kwa wakati huo tunadhani
tunajua kinachofaa kwetu kuliko Mungu anavyojua.
Nyakati nyingine tunajisikia vibaya kumwomba Mungu msaada kwa
sababu tunaingia katika jaribu hilo mara kwa mara. Lakini Mungu haudhiki, hachoshwi,
wala hawi bila subira tunapoendelea kumwendea tena. Biblia inasema, “Na
tuwe na ujasiri basi, tukiendee kiti cha enzi cha Mungu, ambapo kuna neema.
Hapo tunapokea rehema na kupata neema ya kutusaidia tunapoihitaji.” Waebrania 4:16 (TEV)
Upendo wa Mungu ni wa milele, na uvumilivu wake hudumu milele.
Kama unaweza kumlilia Mungu mara mia mbili kwa siku moja akusaidie kushinda
jaribu fulani bado atakuwa tayari kukupa neema na rehema, hivyo mwendee na
ujasiri. Mwombe nguvu za kutenda kitu sahihi na mtumaini atakupatia.
Majaribu hutusaidia kuendelea kumtegemea Mungu. Kama vile mizizi
inavyopata nguvu upepo unapovuma dhidi ya mti, hivyo kila wakati unaposhinda jaribu
unazidi kufanana na Yesu. Unapojikwaa-kitu ambacho utafanya-siyo kifo chako.
Badala ya kukubali jaribu au kukata tamaa, mtazame Mungu, mtumaini akusaidie,
na kumbuka thawabu inayokungojea: “Watu wanapojaribiwa na wakadumu kuwa
imara, wanafurahi. Baada ya kuthibitisha imani yao, Mungu atawapa thawabu ya
uzima wa milele.” Yakobo 1:12 (NCV)
SIKU YA ISHIRINI NA SITA KUFIKIRI JUU YA LENGO LANGU Jambo la Kutafakari: Kila jaribu ni nafasi ya kutenda mema. Kifungu cha Kukumbuka: “Mungu
huwabariki watu wale wanaovumilia majaribu. Baada ya hapo wataipokea taji
ya uzima ambayo Mungu amewaahidi wale wampendao.”
Yakobo 1:12 (NLT) Swali la Kujiuliza: Je, ni sifa gani ya mfano wa tabia ya
Kristo naweza kuikuza kwa kushinda jaribu la mara kwa mara linalonipata? |
Kimbia kutoka
katika chochote kinachokupa mawazo mabaya … lakini
kaa karibu na
chochote kinachokufanya utake kutenda mema.
2 Timothy 2:22 (LB)
Kumbukeni kwamba
majaribu yanayowapata maishani mwenu hayana
tofauti na yale
yanayowapata wengine. Na Mungu ni mwaminifu.
Atalifanya jaribu
lisiwe kubwa kuliko uwezo wenu wa kustahimili.
Mnapojaribiwa,
atawaonyesha mlango wa kutokea ili msije mkaanguka.
1
Wakorintho 10:13 (NLT)
Siku zote kuna mlango wa kutokea.
Unaweza kuhisi kwamba wakati mwingine jaribu ni zito mno kwako
kulibeba, lakini huo ni uongo kutoka wa Shetani. Mungu ameahidi kamwe hataweka
mzigo mzito juu yako kuliko anachoweka ndani yako ili kustahimili. Hataruhusu
jaribu lolote ambalo huwezi kushinda. Lakini, ni lazima wewe pia ufanye sehemu
yako kwa kuweka katika matendo funguo nne za kibiblia katika kushinda majaribu.
Weka
mawazo yako kwa kitu kingine. Inaweza
kukushangaza kwamba hakuna sehemu yoyote katika Biblia tumeambiwa “kupinga majaribu.” Tumeambiwa “kumpinga
Shetani,” (Yakobo 4:7) lakini hiyo ni tofauti, kama nitakavyoeleza
baadaye. Badala yake tumeambiwa kuelekeza mawazo yetu kwa sababu kupinga mawazo
yetu haiwezekani. Badala yake huzidisha mwelekeo wetu katika kitu kibaya na
kuongeza mvuto wake. Ngoja nieleze:
Vita dhidi ya
dhambi unaishinda au kushindwa katika akili yako. Chochote kinachogusa
ufahamu wako kitakupata. |
Kwa kuwa jaribu huanza na wazo, njia ya haraka ya kumaliza mvuto
wake ni kuelekeza mawazo yako katika kitu kingine. Usipigane na wazo hilo, wewe
bedilisha tu mwelekeo wa mawazo yako na kuhusika na wazo jingine. Hii ni hatua
ya kwanza katika kushinda majaribu.
Vita dhidi ya dhambi unaishinda au kushindwa katika akili yako.
Chochote kinachogusa ufahamu wako Kitakupata. Ndiyo maana Ayubu alisema, “Nilifanya
agano na macho yangu yasitazame msichana kwa tamaa mbaya.” Ayubu 31:1 (NLT) Na Daudi aliomba, “Unigeuze macho
yangu, nisitazame yasiyofaa.” Zaburi 119:37a (TEV)
Je, umewahi kuona tangazo la chakula katika televisheni na ghafla
ukahisi njaa? Je, umewahi kumsikia mtu anakohoa na ghafla ukahisi kusafisha koo
lako? Je, umewahi kumwona mtu akipiga mwayo na wewe ukatamani kupiga mwayo?
(unaweza hata kupiga mwayo unaposoma hii!) Hiyo ndiyo nguvu ya pendekezo. Mara
nyingi ni kawaida kwetu kuelekea kule tunakoelekezea mawazo yetu. Kadiri unavyofikiri
juu ya kitu fulani, ndivyo kinavyokushika.
Ndiyo maana kurudiarudia “Ni lazima niache kula mno … au kuvuta
sigara … au kutamani” ni mkakati wa kujishinda wenyewe. Hukufanya uelekeze
mawazo yako katika kitu ambacho hutaki. Ni kama kutangaza, “Sitafanya kile
ambacho mama yangu alifanya. “Unajiweka sawa kukirudia.
Mambo ya kutawala lishe hayafanikiwi mara nyingi kwa sababu hukufanya
ufikiri juu ya chakula kila wakati, ili mradi tu upatwe na njaa. Vivyo hivyo,
msemaji anajisemea mwenyewe, “usiongope!” anajiandaa kuogopa! Badala yake
anatakiwa kuelekeza mawazo yake kwenye jambo jingine isipokuwa hisia zake-
ajielekeze kwa Mungu, umuhimu wa hotuba yake, au kwa mahitaji wasikilizaji
wake.
Majaribu huanza kwa kuteka mawazo yako. Kinachoshika mawazo yoko
husisimua hisia zako. Kisha hisia zako huchochea matendo yako, na unatenda
kufuata ulivyojisikia. Kadiri unavyojielekeza kwenye “sitaki kufanya hili, “ndivyo
linavyokuvuta kukuingiza kwenye mtandao wake.
Majaribu huanza kwa kuteka mawazo yako. Kinachoshika mawazo yako
husisimua hisia zako. Kisha hisia zako huchochea matendo yako, na unatenda
kufuata ulivyojisikia. Kadiri unavyojielekeza kwenye “sitaki kufanya hili,”
ndivyo linavyokuvuta kukuingiza kwenye mtandao wake.
Kupuuza jaribu ni bora zaidi kuliko kulipinga. Mara mawazo yako
yanapoelekea kwenye kitu kingine, lile jaribu hupoteza nguvu zake. Hivyo jaribu
linapokupigia simu, usibishane nalo wewe kata simu tu!
Wakati mwingine inabidi kuondoka kutoka kwenye mazingira ya
jaribu. Huu ni wakati unaokubalika kukimbia. Inuka na ufunge televisheni.
Ondoka kwenye kikundi kinachosengenya. Ondoka kwenye ukumbi wa filamu. Ili
kuepuka kuumwa na nyuki kaa mbali na nyuki. Fanya kila liwezekenalo ili kugeuza
na kuelekeza mawazo yako kwa kitu kingine.
Kiroho, akili yako ni kiungo kilicho dhaifu. Ili kupunguza
kujaribiwa, jaza mawazo yako na Neno la Mungu na mawazo mengine mazuri.
Unashinda mawazo mabaya kwa kufikiri jambo zuri. Hii ni kanuni ya kubadilisha.
Unashinda ubaya kwa wema. (Warumi 12:21) Shetani hawezi kupata usikivu wako
pale mawazo yako yanapokuwa yamejaa kitu kingine. Ndiyo maana Biblia inatuambia
kwa kurudiarudia kuyapa mwelekeo mawazo yetu: “Elekezeni mawazo
yenu kwa Yesu.” Waebrania 3:1 (NIV) “Fikirini
daima juu na yesu.” 2 Timotheo 2:8 (GWT) “Jazeni
akili zenu na mambo yale yaliyo mema yanayostahili sifa: mambo yaliyo ya kweli,
yenye sifa njema, ya haki, yasiyo na taka, yakupendeza, na ya heshima.” Wafilipi 4:8 (TEV)
Kama umeamua kushinda majaribu ni lazima uitawale akili yako na
kutawala unavyopewa taarifa. Mtu mwenye hekima duniani alionya kuwa. “Angalia
unavyofikiri? Maisha yako yanafinyangwa na mawazo yako.” Mithali 4:23 (TEV) Usiruhusu takataka kuingia akilini mwako bia
kuchuja. Uwe na upembuzi. Chagua kwa uangalifu unachofikiri. Fuata kielelezo
cha Paulo: “Tunateka nyara kila fikra ipate kushuka na
kumtii Kristo.” 2 Wakorintho 10:5 (NCV) Hii ni
kazi ya kufanya maisha yote, lakini kwa msaada wa Roho Mtakatifu unaweza
kupanga upya unavyofikiri.
Weka
wazi vitu vyoko kwa rafiki mcha Mungu au kikundi cha kusaidiana. Hauhitaji kuutangazia ulimwengu mzima, lakini unahitaji walau mtu
mmoja unayeweza kumshirikisha wazi vita vyako. Biblia inasema, “Ni
vyema ukiwa na rafiki kuliko kuwa peke yako … ukianguka, rafiki yako aweza
kukuinua. Lakini ukianguka bila kuwa na rafiki karibu, hakika utapata taabu.” Mhubiri 4:9-10 (CEV)
SIKU YA ISHIRINI NA SABA: KUSHINDA MAJARIBU |
Mpango wa Mungu katika kukua kwako na kukupa uhuru unahusisha
Wakristo wengine. Ushirika halisi, na wa kweli ndiyo dawa ya vita vya peke yako
dhidi ya dhambi zisizotaka kutoka. Mungu anasema ndiyo njia pekee
itakayokuwezesha kuwa huru: “Ungamianeni dhambi ninyi kwa ninyi na
kuombeana ili kwamba mpate kuponywa.”
Yokobo 5:16 (NIV)
Je, ni kweli unataka kuponywa na hilo jaribu la daima ambalo
linakuangusha mara kwa mara? Suluhisho la Mungu ni Dhahiri: Usilizuie ndani;
kiri! Usilifiche; lifichue. Kufunua hisia zako ni mwanzo wa kuponywa kwako.
Kuficha maumivu yako hufanya yawe mazito zaidi. Matatizo hukua
gizani yakawa makubwa zaidi, lakini yakiwekwa wazi katika nuru ya ile kweli,
yanasinyaa. Unakuwa mgonjwa sawa na siri zako. Hivyo ondoa vazi la maigizo,
acha kuigiza kuwa u mkamilifu, na utembee katika uhuru.
Ukweli ni kwamba kitu chochote ambacho huwezi
kukizungumzia tayari kimeshavuka uwezo wako wa kukitawala katika maisha
yako. |
Shetani anapenda ufikiri kwamba dhambi na majaribu yako ni ya
kipekee hivyo lazima uyatunze kama siri. Ukweli ni kwamba, ssisi sote tuko
katika mtumbwi mmoja. Sote tunapigana na majaribu yale yale, (1 Wakorintho
10:3) na “Sisi sote tumetenda dhambi.” (Warumi 3:23) Mamilioni ya watu wamewahi kujihisi kama
unavyojihisi na wamepatwa vita kama ulivyo navyo sasa.
Sababu ya kuficha makosa yetu ni kiburi. Tunataka wengine wafikiri
sisi “tunatawala” kila kitu. Ukweli ni kwamba, kitu chochote ambacho kuwezi
kukizungumzia, tayari kimeshavuka uwezo wako wa kukitawala katika maisha yako:
matatizo yako ya kifedha, ndoa, watoto, mawazo, zinaa, tabia za siri, au
chochote. Kama ungeweza kulimaliza mwenyewe tayari ungekwisha fanya hivyo.
Lakini huwezi. Uwezo wa utashi na suluhisho la binafsi havitoshi.
Matatizo mengine yamezama sana, yamekuwa mazoea, na ni makubwa
sana kiasi cha wewe kutoyatatua mwenyewe. Unahitaji kikundi kidogo au rafiki
ambaye mtawajibishana ambaye atakutia moyo, atakusaidia, atakuombea, atakupenda
bila mashariti, na atakuwajibisha. Na kisha unaweza kuwatendea vivyo hivyo.
Kila mtu anapoeleza siri yake, “Sijamwambia jambo hili mtu yeyote
mpaka sasa,” napata furaha kwa ajili yake kwa sababu najua sasa mtu huyu
anakwenda kupata nafuu na uhuru. Msongo wake unakwenda kuondolewa, na kwa mara
ya kwanza wanakwenda kupata mwanga mdogo wa matumaini ya mbele. Hii hutokea
mara kwa mara tunapofanya yale Mungu anayotuagiza kwa kukiri mambo
yanayotusumbua kwa rafiki mcha Mungu.
Hebu nikuulize swali gumu: Je, ni kitu gani unajifanya kusema si
tatizo maishani mkwako? Unaogopa kuzungumzia nini? Hutaweza kulitatua mwenyewe.
Ndiyo, inatunyenyekesha kukiri udhaifu wetu kwa wengine, lakini kukosa
unyenyekevu ndicho kitu kinachokuzuia kupona. Biblia inasema, “Mungu
huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa neema wanyenyekevu. Basi nyenyekeeni
mbele za Mungu.” Yakobo 4:6-7a (NLT)
Mpinge
Shetani: Baada ya kunyenyekeza nafsi zetu na kumtii Mungu, tunaambiwa sasa
kumpinga Ibilisi. Sehemu inayobaki ya Yakobo 4:7 inasema, “Mpingeni
Ibilisi naye atawakimbia.” Hatukai tu na kuyaangalia
mashambulizi yake. Lazima tujibu mashambulizi.
Agano Jipya huyaeleza maisha ya Kikristo kama vita vya kiroho dhidi
ya nguvu za uovu, kwa kutumia maneno ya kivita kama vile kupigana, kushinda,
kupambana, kuzidi nguvu. Wakristo mara nyingi wamelinganishwa na askari
wanaopigana katika himaya ya adui.
Je, tunaweza kumpinga Ibilisi? Paulo anatuambia, “Vaeni
wokovu kama chepeo yenu, na kuchukua upanga wa Roho, ambao ni Neno la Mungu.” Wafeso 6:17 (NLT) Hatua ya kwanza ni kupokea wokovu wa Mungu.
Huwezi kumwambia Shetani hapana mpaka uwe tayari umesema ndiyo kwa yesu. Bila
Yesu sisi hatuna ulinzi wa kumzuia Ibilisi, lakini tukiwa na “chapeo ya wokovu”
akili zetu zimelindwa na Mungu. Kumbuka hili: Kama wewe ni mwamini, Shetani
hawezi kukulazimisha kufanya chochote. Anaweza tu kutoa pendekezo.
Pili, lazima utumie Neno la Mungu kama silaha yako dhidi ya
Shetani. Yesu alitoa kielelezo cha namna hii alipojaribiwa jangwani. Kila wakati
Shetani alipopendekeza Jaribu, Yesu alijibu kwa kunukuu Maandiko. Hakubishana
na Shetani. Hakusema, “sina njaa,” alipojaribiwa kutumia uwezo wake ili kutimiza
hitaji lake binafsi. Yeye alichukua tu Maandiko kutoka katika kumbukumbu yake.
Lazima tufanye vivyo hivyo. Kuna nguvu katika Neno la Mungu, na Shetani
huliogapa.
Usijaribu kamwe kubishana na Ibilisi. Yeye ni bingwa wa kubishana
kuliko wewe, amekuwa na uzoefu wa miaka maelfu. Huwezi kumlaghai Shetani kwa
kutumia akili yako au maoni yako, lakini unaweza kutumia silaha inayomfanya
atetemeke-ile kweli ya Mungu. Ndiyo maana kukariri Maandiko ni muhimu katika kushinda
majaribu. Unayapata mara moja pindi unapojaribiwa. Kama Yesu, unayo ile kweli moyoni
mwako, tayari kukumbukwa.
Kama huna vifungu vya Biblia ulivyokariri, huna risasi katika
bunduki yako! Nakupa changamoto ya kukariri kifungu kimoja kila wiki kwa maisha
yako yaliyobaki. Utakuwa na nguvu sana.
Usijaribu kamwe
kubishana na ibilisi. Yeye ni bingwa wa kubishana kuliko wewe. Amekuwa na
uzoefu wa miaka maelfu. |
Usijingize bila uangalifu kwenye mazingira yanayoleta majaribu.
Yaepuke. Mithali 14:16 (TEV) Kumbuka ni rahisi kukaa nje ya jaribu kuliko
kutoka kwenye jaribu. Biblia inasema, “Msiwe wajinga
sana na wenye kujiamini. Hakuna aliye maalum. Mnaweza kuanguka chini kabisa
kama yeyote yule. Sahauni mambo ya kujiamini, haifai. Jengeni ujasiri katika
Mungu.” 1 Wakorintho 10:12 (Msg)
SIKU YA ISHIRINI NA SABA KUFIKIRI
KWA LENGO LANGU Jambo la Kutafakari: Kuna mlango wa kutokea daima. Kifungu cha Kumbukumbu: “Mungu ni
mwaminifu. Atalifanya jaribu lisiwe zito sana kiasi cha wewe kutoweza
kulishinda. Unapojaribiwa, atakuonyesha na mlango wa kutokea ili kwamba
usije ukaanguka katika jaribu hilo.”
1 Wakorintho 10:13b (NLT) Swali la Kujiuliza: Je, nimwombe nani awe mwenzangu wa kiroho
ili anisaidie katika kushinda jaribu linalonisonga daima kwa kuniombea? |
Siku ya Ishirini na Nane: Huchukua
Muda
Kila
kitu hapa duniani kina wakati wake na majira yake.
Mhubiri 3:1 (CEV)
Nina
uhakika kwamba Mungu aliyeanza kazi njema ndani yenu ataendelea kuwasaidia
ili mkue katika neema yake hadi hapo kazi yake
ndani yenu itakapokuwa
imekamilika
katika siku ile Kristo atakaporudi.
Wafilipi 1:6 (LB)
Hakuna njia ya mkato katika kukua.
Huchukua miaka mingi kwetu kukua na kuwa watu wazima, na huchukua
kipindi kizima cha majira kwa tunda kukua na kuiva. Ndivyo ilivyo hata kwa
tunda la Roho. Kukua katika tabia ya mfano wa Kristo hakuwezi kupelekwa haraka.
Kukua kiroho, kama ilivyo kukua kimwili, huchukua muda.
Unapojaribu kuivisha tunda haraka, hupoteza ladha yake. Katika
nchi ya Marekani, nyanya huchumwa zikiwa mbichi ili zisikwaruzwe wakati wa
kupelekwa ghalani. Kisha, kabla ya kuuzwa, nyanya hizi hupuliziwa gesi ya
kaboni dioksaidi (CO2)
ili kuzigeuza kuwa nyekundu mara moja. Nyanya zenye gesi hii zinalika, lakini
hazina ladha sawa na zile zilizoachwa zikakomaa taratibu na kuivia shinani.
Wakati sisi tunahofu kuhusu tunavyokua karaka, Mungu anahusika na
kiasi cha nguvu tulizoongeza. Mungu hutazama maisha yetu katika mtazamo wa umilele,
hivyo hana haraka kamwe.
Wakati sisi tunahofu kuhusu tunavyokua haraka, Mungu
anahusika na kiasi cha nguvu tulizoongeza. |
Adams alitoa kielelezo hiki: Kabla Kristo hajavamia maisha yetu
wakati wa kuongoka, wakati mwingine anapaswa “kutulainisha” kwa kuruhusu matatizo
tusiyoweza kuyastahimili. Hapo baadhi hufungua maisha yao kwa Kristo mara ya
kwanza anapogonga langoni kwao, wengi wetu hupinga na kujilinda. Hali yetu
kabla ya kuokoka ni Yesu anasema, “Tazama nasimama mlangoni na kupiga
bomu.”
Mara unapofunguka kwa ajili ya Kristo, Mungu anapata “kichwa-cha-ufukweni”
maishani mwako. Unaweza kufikiri umejisalimisha maisha yako yote kwake, lakini
ukweli ni kwamba, kuna mambo mengi maishani mwako ambayo hata huyajui. Unaweza
tu kumpa Mungu kiasi chako unachokifahamu kwa wakati huo. Sawa, mara Kristo
anapopewa kichwa – cha – ufukweni, anaanza mkakati wa kuchukua sehemu zaidi za
utawaha hadi hapo maisha yako yote atakapoyachukua. Kutakuwa na mapambano na
vita, lakini matokeo hayatakuwa na mashaka kamwe. Mungu ameahidi kwamba, “Yeye
alivyeanza kazi njema ndani yenu ataiendeleza hadi ikamilike.” Wafilipi 1:6 (NIV)
Kufanya wanafunzi ni mchakato wa kufanana na Kristo. Biblia
inasema, “Tunafikia kiwango halisi cha kukua – kiwango
cha kukua kinachomaanishwa na utimilifu wa Kristo.”
Waefeso 4:13 (Ph) Mfano wa Kristo ndio hatima yako, lakini safari itadumu kwa
muda wa maisha yako yote.
Mpaka hapa tumeshaona kwamba safari hii inahusu kuamini (kwa njia ya kuabudu), kuwa sehemu ya (kwa njia ya ushirika), na kuwa (kwa njia ya kuwa mwanafunzi). Kila siku Mungu nataka uwe kama
Yeye kidogo: “Mmeanza kuishi maisha mapya, kwa hayo
mnafanywa wapya na kuwa kama Yeye aliyewatengeneza.”
Wakolosai 3:10a (NCV)
Siku hizi tumejawa na haraka, lakini Mungu anapenda nguvu na
uimara kuliko wepesi. Tunataka suluhisho la mara moja, la njia ya mkato, na la
papo kwa hapo. Tunataka mahubiri, semina au tendo fulani ambalo kwa mara moja
litatatua tatizo, kuondoa jaribu, na kutuweka huru na maumivu. Lakini kukua
halisi hakupatikani kwa tendo moja, haijalishi lina nguvu kiasi gani. Kukua ni
hatua ya taratibu. Biblia inasema, “Maisha yetu yaking’aa taratibu na
kupendeza zaidi kadiri Mungu anavyoingia katika maisha yetu na tunakuwa kama
Yeye.” 2 Wakorintho 3:18b (Msg)
KWA NANI HUCHUKUA MUDA MREFU?
Ingawa Mungu angeweza
kutubadilisha mara moja, amechagua kufanya hivyo polepole. Yesu anafanya kwa
makusudi katika kuwaendeleza wanafunzi wake. Kama vile Mungu alivyowaruhusu
wana wa Israeli kuichukua nchi ya ahadi “kidogo kidogo” (Kumbukumbu 7:22) ili wasije wakalemewa, anapenda kufanya hatua
kwa hatua katika maisha yetu.
Kwa nini huchukua muda mrefu kubadilika na kukua? Kuna sababu
kadhaa.
Sisi
hujifunza polepole. Mara nyingi tunajifunza somo mara
arobaini au hamsini ndipo tunaelewa sawa sawa. Matatizo yanaendelea kujirudia,
na tunafikiri, “Lisirudie tena! Nimejifunza tayari!” – lakini Mungu anajua
zaidi. Historia ya wana wa Israel hutupa kielelezo cha jinsi tunavyosahau
haraka masomo Mungu anayotufundisha na jinsi ambavyo tunarudi haraka sana
katika mwenendo wetu wa zamani. Tunahitaji kufundishwa kwa kurudiarudia.
Tuna
mengi ya kuacha. Watu wengi huenda kupata ushauri wakiwa
na tatizo la binafsi au la mahusiano ambalo limechukua miaka kukua na wanasema, “nahitaji unitatulie tatizo langu. Nina saa
moja tu.” Kwa kutokuelewa wao hutegemea kupata suluhisho la mara moja kwa
tatizo lililozamisha mizizi yake kwa muda mrefu. Kwa kuwa matatizo yetu yaliyo
mengi-tabia zetu zote mbaya-hayakujitokeza usiku mmoja, si kweli kutegemea
huyaondoa mara moja. Hakuna kidonge, sala, wala kanuni inayoweza kuondoa hapo
hapo uharibifu wa miaka mingi. Huhitajika kazi ngumu ya kuondoa na kuweka upya.
Biblia huita jambo hili “Kuondoa utu wa kale” na “kuvaa utu mpya.” (Warumi 13:12; Efeso 4:22-25; Kolosai 3:7-10, 14.) Ingawa
ulipewa asili mpya wakati ulipookoka, bado unazo tabia za kale, mfumo, na
matendo yanayohitaji kuondolewa na kuweka mapya.
Hakuna kukua bila kubadilika, hakuna kubadiliko bila
hofu na hasara, na hakuna hasara bila maumivu. |
Kukua
kunaumiza na kunaogopesha. Hakuna kukua bila kubadilika,
hakuna kubadilika bila hofu au hasara, na hakuna hasara bila maumivu. Kila
dadiliko huja na hasara fulani: ni lazima kuacha njia ya zamani ili upate zile
mpya. Tunaogopa hasara hizi, hata kama njia zetu za zamani zilikuwa
zinajikwamisha, kwa sababu, kama nguo iliyochakaa, ilikuwaa nzuri na umeizoea.
Watu mara nyingi hujenga utambulisho wa utu wao katika mapungufu
yao. Tunasema, “Ni kama mimi tu kuwa …” na “ndivyo nilivyo tu.” Hofu
iliyofichika ni kwamba kama nitaacha tabia yangu, maumivu yangu, mazoea yangu,
je nitakuwa nani? Hofu hii bila shaka itapunguza kasi ya kukua kwako.
SIKU YA ISHIRINI NA NANE: HUCHUKUA
MUDA |
Kuna njia moja tu ya kukuza mwenendo wa tabia ya mfano wa Kristo:
Lazima ujizoeze-na hivyo huchukua muda! Hakuna mwenendo wa mara moja. Paulo
alimsihi Timotheo, “Tenda mambo haya. Toa maisha yako kwa
ajili ya hayo ili kila mtu ayaone maendeleo yako.”
1 Timotheo 4:15 (GWT)
Ukifanyia mazoezi kitu fulani, unakimudu. Marudio ni mama wa tabia
na ujuzi. Mazoea haya yanayojenga tabia mara nyingi yanaitwa “maadili
ya kiroho,” na kuna vitabu vingi vizuri vinavyoweza kukufundisha mambo
haya. Angalia nyongeza ya 2 kwa ajili ya vitabu vilivyopendekezwa kusoma kwa
ajili ya kukua kiroho.
USIHARAKISHE
Kadiri unavyokua kiroho, kuna njia kadhaa za kushirikiana na Mungu
katika mchakato huo.
Amini
Mungu anafanya katika maisha yako hata pale unapokuwa huhisi kitu. Kutua kiroho wakati mwingine ni kazi inayochosha, unapiga hatua
moja ndogo kwa muda. Tegemea maendeleo ya polepole. Biblia inasema, “Kila
kitu hapa duniani kina wakati wake na majira yake.”
Mhubiri 3:1 (CEV) Kuna majira katika maisha yako ya kiroho pia. Wakati mwingine
utakuwa na kipindi kifupi cha kukua (wakati wa vuli) kikifuatwa na kipindi cha
kuimarishwa na kujaribiwa (kipupwe na masika).
Vipi kuhusu matatizo hayo, mazoea, na maumivu ambayo ungependa
yaondolewe kimiujiza? Ni vyema kuomba ili kupata miujiza, lakini usivunjike
moyo kama jibu litakuja katika mabadiliko ya taratibu. Baada ya muda, kijito
cha maji cha polepole na cha kudumu kitamomonyoa mwamba mgumu na kugeuza miamba
mikubwa kuwa vipande vidogo vidogo. Baada ya muda mrefu, mmea mdogo unaweza
kugeuka na kuwa mti mkubwa wenye urefu wa futi 350.
Tunza
kitabu cha kumbukumbu (journal) kwa ajili ya masomo uliyojifunza. Hiki siyo kijitabu cha matukio ya kila siku, lakini ni cha rekodi
ya mambo unayojifunza. Andika ufahamu na masomo ya maisha Mungu anayokufundisha
kumhusu, kuhusu wewe, kuhusu maisha, mahusiano, na kila kitu. Yaandike ili
upate kuyarudia na kuyakumbuka na pia kuwapa kizazi kijacho. (Zaburi 102:18; 2
Timotheo 3:14.) Sababu ya kujifunza tena somo ni kwamba tunasahau. Kurudia
kijitabu chako cha mambo yako ya kiroho mara kwa mara kwaweza kukuponya na
maumivu mengi ya moyo yasiyo ya lazima. Biblia inasema, “Imetupasa
kuyashika sana hayo tuliyosikia ili tusije tukapotoka.” Waebrania 2:1 (Msg)
Uwe
mvumilivu kwa Mungu na kwako mwenyewe.
Moja ya mambo ya kukatisha tamaa katika maisha ni kwamba ratiba ya Mungu ni
mara chache sana hufanana na yetu. Mara nyingi sisi tuna haraka wakati Mungu
hana haraka. Unaweza kuhisi kukata tamaa kwa maendeleo kidogo unayofanya katika
maisha. Kumbuka kwamba Mungu kamwe hana haraka, lakini anatunza muda daima.
Atatumia muda wa maisha yako yote kukuandaa kwa ajili ya maisha ya milele.
Mungu kamwe hana
haraka lakini anatunza muda daima. |
Kinyume na vitabu vingi vinavyopendwa, hakuna hatua rahisi za
kufikia kukuka au siri za kuwa mtakatifu mara moja. Mungu anapotaka kutengeneza
uyoga, hufanya hivyo kwa usiku mmoja, lakini anapotaka kutengeneza mti mkubwa
(oak), huchukua miaka mia moja. Nafsi kuu zimejengwa kwa mapambano na dhoruba
na majira ya mateso. Uwe mvumilivu na mchakato huo. Yakobo alishauri, “Msijaribu
kutoka katika jambo fulani haraka. Acheni lifanye kazi yake ili mpate kuwa watu
wazima waliokua sawasawa.” Yakobo 1:4 (Msg)
Usivunjike
moyo. Habakuki alivunjika moyo kwa sababu hakufikiri Mungu alikuwa
anatenda kazi haraka, Mungu alisema: “Mambo haya
niyoyapanga hayatatokea mara moja. Polepole, kwa uthabiti, kwa uhakika, wakati
unakaribia ambapo maono haya yatatimizwa. Kama inaonekana kuwa polepole, usikate
tamaa, kwa kuwa mambo hayo kwa hakika yatatimia. Uwe na subira tu! Hayatakawia
hata kwa siku moja.” Habakkuk 2:3 (LB) Kuchelewa sio
kukanusha kutoka kwa Mungu.
Kumbuka ulikotoka, usiangalie tu umbali wa unakokwenda. Hauko pale
unapotaka uwe, lakini pia hauko ulipokuwa zamani. Miaka mingi iliyopita watu
walivaa kifungu chenye herufi PBPGINFWMY. Hii ilisimama badala ya “Tafaddhali
vumilia, tafadhali uwe na subira, Mungu hajamaliza kazi yake kwangu bado.”
Mungu bado hajamaliza na wewe, hivyo endelea kusonga mbele. Hata konokono
alifika kwenye safina kwa uvumilivu!
SIKU YA ISHIRINI NA NANE KUFIKIRI
JUU YA LENGO LANGU Jambo la Kutafakari: Hakuna njia ya mkato katika kukua. KIfungu cha Kukumbuka: “Mungu alianza
kufanya kazi njema ndani yenu, na nina hakika ataiendeleza hadi
itakapokamilika pale Yesu Kristo atakapokuja tena.” Wafilipi 1:6 (NCV) Swali la kujiuliza: Je, ni katika eneo gani la kukua kwangu
kiroho nahitaji uvumilivu na bidii zaidi? |
沒有留言:
張貼留言